Simulizi: Scaila Michael

Simulizi: Scaila Michael

Hahaha ngoja nikwambie sasa ukiona kila uzi sipatikaniki njo chit chat kwenye uzi wa makapuku kule ndio nyumbani lazima niwepo
bora nimekujua Nik login nisikuone Na kuwa mnyonge ghafla umenipa nini? We mtoto
 
Nilishacomment hapa huyu Scaila ni Malaya ndo maana Hiza alipomwona akashtuka nahisi alishakutana nae club anauza papuchi
 
SEHEMU YA 36

Huyu alikuwa muuaji aliyekuwa akitabasamu, alihitaji kuniua huku akiachia tabasamu pana usoni mwake. Sikutaka kuonyesha wasiwasi wowote ule, na mimi nikaendelea kutabasamu huku nikionekana kuwa na furaha tele, kumbe ukweli ni kwamba moyo wangu ulichoma kupita kawaida.

Siku hiyo sikulala usiku mzima, nilikuwa nikimfikisia Scaila tu, yale madudu yake yalinichanganya kupita kawaida. Kuna wakati nilimkumbuka sana Shasta, yule msichana japokuwa alikuwa akiolewa lakini niliamini moyoni mwangu kwamba alikuwa mtu pekee aliyeumbwa kwa ajili yangu.

Nilifanya haraka sana kumchukua Scaila, ilikuwa ni lazima nipate muda wa kumchunguza na ndipo nifanye maamuzi ya kuishi naye lakini sikufanya hivyo, nilivua nguo na kutumbukia baharini pasipo kuangalia ni baridi kiasi gani maji hayo yalikuwa.

Mpaka asubuhi inaingia sikumuonyeshea tofauti yoyote ile japokuwa kwa kipindi hicho nilitakiwa kuwa makini sana. Kama kawaida yangu nilimsogelea na kumbusu shavuni, nikainuka kitandani, nikaenda bafuni na kuanza kuoga.

Kwa kweli moyo wangu ulivurugika mno, kuna kipindi nilifikiria kumuacha lakini nikalifuta wazo hilo kwa sababu sikuwa na ushahidi wa kutosha, yaani kama ningemuacha, angeniuliza kwa sababu gani na mimi nisingekuwa na jibu lolote lile.

Nilichokifanya ni kuendelea kuishi naye huku nikihitaji kukusanya ushahidi kwa kiasi kikubwa, siku nikija kumuacha, basi nimuache huku mwenyewe akiona kweli alizingua na alistahili kuachwa.

Wakati nikiendelea kufikiria hayo, nikamkumbuka Hiza. Siku ambayo alikuja nyumbani na Ally na kuwatambulisha kwa Scaila, alionekana kushtuka sana kumuona mahali pale.

Japokuwa nilimuuliza juu ya mshtuko wake lakini alizungumza mambo ambayo hayakuniingia akilini hata kidogo. Nilihisi kulikuwa na kitu fulani hivi alichokuwa akikifahamu ambacho ilikuwa ni lazima na mimi nikifahamu.

Haraka sana nilipomaliza kuoga na kuvaa, nikamkumbatia na kumuaga nakwenda kwenye biashara zangu, akanibusu mfululizo huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana.
 
SEHEMU YA 37

Nikatoka, nikaingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo huku akili yangu ikiwa imevurugika kabisa. Haraka sana nikampigia simu Hiza na kuomba kuonana naye kwani kulikuwa na mambo nilihitaji kuzungumza.

“Kuna ishu gani mbaba?” aliniuliza Hiza.
“Kawaida tu! Kuna jambo linanisumbua kichwani!” nilimjibu.

“Poa basi! Njoo home kama vipi?”
“Huko Mbezi?”
“Ndiyo! Si una shida, njoo huku dogo,” aliniambia, hiyo ilikuwa kawaida yake, tulikuwa tunataniana kupita kawaida japokuwa nilimpita miaka mingi.

Hilo halikuwa tatizo, nikabadilisha muelekeo na kuanza kuelekea Mbezi huku lengo langu likiwa ni kuonana naye na kuzungumza kuhusu Scaila.

Nilichukua nusu saa kufika nyumbani kwake, nikateremka na kuelekea mahali ulipokuwa mlango wa sebuleni na kuingia ndani.

Kama kawaida yake nikamkuta na wasichana wawili. Kwenye maisha yangu Hiza alikuwa mtu wa hivyo, alipenda sana wanawake, aliwahusudu kupita kawaida na muda mwingi aliwachukua kutoka klabu na kwenda kulala nao mpaka asubuhi.

Niliwasalimia, sikutaka kukaa sana hivyo ilikuwa ni lazima nizungumze naye kuhusu kile kilichokuwa kimenileta mahali pale.
 
SEHEMU YA 38

“Mbona unaonekana hivyo? Kuna nini?” aliuliza Hiza.
“Kuna jambo linanitatiza sana.”
“Lipi sasa?”

“Kuhusu Scaila!”
“Hahah! Umeanza sasa! Bado mapema mno kugombana!” aliniambia huku akicheka.

“Hiza! Naomba unisaidie! Niambie kitu chochote kile unachokifahamu kuhusu Scaila,” nilimwambia.

“Kitu ninachokifahamu kuhusu Scaila? Kitu gani?” aliniuliza.
“Wewe unafahamu nini?”
“Sifahamu chochote! Si nimemuona mara moja tu jamani!” aliniambia.

“Hiza! Mimi ni rafiki yako! Unatamani kuona siku moja naua kisa mapenzi? Unatamani kuona kuna siku nakaa chumbani na kuanza kulia kisa mapenzi na wakati una uwezo wa kunisaidia?” nilimuuliza Hiza.

“Sasa wewe unataka nikwambie nini kuhusu Scaila?” aliniuliza.
“Unachokifahamu! Siku ile ulivyokuja nyumbani, ulivyomuona, ulishtuka! Kwa nini ulishtuka?” nilimuuliza.
“Nyemo! Wapenzi hawaachani!”
“Ila mimi nitamuacha!”

“Hapana! Kuna siku utakaa chumbani na Scaila na kuanza kuniteta kwamba sifai na nilitaka muachane! Kaubebe msalaba wako kaka,” aliniambia huku akinyanyuka na kwenda kwenye friji kuchukua juisi, na mimi nikasimama na kumfuata.

“Hiza! Naomba unielewe! Nimechanganyikiwa!”
“Kilichokuchanganya?”

“Nimegundua kwamba Scaila si mwanamke aliyetulia, ni mwanamke wa klabu, ni malaya tu, anatembea na vibabu, yaani naweza kusema anajiuza,” nilimwambia kwa unyonge.

“Hahaha! Pole sana rafiki yangu!”
“Nashukuru sana! Naomba uniambie kuhusu yeye!” nilimwambia.
“Hahaha...Scaila...Scaila...Scaila...” alisema Hiza huku akicheka kivivu.


|
|
|
Je, nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom