Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,860
- 12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam RC Albert Chalamila, jana alitangaza kuwa mkoa wa Dar es salaam utakuwa katika operation ya kufanya usafi siku ya tar 24/01/2024, siku ambayo pia ilipangwa kufanyika maandamano ya chama cha upinzani nchini Chadema.
Watu wengi wamekuwa wakihisi kuwa huenda ratiba hiyo ya kufanya usafi imepangwa ili kuzima maandamano hayo ya Chadema yaliotangazwa kufanyika tarehe hiyo hiyo ya 24, mwezi wa kwanza na mwenyekiti wao taifa mh Freeman Mbowe. Kwa kawaida kwa vile vyombo vyote vya ulinzi na usalama vitashiriki katika operation hiyo ya usafi basi itakuwa ngumu chama hicho kuingia barabarani kuandamana, na ikitokea watu wakaingia kuandamana basi kila mtu anajua nini kitachotokea.
Sasa kutokana na swala hilo la maandamano kuingiliana na ratiba za dola, inasemekana viongozi wa Chadema ambao ndio walioandaa maandamano hayo wameamua kuja na plan B ili kumtoa mh Chalamila mtegoni.
Taarifa nilizopata kupitia kwa mtu wa ndani, na wa karibu wa chama hicho ambae hakutaka kutaja jina lake, ni kwamba mwenyekiti wa chama hicho taifa amepanga kuwaita watoto wake wote waliopo Marekani warudi mara moja nchini kuja kuungana na wazazi wao, pamoja na ndugu zao (wadogo zao na kaka zao) katika maandamano hayo, halikadhalika M/mwenyekiti mh Lisu nae amepanga kufanya hivyo kama Mbowe. Na yeye amepanga kuwaambia watoto wake warudi mara moja kidharura ili kuungana nao katika maandamano hayo kwa lengo la kuonesha mshikamano wao na wazazi wao.
Ikumbukwe kuwa watoto hao baadhi ni raia wa Marekani, lkn pia ikumbukwe kuwa maandamano hayo yamepangwa kuwa ni ya amani, hivyo kushiriki kwao hakutakuwa na athari yoyote kwa uraia wao.
Hii ni baada ya kuona watu wengi kuhofia kushiriki katika maandamano hayo ambayo wanasema yatakumbana na balaa lisilotabirika. Hivyo wao kama viongozi walioandaa maandamano, wameamua kuwa mbele ya maandamano hayo na familia zao hata kama raia wa kawaida hawatojitokeza.
Swali je hivi RC Chalamila akitaka kutumia nguvu siku hiyo, ataweza kuwagusa vigogo hao na familia zao, special wale ambao tayari ni raia wa Marekani?
Mwenye jibu aje ajibu.
Karibuni.