Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

singanojr

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
1,420
7,901
NILIEMDHANIA NI KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI:SINGANOJR .
AGE:18+


NB
:SIMULIZI HII NI YA KUTUNGA


PDF KUTOKA SEHEMU YA KWANZA MPAKA YA 390 IPIO NITAFUTE WATSAPP 0687151346

PROLOGUE../DIBAJI


Ilikuwa ni muda wa usiku saa tisa kamili ndani ya chumba kikubwa anacholala mheshimiwa Rais Senga , akiwa amepumzika na mke wake mara simu yake kubwa ya I phone 13 ilianza kuita mfuliulizo kiasi cha kumuamsha na kushangaa ni nani anampigia muda huo kwani sio kawaida yake , na mara nyingi akipokea simu usiku sana huwa ni za dharula na kuna tatizo kubwa ambalo wasaidizi wake wameshindwa kulitolea maamuzi, aliangalia jina la mpigaji na kujikuta usingizi ukimuishia, jina kwenye kioo lilionekana limeandikwa Senior(Mkubwa kazini).

“Senior kuna nini? , maana sio kawaida kunipigia muda huu”.

“Senga ulinihakikisha kuwa Edna atakuwa salama ndani ya taifa lako , lakini nini hiki kinaendelea ndani ya nchi yako”

“Naomba upunguze jazba Senior nini tatizo?”

“Vijana wangu wamenitumia ripoti kwamba Edna alitekwa”

“Nini..!! , unahakika na hio taarifa Senior?”

“Nina uhakika na vijana wangu wangu Senga , nimewapa kazi hio moja tu ya kumlinda Edna kwa siri”

“Vipi hali ya Edna kwa sasa??”.

“Ni bahati kwamba sasa hivi ana mume , kwa hilo namsifia sana , yule mtoto ana akili sana kachagua mume bora”

“Unamaanisha Roma ni mume bora kwa Edna?”.

“Ndio Senga mchunge sana huyo kijana sio mtu wa mchezo mchezo na ni mtu katili kuwahi kutokea katika huu ulimwengu, hakikisha unakuwa upande mzuri na yeye kukusaidia kwenye mpango wako, mimi yangu ni hayo tu na nikwambie Senga haupo makini kabisa Edna anatekwa huna habari , mimi niliopo ng`ambo ya pili ya nchi yako nimepata taarifa kabla yako , nimekasirishwa sana na jambo hili ,Usiku mwema nadhanni tutaongea Zaidi juu ya mipango yetu siku tukionana”Aliongea Senior na kisha kukata simu.

“Who is this Guy?”Alijiuliza mheshimiwa Senga huku akiwa ni mwenye kushangaa Senior anamfahamu vipi Roma.

“ My guess was right he is not normal , there is more hidden info about him , I have to dive deep to discover more details”.Aliwaza mheshimiwa.

Kabla haujaendelea jiulize haya maswali:

Roma ni nani katika hii simulizi , kwanini Senior anasema ni mtu katili kuwahi kutokea kwenye huu ulimwengu?.

Edna ni nani , kwanini Senior anamlinda kwa siri ?”

Senior ni nani na ni mipango gani anayo yeye pamoja na Senga Raisi wa Tanzania.

UTANGULIZI
Roma mbeba mizigo ndani ya soko la Mbagala Rangi Tatu anamdhania Edna Kama mwanamke anaejiuza ,baada ya mwanadada huyu kuwekewa dawa ya usingizi kwenye kinywaji na maadui zake katika ulimwengu wa Biashara akiwa ndani ya hoteli na Roma anambeba Edna na kumpeleka Geto kwake na afanya nae mapenzi.

Edna kwa Mara ya kwanza analala na Roma pasipokujitambua na kupoteza usichana wake ,baada ya tukio Hilo anaamua kuolewa na Roma kwa mkataba wa Miezi sita ili kuepuka kuolewa na mwanaume asiempenda ,baada ya Roma kufunga ndoa na Edna anakuja kugundua kuwa mke wake anamiliki kampuni kubwa Nchini huku akiwa na utajiri wa kutisha.

Edna anamuona Roma kama mtu asiyekuwa seriasi na maisha kutokana na aina ya mfumo wa maisha yake ,maisha ya kuwa na wanawake wengi swala linalomkasirisha Edna.

Edna anajitahidi kuweka ukaribu na Roma ili kujua sababu ya mume wake macho yake kubadilika Rangi anapokuwa na hasira na kuwa ya kijani huku akiwa na roho ya ukatili mno

Idara na mamlaka za kiusalama Nchini zinashangazwa na uwezo wa Roma wa kuzungumza Lugha zaidi ya ishirini na mbili na wanaanza kutafuta taarifa zinazomuhusu Roma lakini licha ya kupata taarifa inayoonyesha Roma kusomea ndani ya chuo kikubwa Duniani Cha Harvard wanakosa taarifa zingine zinazomuhusu Roma na kuishia kujiuliza Roma ni Nani haswa


SEHEMU YA KWANZA

Ni muda wa saa moja za jioni ndani ya soko la Mbagala Rangi tatu pilika pilika zilionekana kuwa nyingi sana kwa wafanya biashara , kwani muda huu kwa wafanya biashara wengi ndani ya soko hili ndio muda ambao walikuwa wakifunga biashara zao na kurudi majumbani , hususani wale waliokuwa wakifanya biashara za nguo na vyakula.

Kikawaida ndani ya hili soko wafanyabiashara wengi walikuwa wakihifadhi mizigo yao sehemu salama kwa wale ambao walikuwa na mizigo mikubwa ambayo hawakuwa na uwezo wa kurudi nayo nyumbani , ambao pia hawakuwa na maduka maalumu ya kufanyia biashara , hivyo mara nyingi hulazimika kuhamisha mizigo yao kutoka eneo wanalo fanyia biashara mpaka sehemu ya kuhifadhia.

Kazi hii ya uhamishaji wa mizigo ni kubwa kwa wafanyabiashara hivyo huomba msaada kwa waendesha mikokoteni na wabeba mizigo kuwasaidia kuhamisha huku wakiwalipa kwa kiasi cha mizigo wanayobeba.

“Roma njoo leo unisaidie kubeba mizigo yangu basi nikahifadhi muda umeenda sana” aliongea mwanamama mmoja hivi mweupe wa wastani mnene aliekuwa akifanya biashara ya kuuza madela , vijoli pamoja na viatu vya kike ndani ya soko hili la Rangi tatu.

“Mama Nasra wala hata usiwaze , nitakuhamishia haraka haraka maana nina kazi pia ya kuhamisha na mzee Saidi”.

“Haya mwanangu nashukuru sana”Aliongea mwananamama huyu huku akimuonesha Roma mizigo ya kuingiza kwenye mkokoteni wake kwa ajili ya kwenda kuhifadhi sehemu husika.

Ndani ya dakiika kadhaa tu Roma alikuwa ameshamaliza kazi ya kuhamisha mizigo yote ya kibiashara ya Mama Nasra na kulipwa buku lake na sasa alikuwa bize na kuhamisha mizigo ya Mzee Saidi , ambaye alikuwa ni muuza Viatu vya mtumba.

Uchapakazi na uaminifu wa Roma ulikuwa ukiwafurahisha sana wafanya biashara wengi sana wa soko hili kiasi cha kupelekea mara nyingi kumtaka Roma awasaidie kila linapokuja swala la kubeba mizigo kuitoa sehemu moja kwenda nyingine , alikuwa akifanya kazi kwa haraka sana , kiasi ambacho hata wenzake abao aliokuwa akifanya nao kazi hio hio walikuwa wakimshangaa kwa uwezo na nguvu alizokuwa nazo Roma .

“Kijana Asante sana kwa kuhamisha kwa haraka haraka maana nina dharula”

“Usijali mzee wangu” Aliongea Roma kwa kuweka tabasamu usoni mwake na kisha alipokea noti yake ya shilingi elfu mbili na kisha kuingiza mfukoni.

Mpaka kufikia muda wa saa nne za usiku Roma alikuwa amesomba bidhaa nyingi za wafanya biashara na kwenda kuzihifadhi na sasa alikuwa amekaa kwenye moja ya meza tupu iliokuwa haina kitu akihesabu hela zake.

“Hatimae nimeingiza Elfu kumi na tano , ni kiasi kikubwa sana hiki kwa leo , ngoja nikale ugali na nyama ya Mbuzi kwa mama Joshua nisepe home nikalale”Alijiongelesha Roma huku akinyanyuka mahali alipkuwa ameketi na kusogelea mkokoteni wake na kuuweka pembeni sehemu ambayo mara nyingi anauhifadhi yeye pamoja na wenzake mpaka siku inayofuata .

“Oy mwanaa , leo umepiga kazi sio poa”.

“Kawaida tu Juma , japo ni kweli siku ya leo haikuwa kama jana”Aliongea Roma akiongozana na rafiki yake Juma wakielekea uelekeo mmoja . Juma ni rafiki yake Roma wa muda na walikuwa wakifanya kazi pamoja , utofauti wa Juma na Roma ni kwamba Juma yeye alikuwa ni mwenyeji wa jiji hili la Dar es salaam , akiwa amezaliwa ndani ya jiji hili na Roma alikuwa na muda wa miezi sita tu tokea aingie ndani ya jiji hili la Dar es salaam kutokea mikoani na alikuja ndani ya jiji la Dar kama moja ya vijana wengi wanaokuja kwa kisingizio cha kutafuta maisha.

Roma alikuwa ni mrefu wa wastani , mwenye mwili uliokuwa umejengeka vyema kimazoezi , hakuwa handsome sana wala hakuwa mwenye sura mbaya , alikuwa ni wale wanaume ambao walikuwa wakionekana kawaida sana katika macho ya wengi na moja ya sababu kubwa iliompa Roma umaarufu ni kutokana na uchapaji kazi wake ndani ya soko hili la Rangi tatu.

Baada ya marafiki hawa kuvuka upande wa pili wa barabara hatimae walikuwa ndani ya mgahawa wa Mama Joshua kwa ajili ya kupata chakula cha usiku , waliungana na wenzao wengi waliokuwa ndani ya eneo hilo na kuagiza chakula huku wakiendelea kupiga stori za hapa na pale ili mradi kunogesha maongezi yao.

“Oya Wadau leo Club B kuna bonge la Party , leo ni full bia nusu bei”Aliongea jamaa mmoja mbeba mizigo aliekuwa maarufu sana ndani ye eneo hili la Rangi tatu aliekuwa akifahamika kwa jina la Yusuph.

“Tukitoka hapa lazima tukatembelee eneo hilo, ila hio parti inahusu nini?” aliuliza jamaaa mmoja mwembamba hivi.

“Mrembo Rose leo ni siku yake ya kuzaliwa na kuna bosi anaetoka nae hapa town ndio kaamua kumfanyia bonge la sherehe”.

“Kama ni hivyo hapo ni sawa kwa sisi kwenda kutembelea , au unaonaje Roma “ aliongea Juma akionekana ni mwenye kufurahia tukio hilo linalokwenda kutokea kwani alikuwa ni mwenye kupenda sana kunywa bia hasa zile za ofa.

“Nyie mtatangulia mimi nitarudi Getto kwanza nikaoge then nitaungana na ninyi”

“Ahaaa.. mzee unazingua , hapa hata sisi tutaenda kuoga kwanza ndio turudi kwenye Parti”aliongea Juma na kuwafanya wengine wote wamsapoti.

Naam ni muda wa lisaa limoja tu Juma akiwa ameongozana na Roma walikuwa mbele ya nyumba iliokuwa na geti jekundu Mbagala Biasi pembezoni kabisa na kilipokuwepo kituo cha Tanesko , taa kubwa za kituo hiki ziliwamulika na kufanya waonekane vyema kwa wapiti njia , kwani licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda sana , lakini bado pilikapilika za watu wa eneo hili zilikuwa zikiendelea.

Baada ya kusimama kwa madakika kadhaa hatimae mlango mdogo wa geti hilo ulifunguliwa na mwanadada mmoja mrembo aliekuwa amevalia shungi na kuwakaribisha ndani.

“Najma vipi , ulikuwa umelala mbona umechelewa kfungua mlango?”.

“Hapana nilikuwa chumbani na hata sikusikia” aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake iliokuwa ikisikika vyama na kisha alimwangalia Roma na kumsalimia.

“Roma mambo”

“Poa Naj , habari za siku nzima”.

“Safi tu”

“Oya Roma kajiandae chap tuondoke muda unakwenda wenzetu watatangulia kufika” aliongea Juma ilimradi tu akatishe maongezi yaliokuwa yakiendelea kati ya Roma na Najma .

Najma alikuwa ni mdogo wake Juma , alikuwa akiishi ndani ya nyumba hio ambayo ilikuwa ni yakwao walioachiwa ya urithi , ilikuwa ni nyumba kubwa tu ambayo ilikuwa wameigawa nusu wapangaji na nusu walikuwa wakiishi yeye pamoja na kaka yake.

Najma alikuwa akifundisha shule ya chekechea eneo moja lililokuwa likifahamika kwa jina la Kiramba, licha ya kwamba alikuwa akilipwa ujira mdogo , lakini alikuwa pia akionekana kuipenda kazi yake hio ya ufundishaji.

Tokea siku ambayo Roma anafika ndani ya nyumba yao na kupanga , Najma alitokea kumpenda Roma, Najma alikuwa si mwenye furaha asipomuona Roma , na kutokana na shughuli za kaka yake na Roma kuwa ni za kuwaruhusu kurudi usiku na kudamka asubuhi asubuhi , hivyo mara nyingi alikosa muda wa kuonana na Roma , hali ambayo ilimfanya kuhakikisha kila siku yeye ndio anaewafungulia mlango kila wanaporudi kutoka kazini.

Licha ya Najma kumpenda Roma kwa kaka yake ilikuwa ni tofauti , hakupenda kabisa Najma kujihusisha kimapenzi na Roma kabisa na hii yote ilisababishwa na hali ya kimaisha aliokuwa nayo Roma ,Juma alimuona Roma kama mtu ambaye hakuwa na malengo na maisha yake , hivyo aliona kitendo cha dada yake kuingia katika mapenzi na Roma dada yake asingefika mbali kimaisha na angeendelea kuishi katika hali ya maisha duni jambo ambalo hakuwa akitaka litokee kwani aliamini kwa uzuri aliokuwa nao dada yake , kama ni kupata mwanume mwenye pesa na kumuoa lisingekuwa jambo gumu , lakini asiliolijua Juma ni kwamba ni wanaume wengi sana walikuwa wakikataliwa na Najma licha ya kutaka kumhonga pesa nyingi na hata kumuahidi kumuoa ,mlimbwende huyu alikuwa amekufa na kuoza kwa mwanaume ambaye hakuwa na chochote cha kutishia jamii , mwanaume wa kawaida sana na maskinini mpangaji wao anaenda kwa jina la Roma.

Katika akili ya mwanadada huyu mrembo Najma aliamini siku moja Roma atamtamkia tu kuwa anampenda na yeye pia atamkubali na watayaanza maisha yao pamoja , hio ndio Imani aliokuwa nayo Najma juu ya Roma.

Kwa upande wa Roma alikuwa akijua fika kuwa Najma alikuwa akimpenda sana kimapenzi , lakini pia alikuwa akijua sana kwamba Juma hakuwa akitaka dada yake kutoka na yeye kimapanzi kutokana na hali yake ya kimaisha , hivyo licha ya yeye kumuona Najma kama mwanamke mrembo ambayey yeye kama mwanaume rijali anapaswa kuwa naye katika mahusiano , lakini alijitahidi sana kujizuia kumuonyeshea mapenzi mwanadada huyo , kwani hakuwa ni mtu mwenye kutaka ugomzi na rafiki yake Juma , kifupi alikuwa amependa sana chumba alichopanga ndani ya nyumba hii ya Roma na dada yake.

Basi baada ya Roma na Juma kujiandaa na kubadilisha nguo hatimae walitoka kwa kupitia geti dogo na kisha kutoka ndani ya nyumba hio na kuelekea uelekeo wa Club B , kutoka Bias mpaka ilipokuwa ikipatikana Club B hapakuwa mbali sana , Club hii ilikuwa ikipatikana Chalambe nyuma kidogo kabla haujafika sehemu iliokuwa ikifahamika kama Maji Matitu , ilikuwa ni moja ya Club kubwa sana na ya kuvutia iliokuwa ikipatikana ndani ya eneo hili , lakini pia ilikuwa maarufu sana kiasi kwamba ilikuwa ikitembelewa na watu waliokuwa wakiishi ndani ya mji huu pamoa ambao waliokuwa wakiishi nje ya eneo hili , ikiwemo Chamazi , Temeke , Kisemvule na baadhi ya meneo ya karibu.

“Wadau mmechelewa sana tena Sanaa yaaniii ….. bia ya tatu hii”Aliongea Yusph huku akigida bia yake kwa mbwembwe iliokuwa na chapa la Safari Lager .

“Usijali Yusuph tutakufikia tu “Aliongea Juma huku akiangaza macho huku na kule akikagua mandhari ya hapa ndani na hata kwa upande wa Roma hivyo hivyo.

“Siku hii ya leo watu walionekana kuwa wengi , kwani makelele yalikuwa mengi , huku harufu ya Pombe ikiwa imetapakaa kwa hali ya juu ndani ya eneo hili.

“Handsome Boys karibuni niwahudumie”Ilikuwa ni sauti moja nyororo iliosikika kwa vijana hawa na kuwafanya wamuangalie aliekuwa akiongea na hapo kila mmoa alitoa macho ya uchu baada ya kumuona mwanamke wa haja. Mrembo alievalia suruali ya kitambaa iliomchora vyema umbo lake namba nane , mwanamke huyu alikuwa ni mzuri kweli , si kujaliwa tu shepu lakini pia alikuwa amejaliwa sura nzuri yenye urembo wa asili ambao huwafanya wapenda ngono wengi kummezea mate.

“Aaaaa..hhh Sister Rose sjijatarajia kukuona leo ukihudumia bhana”Aliongea Juma kwa mshangao na kumfanya Rose kutabasamu huku macho yake yote akiwa ameyaelekeza kwa Roma ambaye alionekana kama mtu ambaye hakuwa na habari na mtu aliekuwa mbele yake kwani alikuwa ni mwenye kukagua kila mtu aliekuwepo ndani ye neo hilo kama jasusi anaetafuta adui.

“Mimi nipe Safari kama Broo wangu yusuph hapo , nipe ya baridiii”Aliongea Juma huku akikaa vizuri kwenye viti hivyo virefu huku akiwa amechia tabasamu pana usoni mwake.

“Na wewe Roma vipi leo” Aliongea huku akimwangalia Roma kwa madaha kiasi kwamba wenzake wote walikuwa wakimuonea wivu kwa kuangalia na mwanamke mrembo kama Rose kwa staili hio.

“Nataka ofa leo , nipe Heinken gharama ni juu yako”Aliongea Roma pasipo kupepesa macho na kumfanya Rose atabasamu na kisha kumwambia asijali anamletea na atalipia kwa kila kinywajia atakachokunywa kwa siko hio , jamboa mbalo liliwafanya marafiki zake waone ni upendeleo , lakini wala Rose hakuwajali.

“Oya mwanangu Roma huyu Manzi anakukubali sana kitambo tu , nashangaa mzee huchangamki , au unaogopa ni vya wakubwa”Aliongea jamaa mmoja aliekuwa pembenni ya yuspuh ,jamaa huyu alikuwa akifahamika kwa jina la Samia.

“Kweli kabisa Samia , Manzi anamkubali sana Mwamba hapa , lakini jamaa anazembea zembea , ningekuwa mimi ningekuwa nisharekebisha tayari na hapa ningekuwa nakunywa bia fulu fulu bureeee”Aliongeezea Yusuph na muda huo huo alikuja Rose na kuweka vinywaji huku akimpatia kinywaji Roma.

“ Bebi kuna ,mbuzi choma nikuleteee” wote waliangaliana kwa macho ya kimshangao na ya kutamani kile kilichosemwa , lakini hawakuambiwa wao , mtu aliekuwa amepewa ofa hio alikuwa ni Roma.

“Kweli mama leo umezaliwa upya , kama ni ofa mimi sina tatizo na nipo tayari kwa kila ofa inayopatikana”Alionea Roma .

“Ofa nyingine hautaweza , siku zote umekuwa ni wa kunikimbia” aliongea Rose kwa kumnong`oneza Roma na kumfanya atabasamu , kwani alikuwa akijua alichokuwa akimaanisha Mrembo huyu.

Huu usiku kama walivyotegemea vijana hawa ndio kile walichopata , kwani walilewa chakalii kwa bia za ofa ambazo zilikuwa zimetolewa na kibosile ambaye ilikuwa ikiaminika alikuwa akitoka kimapenzi na mwanadada Rose.

Baada ya masaa matatu baada ya ya keki kukatwa na sherehe kukaribia kumalizika , huku waliokuwa wakiendelea kula mziki na kunywa bia wakiendelea , alikuja jamaa mmoja aliekuwa mhudumu wa hii Club na kumpa kijimemo Roma, ambaye licha ya kunywa bia nyingi alionekana kuwa ngangari kuliko wenzake wote , baada ya kufungua kimemo hiki , alitabasamu na kisha alinyanyuka na kuoelekea nje , na kukata kushoto na ndani ya dakika chache alikuwa nje ya chumba na kugonga , na mlango ulifunguliwa na mrembo Rose aliekuwa amevaa khanga moja tu, alionekana alikuwa ametoka kuoga.

“Karibu Mpenzi”Aliongea Rose kwa namna ya kudeka huku akimvuta Roma ndani na kuzama mzima mzima .
iNAENDELEA HIVI PUNDE .
DEMU 1.png
 
SEHEMU YA PILI

Rose ni mwanadada ambae alikuwa ni bosi na mmiliki wa baa hiii kubwa iliokuwa ikifahamika kwa jina la Club B. Alikuwa ni mwanadada maarufu kwa eneo hili na hii yote ni kutokana na umiliki wake wa hii Bar ambayo ilikuwa kubwa mno, lakini jambo lingine ambalo lilimfanya mwanadada huyu kupata umaarufu ni kutokana na uzuri wake ambao Mungu alikuwa amembariki.

Sifa kubwa ambayo wanaume walevi na wale wapenda starehe ambao walikuwa wakimjua , sifa yake ilikuwa ni ugumu , mwanamke huyu alikuwa akiaminika sana kwa kutojirahisisha kwa wanaume , na ni Zaidi ya miezi kumi sasa tokea Club hio ifunguliwe na mwanadada huyu , hakuna mwanaume ambaye ashawahi kuhisiwa kutoka kimapenzi na mrembo huyu mfanyabiashara.

Lakini kwa upande wa Rose sababu kubwa ya kutojirahisisha kimapenzi ni kutokana na kuwa na mtu ambaye alikuwa akimpenda sana na huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Roma ,haikueleweka mara moja ni lini mwanadada huyu alianza kumpenda Roma kwani ujio wa Roma ndani ya jiji hili ulikuwa ni wa miezi sita tu , lakini kwa wawili hawa walionekana kufahamiana sana.

“Rose nimeitikia wito wako , naomba nikusilize na kisha niondoke”Aliongea Roma mara baada ya kujinasua kwenye mikono ya mrembo huyu, ambaye kama wewe ni mwanaume ambaye ungekuwa upo katika nafasi ya Roma ni hakika kwamba usingeshindwa kuukwepa mtego wa mwanamke huyu , lakini kwa kijana huyu Roma alionekana kushinda swala hilo.

“Jamani Roma , kwanini kila siku ni wakunifanyia hivi, wewe ni mwanume Roma mpaka sasa ushajua kwanini nimekuita , acha kunifanyia hivyo bhana”Aliongea Rose kwa sura ya kutia huruma huku machoni mwake kukionekana hali ya mtu anaetaka kulia , lakini kwa upande wa Roma alionekana sio mwenye kujali maneno ya mrembo huyo.

“Rose nishakuambia kila siku kuwa sipo tayari kufanya jambo unalotaka tufanye kwa sasa , naomba unielewe na naondoka kama hili ndio jambo uliloniitia”Aliongea Roma huku akigeuka kutaka kuondoka , lakini kabla hajashika kitasa cha mlango Rose alimkimbilia na kumkimbilia kwa nyuma na mikono yake kutua kwenye kifua cha Roma.

“Nitakusubiri mpaka lini Roma , nipo kwenye hali mbaya nakuhitaji sana Roma kwa wakati huu hata kwa nusu saa tu mpenzi.. nakupenda sana Roma”.

Roma alifumba macho huku akivuta pumzi nyingi , hisia za kimapenzi zilikuwa nyingi kwake , lakini alionekana hakuwa tayari kufanya kitu na Rose , na kwa kutumia nguvu kubwa ya kihisia alishika mikono ya Rose na kisha alijinasua kwake na bila ya kuongea neno lolote alitoka nje huku akimuacha Rose akiwa ni kama mtu ambaye hakuwa akiamini kile ambacho kimetokea , hakuwa akiamini kwamba kwa uzuri wake aliokuwa nao ameshindwa kumpagawisha mwanaume kama Roma , alijishangaa , kwani alichokuwa aakiamini alikuwa ni mwanamke mzuri sana ambaye kwa mwanaume yoyote yule ambaye angemtaka asingemkataa , lakini kwa Zaidi ya mara tano anakataliwa na Roma , hili kwake lilimshangaza sana , lakini pia lilimfikirisha na kuona huenda Roma ana matatizo.

Upande wa Roma alionekana kama ni mtu ambae alikuwa amechanganyikiwa, kwani hata kule bar alikowaacha wenzake hakurudi tena bali alitembea kwa miguu pembezoni mwa barabara , huku akionekana ni mwenye kushindana na hali iliokuwa ikiendelea katika mwili wake.

“Hapana leo siwezi kulala hivi hivi bila kukutana na mwanamke , lazima nitafute kahaba yoyote yule niende nae Geto”Aliongea Roma huku akiongeza mwendo , alionekana alikuwa ni mwenye hisia kubwa sana ya kufanya mapenzi , na alichodhamiria katika kichwa chake ndio alipanga kukitimiza kwa namna yoyote ile , kwani kitendo cha kuingia kwenye chumba cha Rose na kumuona akiwa nusu Uchi kilikuwa kimemfanya kuwa na hisia kubwa sana za kufanya mapenzi.

“Rose ni mwanamke ambaye sitaki kabisa kujihusisha nae , hapana siwezi kuwa naye katika mahusiano kwa sasa ni mapema mno , bado sijiamini”Aliongea Roma na wakati huu alikuwa mbele kabisa ya jengo ambalo ambalo lilikuwa na maandishi ya JR Hotel.

Hii ni hoteli ambayo ilikuwa ikisifika sana kwa eneo hili kwa kuwa na warembo wa bei ghali kuliko maeneo yoyote , ilikuwa ni hoteli lakini ilikuwa na Bar kubwa pamoa na Casino , lakini pia ilikuwa ikiruhusu machangudoa kuingia ndani ya hoteli hio na kutoa huduma kwa wateja kwa kiingilio maalumu.

Roma hapo ndio mahali ambapo aliona anaweza kutatua shida yake , japo bwana huyu alikuwa amekunywa bia nyingi Club B lakini alionekana hakuwa amelewa , kwani mwendo wake haukuonekana wa kilevi hata kidogo.

Lilikuwa ni eneo tulivu sana ndani ya hili eneo ambalo lilikuwa na harufu mbalimbali za mchanganyiko , Roma baada ya kuingia ndani ya eneo la Bar alianza kuangaza macho yake upande wa kulia kushoto na mbele kutafuta kitoeo kwa ajili ya usiku huo , licha ya muonekano wake kuwa wa kimasikini , lakini hakuna aliekuwa akimali kwani kila mtu alikuwa kwenye starehe zake.

Ndani ya sekunde chache tu za kukagua eneo hili hatimae alivutiwa na meza moja ambayo ilikuwa na mwanamke ambaye alikuwa amezika kichwa chake kwenye meza huku nywele zake ndefu zikiwa zimemfunika kwa mtindo wa kutapakaa na kufanya sura yake ishindwe kuonekana vizuri , huku juu ya meza ya kukionekana kuna bia zilizotapakaa pamoa na glasi nusu iliojaa juisi.

Roma alitabasamu na kuona sasa amepata tageti yake ,alisogea mpaka kwenye meza na kisha aliona mkoba wa mwanamke huyu ukiwa juu ya kiti pembeni , huku mita kadhaa kwenye meza nyingine kulionekana wanaume watatu waliokuwa wakinywa bia tararibu taratibu , lakini macho yao yote yalikuwa kwa Roma ambaye alikuwa akisogelea meza iliokuwa mbele yake. Wanaume hawa walionekana pia walikuwa wakimmezea mate mwanamke aliekuwa amezika kichwa chakekwenye meza.

Roma hakutaka kuwajali wanaume hao , kwani kumuangalia kwao aliona ni kwasababu ya wao kushindwa kupata ujasiri wa kukaa katika meza hio , jambo ambalo kwake aliliweza , hivyo baada ya kuvuta kiti , aliaribu kumshitua mwanamke huyo , lakini hakukuwa na majibu yoyote kwani bdada huyo alionekana kuwa yupo kwenye usingizi mzito sana.

Roma alishika kichwa cha huyo mwanamke huku akijaribu kuzikusanya nywele zake zote na kuziweka upande mmoja kwa ajili ya kuangalia sura ya mwanamke huyo.

“Mh! ,Leo nadhani bahati imeniangukia , huyu mrembo ni kisu Zaidi ya Rose , usiku wangu unaenda kuwa wa kipekee”Alijiongelesha Roma kwa namna ya kujipongeza huku tabasamu likiwa limepamba uso wake, na baada ya kama dakika mbili tu alifanya maamuzi ya kumuinua mwanamke huyo na kisha alichukua mkoba wake uliokuwa juu ya meza na kuuvaa kama mwanamke na kisha alimnyanyua mwanamke huyu ambaye kwake alikuwa ni kahaba tu na kisha alimuweka begani na kuanza kupiga hatua kuelekea nje , hakutaka kubaki ndani ya hoteli hii na kuchukua chumba kwani hakuwa na hela hio ya kulipia hivyo mahali sahihi alipoona panamfaa ni geto kwake Bias.

Wakati yeye anafanya hayo watu waliokuwa ndani ya hili eneo , walikuwa wakimshangaa sana Roma kwa kitendo hicho , lakini hakuna hata mmoja alieongea mpaka pale wanamuona Roma akitoka kabisa ya Mlango , lakini wakati Roma akitokomea nje mabwana hawa watatu waliokuwa kwenye Meza ya mbele ni kama walishituka.

“Shit Huyu fala ni nani anaejiamini kwa namna hii , anatuharibia mpango wetu , mfateni haraka kabla hajaenda mbali na mchukueni yule mrembo na mleteni kwenye chumba changu”Aliongea mwanaume mmoja ambae alionekana kuwa ni kiongozi katika kundi la watu hao, kisha alinyanyuka huku wale vijana watatu na wao wakinyanyuka na kutoka nje kwa haraka sana.

Roma baada ya kutoka nje haraka aliita Bajaji na kisha alimwingiza mwanamke yule ambaye alikuwa kahaba kwenye macho ya Roma , baada ya kumpandisha na yeye aliingia na kisha bajaji ilitoka na kuingia barabarani , lakini wakati huo huo Gari aina ya Lexus Dualis nyeusi , iliunga nyuma na kuifatisha bajaji aliokuwa amepanda Roma .

Muda huu magari hayakuwa mengi sana , lakini vijana waliokuwa wakiendesha gari hii , walionekana kuwa makini kutokuvunja sharia za barabarani , kwani waliogopa kusababisha ajali.

Wakati yote haya yakiendelea ilikuwa ni usiku kama wa saa nane hivi , mwendesha bajaji hakuwa ni mwenye kujali gari iliokuwa ikiwapigia honni nyuma yake na hii yote ni kutokana na Roma kumwambia aachae nayo na azidi kuendesha kwa kasi.

Dereva wa bajaji alionekana kuijua mitaaa vizuri ya Eneo hili la Chalambe Rangi tatu kwani baada ya kutembea mita chache aliingia chocho na kuendelea na safari , kitendo ambacho kwanza kilimfurahisha Roma , lakini pia kilifanya gari ambalo ilikuwa ikiwafata nyuma kushindwa kuingia chocho ambayo bajaji hio ilikuwa imeingia , na kwenda kusimamisha gari mbele huku wakitoa matusi.

“Amosi hatuwezi kuingia na gari huku kwenye vichochoro inabidi tutembee kwa miguu chapu , tusije kuwapoteza ikawa shida kwetu na bosi”:Aliongea jamaa mmoja aliekuwa na nywele za marasta aliekuwa akifahamika kwa jina la Jose.

Baada ya wawili hao kukubaliana walitoka haraka na kuingia chocho kwa kufukuzia bajaji , lakini walikuwa wameshaipoteza kwani walionekana kuwa sio wenyeji wa haya maeneo hivyo , walishinda kujua uelekeo.

“Shi**t Boss leo atatuaa”Aliongea Amosi huku akishika kiuno.

“Hakuna namna turudi tukamueleze halihalisi”Aliongea Jose huku wakigeuka na kurudi barabarani.

Upande wa Roma alikuwa ni mwenye kupandwa na hisia kilia alipokuwa akinusa harufu nzuri ya mrembo aliekuwa kwenye mikono yake.

“Bosi Huyo mtoto ni balaa , kama ni demu wako umepata demu”Aliongea mwendesha bajaji mara baada ya kuwafikiasha Roma mbele ya geti jekundu na Roma hakumjibu Zaidi ya kutabasamu na kisha alitoa buku na kumpatia muendesha bajaji na kisha alimbeba mrembo wake begani na kisha kufungua geti dogo na kuingia ndani.

Baada ya kuingia kwenye chumba chake hakutaka kufanya jambo lingine Zaidi ya kufanya kile alichodhamiria , alimwangalia mrembo aliekuwa juu ya godoro lake alilotandika chini na kisha akatabasamu na kuanza kuvua nguo , baada ya kumaliza alimtoa nguo moja moja mwanamke aliekuwa mbele yake na kisha alimuweka kwenye mkao mzuri na kutoa mhogo wake na kuupaka mate na kisha aliulengesha sehemu husika , na kilichosikika ni mguno ambao kwake hakujua ni mguno wa maumivu kutoka kwa mwanamke huyo au ulikuwa wa utamu , kwani bidada huyo bado hakuwa akijitambua.

Roma alifanya kwa muda mrefu kidogo Zaidi ya dakika sitini mpaka pale aliposhusha mzigo wake huku akihema kwa nguvu na kujilaza pembeni ya mrembo huyo na kupitiwa na usingizi moja kwa moja.

Ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu ndio muda ambao Roma alishituka kutoka usingizini , aliangalia saa kwa kutumia simu yake ya kitochi na kuona siku hio alikuwa amelala kuliko isivyokawaida , baada ya kurudisha simu yake chini ya sakafu alimgeukia mrembo wake aliekuwa pembeni yake akiwa amelala bado .

“Siawahi kudhania naweza kupata kahaba mrembo kama huyu sehemu kama JR Hotel”Aliongea Roma huku akiwa anamwangalia mwanamke mrembo aliekuwa mbele yake , lakini wakati akiendelea kuwaza mara mlango uligongwa kwa nguvu kitendo ambacho kilimfanya mwanamke mrembo kushituka kwa nguvu na kukaa kitako , huku akiwa ni mwenye kushangaa eneo alilokuwepo , alimwangalia Roma na kuona ni mtu ambaye hakuwa akimtambua , alijiangalia na kujiona hana nguo na haraka haraka , alijifunika kwa kipande cha shuka huku akianza kuvuta kumbukumbu kitendo amhacho kwa dakika mbili tu mboni za macho yake zilijaa machozi , wakati huo Roma hakuwa akijua kinachoendelea nyuma yake kwani alikuwa akiongea na Juma nje.

Baada ya kurudi ndani alimuona mwanamke kahaba mrembo akiwa tayari ashavaa nguo zake zote huku akiwa ni mwenye kutafuta kitu.

“Hey ! Mrembo unahangaika kutafuta nini?”Aliongea Roma huku akisogea mpaka ilipokuwa suruali yake na kuinyanyua na hapo mwanadada huyo aliona alichokuwa anatafuta , ilikuwa ni nguo yake ya ndani ambayo aliichukua kwa haraka na kisha aliingiza kwenye mkoba wake na kisha bila ya kuongea chochote na Roma alitoka nje ya chumba , huku akimuacha Roma akizubaa , lakini Roma baada ya kuona mrembo yule katoka nje alimkimbilia.

“Hey ! Sista umesahau malipo yako”Aliongea Roma baada ya kutoka huku akikutana na macho ya Najma aliekuwa akiangalia kitendo cha mwanamke mrembo kutoka katika chumba cha Roma , lakini pia akizidi kushangazwa na Roma kutoka na kuanza kumkimbilia yule mdada .

Najma alikerwa sana na kitendo kile na ni kama moyo wake ulikuwa ukiungua kwa hali aliokuwa akiiona , na hakuweza kusimama Zaidi kwani alikimbilia ndani .

Kwa upande wa Roma ni kama alichelewa kwani ile anatoka nje tu mwanadada yule alionekana kupanda kwenye bodaboda na kupotea kwenye macho ya Roma.

“Oya kaka una hatari sio poa , kile chombo umekipatia wapi … ndio maana jana sikukuona kumbe ulikuwa na misheni zako”Aliongea Juma ambae alikuwa ni kama mtu asieamini kile alichokiona , kwani mwanamke yule alikuwa mrembo kiasi cha kwamba hakuwahi kuwaza kumpata katika maisha yake , lakini siku ya leo anamuona akitoka kupigwa bao na Roma.

“Kaka una bahati sana , sio pooa .. yaani una nyota ya kupendwa na warembo”Aliongea Juma pasipo kujibiwa na Roma huku Roma akirudi kwenye chumba chake na Juma baada ya kuona hajibiwi alielekea ndani kwao , huku akiwa ni mwenye kufurahia kitendo kilichokuwa kimetokea asubuhi , kwani alimuona Najma akikimbilia ndani baada ya kuona kila kitu.

“Najma nimekuambia Roma hakufai kabisa , licha ya kwamba ni masikini wa kutupwa lakini pia ni mchafu wa tabia , ulifikiri nitakaa chini nikuruhusu utoke kimapenzi na Roma , sahau na futa katika kichwa chako na nadhani umeona mwenyewe”Aliongea Juma baada ya kuingia kwenye chumba chake na kuongea maneno hayo huku akiamini dada yake atayasikia vyema kwani nyumba yao hio haikuwa na Ceiling Board hivyo sauti ilikuwa ikipita moja kwa moja.

Upande wa Roma baada ya kurudi kwenye chumba chake alitoa shuka la kujifunika huku akidhamiria kwenda kufua lile ambalo ni la kutandika , lakini mara baada ya kutoa shuka hilo , alijikuta akitoa mshangao , wa doa kubwa lililokuwepo kwenye shuka lake hilo la rangi ya kijivu.

“Hii si damu hii… ina maana yule mwanamke alikuwa Bikra .. hahaha.. nafikiria ujinga tangu lini kahaba akawa bikra , inaonekana alikuwa kwenye siku zake za mwezi .. hehehe.. nimeweka historia ya kumbandua mwanamke akiwa kwenye Period”Alijiongelesha Roma huku akiweka tabasamu lake la kifedhuli huku akinusa harufu ya marashi iliokuwa kwenye mashuka yale na kutabasamu.. huku akijiona mwepesi sana kwa siku hio.

INAENDELEA
 
SEHEMU YA TAT U.

Siku tatu zilikuwa zimepita pasipo ya Roma kuonana na Najma , jambo ambalo halikumshangaza kwani alikuwa akikumbuka vyema kuwa Najma alimuona mwanamke kahaba alielala nae siku mbili zilizopita , hivyo alijua fika kuwa mrembo huyo atakuwa na hasira kali sana juu yake , kwani alikuwa akijua sana kwamba alikuwa akimpenda , hivyo hata yeye hakutaka kujishugulisha sana juu ya Najma , kwanza aliona ni jambo zuri kwani angejiweka mbali na Najma.

Upande wa Juma pia jambo hilo lilimfurahisha sana , kwani aliamini kwa jambo ambalo Roma amefanya litamfanya dada yake kutomfikiria kabisa Roma na kuendelea na maisha yake huku akimtafutia mpango wa kueoelwa na mwanamke mwenye pesa zake na ili kuhakikisha Najma hafikiriii kabisa kuendelea kumpenda Roma alifanya kila njia kuhakikisha taarifa za Roma kulala na kahaba mpaka asubuhi zinasambaa ndani ya wapangaji pamoja na majirani.

“Mh! Roma kabisa … siku zote nilikuwa namuona kama anamatatizo flani hivi kumbe anaonekana na yeye anapenda wanawake . lakini alishindwa nini kumchuku Najma mwanamke mrembo mpaka kwenda kuchukua mwanamke kahaba mtaani”

“Heheee… huenda Najma kuna kitu anakosa katika mwili wake ambacho hakimvutii Roma” Hao walikuwa ni wapangaji waliokuwa wakiongea kishambenga wakiwa wanasukana , na yote hio ilikuwa ni kumuumiza Najma ambae alikuwa akiingia kutoka kazini , na Najma aliwasikia vizuri tu na kuzidi kumchukia Roma kwa kitendo cha kuleta kahaba kwenye nyumba yao.

Najma alionekana ni mwenye mawazo , mengi mno , lakini licha ya hayo yote ambayo yalikuwa yakiendlea kwa wapangaji , moyo wake ni kama umegawanyika vipande viwili , kwani kuna upande ulikuwa bado ukimpenda sana Roma na hakuwa tayari kumuacha , lakini pia kuna upande ambao ulikuwa ukimchukia sana Roma, Pande zote mbili zilionekana kushindana vikali sana , huku upande unaompenda Roma ukichukua ushindi kila baada ya pambano., baada ya upande huo kushinda kila mara , hamu ya kutaka kumuona Roma ilizidi kujaa katika moyo wake , alikuwa amemkumbuka sana na alipanga usiku wa leo kumuona kwa namna yoyote ile.

Muda nao haukukawia sana kwani ulienda kwa haraka haraka , kwani ile Najma anakuja kushituka kutoka usingizini ilikuwa ni saa kumi na mbili , alinyanyuka haraka haraka na kisha alielekea gengeni kununua mboga za usiku , na siku hio alipanga kupika wali na Choroko , hivyo alinunua choroki na kuzichemsha na kuanza kuandaa chakula cha usiku.

“Noja leo nipike kingi , nitamuwekea Roma wangu katika chumba Chake akirudi ale”Alijiongelesha mwenyewe wakati huo akichambua mchele.

“Vipi mwenzetu mbona leo unaonekana ni mwenye furaha hivyo”Aliuliza mama Debora moja ya wapangaji , huku akimwangalia Najma usoni, Mama Debora ndio mpangaji pekee ambaye hakuwa na umbea mwingi na alikuwa ni Mlokole katika kanisa flani lililokuwa mita chache kutoka nyumbani kwa Najma na pia ndio mpangaji pekee aliekaa kwa muda mrefu mno , kwani yeye pamoja na mume wake walianza kupanga hapo kwao tokea wakianza kuona na mpaka sasa ambapo walikuwa na mtoto mkubwa tuambaye alikuwa chekechea anaefahamika kwa jina la Debora ,Mama Debora hakuwa mtu wa Nyumbani sana kwani alikuwa akifundisha shule ya msingi Ikwiriri , sehemu ambayo ilikuwa mbali na kumfanya kudamka sana asubhi na kurudi jioni , hivyo hakuwa akijua maswala yoyote yaliokuwa yakimuhusu Roma kuingiza kahaba.

“Hakuna jipya mama Debo , ni ile tu leo nimejikuta kuwa ni mwenye furaha”Aliongea Najma na kumfanya Mama Debo atabasamu.

“Hehehe .. acha kunificha Roma kakutamkia anakupenda nini?” Najma aliona aibu kwa sentensi hio na kuzidisha tabasamu .

“Nilijua tu , unaonekana kumpenda sana Roma Najma”

“Hhaha .. ndio”

“Muone sasa anavyoona aibu … nimekuja kuweka umeme mimi”Aliongea Mama Debo huku akimpita Najma na kuingia ndani kwa ajili ya kuweka umeme kwani Luku ilikuwa kwa ndani.

Najma alidumu sebuleni kwao kwa muda mrefu sana huku akiwasubiria kaka yake na Roma kurudi kazini licha ya kwamba alikuwa na usingizi mzito uliokuwa ukimnyemelea , lakini hamu yake ya kutaka kumuna Roma iliushinda usingizi na kuendelea kusubiri , siku hii ya leo si kama siku zingine kwani walichelewa kurudi mno , kwani mpaka inafika saa tano na nusu kaka yake hakuwa amerudi , baada ya kusubiri kwa takribani dakika ishirini hatimae mlango uligongwa na Najma haraka haraka alikwenda kufungua mlango.

“Najma hujalala tu , leo mbona umekua kunifungulia wewe”Aliongea Juma huku akiwa ni mwenye kumshangaa dada yake ,kwani siku mbili za nyuma alionekana sio mwenye kujali kuwafungulia yeye na Roma.Kwa Najma licha ya swali hilo , hakujali kabisa kwani alichokuwa akitaka kuona ni Roma Tu , lakini kilichomshangaza ni kwamba siku hio alimuona kaka yake pekee jambo ambalo lilimshangaza.

“Roma yuko wapi kaka , mbona haingii”

“Nilijua tu unataka kumuona Roma”Aliongea Juma huku akiweka uso wa hasira na kumpita baada ya kufunga mlango , lakini Najma hakuridhika alifungua mlango na kuangalia nje lakini Roma hakuonekana , jambo ambalo lilimfanya kuwa katika hali ya maswali , alifunga mlango na kukimbilia ndani.

“Kaka Roma yuko wapi , mbona hujaja nae”.

“Bwana eeh usiniulize maswali yako mimi , kwani umeona natembea nae mfukoni”Aliongea Juma na alikerwa sana na maswali ya mdogo wake , na aliona kabisa si kama alivyofikiria kuwa Najma alikuwa ashaachana na Roma baada ya kumuingiza kahaba geto kwake, alikula chakula alichowekewa na mdogo wake huku akitabasamu kwa kuona kuwa mdogo wake anajua kupika na baada ya kushiba aliignia kwenye chumba chake na kujilaza.

“Najma akiolewa na mimi naoa , nyumba yote inakuwa yangu na ili hili litimie sitaki Najma aolewe na Roma maana nina uhakika kwa maisha ya Roma atataka aishi na Najma hapa hapa”Alijiongelesha huku akiwa amejilaza na kukodolea macho taa mpaka pale alipopitiwa na usingizi pasipo ya kuzima taa.

Upande wa Najma yeye hakuweza kupata usingizi kabisa , muda wote masikio yake yalikuwa kwenye geti tu , ili asikie geti likigongwa ili akamfungulie Roma , lakini muda ulizidi kwenda , lakini alichokuwa akitegemea hakikuweza kutokea kabisa, baada ya kuona atasinzia alienda kusbiria Sebleni mpaka pale alipokuja kupotelea usingizini , na alikuja kushituka kukiwa kumekucha kabisa na hii ni baada ya kaka yake kumkuta Najma akiwa Sebleni, alijikuta hasira zikimpanda baada ya kuona dada yake kalala hapo sebleni na kung`atwa na mbu huku akimsubiria fukara Roma arudi.

“Huyu mpuuzi akirudi leo na mfukuza akapange kwingine , kwa hali hii Najma hawezi kuoelewa”Aliongea Juma na kisha alitoka mpaka vyumba vya nje vya wapangaji na kwenda kwenye chumba cha Roma na kukifungua na kuingia , ndani na kitu cha kwanza alichoona ni mabakuri mawili makubwa ambayo alikuwa akiyafahamu yakiwa kwenye kijimeza , aliyasogelea na kisha kufungua bakuli la kwanza na hapo nipo alipotoa macho huku sura yake ikianza kujikunja.

“Yaani huyu mpuuzi anamuwekea Roma mapaja ya kuku halafu mimi kaka yake ananiwekea wali na Choroko, hii haiwezi kuendelea hivi”Aliongea Juma kwa hasira huku akinyanyua yale mabakuli na kutoka nayo nje huku akipishana na Najma ambaye alimkata jicho , baada ya dakika chache Juma alitoka akiwa na kufuri lingine na kisha alifunga mlango wa Roma na kisha kurudi ndani na kupasha kiporo kile na kula.

Wakati yote hayo yakiendelea Najma ambaye alikuwa kwenye hali ya wasiwasi , alikuwa akimwangalia kaka yake tu , huku akiogopa hata ya kumuuliza chochote kuhusu Roma alipo , baada ya kusimama nje kwa dakika kadhaa , Juma alitoka nje huku akionekana safari ya kwenda kazini kwake ikiw aimewaidia.

“Kaka najua umekasirika lakini naomba uniambie Roma yuko wapi”.

“Usiniulize maswali ya kupuuzi na , kwa upendo wako wa kijinga jinga Roma kwanzia leo akirudi anaenda kutafuta chumba kwingine na nisikie fyoko fyoko uone”Aliongea Juma huku akiweka kibakrashia chake vizuri na kutoka huku mlango wa geti ukiipigiza kwa nguvu.

“Halafu huyu Mpuuzi kaenda wapi , tokea jana mchana sijamuona tena alipofuatwa na yule mtu mwenye suti”

****

JANA YAKE SAA SABA MCHANA

Roma mpaka kufikia muda wa Saa saba mchana alikuwa amepiga kazi kubwa sana ya kuteremsha mizigo ya Cement , kwenye Duka kubwa la vifaa vya ujenzi la Bozi , yeye pamoja na wenzake walikuwa wamechafuka mno kiasi kwamba hawakuwa wakitamanika , lakini wala hawakujali sana , kwani kwao pesa ilikuwa ndio kila kitu.

Njaa nayo haikuwaacha salama , na baada ya kupewa ujira wao , Juma aliwaongoza wenzake kuelekea upande wa pili wa barabara ili kwenda kujipatia chakula cha mchana kwa Mama Joshua. Kama ilivyokuwa desturi yao.

Baada ya dakika kadhaa tu Roma alikuwa ndio alikuwa mtu wa mwisho kunawa mikono , alianza kunawa uso ili kutoa vumbi la Cement na kisha alimalizia mikono , lakini ile anamaliza tu mita kadhaa kwenye barabara kuu , ilisimama gari aina ya V8 nyeupe , gari ambayo iliwafanya baadhi ya watu kuikodolea macho .

Baada ya gari hii kusimama , alitoka mwanadada mmoja aliekuwa amevalia suti ya rangi ya bluu na viatu vya rangi ya Pink , mwanadada huyu alitoa picha kwenye mkoba wake na kisha aliangaza kulia na kushoto huku akitoa simu yake iliokuwa ikiita na kisha kuiweka sikio mara baada ya kuipokea na baada ya maongezi machache alikodolea upande wa kimgahawa cha Mama Joshua huku akikagua mtu mmoja mmoja na baada ya kuona kile alichokuwa akitafuta alisogea kuelekea upande huo wa mgahawa ,. Huku baadhi ya watu wakishangazwa na urembo na shepu ya mwanamke huyo , lakini hakuna aliekuwa ni mwenye kujali.

“Habari yako kaka”Aliongea mwanamke huyu kwa sauti ya kujiamini kabisa na kuwafanya wakina Juma na wenzake kushangazwa na kitendo hicho , kwani mtu aliekuwa akisalimiwa alikuwa ni Roma.

“Salama”Aliitikia Roma pasipo kujali uzuri wa mwanamke aliekuwa mbele yake na kusogelea meza ya plastiki ya rangi ya bluu na kuketi kwenye kiti huku mrembo huyu kuonesha kuchukizwa na kitendo cha Roma kutokumuangalia usoni , licha ya kumsemesha , kwake alitafsiri kama dharau kubwa ambayo ameonyeshwa kwa mwaka huo , yaani katika maisha yake na urembo wake , hakuwahi kudharauiwa na mwanaume wa aina yoyote ile , lakini kwa Roma ilikuwa tofauti na hio aliingiza katika Top Ten ya dharau alizowahi kuonyeshwa katika maisha yake, lakini licha ya hivyo , mwanadada huyu bado alionekana kuwa ni mwenye shida ya kuongea na Roma kwani alisogea mpaka kwenye meza aliokuwa amekaa Roma na kumwangalia kwa kumshusha kwa mavazi yake ya kimasikini na uchafu uliomjaa.

“Mama Joshua nipe ugali mkubwa na Samaki “Aliongea Roma na kuwafanya marafiki zake wazidi kumshangaa Roma kwa kitendo hicho cha kutokujali , licha ya kuongeleshwa na mwanamke mrembo kama huyo ambaye kwao , ilikuwa ni kama ndoto kupata bahati ya kuongeleshwa na mrembo kama huyo.

“kaka nimekusalimia”

“Ooh !,, sorry sister , nilikuwa bize kidogo , kumbe ulikuwa ukiniongelesha mimi”.

“Ulifikiri na muongelesha nani , au dharau tu kaka yangu , sio vizuri”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake ya kuvutia huku akionekana amekereka kweli kwa kitendo cha Roma kujifanya hakumsikia wakati wote huo aliokuwa anamsalimia , na kilichomkera Zaidi mwanadada huyu ni kutokana na watu waliokuwa wakimwangalia , alichokuwa ametegemea mwanamke huyu ni Roma kumnyenyekea , lakini swala hilo likawa nje ya mategemeo yake na kumfanya yeye ndio aonekane mwanamke mwenye shobo na katika baadhi ya watu waliamini huenda huyo mwanadada alikuwa ni demu wake.

“Ulikuwa unasemaje sista”.

“Wewe si ndio Roma”

“Ndio ni mimi”

“Basi naomba utangulizane na mimi kuna mtu muhimu sana anataka kuonana na wewe”Aliongea mwanadada huyu na kuwafanya watu wote waliokuwa hapo mgahawani kushangazwa na maneno hayo , ila kwa Roma hakuonekana ni mwenye kushangaa sana , kwani alipokea chakula chake na kuanza kula.

“Sister naomba ukae , kwanza unisubirie nimalize nipige msosi ndio tuongee maswala ya mtu Muhimu .. maana hii ni moja ya starehe yangu na mara nyingi ni kila sipendaki kusumbuliwa”Aliongea Roma kwa kujiamini huku akianza kumega bonge la tonge na kulichovya kwenye mchuzi na kisha kulimeza lote , kitendo ambacho kilimshangaza sana huyu mrembo , na kumkera kwa wakati mmoja.

“Nitasubiri kwenye gari , ukimaliza naomba tufutatishane kama nilivyokuambia”Aliongea ule mwanadada pasipo kusubiri jibu , na kisha kuondoka .

“Halafu we Ms**nge unapenda kuifanyisha matawi ya juu , mtoto mkali kama yule anakuongelesha unajifanya unaongea kama hutaki kama vile Mondi , vile au unatuoshea tu washikaji zako hapa”Aliongea Yusuph huku akiungwa mkono na wenzake.

“Ila jamaa nimemkubali sana , ile pia ni heshima”:Aliongea jamaa mmoja ambaye yeye hakuwa muongeaji sana , ila siku hio alionekana kuchangia.

“Hahaha .. Mhando hata wewe leo umechangia mada , inaonekana pia umeguswa sana na jambo hili”Aliongea Juma na kuwafanya wengine wacheke maana ni kwa mara ya kwanza kwa Mhando kuchangia mada , yeye alikuwa ni mkimya wa hali ya juu

Baada ya Zaidi ya nusu saa ya Roma kumaliza msosi wake , alipiga maji kwenye kikombe , na kisha alijishika tumbo lake na kujiona kushiba vyema na kutoka mgahawani na moja kwa moja alielekea kweye gari , na kugonga mlango wa kioo ulioshushwa.

“Ingia kwenye gari”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti iliojaa machukizo na kwa Roma wala hakujali , baada ya kuingia kwenye gari , ilitolewa nduki kuelekea upande wa Kongonwe na kuja kugeuzwa na kurudi upande wa kuelekea kariakoo.

“Unanipeleka wapi Mrembo”Aliongea Roma lakini hakujibiwa , Zaidi ya kusonywa na Roma aliamua kutulia kwenye kiti chake , huku akifurahia kiyoyozi kilichokuwa kwenye gari hilo, na kutokana na uchomvu aliokuwa nao , alipitiwa na usingizi na hata pale alipokuja kushituka alijishangaa akiwa mbele ya jengo refu mno maeneo ya Mawasiliano Sehemu ambayo alijua haraka kwani alikuwa ni mwenyeji wa maeneo hayo , baada gari hii kusimama kwenye jengo hili Geti lilifunguliwa na gari ile iliingizwa mpaka ndani na kuegeshwa na kisha mwanamke yule mrembo alishuka .

“Karibuni Grand palace hoteli wateja wetu”Ilisikika sauti ya muhudumu iliowakaribisha kwa tabasamu na ucheshi wa hali ya juu ,Roma alimwagalia mwanamke huyo aliekuwa amevalia sare ya hoteli hio na kisha alimkonyeza kitendo ambacho yule mwanadada aliekuja na Roma kukiona na kubetua midomo , lakini kwa muhudumu alirudisha kwa tabasamu la kuita.

“Watu wenye pesa wanakula maisha sio poa”Aliongea Roma baada ya kuingia kwenye lift huku akiwa si mwenye kuacha kumkonyeza mrembo huyu ambaye amenuna kama muuza sumu.

Baada ya lift kufunguka katika Floor namba kumi na nane , Roma alifuata nyuma nyuma mpaka walipofika kwenye mlango wa chumba namba 708 na kisha huyu mrembo aligonga mlango na ndani ya dakika kadhaa mlango ulifunguliwa na mwanaume alievalia suti.

“Karibu Suzzane”Aliongea mwanaume huyu alievalia suti huku akiwa ni mwenye tabasamu lakini pia macho yake hayakuwa mbali na uso wa mwanaume aliekuwa nyuma ya Suzzane , mwanaume ambaye kwa macho ya haraka haraka alionekana kama Fukara.

“Bossi nisharudi na nimemleta”Aliongea mrembo Suzzane kikakamavu huku akimwangalia mwanamke aliegeukia dirishani , akionekana kuangalia nje akiwa amewapa watu wote katika chumba hiko mgongo.

Mwanamke huyu alikuwa amependeza mno kwa vazi lake la suti alilokuwa amevaa ,suti ya rangi nyeupe

“Asante Suzzane , mnaweza kuondoka mpaka pale nitakapowaita”

“Boss!!”Aliongea Suzzane kwa hali ya wasiwasi .

“Fanya kama nilivyosema Suzzane”Aliongea mwanadada huyo kwa sauti ya Amri na kumfanya Suzzane amkate jicho Roma ambaye alikuwa akikagua uzuri na ufahari wa chumba hiko.

Licha ya Roma kushangazwa na ufahari wa chumba hicho , lakini pia sauti ya mwanadada aliekuwa mita kadhaa mbele yake aliempa mgongo ilikuwa ikimsisimua mno , ilionekana kama inamkumbusha mbali sana.

Baada ya Suzzane na mwanaume yule kutoka nje , mwanadada yule aligeuka na kumwangalia Roma , kitendo ambacho kilimfanya Roma atoe mshangao na kutamka:

“Kahabaaa…!!!”

ITAENDELEA SIKU YA KESHO JIONI..
 
SEHEMU YA NNE.

Ndani ya jengo moja lefu lililopenezesha jiji katikati ya Posta , huku juu kabisa likiwa na maandishi ya JR Tower , katika Floor namba Ishirini na Mbili alionekana mwanume mwenye asili ya kisomali akiwa amesimama kwenye dirisha ambalo lilikuwa likimpa uwezo wa kuona Madhari ya Baharini , bwana huyu alikuwa katika lika la Ujana , mwenye nywele zake zilizompendezesha , hakuwa mfupi sana wala hakuwa mrefu sana , mwenye mwili wa saizi ya kati, na kwa haraka haraka ungejua bwana huyu alikuwa ni mtu wa kujipenda kutokana na mavazi ya gharama aliovaa .

Nyuma ya mgongo wake , kulikuwa na meza kubwa iliokuwa na tarakishi kubwa ya kampuni ya Apple , ikiwa inatoa mwanga hafifu huku ikionekana ilikuwa ikitumiwa na bwana huyu , huku mbele ya Tarakishi hii kulikuwa na Kibao kikubwa mfumo wa kioo kilichokuwa na jina lililosomeka CEO Abubakar Hamadi, JR Group Of Compenies.

Dakika chache za mwanaume huyu kusanifu mandhari ya nje , kama mtu ambaye alikuwa akitafuta dosari , hatimae mlango wa ofisi yake ulifunguliwa na alionekana kijana mwenye nywele za Marasta akiingia na kumfanya bwana huyu atambue uwepo wa kuingia kwa mtu ofisini kwake.

“Boss nimafanikiwa kupata taarifa yake”Aliongea bwana huyu kwa heshima huku akisogelea Meza ya bei ghari iliokuwa hapo ofisni.

“Nipe ripoti”Aliongea CEO Abu huku akikalia kiti chake na kisha alipokea bahasha iliokuwa mikononi mwa Marasta na kisha aliifungua na kuanza kupitisha macho yake huku akizidi kushangazwa na kile anachokisoma.

“Una uhakika hii ripoti ni sahihi , haujaichanganya na ya mtu mwingine”

“Ni sahihi kabisa bosi , vyanzo vilivyonipatia hio taarifa ni vya kuaminika”Aliongea Marasta.

“Unaweza kwenda , lakini nataka mumfatilie huyu mtu na mnipe taarifa zote kwa kila anachokifanya”

“Sawa bosi”Alijibu na wakati huo huo simu ya mezani ilitoa mlio kuonesha inaita , alinyanyua mkonga huku akimpa ishara Marasta kuondoka.

“Boss kuna mgeni wako”Ilikuwa ni sauti ya katibu Muhtasi wake afahamikae kwa jina la Sarah.

“Sawa mruhusu”Aliongea Abu na ndani ya dakika chache mlango ulifunguliwa na mwanaume mzee alievalia suti yake ya aina ya Navy black , akiwa anapata sapoti kwenye mkongojo uliokuwa unang`aa kwa madini ya Shaba, mzee huyu licha ya kuonekana umri wake umeenda lakini Afya yake haikuwa mbaya sana.

“Mr Alex ! karibu sana”Aliongea Abuu kwa sauti ya kiheshima huku akinyanyuka na kumkaribisha mzee huyu na kwenda kukaa kwenye masofa ya gharama yaliokuwa ofisini hapo.

Mzee huyu alimwangalia Abuu kwa namna flani ya kukatishwa tamaa , na kisha aliketi huku akivuta pumzi.

“Ni ujinga gani unafanya Abuu mpaka kunifanya nije mwenyewe ofisini”Aliongea mzee huyu kwa ghadhabu huku Abu akionekana ni mwenye kujua kosa lake.

“Nisamehe sana baba, najua mpango wa awali ulifeli lakini naamini mpango B utafanikiwa”.

“Swala sio mpango A wala Mpango B ninachotaka kujua ni kwanini swala la The Doni linachelewa kufanikishwa, nimekupa uongozi wa kampuni yangu kwakuwa nilikuwa najua uwezo wako , kwanini swala dogo kama hili linashindikana”Abuu kimya , alionekana ni mwenye kutetemeka.

“Anza kuniambia ni kipi kilifanya mpango wako wa kwanza kushindwa na huo mpango wako B ukoje na kama mipango yote ni ya kijinga nitakufukuza na kumpa mtu mwingine wa kuongoza makampuni yangu , siwezi kuvumilia ujinga katika swala hili”.

Mzee Alex ni mmiliki wa makampuni ya JR yote yaliokuwa yametapakaa ndani na nje ya nchi, makampuni yake yalikuwa yakitoa huduma nyingi sana kuanzia Maradhi , Nguo na chakula.

Mzee Alex alikuwa ni moja ya matajiri wakubwa ndani na nje ya taifa la Tanzania na alikuwa ndio kiongozi mkuu wa makampuni haya akihudumu kwa muda mrefu kama mkurugenzi mtendani na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi , miaka miwili nyuma alistaafu katika nafasi yake ya ukurugenzi mtendaji na kumpa nafasi hio kijana wake aliemlea afahamikae kwa jina la Abubakari Hamadi , moja ya sababu kubwa ya kumpatia nafasi hio kijana huyo ni kutokana na kwamba Mzee huyu katika uzao wake hakuwahi kubahatika kuwa na mtoto wa kiume , kwani watoto wake wote wawili walikuwa ni wa kike , huku Abu akiwa ni mtoto aliemlea na kumchukulia kama mwanae , ukijumlisha uwezo mkubwa wa akili wa kijana Abuu na ukaribu wao , aliona anafaa kuongoza makampuni yake na ndio hapo alipomteua kuwa mrithi wake.

*****

Alijikuta akiwa ni mwenye kukasirika mara baada ya kusikia neno ‘kahaba’ likitoka katika kinywa cha mwanaume aliekuwa mbele yake , mwanaume ambae kwa muonekano wake hakuwa kitu mbele yake , moja ya hasira aliokuwa nayo si kutokana na yeye kuitwa kahaba na mwanaume huyu ila ni kutokna na kutokuwa kwake makini mpaka kujikuta akitolewa usichana wake alioutunza miaka mingi tokea ajitambue , licha ya kusumbuliwa na wanaume mbalimbali , wenye sifa tofauti kubwa na ndogo , lakini kosa dogo alilolifanya katika maisha yake la kuamini watu , lilimpelekea kuingia katika mikono ya mwanaume aliekuwa mbele yake , ambaye baada ya kumuangalia kwa muda aliona hana hadhi yoyote ya kuwa nae katika ulimwengu wa mapenzi.

“Naitwa Edna Adebayo na sio kahaba kama unavyonitambua”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti yake nyororo huku akimwangalia Roma kwa sura iliojaa kujiamini , kama vile hakukuwa na kitu kilichotokea kati yao.

“Kama sio kahaba wewe ni nani , au kwasababu upo kwenye mjengo kama huu wa gharama kubwa , kifupi wewe ni kahaba wa hadhi ya juu ambaye kapuku kama mimi nilikuotea na kukufaidi”Aliongea Roma na kuzidi kumchafua roho mwanamke huyu na kwa Roma ni kama alikuwa amekusudia kuongea hayo maneno ili kumsoma mwanamke huyu aliokuwa mbele yake , kwani kuna kitu tokea aingie hapo ndani na kumuona huyu mwanamke ashakigundua , hakuwa mjinga kiasi cha Rami kuona mwanamke anafahamika kwa jina la ‘Bossi’ kuwa kahaba kama alivyomdhania siku tatu zilizopita.

Lakini licha ya Roma kutamka maneno hayo kwa mwanadada huyu , alionekana ni mwenye kuzuia hasira zake zisitawale akili yake.

“Naomba uketi , nina mazungumzo na wewe”Aliongea kwa sauti ya upole huku akitangulia kukaa yeye na Roma alitabasamu na kisha kuketi.

“Nimeitikia wito , naomba uende moja kwa moja kwa lile uliloniitia” Aliongea Roma na kumfanya mwanadada huyu agundue mwanaume aliekuwa mbele yake ni wa namna gani , kwani alitegemea kuona Roma kuwa katika hali ya uoga kama tu angegundua uwezo wa kipesa aliokuwa nao , lakini kila kitu kilimjibu kivingine , kwani kijana huyu alionekana kujiamini mno , jambo ambalo lilimfanya aone maamuzi alioyafanya nisahihi , alichukua glasi yake ya wine iliokuwa kwenye meza ya kioo na kisha alikunywa mara mbili na kisha akaweka chini kwa mapozi ya kike .

“Naomba unioe”Aliongea mwanadada huyu , huku akionekana ni mwenye kuanza kukosa ile hali ya kujiamini aliokuwa nayo mwanzo.

Kwa upande wa Roma ni kama mtu ambaye hakusikia vizuri maneno yaliomtoka mrembo huyu mwenye haiba ya upole , aliekuwa mbele yake.

“Inawezekana sijakusikia vizuri mrembo wangu my one night stand , naomba urudie kauli yako tafadhari”.

“Naomba unioe tafadhari , ndio jambo pekee nililokuitia mahali hapa , nitakulipa kiasi chochote cha fedha”Aliongea mwanadada huyu huku muda huu akiweka sura ambayo ni kama mtu aliekuwa akiongea na mfanya biashara mwingine swala la kibiashara.

“Unaonekana kuwa mpole , lakini pia unamuonekano wa kuwa na tabia nzuri , lakini wito wako na ombi lako linanifanya nikufikirie kivingine , labda unieleze vizuri ni kuelewe vinginevyo nakataa ombi lako , kwani ndoa sio kitu cha kuombwa na mwanamke kiholela kilichotokea baina yetu ni kosa langu na lako pia”Aliongea Roma huku akichukua Chupa ya wine na hakujali glasi iliokuwa mbele yake , yeye aigida karibia yote na kurudisha chini.

“Nataka unioe kwa mkataba wa miezi sita , baada ya hapo tutaachana kwa talaka na nitakulipa kiwango kizuri cha pesa , nafanya haya kwani kuna mwanaume ambaye baba yangu mzazi ananilazimisha kuolewa nae , mtu ambae simpendi”.

Kwanza Roma alishangaa , lakini pia swala hilo lilimpa ukakasi kwa wakati mmoja , aliona swala la baba yake Edna kumlazimisha kuolewa na mwaname mwingine ni swala ambalo linaweza kutatuliwa kwa kumkataa huyo mwanaume na si kutaka kuoelwa na mwanaume yoyote yule ilimradi tu kuepuka kuolewa na mwanume asiempenda.

“Nakataa , sitaki kujua mengi kuhusu wewe , lakini swala lako lipo nje ya uwezo wangu , siwezi kuoa mtu kwa ajili ya kujipatia pesa huku ni sawasawa na kuuza utu wangu dada, hili swala lako kuna njia nyingine za kulitatua”.

“Kaka wewe kama mwanaume unatakiwa kuwajibika kwa matendo yako , ulinitoa bar pasipo ruhusa yangu ukanipeleka mpaka geto kwako ukanitoa usichana wangu pasipo ridhaa yangu , lakini juu ya yote nikaacha kukufanya jambo baya kwani ulichofanya ni kinyume na Sheria , lakini leo hii ninakupa ofa ya kunioa tena kwa kukulipa halafu unakataa ,nina nguvu ya kukufanya uozee jera Zaidi ya miaka therathini”Aliongea mwanadada huyu kwa sauti ya hasira.

“Nakubari kosa langu Dada na nipo tayari kwa ajili ya adhabu nitakayopewa , lakini swala la mimi kuuza utu wangu kwako ni swala ambalo haliwezekani”Aliongea Roma kwa hasira huku akinyanyuka akitaka kuondoka .

“Ukipiga hatua mbili kutoka nje ya mlango najitosa nje ya hili jengo , siwezi kuishi kwa aibu ya kubakwa na mwanaume kwenye maisha yangu na nakuapia dunia nzima itajua kuwa ulinibaka na sidhani kama utakua kuishi kwa Amani, na namna pekee ni kukubali ombi langu”Aliongea mwanadada huyu ila Roma hakugeuka aliendelea kutembea kuelekea mlangoni , lakini ile anataka kushika kitasa , alisikia mlango wa dirisha nyuma yake ukifunguliwa , aligeuka nyuma na kumuona Edna akimaanisha kile ambacho anataka kufanya .

Roma alijikuta akipigwa kama na radi kwenye kichwa chake na kuchuchumaa chini kwa maumivu ya kichwa , huku picha mbalimbali za maisha yake ya nyuma zikipita kwa kasi ,mboni za macho yake zilibadilika ghafla nakuwa za kijani na ndani ya sekunde kadhaa tu kwa tukio ambalo halikueleweka lilifanyika vipi alikuwa amembeba juu mrembo Edna huku akimrudisha kwenye sofa , kitendo hicho hata kwa mrembo huyu ambae machozi yalijaza mboni za macho yake alishangazwa na kitendo hiko.

“Sipo tayari kuona mwanamke wa pili anapoteza uhai kwa ajili yangu”Aliongea Roma kwa sauti nzito baada ya kumkalisha Mrembo Edna kwenye sofa.

“Kwa hio umekubali kunioa?”

“Sina jinsi”Aliongea Roma huku akifungua chupa nyingine ya Wine na kuigida kama maji.

Edna hakujali tabia ya Roma alitoa bahasha kwenye mkoba wake na kisha alichomoa karatasi yenye mkataba wa ndoa na kisha akampatia Roma na karamu, na Roma baada ya kupokea karatasi ile , wala hakutaka kuangalia ni kipi kipo ndani ya hio karatasi , aliweka sahihi yake sehemu husika.

“Mbona husomi mkataba kwanza?

“Sina haja ya kusoma , kwani nishajua kilichopo kwenye huu mkataba”

“Kama nini”

“Kama vile kuweka umbali katikati yetu , kutogusana na mengineo mengi”

“Ni kweli , lakini pamoja ya hayo sheria kubwa ni juu ya ndoa yetu kuwa siri baina yetu”Aliongea Mrembo Edna.

“Nini kinafuata baada ya hapa?”

“Tutaenda Bomani kwa ajili ya kusajili ndoa yetu na kuwa mke na mume kihalali , lakini kabla ya hayo inabidi ubadilishe mavazi na uoge utakate”Aliongea mwanadada huyu na kisha alitoa simu yake na kutoa maagizo na ndani ya sekunde chache tu Suzzane aliingia akiwa na suti ,viatu na makorokoro mengine na Roma alienda kuoga na alitumia muda mchache sana kuoga na kuvaa nguvo ambazo aliletewa na Suzzane.

Roma alikuwa amependeza mno na suti yake ya rangi ya blue , suti ya bei ghali ambayo ilimbadilisha kwa asilimia kubwa muonekano wake na kuwa na muonekano wa kipedeshee.

Baada ya kutoka kwenye chumba hiki cha kubadilishia nguo , waliokuwa ndani ya chumba hiko ni kama wamemsahau kama fukara , licha ya Roma kuwa na sura ya kawaida sana ambayo haikuwa kama ya mahadsome boy wa mjini lakini Suti aliokuwa amevaa ilimpendezesha na kumbadilisha.

Baada ya masaa kadhaa ,Roma akiwa ameongozana na Mrembo Edna walitoka kwenye gari ya gharama sana ana ya Mercedenz Benz toleo jipya na kuingia ndani ya jengo la Bomani , na haikuwachukiua muda Mrefu kila mmoja alisaini cheti cha ndoa na kisha walipiga picha ya uthibitisho na kuwa mke na mume halali.

“My wife mrembo … Mungu kweli ananipenda siamini kama nimepata mke mrembo kama wewe”Roma alianza utani wake pasipo kumzingatia Mrembo Edna huku akijifanya kumsogelea kwa ajili ya kumkumbatia , lakini aliishia kukatwa jicho na kupigwa kikumbo na mwanadada huyu.

Waliingia kwenye gari huku dereva akiwa mrembo huyu na ndani ya madakika kadhaa ya barabarani gari ilikuja kusimama kwenye geti lenye ukuta mkubwa maeneo ya ushuani Osterbay na baada ya dakika chache geti lile lilifunguliwa na mlinzi na kisha Edna aliingiza gari na kwenda kulipaki katika eneo husika na kisha alishuka kwenye gari.

Lilikuwa ni jumba la kifahari mno lililokuwa mbele yao , Roma alishangazwa na mandhari mazuri ya jumba hili , na kwa harakaharaka aliona mtu anaeishi kwenye hii nyumba alikuwa mtu mwenye ukwasi mkubwa wa pesa.

“Hapa ni nyumbani kwa baba yangu na tumekuja hapa kujitambilisha kwake , hivyo tujitahidi kuonekana kama wanandoa kweli”.

“Unaongea kama vile sisi sio wanandoa, tunahistoria ndefu kabla hatujafanya maamuzi ya kufunga ndoa mke wangu , au ushasahau kuwa mimi ndio niliokuingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi, my babe Edna acha zako bhna”Huku akimshika mkono na kumvuta kifuani , swala ambalo juu kabisa ya gorofa ya nyumba hii alionekana mzee akishuhudia kitendo kinachofanyika , Edna alitaka kujinasua kwenye mikono ya Roma , lakini Roma alimpa ishara kwamba baba yake yupo juu ya ghorofa anawaangalia na yeye aliangaza macho yake juu na kuona kivuli cha mtu kikitokomea kwenye Balcony.

“Kwenye wanaume wote ambao nishawahi kukutana nao sijawahi kuwaza nitakutana na mwanaume ambae huna aibu kama wewe”.Aliongea Edna kwa hasira huku akitangulia kwenda mbele na kumfanya Roma atoe tabasamu la kifedhuli na kumfata.

“Baba , nimekuja kumtambulisha mume wangu , sitaki tena kusikia juu ya kuolewa na mwanaume mwingine . nampenda Roma na nitaishi nae mpaka kifo kitakapotutenganisha maana tunapendana “Huku akimwegamia Roma ambaye alikuwa ni mwenye tabasamu zito huku akimwangalia mwanaume alikuwa mbele yake kwenye sebule hii kubwa iliojaa thamani za bei ghali.

“Mzee kama alivvyosema bebi wangu hapa , mke wangu kipenzi , nyongo mkalia ini , nimekuja kujitambulisha , na naomba unisamehe kwa kuja tukiwa mke na mume , kwa majina naitwa Roma Ramoni ni mwenyeji wa hili jiji , kazi yangu ni kubeba mizigo soko la Mbagala Rangi tatu”Aliongea Roma na kumfanya mzee huyu aanze kuhema kwa taabu , huku Edna akiwa ni mwenye kushangaa namna ambavyo Roma alikuwa akijiamini na kukosa aibu.

“Unasemaje wewe , kikaragosi .. Ednaa..!! ni laana gani unaniletea ndani ya familia yangu??”Aliongea mzee huyu huku akikaa na kuanza kuhema kwa taabu , lakini wawili hawa hawakuwa ni wenye kujali.
INAENDELEA .
 
SEHEMU YA TANO

Licha ya mzee huyu kwa Roma kujitambulisha kama Mbeba mizigo , hakutaka kuamini kirahisi hivyo , alipiga simu mahali na kuomba taarifa ya Roma na ndani ya dakika chache alitumiwa na kuianza kuisoma huku akionekana ni mwenye kushangazwa na taarifa hio.

“Haiwezekani , kama hii ni kweli kwanini afanye kazi inayomshusha hadhi yake, hata kama hii ripoti ni sahihi siwezi kukubali Edna aolewe na mwanaume kama huyu ,Edna ni mtu mkubwa haendani na huyu mpuuzi isitoshe nikiruhusu ndoa hii nitakuwa kwenye wakati mbaya na The Doni ”Aliongea mzee huyu huku akikaa chini kwenye sofa huku akiendelea kufikiria.

“Abuu alishindwa vipi kumdhibiti Edna nilimpa kazi ya kuhakikisha anamuweka kwenye himaya yake na kumuoa ili mipando yetu iende sawa , lakini kakwama katika hili , huenda nilikosea kumchagua kama mwanaume wa kuwa na mwanangu , Hebu ngoja nimpigie simu huenda hata hili swala halifahamu”Aliongea Baba yake Edna afahamikae kwa jina maarufu kama Mzee Adebe kifupi cha Adebayoo.

“Abu umeshindwae kumdhibiti Edna… amekuja leo kumtambulisha Mume wake , huo mpango uliokuwa unajigamba nao uliishia wapi, Vipi swala la The Doni tunalikamilishaje?”

“Mzee naomba utulie uniambie vizuri nini kimetokea?”Aliongea Abuu kwa pupa .

“Muda mchache Edna alikuja nyumbani kwangu na mwanaume aliejitambulisha kwa jina la Roma anaefanya kazi kama mbeba mizigo kutoka Rangi tatu na Edna amesema ni Mume wake kihalali na hataki kusikia ndoa tena na wewe ,hivi unaniambia umezidiwa kete na mtu kama Roma wewe”Aliongea mzee huyu kwa hasira na upande wa pili wala haukutoa jibu Zaidi ya simu kukatwa.

“My wife , nimejitambulisha vizuri eh”Aliongea Roma huku akimwangalia Venus aliekuwa makini na usukuni , lakini baada ya kutembea hatua kadhaa , alikamata breki na kusimamisha gari na kisha alimuamuru Roma kutoka kwenye gari yake, na Roma hakuwa mbishi alitoka , na alishangaa kurushiwa kadi kwa kupitia dirishani.

“Hakikisha saa moja kamili upo nyumbani , mahali unapotakiwa kufika angalia kwenye hio kadi ole wako uchelewe ”Aliongea mwanadada huyu kwa hasira na kisha alitoa gari yake hio kwa spidi na kutokomea akimuacha Roma kwenye hali ya mshangao.

“Mwanamke ana kisirani huyu , au bado ana hasira na mimi ya kumtoa bikra yake”Alijiongelesha huku akiangalia saa kwenye kijisimu chake na kuona ni saa kumi na nusu , aliangalia kadi iliokuwa kwenye mikono yake na kuona mahali ambapo anatakiwa kwenda kwenye makazi yake mapya.

“Mwanamke anadhambi huyu yaani anataka nitembee kutoka hapa Moroco mpaka Kigamboni”Alijisachi mfukoni na kukumbuka kuwa hakuwa na kitu mfukoni kwani nguo alizokuwa amevaa ni mpya na za kwake zilizokuwa na malipo aliziacha kule hotelini.

“Huyu ndio mke wangu niliekubali mwenyewe kumuoa , anamuacha mume wake barabarani , kazi ninayo”Alijiongelesha huku akitembea kwa umbali mrefu mpaka pale magari yaliposimama kwenye mataa , wakati akiwa anakagua magari hayo mara aliona mwanamke mmoja mrembo akinunua maji akiwa ndani ya gari aina ya Aud , wakati huu magari yakiwa yamesimama.

Roma alisogelea gari hili na kisha alisubiria biashara ile iishe atekeleze jambo lake lililompeleka hapo.

“Hey mrembo ! mambo”Alisalimiana na mwanadada huyo na kujibiwa bila dharau na kuona yupo mahali sahihi.

“Sasa mrembo naomba unisaidie jambo , mke wangu kaniacha njiani na sina kitu mfukoni hata hea ya nauli , naomba unisaidie kiasi chochote nipate nauli ya kunifikisha Kigamboni”Aliongea Roma bila aibu na mwanadada huyo alimwangalia Roma kwa mavazi yake na kuona huenda kuna ukweli ndani yake kwani Suti na kiatu alichovaa kilionekana cha bei ya juu na ni watu wachache sana wana uwezo wa kumudu aina hio ya mavazi.

“Pole kaka hela hii , hapa nadhani inatosha”Aliongea mwanamke huyu na kumpatia noti ya elfu tano Roma na hapohapo gari zilianza kuondoka na hata Roma alishindwa kutoa shukrani yake , ila alifurahi alikuwa amepata hela ya nauli.

Muda wa saa kumi na mbili na Nusu Roma alikuwa mbele ya geti kubwa ambalo kwa ndani ya fensi hii lilionekana jumba kubwa la kifahari ndani ya mtaa huu uliokuwa ukifahamik kwa jina la Sunlight Villa Hub , ni mtaa ambao hakukuwa na nyumba ya kizembe , majumba yote yaliokuwa yanapatikana ndani ya eneo hili yalionekana kuwa ni ya kifahari sana na hili lililifanya eneo hili kuwa maarufu kama eneo la Matajiri ndani ya mji huu wa Kigamboni.

Roma aliminya kengere baada ya kuona yupo mahali sahihi na ndani ya dakika , alifungua bwana mmoja mweusi alievalia suti huku sikioni akiwa na visikilizishi.

“Wewe ni nani?”

“Mimi ni Roma na ni baba mwenye nyumba kwanzia siku ya leo a.k.a boss wako mpya ”Aliongea Roma huku akiwa ameweka tabasamu na kumfanya mlinzi huuyu ashangae na kuona chizi wa leo alikuwa wa aina yake.

“Sasa Bosi wangu mpya kutokana na kwamba wewe ni chizi msafi leo naomba uondoke kimya kimya kabla sijachukua maamuzi makubwa”.Aliongea bwana huyu huku akimwangalia Roma kwa kumtathimi, lakini wakati akiendelea kumwangalia Roma ,mara alihisi uwepo wa mtu nyuma yake na aligeuka .

“Madam Boss..!”Aliongea kwa hali ya mshangao baada ya kumuona Edna alievalia gauni lililompendeza lililomfikia magotini na kumfanya aonekane kama malaika kiasi cha mwanaume huyu mlinzi kumeza mate ya kimatamanio.

“Nani yupo mlangoni Derick??” Aliuliza Edna na kabla Derick hajajibu alijishangaa akivutwa nje kwa spidi ambayo hakuitarajia na Roma kuingia ndani.

“Bebi wife ni mimi mumeo nimefika ndani ya muda..hehe bebi usiniambie ulikuwa ukinisubiria??”Aliongea Roma huku akiwa ni mwenye kuweka tabasamu usoni , akinyoosha mikono kuashiria anataka kumkumbatia , ila Edna hakumjali Zaidi ya kumkwepa.

“Derick huyu ni mume wangu Anaitwa Roma , kwanzia leo ataishi hapa na mumpe heshima yake kama mume wangu”Aliongea Edna kwa lugha ya kiupole ila iliojaa usiriasi kuonyesha kile anachokisema.

“Sawa Madam bosi”Aliitika Derick kwa kubabaika kwani sekunde kadhaa alimdhania mwanaume aliekuwa mbele yake kama kichaa msafi

“Utawaambia na wenzio”Aliongea Edna kwa sauti yake nzuri na kumfanya Roma atabasamu kwa utambulisho huo na akajiona angalau licha ya mwanamke huyu alikuwa akimdharau ,lakini afadhali alikuwa akimpa heshima yake kama mume.

Derick aliekuwa amesimama alishangazwa sana na utambulisho huo , kilichomfanya bwana huyu kushangaa ni ile hali ya kutokuamini kwamba mtu kama Roma anaweza kuwa mume wa bosi wake , kwake Edna alikuwa mzuri na mrembo sana kumilikiwa na Roma hivyo matarajio yake ni kuona mtu mwenye hadhi ya juu Zaidi kuwa mwanaume wa bosi wake , lakini leo jambo hili lilimshangaza , lakini hakutaka kujiuliza maswali mengi , Zaidi ya kutii na alipanga kumuomba msamaha Roma pale atakapo pata nafasi ya kufanya hivyo kwa kitendo cha kumuita kichaa.

“Kuna wanaume wamezaliwa na bahati sana , yaani jamaa kama yule ndio anamsugua bosi daah! Kweli wanawake sio wakuwaelewa kabisa”Alijiongelesha Derick mpaka pale aliposhituliwa na mlinzi mwenzake.

Roma alikubali uzuri wa nyumba aliokuwa akiishi Edna , ilikuwa ni nyumba kubwa mno kiasi kwamba ilimfikirisha kwa wakati mmmoja kwa kazi ambayo Edna alikuwa akifanya hapa mjini.

Jumba hili lilikuwa la gorofa tatu kwenda juu , lililokuwa na mandhari ya kuvutia sana , baada ya Roma kukaribishwa ndani na Edna alipokelewa na mama mmoja mtu mzima.

“Karibu sana Mister Roma ”Roma alitikia kwa heshima huku akisubiri utambulisho kutoka kwa mke wake.

“Roma huyu ni Bi Wema ni kama mama kwangu , ndio alienilea tokea nikiwa mtoto baada ya mama kufariki, Bi Wema huyu ni Roma niliekuambia , ndio mume wangu”

“Karibu sana Roma kwenye familia , jisikie huru hapa ni kwako”Aliongea bibi huyu na Roma alitabasamu na kukubali utambulisho huo na Edna hakuwa na maongezi mengi na Roma Zaidi ya kumwachia maagizo yote Bi wema .

“Karibu sana Roma , unaonekana ni kijana wa kipekee sana mpaka Miss Edna akakuchagua kuwa mume wake , niseme tu mimi nimemuona Edna tokea akiwa mtoto na hajawahi kutambulisha mwanaume yoyote kwangu kuwa nae kimahusiano , Edna amekuwa ni mtoto mpweke sana ambae amekuwa peke yake mpaka pale aliporithishwa kampuni na marehemu mama yake, hivyo nakuomba usije ukaamuumiza”Roma alipewa nasaha hizo na bibi huyu na kuzingatia , baada ya hapo alionyeshwa chumba chake ambacho atakuwa analala.

Chumba chake kilikuwa kwenye Floor ya pili , kilikuwa ni chumba kikubwa cha kifahari kilichokuwa na kila kitu kwanzia Tv kubwa ya Inch 64 , pembeni kulikuwa na meza iliokuwa na komputa kubwa ya kamouni ya Apple , masofa na makorokoro mengine ya gharama , Roma alilirdhika na chumba hiki na kumshukuru Bi wema kwa maandalizi ya chumba chake.

Roma aliingia bafuni na kuoga na kisha alifungua kabati la nguo na kukuta nguo nyingi zinazomtosha zikiwa zimepangiliwa kwenye kabati , alijiuliza maswali nin muda gani nguo hizo ziliwekwa humo , ila majibu yake aliyapata kwani nguo zote zlionekana kuwa mpya.

Baada ya kupigilia tisheti iliomkaa vyma na kipensi chake , alijilaza kitandani mpaka pale alipopitiwa na usingizi , alikuja kushituka usiku wa saa mbili na ilikuwa ni muda wa chakula cha usiku , alishuka mpaka chini sehemu ya chakula na kuungana na Bi wema na Mke wake na kisha kukaa.

Jumba hilo lote lilikuwa likiishi wanafamilia wawili tu , jambo ambalo lilimshangaza sana Roma.

“Babe Edna usiniambie jumba lote hili mnaishi wawili tu”

“Ndio Mr Roma tupo sisi tu na Miss hana ndugu wengi zaidi ya baba yake”

“Kwa hio na baba yake kule anaishi peke yake?”.

“Miss na mimi tulikuwa tukiishi nae wote ila baada ya wao kugombana mara kwa mara ndio tukahamia hapa”

Roma alitikia huku akiendelea kula bila wasiwasi kama vile ni wa siku nyingi ndani ya nyumba hio , kwani wakati wenzake walipokuwa sahani ya kwanza yeye alikuwa ameongeza Zaidi ya mara tatu na kumfanya Bi wema kutabasamu , lakini upande wa Edna alimwangalia kwa kumshangaa huku akijisemea ndani kwa ndani kuwa Roma ni mwanaume ambaye hakuwa na aibu hata kidogo

“Bi wema unajua kupika sana , mpaka miezi sita ikiisha nitakuwa na kitambi”.

“Kweli eh , kula kabisa wala usione wasiwasi na kuna chakula kingine kimebaki jikoni”

“Asante leo ngoja nipumzike mpaka siku ya kesho”Aliongea Roma na baada ya kula hakukuwa na stori sana na Edna kwali bado alionekana kumchunia mno na hakutaka stori nyingi Zaidi ya mwanadada huyo kupandisha juu kabisa kwenda kwenye chumba chake cha kujisomea.

Siku iliofuata asubuhi Roma aliamka mapema na alionyeshwa chumba cha mazoezi na Bi wema na kuingia kuanza kufanya mazoezi , alivyomaliza chai ilikuwa tayari na Edna alievalia gauni lililompendeza kama malaika alionekana akishuka huku akiwa na mkoba wake , aliweka kwenye sofa na kisha aliungana nao kwa ajili ya chai.

“My wife umeamkaje?”

“Safi”

“Niko poa babe”aliongea Roma ila hakuzingatiwa sana , kwani Edna aliendelea kunywa chai iliokuwa Zaidi ya chakula cha mchana kwa wingi wa vyakula , kwa Roma hakuwa mnyonge, kwani alikula kama hatokula tena .

“Babe Edna nikitoka hapa narudi Mbagala kazini kwangu”

“Hapana kuanzia leo ile kazi yako achana nayo, tafuta kazi nyingine yenye hazi na ufanye hapa utakaa lakini kumbuka wewe ni mwanaume hela ya matumizi siwezi kukupatia”Aliongea Edna kwa msisitizo na kisha alimuaga Bi Wema kama anaelekea kazini kwake na kuondoka.

“Ni kweli Mr unapaswa kuacha hio kazi , zipo kazi nyingi ambazo zinaendana na wewe na unaweza kufanya”.

Roma alifikira kwa muda na kuona maneno yao yana mantiki na aliona ni bora akafanya hivyo , lakini aliona ugumu wa kupata kazi inayoendana na hazi yake.

Baada ya kuwaza kwa muda aliona ni muda muafaka kwanza wa kurudi Mbagala kwa ajili ya kuchukua vitu vyake, alimuaga Bi Wema na kabla hajaondoka ,bibi huyu alimwambia amfuate nyuma ya nyumba na ndani ya dakika chache walikuwa mbele ya magari yaliokuwa yamehifadhiwa , yalikuwa ni magari kumi ya kifahari ambayo yalikuwepo hapo ndani.

“Miss Edna alinipa maelekezo kama ukitaka kutoka unaweza kuchagua gari yoyote unayopenda na itakuwa yakwako, nadhani unajua kuendesha gari”

“Ndio Bi wema niko vizuri”Aliongea kwa kutabasamu akiangalia magari hayo , kwani moja ya Starehe pia aliokuwa akipenda Roma ni kuendesha magari .

Alilisogelea gari moja aina ya BMW X7 na kumwabia Bi Wema atatumia gari hio kwanzia siku hio.

Basi baada ya kupewa ufunguo wake , kwa mbwembwe zote alitoa gari nje ya geti na safari ya kuelekea Mbagala Rangi tatu ikiwa imeanza.

“Leo watanikoma, ,Juma na wenzake wanaongea sana”Alijiongelesha Roma huku akikanyaga pedeli na kuongeza mwendo , huku kila alipokuwa anapita na gari lake watu walikuwa wakilikodolea macho.

Ni muda wa saa nne za asubuhi ,Roma alisimamisha Gari katika soko La mbagala Rangi tatu na kisha alishuka , huku wengi waliokuwa wakimfahamu wakimwangalia kwamshangao kama hawakuwa wakimjua.

“Oy Roma kaka ni wewe?”

“Nni mimi kaka , vipi mishe za hapa?”

“freshi kaka umebadilika sana aisee”

“Hahaha.. kawaida Seif”Aliongea Roma baada ya kusalimia na Seif aliekuwa akiuza Zabibibu ndani eneo hili la Stendi ya Rangi Tatu.

“Oya mwanaaa…!!! Aaah Romaaa .. daah ni wewe kweli?”

“Ni mimi Yusuph , hujanifananisha , ni maisha tu haya hahaha.. unaweza ukalala masikini ukaamka tajiri ndio kilichonitokea”

Yusuph hakuwa ni mwenye kuamini hivyo kiharaka ,Roma alimtafuta Juma mpaka akampata katikati ya soko akiwa anashusha mihogo kwenye kirikuu.

“Juma!” Roma aliita na kumfanya Juma ashanagae.

“Roma!” Juma alianza kumkagua Roma kuanzia juu hadi chini na akawa sio mwenye kuamini kama aliekuwa mbele yake ni yule aliekuwa akimdharau kiasi cha kumuita fukara na kutotaka amsogelee dada yake.

“Yes bro nimerudi , kuchukua mazaga na kumalizia hela ya kodi unayonidai nahamia town man”Aliongea Roma na kumshangaza Zaidi Juma , ambae hakufurahi sana kumuona Roma kwenye hali kama hio kwani siku zote alikuwa akijilinganisha nae na kuona yeye ndio mwenye unafuu mkubwa wa kimaisha , lakini kwa muonekano mpya aliomuona nao Roma aliona bwana huyo sio level zake.

“Poa ngoja nije tuelekee maana nilikuwa pia na wazo hilo hilo la kukuambia utafute mahali pengine , ila kama umepata itakuwa poa sana”Aliongea Juma huku akionekana sio mwenye kufurahia mafanikio ya ghafla ya Roma na Roma alitikia kwa kichwa na kisha alimwambia amsubirie anakuja na Juma alimwambia poa.

Roma alienda na kuchukua Gari yake na kuja nayo mpaka eneo alilokuwepo Juma , mwanzoni Juma hakujua nani anaendesha gari hio, na akawa mmoja ya watu wanaoishangaa.

Roma alishusha kioo na kumuita Juma alizidi kushangaa Zaidi baada ya kugundua anaendesha gari hio ni Roma.

“Roma ni wewe mwanangu??”

“Ndio ni mimi Mama Nasra”

“Hio gari ni ya kwako?”

“Ndio Mama Nasra hii nimepewa kama zawadi na mke wangu”Aliongea Roma na kuwafanya waliosikia neno ‘mke’ washangae.

“Umeoa lini Roma mbona hatujui muda wote huo kama una mke?”

“Nimeoa jana Mama Nasra ilikuwa ghafla na nilishindwa kupata muda wa kuwaambia”Aliongea Roma na watu walishangaa huku wakizidi kujawa na maswali ni mke gani amekubali kuolewa na mtu kama Roma asiekuwa mbele na nyuma na mpaka kumdhawadia gari.

“Ama kweli usimdharau mtu .. maana nyota zetu hazifanani”Alisikika mzee mmoja aliekuwa akimenya machungwa akiongea wakati huo Roma akiwa anapitisha gari lake kwa mbwembwe kielekea Bias.

Ndani ya gari hakukuwa na stori nyingi kati ya Juma na Roma , japo Juma muda wote macho hayakuwa yakitulia , kwenye maisha yake hakuwahi kuwaza kama atakuja kupata hata lift kwenye gari kali kama hii.

“Hongera kaka kwa kupata mke mwenye hela , nadhani Najma atakusahau na kuendelea na maisha yake sasa”.Roma hakujibu kitu Zaidi ya kutabasamu na kutingisha kichwa , iliwachukua dakika tano kufika Bias.

Roma baada ya kusimamisha gari huku majirani wakiwa wanamshangaa kwani ni siku ya jana tu habari zake za kutorudi zilikuwa zimesambaa kuwa hakurudi jana yake baada ya kuja kuchuliwa na mwanadada alievalia suti , kuna waliohisi huenda alitekwa nyara , na kuna wengine waliokuwa wakidhania huenda Roma alikuwa mtu mkubwa tu na alikuuwa akijifanyissha kuwa mbeba mizigo , kwani kitendo cha kufuatwa na mwanadada ambae alikuwa mrembo , kiliwashangaza wengi na hakikua cha kawaida na cha bahati mbaya , kila mtu alilipa wazo lake sababu na kuwa na nguvu ndani ya kichwa chake.

Moja ya watu waliokuwa katika hali ya wasiwasi ni mwanadada Najma , alikuwa ni mwenye mawazo kweli kiasi kwamba hata kazini hakuweza kwenda kwa siku hio , kwani ndani ya kichwa chake alikuwa akimuwazia Roma tu , alikuwa na taarifa zote zilizokuwa zikimhusu Roma jana yake kufuatwa na Gari la kifahari aina ya V8 jambo ambalo alipojumlisha na mawazo ya kimbea ya watu aliona huenda kuna ukweli wake, Roma hakuwa mwenzao kama walivyodhani , lakini licha ya hivyo bado aliamini kwamba Roma alikuwa akimpenda yeye na pia yeye alikuwa akimpenda na hivyo hakukuwa na kitu ambacho kinaweza kuwatenganisha, hayo ndio mawazo aliokuwa nayo Najma karibia asubuhi yote kaka yake alipoelekea kazini.

Najma alifkiria matendo ya kikarimu ambayo Roma ashawahi kuyafanya juu yake , alikumbuka kipindi Roma alivyomsaidia kiasi kikubwa cha pesa Zaidi ya laki nane kwa ajili ya kwenda kulipia malipo ya nusu umiliki wa shule aliokuwa akifundishia huku Roma akimwambia kuwa hakupaswa kulipa kiasi hicho na achukuliea kama fedha zilizotoka kwa ndugu , alifikiria pia siku ambayo pia aligharimikia matibabu yake kiasi cha shilingi laki moja huku Roma akikataa malipo , kwake aliona matendo yote hayo yalikuwa ni ya kimapenzi, aliamini Roma alikuwa akimpenda yeye na kikwazo kikubwa ilikuwa ni kaka yake, lakini licha hivyo Najma aliamini kama siku zote ataendelea kumpenda Roma basi siku moja kaka yake atakata tamaa na kuwaruhusu wawili hao wapendane.

Najma aliendelea kukumbuka miezi sita nyuma siku ambayo Roma alifika ndani ya nyumba yao na kumkuta akifua nguo muda wa jioni na kumueleza shida yake kwamba alikuwa akitokea mikoani na alikuja mahali hapo kwa ajili ya kutafuta uwezekano wa kupata chumba , hio ndio siku ambayo Najma alijikuta akivutiwa mara moja na mwanaume huyo , hakujua ni nguvu gani iliokuwa ikimvuta kwa mwanaume huyo , lakini katika akili yake aliona kuwa mtu aliekuwa mbele yake hakuja hapo kwao kwa bahati mbaya na ni Allah ndie ambae amemleta hapo kwake , na mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ndio mume wake aliekuwa akimuota kila siku , siku hio ilichuku takribani ya madakika kadhaa kwa Najma kuacha kumshangaa Roma na kumtathimiini mwanaume huyo huku akiwa si mwenye kuamini kwamba mume wake hatimae amefika na kuja kumchukua.

“Kipo chumba kaka .. karibu”Najma aliitikia mara moja huku akiwa ni mwenye kupagawa .. alimuonesha Roma chumba hiko huku jambo moja ambalo Roma alikosa kwa muda huo lilikuw ani godoro na Najma bila ya kujifikiria mara mbili alimwambia Roma atamsaidia Godoro na atalalaia bure mpaka pale atakapokuwa na uwezo wa kununua la kwake , upande wa Roma alitabasamu na kupendezwa na roho nzuri aliokuwa nayo Najma , kwani mwanamke aliekuwa mbele yake sio kuwa mzuri tu na mrembo lakini pia alionekana kuwa mwenye kujali watu pasipo ya muonekeano wao, kwanzia siku hio Roma alianza kuwa na ukaribu na mrembo Najma , na hata pale kaka yake aliporudi kutoka kazini na Najma kumpa habari ya ujio wa Roma ,Juma yeye hakuwa na shida kwani alimini ujio wa Roma ni ongezeko la pesa katika walipa kodi.

Kutokana na Roma siku za mwanzoni kushinda Nyumbani walijikuta wakiwa karibu sana na Najma na kuzoeana kwa haraka , kwa upande wa Najma kila siku alipokuwa akikaa na Roma na kupiga stori kitu kipya kilijijenga ndani ya moyo wake.

“Huyu ndie mwanaume niliekuwa nikimuota , ni mwenyewe na sijakosea bila shaka

Ndio sentensi aliokuwa akiongea Najma kila siku wanapokutana na Roma na kupiga Stori , mwanadada huyu alijikuta akijaa Huba ndani ya moyo wake dhidi ya Roma, matendo yote ya Roma kwa Najma yalikuwa yakiongeza kipande cha upando ndani ya Moyo wake.

Hata pale Roma alipoanza kuzoeana na kaka yake na wakawa marafiki na kuanza kufanya wote kazi katika soko la Rangi Tatu,Najma bado alisubiri muda wa kurudi kwa Roma awafungulie amuone Roma wake moyo wake utulie ,Roma nae kila alipokuwa akirudi kwenye chumba chake alikuta chakula kitamu kikiwa kinamsubiri aliishia kutabasamu na kula chakula hiko na kisha kuacha kimemo cha Asante kwa Najma , na mrembo huyu kila siku alipokuja kuchukua vyombo na kukuta kikaratasi hiko cha Asante na kusifiwa kama mpishi mzuri kiliufanya moyo wake uzidi kuloea juu ya Roma , kila kitu kwake Najma ilikuwa ni Roma , akila chakula ilikuwa ni Roma , akioga ilikuwa ni Roma ,, ilikuwa ni Roma , Roma, Roma kila siku ,kitendo ambacho kilimfanya kaka yake Juma kugundua dada yake alikuwa amempenda Roma.

Gunduzi hio ya mapenzi ya dada yake juu ya Roma ndio yalioibua hali ya chuki baina ya wawili hao , upande wa Juma aliona dada yake alikuwa mzuri sana kuolewa na mwanaume Fukara kama Roma hivyo mapenzi hayo kwake hakutakata yatokee , kila siku alijitahidi kumshawishi Roma wachelewe kurudi na kuwahi kazini , ili wawili hao wasipata nafasi ya kuonana , lakini bado Juma alishindwa kuwazuia wawili hawa kutokuwasiliana , kwani baada ya siku kadhaa Roma alinunua simu na namba ya kwanza kumpigia katika simu yake ilikuwa namba ya mrembo Najma, walitakiana heri kwa kila waamkapo wakielekea kazini na walitakiana heri walakati wa kulala , walishirikishana mambo mengi, mapenzi baina yao yalionekana kuwa na nguvu sana, matendo ya Roma yalionyesha wazi alikuwa akimpenda Najma na matendo ya Najma yalioneysha anampenda Roma ,Licha ya wawili hawa kutokuongea kuwa wanapendana lakini matendo yao yalikuwa ndio kila kitu kwao.

Baada ya muda mrefu wa Juma kuwa na mawazo , leo hii anajikuta moyo wake ukitulia mara baada ya Roma kupata mke , lakini mwanzo wa swala hili linaibuka swala linguine katika moyo wake na swala hilo lilikuwa juu ya mafanikio ya Roma , hakuamini mtu aliekuwa akimdharau leo hii alikuwa na mafanikio makubwa kuliko yake , jambo hili kwake hakutaka litokee kabisa.

“Nitamwendea kwa mganga huyu , na siku sio nyingi anakuja kulilia hapa nimpe hiki chumba , kwanza hela sio zake akiachwa anakuwa masikini , nitahakikisha mke wake anamuacha huyu mpuuzi”

Juma aliingia ndani ya nyumba yao na kisha alitoa ufunguo na kurudi nje na kumpatia Roma , Roma baada ya kuingia ndani ya chumba chake , alishangaa kukuta upekuzi uliokuwa umefanyika ndani ya hiki chumba,Juma nayeye alishangaa , kwani ni asubuhi tu alifunga , lakini hali aliokuta humo ndani ilimshangaza , alifikiria ni nani anaweza kufanya jambo hilo kwani mlango ulikuwa umefungwa na Zaidi pia aliukuta umefungwa kama alivyofunga, na ufunguo alikuwa akijua yeye tu lakini hakutaka kujiuiza maswali sana , kwanza aliamini Roma hana kitu cha thamani hapo ndani kiasi cha kuwaza.

Roma yeye alishangazwa na upekuzi huo , lakini yeye hakujali Zaidi , alisogea mpaka lilipokuwa gororo lake na kulinyanyua juu na akaangalia chini na alijikuta akivuta pumzi ya ahueni.

“Inaonekana walichokuwa wakikitafuta hawajakipata”

Aliongea Roma na kisha alichuchumaa na kusogea mpaka sehemu ambayo ilikuwa na alama ya mchoro wa Zero , wakati huu Juma alikuwa yupo nje akimpa nafasi Roma ya kufanya mambo yake amkabidhi hela zake .

Baada ya Roma kusogelea alama ile ya Zero alivuta pumzi na kukunja ngumi na kwa spidi alipiga katikati ya lile eneo na pakabaduka na kuacha uwazi , Roma alitoa mchanga na kiisha alivuta mfuko wa Rambo na kuutoa nje na kisha akaufungua , ndani ya mfuko huu ulionekana kuwa na kiboksi flani kirefu mfano wa mstatiri , alikifungua kiboksi hiki na kuona vitu vyake vyote vipo, alitoa kiburnguti cha hela na kutoa hela iliosomeka kwa mfumo wa Dola , ilikuwa ni Dolla Mia ambayo kwa hela za kitanzania ilikuwa ni Zaidi ya laki mbili, baada ya kutoa baadhi ya vitu vyake hivyo aliviingiza kwenye begi lililokuwa pembeni yake kubwa kubwa la kusafiria na kisha alisimama na kuvuta pumzi huku akionekana kama mtu anaeonekana kuaga chumba hiko, baada ya hapo alitoka nje na kumkuta Juma , Alitoa ile noti ya Dola Mia na kumpatia Juma na kumfanya ashangae , kwani Juma pia hakuwa kilaza ashindwe kujua thamani ya dolla Mia.

“Nadhani hio italipa deni langu la Kodi , lakini pia kunasehemu nimeharibu huko ndani so inayobaki itakuwa fidia”

“Sawa kaka Asante”

“Romaa..!!!”Ilisikika sauti ilioingia kwenye ngoma za masikio yake na kuitambua.

“Najma .. nilidhania upo kazini”Aliongea Roma huku akimwangalia mwanadada aliekuwa mbele yake , aliekuwa amesahau hata kuvaa Hijab kwa siku hii ya leo na kwa mara ya kwanza Roma anamuona mwanamke huyu akiwa hana Hijab na kuuona uzuri kamili wa Najma.

“Najma mzuri aisee”
ITAENDELEA KESHO JIONI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom