Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,167
- Thread starter
- #41
*DORCAS-08*
Baada ya kuwaeleza hivyo, mama alianza kulia na kusema kama baba yangu angekuwepo yote yaliyokuwa yakinitokea yasingetokea, nami nikaanza kulia.
Kufuatia mama kulia, mama mkubwa alimsihi na kumwambia hata kama baba angekuwepo mambo hayo yangetokea kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa tabia ya wachawi.
Licha ya mama mkubwa kutoa kauli hiyo, mama alisisitiza kwamba anaamini baba asingekubalia nichezewe namna ile akaendelea kulia jambo lililonifanya name niungane naye.
Mama mkubwa alifanya kazi ya ziada kutunyamazisha, tukiwa tumetulia alimwambia mama Jumamosi twende tena kwa yule mganga wa Songwe tukamwelezee kilichotokea.
“Kwa hali ilivyo lazima twende tukamuone,” mama alimwambia mama mkubwa.
Baada ya kupata chakula, niliondoka na akina mama kwenda kwenye biashara zao ambapo tulirejea nyumbani saa 12 jioni, tuliendelea na mambo mengine kisha tulilala.
Usiku wa siku hiyo tulilala vizuri hadi kulipokucha ambapo nilijiandaa na kwenda shuleni, nikiwa shuluni baadhi ya walimu waliniuliza kuhusu maendeleo yangu niliwaambia yalikuwa mazuri.
Alasili niliporejea nyumbani, nilimkuta mama akiwa amelala akilalamika maumivu ya tumbo na juu ya meza ndogo palikuwa na vidonge.
Nilipouliza alianza kusumbuliwa na tumbo muda gani mama mkubwa alinifahamisha kwamba lilianza kumuuma ghafla wakiwa sokoni kwenye biashara zao.
Kitendo cha mama kuumwa kilinikosesha raha, licha ya maradha kadhaa kupenda kwenda kucheza na wenzangu baada ya kutoka shuleni, siku hiyo sikutoka kabisa.
Mama alisumbuliwa na tumbo hilo kwa siku mbili, ilipofika Jumamosi tulikwenda kwa yule mganga, alipoangalia kupitia zana zake alibaini mama alitupiwa kitu tumboni.
Mganga huyo alitufahamisha kwamba yule mama mchawi ndiye aliyfanya hivyo na kuongeza kwamba bila ya kutuchanjia dawa mimi au mama tungekuwa tumepoteza maisha.
Aliongeza kuwa siku niliyotokewa nap aka alikuwa yeye na alipanga kunimaliza lakini alishindwa na baadaye alinifuata nyumbani nikiwa nimelala lakini pia alishindwa kunidhuru.
Mganga huyo aliwauliza akina mama amfanye nini mchawi yule ambaye alipanga kutuletea madhara makubwa, mama mkubwa aliomba kama anaweza amamalize kabisa lakini mama alipinga.
Mganga hakuwa na la kufanya, alimpatia mama dawa ambayo alisema akinywa atatapika na kitu alichorushiwa kitatoka na atakuwa mzima.
Baada ya kufika nyumbani, mama alichemsha dawa aliyopewa ilipopoa alikunywa kikombe kizima, hakumaliza dakika tano alianza kuharisha na kutapika mpaka akaishiwa nguvu.
Alipomaliza mama mkubwa alimpikia uji, alipokunywa alianza kutapika na kuanza kusema shingoni kulikuwa na kitu kikimkaba akaanza kutapika tena ndipo kilitoka kitambaa cheusi kilichofungwa.
Mama mkubwa alipokifungua, wote tulipigwa butwaa kuona ndani mkiwa na mchele, maharage, unga na njugu mawe, jambo hilo lilitushangaza na kuamini kweli duniani kulikuwa na uchawi.
Mama mkubwa alichukua zile nafaka na kitambaa na kwenda kuvichoma moto nje, tangu hapo mama aliacha kulalamika kupata maumivu zaidi kilichomkabili ni mwili kuishiwa nguvu.
Kama alivyofanya awali alimpikia uji akaweka limao, mama alipokunywa hakutapika tena, siku iliyofuata asubuhi na mapema alituambia kwamba aliota ndoto kwamba baba yangu alikuwa Nkasi hivyo alitaka kwenda kumtafuta kwani aliumia sana mimi kuendelea kuteseka bila kumuona baba yangu.
Licha ya mama mkubwa kumshauri kwamba ndoto zilikuwa ndoto tu asiende kwani angepoteza muda wake na kwamba ipo siku baba angejitokeza kama huko alikokuwa alikuwa hai lakini mama alisema atakwenda Nkasi.
Kwa kuwa alikuwa na fedha, baada ya maandalizi ya siku mbili aliondoka kuelekea Rukwa na kuniacha na mama mkubwa, tangu alipoondoka sikupatwa na tatizo lolote.
Wiki mbili baadaye, tulipata taarifa ya kuhuzunisha kuhusu kifo cha mama kilichotokana na ajali ya gali, siku hiyo nililia sana, kwa upande wa mama mkubwa aliishia kuzungumza peke yake na kusema kifo cha mama kilikuwa na mkono wa mtu.
Ukweli sitakaa nisahau siku hiyo ambayo kila ninapoikumbuka huwa nalia, baada ya taarifa hiyo tuliondoka na mama mkubwa na kwenda Mpanda kwa babu.
Nilipofika nilipokelewa vizuri na ukoo wa mama ambao siyo mkubwa sana na baada ya wiki moja mama mkubwa aliwaaga tayari kwa kurejea Mbeya.
Hata hivyo, bibi na mjomba wangu mmoja walimuomba mama mkubwa aniache kule kijijini lakini alikataa na kuwaeleza kwa kuwa rafiki yake alifariki dunia yeye atanilea na kunisomesha hivyo wasiwe na wasiwasi.
Baada ya kuwaeleza hivyo, hawakuwa na kipingamizi ndipo tuliondoka na mama mkubwa tukarudi Mbeya kuendelea na maisha ya upweke.
Siku za mwanzo nilikuwa katika wakati mgumu sana lakini kwa kuwa binadamu tunasahau kadiri siku zilivyosonga mbele nilizoea na kumchukulia mama mkubwa kama mama yangu mzazi.
Wakati huo nilikuwa sielewi kama katika maisha yangu ningekumbwa na masaibu ambayo yangenifanya niichukie dunia na kutamani kumfuata mama yangu.
Baada ya kurejea kutoka msibani, nilikaa mwezi mmoja bila kupata tatizo lolote, siku moja usiku nikiwa nimelala nilishtuka usingizini nikakiona kimvuli cha mtu kikiwa kimesimama pembeni ya mlango.
Kutokana na uwoga niliokuwanao nikaamua kumwita mama mkubwa lakini katika hali ambayo mpaka leo nashindwa kuielewa sauti haikutoka, ghala nikashtikiwa nakabwa shingoni huku mtu aliyenikaba akisem nitamtambua.
Kila nilipojitahidi kumwita mama nilishindwa ndipo nikaanza kumuomba Mungu kimoyomoyo na kusema; Mungu nisaidie, Mungu nisaidie, niliendelea kusema hivyo ndipo yule mtu akaniacha na kutoa msonyo.
“Leo ningekuuliza mbali mweu wewe na ipo siku nitafanikiwa eti unamuita Mungu wako, nani ambaye hana Mungu,” mtu huyo alitoa kauli hiyo na kutoweka.
Baada ya kutoweka, nilimuita mama mkubwa ambaye alikuja chumbani kwangu na kunikuta nalia, aliponiuliza sababu nilimweleza kila kitu, nikahamia chumbani kwake.
Kulipokucha alinifahamisha kwamba alivumilia sana vitimbi vilivyokuwa vikitokea kwenye ile nyumba na kusema kodi yake ikiisha angetafuta nyumba sehemu nyingine.
Nilimshukuru sana kwa uamuzi huo, baada ya kujiandaa nilikwenda shuleni ambapo muda mwingi nilikuwa namuwaza mama na kujiuliza hivi ni lini nitaacha kusumbuliwa na wachawi ili nami nilale kwa amani!
Nakumbuka siku ya Jumamosi nikiwa nyumbani alifika yule mama rafiki yake mama mkubwa wa Shinyanga, mama mkubwa alipomkea kwa furaha.
Baada ya salamu, alimwuliza mama mkubwa mama alikuwa wapi, badala ya kumjibu mama mkubwa alinitazama usoni kisha akamtazama yule mgeni na kuishia kuguna.
Mgeni alipomuuliza sababu za kuguna alimwambia basi tu, alipotoa kauli hiyo nikajikuta natiririkwa na machozi na kuanza kujifuta kwa kutumia viganja.
Kitendo hicho kilimshtua yule mama akamwuliza sababu za kulia ndipo alimfahamisha kwamba mama alifariki dunia na kulia kwangu kulisababishwa na kumkumbusha msiba wa mama.
Yule mgeni alipata huzuni na kumuuliza mama mkubwa kama alichokisema kilikuwa kweli, akamwambia hakuwa na sababu ya kumuongopea kwenye suala la kifo, alijongea kwa mama mkubwa na kumkumbatia akaanza kulia na kumpa pole.
Alipomaliza kumpa pole alihamia kwangu, licha ya kwamba nilikuwa binti mkubwa alinipakata na kunipa pole, kwa dakika kadhaa nyumba ya mama mkubwa iligubikwa na vilio lakini baadaye tulinyamaza.
Baada ya kunyamaza, yule mama alimuuliza mama mkubwa sababu za kifo cha mama, alimfahamisha kwamba kilitokana na ajali.
Taarifa hiyo ilimhuzunisha sana yule mama akatupa pole na kusema kama angepata taarifa za msiba wa mama tungeungana naye kwenda Mpanda.
Baada ya kutufariji kwa muda, yule mama alifungua mkoba wake na kutoa pochi ndogo ambayo aliifungua na kutoa shilingi 20,000, elfu kumi alinipatia na kumi nyingine alimpatia mama mkubwa kama pole.
Hakuishia hapo, alifungua begi lingine akatoa kitenge kimoja akampatia mama mkubwa, mimi alinipatia gauni zuri sana ambalo alisema alikuwa ameliandaa kama zawadi yangu.
Je, nini kitaendelea?