Simulizi: Scaila Michael

Simulizi: Scaila Michael

SEHEMU YA 33

Hapo akili yangu ikapiga kengele. Jina hilo halikuwa geni, niliwahi kulihisi kabla. Siku ile nilipokuwa nikila chakula na Scaila, namba hiyo ilipiga kwenye simu yake, sikuwa na uhakika kama jina lilikuwa Alfred ama Albert, ila leo nikapata uhakika kwamba mtu aliyepiga alikuwa huyo Alfred, ila yeye aliniambia alikuwa Janeth.

Hapo nikashikwa na machale zaidi, nikahisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, ila kwa sababu nilikuwa mwanaume, sikutaka kujali sana, nikajifanya kupotezea na hapo ndipo nilipoanza kazi rasmi ya kumchunguza huyu Scaila.

Niligundua inawezekana alikuwa na michezo mingi nje ya kumi na nane aliyokuwa akiicheza ila sikuwa nikiijua kwa undani. Ilikuwa ni lazima nifanye kila linalowezekana kuhakikisha naujua ukweli kabisa.

Scaila hakuwa demu, alikuwa mchumba wangu ambaye nilipanga kufunga naye ndoa, hivyo kupoteza muda wangu kwa lengo la kumchunguza halikuwa tatizo hata kidogo.

“Akitoka Alfred ndiyo anaingia Scaila,” aliniambia mama yake bila kuona aibu hata kidogo.

“Nimefurahi kumfahamu!” nilisema huku nikiwa nimetoa tabasamu pana kweli, yaani sikutakiwa kuonekana nikiwa na shaka hata kidogo.

Basi tukaongea mambo mengi, muda mwingi nilikuwa na furaha mno, nilihitaji kuwaaminisha kwamba sikuwa na wasiwasi na Alfred hata kidogo, hivyo ilikuwa ni lazima nionekane nipo kawaida kumbe upande wa pili niliamua kuanza kazi yangu ya kumpeleleza huyu Scaila, alikuwa nani na alijishughulisha na nini?
Nikamchukua na kuanza kurudi naye nyumbani.

Nilimletea unafiki mwingi, stori zilikuwa nyingi mno, nilichangamka kupita kawaida kumbe moyo wangu ulikuwa na maumivu makali mno.

Tukafika nyumbani na kuelekea sebuleni. Tukaingia na kuendelea kupiga stori, tulicheka pamoja na kula kisha kuelekea chumbani.

Siku hiyo nilihitaji kujifanya kuwa bize na mambo yangu kumbe nilihitaji kufanya jambo fulani kubwa. Nilijua kuhusu mambo ya kompyuta, jinsi application ya WhatsApp ilivyokuwa ikifanya kazi kwenye kompyuta kupitia kitu kiitwacho WhatsApp Web.
Alijua kapata Manzi kumbe kapata Jambazi....

Nyemo pole yako wenzio huingia mguu mmoja wewe umeingia mwili mzima.
 
Hatari sana...

Rafiki yake Nyemo atakua anajua mengi sana kuhusu Scaila...

Nahisi Scaila atakua anajiuza ila akifichwa na mama yake...
Ngoja tuone...


Cc: mahondaw
 
SEHEMU YA 34

Kwa wale wasiojua ni kwamba hii ni system ambayo wenyewe waliiweka kuhamisha mawasiliano yako ya WhatsApp kwenye simu na kuwa kwenye kompyuta, yaani kile kitu ambacho ungeweza kukifanya kwenye simu yako, ulikuwa na uwezo wa kukifanya kwenye kompyuta yako kupitia hiyo WhatsApp Web.

“Bebi naomba tukaoge!” aliniambia Scaila huku akiniangalia.
“Kuna kazi nafanya mamiii, nenda tu halafu nitaoga baadaye,” nilimwambia kwa mahaba yote.

“Nataka kwenda kuoga na wewe mpenzi!” aliniambia kwa sauti ya kudeka.
“Nenda tu! Mimi nitakwenda mpenzi,” nilimwambia, sikuishia hapo, nikambusu mdomoni na kujifanya kuwa bize mno.

Akajifanya kama kuchukia hivi, akachukua simu yake, sijui alikuwa akifanya vitu gani lakini akili yangu iliniambia alikuwa akifuta mawasiliano fulani hivi.

Baada ya kumaliza, akavua nguo zake, akavaa taulo na kuelekea bafuni. Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yangu, niliposikia ameanza kujimwagia maji, nikachukua simu yake, haraka sana nikafungua WhatsApp na kisha kwenye kompyuta yangu kufungua WhatsApp Web na kuanza kuscan barcode nilizokuwa nimepewa.

Ni ndani ya sekunde tano, kitu kikajipa, ile WhatsApp yake ikaanza kuonekana kwenye kompyuta yangu, hivho ndicho nilichokuwa ninakitaka, nikafunga kwenye simu yake na kuirudisha ilipokuwa.

Nilihitaji kumfuatilia bila kufahamu lolote lile. Nilitulia chumbani kimya huku nikijifanya kuwa bize. Baada ya kumaliza, akatoka, akavaa nguo ya kulalia na kuja pembeni yangu kuona nilivyokuwa nikifanya mambo yangu.

Alikaa na kuangalia kompyuta kwa dakika kadhaa, akachoka na hivyo kuchukua simu yake, akageukia upande wa pili na kuanza kuchati na watu wake.

Haraka sana nikafungua WhatsApp yake kupitia kompyuta yangu na kuanza kufuatilia, yaani nilitaka kujua kama alikuwa akichati WhatsApp au sehemu nyingine. Ghafla nikaona meseji imetumwa kwenda kwa mtu aliyeseviwa kama Alfred.

Scaila: Baby!
Alfred: Leo nimeshikwa na wivu mkali sana.

Scaila: Kwa sababu gani?
Alfred: Yule jamaa aliyekuja, unayemuita mpenzi wako!
Scaila: Hahaha! Asikuogopeshe bwana! Lile buzi langu tu, ameleta shobo na mimi naruka naye!
 
SEHEMU YA 35

Nilishikwa na hasira sana lakini nikajikaza kisabuni. Nilijifanya kuwa bize kupita kawaida. Mwili wangu ulikuwa unatetemeka mno huku kijasho chembamba kikinitoka mwili mzima.

Yaani mtu ambaye nilipanga awe mke wangu wa ndoa, niliyemshirikisha kila kitu kwenye biashara zangu leo hii alikuwa akiniita buzi kwa mwanaume ambaye inawezekana hakuwa na ndoto naye kabisa.

Alfred: Ila leo umekatika kwa kiwango cha juu kabisa. Jamaa alikufundisha nini?

Scaila: Hakuna! Maufundi yangu mwenyewe tu. Ila hata wewe umenikuna mno, yaani hapa jamaa nitambania hata kwa siku tatu, sina hamu kabisa mpenzi.

Nikashusha pumzi ndefu, Scaila akaniangalia lakini nikajifanya kuwa bize mno. Moyo wangu ulikuwa na hasira, ulivimba lakini sikutaka kabisa kumuonyesha mabadiliko hayo.

Baada ya sekunde kadhaa, nikaona Janeth ametuma meseji.
Janeth: Kipenzi....
Scaila: Niambie kipenzi.

Janeth: Lini tutaenda klabu?
Scaila: Mh! Klabu? Sijajua! Huyu jamaa ananichunga sana, ila nimepamiss, nimewamiss wapenzi wangu, nimemiss kufanya mapenzi kwenye gari jomoniiiiiiii.
Janeth: Jitahidi siku twende, mabuzi yako yanakuulizia sana, hasa yule mzee wa Mbezi Beach.

Scaila: Yule mwenye V8 ama Hummer?
Janeth: Range Rover SUV.

Scaila: Ooh! Nimemkumbuka! Basi kuna siku nitakuja na kuonana nao wote.
Wakati nikisoma mawasiliano hayo moyo wangu ulikuwa ukichoma kama pasi, sikuamini hata kidogo juu ya kile nilichokuwa nikiakiangalia.

Yaani huyu Scaila ambaye nilikuwa nikimpenda, kumuahidi mambo mengi ndiye ambaye alikuwa akiafanya hayo yote.

Niligundua alikuwa malaya, hakuwa msichana wa kutulia. Hapo ndipo nilipoamini wanawake wengi hawakuwa na akili hata kidogo.

Wengi wao walihitaji ndoa, lakini wale waliokuwa na nafasi ya kuolewa hawakutaka kujali hata kidogo. Hebu mfikirie mtu kama Scaila, nilimwambia kabisa lengo langu lilikuwa ni kumuoa, nilimshirikisha kwenye mambo yangu mengi lakini mwisho wa siku anaamua tu kutamani kuyaishi maisha aliyokuwa akiyaishi hapo kabla.

Alipomaliza kuchati na Janeth, akayafuta mawasiliano hayo na yale ya Alfred. Kiukweli siku hiyo niliumia sana moyoni mwangu, aliniangalia huku akitoa tabasamu pana kupita kawaida.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom