Sinkala Ulishaoa?

Mkuu Sinkala mwaga hapa mauzoefu yako na ma expiliensi yako ya ndoa hadi sasa,vipi unashauri na wengine wajitose au ndo yashakuwa yale ya walio nje wanataka waingie na walio ndani wanataka kujongomea?
 
Tumebaki sisi sasa kuiga mfano wako mzuri mimi natarajia hapo mwaka 2012 nitangaze live lakini tatizo bado sijampata.

Soma Bible,Mwanzo 2:18. Neno linasema Mungu atakupa wa kufanana nae,mfano kama wewe fisadi wa mapenzi ,utampata fisadi wa mapenzi.Hivyo take good care.
 
Soma Bible,Mwanzo 2:18. Neno linasema Mungu atakupa wa kufanana nae,mfano kama wewe fisadi wa mapenzi ,utampata fisadi wa mapenzi.Hivyo take good care.

Nitapata lini sasa maana muda unakwenda na kusali na sali au huyu Mungu anataka nizeeke ndo anionyeshee?
 
... mimi natarajia hapo mwaka 2012 nitangaze live lakini tatizo bado sijampata.
Ha ha haaa :D !! Fidel, ni kweli hujampata? Sasa na yule anayekung'ata ni nani? Na yule mwingine uliyesingiziwa kuwa ana mimba yako je? Mimi nadhani umempata/umewapata ila hujaamua tu !!
 
Ha ha haaa :D !! Fidel, ni kweli hujampata? Sasa na yule anayekung'ata ni nani? Na yule mwingine uliyesingiziwa kuwa ana mimba yako je? Mimi nadhani umempata/umewapata ila hujaamua tu !!

Unajua mkuu hawa naona sio chagua langu kabisa wapo wapo tu ndo kama hivi namega tu lakini kusema tunaweza pikika katika chungu kimoja hapana wajanja mno wamenizidi ujanja ndo maana mguu mmoja ndani mguu mwingine nje. Ndo maana bado natafuta ambae tutaweza tukaenda pamoja. Ni vigumu kupata right choice.
 
Du...hii kali.
Na Fidel180 alikuwepo! huoni kuwa ni tishio kwa usalama wa ndoa yako! Ni mchafuzi sana huyu jamaa, usicheke nae bana! Chunga sana simu ya mkeo mzee, usikute keshaanza kumdipudipu!

Hahahahahahahahahahahahahahahaha teh teh teh teh dah mbavu sina ngoja nikapate mzinga wa Konyagi kwanza nitulize mbavu zangu
icon10.gif
 
Mkuu Sinkala mwaga hapa mauzoefu yako na ma expiliensi yako ya ndoa hadi sasa,vipi unashauri na wengine wajitose au ndo yashakuwa yale ya walio nje wanataka waingie na walio ndani wanataka kujongomea?
Mkuu, ni mapema mno kwangu kuzungumzia experience ya ndoa kwani ndo kwanza nipo katika wiki ya pili, ukizingatia kwamba wiki moja ilikuwa ya honeymoon! Kwa sasa siwezi kuongelea experience ya ndoa, ila naweza kuongelea experience ya harusi !!! However kufunga ndoa ni wajibu.
 
Nitapata lini sasa maana muda unakwenda na kusali na sali au huyu Mungu anataka nizeeke ndo anionyeshee?

Inawezekana unachagua saaaaaaaaana.Yani yule Mungu anayekupa na anaona anakufaa,wewe unamkataa kwa sababu zako,labda unaona hajasoma na vitu kama hivyo.Lakini endelea kuvumilia utampata tu.Sio mbaya ukimuuliza Sinkala akupe desa wake alimpataje? Sababu anaonekana amepata mke mwema.
 
Tatizo nao wataka wananipiga chini na ambao siwataki ndo hao wananipenda mpaka wananing'ata.
Sinkala naye alikuwa na vigezo vyake mpaka akampata ampendae kwa dhati mpaka akaamua kufunga pingu za maisha.
 
Tatizo nao wataka wananipiga chini na ambao siwataki ndo hao wananipenda mpaka wananing'ata.
.

hiyo ipo sana mkuu!
demu kama humzimii basi ndio utakuta anakung'ang'ania kama luba, duh.
 
Usijali Fidel80! I guess umezaliwa 80's,muda bado kidogo.Vizuri mara nyingi vina gharama ,na gharama mojawapo ni muda.Endelea kumsaka wako ,wakati ukiwadia utamshukuru Muumba.Mie nakushauri lipia gharama tu ya kutulia na kuchagua kwa makini,usiwe na papara kwa kudhani eti umechelewa.
 
Usijali Fidel80! I guess umezaliwa 80's,muda bado kidogo.Vizuri mara nyingi vina gharama ,na gharama mojawapo ni muda..

Jamani muwe mnanisaidia basi angalau angalizo ukisikia kabinti kanataka kuolewa unaniacha kwa Sadala kisha unatugonganisha tufanye maelewano yetu may be kanaweza kunifaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom