Hizo contrast ndizo hata Mungu kaziweka kwa kusudi la asili ili wenye upeo waelewe maana halisi ya kusudi la uwepo wao,duniani ni mahali pa kuelewa maana hata uwapo gizani,ni mahali pa makamnda wa roho kuzisoma alama za nuru katikati ya giza na kelele za dunia,wewe ni moja wapo wa kelele za dunia,wewe ni mojawapo ya walio gizani wakashindwa kuona misimbo ya kupita ili utoke vitani ukiwa salama…kila aina ya maisha unayoyajua yanahitimishwa na nukta ya kifo,bado huelewi kuwa huna udhibiti na jeuri ya kiburi chako? Any way utakapofumba macho jumla kamwe hautarudi kutusimulia utakacho kiona,ila utakuwa umeelewa kuwa Mungu ni hadithi ama chanzo cha uhai- kila siku kila kona ni misiba tu bado huna hofu kwamba angalau uitafute maana ya uwepo wako kabla hujafutwa katika orodha ya walio hai.