Singa: Kijiji kilichokuwa tajiri kuliko vyote Tanzania kabla na baada ya uhuru

Kibosho1

JF-Expert Member
Dec 12, 2017
2,491
3,998
Singa ni kijiji kilicho katika kata ya Kibosho mashariki, wilaya ya Moshi vijijini katika mkoa wa Kilimanjaro.

Wakaazi wa eneo hili ni Wachagga wa Kibosho japo siku hizi kuna wapare wengi na makabila mengine kama wasambaa na hata wahaya(wengi ni wajenzi).

Kijiji cha Singa kimegawanyika sehemu maeneo matatu,Singa juu, Singa kati na Singa chini. Sehemu zote zimeunganishwa na barabara kubwa inayoenda Kibosho mission.

Kijiji hiki kilikuwa na kila kitu miaka hiyo.
Kilikuwa na kina huduma zote za kijamii kama Shule za msingi, shule za sekondari vyuo mbalimbali, hospitali na hata nyumba za ibada (kasoro msikiti)

Kijiji kilikua kinalima mazao mbalimbali pia. Kilikua na basi kubwa la abiria maarufu kama Ndewedo.

Kijiji hiki kina historia kubwa sana kiroho,kwani wajenzi wa kanisa la Kibosho walifia kwenye mto unaoitwa Nsoo na kuliwekaa msalaba kama kumbukumbu, kila mwaka kulifanyika ibada eneo hilolakini msalaba huo ulivunjika miaka ya 2003 na haukurushwa tena.

Kuna eneo linaitwa "Odaa" lina historia ya kushangaza sana (kuna kitabu cha historia ya hapa).

Kijiji kilikuwa na sifa zote ujuazo lakini kwa sababu ya utendaji mbovu mbovu wa serikali basi kimefilika kwa sasa.

Jambo la kushangaza pamoja na yote lakini hakuna kituo cha polisi hata kimoja na bado barabara yake mpaka leo haina lami japo ndio inayopitisha wagonjwa mbalimbali, dawa na mizigo inayokwenda hospitali ya Kibosho na kanisa Katoliki Kibosho.

Serikali na wadau wanakwama wapi kujenga kituo kidogo cha polisi? Kuna majumba makubwa ka mahekalu lakini kituo cha polisi hakuna.

Kijiji gani zaidi ya hiki Tanzania?
 
Sio kweli kwamba ndiyo Kijiji tajiri Moshi
Kijiji nnachotoka mimi Moshi hukohuko
Kwanza kina mitaa viwanja vimepimwa kabisa
zamani wakati nipo mdogo kulikuwa na
Mashine ya kusaga na kukoboa ya Kijiji
Mpaka leo ipo
Trekta la Kijiji limekufa miaka ya karibuni
Dcm la Kijiji limekufa pia
Duka la Kijiji wameshalinywa halipo tena
Duka la kilimo la Kijiji pembejeo za kilimo aina zote zilikuwepo hapo
Kulikuwa Kuna mifugo ya Kijiji ni kama ranch sijui ndiyo ranch mnaita
Kubwa kabisa ngombe wale wakisasa wanaitwa kulikuwa kuna wafanyakazi wa huo mradi kabisa asubuhi tulikuwa tunaenda kununua maziwa tunapanga foleni
Kuna mashamba ya Kijiji makubwa Sana
Na yapo vizuri sana utaratibu uliokuwepo Kama mwanakijiji unahitaji kulima kwenye shamba kwenye eneo la Kijiji unaenda ofisi ya Kijiji unawaambia unalipia elfu 10 unaenda kupewa eneo la heka moja unakuwa unalima kila mwaka unalipia elfu 10 inakuwa hivyo miaka yote linakuwa Ni Kama lako ila sio lako ni lakijiji sijajua Kama wamebadili utaratibu kwa Sasa

Lakini pia wajapani walikuwa na shirika lao kule wakaleta mradi wa kilimo cha mpunga eneo la mashamba ya wananchi yaligeuzwa kuwa mashamba ya mpunga
Na baadhi ya mashamba ya Kijiji yalifanywa kuwa ya mpunga pia
Ni mashamba ambayo yapo katika vipimo maalumu na yamewekwa level sawa kwaajili ya wepesi wa kumwagilia miferegi ya maji imejengwa kwa zege vizuri

Kijiji kina mashamba hayo ya mpunga ambayo nadhani yanaweza kufika 100 au kukaribia idadi hiyo
Na kwa Sasa kukodi shamba moja ili ulime mpunga ni laki nne
Katika mashamba ya mpunga ya wanakijiji,uongozi wa Kijiji ndiyo unaratibu kila kitu na maji huwa yanalipiwa ofisi ya Kijiji ili kubalance maji kwa kuwa mashamba ni mengi Sana kuna wakati watu hutakiwa kulima mahindi na wengine hulima mapinga kwa kuwa mahindi hayahitaji maji mengi Kama mpumga

Kuna maeneo kwa ajili ya shule na makanisa kuna kanisa la roma na kkkt
Kanisa la roma ni poroki kwa waroma wanaelewa
Eneo la shule ni kubwa sana zamani ilikuwa ni shule ya msingi ila ilikuja kujengwa shule nyingine ya msingi na likagawanywa eneo kwaajili ya sekondari pia ukiangalia jiografia ya Kijiji ni kama eneo la msikiti halikutengwa ila msikiti upo na eneo lake ni dogo tu nadhani waisilamu walikuja baadae baada ya Kijiji kuwa kimeshaanzishwa
Kuna mchanganyiko mchanganyiko wa watu makabila mengi tu japo wachaga ni wengi
Kila mwaka barabara muhimu zilikuwa zinachongwa
Adhani miradi mingi imekufa kwa ufisadi tu
Kuna muingiliano mkubwa tu wa watu. Kwa Sasa
Hata viongozi wa Kijiji wengine ni wakuja tu
 
Sio kweli kwamba ndiyo Kijiji tajiri Moshi
Kijiji nnachotoka mimi Moshi hukohuko
Kwanza kina mitaa viwanja vimepimwa kabisa
zamani wakati nipo mdogo kulikuwa na
Mashine ya kusaga na kukoboa ya Kijiji
Mpaka leo ipo
Trekta la Kijiji limekufa miaka ya karibuni
Dcm la Kijiji limekufa pia
Duka la Kijiji wameshalinywa halipo tena
Duka la kilimo la Kijiji pembejeo za kilimo aina zote zilikuwepo hapo
Kulikuwa Kuna mifugo ya Kijiji ni kama ranch sijui ndiyo ranch mnaita
Kubwa kabisa ngombe wale wakisasa wanaitwa kulikuwa kuna wafanyakazi wa huo mradi kabisa asubuhi tulikuwa tunaenda kununua maziwa tunapanga foleni
Kuna mashamba ya Kijiji makubwa Sana
Na yapo vizuri sana utaratibu uliokuwepo Kama mwanakijiji unahitaji kulima kwenye shamba kwenye eneo la Kijiji unaenda ofisi ya Kijiji unawaambia unalipia elfu 10 unaenda kupewa eneo la heka moja unakuwa unalima kila mwaka unalipia elfu 10 inakuwa hivyo miaka yote linakuwa Ni Kama lako ila sio lako ni lakijiji sijajua Kama wamebadili utaratibu kwa Sasa

Lakini pia wajapani walikuwa na shirika lao kule wakaleta mradi wa kilimo cha mpunga eneo la mashamba ya wananchi yaligeuzwa kuwa mashamba ya mpunga
Na baadhi ya mashamba ya Kijiji yalifanywa kuwa ya mpunga pia
Ni mashamba ambayo yapo katika vipimo maalumu na yamewekwa level sawa kwaajili ya wepesi wa kumwagilia miferegi ya maji imejengwa kwa zege vizuri

Kijiji kina mashamba hayo ya mpunga ambayo nadhani yanaweza kufika 100 au kukaribia idadi hiyo
Na kwa Sasa kukodi shamba moja ili ulime mpunga ni laki nne

Kuna maeneo kwa ajili ya shule na makanisa kuna kanisa la roma na kkkt
Kanisa la roma ni poroki kwa waroma wanaelewa
Eneo la shule ni kubwa sana zamani ilikuwa ni shule ya msingi ila ilikuja kujengwa shule nyingine ya msingi na likagawanywa eneo kwaajili ya sekondari pia ukiangalia jiografia ya Kijiji ni kama eneo la msikiti halikutengwa ila msikiti upo na eneo lake ni dogo tu nadhani waisilamu walikuja baadae baada ya Kijiji kuwa kimeshaanzishwa
Kuna mchanganyiko mchanganyiko wa watu makabila mengi tu japo wachaga ni wengi
Kila mwaka barabara muhimu zilikuwa zinachongwa
Adhani miradi mingi imekufa kwa ufisadi tu
Kuna muingiliano mkubwa tu wa watu. Kwa Sasa
Hata viongozi wa Kijiji wengine ni wakuja tu
Elewa sio kwa sasa kabla na baada ya uhuru mwisho ilikuwa miaka ya 90s. Kama unakataa taja kijiji chako na mambo niliyotaja hapo.
Kumbuka hapo hakuna ufadhilii hata sent!!
 
Hahaha,my mother's land.Singa juu.Hivi ndewedo manake nini?Kumbe ndo kulikua kijiji chenye maendeleo hivo?
 
Mimi kijiji chetu kina/kilikuwa na vyote hivyo,huku kwetu watu walitoka mpaka Burundi kuja kufanya kazi,kuna wafanyabiashara walikuwa wanatoka wilayani kuja kufungasha vitu vya maduka yao,makocha wakubwa wakubwa washakuja kuishi hapa kufundisha mpira wa miguu,yaani kulikuwa na timu kubwa kabisa! Wazungu waliweka hospital mbili,kulikuwa na mabasi kubwa linaloenda dar kutokea kijijini,ila kwa sasa zote ni story tu
 
Wapi na kijiji gani?
 
Mgombezi korogwe Tanga,maarufu kwa kilimo cha mkonge enzi hizo,hadi kuna topic tulisoma "kilimo cha mkonge Ngombezi' nafikiri ni darasa la nne au Tano
Haa 😁😂😅😄😄😁😂🤣
Wewe Jamaa Ni Ujanjaujanja
Korogwe Hapo Mgombezi,
 
Back
Top Bottom