Mimi niliwahi kupotea ndugu, wakati nipo darasa la tano, kisa ka mbwa, kuna ka mbwa kalipita mitaa ya home, enzi hizo tulikuwa tunafuga mbwa kama watano, wale mbwa wetu walikuwa na wakali sana, brother alikuwa anawachanganyia bangi na gongo ktk msosi wao, sasa hiyo cku cjui kalikotokea nilipomuona nikaanza mkimbia alikuwa kakonda sana, nikapanda juu ya mpera, sasa wale mbwa wetu c wakamuona wakawa wanabweka sana, kiasi walivunja mlango wa banda wakaanza mkimbizayule mbwa, sasa mimi kuona huu msala ikanibidi nianze kuwafuatilia wale mbwa wetu kila nilipokuwa nawaita ndivyo walivyokuwa wakitokomea porini, nakumbuka ilikuwa saa tatu asubui niliwafuatilia huku na mimi nawakimbiza maana wale mbwa wetu walikuwa wakorofi sana, nikajua nikiwaacha watauma watu, hivyo nia yangu ilikuwa niwarudishe home, haikuwa hivyo, nilipotelea msituni na nilikuja pata ufumbuzi wa kutoka huko baada ya siku tatu, niliona mengi ya kuogofya ila Naamini mungu tu aliamua kunilinda, sitokuja niisahau hii...hakuwa mbwa yule, nikuja kujua huko porini baada ya kumuona akichange....aaagh ndo hivyo....