Single Mother ananilazimisha kulipa ada ya mwanaye

Single Mother ananilazimisha kulipa ada ya mwanaye

MREJESHO
SHULE ZIMEFUNGULIWA TOKA WIKI ILIYOPITA MIMI NIMESHINDWA KULIPA HIYO ADA,
SINGO MAZA ANAMPIGIA SIMU BABA MTOTO WIKI NZIMA SIMU HAZIPOKELEWI
Kama inawezekana nenden mguu kwa mguu kwa baba mtoto mkazungumze naye kuhusu mkwamo mnaopitia na yeye aone namna anavyoweza kuwakwamua.
 
Kama inawezekana nenden mguu kwa mguu kwa baba mtoto mkazungumze naye kuhusu mkwamo mnaopitia na yeye aone namna anavyoweza kuwakwamua.
SHIDA HUYU SINGO MAZA ALIMZALILISHA SANA BABA MTOTO WAKE LAST TIME NA AKAMWAMBIA HAHITAJI MSAADA WAKE WOWOTE ULE, IMEPITA MIEZI MIWILI JAMAA HAJAWAHI PIGA SIMU WALA MESEJ KUULIZIA HATA HALI YA MTOTO
 
SHIDA HUYU SINGO MAZA ALIMZALILISHA SANA BABA MTOTO WAKE LAST TIME NA AKAMWAMBIA HAHITAJI MSAADA WAKE WOWOTE ULE, IMEPITA MIEZI MIWILI JAMAA HAJAWAHI PIGA SIMU WALA MESEJ KUULIZIA HATA HALI YA MTOTO
Dharirisha vs Zalilisha.

Waliovuliana chupi na boxer wakikutana wana namna yao ya kuzungumza. Trust me mpeleke mwenzako kwa mume mwenza, lazima jamaa atawasaidia tu ila uwe tayari wapashe kiporo.
 
Dharirisha vs Zalilisha.

Waliovuliana chupi na boxer wakikutana wana namna yao ya kuzungumza. Trust me mpeleke mwenzako kwa mume mwenza, lazima jamaa atawasaidia tu ila uwe tayari wapashe kiporo.
Unataka mwenzio amwagiwe uji wa moto usoni sio? Haya endelea kumdanganya!
 
Masingo maza wanazidi kuwa wengi huku wakijifanya kuwakaushia wazazi wenza kwamba hawataki misaada yao kwa watoto, Ni upumbavu tu singo mama kukataa msaada wa baba mtoto huku ukimtwisha mzigo fala ndiye agharamikie matunzo ya mtoto wakati baba yake yuko hai
Huyo ni simp,masimp huwa ndio wanaume mabwege ambao wanatumika na wanawake na kuwapa jeuri nje ya mahusiano ya ndoa na ndani.

Hawa masimp ndio wanafanya wanawake waseme "sio wanaume wote hawapendi single mothers wapo wengi tu wanaolea watoto ambao sio wao kama watoto wao".
Kwakifupi masimp ni toleo dhaifu la wanaume kitabia na hawa ndio hutumika na wanawake katika ajenda zao za kuvuruga jamii.

Mfano huyo dada,anafanya kazi Pub sehemu ambayo hukaa wanawake wanaotumika kingono. Mwanaume timamu hawezi ishi na mke anayefanya kazi bar au pub kwasababu ni haramu katika ustawi wa jamii.

Ni aidha atamwambia aache hiyo kazi ya Bar atafute nyingine au akae nyumbani kutunza familia. Mwanamke akigoma huwa anajua kuna masimp yatatokea kumkubali na kiburi chake na yatakusanyika kwake kumlipia mahitaji yake.

Huyu mojawapo kaingia katika mfumo. Ilitakiwa akimwambia single mother sitaki moja mbili tatu aseme sawa baba nakusikiliza. Kuanzia hapo maisha yanakwenda. Ila sio mwanaume unasema sitaki moja mbili tatu na mwanamke anasema na mimi sitaki moja mbili tatu,huyo anajeuri sasa dawa yake kumuacha aishi kwa code zake za jeuri akakutane na masimp awatumie.
 
Kazi yangu ni bodaboda, na nilijuana na huyu single maza kupitia kazi yangu hii, maana yeye anafanya kazi bar hivyo uwa anatoka usiku sana, basi akachukua namba yangu ikawa kila usiku anapiga simu nimfate mda wa kutoka kazinina mazoea yakaanzia hapo.

Baba mtoto wake ni dereva wa halmashauri fulani huko mkoani, na anampenda sana huyu dada, kiufupi baba mtoto anaonekana alikuwa na malengo na huyu single maza, hata kuhudumia alikuwa anahudumia kwa uwezo wake aliyojaliwa.

Sasa huyo baba mtoto baada ya kugundua mimi Nina mahusiano na huyu single maza wake, amekata mawasiliano kabisa na huyu single maza yaani hatoi hata Mia, siyo kodi, chakula wala Ada ya mtoto.

Nimejahidi kuwa nasaidia kuhusu chakula na kumchangia kodi(tukaanza kuishi wote) nasaidia pia mahitaji mengine madogo madogo, kwa bodaboda yangu nimekuwa nikimpeleka kazini na kumrudisha usiku wa manane bure kabisa,, ila mambo yamekuwa magumu ananitaka nilipe na Ada ya mtoto wake sasa.

Nimemwambia amshirikishe baba wa mtoto wake, anakataa anasema hataki msaada wowote kutoka kwa baba mtoto, kwamba ananipenda mimi kwasasa hivyo mimi ndiyoo nimsaidie hiyo hela ya Ada.

Kipato chake yeye ni 300000 kwa mwezi
Nyumba tunayokaa 100000 kwa mwezi
Dada wa kazi 50000
Mtoto wao anasoma private Ada 250000 kila robo muhula hivyo kwa mwaka milioni,
School bus 50000 kila mwezi

Hapo chakula bado na mahitaj mengine,

Kuhusu mimi kipato changu ni 15000 kwa siku nikitoa mafuta na hela ya tajiri,

Wakuuu hivi natoboa kweli hapaaaaaa

Baba wa mtoto kasusaaa kabisa
Kwa akili yako ya kibodaboda kweli huyo mwanamke Hana mawasiliano na aliyezaa nae?
 
Back
Top Bottom