Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,058
- 79,403
Hamjambo!
Sisi wengine hatunaga shida na mtu kuongoza au chama Fulani kuongoza. Ili mradi ni mtanzania na yupo chama cha Watanzania sisi hatuna shida na hilo.
Shida yetu(Mimi na Watibeli) wapigania na wapenda Haki ni kuona Sheria, haki na katiba vikikanyagwa. Hapo ndio shida yetu ilipo.
Nilishasema, sisi hatuapi kumlinda yeyote. Au hatutaki mtu kuapa kutulinda. Sisi tunaapa kulinda Haki, na Sheria za Haki.
Tuna marafiki, ndugu, jamaa na familia. Tunaowapenda, lakini tutatumia ujuzi wetu kuwaelekeza kufuata Haki. Na pale wanapokengeuka kuwarejesha.
Hatuna Shida na Samia sisi. Hivyo tunaposema taratibu zifuatwe haimaanishi tunamchukia Samia na kumpendelea mwingine. Au tunawachukia CCM na kutaka kuwapendelea Chadema au vyama vingine. Nope! Tunataka Haki. Kwa sababu sisi ni Taifa Moja.
Tumetoka katika ardhi hii na bila Shaka mifupa yetu wengi wetu itarudi katika ardhi hii. Sisi ni ndugu.
Samia kufuata utaratibu ni kwaajili ya Taifa, sio kwaajili yake au ya yeyote. Ni kuheshimu Haki.
Maana kuna wahuni pia hutumia Haki kama mwamvuli ili kupata wanachokitaka lakini wakikipata ndani yao ni wahuni na washenzi.
Ndio maana tunahitaji Reforms, Katiba mpya, na Sheria zinazoweka watu wote chini Kuwa sawa.
Tunataka mabadiliko ili kuboresha tulichoachiwa na Watangulizi wetu.
Sheria za Haki
Wazee wetu waliona mpaka 6 sisi tuone mpaka 10 wakija kizazi kingine kiongeze kadiri itakavyoboreka ili nchi yetu iwe Taifa Bora.
Hatupo kwaajili ya yeyote. Tupo kwaajili ya Wote. Taifa.
Taratibu zifuatwe!
Taratibu ndani ya CCM, taratibu ndani ya vyama vya siasa.
Kisha mabadiliko ya kitaifa.
Kama tutashindwa kufuata taratibu za kichama tutawezaje kufuata taratibu za Taifa?
Kama ndani ya chama hamtendeani Haki, mtawezaje kutendea Haki watu wasio wa chama chenu au sisi tusio na vyama?
Tupo! Tunafuatilia