Simwelewi rafiki yangu anataka nini kwangu

Habari za kutwa waungwana,
Nina rafiki tumefahamiana miaka minne iliyopita, kufahamiana kwetu tulikutana kwenye sherehe na tulikaa viti vya karibu na tuliongea na kucheza mziki pamoja. Wakati sherehe ikiendelea nilianza kufikiria usafiri wa kunirudisha nyumbani, nilianza kumuuliza jinsi nitakavyopata tax, aliniuliza kuelelekea wapi? Hapo ndipo niligundua ni jirani yangu kabisa. Tulichukua tax moja, na baada ya pale tulibadilishana namba za simu.
Kesho yake alinipigia simu, alinialika niende kanisani kwao, nililipenda lile kanisa, niliendelea kusali pale kwa muda. Nilikuja kufahamu huyu kaka ni mlokole wa kufa mtu, mara nyingi ananipigia simu tunachat, mazungumzo mengi ni current affairs, dini, na mara nyingine ananipa offer za dinner.
Kuna wakati nilimwambia nitakwenda nyumbani kuwaona wazazi, aliniambia nisiondoke bila kumuaga, siku ninaondoka alikuja na bahasha nzito. Niliifungua nikiwa njiani, aliniwekea mpunga wakueleweka. Nilimtumia message ya asante, alinijibu asante na karibu. Nilivyorudi nilimfahamisha nimerudi basi. Hajawahi kunisimulia habari ya girl friend, wala hajanitongoza ni mwaka wa nne huu.
Simuelewi huyu rafiki yangu nisaidieni ndugu zangu.

Ni kaka yako katika bwana, sasa unataka akutongoze? Hii ndio miana mke eti ya kuoa? Yani mtu akiishi vizuri dunia inamshangaa, ulitaka akutongoze? Eti? Halafu akuoe? Akishakuoa ubadilike uanze kumtesa na mi X yako?
 
Jaribu kumuonesha kuwa unampenda na kumuhitaji ila husivuke mipaka
 
Kua karibu nae zaidi uwe unaanzisha conversation zitakazomfanya afunguke. Wanaume kama hao hata kama ni domo zege ila pia ni mwelewa, anaelewa anataka nini . Usimtege mpendwa ndio hapo itakua mwisho atajua ni shetani
 
Habari za kutwa waungwana,
Nina rafiki tumefahamiana miaka minne iliyopita, kufahamiana kwetu tulikutana kwenye sherehe na tulikaa viti vya karibu na tuliongea na kucheza mziki pamoja. Wakati sherehe ikiendelea nilianza kufikiria usafiri wa kunirudisha nyumbani, nilianza kumuuliza jinsi nitakavyopata tax, aliniuliza kuelelekea wapi? Hapo ndipo niligundua ni jirani yangu kabisa. Tulichukua tax moja, na baada ya pale tulibadilishana namba za simu.
Kesho yake alinipigia simu, alinialika niende kanisani kwao, nililipenda lile kanisa, niliendelea kusali pale kwa muda. Nilikuja kufahamu huyu kaka ni mlokole wa kufa mtu, mara nyingi ananipigia simu tunachat, mazungumzo mengi ni current affairs, dini, na mara nyingine ananipa offer za dinner.
Kuna wakati nilimwambia nitakwenda nyumbani kuwaona wazazi, aliniambia nisiondoke bila kumuaga, siku ninaondoka alikuja na bahasha nzito. Niliifungua nikiwa njiani, aliniwekea mpunga wakueleweka. Nilimtumia message ya asante, alinijibu asante na karibu. Nilivyorudi nilimfahamisha nimerudi basi. Hajawahi kunisimulia habari ya girl friend, wala hajanitongoza ni mwaka wa nne huu.
Simuelewi huyu rafiki yangu nisaidieni ndugu zangu.
Kipi tena usichokifahamu anakupenda kwa dhati kashindwa kukuambia anza wewe kumwambua unampenda anatoka ukanda upi wa tz.
 
WAHENGA WALINENA KUWA MAMBO MAZURI HAYATAKI HARAKA.......Kizazi hiki kinakosa mengi mazuri kwa kuwa na pupa hasa katika mambo yanayohitaji subira kidogo kama hayo......
Katika hali ya kawaida hakuna linalofanyika bure na bila ya sababu hasa katika nyakati za leo zilizojaa usheitani......huyo kijana kuna kitu amekiona kwako ambacho kipo tofauti kwa vijana wengine na ndicho kilichomvutia kwako.......amechukua muda mrefu kwa kuwa anataka ajue kuwa hicho alichokiona ni sehemu ya maisha yako ama unamuigizia...!!???

Na pia kuna uwezekano pia akawa ameweka watu wa kukumonitor nyendo zako bila ya wewe kujua.......
Kuendelea kuwa karibu na wewe kwa muda wote huo kuna maanisha kuwa hajaona kasoro au baya lolote kama alivyokusudia na inawezekana akawa amekaribia mwisho wa uchunguzi wake na anakaribia kufanya maamuzi mazito juu yako.....hivyo ninachokushauri ni kuwa jitahidi kuwa kama ulivyo siku zote tangu siku ile mliyokutana kamz kweli na wewe umeingia kwenye ulimwengu wake.........

Kuna baadhi ya mambo hayataki pupa wala papara....hata kwenye vifaa vyetu vya elektroniki pamoja na kusifika kufanya mambo kwa haraka lakini kuna muda vinakuwambia PLEASE WAIT.......

Muumba hajawahi kumpa shari au baya mtu mwenye subira kwa kuwa daima subira huvuta mambo mazuri......

Ridhki ya mtu ipo mikononi mwa mtu.....
 
Sio yeye anataka nini Bali Wewe ndio unataka nini kwake?kwa sababu yeye hajaonyesha kuhitaji kitu kwako Bali wewe Ndio unauliza.kuwa wazi tu
 
n
Habari za kutwa waungwana,
Nina rafiki tumefahamiana miaka minne iliyopita, kufahamiana kwetu tulikutana kwenye sherehe na tulikaa viti vya karibu na tuliongea na kucheza mziki pamoja. Wakati sherehe ikiendelea nilianza kufikiria usafiri wa kunirudisha nyumbani, nilianza kumuuliza jinsi nitakavyopata tax, aliniuliza kuelelekea wapi? Hapo ndipo niligundua ni jirani yangu kabisa. Tulichukua tax moja, na baada ya pale tulibadilishana namba za simu.
Kesho yake alinipigia simu, alinialika niende kanisani kwao, nililipenda lile kanisa, niliendelea kusali pale kwa muda. Nilikuja kufahamu huyu kaka ni mlokole wa kufa mtu, mara nyingi ananipigia simu tunachat, mazungumzo mengi ni current affairs, dini, na mara nyingine ananipa offer za dinner.
Kuna wakati nilimwambia nitakwenda nyumbani kuwaona wazazi, aliniambia nisiondoke bila kumuaga, siku ninaondoka alikuja na bahasha nzito. Niliifungua nikiwa njiani, aliniwekea mpunga wakueleweka. Nilimtumia message ya asante, alinijibu asante na karibu. Nilivyorudi nilimfahamisha nimerudi basi. Hajawahi kunisimulia habari ya girl friend, wala hajanitongoza ni mwaka wa nne huu.
Simuelewi huyu rafiki yangu nisaidieni ndugu zangu.
nilichopenda ni kuwa haujakana kama ndani ya miaka hiyo minne haujawai labuliwa nje ya urafiki wenu na huyo mlokole,inamaana unachomshangaa nikwamba hataki kukuomba unachowapa wengine.
 
Ninaogopa nikimueleza inaweza kuvunja urafiki wetu, jamaa ni mlokole, pili si elewi kama ndiye yeye niliyeletewa jamani mwaka wa nne huu sijui tunaelekea wapi. Pia hua ananipikia chakula nikiwa nimechoka, analeta kwenye hot pot.
Miaka minne mwone mwenzako huruma haya yote anayokufanyia umwelewi.Mwambie umefunuliwa.
 
Huko kupotezeana mda... Kama haweki bayana nia yake muulize tu. Unaweza tumia style ili usionekane too direct. Husije ukapoteza mda nae kumbe kwake wewe ni rafiki tu.
 
Ninaogopa nikimueleza inaweza kuvunja urafiki wetu, jamaa ni mlokole, pili si elewi kama ndiye yeye niliyeletewa jamani mwaka wa nne huu sijui tunaelekea wapi. Pia hua ananipikia chakula nikiwa nimechoka, analeta kwenye hot pot.
Hapo kamba tena..
 
Watu wengine wanausingizia tu ulokole! Kwani walokole hawatongozi? Wanapataje wake? We muulize tu. Sio lazima uwe direct bwana. Kua mbunifu. Utakuja shangaa anakupa kadi ya harusi!
 
On A Serious Note.
1. Jaribu kujiangalia kama kuna kitu au tabia fulani unayo ambayo unahisi mshkaji haipendi ila kwa heshima anashindwa kukuambia. Na ndio inamnyima kukugegeda/kukuoa. (Wanawake wa kisasa mnazo nyingi)

2. Angalia usije ukawa umeutafsiri wema wake tofauti

3. Pengine rafiki ako adui wa Makonda.
 
Hivi ni lazima akutongoze? Kama unampenda si umwambie tu?
 
Back
Top Bottom