Simulizi ya kusisimua

  • Thread starter Kanungila Karim
  • Start date

Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
4,975
Likes
4,403
Points
280
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
4,975 4,403 280
SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 01
MWANZO
Uhamisho wangu wa kikazi kwenda
Tanga
ulikuja kama adhabu kutokana na
ukiukaji wangu wa maadili ya jeshi la polisi
nikiwa
muajiriwa wa jeshi hilo.
Nilijiunga na jeshi la polisi miaka mitano
iliyopita mara tu baada ya kuhitimu
kidato
cha sita huko Kagera ninakotoka.
Nilipomaliza mafunzo yangu ya upolisi
huko Moshi nilipangiwa kuanza kazi jijini
Dar. Mimi na wenzangu kumi na wanane
tuliuopangiwa kwenda Dar tulifurahi sana
na kujiona tulikuwa na bahati
kuchaguliwa kwenda Dar kwani wenzetu
wengi
walikuwa wakililia kupangiwa kazi katika
jiji
hilo.
Kituo changu cha kazi cha kwanza jijini
Dar, kilikuwa kituo cha polisi cha Ilala. Pale
nilipelekwa peke yangu. Wenzangu
walitawanywa katika vituo vingine
vilivyotapakaa sehemu mbalimbali za jiji.
Katika kipindi cha miaka minne ya
mwanzo nilifanya kazi kwa bidii na uaminifu
mkubwa. Kwa vile kazi yenyewe
niliipenda
niliifanya kwa kujituma na kwa weledi.
Mara
kadhaa nilisifiwa na wakuu wangu na
kutolewa mfano kwa wengine.
Siku moja mimi na polisi mwenzangu
tulitakiwa kusindikiza gari lililochukua
mishahara ya wafanyakazi wa kiwanda
cha
bia kutoka benki moja iliyokuwa barabara
ya Samora na kuipeleka kiwandani hapo.
Ilikuwa ni kawaida kila ifikapo mwisho wa
mwezi, mashirika ya serikali huomba
askari
kwa ajili ya kusindikiza mishahara ya
wafanyakazi kutoka benki. Ilikuwa ni nafasi
nzuri ambayo polisi
wadowadogo tulikuwa tunaigombania
kwa
sababu ilikuwa na posho kidogo. Siku
hiyo
nikapata bahati hiyo mimi na mwenzangu.
Tulipakiwa na gari ya kiwanda hicho
lililotufuata kituoni. Mimi na mwenzangu
kila
mmoja alikuwa na bunduki yake aina ya
SMG iliyokuwa na risasi tisini.
Tulipofika benki tulisubiri nje ya gari.
Sanduku la pesa lilipotolewa tulishika
bunduki zetu vizuri na kuangaza macho
kila
upande kuhakikisha usalama wa pesa hizo.
Sanduku hilo lilipopakiwa kwenye gari na
sisi tulijipakia. Gari likaondoka. Tulifika
kiwandani salama. Gari likasimama
kusubiri
kufunguliwa geti ili tuingie ndani ya eneo la
kiwanda.
Wakati askari anakwenda kutufungulia
geti,
gari moja likasimama ghafla ubavuni
mwa gari tulilokuwemo. Ndani ya gari hilo
mlikuwa na watu watano akiwemo
dereva.
Mara tu baada ya gari hilo kusimama
watu
wawili miongoni mwa watano
waliokuwemo ndani, walipenyeza mitutu
ya
bunduki kwenye madirisha na kuanza
kutushambulia kwa risasi za mfululizo.
Mimi na polisi mwenzangu tuliinama
chini. Risasi zilivunja vioo vya gari vya
ubavuni,
zikawa zinapita juu ya vichwa vyetu.
Maafisa
watatu wa kiwanda hicho waliokuwemo
ndani ya hilo gari walipoona
tunashambuliwa walifungua mlango wa
gari wa upande wa pili na kukimbia.
Baada ya maafisa hao kukimbia na
kuliacha
sanduku la pesa ndani ya gari, tulisikia
kimya halafu tukasikia hatua za watu
wakija mbio. Nikahisi walikuwa ni
majambazi
waliokuwa wakitushambulia , sasa
wanalifuata lile sanduku la pesa baada
ya
wenyewe kukimbia.
Hapo hapo nikatoa mdomo wa bunduki
kwenye dirisha na kuanza kufyatua risasi
mwenyewe nikiwa nimeinama.
Mwenzangu
naye alifyatua risasi lakini alikuwa
ameinua
kichwa chake, akapigwa risasi ya kichwa na
kufa pale pale.
Nilipomuona mwenzangu ameuawa
niliacha
kufyatua risasi nikatulia kimya. Nilikuwa
nimeinama chini ya dirisha ili watu hao
wasinione.
Majambazi hao walipoona hatujibu
mapigo
walijua kuwa wameshatuua. Tamaa ya
pesa
ikawafanya waharakishe kufungua mlango
wa gari wakiamini kuwa wameshazipata
pesa hizo.
Vile wanafungua tu mlango huo
walikutana
na mtutu wa bunduki. Niliwafyatulia risasi
majambazi wawili bila wao kutegemea
wakaanguka kando ya mlango wa gari.
Majambazi wengine wawili waliokuwa
nyuma yao walipoona wenzao
wameshambuliwa na risasi zilikuwa
zinaendelea kurindima waligeuka nyuma ili
wakimbie lakini hawakulifikia hata gari
lao
nikawalaza chini wote.
Jambazi mmoja aliyekuwa amebaki
kwenye gari kwenye siti ya dereva aliliondoa
gari
hilo kwa kasi kusalimisha maisha yake.
Sikutakakumkosa yule jambazi,
nikapituka
kwenye siti ya dereva amabayo ilikuwa
tupu. Gari hilo lilikuwa kwenye moto, nikatia
gea
na kulifukuza lile gari.
Wakati naliondoa gari hilo niliwakanyaga
majambazi wawili waliokuwa wamelala
chini na kuwatoa matumbo! Gari hilo
halikufika mbali nikaliingia
ubavuni.
Nililibana na kulibamiza
pembeni mwa barabara kisha nikalichota
na
kulipindua kichwa chini miguu juu, likawa
kama mende aliyekufa huku tairi zake
zikiendelea kuzunguka zenyewe.
Kulikuwa na gari la polisi lililokuwa
kwenye
doria. Polisi hao walipoona tukio hilo
walisimamisha gari. Na mimi nikashukuru
kwa kuona nimepata msaada. Nilishuka
kwenye gari nikaona gari jingine la
kiwanda
cha bia likisimama nyuma ya gari la
polisi.
Bila shaka gari hilo lilikuwa likitufuata
nyuma.
Polisi wanne walishuka kutoka gari la
polisi
na maafisa wanne walishuka kutoka gari
la
kiwanda cha bia, watatu walikuwa ni wale
tuliokwenda nao bemki. Nilijua kwamba
walikuwa wakifuatilia pesa zao.
Nikafungua
mlango wa gari nikalitoa lile sanduku la
pesa na kuwakabidhi. ITAENDELEA
 
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
4,975
Likes
4,403
Points
280
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
4,975 4,403 280
YALIYONIKUTA TANGA (2)ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITAMaafisa hao waliokuwa na nyuso zilizofadhaika walitabasamu walipoliona sanduku hilo likiwa salama na limefungwa kwa funguo kama lilivyokuwa lilipotoka benki.Baada ya kulipakia kwenye gari walilokuja nalo walinipa mikono ya pongezi na shukurani.“Tunakushukuru sana kwa ujasiri wako, umefanya kazi nzuri sana” Afisa mmoja akanimabia kwa furaha.Polisi wanne waliofika hapo waliniuliza kulikoni. Nikawaeleza mkasa uliotokea. Baada ya kupata maelezo yangu walimtoa yule jambazi aliyekuwa amebanwa ndani ya lile gari nililolipindua. Alikuwa hoi. Damu ilikuwa inamtoka puani na mdomoni.Hapo tukagawanyana kazi. Polisi wawili walisindikiza zile pesa kiwanda cha bia. Sisi wengine tulibaki pale pale tukiwasiliana na maafisa wetu.Dakika chache tu baadaye polisi na makachero kutoka makao ya polisi walitinga katika eneo hilo.Kila kachero na kila polisi aliyefika hapo alinipongeza kwa kazi nzuri, kuwaua majambazi wanne na kuokoa kiasi kikubwa cha pesa za mishahara ya wafanyakazi wa kiwanda cha bia. Baadye ilibainika kuwa pesa hizo zilikuwa zaidi ya shilingi milioni mia tatu.Majambazi niliowaua walipelekwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Muhimbili pamoja na yule polisi mwenzetu aliyeuawa. Jambazi aliyejeruhiwa baada ya kumpindua na gari naye alipelekwa kutibiwa katika hospitali hiyo hiyo akiwa chini ya ulinzi mkali.SASA ENDELEASiku ile ile niliitwa makao ya polisi. Niliambiwa kutokana na ujasiri niliouonesha wa kupambana na majambazi wanne na kuwaua na kuokoa pesa walizotaka kuzipora, nimehamishiwa katika idara ya upelelezi ya makosa ya jinai. Hivyo sitatumia tena sare za polisi bali nitakuwa nikivaa kiraia.Mbali na kuhamishiwa katika idara nyingine ya kazi nilihamishiwa pia katika kituo kingine cha kazi. Kutoka kituo cha polisi Ilala nilipelekwa makao ya polisi.Mabadiliko hayo yalinipa furaha na faraja na kwa upande wangu yalikuwa kama cheo kwani yalisogeza karibu na wakubwa.Nikiwa katika idara hii ya upelelezi makao ya polisi ndipo jeuri yangu ilipoanza.Pale nilikutana na makachero wenzangu vijana walionizidi kielimu. Tulikuwa tukivinjari katika mitaa ya jiji la Dar mchana kutwa.Tulikuwa katika vikundi vikundi. Siku tunakuwa wawili, siku nyingine tunakuwa watatu. Kilichonifurahishani kuwa kila mmoja wetu alikuwa amekabidhiwa bastolayake kwa ajili ya kukabiliana na tukio lolote la kiusalama.Nilipoanza kazi hii ya ukachero makao ya polisi nilibadilisha mavazi nikawa napendelea sana kuvaa koti. Watu wengi waliokuwa wananifahamu hawakujua ni kwanini nilikuwa sibandukani na koti. Wengi walidhani ni mbwembwe zangu. Lakini ukweli ni kuwa nilikuwa navaa koti ilikuficha bastola yangu na pia kupata urahisi wa kuitoa na kuitumia pale inapohitajika.Nilipata rafiki kachero mwenzangu aliyeitwa Shaali Shazume. Alikuwa Mzanzibari aliyehamishiwa Dar kutoka Unguja.Mimi na Shaali tulikuwa na tabia ya kutengeza kesi na kujipatia rushwa mara nyingi.Lakini siku moja taarifa zetu zikatua kwenye mez ya mkuu wetu. Akatuita na kutuambia kuwa alikuwa amepata ushahidi juu ya tabia yetu ya kuwatengezea watu kesi na kula rushwa. Kutengeza kesi kulimaanisha kumbambikia mtu kesi.Mimi na Shaali tulizikana tuhuma hizo na tukatolewa ushahidi ambao pia tuliukana kwa kudai kuwa ulikuwa ushahidi wa uongo.Kukana kwetu kulitusaidia tusifukuzwe kazi lakini mimi na Shaali tukatenganishwa. Mimi nilihamishiwa mkoa wa Tanga na Shaali akapelekwa Tanga.Sikuwahi kufika katika mkoa huo kabla ya hapo isipokuwa nilikuwa nikiusikia sifa zake. Na nilipoambiwa ninakwenda Tanga nilifurahi.Nilifanya kazi Tanga kwa takribani mwaka mmoja. Nikagundua kuwa mkoa huo ulikuwa na watu wakarimu sana na pia ulikuwa na wasichana warembo sana.Haukuwa mkoa wenye hekaheka kama ilivyo mikoa mengine ambapo polisin wanakuwa na mchakamchaka mchana wakati wote. Kusema kweli nilipokuwa Tanga nilitulia.Kwenye kituo nilichokuwa nafanya kazi kulikuwa na sajenti mmoja ambaye alikuwa mtu wa nyumbani. Alisoma na kaka yangu Kagera.Alikuwa ni sajenti Erick. Kachero huyo licha ya kunipenda alinichukulia kama mdogo wake. Mara nyingi alikuwa akinipa upendeleo wa kikazi. Siku za mapumziko nilikuwa namtembelea nyumbani kwake ambapo huzungumza na kukumbushana matukio ya kwetu Kagera.Sikuwa nikijua kuwa nilikuwa namtengeza Shaali mwingine badala ya yule niliyekuwa naye Dar kwani baada ya miezi michache tu yalitufika makubwa.Kuna siku nilikuwa kwenye mizunguko yangu ya kikazi. Sajenti Erick akanipigia simu. Nilishituka nilipoonanamba yake kwa sababu hakuwa na kawaida ya kunipigia simu.“Shikamoo afande” nilimuamkia ,mara tu nilipopokea simu yake.“Marahaba Martin. Uko wapi muda huu?” akaniuliza kwenye simu. Martin ndio jina langu. Jina langu kamili ni Martin Philip Lazaro.“Niko eneo la stendi ya mabasi” nikamjibu.“Kuna nini huko?”“Naangaza kwenye mabasi yanayotoka Mombasa. Naweza kushika mirungi”“Sasa umefanikiwa?”“Hakuna kitu, nataka kurudi kituoni”“Hebu njoo hapa hoteli ya Mtendele”Mtendele ni hoteli moja maarufu iliyoko eneo la Chuda.“Wewe uko hapo?”Sikutaka kumuuliza kuna nini. Nilikodi bodaboda ikanipeleka Mtendele. Nilipoingia nilimkuta Erick akinywa bia.Kiumri alikuwa amenizidi kwa miaka isiyopungua minane.“Kaa hapo” akaniambia akinionesha kiti kilichokuwa kwenye meza aliyoketi.“Najua huna pesa, nataka nikupe kazi lakini uwe ngangari” akaniambia mara tu nilipoketi kwenye kiti hicho“Sawa”“Nimepata taarifa moja, kuna mama mmoja na binti yake wana duka la vitu vya dhahabu na mapambo ya wanawake pale barabara ya nane kwa barabara ya jamaa”“Ana nini huyo mama?” nikamuuliza.“Nataka twende tukapekue nyumbani kwake, nimesikia anajishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya. Lile duka ni danganya toto tu”“Sawa. Twende tukafanye hiyo kazi”“Ngoja nimalize bia yangu twende”“Si itabidi twende kituoni tukaandike hati ya upekuzi”“Hapana, twende hivi hivi tu. Si kila kitu kinahitaji hati ya upekuzi. Kwanza watu wenyewe ni wanawake, hawajui sheria yoyote”“Sawa”Erick akamaliza bia yake na kuinuka.“Twenzetu”Tulitoka hapo hotelini. Erick alikodi teksi ikatupeleka barabara ya nane katika hiyo nyumba.Ilikuwa nyumba ya kizamani iliyojengwa kwa mawe lakini ilipigwa lipu na kupakwa chokaa. Ilikuwa na mlango mmoja wa duka lakini kwa muda ule tuliokwenda duka hilo lilikuwa limefungwa.Je nini kitatokea?
 
Eddy Love

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Messages
13,152
Likes
6,635
Points
280
Age
29
Eddy Love

Eddy Love

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2011
13,152 6,635 280
mlete complete
 
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
4,975
Likes
4,403
Points
280
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
4,975 4,403 280
baadae kidogo
 
y-n

y-n

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
1,881
Likes
760
Points
280
Age
32
y-n

y-n

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
1,881 760 280
Ni kisa cha ukweli au kama vya shigongo?
Ni nzuri na nadhani ina mafunzo mengi zaidi ya haya
 
Polisi jamii

Polisi jamii

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Messages
2,527
Likes
1,106
Points
280
Polisi jamii

Polisi jamii

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2013
2,527 1,106 280
Polisi jamii
 
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
4,975
Likes
4,403
Points
280
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
4,975 4,403 280
SIMULIZI : YALIYONIKUTA TANGA
MSIMULIAJI : MARTIN MEKU
MAHALI : TANGA
SEHEMU YA 03


ILIPOISHIA

Tulikwenda kwenye mlango, Erick
akabisha mlango huo na punde tu
ukafunguliwa na msichana
aliyeonekana kama msomali.
Alikuwa mweupe na mwembamba
kiasi. Alipotuona alishituka na
kutuambia.
“Assalam alaykum”
Erick ambaye alikuwa amezoea
salaam hizo za kipwani ndiye
aliyemuitikia.
Nilidhani afande Erick angemuulizia
mwenye nyumba lakinihakufanya
hivyo, alitoa kitambulisho chake
akamuonesha yule msichana.
“Sisi ni polisi wa upelelezi kutoka
jeshi la polisi. Tumepata taarifa
kuwa humu ndani mnauza
madawa ya kulevya. Je ni kweli?”
Msichana aliposikia hivyo
alishituka.
“Si kweli” akajibu kwa kubabaika.
“Sawa. Sasa kilichotuleta hapa ni
kufanya upekuzi katika nyumba
hii”
“Ngoja nimuite mama”
Aliposema hivyo mwanamke
mmoja mzee akatokea nyuma
yake.
“Mnataka nini?” akatuuliza. Kidogo
alikuwa na lafidhi ya kiarabu.
SASA ENDELEA
Erick akamueleza kazi yetu na
kusudio lililotuleta kwenye
nyumba ile.
“Karibuni” mwanamke huyo
akatuambia.
Tukaingia ndani.
“Sisi hatufanyi biashara hiyo na
wala hatuijui. Sisi tunauza
mapambo ya wanawake tu”
Mwanamke huyo akatuambia
tulipokuwa ndani.
“Tumepata taarifa ya kuaminika
kuwa mnauza madawa ya kulevya,
kwa hiyo tunataka tufanye upekuzi
humu ndani” Erick akamwambia.
“Sawa. Fanyeni upekuzi wenu. Sisi
hatuwezi kuwazuia. Lakini kuingilia
faragha ya mtu si jambo zuri”
Tukaanza kufanya upekuzi wetu
bila kuwepo na shahidi wala
mwenyekiti wa mtaa. Tulianza
kupekua kwenye lile duka. Kisha
tukaendelea kwenye vyumba
vingine. Tulipoingia chumbani kwa
yule binti nilimuona Erick akitoa
kitu kwa siri mfukoni mwake kisha
akainama chini ya kitanda.
Aliponyanyuka alionyesha kile kitu
alichokitoa mfukoni mwake,
akauliza.
“Hiki ni nini?”
Erick alikuwa ameshika kete tatu za
madawa ya kulevya. Alikuwa
amemtumbulia macho yule
mwanamke.
“Nimekuuliza hiki nini?”
“Sisi tutajuaje? Kitu umekishika
wewe halafu unatuuliza sisi,
hatuwezi kujua” Yule mwanamke
alimjibu.
Erick alijifanya ananusa zile kete
kisha akaniambia.
“Ni kete za madawa ya kulevya.
Ndiyo haya tuliyokuwa
tunayatafuta”
“Zinaonekana kuwa ni kete kweli”
nikamkubalia.
“Hebu nusa”
Alinisogezea kete hizo kwenye pua
yangu. Nikazinusa.
“Ni kokeni yenyewe!” nikasema na
kuongeza. “Kweli sasa nimeamini
hawa watu wanafanya biashara ya
madawa ya kulevya”
Ilikuwa kama nimemchochea Erick.
Akamtazama yule mwanamke kwa
macho makali.
“Mama ulikuwa unakataa?
Tumekuta kete hizi za madawa ya
kulevya chini ya kitanda cha binti
yako!”
Mwanamke huyo na binti yake
walibaki kushangaa.
“Kete za madawa ya kulevya ndio
nini?” Mwanamke huyo akauliza.
Binti yake akabetua mabega.
“Sijui”
“Bila shaka kutakuwa na kete
nyingi humu ndani. Ngoja
tuendelee kupekua” Erick akasema.
Tuliingia katika chumba kingine
ambacho kilikuwa ni cha yule
mwanamke. Katika kupekua
tulikuta kisanduku cha shaba
kilichowekwa ndani ya kabati.
Tulipokifungua tulikuta kimejaa
mapambo ya dhahabu.
“Mmepata wapi dhahabu hii?” Erick
akawauliza.
“Sisi tunafanya biashara ya
dhahabu” Yule binti akamjibu.
“Hii pia itakuwa mali iliyopatikana
kwa njia ya haramu!”
“Hapana, tunanunua kihalali”
Msichana ndiye aliyekuwa akisema.
Yule mwanamke alionekana kama
amepandwa na presha.
“Mtakwenda kujieleza vizuri polisi”
“Mnataka kutupeleka polisi?” Yule
mwanamke aliyekuwa kimya sasa
aligutuka na kuuliza.
“Kama hamtaki kwenda polisi
tunaweza kuzungumza na
kuyamaliza hapa hapa. Hii kesi ni
kubwa sana”
“Huyu mama pia hataweza
kifungo” Na mimi nikasisitiza.
“Sasa mnataka tuzungumze nini?”
Mwanamke huyo akatuuliza.
“Hujui? Utatupa kiasi gani ili
tukuachie?”
“Mimi siwezi kutoa rushwa kwa
sababu hatujafanya kosa lolote”
Maneno yale yalimuudhi Erick.
Nikaona uso wake umebadilika.
“Hamjafanya kosa lolote, si ndio…?”
akasema huku akitoa simu. Hapo
hapo akawapigia polisi wenzetu
waliokuwa kituoni. Aliwaeleza
kilichotokea na kwamba alikuwa
anahitaji gari.
Je nini kitaendelea? Usikose
kuendelea na hadithi hii hapo
kesho.
 
Moisemusajiografii

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2013
Messages
9,892
Likes
8,396
Points
280
Moisemusajiografii

Moisemusajiografii

JF-Expert Member
Joined Nov 3, 2013
9,892 8,396 280
Simulizi ni nzuri ila sidhani kama Baba Nyangeta ataifurahia. Kwa sababu nyama inaanikwa kwenye kamba na panya ni wengi mnoo!
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,755
Likes
49,642
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,755 49,642 280
Hadithi za alfu lela ulela
 
2011996bd

2011996bd

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2016
Messages
271
Likes
95
Points
45
Age
21
2011996bd

2011996bd

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2016
271 95 45
Aaaaaaa em jaribu kuiandika complete
 
A

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
528
Likes
439
Points
80
A

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2012
528 439 80
simuliz nzur mwandishi iweke yote hapa
 
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
4,975
Likes
4,403
Points
280
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
4,975 4,403 280
YALIYONIKUTA TANGA (4)
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
“Ngojeni gari ije twende kituoni ndipo mtakapojua kosa lenu” Erick aliwambia baada ya kuhakikishiwa kuwa gari la polisi linatufuata.
Yule binti alitutoroka pale pale na kupotea. Tukabaki na yule mwanamke.
“Binti yako ametukimbia lakini tutamtafuta” Erick alimwambia yule mwanamke polisi wenzetu walipofika.
Tulimtoa yule mama, tukamwambia afunge mlango wake. Alipofunga mlango wa nyumba yake, funguo zake nilizichukua mimi. Tukampakia kwenye gari la polisi na kwenda naye kituoni.
Wakati mwanamke huyo anahojiwa ndani ya kituo cha polisi, mimi nilitoka nikakodi bodaboda na kurudi nyumbani kwake. Kile kisanduku cha dhahabu kilikuwa kimenitoa roho na Erick alikiacha baada ya kuona ilikuwa mali halali ya yule mwanamke.
Nilifungua mlango wa nyumba yake kwa kutumia zile funguo ambazo nilikuwa nazo mfukoni. Nikaingia ndani. Nilikichukua kile kisanduku cha dhahabu nikakifunga na kitambaa cheupe nilichokikuta mle chumbani kisha nikatoka. Nilipotoka nilikodi teksi ikanipeleka nyumbani kwangu Msambweni ambako kulikuwa na nyumba za polisi.
SASA ENDELEA
Nlipofika nyumbani kwangu, niliingia ndani. Nilikificha kile kisanduku chini ya mvungu wa kitanda changu kisha nikatoka tena na kurudi na ileteksi kituo cha polisi. Zile funguo zanyumba ya yule mwanamke nilizikabidhi kwa Sajenti Erick.
“Nilizisahau mfukoni mwangu” nikamwambia.
Erick alizichukua nakwenda kuzihifadhi kwenye kabati.
Yule mwanamke alikuwa amehojiwa na baadaye kupelekwa rumande. Niliambiwa alikuwa amekanusha kuhusika na zile kete za madawa ya kulevya. Polisi walikuwa katika pilikapilika za kuandaa mashitaka yake ili kesho yake afikishwe mahakamani.
Kusema kweli kukamatwa kwa yule mwanamke hakukuwa halali Sajenti Erick alikuwa ameweka mtego wake apate pesa kwa njia ya kumtisha yule mwanamke lakini mwanamke mwenyewe hakutishika na akawa tayari ashitakiwe kwa kosa la kukutwa na kete za madawa ya kulevya ambazo alizikana.
Siku iliyofuata mwanamke huyo akafikishwa mahakamani. Alisomewa shitaka la kukutwa na kete tatu za madawa ya kulevya, akakana shitaka hilo. Kesi ikaahirishwa nay eye akarudishwa rumande kwa kukosa mdhamini.
Niliusifu sana ujasiri wa Sajenti Erick, kumfungulia kesi mwanamke huyo mzee huku akijua fika kwamba hakuwa na hatia. Zilikuwa ni chuki za kutopata pesa alizotaka kutoka kwa mwanamke huyo.
Na hata kama angebadili mawazo yake, asingeweza kumuachia kwa sababu mtuhumiwa tayari alishafikishwa kituo cha polisi. Mambo hayoyalitakiwa yamalizikie kule kule nyumbani kwa yule mama.
Polisi hawakushughulika tena kumtafuta yule msichana aliyetoroka, wakamng’ang’ani yule mama. Siku ile ambayo alifikishwa mahakamani siku iliyofuata akakutwa ameshakufa.
Maiti yake ilikutwa asubuhi. Ikachukuliwa na kupelekwa hospitali. Sajenti Erick akapata kazi ya kuwatafuta jamaa zake bila mafanikio. Majirani wa yule mama walimwambia Erick kwamba hawawajui jamaa zake. Walikuwa wakimuona yeye na yule binti aliyekuwa naye ambaye alikuwa ametoweka tangu siku alipokamatwa yule mama.
Kesi yake ikafutwa mahakamani. Na baada ya kutojitokeza kwa jamaa yake yeyote, maiti ya mwanamke huyo ikazikwa na manispaa. Tukio lile tukalisahau.
Zikapita siku kadhaa. Kile kisanduku cha dhahabu kilikuwa bado kipo mvunguni mwa kitanda changu. Sikutaka kuziuza haraka haraka zile dhahabu. Nilikuwa nikisubiri muda upite na tukio lisahaulike kabisa.
Siku moja asubuhi wakati natoka nyumbani kwangu naenda kazini simu yangu iliingia meseji. Nilipoisoma ilisema.
“Sitalisahau penzi lako”
Namba iliyotuma meseji hiyo nilikuwa siifahamu. Na mimi nikatuma meseji ya kuuliza.
“Wewe nani?”
Baadaye likaja jibu likisema.
“Samahani, nimekosea namba”
Ile namba nikaizingatia. Jioni nilipotoka kazini nikaipiga. Simu yangu ikapokelewa na msichana.
“We nani?” akaniuliza.
“Mimi ni yule uliyenitumia meseji asubuhi” nikamwambia.
“Ahaa samahani, nilikosea namba”
“Ulikuwa unamtumia mpenzi wako?” nikamuuliza.
“Ndiyo” akanijibu.
“Nilijua kuwa ulikosea namba lakini nilipenda tu kukufahamu, uko wapi?”
“Mimi?”
“Wewe ndiyo”
“Niko Magomeni”
Magomeni ni eneo lilioko pembeni kidogo mwa mji huo. Wakati huo viwanja ndio vilikuwa vinatolewa na watu kuanza ujenzi wa nyumba.
“Unafnyaje huko?” nikamuuliza baada ya kukosa la kumwambia.
“Ndiko ninakoishi”
“Nataka nije nikuone”
“Kwa ajili gani?”
“Tujuane tu”
“Kwa lini?”
“Kwa leo”
“Haitakuwa rahisi”
“Kwanini…”
Alikuwa ameshakata simu. Nikampigia tena lakini simu yake ikawa haipatikani. Nikaachana naye.
Jioni ya siku ya pili yake nikampigia tena. Simu yake ikawa inaita. Iliita kwa muda mrefu kasha ikapokelewa.
“Hallow!” Sauti yake laini ikasikika kwenye simu.
“Hujambo?” nikamuuliza.
“Sijambo”
“Habari ya tangu jana?”
“Ahaa… wewe ndio yule jamaa wa jana?”
“Ndiye mimi. Nimekumiss…”
“Kumbe wewe uko Tanga?”
ITAENDELEA
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
22,755
Likes
49,642
Points
280
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
22,755 49,642 280
Inaingia episode 5
 
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
4,975
Likes
4,403
Points
280
Age
22
Kanungila Karim

Kanungila Karim

Verified Member
Joined Apr 29, 2016
4,975 4,403 280
YALIYONIKUTA TANGA (5)
ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA
“Unafanya kazi gani?” Msichana akaniuliza.
Niliona nisimueleze ukweli kwani watu wengi huwaogopa polisi na makachero.
“Mimi ni afisa ardhi”
“Afisa ardhi unagawa viwanja?”
“Ni moja ya kazi zangu. Sasa naweza kuja kukuona?’
“Kwani unataka nini?”
“Kujuana na wewe”
“Tukishajuana iweje?”
Nikajidai kucheka.
“Mbona unacheka?” Msichana akawahi kuniuliza.
“Unanifurahisha sana. Kwani hupendi tukiwa marafiki?’
“Wewe unapenda kuwa rafiki na mtu ambaye humjui?”
SASA ENDELEA
“Ndiyo sababu nikataka tuonane tujuane”
Baada ya kimya kifupi msichana akaniambia.
“Usiwe na haraka, subiri kwanza”
“Hadi lini?”
“Nitakwambia. Sawa?”
“Inabidi nikubali kwa shingo upande”
“Mwanaume wewe wa ajabu sana!” Msichana akaniambia kisha akakata simu. Sikujua alikuwa na maana gani kuniambia hivyo.
Ikapita karibu wiki nzima bila kuwa na mawasiliano na msichana huyo. Si tu nilikuwa nimetingwa na kazi pia simu ya msichana huyo ilikuwa haipatikani. Ilikuwa imezimwa kabisa. Mpaka nikafikiria kuwa alikuwa amebadili namba.
Nilijaribu kumpigia mara kadhaa. Nilipoona sipati jibu nikaacha kumpigia. Baada ya kupita wiki moja nilikuwa nikichaji simu yangu. Ilikuwa jioni na ndio kwanza nilirudi kutoka kazini. Kwa kawaida ninapochaji simu yangu huwa naizima.
Nilianza kuichaji kutoka saa kumi na mbili jioni hadi saa tatu usiku nilipoiwasha. Simu yangu ilipowaka nikaona meseji iliyotoka kwa yule msichana ikiuliza.
“Utakuwa na nafasi leo?”
Sikujua meseji ile aliituma muda gamin nikaijibu haraka.
“Ninayo nafasi, uko wapi?”
Baada ya kutuma jibu hilo sikupata jibu jingine. Nilipoona muda unazidi kwenda nikaamua kumpigia.
Simu iliita kwa muda mrefu kisha ikapokelewa.
“Hallow…mbona umechelewa kunipigia?” Sauti ya msichana ikauliza.
“Nilikuwa nachaji simu, meseji yako nimeiona sasa hivi”
“Niliituma tangu saa moja, nikaona kimya”
“Kwani hatuwezi kuonana muda huu?”
“Tunaweza kama utaweza kufika huku muda huu”
“Kwanini nisiweze wakati boda boda zipo”
“Sawa, njoo basi”
“Nitakukuta wapi?”
“Njoo hadi hapa Mbuyu Kenda kisha nipigie simu”
Sikuwa nikipafahamu mahali hapo lakini nilijua mwenye bodaboda nitakayemkodi atakuwa anapajua mahali hapo.
“Sawa, ninakuja” nikamwambia.
“Ukifika Mbuyu Kenda utanipigia simu” akarudia kuniambia.
“Sawa”
Msichana akatangulia kukata simu. Nilikuwa nimejilaza kitandani, nikakurupuka na kuvaa shati kisha nikatoka. Wakati naelekea barabarani nilimpigia simu jamaa mmoja mwenye bodaboda niliyekuwa namfahamu.
“Uko wapi?” nikamuuliza mara tu alipopokea simu.
“Niko stendi” akanijibu.
“Nifuate hapa Mabanda ya Papa”
“Sawa, ninakuja”
“Usichelewe”
“Nimeshawasha pikipiki, ninakuja”
Nikakata simu. Nilitembea haraka haraka kutoka zilipokuwa nyumba za polisi hadi eneo hilo la Mabanda ya Papa. Ulikuwa mwendo ulionichukua dakika tatu tu.
Nikasimama pembeni mwa mzunguko wa barabara nne uliokuwa mahali hapo. Mara nikamuona mwenye bodaboda niliyempigia simu, nikampungia mkono. Alipunguza mwendo akaja kusimama karibu yangu.
Nikapanda nyuma yake.
“Twende wapi?” akaniuliza.
“Twende Magomeni”
“Magomeni ipi?”
“Unapafahamu Mbuyu Kenda?”
“Ndipo unapokwenda?”
“Nipeleke hapo hapo”
Nikaondoka na yule mwenye bodaboda. Tuliliacha jiji tukashika barabara ya Majengo. Tulipoiacha Majengo tukaingia Mapinduzi. Barabara ya Mapinduzi ndiyo iliungana na barabara ya Magomeni.
Robo saa baadaye mwenye bodaboda akanisimamisha pembeni mwa mbuyu uliokuwa kiza. Mbuyu huo ulikuwa kando ya barabara.
“Ndio hapa?” nikamuuliza yule kijana huku nikiangaza macho kila upande. Kote kulikuwa kiza. Nyumba chache tu zilizokuwa zinawaka taa ya umeme.
“Ndio hapa”
Nilitaka nitoe simu nimpigie yule msichana nimwambie kuwa nimefika lakini sikutaka yule kijana ajue nilimfuata nani pale, nikashuka kwenye pikipiki.
“Nisubiri” nikamwambia na kwenda kusimama kando.
Nikatoa simu na kumpigia msichana niliyekuwa nimemfuata pale.
“Nimeshafika” nikamwambia alipopokea simu.
“Upo Mbuyu Kenda?” akaniuliza.
“Ndiyo”
“Subiri” akaniambia.
Je nini kitatokea?
 
2011996bd

2011996bd

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2016
Messages
271
Likes
95
Points
45
Age
21
2011996bd

2011996bd

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2016
271 95 45
Dah hadithi tam sana jamani
 

Forum statistics

Threads 1,236,682
Members 475,218
Posts 29,266,712