Singa Singa ameiweka serikali ya Kikwete mfukoni

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,267
2,000
Mwalimu Nyerere katika hotuba zake humueleza jamaa mmoja aliyejidai kuiweka serikali yake mfukoni jinsi alivyoshughulikiwa. Sasa jambo hili naona limejirudia kwa awamu hii kwa mtu anayeitwa billionea wa IPTL almaarufu Singa singa. Tumeona kwenye vyombo vya habari jinsi alivyaonza kuivimbia serikali na TRA yake juu ya ulipwaji wa kodi inayodaiwa alikwepa na kusema hawezi kuilipa.

Ameenda mbali na kudai kuwa yale maamuzi ya bunge ya kutaka kuitafisha mitambo ya IPTL ni jambo lisilowezekana. Huyu mtu kwa kwa kuwa ameisha toa rushwa kwa mfumo mzima wa nchi basi naona huyu jamaa kaiweka serikali mfukoni.

Nimuonea huruma sana Mwigulu Nchemba na kauli yake kama naibu waziri juu ya ulipwaji wa kodi huyu jamaa kwa kifupi hawamuwezi sababu serikali imeshakuwa serikali corrupt

UPDATES
Singa Singa tayari amefungua kesi mahakama kuu akiamuru bodi ya rufaa ya kodi imkamake na kumfuga jela kamishna mkuu wa TRA kwa madai ya kutakiwa kulipa kodi

UPDATES:
Leo rais atalihutubia taifa, je atawekwa mfukoni au atajitoa mfukoni? Kumbukeni IPTL wameshafungua shauri katika mahakama kuu la kuzuia utekelezaji wa maazimio ya bunge
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
19,833
2,000
Nukuu ya maneno ya Mwalimu kuhusu Serikali corrupt.....

Serikali corrupt popote pale, haitozi kodi. Serikali corrupt inatumwa na wenye mali.
Inawafanyia kazi wenye mali. Serikali corrupt itamwambiaje mwenye mali, kwamba "utalipa, usipolipa utakiona!" Atacheka tu huyu.
Atakwambia"unaniambia hivyo wewe? kesho siji basi!"

Serikali corrupt haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi basi.

Yametimia - maana hawa mafisadi wana uwezo wa hata kutuchagulia viongozi wetu ndani ya serikali.
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,764
2,000
.........nani atakuja kutukomboa nchi hii na genge hili la mafisadi? hivi Jeshi lipo kweli?TISS wapo kweli?Singa Singa anakuja kututawala mchana kweupe!! kweli jamani??Tena amekuja akiwa mtupu pesa ni zutu wenyewe....!!Hizi nafasi kubwa wasigombanie tu...inabidi mfumo ubadilishwa tunapata watu wenye uwezo mdogo sana au waliowekwa na mafisadi.....
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,825
2,000
Tena kaiweka kwenye mfuko wa shati ili iwe rahisi Kila anapohitaji kuitumia asipate tabu kupekua kwenye mfuko wa suruali....... Hii Nchi imekuwa laini sana kwa wezi,Naungana na wanaorudia msemo wa Mwalimu kuwa Serikali corrupt inaburuzwa na watu wachafu........ JK tazama Nyumba yako.
 
nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,267
2,000
Nukuu ya mameno ya Mwalimu kuhusu serikali corrupt.....

Serikali corrupt popote pale, haitozi kodi. Serikali corrupt inatumwa na wenye mali.
Inawafanyia kazi wenye mali. Serikali corrupt itamwambiaje mwenye mali, kwamba "utalipa, usipolipa utakiona!" Atacheka tu huyu.
Atakwambia"unaniambia hivyo wewe? kesho siji basi!"

Serikali corrupt haikusanyi kodi. Itabaki kufukuzana fukuzana na vijitu vidogo vidogo mabarabarani hivi basi.

Yametimia - maana hawa mafisadi wana uwezo wa hata kutuchagulia viongozi wetu ndani ya serikali.
Umepigilia mulemule
 
bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,152
2,000
Naomba kuuliza kama ndo huyuhuyu aliyekuwepo wakati Luwassa anajiuzuru uwaziri mkuu. Kama ndo hivyo basi anatisha sana na nampa shikamoo
 
AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,011
2,000
kumbe amerudi nchini, nilisikia katoroka. kama yupo kwanini asikamatwe kusubiri upelelezi akakae ndani pale segerea? polisi wanamchelewesha nini? huyo anatakiwa kukamatwa haraka kabla hajakimbia nchi.
 
Nani amkamate huyu jamaa alishajipenyeza ndani ya jeshi la polisi kwa kifupi serikali haina kauli juu ya bwana huyu
 
AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,011
2,000
Nani amkamate huyu jamaa alishajipenyeza ndani ya jeshi la polisi kwa kifupi serikali haina kauli juu ya bwana huyu
yeye anasema ni mtu wa iringa, hivi mtu wa iringa anaweza kuwa na class ya uwekezaji kama yake, na anataka kesi ikaamuliwe uingereza wakati yeye ni tz? yaani mtz aingie mkataba na serikali yake ya tz halafu aseme kesi ikaamuliwe uingereza?hahahaha, anamdanganya nani? mtz aje aishi hapa tz kwa permit ya muwekezaji? au aliukana utz
 
Fx Trader

JF-Expert Member
Jun 10, 2014
489
195
CCM has killed this country. As we continue to suffer from the freeze of donor aid- our government is num over the allegations. This is a clear sign of a failed state!! Well done CCM!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom