Mkushi w jani
JF-Expert Member
- Oct 2, 2021
- 1,576
- 1,302
HUmu tunsubili kuliwa kwa edna sanaaaaHaha hapo safi mkuu! Kumbe una ndoto kama zangu.
Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
HUmu tunsubili kuliwa kwa edna sanaaaaHaha hapo safi mkuu! Kumbe una ndoto kama zangu.
Sent from my itel W4001P using JamiiForums mobile app
Twende kazi bado mkuu, nko home tu Leo sioni ata kitu cha kufanya online uku zaid ya ilo simulizi basi siku inakuwa mzigo kweliHahaha.... Haachwi mtu
Inaonekana humu mpo wamburu watupuMkuu singanojr ,huyu Raheli ni wa babati yetu hii hii ya Manyara au kuna Babati nyingine?😂.. Atakuwa mburu wa Dareda au Bashnet huyu,maana kama namkumbuka kumbuka,😂..yani sura yake kama inakuja halafu inakataa😂😂
Mpaka kielewekeTUPO HAPA HATULALI LEO
nitaweka morning mambo hayako vizuri this time
Kule watisap Iko mbaliSEHEMU YA 218.
Haikueleweka Roma alikuwa wapi muda wote wa mchana ila muda wa usiku alikuwa ndani ya Upepo Beach Garden akijipatia Sea Food kutoka kwa mgahawa wa Mzee Chino , kwa jinsi alivyokuwa akifurahia msosi ni kama hakuna kilichotokea mchana.
Wakati akiendelea kufurahia na msosi wake , alijikuta akifumbwa macho na mikono milaini ya mtoto wa kike na kujikuta akiweka kijiko chini.
“Bebi Neema usiniambie Mzee Chino kakuambia nipo hapa”Aliongea Roma na mrembo yule akamuachia na ni kweli alikuwa ni Neema Luwazo , Naibu Waziri wa Sanaa na utamaduni.
“Sikutarajia kama nitakukuta hapa?”Aliongea Neema huku akiweka mkoba wake pembeni na kukaa kwenye kiti cha mbele yake Roma.
“Nikajua yule mzee ndio kakuambia nipo hapa”
“Hapana .. ila kwa nilivyokumisi nilitamani kukukipigia simu muda wowote, sikuwa sawa kimawazo tokea nimetoka bungeni”Aliongea Neema kwa sauti chini na kumfanya amwangalie mrembo huyu , licha ya kuonekana mtu mzima , ila alikuwa anaita na kuvutia balaa.
“Nadhani leo tunahitajiana kufarijiana , nimefika hapa kwasababu sikuwa kwenye mudi nzuri”
“Mh!, nilitegemea utakuwa kwenye mudi nzuri kutokana na Kwenda na mkeo Ufaransa”Aliongea Neema na kumkumbusha Roma kuhusu Edna , alikumbuka tokea siku wanarudi hawakuongea Zaidi ya Edna kujifanyisha kuwa bize na kumkwepa muda wote.
“Bebi Neema unakumbuka mara ya mwisho hatukumaliza , leo nadhani ni siku iliopangwa maana wote hatupo kwenye mudi”Aliongea Roma huku akimkonyeza Waziri na mwanamke huyu alijikuta akicheka kicheko cha kwikwi na haikueleweka alifurahishwa na nini.
Ila ndani ya nusu saa mbele walikuwa ndani ya hoteli ya Mapple huku Neema akiwa amekodolea bahari ya Hindi huku Roma akiwa nyuma yake akicheza Boringo na kwa upande wa Neema network zilikuwa zikija na kukata.
“Hehe… hii staili ya kuiangalia bahari inafurahisha,unaonaje”
“Roma… Arggh .. miguu”
“Imefanyaje tena”.
“Inakosa..aa nguvu” Aliongea Neema Luwazo kwa kulalamika na Roma alimbeba juu juu na Kwenda kumtupia kitandani na kilichoendelea ni Neema kuyaita maji MMA”
Muda wa asubuhi saa mbili ndio Roma alifika Kigamboni kwa kutumia V8 mpyaa , yenye namba za serikali, na Roma alikuwa akiendeshwa na Dereva wa Neema Luwazo na Roma hakutaka kuingia nayo ndani na ndio maana baada ya kufika getini ilisimama na yeye akashuka.
Edna alionekana bado hakwenda kazini kwani gari yake anayoipenda kuitumia ilikuwepo , ila Roma hakujali sana alipiga hatua na Kwenda ndani na Sebule ilionekana kupoa sana, kwani hata Bi Wema hakuonekana kabisa sebuleni kama Alivyozoea , lakini Roma aliamini atakuwa amepumzika.
Roma aliingia kwenye chumba chake na kisha alivua nguo na kubadilisha zingine, alikuwa na mpango wa Kwenda kazini muda huo na ndio maana aliwahi kurudi.
Lakini baada tu ya kumaliza kuvaa koti, mlango wake ulifunguliwa bila hodi na ile anainua macho yake Edna alionekana kwenye mavazi ya kawaida kama mtu asiekuwa na mpango wa Kwenda kazini alionekana akimsogelea Roma kwa kasi na kumkumbatia Roma.
Jana yake usiku tokea Roma aondoke Edna hakulala kabisa , alikesha mpaka saa saba usiku akimsubiria Rona mpaka pale alipopotelea usingizini akiwa kwenye sofa na Bi Wema ndio aliekuja kumuamsha na kumwambia akalale chumbani.
Roma alishangazwa na kupokewa na kumbatio lililoambatana na kilio, Roma alijiambia siku zote Edna atakuwa mbabe tu mbele za watu akiwa kwenye biashara zake lakini alikuwa mdhaifu sana likija swala la mahusiano , alipewa mchunio wa siku mbili zote lakini leo hii anakumbatiwa na kilio juu.
“Wife una machozi ya karibu mno.. ndio mana unazidi kuwa M’cute”Aliongea Roma akiwangalie Edna akiwa ameshika mabegani kwa mikono miwili na Edna aliona aibu na kuangalia chini.
“Ulikuwa wapi nilikuwa na wasiwasi , na umeamua nini?”Aliuliza Edna maswali mawili kwa mpigo na Roma ilibidi amkalishe Edna kwenye kitanda kwanza.
“Nianze kukujibu swali lipi?”
“Ni jibu swali la pili?”
“Unamaanisha kuhusu yule Kikongwe asie na akili aliekuja kubwabwaja jana, nimeamua kumpotezea”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida , lakini kwa Edna lilionekana jibu la kuumiza , aliamini Roma anaficha kile anachojisikia moyoni kwa kuamua kupotezea.
“Roma najua unajisikia vibaya kwa muda huu na hujui cha kufanya na ndio maana unaamua kupotezea , sijui nini kilichotokea lakini katika mazungumzo yote nimezingatia sana maneno ya mwisho ya Afande Kweka”Aliongea Edna..
“Yapi hayo?”
“Kuhusu mama yako , amesema anateseka na aliteseka sana kwa ajili yako , Roma unajua nilichojisikia siku nilivyosikika baba yangu ambaye nilijua ni mzazi wangu wa damu siku nilivyopokea kifo chake..”
“Ile siku nilijutia sana kutokwenda kumtembelea na kumuona hata mara moja , licha ya kwamba hakuwahi kunipenda kwenye Maisha yangu yote , lakini iliniuma baada ya kuambiwa kafariki kabla sijamuoa kwa mara ya mwisho”
“Ninachomaanisha ni kwamba wanandoa wanaweza kupeana talaka , marafiki wanaweza wakageukana na kuwa maadui lakini upendo wa mama kwa mtoto siku zote ni wa kudumu na hakuna kitu ambacho kinaweza kumtenganisha mtoto na familia yake .. nakushauri umfikirie mama yako kwa muda huu , najua unaumia na mimi pia najisikia vibaya kwa ajili yako, Usilipotezee hili swala kama vile haujaufahamu ukweli”Aliongea Edna na maneno yalionekana kumwingina Roma vizuri na hata hivyo moja ya misheni yake ilikuwa ni kurudi Tanzania kutafuta familia yake na kuwauliza kwanini walimtelekeza na akajikuta kwenye mikono ya watu waliomtesa.
Roma aliona maneno ya Edna yana ukweli ndani yake , licha mpaka muda huo hakujua ni nini kilichotokea , lakini kama mama yake anateseka kama alivyosema Mzee Kweka aliona anasababu ya kuchukua hatua.
“Una akili sana mke wangu.. kesho nitaenda kumleta Mama Mkwe wako”Aliongea Roma na kumfanya Edna kutabasamu.
Upande mwingine ndani ya familia ya Mzee Atanasi , Jestina alikuwa na furaha isiokuwa ya kawaida mara baada ya kusikia taarifa ya Mzee Kweka kumtembelea Roma.
Kile kilio chake alichokuwa nacho cha kumsaidia dada yake aliamini kinakwenda kujibiwa , hakuweza kujua ni kwa namna gani Blandina dada yake atakuwa na mshangao baada ya kumuona Roma.
*******
Blandina tokea siku aweke msimamo wake juu ya kutotaka kuvaa sura ya bandia tena , swala hili lilifanya kuwe na ugomvi mkubwa sana na mume wake Kamau Kamau.
Mwanamke huyu licha ya kwamba ni siku kadhaa tu tokea atoke Tanzania , lakini pia kujua kuwa mwanae Denis yupo hai , alionekana kukokanda ghafla , haikueleweka kinachomkondesha ni kitendo cha kamau kutomruhusu Kwenda kuonana na mwanae au kuna sababu nyingine.
Wakati Maina akiwa amejilaza chumbani kwake , chini ya ulinzi mkali wa walinzi wa ikulu , mlango wa chumbani kwake ulifunguliwa na akaingia Kamau Kamai raisi wa Kenya.
Kamau alimwangalie mke wake aliekuwa akikodolea picha zilizokuwa kwenye mikono yake na Kamau jambo lile lilimkasirisha sana na aliingia kwa pupa na kumpokonya zile picha na kisha akazichana chana na kumfanya Blandina kuanza kulia.
“Kamau kwanini lakini … nakuliza kwanini umechana picha za Denis , unajua ni kiasi gani nimemkumbika mwana…”
“Paaah!”
Kamau alikasirika maradufu kila mara alipokuwa akisikia jina la Denisi , yaani kwa jinsi alivyomuona Maina haikuwa na tofauti na miaka ishirini na tano iliopita , Blandina amerudi kuwa Blandina yule yule anaempenda mtoto wake kuliko kitu kingine na hakujali tena nafasi yake kama mke wa raisi.
Blandina licha ya kupigwa kibao , wala hakujali alimwangalia Kamau huku machozi yakimtiririka na kuchuchumaa chini na kuanza kukusanya vipande vipande vya picha za utotoni alizokuwa amepatiwa na Linda , msaidizi wa karibu wa Raisi Jeremy.
“Maina utakuwa hivi mpaka lini mke wangu?”
“Mimi sio Maina , niache Kamau…”Aliongea Blandina na kusimama na kusogela kitandani na kuanza kupanga upya picha za Denisi , kwa jinsi alivyokuwa akionekana ni kama akili zimruka kidogo , hakuonekana kama yule mama ambaye anasaidia Watoto Yatima tena.
Kamau kwa jinsi alivyomuona Mke wake aliona kabisa hawezi kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida na alipaswa kukubali ukweli kwamba muda huo Blandina alichokuwa akikiwaza kwenye kichwa chake ni Denisi tu.
Alikaa takribani dakika kumi na tano akiangalia kile ambacho Maina anakifanya na ilimchukua dakika kama tano tu hivi kwa Maina kuweza kuunganisha vipande vyote vya picha vilivyokuwa vimechanwa na Mheshimiwa Kamau na Maina alitabasamu baada ya zoezi lake kufanikiwa.
“Noo.. Siwezi kukubaliana na mpango wa Mwambai , Hades kitu gani bwana akija Kenya namuua”Aliwaza Raisi Kamau na kisha alisogea mpaka kitandani na kisha akampokonya Blandina picha zile na kutoka nazo na kumuacha mwanamke huyo akitoa ukulele wa kilio ndani ya chumba, ila hakujali , na walinzi waliokuwa nje ya chumba cha Blandina First Lady waliishia kushikwa na huzuni.
“Ni mimi…”Alionekana Kamau akiongea na simu.
“Ndio mheshimiwa”
“Nataka ufanye mpango, kuna mwanamke analetwa hapo kambini , nataka ulinzi juu yake uimarishwe kwa masaa ishirini na nne na yoyote ataketaka kuongea nae , lazima ruhusa itoke kwangu”
“Sawa mheshimiwa , lakini tunaweza kumfahamu huyo mwanamke?”
“Hilo sio juu yako , ninachotaka ni ulinzi kwake , maswali mengi sitaki”Aliongea Mheshimiwa na kukata simu na kurudi alikotoka.
“Njiro nifuate”Aliongea Kamau na Njiro mlinzi wa First Lady alimfuatisha Kamau mpaka kwenye ofisi yake.
“Ndio mheshimiwa”
“Nataka mfanye utaratibu na mke wangu atapelekwa Kambi ya Moi Airbase kwa ajili ya usalama wake”Aliongea Mheshimiwa Kamau na kumfanya Njiro kushangaa.
“Kwanini mhesh..”
“Fanya utaratibu wa mke wangu kuepelekwa huko , na jambo hilo liwe siri , hakuna mtu anaeruhusiwa kumjua Blandina ndio Maina , nafikiri unajua ninchomaanisha, unaweza Kwenda”
“Sawa mheshimiwa”Aliongea Njiro
“Nishaongea na mkuu wa Kambi hivyo kazi yenu ni kumfikisha tu , hakikisha unampa maelezo ya kupewa huduma nzuri”
“Sawa mheshimiwa”Aliongea Njiro na kutoka kwa ajili ya Blandina kupelekwa kambi ya Moi.
ITAEND3LEA
HAYA NIMEWAPUNGUZIA LIPENI 2000 MKUKE WATSAPP TUENDELEE TUPO 278 NICHEKI 0687151346.WATSAPP ONLY