Naomba iwe na uchawi mwingi + lovedavi ya kutosha uko mbeleni.*SIMULIZI YA DORCAS-04*
Baada ya akina mama kufika, mama mkubwa aliniuliza nini kilinisumbua kufikia hatua ya kulia, nilimwambia kichwa, akaniuliza kilinianza saa ngapi nikawaambia.
Mama alipomuuliza daktari kuhusu matibabu, alimweleza alikwisha nipima kwa lengo la kujua kama nilikuwa na malaria lakini sikuwa nayo.
Kufuatia hali hiyo daktari alishauri niendelee kutumia dawa za kutuliza maumivu na kama hali ingekuwa si shwari wanirudishe tena pale hospitali.
Akina mama walipopewa ushauri huo, tulirudi nyumbani lakini wakati huo nilikuwa nimepata nafuu kiasi, nafikiri ni kwa vile niliwaona wazazi wangu.
Tulipofika nyumbani, mama mkubwa aliniandalia uji wa ulezi, nilipokunywa nilikwenda kulala kisha nikapitiwa na usingizi kwa muda mrefu.
Nilipoamka kichwa kilianza kuniuma sana, nilishindwa kuvumilia nikaanza kulia, akina mama walinipeleka tena pale zahanati.
Kutokana na hali niliyokuwanayo, daktari alishauri wanipeleke Hospital ya Rufaa ya Mbeya, walikodi gari na kunipeleka huko.
Daktari wa hospitali hiyo alinipima tena malaria, sikuwa nayo ndipo alinilaza kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kubaini kilichokuwa kikisababisha kichwa kuuma.
Nikiwa nimelazwa pale, daktari alishauri niwe napewa maji mengi na kutumia dawa za maumivu, kesho yake jioni kichwa kiliacha kuuma na siku iliyofuata niliruhusiwa kurudi nyumbani.
Baada ya kukaa nyumbani siku mbili kwa ajili ya mapumziko ya kuumwa, nilianza masomo bila kujua mbele yangu hakukuwa na amani.
Niliendelea na masomo kwa muda wa miezi miwili bila kusumbuliwa na jambo lolote ndipo siku moja usiku nikiwa nimelala nilishtuka usingizini kufuatia kusikia watu wakicheka.
Nilipoamka zile sauti sikuzisikia, nikawa najiuliza kama nilikuwa naota au lilikuwa tukio halisi, hata hivyo baadaye niliamua kulala nikapitiwa na usingizi.
Katikati ya usingizi, nikasikia tena watu wakipiga filimbi, kucheka na wengine wakizomea, nikaamka kama ilivyokuwa awali wale watu sikuwasikia tena.
Kitendo hicho kiliniogopesha nikaamka na kwenda kwenye mlango wa chumba cha akina mama, nikawaita, mama aliamka na kuniuliza sababu za kuwaamsha.
Niliwasimulia kila kitu, lakini cha kushangaza mama alisema zilikuwa ndoto za kawaida, hata hivyo niligoma kwenda kulala chumbani kwangu.
“Na wewe Dorcas unaonekana muoga sana, hata mambo unayoota yanakuogopesha?” Dorcas anasema mama yake alimwambia.
Kulipokucha, nilijiandaa na baada ya kunywa chai niliwaaga akina mama nikaondoka kuelekea shuleni.
Kama ilivyotokea siku ile, nilipopita nyumbani kwa yule mama ambaye hakuitikia salamu yangu, kama kawaida yake ya kupenda kufanya usafi asubuhi na mapema, nilimkuta akifagia.
Kwa kuwa ni jirani yetu na ninamheshimu kama mzazi wangu, nilimwamkia kwa uchangamfu lakini hakunichangamkia na wala hakuitikia salamu yangu.
Kufuatia kitendo hicho kujirudia mara mbili, nilihisi huenda nilifanya kosa ambalo sikulielewa, nikamuuliza na kumuomba kama nilikosea sehemu anisamehe.
Jambo la kushangaza, aliniangalia kwa dharau kisha akaendelea kufagia, nikaamua kuelekea shuleni huku nikijiuliza sababu za mama yule kunifanyia vile.
Nikiwa njiani nilipanga nikifika nyumbani niwaeleze akina mama kuhusu yule mama ambapo niliamini wangeenda kuzungumza naye kwa lengo la kujua sababu ya kutoitikia salamu yangu.
Kama ada, nilipofika shuleni tulifanya usafi wa mazingira kisha kengele ya kuingia madarasani iligongwa, wanafunzi wote tulikusanyika kwa ajili ya kukaguliwa usafi.
Nikiwa nimesimama mstarini, ghafla nilipata kizunguzungu nikaanguka na kupoteza fahamu, nilipozinduka nilijikuta nikiwa kwenye ile zahanati ya karibu na shule.
Niliwaona akina mama, walimu wawili na madaktari wawili, mama akaniita; “Dorcas!”
Baada ya kuitika akaniuliza nilipatwa na nini, sikumjibu kwani nilikuwa najiuliza nilikuwa wapi na nilifikaje pale, nikamuuliza pale nilifikaje!
Mama aliniuliza kwani sikukumbuka chochote kilichonitokea mpaka nikapelekwa pale? Nikamwambia sikukumbuka ndipo daktari mmoja akasogea, akanishika kichwani na kuniuliza:
“Sasa unajisikiaje?”
Nikiwa nimeshajua nilikuwa nipo hospitali, nilimwambia nilijisikia vizuri na kuomba wanieleze nilipatwa na nini kilichonifanya nilazwe wakati nilikuwa shuleni.
Yule daktari ili kuhakikisha kama nilikuwa sawa, aliniambia nivute kumbukumbu nikiwa shuleni nilipatwa na nini kisha niwaambie, nilipofanya hivyo nilikumbuka matukio yote mpaka tuliposimama mstarini na kupata kizunguzungu.
Niliwapowaambia, mama alisema alishangazwa sana na matukio ya kuumwa yaliyokuwa yakiongozana mfululizo ambayo awali sikuwa nayo.
“Unasema, hana tatizo la kupatwa na kizunguzungu?” yule daktari alimwuliza.
Kufuatia kuulizwa hivyo, mama alimweleza yule daktari kwamba sikuwa nasumbuliwa na tatizo hilo na kwamba alishangazwa na hali hiyo iliyokuwa ikimkosesha amani.
Baada ya mama kumweleza hivyo, yule daktari aliniandikia dawa flani ambazo nilipaswa kuzitumia siku tano, akasema ikitokea tena tatizo hilo wanipeleke hospitali ya rufaa.
Alipotukabidhi zile dawa, nikiwa nimeanza kuchangamka tuliondoka pale zahanati nikiwa na walimu, mama na wanafunzi wenzangu hadi nyumbani ambapo walimu walituaga.
Kilichowaweka akina katika wakati mgumu ni kitendo cha kupata kizunguzungu na kuanguka na wakati mwingine kuumwa na kichwa maradhi ambayo sikuwa nayo.
Akina mama walishindwa kuelewa kiini cha maradhi hayo, nakumbuka hadi jioni ya siku hiyo nilikuwa nimepona na kuchangamka kama siyo mimi niliyeanguka shuleni.
Kwa kuwa nilikuwa nimeandikiwa dawa za kumeza, niliendelea nazo hadi nilipozimaliza, nikawa nahudhuria shuleni kama kawaida nikiwa buheri wa afya.
Wiki mbili baadaye, siku moja nikiwa nimelala usiku, nilihisi nywele kunisisimka pamoja na mwili, nilipoamka niliona kimvuli cha mwanamke aliyenipa mgongo kikiishia kupitia kwenye kingo za ukuta.
Awali nilijiuliza niliona kitu halisi au nilikuwa naota, lakini kwa kuwa nilikuwa nimeamka niliamini yule alikuwa mtu, kwa uoga nikapiga kelele na kuwaita akina mama.
Wa kwanza kuamka alikuwa mama, ambaye tulikutana mlangoni akitaka kuingia nami nikitaka kutoka, akaniuliza kulikoni, nikamwambia nimemuona mtu chumbani kwangu.
Kauli yangu ilimshtua na kuniuliza huyo mtu aliingiaje, nilimfahamisha sikuelewa, wakati tukizungumza na mama, mama mkubwa alikuwa yupo jirani yetu.
“Mama Dorcas, vipi mtoto amepatwa na nini?” Dorcas anasema mama mkubwa alimwuliza.
Kama nilivyomwambia, naye alimjulisha mama mkubwa ambaye alishangaa na kuhoji kama yule mtu bado alikuwepo.
Niliwafahamisha kwamba alitoweka ghafla kwa kupitia pembe ya ukuta, nilipotoa kauli hiyo, mama mkubwa alisema alihisi hakuwa mtu nilikuwa naota ndoto.
Niliwahakikishia kwamba sikuota ni kweli nilimuona laivu mtu akitoka huku kanipa mgongo, akina mama wakabaki wakishangaa nilichowaambia.
Mama mkubwa aliniambia twende tukalale chumbani kwao huku akisema huenda kuna mchawi alikuwa akija kunisumbua usiku, mama alikubaliana na maneno ya mama mkubwa.
Alfajiri ya siku hiyo kichwa kilianza kuniuma sana, nikaishia kulia, mama mkubwa alinipatia panadol, hata baada ya kuzimeza hali iliendelea kuwa mbaya.
Kama walivyoshauriwa, walinipeleka hospitali ya rufaa, huko daktari aliwauliza historia ya maradha yangu wakamwambia, akasema huenda kuna tatizo kwenye mishipa flani ya kichwa changu.
Kwa kuwa kichwa kiliendelea kuniuma, nililazwa katika hospitali hiyo kwa muda wa siku nne lakini daktari ambaye alinifanyia vipimo alisema sikuwa na tatizo na kushauri niendelee kutumia dawa za kutuliza maumivu.
Miongoni mwa akina mama waliokuwa wakija kuniona hospitali alikuwa ni mama Jacob aliyekuwa rafiki wa akina mama, mama huyo alipoona sipati nafuu alishauri nirudishwe nyumbani.
Tukiwa nyumbani, aliwaambia akina mama kwamba maradhi yangu hayakuwa bure, alihisi yalitokana na nguvu za giza akashauri nipelekwe kwa mtaalamu wa mambo ya jadi.
Baada ya kujadiliana na kufuatilia historia ya maradhi yaliyokuwa yakinisumbua, akina mama waliamini kabisa kwamba nilikuwa nachezewa na mtu, wakamuomba mama Jacob awaelekeze au awapeleke kwa huyo mtaalam.
Mama huyo alikubali, siku iliyofuata alfajiri tuliondoka Isanga kwenda Songwe, nje ya Jiji la Mbeya kwa mtaalam huyo ambapo kwenye saa moja kasoro tulifika.
Mganga huyo aliyekuwa akifahamiana vizuri na mama Jacob alitupokea vizuri, zaidi walichangamkiana sana na mama Jacob kisha alitukaribisha sebuleni kwake.
“Naona umekuja na wageni?” yule mganga alimwuliza mama Jacob ambaye aliitikia kwa kusema ndiyo.
Mama huyo alitutambulisha kwa yule mganga na kumweleza kilichotupeleka pale ni matatizo yangu, mganga akaniangalia na kunipa pole.
Je, nini kitaendelea?
Imeanza hamisisha hamasisha!! Hapa muendelezo ndo mpaka siku 3 tena zipite.*DORCAS-05*
Baada ya kunipa pole, nilimshukuru ndipo alituambia kwamba mara atakapoangalia na kuzungumza na watu wake angebaini chanzo cha matatizo yangu.
Kwa kuwa pale sebuleni hapakuwa sehemu aliyokuwa akifanyia uganga wake, alituambia mimi na akina mama twende kwenye chumba cha kazi yaani kilingeni kwake.
Mganga huyo alituongoza tukapita mlango wa uani na kutoka nje ambapo kulia mwa nyumba yake kulikuwa na nyumba ndogo ambapo nje palikuwa na mwanamke na kijana aliyekuwa akitwanga dawa na yule mwanamke alikuwa akichambua mboga ya majani.
Tulipowakabiria, wote walitusalimia ndipo yule mganga akatutambulisha kwamba yule mwanamke alikuwa mkewe na yule kijana alikuwa msaidizi wake, tukasalimiana.
Tulipofika mlangoni, yule mganga alivua ndala alizokuwa amevaa nasi tukafanya hivyo, akatukaribisha ndani, tukaingia.
Kama ilivyo kawaida ya waganga kuwa na masharti, tulipoingia aliwaambia akina mama wakae kwenye mkeka uliokuwa karibu na tunguri zake, nami akaniambia nikae juu ya ngozi nyeusi ambayo sikujua ilikuwa ya mnyama gani.
Hata hivyo, mapigo yangu ya moyo yalikwenda kwa kasi kufuatia wasiwasi niliokuwanao, nilipokaa mganga huyo alichukuwa kipande cha ngozi kilichokuwa na tundu akakivaa shingoni.
Haikuishia hapo, alichukua usinga akaushika mkono wa kushoto na kuupunga kuzunguka chumba kizima akauweka alipouchukua, akakaa kwenye kigoda cha ngozi na kupiga mbinja iliyokwenda sambamba na chafya nne.
Baada ya kufanya hivyo, alichukua tunguri iliyokuwa imevilingwa shanga akamimina kitu kama mafuta kiganganjani na kujipaka usoni.
Alipomaliza kufanya hivyo, alichukua kioo kilichotengenezewa fremu nyeusi na kuzungushiwa shanga, akaniambia niiname kwani alitarajia kuzungumza na wazee ili kujua chanzo cha matatizo yangu.
Wakati akifanya hivyo, akina mama walikuwa wametulia wakimwangalia kwa makini na woga, nilipoinama akaanza kuvuta pumzi na kusema maneno yasiyoeleweka na kutikisa kichwa.
Alifanya hivyo kama dakika tano, akaniambia niinue kichwa na kusema:
“Akina mama, kuna mtu mwanamke ndiye anamuumiza binti yenu, huyo mwanamke ni mtu mzima, kaamua kumtesa kwa wivu wake tu, kwa sababu mtoto ana nyota ya kupendwa, tena anashirikiana na mwenzake mmoja.”
Baada ya mganga kutueleza hivyo, wote tulitazamana kwani taarifa ile ilitufanya tupigwe butwaa, mganga akatuambia isingekuwa miiko ya kazi yake angetuonesha wanawake hao.
Mama mkubwa alimuomba mganga asijali atuoneshe, lakini yule kalumanzila aligoma na kutuambia atanitibu na kuondoa vitu nilivyotupiwa mwilini ambavyo vilikuwa vikinitesa.
“Ametupiwa vitu?” Dorcas anasema mama yake alimwuliza yule mganga.
Mganga alitufahamisha kwamba nilitupiwa vitu vitatu, kimoja kilikuwa kichwani, tumboni na mgongoni na lengo lao walitaka nilale ndani maisha yangu yote.
Mimi na akina mama tulinyong’onyeshwa na taarifa hiyo ndipo yule mganga alisema tusijali kwani uchawi walionifanyia ulikuwa mdogo kikubwa tumtafutie kuku mweusi, kitambaa cheusi, mbegu kavu za papai, kipande cha kanga niliyokuwa nikitumia na kwamba vitu vingine angeviandaa mwenyewe.
Baada ya mganga kusema hivyo, mama aliyekuwa na dukuduku la kumjua yule mama alimuomba sana awaoneshe wale akina mama lakini yule mganga alisisitiza asingeweza kufanya hivyo.
“Ila kama mnataka niwachape kwa sababu wamemuonea tu huyu binti niruhusuni, akishapona nao nitawapa adhabu ili wakome kuwasambua watu,” Dorcas anasema mganga aliwaambia.
Mama alikubali mganga huyo kuwaadhibu watu hao lakini mama mkubwa alipinga na kusema awaache kwani Mungu pekee ndiye anayepaswa kutoa hukumu.
Baada ya mama mkubwa kusema hivyo, mganga alicheka na kusema alichosema ni sawa lakini pia kuwaadhibu watu wanaowatesa wenzao pia ni sawa.
Hata baada ya mganga kutoa kauli hiyo ya ushawishi ili mama mkubwa akubali awaadhibu wale akina mama wachawi, mama mkubwa alipinga.
Baada ya maongezi hayo, mganga aliwauliza akina mama ni lini wangeleta vitu alivyowaagiza, kwa kuwa vyote ilikuwa rahisi kuvipata walimwambia kesho yake.
“Kwa kesho hapana, nitaenda porini kuchimba dawa njooni keshokutwa au siku ninyingine yoyote,” Dorcas alimkariri mkanga huyo.
Baada ya kutuambia hivyo, mganga alivua ngozi aliyokuwa amevaa kisha tuliinuka akatuongoza kwenda nyumba kubwa tulikomuacha mama Jacob rafiki wa akina mama.
Tulipofika mganga ambaye alikuwa mkarimu sana alituuliza tulikuwa tunakunywa soda gani, wote tulimshukuru na kusema tungekunywa siku nyingine.
“Hapana, lazima mnywe soda jamani, wala hazifuatwi mbali,” Dorcas anasema mganga aliwaambia kisha alimwita kijana wake ambaye alifika haraka.
“Hebu waletee soda wageni,” Dorcas anasema mganga alimwambia kijana wake.
Yule kijana alituuliza soda ambazo tulikuwa tukinywa, aliingia chumbani akatuletea na tulipomaliza kunywa, tuliondoka nyumbani kwa mganga huyo na kuanza safari ya kurudi Mbeya mjini.
Licha ya kwamba kila mmoja alitaka kulizungumzia suala la wale akina mama walionekana kwa mganga, lakini hatukuweza kuongea ndani ya basi hadi saa nane alasiri tulipofika nyumbani.
Tukiwa tumeketi sebuleni, mama alianza kumuuliza mama mkubwa kama aliweza kuwatambua akina mama hao, mama mkubwa akasema kama waliofanya hivyo ni majirani zetu, akamtaja yule mama ambaye kila nilipomsalimia hakuitikia kwamba alikuwa mmoja wao.
Baada ya kumtaja, kwa mbali mama alionekana kuamini nami nilipokumbuka kitendo cha mama huyo kutoitikia salamu yangu nikahisi huenda ndiye aliyetajwa na yule mganga.
“Mama mkubwa nahisi hujakosea, kwa maelezo yako nahisi mama (akamtaja jina) ndiye anayemtesa Dorcas, lakini mtoto amemkosea nini?” mama alimwuliza mama mkubwa.
Hata hivyo, kwa kuwa hatukuwa na ushahidi kama ni kweli mama huyo alihusika mama mkubwa alishauri tuanze kumchunguza tungebaini ukweli.
Baada ya kusema hivyo, moyoni nilisikia sauti moja ikiniambia yule mama ndiye haswa alikuwa akinitesa, nikaanza kutafakari tabia yake ya kutoitikia salamu zangu na kuninua bila sababu.
Sikuishia hapo nilipotafakari kwa undani nikagundua karibu mara zote ambazo nilikumbwa na ugonjwa wa kuumwa kichwa na lile tukio la kuanguka shuleni, yalitokea baada ya kumsalimia yule mama na kutoitikia salamu yangu.
Nilipowaambia akina mama moja kwa moja walikubaliana nami ndipo mama mkubwa ambaye hakuwa na simile akataka kumfuata mama huyo kwa lengo la kumchana laivu lakini mama akamzuia.
“Hata kama ni kweli ndiye anayefanya hivyo, utafanya kosa kubwa sana kumfuata na kumwambia anamroga mtoto, tena akikupeleka mahakamani utaingia kwenye matatizo,” mama alimwambia mama mkubwa.
“Hapana inauma sana, mtoto kila siku anaumwa kumbe yeye ndiye anayemroga, Dorcas kamkosea nini? Ngoja nikamchane laivu,” mama mkubwa aliyepatwa na hasira alisema.
Kwa kuwa mama alijua hatari ambayo ingetokea, licha naye kuamini yule mama ndiye aliyetajwa na mganga japo hakuweka wazi, alimsihi mama mkubwa awe mpole.
“Haya, ila nafikiri keshokutwa tukienda kwa mganga tumwambie amuadhibu ili naye aonje machungu ya kuwatesa wenzake,” mama mkubwa alimwambia mama.
Pamoja na kupanga kufanya hivyo, mama alituambia kama kweli yule mama ndiye aliyekuwa akiniroga lilikuwa jambo la ajabu sana kutokana na jinsi tulivyokuwa tukicheka na kushirikiana kama majirani.
“Na wewe mama Dorcas, hivi huwajui wachawi walivyo, huwezi kuwadhania na ni wapole na wenye upendo lakini ni balaa kwa kuwatesa watu,” mama mkubwa alimwambia mama.
Baada ya maongezi yaliyochukua muda mrefu mama akainuka na kusema tangu tulipofika tulifikia kumzungumzia Yule mama na kusahau kama hatukula.
Kwa kuwa ndani kulikuwa na mboga, akaniambia niwashe mkaa kisha niinjike maji ya kusongea ugali, mama mkubwa huku akionekana kuwa na jazba na Yule mama akainuka na kwenda chumbani.
Tulipomaliza kula, mama mkubwa alikwenda sokoni kununua vile vitu tulivyoagizwa na mganga, kwa upande wa mama akaenda kuoga.
Siku hiyo hawakwenda kabisa kwenye biashara zao.
Siku ya tatu, tukiwa na vitu alivyotuagiza mganga huku tukiwa tayari tumeshamjua mbaya wetu, alfajiri tuliondoka kuelekea Songwe kwa mganga, lakini hatukuwa na mama Jacob.
Tulipofika mganga alitupokea na kutupeleka kilingeni kwake, kwa kuwa tayari alikwisha niagua, sikukaa kwenye ile ngozi nyeusi bali nilikaa kwenye jamvi na akina mama.
Tukiwa pale alituuliza kama tulifanikiwa kupata vitu alivyotuagiza, mama mkubwa akasema tulivipata akammkabidhi ambapo alituambia naye alikwisha andaa vyake.
Baada ya kumkabidhi alituambia twende tukakae nje sehemu palipokuwa na viti vya wageni, tukafanya hivyo.
Je, nini kiliendelea?
Mama mkubwa naye anaoneka ni mzee wa matunguri!! Hii inaitwa kikulacho kipo......Asante shunie. Ila mbona Nina wasiwasi na mama mkubwa pia
Ya Leo inatisha na Giza hili la kuelekea saa 6 nimejikuta nasisimka*DORCAS-07*
Baada ya mama ambaye alikuwa mpole sana kusema mchawi huyo asamehewe kwa kuwa nilikuwa nimepona, mama mkubwa alimpinga na kusema:
“Huyo hafai kuendelea kuishi, hivi mama Dorcas kama angekuulia huyu mtoto wako wa pekee ungejisikiaje, mimi sioni kama kuna sababu ya kumuonea huruma.”
Kwa kuwa mama hakuwa tayari mchawi huyo aadhibiwe, mganga hakuwa na kusema akanipatia dawa kisha alitufahamisha kwamba baada ya kutumia zile dawa siku tatu turejee kwa ajili ya kunipa kinga.
“Itabidi akimaliza hizo dawa aje nimpe kinga sababu kwa ninavyowafahamu wachawi huwa hawakubali kushindwa, yule mama atarudi tena tena anaweza kuwaalika hata wenzake ili wamsaidie,” Dorcas alimkariri yule mganga.
Kufuatia mganga kutoa kauli hiyo, mama ambaye kama akumuelewa alimwuliza mganga kwamba yaani pamoja na kuharibu uchawi wake bado wangekuja tena!
“Kuja ni lazima ndiyo maana nimesema akimaliza hizo dawa siku ya tatu kuanzia leo aje nimkinge vinginevyo mnaweza kumpoteza mtoto,” Dorcas alimkariri yule mganga.
Baada ya mganga kumweleza hivyo mama, mama mkubwa alisema:
“Mdogo wangu unasikia anachokisema baba, huyo mchawi inatakiwa tummalize kabla hajammaliza mtoto, hivi ujue huo upo wako utakuponza.”
Hata baada ya mama mkubwa kutoa ushauri huo, mama hakuwa tayari kulipa kisasi ndipo mganga akasema cha muhimu siku ya tatu turudi kwake ili anipe kinga.
Baada ya kukabidhiwa dawa tulirudi nyumbani, tulipofika tu mama mkubwa alichemsha dawa na jioni nikaanza kunywa, usiku tukiwa tunapiga stori maongezi yetu yalikuwa ni juu ya vitu nilivyotupiwa na yule mchawi.
“Jamani hii dunia kuna watu wabaya sana, mtu anachukua maharage, mchele na nguo anazifanyia uchawi wa kumtesa mtu, Mungu atusaidie,” mama alituambia.
Baada ya mama kutoa kauli hiyo, mama mkubwa alimwambia tena wapo watu wanaweza kuwaua wenzao kwa dakika moja kutokana na uchawi wao.
Siku hiyo tulizungumza kwa muda mrefu ndipo mama akaniambia nikalale lakini kwa hofu niliyokuwanayo nilikataa kwenda kulala peke yangu wote tukalala chumbani kwao.
Kwa kuwa zile dawa nilitakiwa kunywa asuhubi, mchana na jioni, kabla sijaenda shuleni mama mkubwa aliniandalia na baada ya kunywa niliwaaga na kuelekea shuleni.
Asubuhi sikupita ile njia ya kutokea kwa yule mama tuliyehisi mchawi, niliamua kumpitia rafiki yangu Yasinta aliyekuwa akiishi mtaa mwingine kisha tukaelekea shuleni.
Siku hiyo mwili wangu ulikuwa mwepesi tofauti na kabla sijatolewa vitu vya ajabu kichwani mwangu ambapo sikuwa sawa kabisa, pia nilichangamka sana.
Kama tulivyoambiwa na mganga, siku ya tatu tulikwenda kwake ambapo alitueleza kwamba kupitia watu wake alimuona yule mama alivyokuwa akilalamika uchawi wake kuharibika.
Aliongeza kuwa licha ya kila siku kuja kuniwangia pale nyumbani hakuweza kufanikiwa kwa sababu ya zile dawa alizonipatia na kwamba kwa hasira alikwenda kichawi kwa yule mganga mchawi wa Mbozi kumweleza kilichotokea.
Mganga alitueleza kwamba tusihofu kwa sababu kinga atakayotupatia ni kiboko na kwamba yule mchawi akirudia angeweza kupatwa na balaa.
Tukiwa kwa yule mganga alinichanja chale sehemu mbalimbali za mwili wangu akanipaka dawa na kuniwiza kwamba mtu yeyote atakayekuja kunichezea asifanikiwi na uchawi wake umrudie mwenyewe.
“Wanangu, kwa kuwa nyinyi ndiyo wazazi wa huyu binti na mnaishi nyumba moja ni vizuri nanyi niwape kinga kwa sababu wachawi wanaposhindwa kumfikia mtu waliyemkusudia umalizia hasira zao kwa wengine,” mganga aliwaambia akina mama.
Baada ya kutoa kauli hiyo, mama mkubwa ambaye kwa sehemu alikuwa anaelewa mambo ya wachawi alikubali lakini mama alisita, mpaka leo nashindwa kuelewa sijui kwa nini marehemu mama hakupenda mambo ya kishirikina.
Hata hivyo, kwa ushawishi mkubwa wa mama mkubwa na yule mganga mama alikubalia ambapo nao walichanjwa na kupakwa dawa ya kinga.
“Wanangu kutokana na hii dawa ya kinga niliyowachanjia leo msioge mpaka kesho jioni,” mganga alituambia.
Mganga huyo aliongeza kuwa, usiku tukiwa tumelala yule mama mchawi akiwa na wenzake watakuja lakini tusiwe na hofu tutakaposikia upepo ukivuma juu ya bati ni kwamba kinga yake itakuwa ikifanya kazi kuwazuia.
Mama mkubwa alimshukuru kwa taarifa hiyo na kumuuliza kama ukizidi tufanye nini, akamwambia tutulie hadi watakapoondoka.
Kabla hatujaondoa kwa yule mganga, mama mkubwa aliuliza kiasi cha fedha alichohitaji ambapo mganga alisema hakuhitaji fedha isipokuwa kuna kitu alihitaji kama angekipata hicho ingekuwa malipo ya kazi yake.
Mama mkubwa alipomuuliza ni kitu gani akasema redio kwani aliyokuwanayo iliharibika na alipenda sana kusikiliza taarifa ya habari na vipindi vingine.
Mganga alipotoa ombi hilo, mama mkubwa ambaye pale nyumbani alikuwa na redio mbili alimwambia angempelekea, mganga alifurahi sana na kabla hatujaondoka alimwita mkewe na kumwambia atufungashie maharage pamoja na mahindi.
“Wanangu nimefurahi sana kunikubalia ombi langu kwani muda sasa nashindwa kusikiliza redio hapa nyumbani,” mganga aliwaambia akina mama.
Mama alimwambia asijali angepata redio hiyo ndipo tuliwaaga ambapo walitusindikiza kidogo kisha wakarudi nasi tukaenda kupanda gari la kwenda Mbeya mjini.
Tulipofika nyumbani kabla ya kufanya kitu chochote tuliketi sebuleni na kuanza kuzungumza mambo ya kwa yule mganga, mama mkubwa alimsifia kwamba alikuwa mganga mahiri na angetusaidia sana.
“Mimi nashukuru alivyoamua kutupa kinga hata sisi, amefanya jambo la muhimu sana,” mama mkubwa alituambia.
Wakati tunazungumza hakuna aliyejua kwamba huko mbele kungekuwa na vita kubwa dhidi yetu na wachawi ambayo ingesababisha mama kupoteza maisha katika mazingira tata.
Kwa upande wangu pia sikujua mikosi ambayo ningekutana nayo likiwemo balaa la kubakwa ambalo limeharibu kabisa maisha yangu.
Tulipopumzika, niliwasha jiko nikainjika maji kwenye sufuaria kubwa ambapo mama mkubwa aliniuliza yale maji yalikuwa ya nini, nikamwambia ya kuoga.
“Wewe Doracs kwani hukusikia alichotuambia mganga kwamba leo hatupaswi kuoga hadi kesho jioni,” mama mkubwa aliniambia.
Aliponieleza hivyo, nilikumbuka ni kweli mganga alitupa sharti hilo nikaishia kucheka na kumwambia nilisahau.
“Hapo kama ungekuwa peke yako ungeoga na kuharibu kinga yote, sisi wazee ndiyo tulitakiwa tusahau lakini siyo wewe,” mama mkubwa akaniambia nikaishia kucheka tu!
Wakati tukizungumza na mama mkubwa, mama alikuwa akiendelea kuchambua mchele name nilibadili ile sufuria na kuweka ambayo ilikuwa ikitumika kupikia wali.
Siku hiyo kila mmoja wetu alishirikia mapishi ya jioni na chakula kilipokuwa tayari saa mbili usiku mama mkubwa alikiandaa mezani, tukala na kwenda kulala.
Wote tukiwa tumelala kwenye kitanda cha futi sita kwa sita cha mama mkubwa, ilipotimu saa nane usiku nilisikia upepo mkali ukivuma na kutikisa bati la nyumba.
Hali hiyo pia ilisikiwa na akina mama lakini hakuna kati yetu aliyeshtuka sana kwa sababu tulikwishaambiwa na mganga kuhusu tukio hilo, tulitulia mpaka upepo ukatoweka.
“Mmeamini maneno ya mganga?” mama mkubwa alituuliza.
“Nimeamini dada yangu, kweli hii dunia ina mambo sasa nimeanza kuamini,” Dorcas anasema mama yake aliwaambia.
Kufuatia tukio hilo, tulitumia muda mrefu kulizungumzia hadi tulipotiwa na usingizi, niliposhtuka ilikuwa kwenye saa 12 alfajiri ambapo niliamka ndipo mama mkubwa aliniuliza nilitaka kwenda wapi, nikamwambia shuleni.
“Hapana mwanangu leo usiende utaenda kesho,” mama mkubwa aliniambia.
Nilipomuuliza sababu akaniambia nisiende tu nisubiri mpaka siku iliyofuata, kwa kuwa nilikuwa mtoto sikutaka kumbishia kwa sababu wakubwa wanaposhauri jambo ni vyema kuwasikiliza.
Kwa kuwa ratiba ya kwenda shule haikuwepo, sikutaka kurudi kulala nikataka kutoka nje nikafagie uwanja, kuosha vyombo na kufua nguo.
“Mwenzetu mbona umeduaa, kwa kuwa huendi shule rudi ulale,” Dorcas anasema mama yake mkubwa alimwambia.
Mama mkubwa aliponiambia hivyo nilimweleza kwa kuwa nilikuwa nimeamka ngoja nikafagie uwanja, kuosha vyombo na baada ya kupata kifungua kinywa ningefua nguo.
Licha ya kumwambia hivyo, mama mkubwa alinizuia kwenda kufangia na kunitaka nirudi kulala kwa sababu nje kulikuwa na baridi, nikaamua kurudi kulala.
Ilipofika saa moja, tuliamka na baada ya kupata kifungua kinywa, akina mama walinianga kwamba wanakwenda kwenye biashara wakaniachia hela za matumizi, nakumbuka mama aliniambia nikanunua nyama wangerejea na ndizi kwa sababu zilipita siku kadhaa bila kula chakula hicho.
Walipoondoka, niliosha vyombo kwenye saa tatu hivi na nusu niliamua kwenda sokoni kununua nyama pamoja na viungo, wakati narudi nikiwa nimepita kwenye uchochoro ghafla nilimuona paka mweusi akiwa amesimama mbele yangu, nywele zikanisisimka.
Nakumbuka siku moja tukiwa tunazungumza na akina mama, mama mkubwa aliwahi kusema ikitokea mtu anatembea usiku au mchana halafu akahisi nywele kumsisimka hali hiyo inaashiria hatari ipo mbele yake.
Kutokana na hali hiyo, nilihisi sikuwa sehemu salama, nikapa wazo la kurudi ili nipite njia nyingine, wakati nawaza hivyo yule paka alikuwa amesimama akiniangalia.
Jambo la kushangaza nilipogeuka nyuma ili nirudi kwa lengo la kupita njia nyingine nikashangaa kumuona paka aliyefanana na yule aliyekuwa mbele yangu akiwa amesimama ananiangalia, moyo ukapiga paa!
Kutokana na tukio hilo, niligeuka tena nyuma ili kumwangalia yule paka wa awali, sikumuona nikabaki nikijiuliza alihamaje na kuja kusimama nyuma yangu.
Kwa kuwa lengo langu lilikuwa ni kutoka pale uchochoroni niliamua kusonga mbele, cha ajabu nilipotembea hatua tatu ghala yule paka alitokea mbele yangu.
Tukio hilo ambalo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukumbana nalo liliniogopesha sana, nilishindwa kuvumilia nikaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada.
Cha kushangaza ni kwamba licha ya kupiga mayowe yule paka hakuondoka mbele yangu, wa kwanza kufika pale uchochoroni walikuwa akina mama wawili, mama Thabi, mama Elisha kisha walitokea vijana watatu na dada mmoja.
“Wewe Dorcas umepatwa na nini?” Dorcas anasema mama Thabi ambaye alikuwa akimfahamu vizuri alimwuliza.
Nikiwa mwenye hofu niliwaonesha paka ambaye bado alikuwa mbele yangu na kuwaeleza alikuwa akinizuia, wakashangaa na kuniuliza paka huyo alikuwa wapi!
Kwa kuwa mnyama huyo alikuwa amesimama karibu kabisa na mama Elisha, nikawaonesha lakini hawakumuona, mzee mmoja akasema huenda malaria ilinipanda kichwani.
Niliwahakikishia kwamba sikuwa na malaria na kusisitiza kuwauliza kama ni kweli hawakumuona yule paka, jambo la ajabu ni kwamba nilipoangalia sehemu aliyokuwepo yule paka sikumuona.
“Dorcas huyo paka mbona sisi hatumuoni,” mama Elisha aliniuliza.
Kwa kuwa paka alikuwa ametoweka niliwaambia aliondoka wakabaki wameduwaa ndipo yule mzee alisema kama kweli nilimuona paka muda ule anaweza kuwa wa miujiza.
Hata hivyo, mama Elisha alimpinga kwamba hapakuwa nap aka kwa sababu walipofika hawakumuona mnyama huyo, aliponiuliza tena kama nilimuona paka, niliwasisitizia kwamba nilimuona.
Mmoja wa wale vijana aliniuliza nilikuwa najisikiaje nikamwambia nilikuwa mzima, akasema kama sikuwa na tatizo basi niende nyumbani kisha wakaondoka.
Baada ya wale vijana kuondoka, yule mzee aliwaambia akina mama Elisha, yule dada na mama Thabi kwamba huenda ni kweli nilitokewa nap aka kwani isingekuwa rahisi katika hali ya kawaida kupiga mayowe na kusema nilimuona paka.
Mzee huyo alimuomba mama Thabi anisindike nyumbani kisha kila mmoja akaendelea na mambo yake nikaongozana na mama Thabi kwenda nyumbani.
Kwa kuwa sikuwa na tatizo, tulipofika aliniaga na kuniambia akina mama wakirudi niwasimulie nikamwambia sawa.
Mama Thabi alipoondoka, nilitoa kitoweo na vitu vingine nilivyotoka kuvinunua na kuanza mapishi kwa kuinjika nyama jikoni kisha kukatakata viungo.
Nyama ilipoiva niliipua na kwa kuwa sikuwa nahisi njaa, niliamua kujipumzisha kuwasubiri akina mama warejee ili tuandae chakula cha alasiri kwani walikuwa wanapenda sana kula nyumbani.
Wakati wanawasubiri niliingia chumbani kwangu nikajilaza kitandani, nikiwa sijapitiwa na usingizi ghafla nilishtukiwa nikikabwa shingoni na mtu.
Kwa kuwa mle chumbani nilikuwa peke yangu, kila nilipojaribu kupiga mayowe ya kuomba msaada sikuweza kwani aliendelea kunikaba huku akisema atahakikisha ananiondoa duniani.
Mtu huyo ambaye alikuwa amejitanda nguo nyeusi kila nilipojaribu kujinasua aliendelea kunikaba huku akikwepesha sira yake nisiione ndipo nikaanga kusema; ‘Mungu wangu niokoe, Mungu wangu niokoe ghafla alianiachia na kutoa msonyo wa nguvu na kuniambia nilikuwa nina bahati.
Alipotoa kauli hiyo, nikajikuta mle chumbani nimebaki peke yangu lakini nikasikia sauti ikiniambia nichungulie dirishani, nilipofanya hivyo nilimuona mama mmoja aliyekuwa kanipa mgongo akitembea.
Mama huyo aliyekuwa amejifunga nguo nyeusi, kwa muonekano wake wa nyuma na tembea yake alifanana na yule mama tuliyekuwa tukimhisi alikuwa akituchezea kichawi.
Nilimwangalia mpaka alipotoweka kwa kukata kona na kuingia kwenye uchochoro ndipo nilitoka pale dirishani na kwenda kukaa kitandani, nikashusha pumzi kwa nguvu.
Baada ya kufanya hivyo, ghafla nikaanza kulia mpaka nikaanza kukohoa huku ndipo nilishangaa nikiwa nimeshikwa na mama mkubwa akaanza kuniuliza nilipatwa na nini!
Nikiwa nalia mama aliingia akapigwa butwaa kuniona nikilia, baada ya kunibembeleza kwa muda nilinyamaza ndipo nikawasilimulia kila kitu kuhusu yule paka na mama aliyekuwa akinikaba.
Baada ya kuwaeleza hivyo, mama alianza kulia na kusema kama baba yangu angekuwepo yote yaliyokuwa yakinitokea yasingetokea, nami nikaanza kulia.
Je, nini kitaendelea?
*SIMULIZI YA DORCAS-03*
Kutokana na ukarimu aliokuwa nao mama huyo, mama alihuzunika sana alipoambiwa kwamba mumewe alikuwa amefariki dunia ndipo alimwuliza mama mkubwa kama alikuwa na watoto.
“Aliniambia kwamba ana watoto watatu, wawili wa kike na wa kiume anaitwa Evance,” mama mkubwa alimfahamisha mama.
Mama na mama mkubwa waliendelea kumzungumzia mama huyo wa Shinyanga jinsi alivyokuwa na upendo kwa watu wengine ndipo niliwaacha na kwenda kulala.
Katikati ya usingizi niliota ndoto tupo sokoni mama ambapo alikuwa akiuza mchele na watu walikuwa wengi sana, wakati mama akiwa bize kuwahudumia wateja mtu nisiyemfahamu alinigusa begani.
Nilipogeuka kumwangalia, alikuwa ni mtu mzima ambaye alitabasamu na kunionesha mwenzake na kuniuliza:
“Unamfahamu huyu hapa?”
Kabla sijamjibu, mama aliyewasikia watu hao alipogeuka kuwaangalia aliruka kwa furaha na kumkumbatia yule bwana niliyeulizwa kama nilikuwa namfahamu.
“Gilbert, hivi ni wewe kweli au naota ndoto ya mchana, siamini macho yangu!” mama alimwambia yule bwana.
Jamaa huyo akiwa amekumbatiana na mama huku akitabasamu, alimjibu kwamba alikuwa yeye ndipo mama aliniita na kunifahamisha kuwa yule alikuwa baba yangu.
Kama alivyofanya mama, nami kwa furaha nilimkumbatia baba yangu na kuanza kulia huku nikimuuliza alikuwa wapi muda wote.
Baba ambaye alikuwa amepigwa butwaa kuambiwa mimi nilikuwa mwanaye, akamuuliza mama nilikuwa mwanaye kivipi, ile mama anataka kumwambia nilishtuka kutoka usingizini.
Ndoto hiyo ilinikosesha raha sana nikajikuta ninalia kwa sauti kitendo kilichosababisha mama mkubwa na mama kuamka na kuingia chumbani kwangu kujua nilipatwa na nini.
“Dorcas mwanangu umepatwa na nini mbona unalia?” mama aliniuliza.
Baada ya kuwaona akina mama nikazidisha kulia bila kuwaambia sababu, mama mkubwa aliketi kwenye mfumbati wa kitanda na kuanza kuniuliza sababu ya kulia.
“Nimemuona baba yangu, lakini kabla sijazungumza naye ameondoka,” nilimwambia mama mkubwa.
Kauli yangu iliwashtua ambapo mama aliniuliza baba yangu nilimuona wapi na kusema mbona niliwaacha njia panda!
Niliwafahamisha kwamba nilimuona kwenye ndoto, akiwa na rafiki yake kisha kwa hamaki nikamwambia mama nilimtaka baba yangu, kauli ambayo ilimuumiza sana akaanza kulia.
Kitendo cha mama kulia, kilinifanya nami niendelee kulia, mama mkubwa akawa na kazi ya ziada ya kutubembeleza kisha aliniita:
“Dorcas!”
Nilipoitika aliniuliza kwa nini nilikuwa namuweka mama katika wakati mgumu na kwa nini sikupenda kumuelewa aliponiambia nivumilie ipo siku ningekuja kumuona baba yangu!
Kufuatia kuniuliza hivyo, nilimwambia kilichoniliza ni kitendo cha baba kunijia kwenye ndoto wakati nilitamani sana kumuona laivu ili nami nifurahi naye kama wenzangu.
Kama ambavyo alikuwa akifanya mara kwa mara nilipokuwa nalia kuhusu kuhitaji kumuona baba, aliniomba nisilie na kunipa moyo kwamba ipo siku ningekutana naye.
“Mwanangu Dorcas, kwa kuwa umeanza kumuota baba yako ni dalili kwamba karibu mtaonana, hivyo kuwa na subira, sawa mama?” Dorcas alimkalili mama mkubwa.
Nilimwambia sawa japo sikufahamu ningeonanaje na baba yangu ambaye katika ndoto niliyoota nilisikia mama akimwita kwa jina la Gilbert.
Baada ya mama mkubwa kuniambia hivyo alinieleza nilale kwa amani kisha wakaniacha na kwenda kulala chumbani kwao, sikujua walichoongea huko.
Japo nilikuwa bado mdogo, nikiwa nimejilaza kitandani, sikuweza kupata usingizi kwa wakati kwani muda mwingi nilikuwa namuwaza baba yangu.
Hata hivyo, baadaye nilipitiwa na usingizi hadi nilipokuja kushtuka saa kumi na moja alfajiri na kujikuta kichwa kikiuma sana.
Kutokana na maumivu niliyopata nikaanza kulia na kumwita mama, wote waliamka na kuja chumbani nilikokuwa nalala wakifikiria sababu iliyoniliza ilihusu baba.
Mama mkubwa aliponiuliza nini kilinisibu niliwaambia kichwa kilikuwa kinauma sana, waliniuliza kilianza muda gani niliwafahamisha kwamba ni baada ya kushtuka kutoka usingizini.
Kwa kuwa ndani kulikuwa na panadol, mama mkubwa alizifuata pamoja na maji nikameza kisha akaniambia nilale kitapoa, cha kusikitisha ni kwamba sikupata nafuu.
Haukupita muda mrefu nikaanza kulia kwa sauti huku nikipiga kelele, mama mkubwa akamwambia mama alihisi malaria ilipanda kichwani.
Kutokana na hali niliyokuwa nayo, baadhi ya majirani zetu waliamka na kuja kujua sababu ya kulia kwangu, wakawaambia walihisi malaria ilipanda kichwani.
Akina mama walijiandaa, wakaniandaa na kunipeleka kwenye zahanati moja iliyopo Isanga, daktari aliyekuwepo zamu baada ya kuona situlii, kwa mujibu wa mama mkubwa, alinichoma dawa ya usingizi, nikalala.
Nililala saa nzima, dawa hiyo ilipoisha nguvu niliamka na kujikuta nimepumzishwa pale hospitali nikawauliza nilipatwa na tatizo gani, mama akaniambia nilikuwa naumwa.
Tukiwa tunazungumza na mama, yule daktari aliingia akaniita jina langu na kusema: “ Unajisikiaje sasa?”
Nilimwambia nilihisi kichwa kuniuma akanipa pole na kuniambia nilikuwa nina malaria, kumbe tayari alinichukua damu na kuipima.
Baada ya daktari huyo kuniandikia dawa alimpa mama maelezo ya namna ya kutumia kisha alinitania kwamba niache uoga wa kuumwa, tukarejea nyumbani huku kila mmoja wetu akiamini nilikuwa naumwa malaria.
Kama mama alivyokuwa amepewa maelezo na daktari, baada ya kula alinipatia dawa kisha nilikwenda kulala, mama mkubwa alikwenda kwenye biashara zake na kumuacha mama aliyekuwa akiniangalia.
Siku hiyo nililala hadi alasiri, nilipoamka nilijisikia nimepata nafuu jambo lililomfarahisha mama. Hata mama mkubwa aliporejea na kunikuta katika hali hiyo alifurahi.
Kufuatia kuumwa, sikwenda shuleni siku tatu hadi nilipopa kabisa. Tangu nilipougua nilimaliza wiki mbili ndipo nilianza kutokewa na vitu vya ajabu nikiwa nimelala.
Siku moja nikiwa nimelala chumbani nilijikuta nikikabwa shingoni na mtu ambaye sikumuona, kila nilipojaribu kuwaita akina mama sikuweza kufanikiwa kwani sauti haikutoka.
Hata hivyo, muda mfupi baadaye mtu huyo alianiachia nilipotazama ukutani niliona kama kimvuli cha mtu kikiishia ndipo nikaanza kuwaita akina mama.
Mama mkubwa na mama walipoingia chumbani kwangu walinikuta nimekaa kitandani huku nikihema, mama aliponiuliza nilipatwa na nini nikawaeleza.
“Huenda ulipolala uliangalia juu, mara nyingi mtu akilala chali huota ndoto za kukabwa,” mama mkubwa aliniambia.
Kwa kuwa sikulala chali niliwaambia, mama mkubwa akasema basi kulikuwa na jinamizi lilikuja kunisumbua, kwa hofu niliyokuwanayo niliwaambia siwezi kulala peke yangu mle chumbani.
Akina mama walikubaliana nami tukaenda chumbani kwao ambako tuliendelea kuongea kuhusu jinamizi hilo.
Mama mkubwa alisema alishangazwa sana na jambo hilo kwani tangu alipohamia pale aliwahi kukabwa mara mbili tena zamani, baada hapo haikuwahi kutokea tena.
Kulipokucha nilijiandaa, kutokana na baridi ya Mbeya nilikunywa chai na kipande cha mkate mweusi ulioandaliwa na mama mkubwa ambaye alikuwa akipenda sana kitafunwa hicho kisha niliwaaga akina mama.
Wakati wa kwenda shuleni ilikuwa lazima nipite kwenye uwanja wa nyumba ya mama mmoja sitapenda kumtaja kwa jina, nikamkuta akifagia, nilipomsalimia hakuitikia.
Awali nilifikirim hakunisikia, nikamwamkia tena akawa bize kufagia, nikaamua kumuacha nikaongeza mwendo kuelekea shuleni lakini nikawa najiuliza nilimkosea nini yule mama mpaka asiitikie salamu yangu.
Hata hivyo, kwa akili za kitoto wala sikumfuatilia. Nilipofika shuleni, tulifanya usafi wa mazingira kisha tuliingia darasani tayari kwa kuanza vipindi.
Nakumbuka siku hiyo mwalimu wa kwaza kuingia darasani alikuwa wa kipindi cha hesabu, alipokuwa akitufundisha ghafla nilihisi kichwa kuniuma.
Mwanzo nilifikiria kingepoa lakini kadiri muda ulivyosonga mbele kikazidi kuniuma, nikainama chini ya dawati.
Mwalimu aliponiona aliniuliza sababu za kuinama chini, nilimwambia kichwa kilikuwa kinauma, jambo la kushangaza nilipomweleza hivyo mwalimu, kichwa kikazidi kuuna nikashindwa kuvumilia nikaanza kulia.
Yule mwalimu kwa kushirikiana na wanafunzi watatu walinibeba na kunipeleka ofisini ambako niliendelea kulia, mwalimu alimuuliza mmoja wa wale wanafunzi kama alikuwa akipahamu nyumbani ili akamwambie mama.
Kwa kuwa yule mwanafunzi alikuwa anapajua nyumbani, alikwenda mbio, kwa bahati mbaya hakumkuta mama wala mama mkubwa kwani walikuwa wamekwenda kwenye biashara zao.
Kwa kuwa kutoka pale shuleni kwenda ilipokuwa zahanati hapakuwa mbali, walimu wawili na mwanafunzi mmoja walinipeleka, nikafanyiwa kipimo cha malaria
Majibu yalipotoka sikuwa nayo, nilipewa dawa ya kutuliza maumivu, hata baada ya kumeza bado kichwa kilikuwa kikiuma sana.
Wakati walimu na daktari wakitafakari, akina mama walipopewa taarifa nwa mwanafunzi mmoja walifika na kuniuliza nini kilikuwa kikinisumbua, kwa shida niliwaambia kichwa.
Je,nini kitaendelea?