Simulizi: Penzi lisilo Na Mwisho

Simulizi: Penzi lisilo Na Mwisho

Dah nilikuwa ni msomaji tu wa hizi hadithi ila hii imenisikitisha sana.Big up uko vizur dada.
 
Sehemu ya 36

“Bosi...bosi...bosi...” ilisikika sauti kutoka upande wa simu ya Razak.
“Unasema Casmir...”
“Yadi inaungua...”
“Unasemaje?”

“Yadi ya magari inaungua bosi...inateketea kwa moto muda huu,” ilisikika sauti ya mfanyakazi huyo.
“Ipi?”

“Hii ya Kinondoni...wahi bosi, inateketea kwa moto...” aliendelea kusisitiza Casmir.
“Moto umean...” alitaka kuuliza swali lakini kabla hilo swali halijakamilika, simu ikakatwa na kubaki akiita tu lakini simu hiyo haikuwa hewani tena.

Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kuangalia saa yake, tayari ilikuwa ni saa saba usiku, harakaharaka akakurupuka kutoka kitandani, akawasha taa na harakaharaka kuvaa suruali yake kwa ajili ya kuondoka mahali hapo.
Wakati anajiandaa, Aisha akashtuka kutoka usingizini.

Akapigwa na mshangao, hakujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea mpaka mpenzi wake kuvaa nguo harakaharaka namna ile tayari kwa kuondoka mahali hapo.

“Kuna nini tena?” aliuliza Aisha.
“Yadi inateketea kwa moto...”
“Unasemaje?”

“Nakuja...”
Razak hakutaka kubaki mahali hapo, kwa haraka sana akachomoka chumbani na kuelekea nje, huko, akapanda ndani ya gari lake, mlinzi akafungua geti na kuondoka mahali hapo huku akiwa amechanganyikiwa.

“Yaani yadi inateketea kwa moto, haiwezekanio...haiwezekani...” alisema Razak huku akionekana kuchanganyikiwa kwani miongoni mwa biashara zilizokuwa zikimuingizia kiasi kikubwa cha fedha, ilikuwa hiyo yadi ya magari.
*****
Razak aliendesha gari kwa kasi, alikuwa amechanganyikiwa, taarifa ile ya kuteketea kwa yadi yake ya magari ilimchanganya mno. Kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana hakukuwa na foleni barabarani hivyo hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika katika eneo hilo.

Kitu cha ajabu kabisa alichokiona, hakukuwa na dalili za moto wowote ule. Alibaki akishangaa, yadi yake ya magari ilikuwa salama kabisa, sasa kwa nini msimamizi wake wa yadi hiyo alimwambia kwamba yadi yake ya magari ilikuwa ikiteketea kwa moto?

Hakutaka kubaki garini, akateremka na kuelekea ndani ya yadi ile. Ukimya mkubwa ulikuwa umetawala mahali hapo, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

Hakukuwa na mlinzi wala hakuwepo Casmir kitu kilichomshangaza sana kwani haikuwa kawaida hata kidogo. Alichokifanya ni kuanza kuita lakini hakukuwa na mtu aliyeitikia.

Akaanza kuyahesabu agari yaliyokuwa mule ndani, hakukuwa na gari lolote lile lililopungua, yote yalikuwa kama alivyoyaacha, magari mia moja na hamsini.

Hakuridhika, hatua iliyofuata ni kwenda kwenye kibanda cha mlinzi, mlango ulikuwa umefungwa kwa nje na ufunguo kutolea, alichokifanya ni kuanza kuugongwa.

Hakusikia sauti za watu zaidi ya miguno ya watu wawili iliyomfanya kujua kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea humo ndani.

Harakaharaka akaanza harakati za kuuvunja ule mlango, wala hakukuwa na tatizo, mlango ukafunguka, alichokiona ni kwamba mlinzi na Casmir walikuwa wamefungwa kamba na kulazwa chini, akawafungua.
“Kuna nini?” aliwauliza.
“Kuna watu walikuja, wakatufunga kamba...”

“Ni majambazi?”
“Hatujui, ila walikuja na kutufunga kamba kisha kumwambia Casmir aongee nawe maneno waliyoyataka ayaongee huku wakikuita mahali hapa,” alisema mlinzi, wakati huo Casmir alikuwa kimya.
“Ni wakina nani?”

“Bosi...sijawahi kuwaona kabisa, ila walikuja na bunduki...” alisema Casmir.
Wote wakatoka ndani ya kijumba kile, kuhesabu magari haikutosha, walichokifanya ni kuanza kufungua gari moja baada ya jingine ili kuona kama kulikuwa na vifaa vimetolewa, kila gari lilikuwa salama kabisa.

“Labda kuna mtu alitaka kunisumbua tu...nyie endeleeni na kazi, tutazungumza kesho nikija,” alisema Casmir, akaingia ndani ya gari na kuondoka.

Mpaka kipindi hicho, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alibaki akiwashangaa majambazi hao ambao waliwateka watu wake na kisha kumwamuru Casmir kumpigia simu na kumwambia habari mbaya ambayo haikuwa na ukweli wowote ule.

Alibaki akitabasamu, alitoa kicheko kidogo na kuwaona watu hao kwamba walikuwa wajinga sana.

Hakuchukua muda mrefu akawa amefika nyumbani kwake, kitu kilichomshangaza sana, alianza kupiga honi lakini kitu cha ajabu, mlinzi hakutokea kufungua geti.

“Amelala au?” alijiuliza huku akiteremka.
Akalifuata geti kisha kulifungua, akaingia ndani na kuanza kuelekea katika kibanda cha mlinzi, kilichomshangaza, hakumkuta, hakujua alielekea wapi, hakutaka kujali sana, akalifungua geti, akalirudia gari lake, akaingia kisha kuliingiza.

Alipohakikisha amelipaki sehemu sahihi, hapohapo akateremka na kuelekea ndani. Huko ndipo alipogundua maana ya ile simu aliyokuwa amepigia, walipoingia ndani, kitu kilichomshtua, mpenzi wake Aisha hakuwepo.

Alichanganyikiwa, akaanza kumtafuta huku na kule, alihisi kwamba inawezekana alikwenda nje baada ya kuona ametoka usiku sana huku akiwa amechanganyikiwa, aliita kwenye kila chumba, hakuisikia sauti ya Aisha kitu kilichomfanya kuwafuata wasichana wa kazi.

“Aisha yupo wapi?” aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
“SI yupo ndani!”
“Ndani hayupo...hakuja huko kwenu?”
“Wala hakuja...”

Razak akatoka nje, akazunguka katika eneo zima la nyumba yake, alipofika katika bustani ya maua, akakutana na mlinzi akiwa hoi chini, amefungwa kamba huku damu zikimtoka kichwa.

“Kuna nini tena?”
“Tulivamiwa, nimepigwa na watu nisiowajua...” alijibu mlinzi...”
“Wakina nani?”
“Sijui ila walikuja na bastola....wakaingia ndani...”
“Kisha....”

“Sijui ila nilisikia wakilitaja jina la shemeji...” alijibu mlinzi yule.
Hapo ndipo Razak akachanganyikiwa zaidi, akatoka nje mbio na kuanza kukimbia katika barabara huku akiangalia huku na kule. Muda wote mikono yake ilikuwa kichwani, hakuamini kile kilichokuwa kimetokea.

Alizunguka sehemu kubwa ya Kijitonyama, alikwenda mpaka Tandale na Mwananyamala, kote huko aliambulia patupu hivyo akarudi na kuwapigia simu wazazi wake.

“Unasemaje?”
“Aisha ametekwa...”
“Na nani?”
“Hakuna anayejua....naomba mje...” alisema Razak.

Hakutulia, simu nyingine kupiga ilikuwa ni ya Kituo cha Polisi cha Mabatini, akawaeleza polisi kile kilichotokea, baada ya muda, polisi hao wakafika nyumbani kwake, kitu cha kwanza kabisa wakaanza kuzungumza na mlinzi.

“Walikuwa wangapi?”
“Kama wanne...”
“Kama wanne au wanne?”

“Nasema kama kwa sababu walikuja wawili, wengine nilisikia sauti zao kwa nyuma...”
“Ikawaje?”
“Wakanipiga, wakanifunga kamba na kuingia ndani..”

“Walikuwa na silaha gani?”
“Bastola ndogo...”
“Usoni walivaa vinyago?”
“Hapana...”
“Hukuwatambua?”
“Nilishindwa kuwatambua mkuu...” alijibu mlinzi huyo.

Wakati wote wa mahojiano, Razak alisimama pembeni, alionekana kuwa na hasira mno, alichanganyikiwa, mwili wake ulikuwa ukimtetemeka, alionekana kutokuamini kilichokuwa kimetokea.

Mtu wa kwanza kabisa aliyemfikiria alikuwa msichana Sabrina, alijua hali aliyokuwa nayo na msichana huyo, baada ya kumuomba kuachana naye, aliachana naye na hata msichana huyo aliporudi, tayari alikuwa na msichana mwingine hivyo kuhisi kwamba ili kulipa kisasi, msichana huyo aliamua kumteka Aisha.

“Huyu atakuwa Sabrina tu...haiwezekani, lazima nimtafute...” alisema Razak huku akionekana kuwa na hasira mno.
****

Je nini kitaendelea....
Sabrina.....at work
 
Sehemu ya 37

“Bosi...bosi...bosi...” ilisikika sauti kutoka upande wa simu ya Razak.
“Unasema Casmir...”
“Yadi inaungua...”

“Unasemaje?”
“Yadi ya magari inaungua bosi...inateketea kwa moto muda huu,” ilisikika sauti ya mfanyakazi huyo.
“Ipi?”

“Hii ya Kinondoni...wahi bosi, inateketea kwa moto...” aliendelea kusisitiza Casmir.
“Moto umean...” alitaka kuuliza swali lakini kabla hilo swali halijakamilika, simu ikakatwa na kubaki akiita tu lakini simu hiyo haikuwa hewani tena.

Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kuangalia saa yake, tayari ilikuwa ni saa saba usiku, harakaharaka akakurupuka kutoka kitandani, akawasha taa na harakaharaka kuvaa suruali yake kwa ajili ya kuondoka mahali hapo.
Wakati anajiandaa, Aisha akashtuka kutoka usingizini.

Akapigwa na mshangao, hakujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea mpaka mpenzi wake kuvaa nguo harakaharaka namna ile tayari kwa kuondoka mahali hapo.
“Kuna nini tena?” aliuliza Aisha.
“Yadi inateketea kwa moto...”

“Unasemaje?”
“Nakuja...”
Razak hakutaka kubaki mahali hapo, kwa haraka sana akachomoka chumbani na kuelekea nje, huko, akapanda ndani ya gari lake, mlinzi akafungua geti na kuondoka mahali hapo huku akiwa amechanganyikiwa.

“Yaani yadi inateketea kwa moto, haiwezekanio...haiwezekani...” alisema Razak huku akionekana kuchanganyikiwa kwani miongoni mwa biashara zilizokuwa zikimuingizia kiasi kikubwa cha fedha, ilikuwa hiyo yadi ya magari.

*****
Razak aliendesha gari kwa kasi, alikuwa amechanganyikiwa, taarifa ile ya kuteketea kwa yadi yake ya magari ilimchanganya mno.

Kwa kuwa ilikuwa ni usiku sana hakukuwa na foleni barabarani hivyo hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika katika eneo hilo.

Kitu cha ajabu kabisa alichokiona, hakukuwa na dalili za moto wowote ule. Alibaki akishangaa, yadi yake ya magari ilikuwa salama kabisa, sasa kwa nini msimamizi wake wa yadi hiyo alimwambia kwamba yadi yake ya magari ilikuwa ikiteketea kwa moto?

Hakutaka kubaki garini, akateremka na kuelekea ndani ya yadi ile. Ukimya mkubwa ulikuwa umetawala mahali hapo, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

Hakukuwa na mlinzi wala hakuwepo Casmir kitu kilichomshangaza sana kwani haikuwa kawaida hata kidogo. Alichokifanya ni kuanza kuita lakini hakukuwa na mtu aliyeitikia.

Akaanza kuyahesabu agari yaliyokuwa mule ndani, hakukuwa na gari lolote lile lililopungua, yote yalikuwa kama alivyoyaacha, magari mia moja na hamsini. Hakuridhika, hatua iliyofuata ni kwenda kwenye kibanda cha mlinzi, mlango ulikuwa umefungwa kwa nje na ufunguo kutolea, alichokifanya ni kuanza kuugongwa.

Hakusikia sauti za watu zaidi ya miguno ya watu wawili iliyomfanya kujua kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea humo ndani. Harakaharaka akaanza harakati za kuuvunja ule mlango, wala hakukuwa na tatizo, mlango ukafunguka, alichokiona ni kwamba mlinzi na Casmir walikuwa wamefungwa kamba na kulazwa chini, akawafungua.
“Kuna nini?” aliwauliza.

“Kuna watu walikuja, wakatufunga kamba...”
“Ni majambazi?”
“Hatujui, ila walikuja na kutufunga kamba kisha kumwambia Casmir aongee nawe maneno waliyoyataka ayaongee huku wakikuita mahali hapa,” alisema mlinzi, wakati huo Casmir alikuwa kimya.

“Ni wakina nani?”
“Bosi...sijawahi kuwaona kabisa, ila walikuja na bunduki...” alisema Casmir.

Wote wakatoka ndani ya kijumba kile, kuhesabu magari haikutosha, walichokifanya ni kuanza kufungua gari moja baada ya jingine ili kuona kama kulikuwa na vifaa vimetolewa, kila gari lilikuwa salama kabisa.

“Labda kuna mtu alitaka kunisumbua tu...nyie endeleeni na kazi, tutazungumza kesho nikija,” alisema Casmir, akaingia ndani ya gari na kuondoka.

Mpaka kipindi hicho, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alibaki akiwashangaa majambazi hao ambao waliwateka watu wake na kisha kumwamuru Casmir kumpigia simu na kumwambia habari mbaya ambayo haikuwa na ukweli wowote ule.

Alibaki akitabasamu, alitoa kicheko kidogo na kuwaona watu hao kwamba walikuwa wajinga sana.

Hakuchukua muda mrefu akawa amefika nyumbani kwake, kitu kilichomshangaza sana, alianza kupiga honi lakini kitu cha ajabu, mlinzi hakutokea kufungua geti.

“Amelala au?” alijiuliza huku akiteremka.
Akalifuata geti kisha kulifungua, akaingia ndani na kuanza kuelekea katika kibanda cha mlinzi, kilichomshangaza, hakumkuta, hakujua alielekea wapi, hakutaka kujali sana, akalifungua geti, akalirudia gari lake, akaingia kisha kuliingiza.

Alipohakikisha amelipaki sehemu sahihi, hapohapo akateremka na kuelekea ndani. Huko ndipo alipogundua maana ya ile simu aliyokuwa amepigia, walipoingia ndani, kitu kilichomshtua, mpenzi wake Aisha hakuwepo.

Alichanganyikiwa, akaanza kumtafuta huku na kule, alihisi kwamba inawezekana alikwenda nje baada ya kuona ametoka usiku sana huku akiwa amechanganyikiwa, aliita kwenye kila chumba, hakuisikia sauti ya Aisha kitu kilichomfanya kuwafuata wasichana wa kazi.

“Aisha yupo wapi?” aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.
“SI yupo ndani!”
“Ndani hayupo...hakuja huko kwenu?”
“Wala hakuja...”

Razak akatoka nje, akazunguka katika eneo zima la nyumba yake, alipofika katika bustani ya maua, akakutana na mlinzi akiwa hoi chini, amefungwa kamba huku damu zikimtoka kichwa.
“Kuna nini tena?”
“Tulivamiwa, nimepigwa na watu nisiowajua...” alijibu mlinzi...”

“Wakina nani?”
“Sijui ila walikuja na bastola....wakaingia ndani...”
“Kisha....”
“Sijui ila nilisikia wakilitaja jina la shemeji...” alijibu mlinzi yule.

Hapo ndipo Razak akachanganyikiwa zaidi, akatoka nje mbio na kuanza kukimbia katika barabara huku akiangalia huku na kule. Muda wote mikono yake ilikuwa kichwani, hakuamini kile kilichokuwa kimetokea.

Alizunguka sehemu kubwa ya Kijitonyama, alikwenda mpaka Tandale na Mwananyamala, kote huko aliambulia patupu hivyo akarudi na kuwapigia simu wazazi wake.

“Unasemaje?”
“Aisha ametekwa...”
“Na nani?”
“Hakuna anayejua....naomba mje...” alisema Razak.

Hakutulia, simu nyingine kupiga ilikuwa ni ya Kituo cha Polisi cha Mabatini, akawaeleza polisi kile kilichotokea, baada ya muda, polisi hao wakafika nyumbani kwake, kitu cha kwanza kabisa wakaanza kuzungumza na mlinzi.

“Walikuwa wangapi?”
“Kama wanne...”
“Kama wanne au wanne?”

“Nasema kama kwa sababu walikuja wawili, wengine nilisikia sauti zao kwa nyuma...”
“Ikawaje?”
“Wakanipiga, wakanifunga kamba na kuingia ndani..”

“Walikuwa na silaha gani?”
“Bastola ndogo...”
“Usoni walivaa vinyago?”
“Hapana...”
“Hukuwatambua?”
“Nilishindwa kuwatambua mkuu...” alijibu mlinzi huyo.

Wakati wote wa mahojiano, Razak alisimama pembeni, alionekana kuwa na hasira mno, alichanganyikiwa, mwili wake ulikuwa ukimtetemeka, alionekana kutokuamini kilichokuwa kimetokea.

Mtu wa kwanza kabisa aliyemfikiria alikuwa msichana Sabrina, alijua hali aliyokuwa nayo na msichana huyo, baada ya kumuomba kuachana naye, aliachana naye na hata msichana huyo aliporudi, tayari alikuwa na msichana mwingine hivyo kuhisi kwamba ili kulipa kisasi, msichana huyo aliamua kumteka Aisha.

“Huyu atakuwa Sabrina tu...haiwezekani, lazima nimtafute...” alisema Razak huku akionekana kuwa na hasira mno.
****

Je nini kitaendelea...
 
Sehemu ya 38

Razak hakutaka kubaki mahali hapo, tayari kichwa chake kilimwambia kwamba mtu aliyehusika katika utekaji wa mchumba wake hakuwa mtu mwingine zaidi ya Sabrina.

Alikumbuka namna msichana huyo alivyokuwa akimtaka kipindi cha wiki moja iliyopita, alijua fika kwamba aliumia na ndiyo maana katika kipindi hicho alitaka kulipiza kisasi kwa kumfanyia jambo baya mpenzi wake.

Moyo wake ulimuuma mno kwani Aisha hakuwa kwenye hali nzuri, alikuwa mgonjwa ambaye muda wote alihitaji uangalizi wa hali ya juu.

Hakutaka kukumbuka mambo mengine, akaingia ndani ya gari na kuanza kuelekea nyumbani kwa kina Sabrina huku akiwa na hasira mno.
“Anakwenda wapi?” aliuliza polisi mmoja huku akionekana kumshangaa Razak.

“Hata mimi sijui...kwanza kwa nini aondoke na wakati sisi tupo hapa?” aliuliza polisi mwingine lakini hakukuwa na aliyekuwa na jibu zaidi ya kumchukua mlinzi, wafanyakazi wa ndani na kuondoka nao.

Njiani, kila wakati Razak alionekana kuwa na hasira, hakuamini kama msichana Sabrina aliweza kumfanyia upuuzi kama ule alioufanya.

Alimchukia kipindi cha nyuma mara baada ya kufanyiwa mabaya lakini katika kipindi hicho, ile chuki aliyokuwa nayo ilikuwa maradufu.
“Nitamuua huyu malaya...hanijui, nitamuua tu, ngoja tu,” alisema Razak huku akiendesha gari kuelekea nyumbani kwa kina Sabrina.

Hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika nyumbani kwa kina Sabrina. Harakaharaka akateremka kutoka ndani ya gari na moja kwa moja kulifuata geti la kuingilia ndani ya jumba hilo. Akagonga kifujofujo na mlinzi kusikika ndani.

“Nani wewe?” aliuliza mlinzi huyo.
“Razak...fungua mlango Mrisho...” alisema Razak.
“Mbona usikuusiku?”
“Fungua mlango kwanza...” alisema Razak kwa sauti ya juu, kwa kumsikiliza tu, sauti yake ilitoka na hasira kali.

Kwa kuwa alikuwa akimfahamu vilivyo, mlinzi Mrisho hakutaka kubisha, akaufungua mlango ambapo moja kwa moja Razak akapita na kuufuata mlango wa kuingilia sebuleni. Bahati nzuri kwake ni kwamba kabla ya kuufikia mlango huo, tayari wazazi wa Sabrina wakatoka nje kwani walisikia sauti yake tangu akigonga geti kifujofujo.

“Kuna nini?” aliuliza baba yake Sabrina mara baada ya macho yake kukutana na ya Razak.

“Sabrina yupo wapi?” aliuliza Razak.
“Kuna nini kwanza? Mbona unaulizia kwa hasira hivyo?” aliuliza mama yake Sabrina.

“Ninataka kumuona Sabrina...” alisema Razak kwa sauti kubwa.

“Hebu ingia kwanza...”
Wakamchukua Razak na kuingia ndani. Japokuwa alikuwa na hasira mno lakini kutokana na heshima kubwa aliyowapa wazazi hao, akaamua kuishusha hasira yake na kubaki akiongea nao kama kawaida.

Kitu kilichompeleka pale kilikuwa ni kuonana na Sabrina tu ila kwa sababu watu wa kwanza kuonana nao walikuwa wazazi wa msichana huyo, hakuwa na budi kuanza kuwahadithia kile kilichotokea.
Muda wote aliokuwa akihadithia, macho yake yalionyesha maumivu makali yaliyokuwa moyoni mwake. Wazazi wa Sabrina waliligundua hilo na kilichobaki kilikuwa ni kumpoza tu.

“Kwa hiyo ikawa hivyo? Aisha akatekwa?” aliuliza baba yake Sabrina.
“Ndiyo! Kwa nini Sabrina amenifanyia hivi?”

“Sabrina! Haiwezekani, mbona hayupo tangu wiki iliyopita?” aliuliza baba yake.
“Hayupo? Alikwenda wapi?”
“Marekani kwa shangazi yake. Sasa unaposema kwamba alihusika, tunashangaa...” alisema baba yake Sabrina.

Razak hakutaka kuamini alichokisikia, aliendelea kubisha kwamba mtu aliyesababisha hayo yote alikuwa msichana Sabrina. Walichokifanya wazazi hao ni kumpigia simu shangazi yake Sabrina aliyekuwa Marekani na kisha kuzungumza na Sabrina.

“Nilifika salama, kesho nitaelekea Chicago kwa anti Zainabu...” alisikika Sabrina kwenye simu.

Razak akashusha pumzi, alionekana kuchoka mno, hakuamini kile alichokisikia, hisia zake kwamba Sabrina ndiye aliyehusika katika utekaji ule zikaanza kupotea kichwani mwake na kilichofuatia ni kuwaomba msamaha wazazi wa msichana huyo.

Hakutaka kukaa sana mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka kurudi kwake. Mawazo hayakumuisha, alikosa furaha, amani ikatoweka moyoni mwake. Alipofika nyumbani, watu wa kwanza kukutana nao walikuwa wazazi wao.

Razak akaanza kupiga hatua kuwafuata, alipowafikia, akawakumbatia na kuanza kulia kama mtoto.

“Nyamaza Razak....Aisha atapatikana tu...” alisema baba yake huku akimpigapiga mgongoni.

Walichokifanya ni kuanza kuelekea kituo cha polisi ambapo huko waliwashikilia mlinzi na dada wa kazi. Walipofika huko, kitu cha kwanza wakataka kuonana nao ili kujua kama walikuwa salama.

“Mmefikia wapi?” Razak aliwauliza polisi.
“Bado...ndo tumeanza kuwahoji hawa watu ili tujue wapi pa kuanzia...” alijibu polisi mmoja.

“Na inaweza kuchukua muda gani?”
“Msijali...kila kitu kitakuwa salama...mbali na hivyo, tumewasiliana na polisi wengine ili kusaidia katika hili...wala msiwe na hofu, atapatikana tu...” alisema polisi huyo.

Waliambiwa kwamba hawakutakiwa na wasiwasi hivyo wakaambiwa waende nyumbani. Kurudi peke yao lilikuwa jambo lisilowezekana, ilikuwa ni lazima kurudi na watu wao, yaani mlinzi na dada wa kazi hivyo wakawachukua na kuondoka nao.

Walipofika nyumbani, tayari ilikuwa ni saa tisa alfajiri, Razak hakulala, alikuwa nje ya nyumba yao akiangalia huku na kule, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali na muda wote alimwambia Mungu amuonyeshee watu waliomteka mchumba wake ili afanye jambo baya.

Mpaka inafika saa kumi na moja, bado hawakupata taarifa zozote zile kutoka kwa watu wowote kama mepenzi wake, Aisha alikuwa ameonekana mahali fulani.

Ilipofika saa mbili asubuhi, hakutaka kubaki nyumbani, akaondoka kuelekea katika kituo cha polisi kwa ajili ya kujua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea huko. Alipofika, akakaribishwa.

“Karibu sana Razak...” alikaribishwa na polisi ambaye alimwambia kwamba anahitajika na mkuu wa kituo, hivyo akaingia kwenye ofisi hiyo.

Huko, akaanza kuzungumza naye kwa kina juu ya kile kilichokuwa kimetokea, baada ya kumwambia mambo mengi, mwisho kabisa akamwambia taarifa ambayo aliamini kwamba ingemuweka kwenye presha kubwa kwamba kulikuwa na maiti ya mwanamke iliokotwa imetupwa katika mtaro mmoja huko maeneo ya Mbezi kwa Luis.

“Unasemaje?” aliuliza Razak huku akionekana kushtuka.

“Kuna maiti imeokotwa. Ni ya mwanamke, hatujui kama ndiye huyo Aisha au la! Ila imeokotwa na polisi wetu wamekwenda kuiona ili kujua kama ndiye yeye au mtu mwingine...” alisema mkuu yule wa kituo, maneno hayo yalitosha kabisa kumfanya Razak kukiinamisha kichwa chake, kijasho chembamba kumtoka na mwili wake kumtetemeka.

“Mungu wangu...wamemuua Aisha wangu!” alijikuta akiyatamka maneno hayo kwa sauti ambayo ilisikika kabisa masikioni mwa mkuu huyo wa kituo.
****
Polisi wa Kituo cha Polisi cha Mabatini walipigiwa simu na kuambiwa kwamba kulikuwa na mwanamke alikuwa ameuawa na mwili wake kutupwa katika mtaro wa maji machafu huko Mbezi kwa Luis.

Walipopata taarifa hiyo, hawakutaka kufuatilia suala hilo kwani kwa sababu tukio lilitokea huko Mbezi kwa Luis basi polisi ambao wangehusika moja kwa moja walitakiwa kuwa wa hukohuko Mbezi.

Walichokifanya ni kupiga simu ya kituo hicho lakini matokeo waliyoyapata ni kwamba simu iliita na kuita lakini haikuwa ikipokelewa. Hawakutaka kubaki kituoni hapo, walichokifanya, tena kwa haraka sana ni kupanda ndani ya gari lao na safari ya kuelekea Mbezi kuanza.

Mioyo yao iliwaambia kwamba mwanamke huyo aliyekuwa ameuawa alikuwa yule msichana ambaye waliambiwa usiku wa kuamkia siku hiyo kwamba alitekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kusipojulikana.

Kitendo cha kuambiwa kwamba mwanamke huyo alikuwa ameuawa, walishtuka, wakakosa nguvu na kitu pekee walichokuwa wakipanga kukifanya ni kumpa taarifa Razak ambaye hawakujua angeipokeaje taarifa hiyo.
“Hapa ninamfikiria yule bwana...” alisema polisi mmoja, alikuwa akiwaambia wenzake.

“Yule mtoto wa tajiri?”
“Ndiye huyohuyo...kama huyu mtu akiwa ndiye yule aliyetekwa, kitanuka sana, sijui nani atamzuia manake anaonekana mtata sana,” alisema polisi huyo.

Waliendelea kuzungumza mambo mawili-matatu mpaka wakafika huko Mbezi. Wakateremka kutoka ndani ya gari na kuanza kuelekea huko walipoambiwa kwamba kulikuwa na maiti ya mwanamke mmoja.

Kwa kuwa walielekezwa vizuri, hawakupata tabu sana wakawa wamefika huko ambapo kitu cha kwanza kabisa walichokiona kilikuwa ni idadi kubwa ya watu walioonekana kuzunguka kitu kwenye mtaro.

Wakapiga hatua kusogea mahali pale, walipofika, wakawatawanyisha watu na wao kuingia katikati, macho yao yakatua katika mwili wa mwanamke mmoja ambaye uso wake ulikuwa umeelekea katika maji ya mtaro.

“Ni lazima tuutoe...” alisema polisi mmoja ambaye alirudi garini na kuchukua vifaa vikiwemo glavu.

Vifaa vilipoletwa hawakutaka kuchelewa, hapohapo wakaanza kuutoa mwili ule, kila mtu aliyekuwa katika eneo lile akaziba pua yake kwani kutokana na mwili ule kulowanishwa na maji machafu ya kwenye mtaroi ule, uliufanya kunuka hasa.

Hawakutaka kusubiri zaidi ya kuondoka huku wakiongozana na kijana aliyepiga simu na kuwapa taarifa.

Ndani ya gari wakabaki wakiuangalia mwili huo, maswali kibao yakajazana vichwani mwao kwamba ule mwili waliokuwa wameubeba ulikuwa ni wa mwanamke aliyekuwa ametekwa usiku wa kuamkia siku hiyo au ulikuwa mwili wa mtu mwingine.

Hawakuwa na majibu, hawakutaka kusimama, waliendelea na safari yao mpaka walipofika katika Hospitali ya Palestina ambapo mwili ule ukateremshwa na kuingizwa ndani ya chumba kilichoandikwa ‘Mochwari’ mlangoni.

“Hebu mpigieni simu bosi, mwambieni kwamba tumeuleta hapa,” alisema polisi mmoja na mwingine kuchukua simu na kupiga kituoni kwa kamanda wao.
****

Je nini kitaendelea....
 
Shukrani kwa mtunzi mkuu aliyeitunga mm mletaji tu nimeileta
hahahaa big up shunie ake,kuna waletaji wengine full kutuna mibichwa mara cjui ooh msiponipa like nakosa mzuka,ukose mzuka kutuma je alotunga?
 
Asante sana shunie. Imeishia patamu naomba tupe na kamoja kengine
 
Sehemu ya 39

Bado Razak alikuwa na mawazo tele, taarifa aliyokuwa amepewa kwamba kulikuwa na mwili wa mwanamke ulikutwa maeneo ya Mbezi kwa Luis ukiwa umetupwa katika mtaro wa maji machafu zilimshtua.

Muda wote alikuwa amekiinamisha kichwa chake chini, machozi yalikuwa yakimtoka huku moyo wake ukimuuma mno kwa kuamini kwamba mtu aliyekuwa ameuawa alikuwa mpenzi wake, Aisha.

Kamanda mkuu wa kituo hicho cha polisi ndiye aliyekuwa na kazi kubwa ya kumbeleza na kumtaka anyamaze kwani kulia kwake isingekuwa suluhisho kwa kile kilichotokea.

“Wamemuua Aisha wangu....kwa nini?” aliuliza Razak huku akionekana kuchanganyikiwa.

“Usilie Razak....usiweke akilini kwamba aliyeuawa ni mpenzi wako, inawezekana ni mtu mwingine,” alisema kamanda Pwagu huku akimpigapiga Razak mgongoni.

“Najua huyu atakuwa Aisha tu, najua hivyo...ni lazima nitawatafuta hao wauaji...” alisema Razak huku akionekana kuwa na hasira hasa.

Huku wakiwa humo ofisini, mara simu ya kamanda Pwagu ikaanza kuita, hakutaka kupoteza muda, hapohapo akaichukua na kuipeleka sikioni kwani alijua fika kwamba simu hiyo ilitoka kwa wale vijana wake waliokwenda Mbezi.

“Imekuwaje?” aliuliza.
“Tulifika salama na tuliukuta huo mwili na kuuchukua...” ilisikika sauti kutoka upande wa pili.

“Mpo wapi sasa hivi?”
“Tupo hapa Palestina mkuu...”
“Na huo mwili?”
“Ndiyo! Tupo nao hapa...”

Hakutaka kuzungumza sana, alichokifanya ni kumwambia Razak kwamba huo mwili ulikuwa umepatikana na ulikuwa katika Hospitali ya Palestina hivyo walitakiwa kwenda kuuona ili kujua kama ulikuwa mwili wa Aisha au la.

Ndani ya gari, Razak hakutaka kuzungumza kitu chochote kile, alikuwa akilia kwa maumivu makali.

Moyo wake ukagawanyika huku ule uliokuwa ukimwambia kwamba mwili huo ulikuwa wa Aisha ulipata nafasi kubwa zaidi.
“Nitamtafuta muuaji tu...” alisema Razak.

Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika hospitali hiyo. Harakaharaka wakateremka na kuanza kuelekea katika hospitali ya dokta mkuu ambapo baada ya kufika huko wakamwambia kile kilichowaleta.
“Hakuna tatizo...twendeni...” alisema daktari huyo.

Wakaelekea mpaka kule mochwari, mlango ukafunguliwa na wote kwa pamoja kuingia ndani. Humo, kulikuwa na baridi kali, harufu kali ya madawa ilikuwa ikisikika puani mwao huku kukiwa na masanduku mengi yaliyokuwa na maiti.

Wakaanza kupiga hatua mpaka katika friji lililokuwa na maiti ya mwanamke yule huku wakiongozwa na mtu alikuwa akifanya kazi humo kwenye hicho chumba.
“Maiti ile kutoka Mbezi ipo wapi?” aliuliza dokta.

“Ipo humu...” alisema kijana huyo huku akivuta kabati la chuma lililomhifadhi mwanamke yule, baada ya kuhakikisha kwamba limetoka na kufunguliwa, Razak akaupitisha uso wake na kuangalia mwili wa mwanamke huyo, alichokiona, hakuamini macho yake.
*****
Kabla ya kuuona mwili ule, Razak alikuwa akitetemeka mno kwa kuhisi kwamba maiti iliyokuwa katika sanduku ile ambayo ililetwa ndani ya mochwari dakika chache zilizopita ilikuwa ni ya mpenzi wake.

Alipofunguliwa kabati lile la chuma na kuangalia ndani, alibaki akitetemeka, hofu ikamjaa kwani mwanamke mwili wa mwanamke huyo ulifanana sana na mpenzi wake, Sabrina kitu kilichoyafanya mapigo yake ya moyo kudunda kwa nguvu.

“Ndiye yeye?” aliuliza kamanda Pwagu.
“Hebu subiri...ni kama yeye, ni kama si yeye...” alisema Rabak huku akiuangalia mwili wa mwanamke yule kwa umakini kabisa.

Mwili ule haukuwa umesafishwa, ulikuwa na damu nyingi na kuonekana mchafu kitu kilichomfanya Rabak kuwa kwenye sintofahamu kama mwili ule ulikuwa ni wa mpenzi wake au mtu mwingine.

Mpaka anajiridhisha kwamba mwili ule haukuwa mwili wa mpenzi wake, zilipita dakika arobaini na tano, tena baada ya kusafishwa. Akashusha pumzi, akanyanyua mikono yake juu kama ishara ya kumshukuru Mungu, walipohakikisha kila kitu kimekamilika, wakaondoka na kurudi kituoni.

Kila mtu kituoni hapo alikuwa bize, simu zilikuwa zikitumika kwenda huku na kule kuulizia kama msichana Aisha alipatikana au la. Bado mambo yalikuwa magumu, kwa kila simu iliyopigwa kituoni, majibu yalikuwa ni kwamba hawakufanikiwa kupata chochote kile.

“Kwa hiyo hajapatikana?”
“Ndiyo! Yaani sijui hawa watu wamemuweka wapi,” ilisikika sauti kutoka upande wa pili.

Kwa sababu kamanda Pwagu alikuwa na uzoefu na kazi yake, kitu cha kwanza kabisa ni kumuuliza Razak kama alikuwa na adui yeyote yule. Razak akamjibu kwamba hakuwa na adui yeyote zaidi ya msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Sabrina.

Hapo ndipo akaanza kuhadithia mwanzo mpaka alipoonana na wazazi wa msichana huyo na kumwambia kwamba wakati tukio linatokea, tayari wiki moja nyuma msichana huyo alikwenda nchini Marekani.

“Na una uhakika hauna adui mwingine yeyote?” aliuliza kamanda Pwagu.
“Ndiyo mkuu...sina zaidi ya huyo malaya!’

“Bado unatuweka katika wakati mgumu sana, na unaposema kwamba hauna adui zaidi ya huyo mwanamke, unatuchanganya sana...”
“Ndiyo hivyo mkuu...wakati tukio linatokea, yeye alikuwa nchini Marekani..” alisema Razak.

Alichomwambia ni kwamba alitakiwa kuondoka kurudi nyumbani na huku nyuma, yeye na polisi wengine wangehakikisha kwamba mipango inasukwa na kusukika ili hata kama kama itachukua muda gani basi msichana huyo apatikane tena akiwa hai kabisa.

Razak hakutaka kuridhika, kila alipoyaangalia macho ya kamanda Pwagu hakuamini kama kweli mpenzi wake angeweza kupatikana kwa urahisi, tena akiwa hai kama alivyoahidiwa ila kwa sababu mtu aliyeongea alikuwa polisi, hakutaka kuwa na wasiwasi, hivyo akakubaliana naye na kurudi zake, ila pamoja na yote, bado moyo wake ulikuwa na hofu kubwa.

****
“Jamani jamani, hebu nisikilizeni kwa makini...” ilisikika sauti kutoka kwa mwanaume mmoja aliyeitwa Ali, mbele yake kulikuwa na watu wanne ambao alitaka wafanye kazi iliyokuwa mbele yake.

“Tunakusikiliza mkuu...”
“Huyu msichana ni lazima atekwe haraka iwezekanavyo...”

“Ndiyo mkuu!”
“Edwin, nataka ucheze mchezo ambao hatujawahi kuucheza hata siku moja...unamjua huyu Razak?” aliuliza Ali kwa sauti ya utetemeshi.

“Siyo sana, ila details zinasema ni mtoto wa kibopa...”
“Sawasawa...kama baba yake ni kibopa, basi jua kwamba hata yeye ni kibopa, tunachokitaka ni kumteka mpenzi wake katika staili ambayo hakuna mjinga yeyote ataweza kuifikiria...” alisema Ali.
Mipango ilikuwa ikisukwa na watu watano ndani ya jumba kubwa na la kifahari.

Watu hao walikuwa baadhi wa wahuni waliokuwa wakiunda kundi la kihuni liitwalo Gangstar-13 ambalo lilitumika sana katika utekaji ndani ya Jiji la Dar es salaam.

Walitumia saa moja kupanga namna ambavyo utekaji ulitakiwa kufanyika, baada ya hapo, safari ya kuelekea huko ikaanza huku wakiwepo vijana wanne tu ambapo kwanza walitakiwa kwenda kwenye yadi ya magari ya huyo Razak, kumteka mlinzi na yeyote aliyekuwemo humo na kumlazimisha amwambie Razak kwamba yadi yake ilikuwa ikiteketea.

Kilichopangwa ndicho klichotokea, wakati Razak anakwenda katika yadi yake ya magari, tayari wanaume hao walipishana naye njiani na kuelekea nyumbani kwake.
Walipofika, kitu cha kwanza wakamteka mlinzi, wakampiga na kisha kumfunga kamba na kumuweka katika bustani ya maua na wao kuingia ndani.

Walikwishapewa taarifa kwamba msichana waliyetakiwa kumteka alikuwa mgonjwa, maisha yake yalikuwa kwenye kiti cha mataili hivyo waliamini kwamba wasingeweza kupata tatizo lolote lile.
“Chumba chake mnakijua?” aliuliza jamaa mmoja.
“Hatujui, ila inatupasa tutafute kile kona...”

Ilionekana kuwa jambo gumu kujua chumba cha Razak lakini bahati ikaonekana kuwa upande wao kwani mlango wa kwanza kabisa kuufungua ndiyo ulikuwa wa chumba alichokuwa akilala Razak.

“Nyie wakina nani?” aliuliza Aisha aliyekuwa kitandani, sauti yake tu ilionyesha kwamba alikuwa na hofu kubwa.

“Tulia hivyohivyo..ukipiga kelele tu, umekufa...” alisema mwanaume mmoja.
Aisha aliogopa, mapigo yake ya moyo yakawa juu, hakuamini kile kilichokuwa kikitokea kwamba leo hii naye aliingiliwa na watu na kisha kutekwa. Aliogopa hata kupiga kelele kutokana na onyo alilopewa kwamba endapo angepiga kelele tu basi angeuawa.

“Shuka kitandani...tunajua kwamba wewe ni mgonjwa, usijali, tutakulinda kama madaktari..” alisema mwanaume mwingine.

Wakamshusha Aisha kutoka kitandani, wakamuweka katika kiti chake cha mataili na kutoka naye mule ndani, wakaelekea nje ambapo wakamuingiza ndani ya gari, wakakikunja kiti chake, nacho wakakiingiza na kisha kuondoka zao.

Safari yao hiyo iliishia ndani ya jumba kubwa la kifahari, Aisha akashushwa na kukalishwa kwenye kiti chake ambacho kilianza kusukumwa mpaka ndani ya jumba hilo na kuambiwa asubiri sebuleni.

Aisha akabaki ndani ya jumba hilo, alichanganyikiwa, hofu ilimjaa moyoni mwake kiasi kwamba kila wakati alikuwa akitetemeka tu. Hakukuwa na kipindi ambacho alikuwa kwenye wakati mgumu kama kipindi hicho.

Alibaki akiangalia mazingira ya sebuleni pale, alikuwa na wasiwasi kwamba siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kwake kuvuta pumzi ya dunia hii.

Alibaki ametulia mpaka aliposikia mlango ukifunguliwa kutoka huko ndani, akajiweka kitini vizuri, baada ya sekunde kadhaa, mtu mmoja akatokea sebuleni hapo, macho yake yalipotua kwa mtu huyo, akashtuka, mapigo ya moyo yakaanza kudunda kwa kasi, aliyafikicha macho yake vizuri na kumwangalia mtu huyo, hakuamini kama alikuwa yeye au alimfananisha.

Mtu huyo hakuzungumza kitu, uso wake ulikuwa na tabasamu pana, alichokifanya ni kumsogelea Aisha na kumpa kikaratasi kilichosomeka ‘Umebakiza miezi miwili ya kuishi’. Aisha akashtuka. Hakuelewa maneno hayo yalimaanisha nini na kwa nini mtu huyo alimwambia hivyo.
****

Je nini kitaendelea....
 
Daah ni hatari sana...

Bado nina wasi wasi na Sabrina yupo nyuma na issue nzima ya kutwekwa Aisha...

Cc: mahondaw
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom