Sina mashaka na Rais Samia Suluhu Hassan

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Sikuwahi kumfahamu vizuri kabla ya Bunge la Katiba.

Ila wakati wa Bunge la Katiba kuna muda alikuwa anachair vikao kipindi kile kina Tundu Antipass Lissu wana mchecheto kweli.

Kusema kweli Rais Samia hasumbuliwi na siasa za maneno, sijui siasa za vitisho, sijui siasa za kuponda. Kipindi kile pamoja na vituko vyote vya kina Tundu Antipass Lissu ila alikuwaga imara sana kuchair vile vikao vya Bunge la Katiba.

Kwa kifupi she was bold kuliko kina Pandu Amir Kificho na Spika wa Bunge lile.

Kuna watu wanadhani Mama Samia anatishika na matamko yao uchwara, kuna watu wanadhani anakosa usingizi. Napenda kuwaambia hamumjui vizuri Samia Suluhu Hassan. Huyu ana ngozi ngumu kwenye siasa za ushindani nadhani kuliko mwanasiasa yeyote yule tuliyewahi kuwa nae. Ndo mana aliweza hata kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa wapinzani wake Bawacha .

Nikimuangalia sana namfananisha sana na mwanasiasa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Margareth Thatcher ambaye alikuwa bold hadi waingereza walimpa Nickname ya Iron Lady

Poleni sana mnaodhani mnaweza kumtetemesha Rais Samia kwa matamko yenu.
 
Huna ukatoliki wowote we nguchiro... wapeni misikiti DP World maana viwanja na majumba vyote mmeuza kwa bei ya kutupa!!
Hapo ndo tofauti yenu na mimi ilipo na hapa ndo nia zenu ovu zinapothibitika. Mnawaza udini ndo mana wakristo wenzenu wenye akili timamu tusioendeshwa na mihemko tumewakataa.

Nyie hamna tofauti na makaburu na watu waliokuwa wanahamasisha mauaji ya kimbari Rwanda. Mmejaa ubaguzi na chuki tu na kama mkristo mwenzenu nawaambia mpone kwa Jina la Yesu
 
Kumbe shida yako ni uislamu. Sasa kwa taarifa yako mimi ni mkristo na mkatoliki na naunga mkono mkataba wa Tanzania na Dubai
Ila Maaskofu wamekuchanganya sana Mkuu.Maaskofu wameaindikia serikali na si msikiti.Kuna nini nyuma ya pazia?Leo nakuona unapambana kishenzi yaani kila uzi upo.

Angalizo:Usije jikuta unapambania ufisadi wa watu wawili watatu watakaofaidika na huu mkataba ukidhani unaupambania Uislamu.

Waislamu wengi wanaojitambua akiwemo JK hawautaki huu mkataba na ndio waliou expose.

Maaskofu wako nyuma ya waislamu wazalendo wanaoitakia nchi mema.Narudia,aliyevujisha huu mkataba ni muislamu mwenzio kwa sababu anaipenda nchi yake.

Unafikiri mtu mwadilifu kama Katanga angekubali kuendeshwa na Dully?
 
Ila Maaskofu wamekuchanganya sana Mkuu.Maaskofu wameaindikia serikali na si msikiti.Kuna nini nyuma ya pazia?Leo nakuona unapambana kishenzi yaani kila uzi upo...
Umeanza kunifahamu lini? Kama ndo umenifahamu sasa basi karibu JF.

Nipo hapa tangu mwaka 2010. Nilikuwa na ID ambayo niliacha kuitumia mwezi Juni 2015 na ndipo nikawa na ID hii.

Nilimpinga sana Magufuli hapa na sasa napinga sana wapotoshaji hapa.
 
Hivi unajua hii sio Monarchy; Na hakuna mtu mmoja mwenye akili / uwezo na mamlaka kwa watu wote ?

Kwahio nchi inaendeshwa kwa Kanuni na Social Contract baina ya wenye nchi (wananchi) na waliopewa dhamana ya kusimamia mali za hao wananchi.

Hata sisi kizazi hiki tunawatunzia hizi mali vizazi vijavyo..., sasa wewe hukatazwi kuwa na Imani na mtu (its your prerogative) lakini kila mlinzi wa mali ya vizazi vijavyo ana kila wajibu wa kutoa neno iwapo anaona kuna mambo hayaendi sawa ambayo yatawacost vizazi vijavyo.
 
Sikuwahi kumfahamu vizuri kabla ya Bunge la Katiba.

Ila wakati wa Bunge la Katiba kuna muda alikuwa anachair vikao kipindi kile kina Tundu Antipass Lissu wana mchecheto kweli...
Kwa vile wananchi wengi tupo upande wa serikali, basi raisi hawezi kuwa na hofu kuhusu mikwara ya waandika barua za mipasho kupitia kichaka cha dini.

Hili litapita na mkataba utaendelea kama kawaida... Trust me 🤞
 
Umeanza kunifahamu lini? Kama ndo umenifahamu sasa basi karibu JF.

Nipo hapa tangu mwaka 2010. Nilikuwa na ID ambayo niliacha kuitumia mwezi Juni 2015 na ndipo nikawa na ID hii.

Nilimpinga sana Magufuli hapa na sasa napinga sana wapotoshaji hapa.
Sihitaji kukufahamu,nimekupa angalizo.Mkatoliki mwenzangu
 
Kwa vile wananchi wengi tupo upande wa serikali, basi raisi hawezi kuwa na hofu kuhusu mikwara ya waandika barua za mipasho kupitia kichaka cha dini.

Hili litapita na mkataba utaendelea kama kawaida... Trust me 🤞
Na hii ndo sifa kuu ya kiongozi ni kuwa bold na firm kwenye mambo ya msingi haya ya kimaendeleo maana siku ya mwisho unahukumiwa kwa matokeo ya maamuzi yako!
 
Sikuwahi kumfahamu vizuri kabla ya Bunge la Katiba.

Ila wakati wa Bunge la Katiba kuna muda alikuwa anachair vikao kipindi kile kina Tundu Antipass Lissu wana mchecheto kweli...
Hivi ni nani alimpa nguvu za KiSerikali mtoto wa Rais na Ujumbe wake Uganda?

....ni nani kama siye Amri Jeshi mkuu anayetuma Jeshi kuangamiza kabila la Wamasai Ngorongoro?

....ni nani aliyesema Mbowe ana kesi ya Ugaidi mbele ya vyombo vya habari vya nje?
 
Wapi imesemwa alienda kuiwakilisha Serikali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom