Single LADIES and LADS. . .

ndo maana nakuchukiaga.. na hii ndo comment utakayopata kutoka kwangu.. siongezi hata moja ng'oooo.:ballchain: baadaye..
mpaaka unipe ule umbea kwanza..
 
ndo maana nakuchukiaga.. na hii ndo comment utakayopata kutoka kwangu.. siongezi hata moja ng'oooo.:ballchain: baadaye..
mpaaka unipe ule umbea kwanza..
Embu jibu maswali wewe acha kiburi. . .

Umbea ntakupa nikikumbuka.
 
It really isn't.
But the funny thing is, the simplest things are the hardest to get a hold of. Sad ehhh. . . ?

Sad indeed.That happens when we try to get hold of the simplest things in the hardest ways possible.Sometime making a mountain out of an ant-hill is human nature.Lads try to impress ladies so hard,ladies want that one perfect guy.We should relax and enjoy life afterall we are just ordinary people.When the time comes love will knock on our doors as a matter of fact it is impossible to chase love coz love is everywhere.
 
Lizzy haya mbambo ya ndio au hapana kwenye ukoa au kuolewa mimi sipo kabisa, hebu mimi niambie hadithi ya zawadi imefikia wapi
 
Utajuaje hayo ujanani?


kumkabidhi mtu maisha yako yaliyobaki hapa duniani mara mda wa kufanya hivyo unapofika si jambo dogo.....kuna mambo mengi ya kuangalia....kwanza kwa mimi mwanaume lazima nijue je hili ni chaguo sahihi?..ameamua kwa dhati? au ameona wenzake wameingia huko nae akaingia? au ameshinikizwa? au umri umempita sasa ameona anaweza asiolewe ndo akaamua kuja na kunichagua mimi?

mawazao yake ni yapi? lazima awe na mawazo channya mwenye kujua kujenga hoja na kudadisi..lazima ajiamini, lazima apende kila mtu pasipo ubaguzi....


Lizzy, unajua mwili mmoja hauji kwa kusimama mbele ya padri/mchungaji au shehe.. mtumishi wa Mungu anapotamka ninyi ni mwili mmoja ule mwili huwa hauji mara moja pale...kuufikia mwili mmoja ni safari ndefu sana inayoanzia kwenye uchumba na hukamilishwa miaka mingi sana mkiwa ndani ya ndoa...

siku hizi kuna yale mahusiano yanaitwa ''cyber marriage'' ..we lizzy uko uko uliko na mimi niko huku niliko....mahusiano yotu yameunganishwa na mawasiano ya simu,internet,bbm,skype nk......hata tukikutana tunakutana kwa siku 1 au 2 then narudi baada ya mda tunaenda ndugu zangu wanakuja huko kwenu tunatoa mahali then sasa ndo tunaanza kuishi...hakika hapo tunaweza kuishi lakini kwa shida sana na inaweza kutuchukua mda mrefu kuwekana sawa..na ndio maana wengi hawaishi kulalamika na hatimae ndoa kuvunjika....hii idara ya ndoa ni pasua kichwa sana...ntarudi
 
Swala la vigezo huwa hakunaga, binadamu wote wapo spontaneous unaweza kukuta sista du anasema ,"mimi mwanaume mmfupi sipendi hata kusikia" kesho ukamkuta amefunga ndoa na emolo.
 
Una mpango wa kuoa/kuolewa?

Kama jibu ni HAPANA . . kwanini?
Kama ni NDIO. . . je ni VIGEZO gani ambavyo vikifikiwa na mkaka/mdada utashawishika/penda kuingia ndoani?
Na ni MASHARTI (usichukulie neno masharti kwa uzito wake, namaanisha vitu ambavyo ni muhimu kuzingatiwa) gani ambayo yakizingatiwa unaamini ndoa yako itadumu?

Mi kwangu hapana.
Sababu wanawake nyie pasua sana kichwa mazee. Mia
 
Una mpango wa kuoa/kuolewa?

Kama jibu ni HAPANA . . kwanini?
Kama ni NDIO. . . je ni VIGEZO gani ambavyo vikifikiwa na mkaka/mdada utashawishika/penda kuingia ndoani?
Na ni MASHARTI (usichukulie neno masharti kwa uzito wake, namaanisha vitu ambavyo ni muhimu kuzingatiwa) gani ambayo yakizingatiwa unaamini ndoa yako itadumu?

Mimi NDIO tena ya herufi kubwa na msisitizo
Why NDIO:
Ni mpango wa mwenyezi Mungu kuwepo NDOA tangu uumbaji. sasa kama ilivyo mpango wa Mungu sina budi kuolewa.
Vigezo:
1. Awe na umri kati ya 30 - 35. Mimi nina 26 now
2. Awe na elimu ya chuo kikuu yan awe amegraduate na mimi ndiko ninakoelekea
3. Awe mkristo ila co mlokole wala RC
4. Awe na akili za maisha co kila kitu mpk aombe ushauri kwa mama, baba, kaka, dada yan aweze kujisimamia
5. Awe na kipato kinachoeleweka co (deiwaka) mwajiriwea or biashara
6. Awe ananipenda kwa dhati
7. Awe na uvumilivu kwani hakuna binadmu aliye mkamilifu (tuchukuliane udhaifu wetu co kwake pekeyake hata kwangu)
8. Anaye kubali kujifunza na kukosolewa pia
9. Asiwe na hasira sana pia awe mnyenyekevu yan aombe radhi pale anapokosea
10. Asiwe mgonvi na mwenye bugu (kosa umefanya leo baada ya miaka mitano anakumbushia tu)
11. Asiwe mlevi, mvutabangi, madawa na kulvya na vitu kama hivyo!
12. Mwisho awe mchamungu kweli. (manake kuna wakristo ndio ila mlango wakanisa ni cku ya pasaka na christmas tu)
 
he!:shock: I am not a lady, and I am NOT single....what the heck am I doing here?:shock:
 
mmmh vigezo
1.awe na miaka 30 na kuendelea
2.watoto max 2 maana nimeona vijana wengi wana watoto sana siku hz
3.awe mkristo-lutheranor rc walokole sitaki au sda
4.awe na maisha ya kueleweka kazi biashara yaani awe na source ya income iwe low,medium or high yeyote
5.awe na mvuto bana
6.awe na upendo wa kufa na kuoza juu yangu anichukulie nilivo sipendi kuongea saana sipendi ugomvi wala kuonewa
7.simu yake ni yangu na yangu ni yake niiwe free na simu yake na asimaind
8.awe na busara,mpole asiwe anaongea sana bila sababu labda awe ananipa story za kunifurahisha sipendi makelele
9.awe na akili ya maisha i mean aweze kusimama kama baba kwenye familia awe ni mtu mwenye uwezo wa kutoa maamuzi hata kama ni magumu-asiwe mwoga
10-awe na uwezo wa kuniprotect na mambo yote,maadui,magonjwa
11 awe ma best friend the one i can count on evertything sio nakuja kukopa chakula ofsin wakati nimefulia kwa bahati mbayawhile nina mume ndani nina mume ndani
12 tushee kila kitu kwa shida na raha
13 asipende sex saaana mi kila siku siwezi besides siolewi kwa ajili iyo tu at lesat mara 2/3 kwa wk especially wkend
14 asiwe mlevi,mvuta sigara au bangi
15 asiwe mshirikina au mchawi au wa jamii iyo
16 awe mchaga aisee

17 badae nitakupm

Lazima uolewe na mgogo maana hakuna mchaga anayefikia vigezo hivyo. Wao ni wafanya biashara, cha pombe, wakali wa mechi za nje mara moja moja na ukikagua taili wakiwa wamerudi mida hiyo ya maane taili utakuta ina upepo kidogo au aka slow puncture!
 
Una mpango wa kuoa/kuolewa?

Kama jibu ni HAPANA . . kwanini?
Kama ni NDIO. . . je ni VIGEZO gani ambavyo vikifikiwa na mkaka/mdada utashawishika/penda kuingia ndoani?
Na ni MASHARTI (usichukulie neno masharti kwa uzito wake, namaanisha vitu ambavyo ni muhimu kuzingatiwa) gani ambayo yakizingatiwa unaamini ndoa yako itadumu?

Ndiyo mamii, nina mpango wa kuolewa. Nina imani kubwa kuwa na familia ni jambo jema, hivyo inshallah Mola anijalie nipate mwenza yakinifu.

Kwakweli muda mwingine unaweza kuwa na vigezo usikutane navyo vyote ila si haba kuna vitakavyonivutia niweze funga pingu. Awe anajali kwao na kwetu, mpenda maendeleo, mcheshi, muwazi, mcha mungu(hata kama siyo mlokole) na kushirikishana mambo yote muhimu.

Ndoa inadumu kukiweko na upendo, heshima na uvumilivu..kuwasiliana kuwe msingi bora ili kuhakikisha tunaambiana yote muhimu mazuri na mabaya, kumpa kipaumbele mwenza yani nafasi ya mume/mke, kuwa marafiki zaidi tu ya mume/mke. Mume wangu atakuwa ni namba moja maana ndiye nitakae jenga nae familia na panapo majaliwa tuzeeke wote na kuzikana.

Miaka 30-39. Elimu iwepo na kazi awe nayo pia! maisha kusaidiana!

Ntakualika, tuombeane kheri Lizzy!
 
Lazima uolewe na mgogo maana hakuna mchaga anayefikia vigezo hivyo. Wao ni wafanya biashara, cha pombe, wakali wa mechi za nje mara moja moja na ukikagua taili wakiwa wamerudi mida hiyo ya maane taili utakuta ina upepo kidogo au aka slow puncture!
nani aolewe na ombaomba?mwee niombe radhi
 
Back
Top Bottom