Singida: Ajali ya Bus la Takbiir

Singida: Ajali ya Bus la Takbiir

Kuna Jamaa yngu yeye alikuwa kwenye Bus la Ally's amekuta ajali ya Bus la Takbiir linalofanya safari zake kati ya Geita na Dar es salaam likiwa limepata ajali Mkoani Singida, kona ya Hingu

Kama una ndugu au Jamaa ambaye alikuwa anasafiri leo naomba ufanye mawasiliano.

Bus lilikuwa linatoka Geita kuelekea jijini Dar es salaam. Taarifa Rasmi bila shaka itatolewa na mamlaka husika

Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi Majuruhi wote waweze kupona

View attachment 2007116View attachment 2007117View attachment 2007118View attachment 2007119
Tahadhari ya video
 
Poleni wahanga wa ajari hii. Inaonekana bus limehama kutoka kushoto kuja kulia upande wa lori wakapigana pass. Poleni sana, madereva chukueni tafadhari.
Seems jamaa alisinzia, kama Jana usiku ndio walifika Katoro na wakageuza Leo, muda huo anakua amechoka sana. Uzuri nimesafiri sana na hii Kampuni, huwa wanapiga tiktaka sana
 
Seems jamaa alisinzia, kama Jana usiku ndio walifika Katoro na wakageuza Leo, muda huo anakua amechoka sana. Uzuri nimesafiri sana na hii Kampuni, huwa wanapiga tiktaka sana
Takbir huwa madereva wanapita barabara za tanzania wakitumia sheri za Burundi
 
Hivi huwa wanatambua mfano mda mchache ujao anaweza kuwa marehemu?
Halafu mbona watu muwe mnawahi kuokoa majeruhi unakuta hapo wanajiwazia kashakufa kumbe moyo kwa mbali bado unapiga.wanamrekodi
Kikubwa ni kumuomba Mungu kila dakika
 
dah walivyochakazana wote walikuwa kwenye mwendo mkali sana...namaanisha wafuso filimbi ilikuwa inalia na wabasi pedal ilikuwa chini...

Tutaendelea sana kushuhudia vifo vya kijinga hivi miaka na miaka kama akili za watu wetu zitaendelea hivi zilivyo...
 
ukipanda bus ukaona dereva haelewi eleweki, paza sauti...ni bora mkachelewa kufika mkiwa wazima...mijitu unakuta bus linaendeshwa hovyo yenyewe imetulia tu kimya kama ng'ombe wanaopelekwa machinjioni, wengine mizambi kibao halafu mnakubali kuwaishwa mbinguni wakati hata hamjatubu bado...
 
Lile jamaa liliweka utaratibu wa kutumbua MaRPC na RTO mkoa ukiwa na ajali....basi ilikuwa starehe kidogo angalau majamaa yananyata kama kobe huko barabarani...

sasa fungulia mbwa ukiwakuta huko barabarani kama jet fighter vile...

Hakuna demokrasia kwa mpumbavu...
 
makafala ya damu hayo biashara ya mabasi ina siri nyingi sana.
 
tujitahidi haya mabombadia, madilimulaina, maeabasi nauli ziwe chini ili raia wawe wanakwea midege kwa wingi kutua pale kahama, Chato, Mwanza, Bukoba, Tabora nk ikiwezekana wale fasti jeti nao warudi na wale presisheni wote nauli iwe 50K popote pale ndani ya TZ ikonomi klasi kwa wazalendo......lile liesijiara na lenyewe limalizike haraka watu waanze kulikwea....Haya mabus watu watakuwa wanapanda kama utalii tu Dar - Mwanza inakuwa week..
 
makafala ya damu hayo biashara ya mabasi ina siri nyingi sana.

sasa unatoa kafara wenzio uwe tajiri, huo utajiri una maana gani sasa...kama wote tutaamua kutoa kafara binadamu wenyewe si wataisha sasa.... kwanini wasiwe wanatoa kafara ya mbuzi na ngo'mbe watu wanachoma nyama na bia....
 
Singida kuna nn mbona ajali kila mara

RPC na RTO tumbua kwa pua pafomansi..
traffick woote wa mkoa rudisha kuwa askari wa askari wa kawaida halafu hamisha woote peleka nanjilinji, sumbawanga, kilwa, mafia na wengine peleka pemba huko...traffic wote wenye vyeo mkoa huo shusha vyeo woote na hamisha vituo vya kazi...
 
Back
Top Bottom