Dorcas kafanya jambo la msingi kutapika uhozo wa Evance na mama yake....nadhani atakuwa okey now. But also atapata msaada wa hao akina mama.....*DORCAS-17*
Baada ya kufanya hivyo, niliiona pochi ambayo Emmy alikuwa akihifadhia vitu nikahisi ilikuwa na fedha alizoachiwa na mama, nilipoifungua nikaona ilikuwa na noti za shilingi elfu kumi ambazo sikujua idadi yake.
Kwa kuwa lengo langu lilikuwa kuchukua kiasi cha fedha kwa ajili ya nauli ya kwenda Mbeya, nilizihesabu na kubaini ilikuwa shilingi hamsini na nne elfu, nikachukua elfu thelathini.
Kiasi hicho cha fedha niliamini kingenifikisha Mbeya bila matatizo, sikupenda kuchua fedha zote kuhofia ningewapa usumbufu wa kukosa fedha za matumizi wakati sikujua mama angerudi lini.
Baada ya kufanya hivyo, nilizihifadhi kwenye moja ya mifuko ya siketi yangu kisha nilichukua karatasi na kuandika ujumbe ambao hadi leo naukumbuka vizuri.
Ujumbe huo niliandika maneno haya: Emmy mimi Dorcas siyo mwizi na sitakuja kufanya kitendo hicho katika maisha yangu hata kama nitakumbana na wakati mgumu kiasi gani.
Kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wangu nimefungua kabati na kukuta pochi yako ambayo ndani ilikuwa na shilingi hamsini na nne elfu, nimechukua shilingi elfu thelathini.
Najua nitakuwa nimeharibu bajeti yenu wakati huu mama akiwa hayupo lakini naomba mnisamehe kwa sababu sina jinsi nimeamua kuchukua fedha hizo ili nifanye nauli ya kwenda kwa mama mkubwa Mbeya.
Naomba Mungu unisamehe kwa kosa nililofanya kwa sababu sina jinsi, naomba mbaki salama na kwa amani kama Mungu akipenda tuonane tutaonana na asipopenda ipo siku tutaonana mbinguni, nakupenda sana Emmy kuliko mama na Evance.
Niombee nifike salama huko niendako, mimi Dorcas.
Nilipoandika ujumbe huo niliuweka ndani ya pocho niliyochukua zile fedha, nikaweka magauni yangu mawili ndani ya begi nikapanda kitandani kusubiri kuche ili nianze safari ya kwenda Mbeya.
Nikiwa macho, Emmy alijitikisa nikajifanya nakoroma ili asijue kama tangu niliponda kitandani sikupata usingizi, akajigeuza na kuangalia ukutani na kuendelea kuuchapa usingizi.
Alfajiri na mapema wote wakiwa wamelala, niliamka nikaoga kisha nikachukua begi langu, nikafungua mlango wa nyumba kubwa nikatoka kisha nikaufunga kwa funguo na kuziingiza ndani kupitia uwazi wa chini ya mlango.
Nilipofanya hivyo, nikafungua geti la kutokea nje kwa uangalifu bila kushtukiwa na kulifunga nikashika njia ya kwenda stendi, kwa kuwa bado kulikuwa na giza nilikuwa na hofu ya kukutana na vibaka.
Nikiwa natembea nikawa namuomba Mungu anipe ulinzi ili niweze kufika salama kwani sikutka kabisa kuendelea kuishi kwa mama ambaye hakuwa na upendo kwangu.
Wakati nikitembea ghafla nikasikia kengele ya baiskeli ile nageuka ikasimama pembeni yangu, moyo ukapiga pa!
Kijana aliyekuwa akiendesha kwa sauti nzito akanisalimia kwa Kiswahili chenye lafundhi ya Kisukuma; “Wewe msichana hujambo?”
Huku nikumuomba Mungu anilinde nikaitikia salamu yake na kumwamkia, akasema marahaba kisha akashuka kabisa kwenye baiskeli ambayo nyuma alifunga kiroba na kuchomeka panga kwenye mkanda wa kaptura kubwa aliyovaa.
“Unatoka wapi na unakwenda wapi usiku wote huu?” Dorcas anasema yule bwana alimwuliza.
Nilimweleza nilikuwa natoka nyumbani naenda kupanda basi kwani nilikuwa nasafiri kwenda Mbeya, akaniuliza nilikuwa natoka nyumbani wapi, nikamwelekeza mtaa ambao ulipakana na alioishi mama.
Nilipomweleza hivyo akasema sawa na kuniuliza kama nilikuwa nasoma, nikamjibu ndiyo na kumdanganya kwamba nilikuwa naenda Mbeya kwenye msiba.
Nilipomwambia hivyo, alichomoa panga na kunikazia macho.
Alipochomoa panga, akauangalia na kuurudisha kwenye hala kisha akaniuliza nilikuwa naenda kwenye msiba wa nani, kwa hofu niliyokuwanayo awali kwamba jamaa huyo alitaka kunidhuru nilivuta pumzi na kuzishusha kwa nguvu.
Japo mama alifariki dunia muda mrefu nilimwambia msiba wa mama, alisikitika sana akachukua begi langu na kulifunga juu ya kiroba kilichokuwa nyuma ya baiskeli yake.
Alipohakikisha alilifunga vizuri akaniambia nipande kwenye bomba la baiskeli kisha nikashika usukani akaisuma kama mita mbili, akadandia na kuanza kuendesha..
Njiani, alinipa pole tena kwa msiba na kuniuliza mbona nilikuwa nasafari peke yangu nikamdanganya kwamba ndugu zangu wengine walitangulia.
Aliendesha baiskeli kwa kasi hadi sehemu tuliyokuwa tukisubiria magari, kutokana na kunionea huruma, yule bwana hakuondoka mpaka lilipokuja gari aina ya Toyota Land Cruiser ambapo dereva alisema anakwenda Nzega.
Kwa kuwa nilielewa kama ningechelewa kupanda basi huenda Emmy angeamka na kukuta ule ujumbe na kuamua kunifuata, nilipanda gari hilo ambalo ndani kulikuwa na wanawake wawili, mmoja wa makamo, kijana wa miaka 15 hivi, mtoto na dereva.
Nilijua huko mbele ningeunganisha na magari ya kwenda Mbeya, yule bwana aliyenipa lifti ya baiskeli kabla ya kuniaga alinipatia shilingi elfu tatu na kunitakia safari njema ndipo gari likaanza safari.
Gari likiwa limeanza kushika kasi, mama aliyekuwa na mtoto akanisalimia kwa kusema; “ Hujambo binti!”
Nikaitikia salamu yake na kumpa heshima yake akasema marahaba ndipo nikakumbuka kwamba wakati napanda garini hatukusalimaina.
Tukasalimiana wote na kuendelea na safari, hatukutembea umbali mrefu, yule mama akaniuliza nilikuwa nakwenda wapi, nikamwambia akasema wao walikuwa wakienda jijini Dar es Salaam lakini watasimama Nzega kwa siku moja kisha kuendelea na safari.
Nilimwambia nikifika Nzega nitaunganisha safari yangu na magari yanayokwenda Dodoma kisha huko ningepanda la Mbeya, akasema sawa.
Kama unavyojua watu mnaposafiri pamoja huzungumza mambo mbalimbali, yule mama aliniuliza jina langu na Shinyanga nilitoka kwa nani.
Aliponiuliza hivyo, sikumjibu kwa wakati akaniuliza mbona nilionekana sikuwa sawa nikamwambia sikuwa na tatizo, akanibishia na kusema alikuwa mtu mzima hivyo nisingeweza kumdanganya na kusisitiza kwa alivyonioa kuna jambo lilinitatiza.
Alipotoa kauli hiyo, dada aliyekuwemo kwenye lile gari akaniambia kama nilikuwa nina tatizo niwaambie kwa sababu kwa wakati ule nilikuwa kama ndugu yao na hata kama lingetokea tatizo wao ndiyo wangenipatia msaada.
Kama vile waliambiana, dereva naye aliniambia kama nilikuwa na tatizo niwaeleze, awali nilitaka kuwaficha lakini nilisikia sauti ikiniambia niwaeleze kila kitu kilichonitokea.
Niliwafahamisha kwamba kuna mambo yalinitatiza ndiyo yaliyonifanya niwe safarini kwenda Mbeya kwa mama mkubwa, yule mama akaniuliza ni mambo gani, nikawaeleza waelewe tu hivyo nilivyowaambia.
Yule mama na dada walibaini niliwaficha kitu wakanibana kwamba niwaeleze, nilipokumbuka mambo waliyonifanyia mama na Evance nikajikuta natiririkwa na machozi.
Jambo hilo liliwapa wakati mgumu ndipo wakaanza kunibembeleza ninyamaze na kuwasimulia kila kitu, nikaamua kuwaeleza mkasa wangu mwanzo hadi mwisho.
Nilipofika mwisho, yule mama alishindwa kujizuia kulia, yule dada akawa mpole na kuniuliza kama yote niliyowaeleza yalikuwa kweli, nikawaambia yalikuwa kweli, wakasikitika sana.
Yule kijana aliyekuwemo kwenye lile gari alisema mama wa Shinyanga pamoja na Evance walitakiwa kushtakiwa ili sheria ichukue mkondo wake, nikawaambia sikuwa na mpango huo Mungu angenilipia.
Je, nini kitaendelea?
KabisaaaDorcas kafanya jambo la msingi kutapika uhozo wa Evance na mama yake....nadhani atakuwa okey now. But also atapata msaada wa hao akina mama.....
Sent using Jamii Forums mobile app
matukio ya ubakaji huwa huchukua mda mrefu hasa kwa watendwa kusahau, huwa inawapelekea hata kwenye hatua ya kuwachukia wanaume wote dunianiDorcas kafanya jambo la msingi kutapika uhozo wa Evance na mama yake....nadhani atakuwa okey now. But also atapata msaada wa hao akina mama.....
Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseeeh ni kweli. Na hili bado ni tatizo kubwa sana, katika jamii zetu....matukio ya ubakaji huwa huchukua mda mrefu hasa kwa watendwa kusahau, huwa inawapelekea hata kwenye hatua ya kuwachukia wanaume wote duniani
Hata mbakaji akichukuliwa hatua, bado kazi bure, itachukua mda sana mtendwa kusahau tukio, hii ni kama mtoto wa kiume ashikishwe ukuta kwa lazima alafu atolewe marinda unafikiri kovu litakauka mapema ndomana ambao sio wastahimilivu huishia kujiuaWanawake wa liobakwa hata kwenye mahusiano ..wanakuwa watata sana.hasa kama mbakaji hakuchukuliwa hatua yoyote..
wanaishi na maumivu!
Sent using Jamii Forums mobile app
wengi hubakwa na wengi hukaa kimya, kuhofia fedheha tokea kwa jamiiAiseeeh ni kweli. Na hili bado ni tatizo kubwa sana, katika jamii zetu....
Sent using Jamii Forums mobile app
True...wengi hubakwa na wengi hukaa kimya, kuhofia fedheha tokea kwa jamii
Dahnasafiri
Na huwa hawapendi kuliongelea. Huishia maumivu moyoni mwaowengi hubakwa na wengi hukaa kimya, kuhofia fedheha tokea kwa jamii
Asante Shunie nlikua naisubiri kwa hamu*DORCAS-18*
Wote walimuunga mkono yule kijana kwamba nikafungue mashtaka dhidi ya mama na Evance, nikawaambia niliwasamehe na sikuwa tayari kuwashtaki,nikaanza kulia.
Kufuatia kulia, wote wakaanza kunisihi ninyamaze nikawaambia ingawa sikupenda kuwafungulia kesi na kumuacha Mungu, kitendo walichonifanyia kiliniumiza sana.
“Hata sisi tumeguswa na unyama uliofanyiwa ndiyo maana tunakushauri ukawashtaki ili sheria ichukue mkondo wake,” dereva aliniambia.
Nilimwambia sawa lakini siku moja Mungu angewahuku kwa sababu yeyote anayewafanyia wengine ubaya, malipo yake yapo hapa hapa duniani.
Walipoona sikukubaliana na ushauri wao,waliniacha tukaendelea na safari huku kila mmoja akiwa ananionea huruma, kabla ya kufika Nzega yule mama aliniita jina langu na kunipa pole kwa yote yaliyotokea na kuwalaani mama na Evance.
Mama huyo ambaye tayari alijua hata Mbeya kwa mama mkubwa nilikokuwa nakwenda hakukuwa kwa ndugu zangu wa damu, aliniomba kama sitajali niongozane naye kwenda nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.
“Mwanangu, mkasa wako umenigusa sana, kama hautajali naomba twende tukaishi wote nyumbani kwangu Dar es Salaam, nitakutafutia shule ili uendelee na masomo na utakuwa miongoni mwa watoto wangu,” Dorcas anasema yule mama alimwambia.
Kwa kuwa nilijua hakuna kitu kitakachonikomboa maishani mwangu kama elimu, nilifurahi sana kupata nafasi hiyo adimu ambayo nilikuwa naamini ilipotea, nikamkubalia yule mama.
“Nashukuru sana mwanangu kukubali kwenda kuishi nami, hata mume wangu nikimwambia habari zako atasikitika na kukupokea bila kinyongo,” Dorcas anasema yule mama alimwambia.
Nilimshukuru sana kwa ukarimu wake huo, hata yule dada alimuunga mkono tukaendelea kuzungumza na huku safari ikiendelea na kuwasili Nzega mapema.
Tulipofika tukaenda nyumbani kwa ndugu yao, katika maongezi yao waliambiwa mama aliyekuwa mwenyeji hakuwepo nalikuwa amekwenda Igunga.
Kufuatia taarifa hiyo, tuliondoka Nzega kwenda Igunga kwa ndugu yao mwingine ambako tulimkuta yule mama, baada ya maongezi waliamua kuelekea Dar.
Njiani tulikuwa tukizungumza mambo mengi utafikiri tulifahamiana muda mrefu, yule dada niliyemkuta mle kwenye gari kumbe naye alikuwa abiria.
Katika maongezi alitusimulia mateso aliyowahi kupata kutoka kwa mama yake wa kambo namna alivyokuwa akilala bila kula huku akiwa amefanya kazi kutwa nzima.
Alitueleza kuwa kila alipomweleza marehemu baba yake mambo ambayo alifanyiwa na yule mama, alimgeuzia kibao na kumchapa na kumtuhumu alikuwa muongo.
Mkasa wake ulituhuzunisha sana ambapo aliniambia nisihuzunike sana kwani kila kinachotkea katika maisha yetu kinakuwa na sababu.
Alisisitiza kama nitarudi shuleni nisome kwa bidii kwani ni elimu pekee ndiyo ingeweza kunikomboa na kunifanya nisahau yote yaliyonitokea, akaniambia nimshukuru sana yule mama aliyeamua kunichukua niende kwake Dar kwa ajili ya kusoma.
Nilimshukuru yule dada kwa kunipa moyo, tulipofika Singida alituaga kwani alikuwa amefika, kwa jinsi tulivyozoeana tulihuzunika lakini hatukuwa na la kufanya zaidi ya kutakiana heri.
Baada ya yule dada kuteremka, yule mama ambaye mpaka muda huo sikuelewa kama lile gari lilikuwa lake au la nani alimwambia dereva akipata abiria amchukue ili tupate pesa ya matumizi njiani.
Dereva aliondoa gari hadi maeneo ya stendi kuu ya Singida akawaeleza akina mama f’lani kwamba alikuwa akielekea Dar na kulikuwa na nafasi ya mtu mmoja.
Mama mmoja mwenye asili ya Kiarabu aliyekuwa na pochi alichangamka akaingia kwenye gari, safari ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya hadi dereva alipoyumbisha gari wakati akiwakwepa mbuzi waliokatiza barabarani.
Kufuatia kuyumba huko kwa gari, yule mama wa kiarabu alipata mshtuko akaangukia upande wa kulia wa kiti alichokuwa ameketi na kupoteza fahamu.
Je, kilifuatia nini? Usikose wiki ijayo. Maoni nicheki kupitia namba hizo hapo juu.
Kitendo cha yule mama kupoteza fahamu kilitukosesha raha, dereva alisimamisha gari pembeni ya barabara tukaanza kumpepea kwa kutumia gazeti lakini hakuzinduka.
“Huyu atakuwa na tatizo la presha, sasa sijui tufanyeje?” dereva alimwuliza mama.
Kwa kuwa mama alikuwa na uzoefu wa mamboya tiba alishauri tutafute sehemu iliyokuwa na kimvuli tuegeshe gari kisha akipigwa na upepo angezinduka.
Alipotoa ushauri huo, dereva alilipeleka gari chini ya mti wenye kimvuli ambapo palikuwa na hewa ya kutosha akafungua milango yote ya gari.
Mama hakuacha kumpepea ghafla yule mama akafumbua macho na kuanza kuangaza huku na huko,hali iliyotupa matumaini, mama akamwuliza alijisikiaje!
Yule mama wa Kiarabu hakujibu badala yake aliendelea kuangaza tu macho yake,mama akasema tumuache kama dakika kumi au zaidi angezinduka kabisa.
Kwelikama alivyosema, baada ya kupita kama dakika kumi na tano, yule mama aligeuza shingo upande aliokuwa mama na kumuuliza tulikuwa wapi.
“Tupo safari tunaenda Dar es Salaam,” mama alimjibu.
Alipoambiwa hivyo, alishangaa na kuuliza; “Tunakwenda Dar es Salaam kwa nani?”
Kufuatia swalilake tulijikuta tukiangua kicheko ndipo mama alimwambia tulikuwa safarini lakini kwa bahati mbaya tulipata tatizo lililomfanya we katika hali ile.
Mama alimwuliza kama hakukumbuka chochote,yule Mwarabu alitulia kwa muda na kuuliza begi lake lilikuwa wapi, mama akamuonesha, alipoliona alitabasamu.
Baada ya kufanya hivyo, aliinuka kisha kuuliza kwa nini dereva aliegesha gari chini ya mti,mama akamsimulia kilakitu kuhusu tulivyonusurika katika jail.
Alipoambiwa hivyo, alimshukuru Mungu ndipo alituambia alikuwa na tatizo la presha ambalo lilimfanya anaposhtuliwa na jambo f’lani alikuwa akipoteza fahamu.
Mama huyo, alifungua begi lake akatoa vidonge akameza viwili na kushushia na maji, akasema alikuwa sawa hivyo tuendelee na safari.
Maongezi yaliyojiri yalikuwa kumlaani mmiliki wa wale mbuzi kufuatia kitendo chake cha kuwaacha wakirandaranda hovyo barabani bila uangalizi.
Dereva aliendesha gari hilo kwa kasi hadi tulipofika Dodoma, tukaenda kula kisha safari ya Dar ikaendelea.
Mungu jalia tulifika Dar, salama salimini na kupokelewa na watoto wa yule mama, yule kaka aliyekuwa akiendesha gari ambaye mpaka muda huo sikufahamu walikuwa na uhusiano gani alituaga na kuondoka na yule kijana mwingine.
Baada kuweka mizigo na mabegi sehemu husika, yule mama alinikaribisha kwa kuniambia pale palikuwa nyumbani kwake hivyo niwe huru kwa kila jambo.
Aliniambia kwamba mumewe hakuwepo na kwamba angerudi usiku ndipo alinitambulisha kwa binti mmoja ambaye alisema ni dada yaani binti wa kazi, akasema anaitwa Tabu.
Je, nini kitaendelea?
@Shunie [emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]Shangazi weee[emoji8][emoji8] na mahugs mengi sana kwako