Simulizi ya kusisimua

Simulizi ya kusisimua

SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 11

ILIPOISHIA

“Mwili na kichwa vimeondolewa.
Nafikiri vimezikwa uani”
nikaongezea maelezo.
“Tumekuta makaburi uani!” Polisi
mwingine akasema.
“”Kwenye hivi vyumba vingine
hamkukuta watu?” Koplo akauliza.
“Hakuna mtu humu ndani. Hii
nyumba iko tupu”
“Hebu twendeni tukayaone hayo
makaburi”
Tukaenda uani. Lile kaburi
nililoliona likichimbwa na yule
mwanamke lilikuwa limefukiwa.
Pembeni yake kulichimbwa kaburi
jingine lililokuwa wazi. Shepe
lilikuwa limeachwa kwenye chuguu
ya mchanga.
“Hili kaburi lililofukiwa ndilo
nililokuta linachimbwa. Bila shaka
mwili wa Sajenti Erick umezikwa
hapa” nikawambia wenzangu.
“Tulifukue tuone ndani” Koplo
akasema.
Lilikuwa wazo zuri.
“Lakini tusitumie hili shepe.
Tutaharibu alama za vidole za
aliyekuwa amelishika” Koplo
akatukumbusha.
“Tunaweza kulifukua hata kwa
mikono. Mchanga wenyewe bado
uko laini” nikawambia.
Bila kujua hatari ambayo ilikuwa
inatukabili, tulianza kulifukua
kaburi hilo kwa mikono.
SASA ENDELEA
Polisi watano nikiwemo na mimi
tuliendelea kulifukua kaburi hilo
kwa mikono. Koplo wetu alikuwa
amesimama na bunduki kuweka
ulinzi. Tulilifukua kaburi hilo hadi
likawa shimo, tukaingia ndani na
kuendelea kufukua.
Wakati tukiendelea kufukua huku
tukimwaga mchanga kwa juu
niliona kiatu cheusi, nikakishika na
kukivuta. Nikaona nimevuta mguu.
“Jamani nimeshika mguu!”
nikawambia wenzangu.
“Ni kweli hapa pamezikwa mtu,
hebu tufukue zaidi” Polisi mmoja
akatuambia.
Tukaendelea kufukua na hatimaye
kuupata mwili kamili usio na
kichwa. Mara moja niligundua
kuwa mwili huo ulikuwa wa Sajenti
Erick na ndio ule uliokuwa
ukining’inia kule chumbani..
“Huu hapa mwili wa Sajenti Erick”
nikawambia wenzangu ambao
walikuwa wameshituka na
kushikwa na mshangao.
“Kichwa chake kiko wapi?” Koplo
akauliza.
“Kichwa hakipo, nadhani
hawakukizika lakini nilikiona
kwenye lile boksi” nikasema.
“Sasa tutauthibitishaje kuwa ni
mwili wa Erick?” Koplo akauliza.
“Lakini unaonekana ni mwili wake
kweli, hili shati ndilo alilokuwa
amevaa jana” Polisi mmoja
akasema.
“Utoeni, tuuangalie vizuri” Koplo
akatuambia.
Tukaubeba na kuuweka juu ya
kaburi.
Koplo akautazama na kutuambia.
“Hata mimi naona ni Sajenti Erick,
hivi viatu ni vya kipolisi. Ngoja
nimfahamishe Inspekta aliyeko
kwenye zamu”
Kiplo alitoa simu akampigia
Inspekta aliyekuwa ameshika zamu
ya usiku ya kuongoza kituo.
“Afande tumefika hapa mahali,
tumeonana na Martin na
tumeukuta mwili wa Sajenti Erick
umezikwa lakini hauna kichwa”
Koplo huyo akazungumza kwenye
simu baada ya simu yake
kupokelewa.
“Hilo kaburi alilozikiwa liko wapi?”
Sauti kutoka upande wa pili wa
simu ikamuuliza.
“Liko uani mwa hii nyumba
tulioingia”
“Mmekamata watu wangapi humo
ndani?”
“Hatukukuta mtu yeyote”
Wakati Koplo huyo akisema hivyo
tulisikia mlango wa mbele wa
nyumba hiyo ukifunguliwa.
Tukamuona yule mwanamke na
binti yake Maimuna pamoja na yule
jini mwanaume wakiingia.
Maimuna na yule jini mwanaume
walikuwa wameshika mapanga.
Polisi wote waliokuwa hapo
walishituka. Walishituka si kwa
sababu tu ya kuwaona viumbe hao,
bali walishituka kwa kuona
maumbile waliyokuwa nayo.
Walikuwa na maumbile ya kijini
huku miguu yao ikiwa na kwato
nyeusi kama kwato za punda!
Koplo aliyekuwa akiongea kwenye
simu alikatiza mazungumzo yake
akaitia simu mfukoni na kuinua
bunduki. Polisi wengine pia
waliinua bunduki zao
kuwaelekezea majini hao.
“Majini wenyewe ndio hao
wanaokuja” nikawambia polisi hao
kwa mshituko. Kwa vile nilikuwa
nyuma nilisimama pale pale
nilipokuwa ili nijikinge kwa
wenzangu waliokuwa na bunduki.
“Simameni hapo hapo!” Koplo
aliwambia majini hao kwa sauti ya
amri.
Moyo ulikuwa ukinienda mbio.
Kwanza sikuziamini bunduki hizo
za polisi kama zingeweza
kuwatiisha majini hao lakini kwa
vile tulikuwa wengi nilipata
matumaini kidogo.
Majini hao hawakusimama,
waliendelea kuja uani kama vile
hawakusikia walichoambiwa.
“Nimewambia simameni hapo
hapo!” Koplo aliwaamuru tena
akiwa amewaelekezea bunduki.
“Afande tuwababue risasi kama
hawasikii” Polisi mmoja
akamwambia koplo huyo kama
kuwatisha majini hao.
“Nyinyi ni kina nani?” Maimuna
akauliza kwa sauti ya ukali huku
akiwatangulia wenzake.
“Sisi ni polisi” Koplo alimjibu.
Walikuwa wameshafika kwenye
mlango wa uani. Sasa walikuwa
wanavuka kizingiti ili watoke uani.
Koplo akafyatua risasi juu.
“Mtakufa nyote, simameni na
tupeni mapanga yenu!”
akawambia kwa sauti kali.
Yule mwanamke aliinua mkono na
kufanya kama anampiga kibao
koplo huyo lakini akiwa yuko mbali
naye. Hapo hapo koplo aliachia
bunduki akaanguka chini.
Hakuinuka tena. Mwanamke huyo
akageukia upande wetu akafanya
vile vile kwa polisi mwingine
ambaye naye alianguka.
Akaendelea kufanya hivyo hivyo
kwa kila polisi. Wote walianguka
na kila aliyeanguka hakuinuka
tena. Mimi nilikuwa wa mwisho.
Alinipitishia mkono kama
ananipiga kibao nikaona kama
dunia inazunguka. Macho yangu
yakafunga kiza. Nikaanguka hapo
hapo na kupoteza fahamu.
Nilipokuja kuzinduka kulikuwa
kumekucha. Kwanza nilianza kuona
miale ya jua ikipiga kwenye macho
yangu. Nikayafumba kisha
nikayafumbua tena. Nilikuwa
nikijiuliza niko wapi. Sikuweza
kuelewa mara moja. Pia macho
yangu hayakuweza kuona sawa
sawa kutokana na miale ya jua
iliyokuwa ikinipiga usoni.
Nikatulia na kuwaza. Nikakumbuka
kilichotokea. Nikainuka kwa haraka
na kuketi. Nilikuwa nimelala
kwenye tuta la mchanga wa kaburi
mahali palepale nilipoanguka.
Niliwaona polisi wenzangu
waliokuwa wamelala kama
nilivyokuwa nimelala mimi. Kila
mmoja alikuwa sehemu yake,
bunduki yake ikiwa pembeni.
Wakati ule nainuka, polisi hao nao
walianza kuinuka mmoja mmoja.
Walikuwa wamezinduka kama
mimi baada ya kupotewa na
fahamu kwa muda ambao
hatukuujua.
Jambo la ajabu tuliloliona ni kuwa
ile nyumba ya Maimuna haikuwepo
tena. Eneo lote lilikuwa makaburi
matupu. Lile kaburi la Sajenti Erick
ambalo tulilifukua lilikuwepo na
mwili wake ulikuwa juu ya kaburi
hilo kama tulivyouweka.
Gari la polisi tulilokwenda nalo
mahali hapo lilikuwepo. Pia
kulikuwa na gari jingine
lililokwenda na polisi wengine.
Polisi hao tuliwaona wamesimama
wakitutazama.
Kila mmoja wetu aliyeinuka
alikuwa akishangaa. Alishangaa
kwa jinsi tulivyokuwa tumepotewa
na fahamu na alishangaa kuona ile
nyumba haikuwepo tena na badala
yake kulikuwa na makaburi
matupu.
“Vipi?” Inspekta Amour ambaye
alikuwa mmoja wa polisi waliofika
alituuliza kwa mshangao.
Je nini kitatokea?
 
SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA

Sote tukasimama. Kila polisi
akachukua bunduki yake.
Tulishindwa hata kujibu, tukawa
tunatazamana.
“Vipi jamani, mbona mmelala
hapa” Inspekta Amour akatuuliza
tena.
Polisi mmoja akaeleza
kilichotutokea. Polisi hao waliokuja
wakashangaa.
Waliusogelea mwili wa Sajenti Erick
na kuutazama.
“Huyu ndiye Sajenti Erick” Amour
akasema baada ya kuutazama
mwili huo. Akaongeza.
“Sasa nini kilitokea?”
“Ni miujiza mitupu” nilijibu mimi.
“Hiyo nyumba imetowekaje?”
“Hatujui. Muda huu tunazinduka
tunaona nyumba haipo”
“Ilikuwa kwa wapi”
“Sisi tulikuwa uani mwa hiyo
nyumba. Lile gari tulilokuja nalo
lilikuwa mbele ya nyumba” polisi
mwingine alijibu.
SASA ENDELEA
“Kwa hiyo nyumba ilikuwa hapa
katikati?”
“Ndiyo. Ilikuwa kati ya sisi na lile
gari” nikajibu.
“Sasa wale watu mnaosema
mliwaona, wako wapi?”
“Hawapo tena, tumezinduka
hatuwaoni” koplo akajibu yeye.
“Walikuwa ni watu wa aina gani?”
“Wale si watu, wale ni majini”
nikasema na kuongeza.
“Wale ndio wamemuua Sajenti
Erick. Yule mwanamke ndiye
tuliyemkamata siku ile kwa
tuhuma za kukutwa na madawa ya
kulevya”
“Lakini yule mwanamke alikufa?”
Amour akasema.
“Kwa kweli tumemuona na ndiye
aliyetupungia mkono, sote
tukapotewa na fahamu” Koplo
akaeleza.
Inspekta Amour akaguna na kutupa
mcho huku na huku.
“Yule binti yake ambaye
aliwatoroka alikuwa pamoja
naye?” akatuuliza tena.
“Walikuwa wote pamoja na
mwenzao mwingine mwanaume”
nikasema.
Nilitupa macho chini nikayaona
yale magazeti ambayo
niliyachukua mle chumbani.
Nikainama na kuyachukua.
“Haya magazeti yana habari ya
yule mwanamke, niliyakuta katika
chumba alichochinjwa Erick”
Nilikunjua gazeti mojawapo
nikampa Inspekta Amour. Amour
alilichukua na kulitazama. Nilimpa
na lile gazeti jingine nalo
akalitazama.
“Itakuwa ni yeye kweli” alisema
baada ya kusoma vile vichwa vya
habari.
Pembeni na eneo hilo kuliwa na
watu wamesimama wakitutazama.
Inspekta Amour alimuita mtu
mmojawapo. Mtu huyo alikuja kwa
uoga akasimama kando ya
Inspekta Amour.
“Wewe ni mwenyeji wa eneo hili?”
Amour alimuuliza.
“Sisi tunaishi kule kando, hapa
tunapita njia tu” Mtu huyo alijibu
huku akionesha kuwa na wasiwasi
“Eti hapa mahali pana nyumba?”
“Hili ni eneo la makaburi tu, hakuna
nyumba” Mtu huyo akamjibu.
“Hujawahi kuona nyumba mahali
hapa jana au juzi?”
“Sijawahi kuona nyumba”
“Sisi tulikuta nyumba tulipokuja
usiku” Koplo akasema.
“Eneo hili ni la makaburi tu” Yule
mtu alisisitiza.
“Kwani jana usiku ulifika hapa?”
Amour aliendelea kumuuliza.
“Jana sikuwahi kufika, nilipita leo
alfajiri nikaona hawa polsi
wamelala hapa, nikaona na ule
mwili umekatwa kichwa…”
Alionesha mwili wa Sajenti Erick.
“Nani aliyepiga simu polisi?’
“Ni mimi. Nilipiga simu baada ya
kuwaona hawa polisi wamelala
hapa na pia ni baada ya kuona mtu
aliyekatwa kichwa”
Inspekta Amour akatutazama.
“Huu ni mkasa mzito, huyu mtu
tutamchukua kwa ajili ya ushahidi.
Sasa tukibebe hiki kiwiliwili
tukiingize kwenye gari”
Baada ya Inspekta Amour
kutuambia hivyo tulikibeba kile
kiwiliwili cha Sajenti Erick na
kukiingiza kwenye gari
tuliyokwenda nayo usiku.
“Tutarudi tena kwa ajili ya kulipiga
picha hili eneo” Inspekta Amour
akatuambia na kumuomba yule
mtu aliyemuita tuende naye polisi
ili akaandikishe maelezo yake na
kisha angerudishwa kwa gari la
polisi.
Baada ya hapo sote tulipanda
kwenye magari tukaondoka. Kwa
mbali nilihisi kichwa kikiniuma na
ile hofu ya usiku bado ilikuwa
ikitambaa kwenye mishipa yangu.
Nilijua nilipata hali hiyo kutokana
na kutolala usiku kucha pamoja na
lile taharuki la usiku. Lazima
kichwa kiume na lazima mwili
usisimke kwa hofu.
Tulifika kituo cha polisi tukashuka
kwenye gari. Tulimkuta kamanda
wa polisi na afisa upelelezi
wakitusubiri. Inspekta Amour
alikuwa amewapigia simu tukiwa
ndani ya gari.
Mara tu tuliposhuka kwenye gari,
maafisa hao walisogea kenye gari
lililokuwa na kiwiliwili cha Sajenti
Erick na kukitazama.
“Kichwa chake kiko wapi?”
Kamanda wa polisi akauliza.
“Kichwa chake hakikupatikana”
Inspekta Amour alimjibu.
Kamanda wa polisi akakunja uso.
“Kwani ilikuwaje? Hebu njoo huku
ndani utueleze”
“Martin twende” Inspekta
akaniambia.
Tukaingia ndani ya kituo. Kamanda
wa polisi alituita kwenye ofisi ya
mkuu wa kituo. Yeye na afisa
upelelezi walikaa. Sisi tukawa
wima.
“Hili tukio ni kubwa hebu tupeni
maelezo, nini kilitokea?” Kamanda
wa polisi akatuambia.
Inspekta Amour alieleza kwa
upande wake. Alieleza
nilivyompigia simu saa tisa usiku
na kuomba msaada wa polisi.
“Alituambia yuko Magomeni na
kwamba alitoroka kutoka katika
nyumba moja ambako aliukuta
mwili wa Sajenti Erick umekatwa
kichwa. Na kwamba yeye
mwenyewe pia amenusurika
kukatwa kichwa na bado hayuko
salama.
“Mimi baada ya kupata habari hii
nilipata hofu kidogo nikatuma gari
na askari sita muda ule ule. Ukapita
muda wa kama nusu saa hivi
Martin akanipigia simu tena
akaniambia lile gari la polisi
limempita, hawakumuona.
Nikawapigia kuwajulisha kuwa
wamempita Martin, warudi nyuma”
“Baada ya hapo kukawa kimya.
Nilijaribu kupiga simu tena
kuwaulizia lakini simu ikawa
haipokelewi. Ilipokuwa inakaribia
kuwa asubuhi mtu mmoja
alitupigia simu akatuambia
ameona polisi wamelala juu ya
makaburi na kuna mtu mmoja
amekatwa kichwa.
“Hapo nilichukua askari na gari na
kuelekea eneo la tukio.
Tulizunguka sana hadi tukafika
katika eneo hilo. Tuliwakuta askari
wamelala kwenye eneo la
makaburi na kiwiliwili cha Sajenti
Erick kipo hapo hapo”
Inspekta Amour aliendelea kueleza
jinsi walivyotuona tukizinduka na
kutuhoji maswali na sisi tukaeleza
kilichotutokea.
Je nini kitafuata? Usikose
 
SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 12

ILIPOISHIA

Baada ya kumaliza maelezo yake
ambayo yaliwashangaza maafisa
hao, kamanda wa polisi akataka na
mimi nieleze kilichotokea.
“Kwanza ulifikaje katika eneo hilo
na ulikuwa na Sajenti Erick au
ulikuwa peke yako?” akaniuliza.
“Nilikwenda peke yangu” nilimjibu.
“Kufuata nini?”
Niliona kama nitauma uma
maneno nitajikuta nikiwekwa
ndani, jambo la msingi ni kueleza
ukweli wote.
“Kuna msichana niliwasiliana naye
kwenye simu akataka nimfuate
katika eneo hilo”
“Ni nani?”
“Wakati tunawasiliana nilikuwa
simjui lakini baadaye niligundua
alikuwa ni yule msichana ambaye
mama yake tulimshitaki kwa
kukutwa na kete za madawa ya
kulevya na mama mwenyewe
akafia mahabusi”
“Umesema wakati mnawasiliana
ulikuwa humjui,?”
“Nilikuwa simjui”
“Uliwasiliana vipi na mtu ambaye
ulikuwa humjui?”
SASA ENDELEA.
Swali hilo lilinifanya nieleze ukweli
wa tukio zima la kuwasiliana na
Maimuna. Nilianzia pale alipokosea
namba akanitumia meseji.
Kamanda baada ya kunisikiliza
aliniuliza.
“Kwa hiyo ulipokuwa unakwenda
kuonana naye ulikuwa na
madhumuni gani?”
“Nilikuwa nataka tuwe marafiki, si
unajua afande mimi sina mke”
Nilipojibu hivyo Kamanda wa polisi
akamtazama Afisa upelelezi kisha
akaendelea kunihoji.
“Enhe, ulipofika hapo mahali
alipokwambia mkutane nini
kilitokea”
“Nilipofika pale sikumkuta,
nikampigia simu kumuuliza yuko
wapi”
“Ndiyo”
“Akanijibu kwamba yuko nyumbani
kwao hivyo nimfuate na
akanielekeza njia ya kufika
nyumbani kwao”
“Ukaenda?”
“Nikaenda. Njia yenyewe ni ya
kwenye mapori. Mahali kwenyewe
kuna nyumba moja moja na kuko
giza”
“Ulipofika?”
“Nilikutana naye njiani.
Akanipeleka kwenye hiyo nyumba.
Tuliingia ndani akanikaribisha
ukumbini halafu yeye aliondoka
akaniambia nimsubiri. Lakini kuna
kitu kimoja nataka kueleza”
“Eleza”
“Yule msichana nilimgundua kuwa
ni yule ambaye mama yake
alishitakiwa kwa kukutwa na
madawa ya kulevya hivi karibuni
akafia mahabusi. Nadhani
unakumbuka afande”
“Nakumbuka na niliambiwa
alikuwa na binti yake ambaye
aliwatoroka” Kamanda
alimwambia.
“Basi huyo binti ndiye huyo
msichana mwenyewe”
“Kwa hiyo hakushituka kukuona”
“Hakushituka”
“Na wewe hukumuuliza kitu?”
“Wakati kumbukumbu zinanijia
kujua ni yeye alikuwa
ameshaondoka na kuniacha peke
yangu pale ukumbini ambako
aliniambia nimsubiri”
“Alikwambia anakwenda wapi?”
“Hakuniambia. Basi pale pale
nilipitiwa na usingizi wa ghafla.
Nilipozinduka ilikuwa saa tisa
usiku. Yule msichana sikumuona…”
nikaendelea kueleza kilichotokea
baada ya hapo.
Kile kisa kiliwafanya maafisa hao
wa polisi watazamane kwa
mshangao.
“Una maana yule mwanamke
aliyekufa ulimkuta akiwa mzima
akichimba kaburi?” Afisa upelelezi
ndiye aliyeniuliza.
“Ndiyo. Mimi nilishangaa sana
kumuona” nikamjibu.
“Umetuambia kwamba watu hao ni
majini?” Kamanda akauliza.
“Ni majini. Hata wenzangu
waliokuja wameona kuwa ni
majini”
“Hivi majini ni imani tu au ni
viumbe kweli?”
“Kwa tukio hili mimi nimethibitisha
kwamba majini si imani, wapo!”
“Kwa hiyo majini ndio
wamemchinja Erick?’
“Ndio. Nafikiri ni kwa kisasi cha ile
kesi kwa sababu yeye na mimi ndio
tuliomkamata yule mwanamke”
“Kwa hiyo walikuwa wanataka
kukuchinja na wewe?”
“Ndiyo”
“Kwa vile kuna tukio la mauaji ya
polisi na kiserikali hatuamini
kuwepo majini, tutawachukulia
kuwa hao ni watu na inabidi tukio
zima lithibitishwe” Kamanda wa
polisi akaniambia kisha
akamtazama Afisa upelelezi.
“Itabidi tufike katika eneo hilo la
tukio, tupige picha pamoja na
kuchukua maelezo kwa watu wa
karibu na eneo hilo” Afisa upelelezi
akamwambia kamanda.
“Sawa, itabidi tufike”
“Kuna mtu mmoja tumekuja naye
kwa ajili ya kuandikisha maelezo”
Yule inspekta niliyekuwa naye
akasema.
“Ni nani?” Kamanda akamuuliza.
“Ni mwananchi tu mkazi wa jirani
na mahali palipotokea hilo tukio na
ndiye aliyetupigia simu kutujulisha
kuwa kuna polisi waliolala juu ya
makaburi”
“Hebu mlete hapa”
Inspekta alitoka na baada ya muda
kidogo alirudi akiwa na mtu huyo.
Aliwasalimia wale maafande kwa
uoga.
“Karibu sana” Kamanda
alimwambia ili kumtoa hofu.
“Asante” Mtu huyo alijibu.
“Hebu tueleze ulichokiona huko
Magomeni hadi ukapiga simu
polisi” Kamanda alimwambia.
“Niliona polisi wamelala juu ya
makaburi saa kumi na mbili
asubuhi wakati nakwenda shamba,
ndio nikapiga simu”
“Hao polisi walikuwa wamelalaje?”
Kamanda alimuuliza.
“Walikuwa wamelala usingizi
kabisa na walikuwa na bunduki”
“Hapo mahali ulipowaona palikuwa
na nyumba?”
“Hapana, lile ni eneo la makaburi
tu”
Kamanda wa polisi akanitazama
kabla ya kuuliza tena.
“Tumepata maelezo kwamba wale
askari waliingia kwenye nyumba,
wakazirai na walipozinduka
wakajiona wako juu ya makaburi
na ile nyumba hawakuiona tena”
“Inawezekana. Pale mahali
panatokea miujiza mara kwa mara.
Inasemekana pana majini”
“Wewe uliwahi kuwaona?”
“Mimi sijawahi kuwaona lakini
kuna mtu aliwahi kuona
mwanamke mrefu kama mnazi
amesimama pale usiku”
“Alipomuona nini kilitokea?”
“Yule mtu alikimbia na aliuporudi
tena akiwa na wenzake, huyo
mwanamke hawakumuona tena”
Je nini kitafuatia?
 
SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 13

ILIPOISHIA

Baada ya kumaliza maelezo yake
ambayo yaliwashangaza maafisa
hao, kamanda wa polisi akataka na
mimi nieleze kilichotokea.
“Kwanza ulifikaje katika eneo hilo
na ulikuwa na Sajenti Erick au
ulikuwa peke yako?” akaniuliza.
“Nilikwenda peke yangu” nilimjibu.
“Kufuata nini?”
Niliona kama nitauma uma
maneno nitajikuta nikiwekwa
ndani, jambo la msingi ni kueleza
ukweli wote.
“Kuna msichana niliwasiliana naye
kwenye simu akataka nimfuate
katika eneo hilo”
“Ni nani?”
“Wakati tunawasiliana nilikuwa
simjui lakini baadaye niligundua
alikuwa ni yule msichana ambaye
mama yake tulimshitaki kwa
kukutwa na kete za madawa ya
kulevya na mama mwenyewe
akafia mahabusi”
“Umesema wakati mnawasiliana
ulikuwa humjui,?”
“Nilikuwa simjui”
“Uliwasiliana vipi na mtu ambaye
ulikuwa humjui?”
SASA ENDELEA.
Swali hilo lilinifanya nieleze ukweli
wa tukio zima la kuwasiliana na
Maimuna. Nilianzia pale alipokosea
namba akanitumia meseji.
Kamanda baada ya kunisikiliza
aliniuliza.
“Kwa hiyo ulipokuwa unakwenda
kuonana naye ulikuwa na
madhumuni gani?”
“Nilikuwa nataka tuwe marafiki, si
unajua afande mimi sina mke”
Nilipojibu hivyo Kamanda wa polisi
akamtazama Afisa upelelezi kisha
akaendelea kunihoji.
“Enhe, ulipofika hapo mahali
alipokwambia mkutane nini
kilitokea”
“Nilipofika pale sikumkuta,
nikampigia simu kumuuliza yuko
wapi”
“Ndiyo”
“Akanijibu kwamba yuko nyumbani
kwao hivyo nimfuate na
akanielekeza njia ya kufika
nyumbani kwao”
“Ukaenda?”
“Nikaenda. Njia yenyewe ni ya
kwenye mapori. Mahali kwenyewe
kuna nyumba moja moja na kuko
giza”
“Ulipofika?”
“Nilikutana naye njiani.
Akanipeleka kwenye hiyo nyumba.
Tuliingia ndani akanikaribisha
ukumbini halafu yeye aliondoka
akaniambia nimsubiri. Lakini kuna
kitu kimoja nataka kueleza”
“Eleza”
“Yule msichana nilimgundua kuwa
ni yule ambaye mama yake
alishitakiwa kwa kukutwa na
madawa ya kulevya hivi karibuni
akafia mahabusi. Nadhani
unakumbuka afande”
“Nakumbuka na niliambiwa
alikuwa na binti yake ambaye
aliwatoroka” Kamanda
alimwambia.
“Basi huyo binti ndiye huyo
msichana mwenyewe”
“Kwa hiyo hakushituka kukuona”
“Hakushituka”
“Na wewe hukumuuliza kitu?”
“Wakati kumbukumbu zinanijia
kujua ni yeye alikuwa
ameshaondoka na kuniacha peke
yangu pale ukumbini ambako
aliniambia nimsubiri”
“Alikwambia anakwenda wapi?”
“Hakuniambia. Basi pale pale
nilipitiwa na usingizi wa ghafla.
Nilipozinduka ilikuwa saa tisa
usiku. Yule msichana sikumuona…”
nikaendelea kueleza kilichotokea
baada ya hapo.
Kile kisa kiliwafanya maafisa hao
wa polisi watazamane kwa
mshangao.
“Una maana yule mwanamke
aliyekufa ulimkuta akiwa mzima
akichimba kaburi?” Afisa upelelezi
ndiye aliyeniuliza.
“Ndiyo. Mimi nilishangaa sana
kumuona” nikamjibu.
“Umetuambia kwamba watu hao ni
majini?” Kamanda akauliza.
“Ni majini. Hata wenzangu
waliokuja wameona kuwa ni
majini”
“Hivi majini ni imani tu au ni
viumbe kweli?”
“Kwa tukio hili mimi nimethibitisha
kwamba majini si imani, wapo!”
“Kwa hiyo majini ndio
wamemchinja Erick?’
“Ndio. Nafikiri ni kwa kisasi cha ile
kesi kwa sababu yeye na mimi ndio
tuliomkamata yule mwanamke”
“Kwa hiyo walikuwa wanataka
kukuchinja na wewe?”
“Ndiyo”
“Kwa vile kuna tukio la mauaji ya
polisi na kiserikali hatuamini
kuwepo majini, tutawachukulia
kuwa hao ni watu na inabidi tukio
zima lithibitishwe” Kamanda wa
polisi akaniambia kisha
akamtazama Afisa upelelezi.
“Itabidi tufike katika eneo hilo la
tukio, tupige picha pamoja na
kuchukua maelezo kwa watu wa
karibu na eneo hilo” Afisa upelelezi
akamwambia kamanda.
“Sawa, itabidi tufike”
“Kuna mtu mmoja tumekuja naye
kwa ajili ya kuandikisha maelezo”
Yule inspekta niliyekuwa naye
akasema.
“Ni nani?” Kamanda akamuuliza.
“Ni mwananchi tu mkazi wa jirani
na mahali palipotokea hilo tukio na
ndiye aliyetupigia simu kutujulisha
kuwa kuna polisi waliolala juu ya
makaburi”
“Hebu mlete hapa”
Inspekta alitoka na baada ya muda
kidogo alirudi akiwa na mtu huyo.
Aliwasalimia wale maafande kwa
uoga.
“Karibu sana” Kamanda
alimwambia ili kumtoa hofu.
“Asante” Mtu huyo alijibu.
“Hebu tueleze ulichokiona huko
Magomeni hadi ukapiga simu
polisi” Kamanda alimwambia.
“Niliona polisi wamelala juu ya
makaburi saa kumi na mbili
asubuhi wakati nakwenda shamba,
ndio nikapiga simu”
“Hao polisi walikuwa wamelalaje?”
Kamanda alimuuliza.
“Walikuwa wamelala usingizi
kabisa na walikuwa na bunduki”
“Hapo mahali ulipowaona palikuwa
na nyumba?”
“Hapana, lile ni eneo la makaburi
tu”
Kamanda wa polisi akanitazama
kabla ya kuuliza tena.
“Tumepata maelezo kwamba wale
askari waliingia kwenye nyumba,
wakazirai na walipozinduka
wakajiona wako juu ya makaburi
na ile nyumba hawakuiona tena”
“Inawezekana. Pale mahali
panatokea miujiza mara kwa mara.
Inasemekana pana majini”
“Wewe uliwahi kuwaona?”
“Mimi sijawahi kuwaona lakini
kuna mtu aliwahi kuona
mwanamke mrefu kama mnazi
amesimama pale usiku”
“Alipomuona nini kilitokea?”
“Yule mtu alikimbia na aliuporudi
tena akiwa na wenzake, huyo
mwanamke hawakumuona tena”
Je nini kitafuatia?e
 
SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 14

ILIPOISHIA

Kamanda akanyamaza na
kututazama. Kikapita kimya kifupi
kabla ya kukitanzua kimya hicho.
“Sasa andikisha maelezo yake,
yatawekwa kwenye faili la
marehemu pamoja na maelezo
yenu nyote” Kamanda
akamwambia Inspekta na
kunigeukia mimi.
“Wewe utatupeleka katika hilo
eneo, tutachukua mpiga picha”
akaniambia.
Wakati Inspekta anachukua
maelezo ya yule mwananchi,
kamanda wa polisi na afisa
upelelezi walitoka nje ya kituo
wakakikagua tena kiwiliwili cha
Sajenti Erick kabla ya kuamuru
kipelekwe hospitali kwa uchunguzi
zaidi.
Baada ya hapo aliitwa mpiga picha
wa polisi. Dakika chache baadaye
kamanda wa polisi, afisa upelelezi,
mpiga picha wa polisi na mimi
tulikuwa kwenye gari tukielekea
katika eneo lilipotokea tukio.
Nikiwa ndani ya gari nilikuwa
nimeinamisha kichwa changu kwa
mawazo. Tukio hilo lilikuwa
limenitia fadhaa sana na sikujua
hatima yake ingekuwa nini.
Hofu yangu ilikuwa kuzuiwa likizo
yangu ambayo ningeianza siku
mbili tu kutoka siku ile.
SASA ENDELEA
Tulipofika katika lile eneo tulishuka
kwenye gari, nikawaonesha
maafande wangu mahali ilipokuwa
ile nyumba.
“Nyumba ilikuwa hapa”
niliwambia.
“Kwa sasa ndiyo imeyayuka?”
Kamanda akauliza.
“Ni kama imeyayuka afande kwa
maana tulipozinduka hatukuiona
tena”
“Na hilo kaburi lililokuwa na mwili
wa marehemu Erick ni lipi?”
Nikawaonesha kaburi hilo ambalo
lilikuwa wazi.
“Ni hili hapa”
Kamanda akamwambia mpiga
picha wa polisi apige picha eneo
hilo.
“Hili kaburi lilioko wazi utalipiga
picha peke yake” aliendelea
kumueleza.
Wakati mpiga picha huyo
akiendelea kufyatua picha., afisa
upelelezi alimwambia.
“Na hii sehemu inayodaiwa ilikuwa
nyumba usisahau kuipiga picha.
Jaribu kupiga picha nyingi zaidi
kwa sehemu tofautu tofauti”
Tuliwa tumesimama katika eneo
hilo huku kamanda wa polisi
akiendelea kunihoji na picha
zikiendelea kupigwa, watu
mmojammoja walianza kufika na
kutuangalia wakiwa wamesimama
kwa mbali.
Afisa upelelezi aliwaita wakasogea
karibu.
“Nyinyi ni wenyeji wa eneo hili?”
akawauliza.
“Ndio ni wenyeji wa eneo hili”
Kijana mmoja akamjibu.
“Nini kilitokea asubuhi hapa?”
“Palikuwa na polisi waliokuwa
wamelala juu ya makaburi”
“Wewe uliwaona?”
“Watu waliokuwa wakipita njia
wote waliwaona”
“Na labda mlijua polisi hao walilala
juu ya makaburi kwa sababu ya
nini?”
“Hatukujua lakini polisi wengine
walifika asubuhi wakawaona”
“Eti hili eneo lina historia gani?”
“Historia ya namna gani?”
“Inasemekana kuna miujiza
inatokea katika eneo hili ni kweli?
“Ni kweli. Siku nyingine ukipita
usiku hapa unakuta mambo ya
ajabu”
“Kama mambo gani?”
“Unaweza kukuta watu wamekaa
wanasoma wamevaa nguo nyepe
tupu au unaweza kukuta
mwanamke mrefu ananyonyesha
mtoto wake”
“Sasa nyinyi wenyeji wa hapa
mnayachukuliaje matukio kama
hayo?”
“Hapa mahali kwa kweli kuna
majini. Wale polisi tuliowakuta
wamelala hapa asubuhi bila shaka
walikumbwa na majini hao”
Mwanamke mmoja aliyekuwa
akisikiliza mazungumzo hayo
aliingilia.
“Pana jini anaitwa Maimuna na
mama yake anaitwa Fatuma. Kuna
siku wanaonekana lakini
hawadhuru mtu”
“Hao majini wanapatikana kwa
wapi?”
“Eneo lao ndilo hili hapa lakini
huwezi kuwaona mpaka usiku”
“Usiku ndio wanaonekana?”
“Mara moja moja wanaonekana”
“Sawa. Asante sana”
Afisa upelelezi akamgeukia
kamanda wa polisi.
“Kinachonishangaza mimi ni kuwa
maelezo ya polisi waliokuja huku ni
kwamba yule mwanamke
waliyemuona ni yule aliyekamatwa
na kete za madawa ya kulevya na
kufia mahabusi, sasa swali
ninalojiuliza muda wote je majini
wanafanya biashara ya madawa ya
kulevya?”
“Au si majini ni watu?” Kamanda
naye akauliza swali lake.
“Hapana ni majini kama
wanavyosema hawa wenyeji
wenyewe. Huyo Maimuna ndiye
yule msichana niliyewaeleza na
yule mwanamke alituambia jina
lake anaitwa Fatuma kama
alivyotueleza huyu msichana hapa”
nikasema.
“Kwa hiyo siku ile nyinyi mlikamata
majini?” Kamanda aliniuliza.
“Ndio, wale walikuwa majini”
nikasisitiza.
“Majini pia wanafanya biashara ya
madawa ya kulevya?’
Hapo sikuwa na jibu kwa sababu
yale madawa ya kulevya, Sajenti
Erick aliwabambikia tu.
“Itabidi tufanye uchunguzi wa
kuthibitisha kama ni kweli hao
majini ndio walikuwa wakazi wa
ile nyumba ya barabara ya nane
alipokamatwa yule mwanamke”
afisa upelelezi akasema.
“Sasa suala la msingi ni kutafuta ile
nyumba ni ya nani na kama
tutakuta watu mle ndani wahojiwe
ili watoe maelezo” Kamanda
akaongeza.
“Sisi tunachofahamu ni kuwa
wanaojenga nyumba au
kupangisha ni watu. Sasa kama
majini pia wanamiliki nyumba au
kupangisha tutakwenda kujua
vizuri” afisa upelelezi akasema.
Baada ya hapo tulirudi kwenye gari
tukaondoka. Kichwa changu
kilikuwa kimevurugika sana. Ile
kesi ilikuwa kama imenilemelea
mimi. Hoja za maafande wangu
zilikuwa zikinitibua mtima. Nikahisi
kama vile mwisho wa siku
nitakamatwa na kushitakiwa mimi.
Nilikuwa na hamu ya kuwaona
wazazi wangu na ndugu zangu
huko kwetu Kagera lakini likizo
yangu ilikuwa kwenye hatari ya
kufutwa kutokana na uchunguzi
huo.
Sikudhani kama polisi
wangeniruhusu niende likizo
wakati kulikuwa na tukio la
uchunguzi kama lile ambalo
lilikuwa linanihusu sana.
Kwa kweli nilifikia mahali nilijuta
kutaka kuanzisha uhusiano na yule
msichana ambaye sikuwa
nikimfahamu. Matokeo yake ndio
hayo ya kukumbwa na mkasa
ulioyatatanisha maisha yangu.
Nilijua kuwa kama polisi
watashindwa kuyathibitisha
maelezo yangu watanihusisha
mimi na mauaji ya Sajenti Erick. Na
kama nitahusishwa na mauaji hayo
ni wazi kuwa nitashitakiwa mimi
kwa kufunguliwa kesi ya mauaji.
Je nini kitaendelea? Usikose
kufuatilia
 
SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 15

ILIPOISHIA

Kwa uzoevu wa kipolisi niliokuwa
nao kesi za mauaji ya aina ile
uhusishwa na imani za kishirikina
na aghalabu ukipatikana na hatia
hukumu yake ni kunyongwa.
Nilikuwa bado kijana mdogo sana.
Nilikuwa sijaoa na wazazi wangu
walikuwa wakinitegemea. Kama
nitanyongwa litakuwa ni pigo kwa
familia yangu.
Tulirudi kituo cha polisi. Timu
nyingine ya polisi ikatakiwa
kwenda kwenye ile nyumba ya
barabara nane kujua kama mle
ndani kulikuwa na watu wanaoishi
na kama wamo watoe maelezo
kuhusiana na ile nyumba na
kuhusiana na yule mwanamke
aliyekuwa na duka la vitu vya
dhahabu.
Kwa bahati njema na mimi
niliingizwa katika msafara huo kwa
vile ndiye niliyekuwa nikiifahamu
vizuri nyumba ile kutoka siku ile
tuliyomkamata yule mwanamke.
Tulipofika katika nyumba hiyo, lile
duka lilikuwa bado limefungwa.
Kiongozi wa msafara wetu Meja
Elias alibisha mlango. Lakini
hatukupata jibu.
“Nadhani hakuna watu humu
ndani” akasema baada ya kubisha
sana.
“Tunaweza kuwauliza majirani
kuhusu wenyeji wa nyumba hii”
polisi mwingine akashauri.
SASA ENDELEA
Nyumba tuliyokuwa tunaifanyia
utafiti ilikuwa katikati ya nyumba
mbili. Tulikwenda katika nyumba
iliyokuwa upande wake wa kulia,
tukabisha mlango.
Mwanamke mmoja alitoka ndani
kuja kutusikiliza lakini alipoona
polisi uso wake ulinywea hapo
hapo.
“Habari ya saa hizi?” Meja Elias
alimsalimia.
“Nzuri. Karibuni” Mwanamke huyo
akatukaribisha bila uchangamfu.
“Samahani. Tuna tatizo kidogo.
Tunaomba msaada kutoka kwa
majirani wa nyumba hii” Meja
alimwambia.
“Msaada gani?”
“Tulitaka kujua hii nyumba ni ya
nani?” Meja alimuuliza
akimuonesha ile nyumba.
“Hiyo nyumba mwenyewe alikufa
zamani. Wakati huo sisi tulikuwa
wadogo. Hatumjui vizuri”
“Alikuwa ni nani?”
“Alikuwa ni bibi mmoja wa
kisomali”
“Hivi sasa wanaishi watu gani?”
“Kuna mama mmoja kama
muarabu hivi na binti yake ndio
waliokuwa wakiishi humo ndani
lakini siku hizi hatuwaoni tena”
“Huyo mama alikuwa amepangisha
au…?”
“Hapo hatujui”
“Kwa hiyo kwa sasa hivi hii
nyumba haikai watu?”
“Kwa mchana hatuoni watu
wanaoingia wala kutoka, inakuwa
kimya tu lakini ikifika usiku mwingi
tunasikia kama watu wamo ndani”
Meja alipojibiwa hivyo
akatutazama.
“Sasa nyinyi majirani mnaelewa
nini mnaposikia kama kuna watu
wakati wa usiku mwingi lakini
mchana hamuwaoni?” Meja
akaendelea kumuuliza yule
mwanamke.
“Hatuelewi kitu, hapa ni mjini
hatuchunguzani”
“Usiku wa jana mliwasikia hao
watu?”
“Ni kila siku usiku”
“Mnawasikia kuanzia saa ngapi?”
“Kuanzia saa nane usiku ndio sauti
zinaanza kusikika, zinaendelea hadi
saa kumi alfajiri”
“Mnahisi ni sauti za binaadamu
au…?”
“Ni za binaadamu”
“Labda tuseme wenyewe wanakuja
usiku na kuondoka alfajiri?”
“Labda”
Pakapita kimya kifupi kabla ya Meja
kumwambia yule mwanamke.
“Asante sana, kama tutakuwa na
maswali mengine tutakuja
kukuuliza”
“Haya karibuni”
Tukaondoka.
Tulipofika kituo cha polisi tukaanza
kufanya mchanganuo wa
mazungumzo yetu na yule
mwanamke. Polisi walibaini
kwamba ingawa wenyeji wa
nyumba ile hawakuwa
wakitambulika, kulikuwa na hali
isiyo ya kawaida kwa wenyeji hao.
Imani kuwa wenyeji hao
hawakuwa watu wa kawaida na
ndio wale waliotufanyia vitisho
kule Magomeni ilianza kuwaingia
polisi, hali ambayo kwa upande
wangu nilihisi ingeweza kunipatia
ahueni.
Kwa vile polisi ni chombo cha dola
na kunaendesha shughuli zake
kisheria ukawekwa mkakati
mwingine wa kwenda usiku katika
nyumba ile ili kuonana na hao
watu ambao sauti zao zinasikika
wakati wa usiku.
Tulipanga twende tukakae kando
kidogo kuanzia saa saba ili tuone
kama kutakuwa na watu wakiingia.
Ikifika saa nane tusogee karibu.
Kama tutazisikia hizo sauti tubishe
mlango.
Mkakati huo ulipokubalika
nikaambiwa kwamba naweza
kwenda kupumzika na nionekane
tena hapo kituoni kuanzia saa sita
usiku. Nikashukuru kuona
sikuwekwa ndani. Nilikuwa
nimechoka sana na nilikuwa na
usingizi. Akili yangu ilikuwa
haifanyi kazi kabisa.
Nikarudi nyumbani. Nilipoingia
chumbani kwangu kwanza nilikitoa
mvunguni kile kisanduku
kilichokuwa na mapambo ya
dhahabu, nikakifungua na
kukiangalia ndani. Nilipoona
dhahabu zilikuwemo, nikakifunga
na kukirudisha mvunguni.
Nilikwenda kuoga. Nilipotoka
bafuni nikajitupa kitandani. Ingawa
kichwa kilikuwa kizito kwa usingizi
lakini mawazo hayakunipa nafasi
ya kulala. Yale matukio ya majini si
tu yalinitia wasiwasi bali pia
yalinipa hofu ya kufungwa.
Nilihisi maisha yangu yalikuwa
hatarini kwa namna mbili. Kwanza
ni endapo wale majini wataendelea
kuniandama ili wanimalize kama
walivyommaliza Sajenti Erick. Na
pili ni endapo polisi wataamua
kunikamata mimi na kunishitaki
kuhusiana na mauaji ya Sajenti
huyo.
Mawazo hayo ndiyo
yaliyonikosesha usingizi japokuwa
sikuwa nimelala usiku kucha
uliopita nikiwa kwenye kizaa zaa
cha majini hao.
Nilisali, niliomba Mungu na
hatimaye usingizi ulinipitia bila
kujua. Wakati niko kwenye usingizi
niliota nikimuona Sajenti Erick
akichinjwa, mwili wake usio na
kichwa ukawa unanijia machoni
mwangu.
Picha ya kuchinjwa kwake ilinijia
kama sinema kwenye ndoto hiyo.
Alikuwa amefungwa kamba
mikono na miguu.
Yule mwanamke wa kijini alikuwa
amemshikia upanga akamuuliza.
“Kwanini mlituzushia kesi mimi na
mwanangu?”
Sajenti Erick hakuwa na la kusema
zaidi ya kuomba msamaha
aachiwe.
“Kisanduku changu cha dhahabu
kiko wapi?” Mwanamke aliendelea
kumuuliza.
“Sijachukua kisanduku” Erick alijibu.
“Unajua kafara lako ni nini?”
“Sijui”
“Ni kuchinjwa kama kuku, damu
yako itakuwa fidia yako”
Hapo hapo upanga ukapita kwenye
shingo ya Erick. Erick alianza
kukoroma na kutoa macho. Upanga
uliendelea kukeketa shingo yake
taratibu. Mkoromo wa Sajenti Erick
wakati anachinjwa ndio
ulioniamsha usingizini.
JE NINI KITATOKEA?
 
Cc topr njoo mama update story. Hii inatisha lakini. Huuuh! Mimi nimeiogopa lakini nimeshindwa kuiacha. Anzia ya kwanza kabisa huko.
 
Huwa sipendi hadithi ila naona kama nashawishika kuisoma yote
 
Cc topr njoo mama update story. Hii inatisha lakini. Huuuh! Mimi nimeiogopa lakini nimeshindwa kuiacha. Anzia ya kwanza kabisa huko.
mbona waanza niogopesha baba angu aya nambie inahabari ya majin nisiisome saiv kigiza chaanza ingia nisije teseka usiku wakati ww walala kwako wakoroma
 
mbona waanza niogopesha baba angu aya nambie inahabari ya majin nisiisome saiv kigiza chaanza ingia nisije teseka usiku wakati ww walala kwako wakoroma
Soma mapema Sana mama. Haitishi Sana. Ila ka muoga Sana kiza kikiingia nipigie simu nije nikupe kampan......
 
Soma mapema Sana mama. Haitishi Sana. Ila ka muoga Sana kiza kikiingia nipigie simu nije nikupe kampan......
Anza kuja tu baba maana kiza icho tayari njoo uwe unasoma kwanguvu me nasikiliza sieti ehhehh
 
Anza kuja tu baba maana kiza icho tayari njoo uwe unasoma kwanguvu me nasikiliza sieti ehhehh
Wapigie basi wale wanaokodisha spika na mike zake. Mimi nikija nafungulia spika tu naanza kukusomea kwa sauti. Fanya haraka
 
Wapigie basi wale wanaokodisha spika na mike zake. Mimi nikija nafungulia spika tu naanza kukusomea kwa sauti. Fanya haraka
unataka na majiran waisikie nn me nataka niisikilize peke angu bwana
 
unataka na majiran waisikie nn me nataka niisikilize peke angu bwana
Hahahaahaha! Unataka nikunong'oneze chumbani eeeegh! Sawa mama. Naja,ntakusimulia taratiiiiibu!
 
Hahahaahaha! Unataka nikunong'oneze chumbani eeeegh! Sawa mama. Naja,ntakusimulia taratiiiiibu!
Ivyo ndivyo sisi wazee tunavyo simuliana adithi njoo kizee chenzangu nakungoja apa barabaran
 
Back
Top Bottom