Singa Singa ameiweka serikali ya Kikwete mfukoni

Singa Singa ameiweka serikali ya Kikwete mfukoni

Wakati Tundu Lissu anachangia saga hili pale bungeni na hasa alipokua anaeleza historia ya IPTL na uhusiano wake na JK and then yule mam wa Kimbulu Mary Nagu alivyokua ana m inter fear Tundu na hawa mawaziri kugoma kujiuzuru basi nikajua ngoma imeisha, hakuna ambacho kitatokea hata JK akirudi; hisia zangu zimekamilika. Source ya hi kitu ni mkuu wa kaya so tusitegemee chochote toka kwenye hi serikali ya ccm.

Jambo pekee ambalo Watanzania tunaloweza kulifanya Watanzania ni kuikataaa ccm na mambo yake yote, ninamwomba Mungu pia wafadhili wakomae hadi mwisho wasitoe chochote kama msaada ili mishahara ikosekane kwa wafanyakazi wa serikali ili tuheshimiane; namwomba sana Mungu hilo litimie cause kama madawa ndio hayo hayapo mahospitalini na wakulima ndio hao tumeona mazao yao yanaharibika huko kwenye maghala yao.
 
Hii Ni Serikali Ya Wapumbavu, Na Cha Mpumbavu Huliwa Na Mjinga
 
.... Nimegundua Kwann Akina Werema, Maswi, Tibaijuka Na Muhongo Wamedinda Kujiuzulu... Muhusika Mkuu Wa Escrow Ni Rais Na Familia Yake
 
Nukuu ya maneno ya Mwalimu kuhusu Serikali corrupt.....

Serikali corrupt popote pale, haitozi kodi. Serikali corrupt inatumwa na wenye mali.
Inawafanyia kazi wenye mali. Serikali corrupt itamwambiaje mwenye mali, kwamba “utalipa, usipolipa utakiona!" Atacheka tu huyu.
Atakwambia“unaniambia hivyo wewe? kesho siji basi!”

Serikali corrupt haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi basi.


Yametimia - maana hawa mafisadi wana uwezo wa hata kutuchagulia viongozi wetu ndani ya serikali.
It is absolutely true.

Si umeona hata huo mgao wa Singasinga/Rugemalira aliokuwa 'akiwarushia' promint figures hapa nchini.

Mgao haujaacha sekta yeyote muhimu ndani ya jamii.

Mabilioni yamerushwa kwa Mwawaziri, yakarushwa kwa Majaji,yakarushwa kwa wenyeviti wa kamati za kudumu, yakarushwa kwa bodi ya Shirika letu la 'mwanga'

Ambako kumestua zaidi haya mabilioni yalikorushwa, ni kwa watumishi wa Mungu, wachunga kondoo wa Bwana!

Ndiyo maana, wakati Mwigulu Nchemba,anajitutumua pale bungeni na kudai kuwa huyo Singasinga na wote waliofaidika na mgao wake, hadi ifikapo Desemba 30 mwaka huu, wawe wote wamelipa hizo kodi, ama sivyo vyombo vya dola viwashughulikie, ninaamini kipindi kile huyo Singasinga, alikuwa akijisemea kimoyomoyo kuwa huyu bwana mdogo kweli anazo kweli kukichwa?!

Hebu tusubiri, Desemba 30 siyo mbali, tutapata ukweli kama serikali hii inao ubavu wa kumwambia Singasinga alipe kodi.

Kwa kuwa tuna experience nyingine hapa nchini, ambapo miaka michache iliyopita, akina Nape and his company, walipita nchi nzima, wakiwaambia Mafisadi ndani ya chama chao, wajivue gamba na kuwaachia chama chao within 90 days.

Tujikumbushe kidogo, baada ya kwisha zile siku 90 nini kilitokea, Mosi, hakuna fisadi yeyote aliyejivua gamba, ukimuacha Roistam Aziz, ambaye 'aliwakandia' sana wanaccm wenzie kuwa wanaendesha siasa uchwara!

Lakini kali zaidi ilitoka kwa mzee wa vijisenti Chenge, ambaye alitamba waziwazi kuwa gamba limeshindikana kuvuka na badala yake, limewishia kiunoni!

Hebu sasa tumsubiri Mwigulu na kuona kama atauweza mfupa wa Mafisadi ndani ya Chama chao, ambao vigogo wenzie ndani ya chama chake, akina Kinana, Mangula na Nape, umewashinda kabisa kuutafuna!
 
Eloi eloi...!lamasabaktani?,Hivi ni kweli JK na CCM mmetuacha ndugu zenu wa damu,rangi na nasaba kiasi hiki?hivi kweli kuna kampuni mnaipatia milioni 400 kwa siku?kwani TANESCO haiwezi kununua mitambo yake?NAUMIA,NAUMIA SAAANA MUNGU AMETUTUPA WATANZANIA.sijawahi kuhuzunika MUNGU akanyamaza!SUBIRINI JIBU LA MUNGU ALIE HAI.
 
Tena kaiweka kwenye mfuko wa shati ili iwe rahisi Kila anapohitaji kuitumia asipate tabu kupekua kwenye mfuko wa suruali....... Hii Nchi imekuwa laini sana kwa wezi,Naungana na wanaorudia msemo wa Mwalimu kuwa Serikali corrupt inaburuzwa na watu wachafu........ JK tazama Nyumba yako.
Ati JK awafukuze wale watuhumiwa wa ESCROW? Thubutu! Tutaona!!
 
Mwalimu Nyerere katika hotuba zake humueleza jamaa mmoja aliyejidai kuiweka serikali yake mfukoni jinsi alivyoshughulikiwa. Sasa jambo hili naona limejirudia kwa awamu hii kwa mtu anayeitwa billionea wa IPTL almaarufu Singa singa. Tumeona kwenye vyombo vya habari jinsi alivyaonza kuivimbia serikali na TRA yake juu ya ulipwaji wa kodi inayodaiwa alikwepa na kusema hawezi kuilipa.

Ameenda mbali na kudai kuwa yale maamuzi ya bunge ya kutaka kuitafisha mitambo ya IPTL ni jambo lisilowezekana. Huyu mtu kwa kwa kuwa ameisha toa rushwa kwa mfumo mzima wa nchi basi naona huyu jamaa kaiweka serikali mfukoni.

Nimuonea huruma sana Mwigulu Nchemba na kauli yake kama naibu waziri juu ya ulipwaji wa kodi huyu jamaa kwa kifupi hawamuwezi sababu serikali imeshakuwa serikali corrupt

UPDATES
Singa Singa tayari amefungua kesi mahakama kuu akiamuru bodi ya rufaa ya kodi imkamake na kumfuga jela kamishna mkuu wa TRA kwa madai ya kutakiwa kulipa kodi
Nchi zilizoendelea kama Marekani Secret Service iko chini ya Wizara ya Fedha, wangekuwa wameshammaliza saa hizi kwa kuchezea "system".
 
Inaanza na kiongozi wa juu kuliko wote katika nchi. Huyu akiwa corrupt basi hakuna litakalofanyika. Ni wizi na fedheha tu. Lakini mzigo wote anabebeshwa mwananchi wa kawaida.

Kodi inayokatwa kwenye mishahara na gharama kubwa za huduma sa kujamii kama nishati na usafirishaji vyoote ni mzigo kwa mwananchi wa kawaida.

Inaanzia kenye kura unayopiga kuchagua kiongozi. Haya ni matokeo tu ya mbegu uliyopanda (kura)

Umma ulidanganya na picha za tabasam na ahadi ya maisha mazuri kwa kila mtanzania na Tanzania yenye neema, yako wapi?
 
Kinachosikitisha ni pale ambapo UHALIFU WA KISERIKALI UNAENDELEA, FEDHA ZA NCHI ZINAKWAPULIWA NA VIONGOZI WENYE DHAMANA YA KULINDA MALI HIZO HUKU: HALI YA WANANCHI IKO HOI TAABANI, HUDUMA ZOTE ZA KIJAMII ZIMEKUFA HAKUNA MSAADA KWA WANACHI, UNGOZI WA NCHI UNANUNULIWA KWA RUSHA, HAKI HAIPATIKANI TENA MAHAKANI, MIHIMILI YA DOLA HAIELEWANI 'AND YET' JESHI LETU LA ULINZI NA USALAMA LIMEKAA KIMYA LICHA YA KUAMINIWA PEKEE NA WANACHI WA NCHI HII.

ENDAPO IMANI HII ITATOWEKA BASI HAKUTAKUWA TENA NA MAUMAINI ITAKUWA KILA MTU NA LWAKE NA MACHAFUKO MAKUBWA YATATOKEA NA HAKUTAKUWA NA MTU WA KUYATULIZA. MUNGU EPUSHA HAYA!


OMBI: JESHI CHUKUA HATUA WANCHI WANAIMANI NA JESHI NA WATAUNGA MKONO 100%. HALI NI MBAYA SANA!! NCHI INAFILISIKA.

NGILENENGO1


Nchi yetu imelemewa sasa kama MBWAI NA IWE MBWAI!!!!
 
.... Wadau, Hili Sakata La Huyo Jamaa Linanikumbusha Hotuba Ya Nyerere, Kuna Jamaa Alitaka Kufanya Kama Huyu Jamaa Kwenye Serikali Ya Nyerere, Alikipata Cha Moto.. Kwa Serikali Dhaifu Na Regerege Ya Jk Chini Ya Ccm Tunaona Jinsi Wanavyopata Kigugumizi Kumchukulia Hatu, Au Kwa Vile Hilo Dili Hata Ikulu Inahusika Kwahyo Wanahofia Kwamba Wakimfanyia Fujo Atatoboa Siri? Jamaa Anamfanyia Fujo Kamshina Wa TRA Lakin Haguswi.! Daaah, Nikisema Huyu Jamaa Kaiweka Serikali Yetu Mfukoni Nitakuwa Nimekosea?.
 
Haujakosea mpaka sasa kuitafta magogoni mpaka ufungue mfuko wa shati
 
Sidhani kama hizi jeuri za Singa singa zingeonekana kwa Kamanda Kagame
 
..... Mkuu Kagame Halei Wezi, Huyu Angekuwa Ameshatandikwa Risasi Tena Hadharani

Namkubali Kagame, kuna mtu alisema Tanzania inahitaji kiongozi dikteta mzalendo, ndicho Hon. Kagame anafanya nchini kwake
 
Back
Top Bottom