Simulizi: Scaila Michael

Asante Sana Dada Mwandishi nimejifunza vitu Katika riwaya hii.
Sehemu ya 61.
Inawezekana huyu Scaila alikuwa akielekea kulekule ila nilimuokoa. Huyu Scaila sikukutana naye kanisani au sehemu ya maana sana, nilikutana naye njiani, sehemu ya hovyo, kwenye ajali mbaya lakini ndiyo hivyo nikaja kumuoa na kuwa mke mwema kwangu.
Kuna watu wanahisi kukutana na mtu kanisani ndiyo ndoa huwa bora! Hapana! Kuna watu wanakutana huko lakini ndoa yao kila siku huwa ni ugomvi kana kwamba hawajui chochote kuhusu Mungu.
Kitu cha kwanza kitakachoifanya ndoa kuwa bora, katika kipindi cha uhusiano wenu, unachotakiwa kufanya ni kumtengeneza mwenzako awe bora, mwanaume amtengeneze mwanamke na hivyohivyo mwanamke amtengeneze mwanaume.
Unapomuona amevaa nguo, msifie, mwambie jinsi unavyojivunia kuwa mke ama mchumba wake. Hakuna mtu asiyependa sifa, msifie mara kwa mara, sifia mapishi yake, sifia jitihada zake, mavazi yake, sifia kila kitu kwani usiposifia, huko nje akisifiwa kidogo tu, ndugu yangu hesabia maumivu.
Na cha kuongezea, kwenye uhusiano huo, hakikisha kuna unyenyekevu, utakapokosea, jutia kosa lako, omba msamaha wa dhati na si kujifanya wewe mwanaume hutakiwi kumuomba msamaha mke ama mchumba wako.
MWISHO
Natumaini wote mmejifunza mengi katika simulizi hii, kwa yale ambayo ni mafunzo kwenu, yachukueni lakini yale ambayo yataonekana kuwa mabaya kwenu, yaacheni humuhumu.
Ninashukuru kwa kunifuatilia mwanzo mpaka mwisho wa simulizi hii fupi. Ninachopenda kusema ni kuwashukuru kwa kuniunga mkono kwenye kazi hii kubwa.
Kumbuka Kitabu changu cha Shambulio la Damu kipo mitaani na kinapatikana kwa shilingi 10,000 tu kwa namba zifuatazo.
Dar es Salaam........0718069269.
Posta.....................0713454152
Kona ya Riwaya, Kinondoni....0655228085.
Mwanza.................0762337673
Dodoma.................0719422001
Mbeya....................0625726640
Kagera/Bukoba.......0692936800
Zanzibar.................0674294643
 
Katika hii story Yan kma mim kbsaa imenigusa ,,kilichoandikwa Apo kimenitokea kabisaa na mschana mmoja ivi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom