Chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) na sakata la tamthilia ya Zahanati ya Kijiji. Ukimya wa Bodi ya Filamu unatoa mwanya wa unyanyasaji

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Chama cha Wauguzi TANNA wametoa waraka unaoelezea sakata lao na waandaaji wa thamthilia ya Zahanati ya Kijiji onayorushwa na kituo cha Azam TV.

Wadau mbalimbali wa sanaa wameonesha kuchukizwa na mwenendo wa chama hiko cha wauguzo kuongilia taaluma ya sanaa hususani kuonesha dalili ya kulazimisha kuiweka masharti taaluma ya sanaa hususani filamu na uigizaji.

Tamko la chama cha wauguzi 👇👇👇

IMG-20230326-WA0002.jpg

IMG-20230326-WA0002.jpg


Mpaka muda huu, Bodi ya Filamu ambayo ndiyo iliyoongoza kikao cha usuluhishi imekaa kimya bila kutoa tamko lolote kuhusu maafikiano yaliyofikkwa baina ya TANNA na waandaaji wa tamthilia ya Zahanati ya Kijiji.


Hapa ni tamko la awali ambalo lilitolewa na asasi ya kutetea Sanaa na Wasanii ambao walishiriki kwa upande wa utetezi yaani waandaaji wa Zahanati ya Kijiji walitoa tamko kwa niaba ya wwaandaaji hao

Tamko la Tanzania Artists Rights Organization (TARO) kabla ya kikao cha kusikiliza malalamiko ya TANNA👇👇

IMG-20230309-WA0020.jpg

IMG-20230309-WA0021.jpg



Press ya TARO baada ya kikao cha masikilizano baina ya TANNA na muandaaji wa tamthilia ya Zahanati ya Kijiji. Ikumbukwe TARO ilihusika katika nafasi ya utetezi wa muandaaji. 👇👇👇

Screenshot_20230327_225348_Instagram.jpg

Screenshot_20230327_225415_Instagram.jpg



Chama cha wauguzi Tanzania kimeonesha dhahiri kuitunishia misuli Bodi ya Filamu kwa kulazimisha hoja zake ambazo nyingi hazikuwa kwenye msingi wa madai yake na kuzifanya kuwa ndiyo maazimio ya kikao hicho.

Ikumbukwe, TARO walisimamia hoja kuu ya kuweka zuio ya kusitisha ama kusimamisha kurushwa kwa tamthiliya hiyo. Na lengo hilo lilifanikiwa hivyo watazamaji na wapenzi wa tamthilia ya Zahanati ya Kijiji wataendelea kuitazama kupitia kituo cha Azam Tv.

Bodi ya Filamu Tanzania imeendelea kuwa kimya bila.kusema lolote kwenye sakata hili ambalo TANNA wanajaribu kuwaridhisha wanachama wake kuwa chama hiko kina uwezo wa kutoa maagizo kwa mamlaka halali za Serikali na kuingilia uhuru wa kutoa maoni kupitia sanaa.
 
Political Correctness Gone Mad.

Sio Dini Sio Kazi za Manesi Duh itafuata hata makahaba na Wezi kuja juu kwamba taaluma yao imezalilishwa....

Sijui wanashindwa kujua nini kwamba hizo ni kazi za sanaa, mbona mtu akipigwa kisu akiigiza kwamba amekufa kweli anakuwa amekufa.

Anyway kama vipi wawe wasanii watoe kazi zao kama wanavyotaka na sio kuingilia kazi za wengine.

Siasa kila mahali isipokuwa wanasiasa nao wamegeuka kuwa waigizaji.

No wonder tunapiga hatua kwenda nyuma
 
Political Correctness Gone Mad...

Sio Dini Sio Kazi za Manesi Duh itafuata hata makahaba na Wezi kuja juu kwamba taaluma yao imezalilishwa...
Inaonesha kuwa, taaluna ya wauguzi ina utakatifu usioruhusu kutumika kwenye kazi za ubunifu.

Sasa wasanii wachoraji nao watapaswa kuomba kibali cha kuwachora manesi
 
Binafsi sijaiona, lakini issue sio uzuri wa hio kazi ni watu kuingilia kazi za watu.....

Ingekuwa hivi hata reggae za kina Gregory Isack Night Nurse zingekuwa hazipo; au hata ni porno ngapi zinadepict manesi hata ma-nuns.., issue sio kuzipigia kelele bali kuacha kuziangalia

To each his/her own
 
Binafsi sijaiona, lakini issue sio uzuri wa hio kazi ni watu kuingilia kazi za watu.....

Ingekuwa hivi hata reggae za kina Gregory Isack Night Nurse zingekuwa hazipo; au hata ni porno ngapi zinadepict manesi hata ma-nuns.., issue sio kuzipigia kelele bali kuacha kuziangalia

To each his/her own
Umenikumbusha wimbo wa wagosi wa Kaya 🎵Wauguzi🎵
 
Back
Top Bottom