Sina hamu ya kuendelea na mchakato wa ndoa tena

single father

Member
Oct 22, 2019
77
117
Za jioni wakuu,

Bila kupoteza muda kama kijana nilipata demu tukaenda sawa na process zote za ndoa ziko tayari bado mwezi mmoja tu ila cha ajabu kila nikimuona saa hivi naona hanivutii kabisa kila siku namtafutia sababu lakini anapangua maskini dada wa watu analia kila Siku sijui nimepatwa na nini wandugu sometimes sitamani hata kumuona ila hajanikosea kitu.

Naweza nisipende tu alivyo vaa nikachukia siku nzima. Akinisemesha najibu mbovu tu, kuna muda nahisi nimekosea kumchagua japo sioni udhaifu mkubwa wakutisha kwani nimehack sim yake sioni SMS mbovu wala maongezi mabaya ila ni hali tu imekuja ghafla tena mbaya zaidi baada ya kujitambulisha kwao.

NB mahusiano yana almost 2yrs

1622186734779.png

 
Sasa mbona sijaona sehemu ambapo inaonyesha huna tena hamu na tendo la ndoa kama heding yako inavyoeleza?

Ninachokiona ni kuwa umemchoka mdada wa watu. Yaani umemkinai.

Japo ni ngumu kwake, muambie akupe nafasi kwa sasa ujitafakari. Asiwe anakueleza juu ya mambo ya ndoa kwa muda.

Mungu amsaidie mdada wa watu akayapokee kwa njia ya kueleweka. Asiumie kulikopitiliza
 
Jipeni mapumziko ya mda, kila mtu afanye yake.

Kwa mda mtakao pendelea.

Ukiona hata humkumbuki unapokuwa mbali naye....basi unaweza kusitisha zoezi zima la ndoa.

Yawezekana ni kipindi cha mapito....hutokea kwenye mahusiano (kukinai mwenza bila sababu)
 
Atakua na historia mbayaaa hembu tuambie huko nyuma yaliyo mkuta huyo binti kiasi ukifikilia unaona hafai kuwa mkeo? Tukusaidie
 
Back
Top Bottom