Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,166
*SIMULIZI YA DORCAS-01*
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 25 ambaye ni yatima niliyezaliwa peke yangu kwa wazazi wangu ambao sikubahatika kuwaona, kwa sasa naishi jijini Dar es Salaam.
Kutokana na mikasa niliyopitia maishani mwangu, sitapenda kuliweka wazi jina langu halisi ila nitambue kwa jina la Dorcas.
Kwa mujibu wa mama niliyejikuta nipo mikononi mwake kimalezi, mama yangu yangu alikuwa mtu wa Rukwa na baba yangu alikuwa raia wa Zambia aliyekuwa akifanya biashara za bidhaa tofauti pamoja na samaki kutoka Ziwa Tanganyika eneo la Nkasi na kuwapeleka kwao Zambia.
Nilielezwa kwamba, mama na baba walikutana Kilando Namanyele, Rukwa wakaanzisha uhusiano wa kimapenzi ambao ulisababisha kupata ujauzito ambao mama aliubaini baada ya baba kurudi kwao.
Nilielezwa na mama huyo ambaye alifahamiana na mama mjini Sumbawanga katika biashara zao kwamba, mama alipobaini alikuwa mjamzito alitarajia baba akifika Kilando angemfahamisha kuhusu hali yake.
Jambo la kusikitisha ni kwamba baba hakurudi tena Tanzania ambapo mpaka leo haijulikani kama alikufa au alikumbwa na masaibu gani.
Kwa mujibu wa mama huyo ambaye naye hivi sasa ni marehemu, mama aliyekuwa amepanga chumba eneo la Chanji Sumbawanga aliendelea kuilea ile mimba peke yake.
Mama mlezi aliniambia kwamba, mama alipokaribia kujifungua alikwenda kwao Mpanda ili Mungu atakapomsaidia kujifungua salama awe chini ya uangalizi wa wazazi na ndugu zake.
Rafiki huyo wa mama aliniambia alimfanyia maandalizi ya safari ambapo mama alikwenda Mpanda akajifungua salama na kurejea Sumbawanga mjini kuendelea na maisha.
Aliongeza kunieleza kwamba, waliendelea kushirikiana na mama waliyeitana mtu na mdogo wake kiasi cha watu ambao hawakuwafahamu vizuri kudhani walikuwa ndugu wa damu.
Maisha yaliendelea lakini kutokana na mama kuwa na mtoto mdogo yaani mimi, hakuweza kusafiri kwenda mbali zaidi ya kuwa bize kunilea na kufanya biashara ndogondogo.
Nilielezwa kuwa nilipofikisha miezi sita, mama aliondoka na mimi kwenda mkoani Mbeya kwa rafiki yake waliyesoma pamoja aliyemuomba aende huko wakashirikiane kufanya biashara.
Kufuatia ombi hilo la rafiki yake, mama alikwenda Mbeya na kufikia Isanga ambapo rafiki yake huyo ambaye ni Mnyakyusa wa Masukulu wilayani Rungwe alikuwa amepanga chumba.
Mama huyo alinieleza, mama na rafiki yake huyo walikuwa wakifanya biashara ya kununua marahage, mchele na mahindi na kwenda kuyauza.
Wakati mwingine, siku ya Jumanne na Ijumaa ambayo inakuwa na mdana sehemu inayoitwa Kiwira, walikuwa wakienda kufanya biashara huko.
Aliongeza kunieleza kuwa, kwa vile hawakuwa na mtaji mkubwa walikuwa wanapata fedha kiasi walizoendeshea maisha yao huku mama akinilea.
Baada ya mama kukaa Mbeya kama miezi sita alikutana na mama mmoja wa Sumbawanga ambaye alikuwa akifahamu uhusiano wake na baba akamwambia aliwahi kumuona baba akifanya biashara zake Nkasi.
Kufuatia habari hiyo ambayo kwa mama ilikuwa njema sana, aliamua kurudi Sumbawanga kwa lengo la kwenda Nkasi akiwa na imani kabisa angeweza kukutana na baba.
Lengo lake lilikuwa ni kumuonesha mwanaye (mimi) na kama angekuwa tayari waanze kuishi maisha ya mume na mke.
Yule mama alinieleza, alipomshirikisha rafiki yake wa Mbeya alifurahi sana. Baada ya maandalizi tuliondoka na mama kwenda Sumbawanga na kufikia kwa rafiki wa mama aliyekuwa anaitwa mama James.
Sumbawanga tulikaa wiki moja tukaenda Kirando lengo likiwa ni kumtafuta baba.
Baada ya kuwasili Kirando, tulifikia kwa mama mmoja Mfipa ambaye alitupokea vizuri, mama huyo na mama walikuwa wanafahamiana vizuri.
Kwa mujibu wa mama huyo, siku iliyofuata, tulikwenda Nkasi ambako baba alikuwa akipeleka biashara zake na kuwauliza watu kama walikuwa wakimuona.
Jambo la kusikitisha ni kwamba, tulipofika huko baadhi ya watu walisema waliwahi kumuona na wengine walisema hawakuwahi kumuona muda mrefu.
Mama huyo alisema kwa jinsi mama alivyokuwa akihaha kumtafuta baba, wapo wanaume waliomtania kwamba kama angewakubalia walipokuwa wakimtokea asingepata tabu lakini kwa kuwa ‘alimshobokea’ Mzambia ndiyo ilikuwa faida yake.
Aliongeza kuwa, kauli za watu hao zilimuumiza mama ambaye licha ya kukaa kule mwezi mmoja akiamini siku moja baba angefika na kuonana naye hazikuzaa matunda.
Baada ya mama kukaa muda huo alikata tamaa akarudi Sumbawanga kwa rafiki yake ambapo aliendelea na biashara zake huku akinilea.
Niliambiwa kwamba wakati wa udogo wangu sikuwa nasumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara na watu walikuwa wakimpongeza mama kwa kunizaa mtoto mzuri.
Maisha yaliendelea huku mama na rafiki yake wakifanya biashara ndogondogo lakini baada ya mwaka mmoja, Yule rafiki wa mama wa Mbeya alimtumia ujumbe kwamba alimhitaji aende huko.
Tulikwenda Mbeya, ambapo mama aliendelea na maisha. Kwa bahati mbaya sana kwa muda wote huo mama hakuwahi kunipeleka Mpanda ili nikaujue ukoo wake.
Nikiwa na miaka minne tukiwa Mbeya, aliwahi kuja mwanaume mmoja ambaye mama alinitambulisha kwamba alikuwa mjomba wangu.
Mama alinitambulisha kwamba mjomba wangu huyo alikuwa anaitwa Samweli na kwamba alikuwa akiishi Morogoro alikokuwa akifanya kazi katika mashamba ya miwa ya Mtibwa.
Mjomba wangu alifurahi sana kuniona, siku hiyo hiyo alipokula alituaga kwamba anakwenda Tunduma kisha Mpanda kuwasalimia wazazi na ndugu wengine.
Ingawa nilikuwa mdogo nilitamani sana kuongozana naye lakini mama aliniambia tungeenda wote atakapopata muda, nikamwambia sawa na maisha yakaendelea.
Kwa kuwa nilikuwa mtundu sana, nikiwa na miaka mitano nilipelekwa katika shule moja ya chekechea ambayo haikuwa mbali na eneo tulilokuwa tukiishi.
Maisha yaliendelea hadi nilipoanza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Isanga, kwa kuwa kipindi hicho nilikuwa nina ufahamu nilitamani sana kumuona baba.
Kila nilipokuwa nikimuuliza mama baba yangu alikuwa wapi, alikuwa akiniambia alikuwa nchini Zambia, nilipomwambia lini angenipeleka nikamuone akawa ananidanganya tu siku zikawa zinakwenda.
Kuna wakati nilipokuwa namuuliza alikuwa akikosa raha na kuanza kulia, nilipohoji sababu za kulia alikuwa akinidanganya kwamba alikuwa anaumwa.
Ukweli ni kwamba kitendo cha mimi kutaka kumuona baba yangu ambaye hakujua alikuwa wapi kilimuweka katika wakati mgumu sana.
Nakumbuka siku moja rafiki yake ambaye nilikuwa namuita mama mkubwa, aliniita.
Nilipoitika aliniambia nikakae karibu yake, wakati huo mama alikuwa amekaa kwenye kiti kilichokaribiana naye.
“Dorcas!” mama huyo aliniita tena.
Nilipoitika aliniambia kwamba nilikuwa mtoto mzuri sana na mwenye akili nyingi, nikamshukuru, wakati huo sikujua mama mkubwa alitaka kuniambia nini.
Nilipomwambia ndiyo, akasema baba yangu alikuwepo hivyo nisiwe na wasiwasi ipo siku nitamuona kikubwa kuomba uzima, akaniomba nisiwe namuuliza mama kila wakati habari za baba.
Baada ya mama mkubwa kutoa kauli hiyo, mama alinitazama kwa huruma akaanza kulia, mama mkubwa akaanza kumbembeleza na kumsihi anyamaze kwani haikuwa vizuri.
“Dada naumia sana niache nilie tu!” mama alimwambia mama mkubwa.
Kitendo cha mama kulia, kilinihuzunisha sana nami nikajikuta nalia bila kujua kilichomliza mama, mama mkubwa akawa na kazi ya ziada kutunyamazisha.
Je, nini kiliendelea?