FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,777
Nyerere(Baba wa taifa la Tanzania) na familia yake wanaheshimika kwa kuheshimu mali ya watanzania na kutocheka na Mafisadi pamoja na Ufisadi.
Naam, Nyerere ana heshimika lakini siasa yake ya Ujamaa imekufa na haifatwi tena kwa hiyo hakuna kutaifishana.
Alipotaifisha hii nchi iliingia kwenye dhiki na umasikini wa hali ya juu, kabla ya kutaifisha kwake ilikuwa nchi ya kwanza katika Afrika inayosafirisha mazao ya shambani nje, baada ya kutaifisha tukawa omba omba hata wa chakula tukawa masikini wa mwisho duniani. Hilo kumbuka.
Au haukuwepo wakati wa utawaa wake na unasikia hadithi tu za kuhadithiwa? nakushauri kama ulikuwa haupo, AlhamduliLllah tungali hai tuliokuwepo, uliza kulikuwaje upate ukweli.
Kikwete pia anamheshimu sana Nyerere lakini juzi kasema live, sasa hivi hatuna siasa ya ujamaa, siasa ya ujamaa Tanzania hii ilikuwa ni ya nani zaidi ya Nyerere?