Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,701
- 6,931
Habari za kutwa waungwana,
Nina rafiki tumefahamiana miaka minne iliyopita, kufahamiana kwetu tulikutana kwenye sherehe na tulikaa viti vya karibu na tuliongea na kucheza mziki pamoja. Wakati sherehe ikiendelea nilianza kufikiria usafiri wa kunirudisha nyumbani, nilianza kumuuliza jinsi nitakavyopata tax, aliniuliza kuelelekea wapi? Hapo ndipo niligundua ni jirani yangu kabisa. Tulichukua tax moja, na baada ya pale tulibadilishana namba za simu.
Kesho yake alinipigia simu, alinialika niende kanisani kwao, nililipenda lile kanisa, niliendelea kusali pale kwa muda. Nilikuja kufahamu huyu kaka ni mlokole wa kufa mtu, mara nyingi ananipigia simu tunachat, mazungumzo mengi ni current affairs, dini, na mara nyingine ananipa offer za dinner.
Kuna wakati nilimwambia nitakwenda nyumbani kuwaona wazazi, aliniambia nisiondoke bila kumuaga, siku ninaondoka alikuja na bahasha nzito. Niliifungua nikiwa njiani, aliniwekea mpunga wakueleweka. Nilimtumia message ya asante, alinijibu asante na karibu. Nilivyorudi nilimfahamisha nimerudi basi. Hajawahi kunisimulia habari ya girl friend, wala hajanitongoza ni mwaka wa nne huu.
Simuelewi huyu rafiki yangu nisaidieni ndugu zangu.
Wewe unaye miaka minne umwelewi sisi ndio tutaelewa kwa post yako moja tu ya leo. Halafu wewe ulitaka iweje? Utongozwe? Wewe umemsimulia ya boy friend wako? Soma nae Biblia mistari ya uzinzi mfano ile ya mke wa Pharaoh kmrukia Yusuph mtoto wa Yakobo. Mwalike kwako halafu piga khanga moja - liwe na liwalo! Halafu umempenda yeye au unafukuzia hiyo mibahasha yenye mifweza zaidi?!
Nijuwavyo mimi 'walokole' wengi wako kwenye maumivu mfano kuumwa na kadhalika. Halafu walokole gani wanasakata muziki ingawaje haujasema ni muziki upi lakini yawezekana ni wa Ali Kiba.
Halafu hizi tabia za mtu upo single unaenda kwenye sherehe zinazohitaji couples hazifai.
Hivi kumbe mwanamke akipewa dinner na mifweza ya nguvu basi naye anataka kulipa kwa kumlisha mwanaume 'natural apple'?
