hadithi Nzuri hongera mtunzi.
Yatakayotokea ni kwamba kina Ally wanamjua scaila ndani njeSEHEMU YA 27
Wakati mwingine nilimchukua na kwenda naye huko ilipokuwa nyumba hiyo, mafundi walikuwa wakiendelea kuijenga kwa nguvu kubwa, kila siku ilikuwa ni lazima wafike hapo na kuendelea na mambo yao.
Nilipanga kuhamia ndani ya nyumba hiyo siku ambayo nitafunga ndoa na Scaila. Nilimueleza hilo kabisa lakini sikutaka kumwambia ni siku gani nilitamani sana kumuoa.
Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni Jumapili ya mwezi wa tatu, nilipokea simu kutoka kwa Hiza na Ally ambao waliniambia walikuwa wakija nyumbani kumuona shemeji yao maana kila siku niliwaambia waje kumuona ila walikuwa na mambo mengi.
Nilimwambia Scaila, nikamwambia ni lazima ahakikishe anavaa vizuri, anapendeza ili marafiki hao watakapokuja basi wachanganyikiwe na kuona nimekuwa mwanaume ninayejua kuchagua mwanamke mzuri.
Hawa wawili huwa wananijua, sikuwa mtu mwepesi kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, ninapenda sana kukaa singo kwa kipindi kirefu nikifanya mambo yangu binafsi ila ninapoamua kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi, huwa ninamchagua mwanamke mzuri mno.
Walinizoea hivyo tangu tulipokuwa chuo mpaka kipindi hicho.
Katika kipindi chote huko nyuma waliniambia siku ambayo ningeoa, basi ningemuoa mwanamke mbaya kuliko wote katika dunia hii kwa sababu tu nilipenda kutembea na wanawake wazuri.
“Huyo mkeo, najua atakuwaje! Nishapata picha yale,” aliniambia Hiza huku akicheka, kipindi hicho tulikuwa chuo.
“Mke wangu atakuwa mkali sana, zaidi ya mkeo, zaidi ya mke wa Ally, yaani atakuwa pini, pini kweli,” nilimwambia.
“Hahaha! Mzee baba utachagua koroma!” alisema Ally.
“Mtaona tu.”
Maneno hayo niliyakumbuka vilivyo, niliwatambia sana na sasa ulikuwa muda wa kuwaonyeshea nilikuwa makini kwa kile nilichowaambia miaka ya nyuma, niliamini kila mmoja angemkubali huyu Scaila kwani hakuwa na uzuri wa kawaida.
Ilipofika majira ya saa tisa alasiri, wakanipigia simu na kuniambiwa walikuwa njiani wakija. Nikawakaribisha na kumwambia Scaila ajiandae.
“Wanakuja!” nilimwambia.
“Haina shida. Nawasubiri!” alisema Scaila, hapohapo akamwambia Grace aandae chakula kabisa kwani muda si mrefu wageni wangeingia.
Nahisi hivyo..... wanatakiwa wawe waungwana ili wamsaidie rafiki yao asiingie mwenye ndoa itakayomtesa baadaeSio kama katembea na mmojawapo
@shunie mamaa ya 30 mbonaa siioniiSEHEMU YA 31
Maisha baina yangu na Scaila yalikuwa matamu sana, tulipendana kwa dhati na muda mwingi tulikuwa pamoja.
Sikuyaona madhaifu yake kwa wakati huo, kila nilipokuwa nikirudi nyumbani nilipokelewa kwa mbwembwe nyingi na mahaba tele.
Kiukweli hapo ndipo niligundua unapokuwa kwenye mapenzi mazito una nguvu ya kufanya kitu chochote kile.
Scaila aliuteka moyo wangu, alilifahamu hilo na alihakikisha kila siku ninakuwa mtu wa furaha katika maisha yangu yote.
Kwa kweli sikutaka kumfuatilia kabisa hasa kwenye simu yake, nilihitaji awe huru, afanye lolote analolitaka lakini aniheshimu na kujua kwamba mimi ni mume wake mtarajiwa.
Mambo yalikuwa mazuri mpaka pale ambapo niliona anakuwa bize sana na simu. Kama ni kuchati, basi kwa Scaila ilikuwa si mchezo, kila wakati aliishikilia simu yake na kuandika meseji kwenda kwa watu wengine.
Kwa sababu nilimpenda, sikutaka kabisa kumfuatilia, sikutaka kuona akikasirika kwani yeye ndiye alikuwa furaha yangu katika maisha yangu kipindi hicho.
Nilianza kuingiwa na shaka kuhusu simu yake, ila wakati mwingine nilijiambia sikutakiwa kuwa hivyo kwa sababu nilipenda, na mtu ukimpenda, jambo la kwanza kabisa unatakiwa kumwamini.
Hivyo ilikuwa ni hivyo, hata alipokuwa akiiacha simu yake hapo, iwe inaita au ujumbe wa maneno kuingia wala sikujishughulisha nao hata kidogo.
Nakumbuka kuna siku nilirudi nyumbani majira ya saa kumi, siku hiyo niliwahi kwa sababu nilimaliza biashara zangu mapema sana hasa kwenye kukusanya mahesabu na hivyo nilihitaji muda mwingi wa kupumzika.
Nilipofika nyumbani, nilimkuta Grace lakini Scaila hakuwepo nyumbani. Sikutaka kuwa na wasiwasi naye kwa sababu nilimwamini sana.
Nilikaa sebuleni huku nikiendelea kufanya mambo yangu kwenye kompyuta yangu ya mapajani.
Muda ulikwenda lakini hakurudi nyumbani, nilianza kuingiwa na wasiwasi, ikanibidi nifanye maamuzi ya kumpigia simu na kumuuliza alipokuwa. Kabla ya kufanya hivyo, kitu cha kwanza nikaona lingekuwa jambo jema nijue mahali alipokuwa, nikamuita Grace na kumuuliza.
“Wifi yako yupo wapi?” nilimuuliza.
“Alikwenda kwa mama!” alinijibu.