Sina hamu ya kuolewa

Sina hamu ya kuolewa

Anasema mchumba ane ila ndio hivyo vimbwanga vya ndoa ndio anaogop

huu ndo upuuzi tusioutaka..... ana mchumba then anasema hataki ndoa, kesho akiporwa mchumba atamlaumu nani?hao anaowaambia anawaamini?......ok kama hataki ya nini kumzibia mwenzie...huyo mchumbake? asimpotezee mwenzie muda.....pumbafu keza.....
 
Penzi ni la ajabu sana na pia hushangaza...wakati mwingine penzi hutufanya tuyajutie maisha na kutaka kujitoa uhai....wakati mwingine penzi hutufanya tuyafurahie maisha na kuona dunia kama paradise kwa raha tuzipatazo penzini...wakati mwingine penzi hutuacha tumebaki na mshangao huku tusiamini kile tunachokishuhudia machoni mwetu....lakini hayo yote hayatuzuii wala haya kutuogopesha kuzifungua tena nyoyo zetu ili tusipende tena kwani tunaamini kuwa safari ya mapenzi ni ndefu sana...kwa kadri tunavyoumizwa penzini ndivyo tunavyopata sugu na kupata fulsa mpya ya kuonja utamu wa penzi jipya.....na hatimaye tunafika mwisho wa safari yetu ya kimapenzi kwa kuwapata wale walioumbwa kwa ajili yetu...wale wanaojua thamani ya mioyo yetu..wale wanaojua thamani ya machozi yetu...na hapo ndipo tunapo ibwaga mioyo yetu na kujihisi kama tumeitua mizigo mizito kwa kuondokana uchovu wa penzi lililopita na kuandika historia mpya kwenye maisha yetu ya kimapenzi kwa kutimiza ule msemo unaosema MAPENZI RAHA, UKIPATA AKUPENDAE.....
 
Nitaufikisha ujumbe kama ulivyo utoa
 
Umenena vyema
 
Mimi siungi mkono kwamba usiolewe hapana, utampata wa kukuoa tena mtu mzuri na utafurahia ndoa yako. Pia usiseme ni dada mmoja wa saloon, sema ni mawazo yako hayo ila achana na huyo shetani. Kwa mwanamke au mwanaume kuwa na ndoa na familia na mkaendana vema inaleta heshima sana katika jamii, ila hata Uwe mwanamke tajiri kiasi gani au hata umiliki hii dunia yote bila kuwa na mume au ndoa bado unaonekana kama ma.la.ya fulani hivi au kahaba....hata jamii haikuelewi....mfano mzuri ni mbunge wa viti maalumu Vicky kamata...nadhani uliona alivyotaka kumuoa Yule kijana mume wa mwanamke mwenzake...ndoa tamu..asikuambie mtu!

Nashukuru kwa ushauri wako ila ukweli ni kwamba ni mdada wa saluni sio mimi
 
Hivi jamani tuambiane ukweli UZURI WOTE ULE WA BAHATI BUKUKU na zile nyimbo zake za kumsifu Mungu na kuzungumzia mambo ya ndoa na jinsi anavyoigizaga ktk nyimbo zake hadi kutoa machozi.....yeye kwanini ndoa ilimshinda? achene ujeuri waimbaji wa injili na achene dhihaka kwa Mungu.....yaani nyie watu sio kioo cha jamii kabisa! There is no correlation between your actions and what your singing to your fans....ndio maana siku hizi nasema miziki ya injili ni biashara tu! You cant imagine Rose Mahenge leo kurudi ktk u bachelor...ni sheeedah

Na hapa ndio kuna tatizo,kama watumishi wa Mungu wanashindwa iweje yeye!!! wanaimba na kusifu utafikiri mbingu inashuka wakati wakiimba,lakini ndoa bado imewashinda wengi wao.
 
Nimekuwa nikisikia na kushuhudia wanandoa wengi wanavyo ishi majirani,ndugu na marafiki huku kukiwa na mikiki mikiki kati yao,ila kilicho nivunja moyo zaidi ni ndoa ya Mbasha sikutegemea wala kudhani kuwa wangefikia hatua hii ya sasa na pale walipokuwa wakihubiri heshima ya ndoa kupitia nyimbo zao.

Ndoa ya Gadna na Jaydee pia ilikuwa kivutio kwangu lakini kumbe sivyo nilivyokuwa nikifikiri,kutokana na yale ninayoyasoma kwenye mitandao na magazeti.

Ama kwa hakika maisha ya ndoa kumbe ni magumu,sina hamu ya kuolewa na wala sihitaji kuolewa,nitatafuta bwana wa kunipa ujauzito tu basi.Dada mmoja aliongea maneno haya akiwa saluni na mashost wake.

Wewe unamtazamo gani aendelee na msimamo wake au abadili msimamo wake.

Pole sana...Ukiolewa au kuoa kwa hamu, lazima hamu itaisha na ndoa itavunjika....hasa ukimpata mwingine mwenye hamu kubwa kwako
 
kwani alitaka kuolewa na mbasha ama gadner mpaka wamkatishe tamaa, hau wanaume wote ni Gardner na mbasha tu.
 
ndoa ni nzuri sana lakini wanandoa wenyewe waipende ndoa yao na kuitendea haki; pia huyo dada si ana akili yake binafsi kwaio inabidi ajiamini yeye mwenyewe siyo kuishi kwa kumuangalia jaydee au mbasha
 
kamagetac,
Get time to know each other and am telling you, hiyo mikiki mikiki hamtaiona... itakuwepo ile tu ya kawaida ambayo, kwa watu wanaoishi pamoja haiwezi kuzuilika... tena inakuwa ni mikiki mikiki ambayo sometimes inageuka kuwa the funny thing kati yenu!

The problem watu hawapeani muda...! Unakuta jamaa anakutana na mrembo kwa kuona cjui ndo mzuri sana anatangaza ndoa ili eti wasije wakamwahi wajanja utafikiri demu mwenyewe kamuopolea kliniki wakati anazaliwa!!! Yaani mwanamke ana 20+ or probably 30+ huko kote wasimuwahi waje kumuwahi kv amekutana na wewe... STUPID!

Wadada nao, kuna wengine wana masharti ya kipuuzi kabisa! Umekutana nae siku mbili tatu, mara oh kajitambulishe nyumbani... wewe?! Nilikutana na mmoja wa aina hii.... Halafu kuna wengine ndo wapuuzi kabisa... hawa wanajifanya ni wana maadili sana kumbe nao ni vicheche tu! unakuta wanakubania vijimambo ili kukushinikiza utangaze nia.

Unakuta couple zingine mara nyingi kama sio zote zinakutana hotelini au guest house...! Hapa hata kama mnaishi kama wapenzi kwa miaka kisha mkafunga ndoa bado hesabuni hamfahamiani! Mwanamke huwezi kumfahamu mwanaume vizuri bila kwenda kuishi nae kwake angalau kwa muda! Tena kuishi kwenyewe sio kule kwa kwenda weekend peke yake kwani hiyo haina tofauti na kukutana nae hotelini au guest!
 
Last edited by a moderator:
Kwa ushuzi huu aliousema Ndoa hataiweza. Tena akae mbali kabisa mana hajitambui. Hata huyo atakayezaa naye atapata shida sana na kujuta kwa sababu huyo mdada anaujua upande mmoja tu wa ndoa yaan raha. Upande wa pili wa ndoa yaani shida haujui. ktk mazingira haya ndoa yake haiwez kudumu. Nafikiri hastahili kuwa mzazi hata kwa bure.
 
Back
Top Bottom