Kibosho1
JF-Expert Member
- Dec 12, 2017
- 2,491
- 3,998
Singa ni kijiji kilicho katika kata ya Kibosho mashariki, wilaya ya Moshi vijijini katika mkoa wa Kilimanjaro.
Wakaazi wa eneo hili ni Wachagga wa Kibosho japo siku hizi kuna wapare wengi na makabila mengine kama wasambaa na hata wahaya(wengi ni wajenzi).
Kijiji cha Singa kimegawanyika sehemu maeneo matatu,Singa juu, Singa kati na Singa chini. Sehemu zote zimeunganishwa na barabara kubwa inayoenda Kibosho mission.
Kijiji hiki kilikuwa na kila kitu miaka hiyo.
Kilikuwa na kina huduma zote za kijamii kama Shule za msingi, shule za sekondari vyuo mbalimbali, hospitali na hata nyumba za ibada (kasoro msikiti)
Kijiji kilikua kinalima mazao mbalimbali pia. Kilikua na basi kubwa la abiria maarufu kama Ndewedo.
Kijiji hiki kina historia kubwa sana kiroho,kwani wajenzi wa kanisa la Kibosho walifia kwenye mto unaoitwa Nsoo na kuliwekaa msalaba kama kumbukumbu, kila mwaka kulifanyika ibada eneo hilolakini msalaba huo ulivunjika miaka ya 2003 na haukurushwa tena.
Kuna eneo linaitwa "Odaa" lina historia ya kushangaza sana (kuna kitabu cha historia ya hapa).
Kijiji kilikuwa na sifa zote ujuazo lakini kwa sababu ya utendaji mbovu mbovu wa serikali basi kimefilika kwa sasa.
Jambo la kushangaza pamoja na yote lakini hakuna kituo cha polisi hata kimoja na bado barabara yake mpaka leo haina lami japo ndio inayopitisha wagonjwa mbalimbali, dawa na mizigo inayokwenda hospitali ya Kibosho na kanisa Katoliki Kibosho.
Serikali na wadau wanakwama wapi kujenga kituo kidogo cha polisi? Kuna majumba makubwa ka mahekalu lakini kituo cha polisi hakuna.
Kijiji gani zaidi ya hiki Tanzania?