So, for a tanzanian parking your money here is not advised? Cause i see its most of Asian Trading Multinationals put their money here...
Maisha mu ghali sana kule. Nilikuwa huko 2012 nikajuta, bora uswazi kwetu.
Nchi kama hiyo unaweza kukuta kuna raia hajui kusoma??
Inategemea. Unataka standard gani ya maisha.
Binafsi, umeme na kodi nalipa zaidi Tanzania kuliko Japan.
Kula baadhi ya sehemu Tanzania ni ghali kuliko Singapore au Japan. Steak ya mkaburu pale Rhapsody's ni ghali kuliko Tokyo au Singapore.
Unaweza kula kwa $5 Singapore au Tokyo ukipenda. Maduka ya 7-11 au supermarket ndiyo bei zao za chakula cha box au "obento" kwa Kijapani.
Japan mkopo wa benki ni $600 kwa mwezi kununua nyumba na unapewa miaka 25 kulipa. Huwezi kupata mkopo wa kiasi hichi na muda mrefu wa kulipa Tanzania.
naskia wakati tunapata Uhuru 1961 tulikuwa nao sawa hao jamaa sijui over take walitupita wapi
Aiseee! Maendeleo ya wengine utafikiri ndoto.Ma-flyover ya kufa mtu! Navyoona, tatizo lao kubwa ni:Ninataka kwenda point B, nitumie flyover zipi kufika haraka?
Mkuu mtawezaje kuwa sawa nao wakati mmekubali kuongozwa kidharura?Daah tukumbuke mwaka 65 uchumi wa Singapore ulikuwa sawa na wa Tanganyika. Lakini tumeachwa mbali sana