SEHEMU YA 34
Kwa wale wasiojua ni kwamba hii ni system ambayo wenyewe waliiweka kuhamisha mawasiliano yako ya WhatsApp kwenye simu na kuwa kwenye kompyuta, yaani kile kitu ambacho ungeweza kukifanya kwenye simu yako, ulikuwa na uwezo wa kukifanya kwenye kompyuta yako kupitia hiyo WhatsApp Web.
“Bebi naomba tukaoge!” aliniambia Scaila huku akiniangalia.
“Kuna kazi nafanya mamiii, nenda tu halafu nitaoga baadaye,” nilimwambia kwa mahaba yote.
“Nataka kwenda kuoga na wewe mpenzi!” aliniambia kwa sauti ya kudeka.
“Nenda tu! Mimi nitakwenda mpenzi,” nilimwambia, sikuishia hapo, nikambusu mdomoni na kujifanya kuwa bize mno.
Akajifanya kama kuchukia hivi, akachukua simu yake, sijui alikuwa akifanya vitu gani lakini akili yangu iliniambia alikuwa akifuta mawasiliano fulani hivi.
Baada ya kumaliza, akavua nguo zake, akavaa taulo na kuelekea bafuni. Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yangu, niliposikia ameanza kujimwagia maji, nikachukua simu yake, haraka sana nikafungua WhatsApp na kisha kwenye kompyuta yangu kufungua WhatsApp Web na kuanza kuscan barcode nilizokuwa nimepewa.
Ni ndani ya sekunde tano, kitu kikajipa, ile WhatsApp yake ikaanza kuonekana kwenye kompyuta yangu, hivho ndicho nilichokuwa ninakitaka, nikafunga kwenye simu yake na kuirudisha ilipokuwa.
Nilihitaji kumfuatilia bila kufahamu lolote lile. Nilitulia chumbani kimya huku nikijifanya kuwa bize. Baada ya kumaliza, akatoka, akavaa nguo ya kulalia na kuja pembeni yangu kuona nilivyokuwa nikifanya mambo yangu.
Alikaa na kuangalia kompyuta kwa dakika kadhaa, akachoka na hivyo kuchukua simu yake, akageukia upande wa pili na kuanza kuchati na watu wake.
Haraka sana nikafungua WhatsApp yake kupitia kompyuta yangu na kuanza kufuatilia, yaani nilitaka kujua kama alikuwa akichati WhatsApp au sehemu nyingine. Ghafla nikaona meseji imetumwa kwenda kwa mtu aliyeseviwa kama Alfred.
Scaila: Baby!
Alfred: Leo nimeshikwa na wivu mkali sana.
Scaila: Kwa sababu gani?
Alfred: Yule jamaa aliyekuja, unayemuita mpenzi wako!
Scaila: Hahaha! Asikuogopeshe bwana! Lile buzi langu tu, ameleta shobo na mimi naruka naye!