Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,976
- Thread starter
- #181
Sehemu ya 46
Huko akamkuta Aisha akiwa kitandani. Alikuwa akilia kama mtoto. Machozi yalikuwa yakimbubujika mashavuni mwake, alionekana kama mtu mwenye maumivu makali mno.
Razak akaanza kumsogelea, alipomfikia, akamshika bega kwa nyumba na kumkumbatia kwa nyua. Aisha hakunyamaza, ndiyo kwanza kilio chake kikaongezeka.
“Naomba unisamehe mpenzi....” alisema Razak kwa sauti ndogo karibu kabisa na sikio la Aisha.
“Naomba uniache Razak, naomba uniache....”
“Hapana! Nimekosa mpenzi, nakiri hilo ila huu si muda wa kukaa na kukasirika, utakasirika mpaka muda gani? Utalia mpaka muda gani? Nimekosa, ninakiri, ninahitaji msamaha wako,” alisema Razak huku akimbembeleza Aisha.
“Nina muda gani mpaka nife?” aliuliza Aisha, Razak akabaki kimya.
“Nimekuuliza wewe...”
“Nisikilize Aisha...”
“Kwanza niambie....”
“Aisha....”
“Utaniambia au huniambii?”
“Aisha...ninaumia....”
“Najua unaumia, niambie nimebakiza muda gani kufa?”
“Miezi miwili...”
“Kwa nini hukuniambia kabla?”
“Kwa sababu sikutaka kukuona unalia, unajua ni kiasi gani ninakupenda. Moyoni niliumia sana lakini sikuwa na jinsi, nilitakiwa kukubaliana na hali halisi iliyokuwepo.
“Aisha, siku ambayo ulilalamika maumivu makali ya tumbo, nilikupeleka hospitali, nadhani unakumbuka....” alisema Razak.
“Ikawaje?”
“Tulipofika huko, wakaniambia kwamba una kansa ya utumbo mkubwa,” alijibu Razak.
“Halafu.....”
“Wakaniambia kwamba utakufa kwani ni terminal cancer...”
“Ndiyo nini hiyo?”
“Kansa ambayo ni lazima ufe...” alisema Razak, Aisha akaanza kulia.
“Aisha...niliumia sana moyoni lakini sikuwa na jinsi, nilitamani kukuona unapona, nikatoka hapa na kukupeleka India kwa kudhani kwamba majibu yangebadilika, kilichonisikitisha, yaliendelea kubaki hivyohivyo kwamba ni lazima ufe...Aisha, ninakupenda, sitaki nikuache, ninataka niendelee kuwa nawe mpaka siku ya mwisho ya uhai wangu...” alisema Razak.
Maneno hayo yaliuchoma moyo wa Aisha, akashindwa kuelewa ni kitu gani alitakiwa kufanya. Alikumbuka kwamba alipelekwa India na mpenzi wake, kote huko ilikuwa ni kumtafutia tiba, apone na kuwa mzima kabisa.
Huo haukuwa mwisho wa uhusiano wao, Aisha akamsamehe Razak na kumkumbatia kwani maneno aliyoyasema yalimchoma sana na hata kama angelia na kukasirika, bado ukweli ungebaki palepale kwamba ni lazima afe.
“Ninakupenda Aisha...nina mapenzi yasiyokwisha moyoni mwangu, haijalishi utaishi kwa kipindi gani, NI LAZIMA NIKUOE...” alisema Razak huku akimwangalia msichana wake usoni.
“Kweli?”
“Ndiyo! Ni lazima nikuoe....”
Huo ndiyo ulikuwa msimamo wake, mchumba wake alikuwa kwenye hali mbaya lakini hakutaka kumuacha, alimwambia wazi kwamba alitaka kumuoa hivyo akahakikisha kwamba mipango ya harusi iliyokuwa ikifanyia iendelee zaidi japokuwa muda mwingi wote wawili walionekana kutokuwa na furaha.
Baada ya kukatika mwezi mmoja, hapo ndipo sherehe ya harusi kubwa ikaanza kufanyika na Aisha kuolewa na Razak, harusi ambayo ilihudhuriwa na watoto wengi wa mitaani ambao walikula na kunywa mpaka kusaza.
“Mbona hauna furaha Razak, umekuwa mume wa Aisha...” alisema rafiki yake Rajabu.
“Nina furaha Rajabu...”
“Hapana bwana, huwa haupo hivyo, hebu changamka kidogo...” alisema Rajabu huku akimtingishatingisha Razak.
Alitamani kuwa na furaha lakini hilo halikuwezekana hata kidogo, mke wake aliyekuwa akimpenda alibakiza mwezi mmoja tu wa kuishi. Huo ndiyo ulikuwa muda wa kumfariji, ndiyo ulikuwa muda wa kumuonyeshea ni jinsi gani alikuwa akimpenda.
Kipindi hicho Razak hakutaka kufanya kitu chochote kile, aliamua kuachana na biashara zake na kuanza kuwa karibu zaidi na mkewe. Kila siku alijitahidi kumfurahisha kwani alijua kwamba yeye ndiye alikuwa furaha yake bila kufanya hivyo, Aisha angeteseka sana nafsini mwake.
Mara nyingi alimchukua na kumpeleka katika mitoko mbalimbali hasa katika fukwe za baharini na hata kwenye hoteli kubwa. Alitaka afurahie maisha yake ya mwisho na msichana huyo.
Walipokuwa wakirudi nyumbani, walijifungia ndani, hawakutoka nje, huko walizungumza mengi huku Razak akimwambia Aisha ni jinsi gani alikuwa akimpenda kwa moyo wa dhati kwamba hata kama alikuwa kwenye kiti cha walemavu, kukaribia kufa lakini bado alimuoa.
“Nitakupenda mpaka kifo changu...” alisema Razak kwa sauti ya chini, kwa kumsikiliza tu alionekana kukata tamaa.
“Nitakupenda pia, hakika umekuwa mtu muhimu sana katika maisha yangu, japokuwa tumekaa kwa kipindi kifupi lakini umenionyeshea jinsi mapenzi yalivyo, sikudhani kama kuna mtu anaweza kupenda kama unavyonipenda...”
alisema Aisha huku machozi yakimbubujika kwa maumivu makali.
“Ugonjwa si kitu, tangu siku ya kwanza nilikupenda na ninakuahidi kukupenda milele,” alisema Razak.
“Kweli?”
“Niamini mke wangu...” alisema Razak na kisha kumkumbatia.
Siku hiyo ikapita, siku zikaendelea kukatika na mwisho wa siku kubakia siku mbili kabla ya mwezi kumalizika, alichokifanya Razak ni kumuita Aisha na kukaa aye sebuleni, mbele ya wazazi wake, alikuwa ameshika karatasi moja ndefu iliyokuwa na maneno mengi, alitaka kuisoma mahali hapo, alitaka kumsomea mke wake kwani hakuwa na zaidi ya siku tatu za kuishi.
Muda wote huo, hapo sebuleni Aisha alikuwa mtu wa kulia tu, hakukuwa na kitu alichotokea kukichukia kama ugonjwa wa kansa ambao ulimfanya kubakiza saa chache kabla ya kufariki dunia.
*****
Je nini kitaendelea...