Simulizi: Penzi lisilo Na Mwisho

Simulizi: Penzi lisilo Na Mwisho

Sehemu ya 27

Sabrina alikuwa akitetemeka, joto lilikuwa likiongezeka mwilini mwake, hakuamini kile alichokuwa akikisoma katika notebook aliyokuwa nayo ambayo aliitoa katika chumba cha Sharifu.

Kitabu kile kilikuwa na majina ya wanawake aliotembea nayo Sharifu, walikuwa wanawake kadhaa na yeye mwenyewe kukiri kwamba wote hao aliotemba nao hakuwa akiwapenda, alitaka kuwaumiza kama yeye alivyoumizwa na msichana wake wa kwanza, Shamsia.

Moyo wake uliwaka kwa hasira, alijikuta akikitupa notebook ile na kujilaza kitandani.

Alishindwa kuvumilia, kilichokuwa kimetokea kwake kilikuwa dharau kubwa, yaanii ampende mwanaume kwa mapenzi yote halafu mwisho wa siku aseme kwamba alitaka hakuwa akipendwa bali kuchezewa, hakika yalikuwa ni maumivu makubwa ambayo hakutarajia kuyapata.

Hasira iliyowaka moyoni mwake, ikayaondoa mapenzi aliyokuwa nayo kwa Sharifu, alimchukia ghafla, kitu pekee alichokitaka ni kumuua mwanaume huyo na kisha yeye kufungwa, hata kama angefungwa kifungo cha maisha, sawa, kama ni kunyongwa, napo ingekuwa sawa ila si kumuacha mwanaume kama Sharifu aendelee kuishi.

Hakutaka kuondoka chumbani pale, alibaki akilia, alimsubiri Sharifu kwa hamu kubwa, alitaka mwanaume huyo atakapokuja basi amchome kisu na kumuua humohumo chumbani, na kama itawezekana, basi hata na yeye ajiue pia.

Aliendelea kumsubiri Sharifu, hakutulia chumbani, mara atoke, mara aingie, alipokumbuka kwamba hakuwa na kisu cha kufanyia mauaji, harakaharaka Sabrina akaondoka chumbani na kuelekea jikoni, huko akachukua kisu na kurudi chumbani.

“Nitakuua Sharifu...nitakuua Sharifu....” alisema Sabrina huku akilia kama mtoto.
Alikumbuka vilivyo kwamba alimuacha mwanaume ambaye aliamini kwamba angemuoa, akaangukia katika penzi la Sharifu ambaye leo hii eti alisema kwamba yeye alikuwa msichana wa kupita, yaani kumuumiza kama kisasi cha yeye kuumizwa na msichana mmoja huko Dubai, hakika hakutaka kusubiri, hakutaka kuona mwanamke mwingine anaumizwa baada yake, ilikuwa ni lazima amuue huyo Sharifu.

Dakika zilizidi kusonga mbele, masaa yalikatika lakini Sharifu hakutokea nyumbani hapo. Hiyo haikuwa kawaida kabisa, alimfahamu mwanaume wake, hakuwa mtu wa kuchelewa kurudi nyumbani, huwa anapokwenda kwa marafiki zake kucheza mchezo wa Darts, hurudi nyumbani haraka na kukaa naye.

Siku hiyo hali ilikuwa tofauti kabisa, hakujua kama Mungu alizungumza na Sharifu na kumpa taarifa kama kule nyumbani alimsubiri kwa hamu ili amuue au la, kwani kuchelewa kwake huko hakikuwa kitu cha kawaida kabisa.

“Ngoja niimpigie simu,” alisema na hapohapo kuchukua simu yake.
Akampigia, simu haikuita sana, ikapokelewa na sauti ya Sharifu kusikika upande wa pili.

Japokuwa ilikuwa ngumu lakini Sabrina alijikaza kwa kuongea kwa furaha, aliilazimisha furaha yake huku akiamini kabisa kwamba moyo wake ulikuwa na kidonda kikubwa kabisa tena huku akiwa na hamu kubwa ya kumwaga damu.

“Mpenzi...” aliita Sabrina.
“Niambie mpenzi! U mzima?” aliuliza Sharifu upande wa pili.
“Nipo poa...unarudi saa ngapi?” aliuliza Sabrina.
“Muda si mrefu...”
“Basi fanya haraka kipenzi, nimekumisi sana...”

“Kweli?”
“Ndiyo! Nataka nikuone, nikupe mapenzi motomoto mpaka upagawe...” alisema Sabrina.
“Nakuja fasta.....”
“Nakupenda mpenzi...”
“Nakupenda pia.”

Baada ya mazungumzo hayo machache, Sabrina akakata simu. Hapohapo kilio kikubwa kikaanza kusikika, hasira alizokuwa nazo hakuweza kuzivumilia, zilimkaba kooni kiasi kwamba kwa jinsi alivyokuwa akitetemeka, hali ile iliongezeka zaidi.

Harufu ya damu ikaanza kusikika puani mwake, hakuona sababu ya kumuonea huruma mwanaume huyo, alichokiona kuwa suluhisho, kumpa furaha moyoni mwake ni kumuua tu.

Baada ya dakika thelathini, akaanza kusikia muungurumo wa gari kutoka nje, harakaharaka akachungulia dirishani, akauona mwanga wa gari lililokuwa likipiga honi, hakuwa na wasiwasi, akajua dhahiri kwamba mtu aliyekuwa kwenye gari alikuwa Sharifu, hivyo harakaharaka akaanza kutoka ndani na kuelekea huko getini, amfungulie mlango, akiingia ndani tu amuue na yeye kujiua.
Akaanza kuelekea getini.
****
Sharifu alikuwa mtoto wa tajiri mkubwa aliyekuwa akiishi Dubai, alitembelea magari ya kifahari, alikuwa akiringa kwa sababu alipata kila kitu alichokitaka kutoka kwa baba yakee, alipewa fedha nyingi ambazo zote hizo alizitumia kwa kutembea na wanawake mbalimbali ambao kwa kifupi aliwaita mademu zake.

Jina lake likawa kubwa katika kumbi nyingi za starehe hapo Dubai, alijukana kila kona kwa kuwa hakuwa na mkono wa birika, kwa mtu aliyekuwa akihitaji kiasi fulani cha fedha, kwake hakukuwa na tatizo, alimpa, hasa wasichana.

Baadaye alipoamua kwenda kwa mama yake aliyekuwa akiishi nchini Tanzania katika jiji la Dar es Salaam, baba yake akamnunulia jumba kubwa lililomgharimu zaidi ya milioni mia saba, fedha halikuwa tatizo, kiasi hicho kilitolewa haraka sana.

Alipofika tu ndani ya nyumba hiyo, kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kumuita mtaalamu wa IT na kumfungia kamera ndogo chumbani kwake ambazo hujulikana sana kwa jina la CCTV.

Kamera hizo zilifungwa kila kona, kuanzia sebuleni, ukumbini, bafuni, chooni mpaka chumbani. Hakuwa mtu wa kujiamini, alijua jinsi watu walivyo kwamba mara unapogundulika umetoka kwenye familia ya kitajiri, kitu cha kwanza kufanya ni kukuteka na kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha.

Alihitaji kujua kila kitu kilichokuwa kikiendelea nyumbani kwake kupitia katika laptop aliyokuwa nayo, tena aliunganisha mpaka kwenye simu yake. Hata kama alikuwa mbali kiasi gani, kupitia vifaa vyake hivyo alijua ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea nyumbani.

Mara baada ya kugombana na Sabrina, alijua fika kwamba ni lazima msichana huyo atafanya kitu kibaya kwani baada ya ugomvi ule wa kumfumania, msichana huyo alibadilika, akawa mtu wa hasira ambaye hakutaka kuzionyesha hasira zake hadharani, yaani alikuwa akiwaka moto moyoni mwake, nje, alijilazimisha kutoa tabasamu pana.

Siku ambayo Sabrina alipanga kumuua kwa kumchoma kisu, alikuwa akifuatilia kila hatua, alimuona msichana huyo akiwa kitandani amejipumzisha, hakuonekana kuwa na furaha kabisa na dalili zilionyesha kwamba alikuwa akilia sana.

Baada ya kukaa kwa kipindi fulani, akatoka ndani ya chumba kile na kuelekea jikoni. Kote huko, Sharifu alikuwa akifuatilia kwa ukaribu, aliona hatua kwa hatua mpaka msichana huyo alipochukua kisu na kwenda nacho chumbani.

“Mmh!” Sharifu alijikuta akiguna.
Hakuishia hapo, aliendelea kufuatilia kwa karibu kabisa, alitaka kuona nini kingetokea baada ya hapo. Alimuona Sabrina akielekea kitandani kwake, alionekana kuwa na hasira na hisia zake zikamwambia kwamba kile kisu kiliandaliwa kwa ajili yake.

Akamuona Sabrina akichukua simu na kuanza kumpigia, japokuwa sauti yake ilisikika vizuri lakini picha aliyokuwa akiiona, haikuwa nzuri kabisa, ilionyesha kwamba alikuwa na hasira kali, tena alikuwa radhi kufanya jambo lolote lile.
“Nakuja...” alisema kwenye simu na kuikata.

Alichokifanya ni kuwapigia simu marafiki zake, aliwaambia kila kitu kinachotakiwa kufanywa kwani hakutaka kurudi tena nyumbani kwake, kwa jinsi hali ilivyokuwa, ilikuwa ni lazima aondoke zake kwani vinginevyo, huyu Sabrina hakuwa mtu tena, alikuwa ni mnyama mwenye hasira kali ambaye kila wakati alikuwa akimuwinda.

“Nyie nendeni, fanyeni kama nilivyowaambia...” alisema Sharifu.

Je nini kitaendelea...
 
Sehemu ya 28

Sabrina alitembea huku akitetemeka, kisu kilikuwa kiunoni mwake na hasira kali zilimkaba moyoni mwake. Hakutaka kitu kingine zaidi ya kumuua Sharifu ambaye kwake alimuona mwanaume katili asiyestahili kuishi katika dunia hii.

Kadiri alivyokuwa akipiga hatua na ndivyo hasira zake zilivyozidi kuongezeka. Ingawa geti lile halikuwa mbali kutoka pale aliposimama lakini aliliona kama lipo mbali na hivyo kuchelewa kufika.

Gari hilo liliendelea kupiga honi mfululizo kama mtu aliyekuwa na uharaka wa kufunguliwa na kuliingiza gari katika eneo la nyumba hiyo, Sabrina alipolifikia geti, akalifungua, macho yake yakatua katika gari ambalo halikuwa la mpenzi wake, lilikuwa gari jingine kabisa.
“Habari shemeji...” alisikia akisalimiwa huku msalimiaji akiteremka kutoka garini.

“Salama tu...” aliitikia Sabrina huku akimwangalia mwanaume aliyemsalimia.
Sabrina akabaki akiwa ameshtuka, alipomwangalia vizuri mwanaume yule, shati lake jeupe lilitapakaa damu kwa kiasi kikubwa kitu kilichomfanya kuogopa.

Hakuwahi kumuona mwanaume huyo na hakujua alikuwa nani, damu hizo zilikuwa za nini na kuna kitu gani kilitokea? Kila alichojiuliza, hakuwa na majibu nacho.
“Kuna taarifa mbaya...” alisema mwanaume huyo, Sabrina akashtuka.
“Taarifa gani?”

“Hapa si ndiyo kwa Sharifu?”
“Ndiyo! Nyie ni wakina nani?”
“Sisi ni washikaji zake, taarifa mbaya ni kwamba Sharifu amepata ajali...”
“Ajali?”

“Ndiyo! Si ya gari, amechomwa kisu ukumbini,” alijibu mwanaume huyo.
“Amechomwa kisu?”
“Ndiyo! Hapa tumetoka kumpeleka hospitali...hali yake mbaya sana,” alisema mwanaume huyo.

“Sharifu amechomwa kisu?”
“Ndiyo! Shemeji, twende hospitali, hali yake mbaya sana...”
“Yupo hospitali gani?”
“St. Augustino...”
“Nakuja...”

Sabrina alionekana kuchanganyikiwa, taarifa aliyopewa ilimuweka katika wakati mgumu, hakuamini kile alichokisikia kwamba mpenzi wake ambaye alipanga kumuua alichomwa kisu na mtu mwingine akiwa klabu.

“Nini kimetokea? Kwa nini Mungu ameamua kunilipia?” alijiuliza huku akijiandaa, alipomaliza, akatoka na kuanza kuelekea huko hospitali huku akiwa na watu hao.

Njiani, hakulia bali alikuwa na mawazo mengi, alimchukia mno Sharifu, aliamini kwamba kifo pekee ndicho alichostahili kufa mwanaume huyo aliyeutesa moyo wake.

Watu wengi waliokuwa ndani ya gari hilo walimshangaa, ilikuwaje apate taarifza za hali mbaya ya mpenzi wake halafu asilie, yaani kuhuzunika tupu haikutosha.

Walipofika hospitalini, wakaelekea mapokezi ambapo nesi aliyekuwa hapo akawaambia kwamba muda wa kuona wagonjwa haukuwa umefika lakini hata hivyo mtu waliyekuwa wakimuulizia alikuwa hoi akifanyiwa upasuaji.
“Kwa hiyo hatuwezi kumuona?” aliuliza Sabrina.

“Haiwezekani dada...labda mpaka upasuaji ukamilike...” alijibu nesi yule.
Moyo wa Sabrina ukagawanyika, kulikuwa na upande ambao ulifurahia kile kilichotokea kwa kuona kwamba amerahisishiwa kazi lakini upande mwingine ulimuonea huruma Sharifu kama binadamu wengine.

Hakutaka kuondoka hospitalini hapo, alitaka kumuona mwanaume huyo akiteseka kitandani kwani ndicho kingekuwa kitu pekee ambacho kingemfanya kufurahi au kuhuzunika zaidi.

Madaktari walikuwa wakipishana tu mlangoni, wakati huyu alikuwa akiingia, mwingine alitoka na kuendelea na shughuli zake. Pole kwenye benchi alipokuwa, Sabrina hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, kama kumuomba Mungu amponye Sharifu au amuongezee maumivu.

Kutokana na kuchoka sana huku muda ukiwa umekwenda sana, akajikuta akilala hapohapo kwenye benchi, na alipokuja kushtuka, tayari ilikuwa saa kumi na moja alfajiri, kitu cha kwanza kabisa alichokitaka ni kumuona Sharifu.
“Kumuona haitowezekana...”
“Kwa nini?”

“Hali yake bado mbaya...hapa tunataka tumfanyie uhamisho...”
“Wa kwenda wapi?”
“Muhimbili....”

“Kwani hali yake ni mbaya sana?”
“Sana...ila kuna kingine pia...”
“Kipi?”
“Wazazi wake walifika na kutaka tumsafirishe aelekee India kutibiwa...”
“Wazazi wake?”

“Ndiyo!”
“Walikuja muda gani? Mbona sikuwaona?”
“Walifika alfajiri kabisa....”
“Alfajiri! Ipi hiyo?”
“Wewe jua alfajiri binti...ngoja nikaendelee na kazi zangu,” alisema daktari huyo huku akionekana kuwa na haraka.

Sabrina alibaki akiwa na mshangao, hakuamini kama majibu yale alipewa na daktari aliyesomea ambaye kila siku alitakiwa kuwa mnyenyekevu kwa wagonjwa au watu waliokuja kuwaona ndugu zake.

Alishangaa alipoambiwa kwamba wazazi wa Sharifu walifika hospitalini hapo, wakamuona mtoto wao na kushauri kwamba ilikuwa ni lazima asafirishwe kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

Kama walifika hiyo alfajiri, ilikuwa muda gani? Kwa nini hakuamshwa na wakati madaktari walifahamu kwamba hata yeye alifika hapo kwa ajili ya kumuona Sharifu? Kila alichojiuliza, akakosa jibu.

Hakutaka kubaki mahali hapo, hakuridhika na majibu aliyopewa na daktari yule, hivyo akamfuata na kumuuliza zaidi, ilikuwaje yote hayo kutokea, majibu ya daktari yalikuwa yaleyale kwamba aachwe kwani alikuwa na mambo mengi ya kufanya.

Moyo wake ukaanza kuwa na wasiwasi, akahisi kama alikuwa akifanyiwa mchezo fulani, ila kwa kuwa alikuwa na namba za wale marafiki zake Sharifu waliokuja kumchukua nyumbani, akaamua kumpigia simu mmoja wao.

“Umesema wamesemaje?”
“Eti wazazi wake hawataki atibiwe hapa....”
“Wamekwambia kwamba yupo?”
“Ndiyo!”
“Wamekudanganya!”

“Wamenidanganya? Kivipi?”
“Huyo daktari hakutaka kukwambia ukweli kwamba Sharifu alifariki, mwili wake ulichukuliwa na kupelekwa sehemu maalumu ya kuchoma moto,” alisikika rafiki huyo.

“Unasemaje?”
“Huo ndiyo ukweli! Madaktari wanakuficha tu, labda kwa kuwa si ndugu yao. Sabrina, pole sana,” alisikika rafiki huyo.

Sabrina alichanganyikiwa, hakuamini kile alichokisikia kwamba mtu aliyetaka sana kumuua, aliuawa mara baada ya kuchomwa kisu ukumbini na mbaya zaidi, mwili wake ulichomwa moto.

Moyo wake uligawanyika, upande wa kwanza ulimwambia kwamba kile kilichotokea, kilikuwa uongo, na kilifanywa hivyo kwa sababu alikuwa na lengo la kumuua mwanaume huyo ila upande mwingine wa pili ukamwambia kwamba kilichokuwa kimetokea, kilikuwa kweli kabisa.

Alichanganyikiwa, hakujua ni upande gani aliotakiwa kukubaliana nao.

Kitu ambacho kidogo kilimuingia akilini ni kwamba kilichotokea kilikuwa kweli kwani kama kilikuwa uongo, Sharifu alijuaje kama alitaka kumuua? Hakumwambia mtu na uamuzi huo ulikuwa ni wa kushtukiza sana.
“Kwa hiyo amekufa?” aliuliza Sabrina huku akitaka kuwa na uhakika.

“Ndiyo! Amekufa na mwili wake kuchomwa moto....” alisema rafiki huyo.
Alichoka sana, moyo wake haukuisha kuwa kwenye majuto makubwa, kila alipokumbuka jinsi mwanaume wake wa nyuma, Razak alivyokuwa akimpenda, alivyomthamini na kutaka kumuoa ila kwa macho ya tamaa kuangukia kwa Sharifu, moyo wake ulimuuma mno.

Wakati mwingine alijiona kuwa mtu mjinga, aliyefanya uamuzi wa kijinga kumuacha mwanaume huyo na kumfuata Sharifu ambaye wala hakuwa na mpango naye zaidi ya kumchezea.

Huku akiwa kwenye kipindi cha majuto, hapo ndipo alipoona kwamba huo ulikuwa muda wa kumfuata Razak, aongee naye, amuombe msamaha na mwisho wa siku wawe kama zamani, na hata ikiwezekana, wafunge ndoa na kuishi pamoja.

“Kweli atakubali? Mhh! Kwa jinsi nilivyomuumiza! Mungu nisaidie,” alisema Sabrina huku akionekana kuwa na mawazo tele.

Watu ambao aliwafikiria kwa mara ya kwanza kuwaomba msamaha walikuwa wazazi wake, walimuonya kabla kwamba mtu aliyeamua kumuacha ndiye alikuwa sahihi kuliko yule aliyeamua kumfuata, aliwapinga, akawaona wabaya, akaondoka zake, akaamua kwenda kwa Sharifu ambaye hakuwa ametulia hata kidogo.
“Nitawaomba msamaha tu....” alisema na kuondoka kuelekea nyumbani.

Alipofika huko, wazazi wake wakashangaa, walishtuka jinsi binti yao alivyokuwa. Walimjua, alipokuwa na furaha, walijua, alipokuwa na huzuni, walijua na hata alivyokuwa kawaida, walijua pia.

Siku hiyo alionekana kuwa tofauti, mtu mwenye mawazo, aliyekata tamaa, walibaki wakimwangalia na kugundua kwamba alikuwa na tatizo, kulikuwa na kitu kilichomsibu, hivyo wakaanza kumuuliza.

“Kuna nini?” aliuliza mama yake, hapohapo Sabrina akaanza kutiririka machozi.

“Naombeni mnisamehe...”
“Tukusamehe, kwa lipi?”
“Kwa nilichowafanyia.....naombeni mnisamehe, dunia imenifunza...” alisema Sabrina huku akilia kama mtoto.
“Kwani kuna kitu gani kimetokea?” aliuliza baba yake.

“Sharifu...Sharifu ameuumiza moyo wangu, Sharifu ameniachana na kumchukua mwanamke mwingine,” alisema Sabrina.

Wazazi wake wakapigwa na mshangao, hawakuamini walichokisikia kwamba binti yao aliachwa na mwanaume ambaye aliwaambia kwamba alikuwa mwanaume wake wa ndoto.

Huo haukuwa muda wa kumlaumu, ulikuwa ni muda wa kukaa naye chini na kumfariji kama mtoto wao. Walijua alikosea lakini wao kama wazazi walitakiwa kumsamehe na kuanza upya kama zamani.

Walichokifanya ni kumwambia wazi kwamba walimsamehe, asahau kila kilichotokea, na walikuwa naye bega kwa bega, wakimsaidia kwa kila kitu alichohitaji kufanyiwa.

“Ninataka kumuomba msamaha Razak, nirudiane naye,” alisema Sabrina.
“Sawa! Tutajitahidi tunakusaidia katika hilo, nahisi atatuelewa kwani ni wiki moja tu imepita, hakuna tatizo,” alisema baba yake.

Kipindi hicho hakuwa na namba ya Razak hivyo mtu aliyempigia simu alikuwa rafiki yake Razak aitwaye Jafari, amgawie namba ya Razak, ampigie na kuzungumza naye ili amuombe msamaha.
“Unataka namba ya Razak?” aliuliza Jafari kwenye simu.

“Ndiyo! Naomba unisaidie...”
“Wewe ya nini?”
“Niwasiliane naye, anisamehe na turudiane...”

“Urudiane na Razak?”
“Ndiyo! Naomba unisaidie Jafari...”
“Haiwezekani kabisa....”
“Haiwezekani nini? Kuwasiliana naye au kurudiana naye?”

“Kurudiana naye, Razak amepata msichana mwingine, na hivi baada ya miezi miwili, anamuoa...” alisema Jafari.
“Unasemaje?”

“Ndiyo hivyo! Ulivyomuacha tu, siku hiyohiyo alikuwa amepata msichana, mzuri kweli, kwani hakukwambia?” aliuliza Jafari.

Sabrina hakujibu swali hilo, kilio kikubwa kikasikika kutoka kwake, akaitupa simu na kuendelea kulia kwa sauti kubwa. Wazazi wake waliokuwa sebuleni, harakaharaka wakakimbilia chumbani kwake, wakamkuta binti yao akiendelea kulia huku simu ikiwa imetupwa karibu na ukuta.

Hawakujua tatizo lilikuwa nini, walijaribu kumbembeleza na kumuuliza tatizo lilikuwa nini lakini msichana huyo hakujibu chochote kile zaidi ya kulia tu.
“Kuna nini Sabrina?” aliuliza baba yake. Hakujibu, aliendelea kulia zaidi kitu kilichowafanya kujiuliza juu ya kilichomsibu binti yao.

Je nini kitaendelea....
 
Sehemu ya 29

“Razak...Razak....baridi linaniumiza...” alisikika Aisha kwa sauti ya chini.
“Baridi linakuumiza?”
“Ndiyo!”
“Subiri nikazime kiyoyozi...” alisema Razak.

Ilikuwa ni usiku wa manane, wote walikuwa wamelala chumbani, ukimya mkubwa ulitawala, dakika zilizidi kusonga mbele lakini ghafla, Aisha akashtuka kutoka kitandani, alikuwa akilia kwa maumivu makali ya tumbo yaliyomfanya kulalamika mno.

Harakaharaka Razak akainuka kutoka kitandani, akaifuata rimoti ya ya kiyoyozi na kuikizima. Bado Aisha alikuwa akilalamika kwa maumivu makali ya tumbo, Razak alishangaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka msichana huyo kulalamika kwa maumivu makali.

Kila alipouliza, hakupewa jibu zaidi ya msichana huyo kuendelea kulalamika zaidi. Razak akaogopa, akahisi kwamba kama asingefanya kitu cha ziada basi mpenzi wake angeweza kuwa kwenye hali mbaya zaidi.

“Inuka twende hospitali...” alisema Razak.
“Siwezi....naumia, tumbo linauma Razak mpenzi....nisaidie...” alisema Aisha kwa sauti ya chini iliyojaa maumivu makali.
Razak hakutaka kusubiri, alichokifanya ni kumbeba Aisha na kuanza kuelekea naye nje ya chumba kile huku lengo likiwa ni kuchukua gari na kuelekea hospitalini.

Walipofika nje, Aisha akazidi kulalamika kwa maumivu makali, baridi walilokutana nalo nje lilimtesa, akapiga kelele mpaka zikafika katika nyumba za jirani, harakaharaka Razak akaufungua mlango na kumuingiza msichana huyo ndani ya gari lake, akaelekea upande wa pili, akaufungua na kuingia ndani.

“Pole mpenzi....vumilia...” alisema Razak, akawasha gari na kuondoka mahali hapo.
Ndani ya gari, kelele zilikuwa nyingi, Razak alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alitamani kumfuata Aisha na kumbeleza lakini upande mwingine, alitamani kuliendesha gari kwa kasi kuwahi hospitalini.

Hakuchukua dakika nyingi, akawa amefika hospitali ambapo akafungua mlango huku akiwaita manesi ambao walifika na machela, wakampakiza na kuanza kuisukuma kuelekea ndani ya jengo la hospitali hiyo.

Walipofika katika chumba kilichoandikwa ‘Theatre’ akaambiwa kusubiri katika mabenchi yaliyokuwa nje, akatulia. Hapo, kichwa chake kilichanganyikiwa mno, hakujua ni kitu gani kilimsibu mpenzi wake, japokuwa ilikuwa ni usiku wa manane lakini hakuweza kupata usingizi kabisa.

Alikuwa mtu mwenye mawazo mengi, alitulia katika benchi lililokuwa nje ya kile chumba huku akionekana kuwa na mawazo mengi.

Hakuishia kukaa tu, wakati mwingine alisimama na kuanza kuzunguka huku na kule, hakika alichanganyikiwa na kilichomuumiza kichwa zaidi, Aisha alikuwa na tatizo gani?
“Tatizo nini?” alijiuliza pasipo kupata jibu lolote lile.

Watu aliowafikiria kwa kipindi hicho walikuwa wazazi wake, alitakiwa kuwapa taarifa na kuwaambia kilichokuwa kikiendelea hospitalini hapo. Muda ulikwenda sana lakini hakutaka kuacha kuwapigia ili hata kama lingetokea tatizo kubwa zaidi basi wawe na taarifa.

Akachukua simu yake na kuanza kuwapigia. Simu ikaanza kuita, iliita na kuita mpaka kukata pasipo kupokelewa. Hakujiuliza sana, alijua kwamba muda huo wangekuwa wamelala, alichokifanya ni kupiga tena simu.

“Haloo...” ilisikika sauti nzito ya baba yake, ilionyesha kabisa kama alitoka kuamka.

“Baba...Aisha amezidiwa, nimemleta hospitali...” alisema Razak kwa huzuni.
“Anaumwa nini?”
“Sijui chochote kile...”
“Mpo hospitali gani?”
“Hospitali ya Mediteranian..”
“Tunakuja...”

Simu ikakatwa na Razak kutulia kwenye benchi. Mawazo hayakumtoka na kila alipokaa, aliisikia sauti ikimwambia kwamba ni lazima mpenzi wake afariki dunia hapohapo kitandani kwani tatizo alilokuwa nalo lilikuwa kubwa mno.

Wasiwasi ukamshika lakini hakutaka kukata tamaa, kila wakati alimuomba Mungu atende muujiza na vipimo vitakavyopimwa basi ionekane hana tatizo lolote zaidi ya tumbo kuchafuka tu.

Dakika ziliendelea kukatika, baada ya dakika kadhaa, wazazi wake wakafika hospitalini hapo na moja kwa moja kuelekea kule alipokuwa. Walipomuona, walijua tu kwamba kulikuwa na tatizo, jinsi alivyoonekana, ilikuwa rahisi mno kugundua kwamba kijana wao alikuwa kwenye matatizo makubwa.

“Pole sana Razak,” alisema baba yake huku akimkumbatia, kumbatio lililomfanya kuanza kububujikwa na machozi kwa mara nyingine.

Wakakaa naye chini na kuanza kumuuliza maswali kadhaa ni tatizo gani alilokuwa nalo Aisha, hapo, akaanza kuwaambia kila kitu kilichokuwa kimetokea kwamba alishtuka usiku wa manane huku akiugulia maumivu, baada ya hapo, akamchukua na kumpeleka hospitali.

“Kwa hiyo haijajulikana tatizo nini?” aliuliza mama yake.
“Bado, tangu waingie ndani, hawajatoka...” alijibu Razak.
“Ngoja tusubiri...”

Muda ulizidi kwenda, dakika zilikatika mpaka ilipofika saa kumi alfajiri, mlango ukafunguliwa na daktari mmoja wa kike mwenye koti kubwa jeupe lililokuwa na kibati kilichoandikwa Dk. Mimi kifuani kutoka ndani ya chumba hicho.

Hapohapo Razak akasimama na kuanza kumsogelea, alitaka kujua ni kitu gani kilikuwa kimeendelea lakini pia alitaka kufahamu ni tatizo gani alilokuwa nalo mpenzi wake.

“Nifuateni...”
Hawakuwa na jinsi, walichokifanya ni kuanza kumfuata Dk. Mimi ambaye alikwenda mpaka kwenye chumba kilichoonekana kuwa ofisi yake na kukaa kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya nyumba huku akiwataka wageni wake kukaa vitini.

Kabla hajazungumza lolote, akachukua baadhi ya mafaili yaliyokuwa mezani kwake, akaandika, akashusha miwani kidogo na kuwaangalia kwa zamu huku akionekana kabisa kutaka kuzungumza kitu.

“Kwanza poleni kwa matatizo mnaliyokutana nayo....” alianza kusema Dk. Mimi.
“Asante sana, nini kinaendelea? Anaumwa nini? Atapona?” aliuliza Razak maswali matatu mfululizo.

“Tumemchunguza kwa kipindi kirefu na tumemkuta ana tatizo ambalo nashangaa ilikuwaje mpaka mkasubiri kwa kipindi kirefu mpaka tatizo kuwa sugu namna hii,” alisema Dk. Mimi.

“Tatizo gani?”
“Kwanza mpo na mgonjwa kwa kipindi gani?”
“Kama miezi miaka miwili..” alidanganya Razak.

“Katika kipindi chote hamkugundua kwamba ana tatizo lolote?”
“Hapana! Kwani kuna nini dokta?”
“Na mlikuwa mnacheki afya yake mara kwa mara?”
“Hapana!”

“Tumekuta binti yenu ana tatizo kubwa sana, lilianza kidogokidogo, likawa linakua, likakua na kukua na mwisho wa siku kuwa kubwa kabisa ambalo haliwezi kabisa kutibika,” alisema Dk. Mimi, taarifa hiyo ilimshtua kila mmoja.
“Tatizo gani?”

“Ana kansa ta utumbo mpana ambayo kitaalamu inaitwa Colon Cancer,” alijibu daktari huyo.

“Unasemaje?”
“Ndiyo hivyo! Ni tatizo kubwa sana ambalo linaua maelfu ya watu kila mwezi hapa duniani. Huwa linaanza taratibu sana, unapolipuuzia, linakua na kukua, kosa kubwa lililofanyika ni kwamba hakuangaliwa afya yake kipindi cha nyuma, ila kitu kinachosikitisha zaidi.....” alisema Dk. Mimi, hata kabla hajamalizia sentensi yake, akabaki kimya.

“Kitu gani?” aliuliza baba yake Razak, wakati huo, kijana wake alikuwa akilia tu.
“Au basi, mengine tutaongea siku nyingine...” aliseema Dk. Mimi.

“Hapana! Haiwezekani, haiwezekani utuache hewani, tuambie hicho kingine ni nini,” alisema mama yake Razak, alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.
“Tutaongea siku nyingine...” alisisitiza Dk. Mimi.

“Dokta, umetuambia kwamba Aisha ana kansa mbaya, tumekubaliana nawe, unajua ni jinsi gani tulivyoumia, naomba usituache njia panda, tuambie hilo lingine ni lipi,” alisema mama yake Razak.
“She has Terminal Cancer,” (Ana kansa isiyopona) alijibu daktari kwa sauti ya chini, hata yeye mwenyewe, alionekana kuumia sana.

“What is that?” (Ndiyo nini hiyo?)
“Hatoweza kupona, hiyo ni kansa inayoua, imesambaa sana, hatoweza kupona, ni lazima atakufa, ni ndani ya miezi mitatu tu,” alijibu daktari huku akiwaangalia wote wawili.

Hakukuwa na siku ambayo Razak alilia kama siku hiyo, ilionekana kama kuna msiba ndani ya ofisi ya daktari, alilia kwa sauti pasipo kuona kama pale palikuwa hospitali au la.

Moyo wake uliumia, hakuamini kile alichokisema daktari kwamba msichana Aisha asingeweza kupona, yaani ile kansa ilikuwa ni lazima imuue. Alitamani kuona kile alichokisikia kiwe ndoto, yaani ghafla ashtuke kutoka katika usingizini, Aisha awe pembeni yake na amwambie kwamba kila kitu alichokiota, kilikuwa ndoto tu.

Hiyo haikuwa ndoto, alijaribu kuziuma lipsi zake ili kuona kama angeshtuka kutoka usingizini lakini wapi, bado kila kitu kilichokuwa kikiendelea kilikuwa kitu halisi na hakikuwa ndoto kama alivyokuwa akihisi.

Watu wote waliokuwa ndani ya chumba kile wakaanza kumbembeleza Razak lakini hakunyamaza, alimpenda Aisha kupita maelezo, alikuwa radhi kupoteza kitu chochote katika maisha yake lakini si kumpoteza Aisha ambaye alionekana kuwa kila kitu kwake.

Kulia sana, kumbembelezwa sana hakukuweza kubadilisha matokea, ukweli ukaendelea kuwa palepale kwamba mpenzi wake alikuwa mgonjwa wa kansa ya utumbo mpana na kamwe asingeweza kupona, ilikuwa ni lazima afariki dunia.
“Siwezi kukaa....ninataka kumuona mpenzi wangu, ninataka kumuona Aishaaaaa...”

alisema Razak huku akionekana kama kuchanganyikiwa, hakutaka kubaki mahali hapo, hapohapo akasimama na kutoka nje, akaanza kukimbia kule kulipokuwa chumba alichoingizwa Aisha....wazazi wake na Dk. Mimi wakaanza kumfuata kwa mwendo wa kasi, walijua ni kwa jinsi gani Razak alikuwa amechanganyikiwa.

Je nini kitaendelea....
 
Sehemu ya 30

Hali ya hewa ilikuwa joto sana, watu wengi walioonekana mitaani walikuwa na nguo nyepesi huku hata wale waliokuwa ndani ya magari yao ilikuwa ni lazima kuwasha viyoyozi kwa ajili ya kuipa baridi miili yao.

Joto ilikuwa moja ya hali ya hewa iliyokuwa ikitesa sana mjini Dubai, kila mtu aliyefika nchini humo, malalamiko yake yalikuwa ni juu ya joto kali lililokuwa likiwatesa watu wengi hasa wale Wazungu na watu wengine waliotoka katika nchi zilizokuwa na baridi kali.

Wakati huo, ndege kubwa ya Fly Emirates ilikuwa ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai ambapo moja kwa moja baada ya ndege kusimama, abiria wakaanza kutembea kuelekea ndani ya jengo la uwanja huo huku wakijipepea.

Miongoni mwa abiria walioteremka ndani ya ndege hiyo alikuwa mtoto wa bilionea, Sharifu ambaye alikuwa akipiga hatua huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana na kujiona mshindi kwa kile alichokifanya.

Alipiga hatua mpaka ndani ya jengo lile ambapo baada ya kuchukua mizigo yake, akaondoka na kuchukua teksi ambayo ilimpeleka mpaka katika jumba la kifahari alilokuwa akiishi.

Tayari aliwasiliana na marafiki zake ambao tayari walifika hapo kwake na kuanza kusherehekea pasipo kujua kwamba huko nyuma alipotoka aliacha kilio na maumivu makali kwa msichana Sabrina ambaye alionyesha moyo wote wa kumjali na kumpenda ila kwa makusudi kabisa, akaamua kumuacha na kufanya mambo yake.

Maisha yake yakaanza upya nchini Dubai, hakutaka kuwasiliana tena na Sabrina, kwake, kila kitu kilionekana kupita na hakujua kama msichana huyo angejua kilichotokea na hivyo kumtafuta.

Ulikuwa muda wa kuyafurahia maisha, hakuacha kuchukua wasichana na kutanua huku na kule, kwake, maisha hayo ndiyo yalikuwa sehemu ya maisha yake, hakutaka kufikiria kitu kingine chochote katika maisha yake zaidi ya kula bata alivyotaka.

Siku zikaendelea kukatika, wiki ya kwanza ilipokatika, hapo ndipo akapokea simu ya ajabu ambayo ilimwambia kwamba alikuwa akitafutwa na mwanamke, hakujua alikuwa nani na alipouliza zaidi, akaambiwa mwanamke kutoka nchini Qatar ambaye alifika hapo Dubai kwa ajili ya kuonana naye.

“Msichana gani huyo?” aliuliza kwenye simu.
“Simjui, ila alifika klabu na kukuulizia, alisema anataka kuonana nawe...”
“Lini?”

“Sikumuuliza...”
“Sasa nitamuonaje? Au ulimpa namba yangu?”
“Sikumpa kabisa...”

“Qadir...huo ni ujinga, msichana anakuja kuniulizia, hata namba yangu humpi!”
“Ila si ulisema kwamba tusiwe tunatoa namba!”

“Ndiyo! Ila si kwa mademu aiseee...”
Sharifu alibaki akilalamika mno, alijua kwamba msichana aliyekuja kumuulizia alikuwa miongoni mwa wasichana aliokuwa akitembea nao na kama si hao basi msichana mpya ambaye alisikia tu kuhusu yeye.

Moyo wake ukawa na hamu ya kumuona msichana huyo, hakumjua alikuwa nani lakini kila alipokaa, kichwa chake kilikuwa juu ya msichana huyo ambaye aliamini kwamba hakuwahi kumuona hata siku moja.
****

‘Wewe msichana mjinga sana, hivi kweli unaamini kwamba Sharifu amekufa?’ ulikuwa ujumbe mfupi ulioingia kwenye simu yake. Hakuamini alichokisoma, alichokifanya, tena huku akiwa kwenye presha kubwa ni kumpigia simu mtu aliyetuma ujumbe huo, simu iliita lakini haikupokelewa mpaka ikakatika.
‘Hapa kuchati tu...” iliingia meseji nyingine.

‘Umesemaje?’
‘Kwani umesomaje?’
‘Kuhusu Sharifu...si alikufa?’
‘Kakudanganya nani? Hakufa, kasepa zake kwenda Dubai, mzima wa afya, aliamua kuchonga dili ili usifahamu kwani alijua usiku wa siku hiyo ungemuua...’

ujumbe wa mtu huyo ulisomeka.
‘Ningemuua! Alijuaje?’
‘Kwa kamera za CCTV zilizokuwa nyumbani kwake...’

Aliendelea kuchati na mtu huyo wa upande wa pili. Kila alichotumiwa, kilimuongezea hasira na kumchukia mwanaume huyo zaidi. Hapo ndipo alipogundua kwamba kweli kila kitu kilichotokea kilikuwa kimesukwa na ndiyo maana hata hiyo siku ambayo aliambiwa kwamba amekufa, siku hiyohiyo akapewa tena taarifa kwamba alizikwa.

Akabaki akilia tu, moyo wake ukawa kama umetoneshwa, hakutaka kukubali, kitu alichotaka kuona ni kumuua mwanaume huyo ambaye aliutesa moyo wake kwa kiasi kikubwa.

Akahisi maumivu makali, hakutaka kukubali hata mara moja. Kitendo cha Sharifu kuwa hai, kilimuudhi na hakuona kama kulikuwa na sababu ya mwanaume huyo kuendelea kuvuta hewa ya dunia hii.
“Ni lazima nisafiri nielekee Dubai, siwezi kumuacha hai,” alisema Sabrina.

Huo ndiyo ulikuwa uamuzi wake, hakutaka kukubali hata kidogo, roho ya mauaji iliendelea kumuandama moyoni mwake, hakutaka kuona mwanaume aliyemuumiza kiasi kile akiendelea kuishi.

Alichokifanya ni kuanza kufanya mikakati ya safari, akaanza kufuatilia vibali vyote, vilipokamilika, akaanza safari ya kueleka mjini Dubai. Njiani, alikuwa akilia tu, maumivu hayakupungua moyoni mwake na kadiri ndege ilivyokuwa ikikata mawingu na ndivyo alivyozidi kuumia moyoni mwake.

Baada ya saa kadhaa, akafika nchini humo na moja kwa moja kuteremka na abiria wenzake na kwenda kuchukua teksi iliyokuwa nje ya uwanja huo na kuondoka mahali hapo.

Hakuchukua muda mrefu, akafika hotelini, akachukua chumba alichokuwa amebooking na kuingia ndani. Kitu cha kwanza kabisa alichokipanga kilikuwa ni kujua mahali alipokuwa akiishi Sharifu.

Alitaka kujua kwanza mahali alipokuwa akiishi na ndipo hapo angeweza kujua nini cha kufanya kwani hakutaka kuchukua muda mrefu huko Dubai, alitakiwa kumuua haraka iwezekanavyo na kurudi nchini Tanzania kwa ajili ya kumuomba msamaha Razak.

Alimjua Sharifu, alikuwa mtu wa kupenda sana starehe, alikuwa tayari kushinda kwenye klabu akitumbua fedha lakini si kulala usiku. Alichokiona, kitu ambacho kwake kilionekana kuwa rahisi sana ni kumtafuta katika kumbi za starehe.

Usiku wa siku hiyohiyo hakutaka kubaki chumbani, akamuuliza mfanyakazi mmoja wa humo sehemu kulipokuwa na klabu ambapo watu wengi walikwenda na kula bata, akaambiwa kwamba hata humo hotelini kulikuwa na klabu kubwa, kama alitaka starehe, basi angeanzia humo.

Hakukataa, akakubali na hivyo ilivyofika saa nne usiku, akashuka kwenye lifti mpaka chini kabisa na kwenda kwenye klabu hiyo ilikuwa na watu wengi, hasa wanawake waliokuwa na uzuri wa sura. Kila mmoja alikuwa bize akicheza, ni wachache ndiyo waliokuwa kwenye makochi.
****

Razak alikuwa akikimbia huku akionekana kuchanganyikiwa mno, kitu pekee alichokitaka mahali hapo ni kumuona mpenzi wake ambaye aliambiwa kwamba alikuwa na kansa ambayo ingemuweka kitandani kwa kipindi kichache na kisha kufariki dunia.

Alichanganyikiwa, alikuwa kwenye hali mbaya mno, alimpenda sana mpenzi wake lakini leo hii aliambiwa kwamba ilikuwa ni lazima Aisha afariki dunia kutokana na kansa ya utumbo aliyokuwa nayo.

Wakati anafika katika chumba kile na ndipo machela aliyolazwa mpenzi wake ikawa inatolewa ndani ya chumba kile cha upasuaji, moja kwa moja akaisogelea na kuisimamisha, manesi wote wakabaki wakimwangalia kwa macho ya huruma.

“Aisha mpenzi...Aisha mpenzi usiniache....” alisema Razak huku akibubujikwa na machozi, kilio chake kilisikika sana.

“Aisha...amka uniangalie, niangalie mpenzi...fumbua macho uniangalie,” alisema Razak huku akiendelea kumwangalia mpenzi wake ambaye hakuwa akijitambua kitandani pale.

Hapohapo wazazi wake na Dk. Mimi wakafika mahali hapo, wote wakaanza kumfariji na kumwambia kwanza aachane na mgonjwa, alitakiwa kupumzika baada ya upasuaji uliochukua saa kadhaa.

Hakutaka kuiachia machela ile, alitaka isukumwe kuelekea ndani ya chumba huku naye akiwepo kuisindikiza. Wazazi wake waliendelea kumbembeleza aiachie machela ile lakini hakutaka kufanya hivyo.

“Ninataka kwenda naye popote aendapo,” alisema Razak huku akionekana kumaanisha.

“Razak...subiri kwanza, Aisha anatakiwa kupumzika,” alisema baba yake kwa sauti ya kubembeleza, bado alimtaka kijana wake kuiachia machela ile.

“Ninampenda Aisha...ninampenda Aisha baba...ninampenda...” alisema Razak huku akiendelea kumwangalia mpenzi wake kwenye machela ile.

Walipata wakati mgumu sana kumbembeleza, mpaka alipokubali kuiachia machela ile, tayari dakika ishirini zilikuwa zimepita. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali na kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kusonga mbele ndivyo alivyozidi kuumia zaidi.

Kwake, Aisha alikuwa kila kitu, alimpenda zaidi ya msichana yeyote yule japokuwa penzi lao halikuwa hata na muda wa mwezi mmoja. Alipoiachia machela ile, manesi wakaanza kuisukuma mpaka katika chumba kilichoandikwa ICU kwa juu.

Alibaki akiisindikiza kwa macho mpaka ilipoingizwa ndani kabisa. Razak akalifuata benchi lililokuwa pembeni na kisha kutulia. Hapo, alikuwa akilia tu, hakuamini kama kweli alikuwa akipitia kile alichokuwa akikipitia.

Maneno ya Dk. Mimi ambaye alimwambia kwamba msichana wake, Aisha ni lazima angekufa yakaanza kujirudi kichwani mwake, yalimuumiza mno na muda mwingi alikuwa akibishana na sauti hiyo na kusema kwamba mpenzi wake angepona na isingekuwa rahisi kufa.

Waliendelea kukaa hospitalini hapo mpaka saa sita mchana ambapo wakaruhusiwa kuingia ndani ya chumba kile na kumuona mgonjwa. Alipofika chumbani, moja kwa moja akakifuata kitanda kile na kuanza kumwangalia mpenzi wake kwa mara nyingine tena.

Machozi yalibubujika mashavuni mwake, kila alipomwangalia, aliisikia sauti moyoni mwake ikimwambia kwamba ni lazima mpenzi wake angefariki dunia, atake asitake lakini ukweli ulikuwa huo.

“Usiniache mpenzi....siwezi kuishi bila wewe,” alisema Razak kwa sauti ya chini masikioni mwa Aisha, kwa mbali msichana huyo akaonyesha tabasamu.

“Ninakupenda Aisha...wewe ni kila kitu katika maisha yangu, sijiwezi pasipo wewe, ili nikamilike, nahitaji uwe karibu yangu mpenzi,” aliendelea kusema Razak huku machozi yakimbubujika na kumdondokea Aisha usoni.

Wazazi wake waliokuwa pembeni walibaki wakimwangalia, walimfahamu kijana wao, tangu alipozaliwa mpaka siku hiyo hawakuwahi kumuona akiwa kwenye hali ya majonzi kama aliyokuwa nayo siku hiyo.

Wao wenyewe walisikia maumivu makali mioyoni mwao mpaka kuona wakilengwalengwa na machozi.

Huo ndiyo ukawa mwanzo wa mateso ya msichana Aisha, aliendelea kuteseka kitandani, hakuyafumbua macho yake, alibaki kimya, hakuwa akila kwa kutumia mdomo, mipira ilichomekwa puani mwake ambayo ilitumika kupitishia vyakula laini kabisa ambavyo havikuhitaji kutafunwa.
“Hivi baba, ni kweli Aisha atakufa?” alimuuliza baba yake swali lililokuwa gumu kujibika.

“Unasemaje?” aliuliza baba yake huku akitafuta jibu.
“Hivi kweli Aisha atakufa?”
“Hawezi kufa...tutapambana usiku na mchana apone....”

“Siwezi kuona mpenzi wangu akifa, ni lazima apone, nitatumia kila kitu nilichokuwa nacho mpaka apone,” alisema Razak kwa sauti yenye ushujaa.

Walitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba Aisha anapona na kuwa mzima kabisa, baba yake Razak alikuwa na fedha nyingi, alikuwa mzee tajiri ambaye kila siku aliogelea katika dimbwi la fedha tu.

Hakutaka kumuona kijana wake pekee akipata maumivu, alitamani kumuona akiwa na furaha kila siku hivyo kitu alichokifanya ni kutumia fedha zake kuhakikisha kwamba Aisha anakuwa mzima wa afya.

Hakutaka kuziamini hospitali za Tanzania, alichokifanya ni kuzungumza na familia yake na kuwaambia kile alichofikiria kukifanya ili Aisha apone na kuwa mzima japokuwa daktari aliwaambia kwamba ana terminal cancer.

Mpango uliokuwepo ulikuwa ni kumsafirisha na kumpeleka nchini India kwa ajili ya matibabu kwa kuamini kwamba kutokana na hospitali za huko kuwa na madaktari wengi wenye utaalamu wa hali ya juu basi tatizo la Aisha lingeweza kutibiwa na kupona kabisa japokuwa hapo hospitali waliambiwa kwamba ilikuwa ni lazima msichana huyo afe ndani miezi mitatu.
“Tukajaribu hukohuko, natumaini wataweza na Aisha atapona,” alisema baba yake.

Kilichofanyika ni kuwasiliana na daktari mkuu wa Hospitali ya Apollo ya nchini India na kumwambia kwamba kwa jinsi hali ilivyokuwa ilikuwa ni lazima mgonjwa wao asafirishwe na kupelekwa nchini India.

Hilo halikuwa tatizo, wakakubaliana na hivyo kilichokuwa kikisubiriwa ni mgonjwa huyo kupelekwa huko kwa ajili ya matibabu.

Razak akawasiliana na mapacha, Ahmed na Mohammed ambao walikuwa kama ndugu kwa Aisha, akawaambia ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea na hivyo kuwaambia wajiandae kwani safari ya kwenda nchini India haikuwa yake na familia yake bali hata hao pia walitakiwa kwenda huko.

Je nini kitaendelea...
 
Sehemu ya 31

Siku mbili zilizofuata, wote walikuwa ndani ya ndege na kuanza kuelekea nchini India. Muda wote Razak alikuwa karibu na kitanda cha Aisha, moyo wake uliendelea kumuuma na muda wote alikuwa akimwangalia Aisha huku akionekana kuumia zaidi juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwa mpenzi wake.

Wakati ndege imetua nchini Kenya, Aisha akayafumbua macho yake, mtu wa kwanza kabisa kumuona mbele yake alikuwa Razak. Hakujua ni mahali gani alipokuwa, akaanza kuangalia huku na kule.

“Mpenzi...kuna nini kilitokea?” aliuliza Aisha huku akionekana kutokuelewa, ndege ilizidi kukata mawingu.

“Tunakwenda India...”
“Kufanya nini?”
“Unakumbuka mara ya mwisho uliniambiaje?” aliuliza Razak, hata kwa kumwangalia tu, hakuwa sawa.
“Nakumbuka nilikwambia kwamba naumwa, baada ya hapo sijajua nini kilitokea,” alijibu Aisha.

Razak hakutaka kumwambia ukweli kwamba walikuwa wanakwenda nchini India kwa sababu alikuwa akisumbuliwa na kansa, alimwambia tu kwamba alikuwa na maumivu y kawaida ya tumbo na hivyo walikuwa wakimpeleka nchini India kwa ajili ya matatibabu.

Hilo likamtia hofu Aisha, haikuwezekana eti ugonjwa mdogo wa tumbo ndiyo umpeleke nchini India, alimwambia Razak amwambie ukweli lakini bado mwanaume huyo aliendelea kumwambia kwamba hali aliyokuwa nayo ilikuwa ya kawaida, ni maumivu ya tumbo ndiyo yaliyokuwa yakimsumbua.
“Kwa hiyo tatizo siyo kubwa?” aliuliza Aisha.

“Siyo kubwa, ni la kawaida sana.”
“Nashukuru mpenzi kwa kunijali....”
“Usijali...”
“Ila naomba niulize swali...”
“Uliza...”

“Mbona hauna furaha, macho mekundu, nini kinaendelea?” aliuliza Aisha.
Razak akashindwa kulijibu swali hilo, akabaki kimya na hapohapo machozi yakaanza kumbubujika mashavuni mwake.

Moyo wake uliumia sana, kila alipomwangalia Aisha, sauti ilimwambia kwamba hicho ndicho kilikuwa kipindi cha mwisho kumuona msichana huyo na baada ya muda fulani, angekufa na kamwe asingemuona tena.

Hakutaka hilo litokee, kiti alichokitaka ni kumuona msichana huyo akiwa mzima, wakiyafurahia maisha, wakioana na kuishi pamoja na kuwa na familia yao.

Kitendo cha kububujikwa machozi kilimtia hofu Aisha kwa kuhisi labda kuna kitu kibaya kilikuwa kikiendelea na hakuambiwa, hivyo akaanza kudadisi.
“Kuna nini mpenzi? Mbona unalia?” aliuliza Aisha.

“Unajua kwamba tunaoana miezi miwili ijayo?” aliuliza Razak.
“Nakumbuka mpenzi....hilo ndilo linalokufanya ulie?” aliuliza Aisha.
“Silii kwa maumivu, ninalia kwa furaha, siamini kama nitakuoa msichana wangu mrembo,” alisema Razak, akalilazimisha tabasamu usoni mwake.

Walichukua saa kadhaa ndipo ndege ile ikaanza kushuka katika Uwanja wa Kimataifa wa Chennai nchini India. Gari la wagonjwa kutoka katika Hospitali ya Apollo lilikuwa mahali hapo, moja kwa moja akachukuliwa na kuingizwa ndani na safari ya kuelekea hospitalini kuanza.

Huko, wakapokelewa na madaktari waliokuwa na utaalamu wa hali ya juu katika magonjwa ya kana, kitu cha kwanza walichokichukua ni ripoti ya mgonjwa waliyokuja nayo kutoka Tanzania, wakaichukua na kuelekea nayo ndani ya chumba kimoja na kuanza kuizungumzia.

Walikuwa madaktari saba ndani ya chumba hicho, wote hao walikuwa na uwezo mkubwa na ndiyo walikuwa kimbilio kwa wagonjwa mbalimbali wa kansa nchini India au hata nje ya nchi hiyo.

Walipoisoma vizuri ripoti ile, wakagundua kwamba mgonjwa waliyempokea alikuwa na terminal cancer na alikuwa na miezi mitatu kufariki hivyo hata kama wangefanya vipi, ingekuwa kazi kubwa sana kupona.

“She has terminal cancer,” (Ana saratani isiyotibika) alisema Dk. Santesh, mmoja wa madaktari bingwa wa upasuaji hapo hospitali.

“Is there anything we can do?” (Kuna lolote tunaweza kufanya?) aliuliza Dk. Maliki, daktari pekee mweusi hospitalini hapo.

“There is nothing we can do,” (Hakuna tunaloweza kufanya)
Hata kwao, pamoja na utaamu wao katika kuwatibu wagonjwa lakini tatizo alilokuwa nalo Aisha lilikuwa kubwa mno, si kwao tu, mahali popote duniani ambapo angepelekwa Aisha, asingeweza kupata tiba bali ukweli ungebaki palepale kwamba ni lazima afe.

Hilo liliwaumiza hata wao wenyewe, kila walipomkumbuka Aisha, alikuwa binti mdogo ambaye waliamini kwamba hakuwa amekamilisha baadhi ya ndoto zake alizokuwa amejiwekea, pamoja na kuwa na ndoto nyingi maishani mwake, lakini alibakiza kipindi cha miezi mitatu tu kuishi.

Hakukuwa na kilichoendelea zaidi ya kutoka ndani ya chumba kile. Nyuso zao tu zilionyesha kukata matumaini ya kumponyesha Aisha ambaye alikuwa hoi kitandani.

Walipowafikia Razak na wazazi wake pamoja na wale mapacha, Dk. Santesh akawaambia wamfuate ambapo wakaenda naye mpaka katika ofisi yake na kuanza kuzungumza nao.
“Tumejitahidi kuisoma ripoti hii,” alisema Dk. Santesh.

“Sawa...”
“Ripoti inaonyesha kwamba huyu Aisha ana kansa isiyotibika, mliambiwa hilo huko?” aliuliza daktari.

“Ndiyo tuliambiwa! Hatukutaka kushindwa na ndiyo maana umetuona hapa, tunaamini kwamba huku kwenu kila kitu kinawezekana,” alisema baba yake Razak.

“Kila kitu kinawezekana, hakuna kinachoshindikana ila nikiangalia katika tatizo hili, kuna kitu mlifanya,” alisema daktari.

“Kitu gani?” akaingilia Razak.
“Hamkumuwahisha mgonjwa hospitalini mpaka tatizo lake limekuwa kubwa,” alisema daktari huyo huku akijitahidi kuuma manenno.

“Naomba utuambie moja, itawezekana kupona?”
“Kupona?”
“Ndiyo! Tuambie ukweli tu...”
“Kwa kweli ni kazi kubwa. Sipendi kuwaambia hili lakini sina jinsi kwa kuwa sitaki niwapotezee muda....”
“Wewe tuambie tu..”

“Mgonjwa wenu ana saratani isiyopona, hatoweza kupona,” alisema daktari huyo.
Haikuwa mara ya kwanza kuambiwa hivyo, ni kama walikuwa wamekumbushwa tu kile walichoambiwa kule nchini Tanzania, Razak akaanza kulia tena, tumaini lake kubwa lilikuwa nchini India, aliamini kwamba kama wangefika huko basi kila kitu kingekuwa salama lakini kitu cha ajabu, hata huko pia daktari aliwaambia kwamba hilo halitowezekana, ilikuwa ni lazima Aisha afe.

Razak hakuweza kuvumilia, taarifa ile ikamfanya kuanza kutetemeka mwili, nguvu zikaanza kumuisha, ghafla, giza likatanda machoni mwake na kuanguka chini, kilichoendelea baada ya hapo, hakukifahamu.
*****
Sabrina akaanza kuzunguka huku na kule ndani ya ile klabu, macho yalikuwa makini kumwangalia kila mtu aliyekuwa ndani ya klabu ile, mtu aliyekuwa akimtafuta alikuwa mmoja tu, Sharifu ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua alikuwa wapi.

Haikuwa kazi ndogo, alizunguka sehemu zote, alimkosa, akaenda kusimama karibu na choo cha wanaume lakini napo hakuweza kumuona mwanaume huyo.

Hakukata tamaa, huo ulikuwa mwanzo tu
Usiku wa siku hiyo hakutaka kwenda katika klabu nyingine, alibaki ndani ya klabu hiyohiyo na hakufanikiwa kumuona mwanaume aliyekuwa akimtafuta.

Moyoni alihuzunika lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni mara ya kwanza kumtafuta mtu huyo hivyo aliona kwamba kama angeendelea kufanya hivyo hata kwenye klabu nyingine, angeweza kumuona na kukamilisha azma aliyojiwekea ya kumuua.

Akarudi chumbani kwake, alionekana kuwa mnyonge mno, mwili ulichoka, alichokifanya ni kujilaza kitandani mwake. Hapo, kumbukumbu za maisha yake ya nyuma zikaanza kujirudia kama mkanda wa filamu.

Alimkumbuka mwanaume Razak ambaye alimpenda kwa moyo wote lakini kutokana na kurubuniwa na Sharifu, akajikuta akiingia kwenye uhusiano naye na mwisho wa siku kumuharibia maisha yake.

Kitu kilichokuwa kikimuuma zaidi ni kwamba yule mwanaume aliyekuwa amemuacha ambaye kwa wakati huo alikuwa tayari kumrudia aliambia kwamba isingewezekana kumrudia kwa sababu alikuwa na msichana mwingine aliyekuwa akimpenda mno.

“Haiwezekani, atanikubali tu,” alijifariji pasipo kujua kwamba kwa kipindi hicho, mwanaume aliyekuwa akimzungumzia wala hakuwa na mapenzi naye, alimsahau, moyo wake ulikuwa kwa mwanamke mwingine ambaye kipindi hicho alikuwa akiteseka mno kitandani.
****

Je nini kitaendelea....
 
Sehemu ya 32

Razak akashtuka kutoka usingizini, kitu cha kwanza kabisa kufanya ni kuangalia chumba alichokuwemo. Hakikuwa chumba chake, akajiangalia mkononi mwake, alikuwa amechomwa sindano huku juu yake dripu ya maji ikining’inia na taratibu maji kuingia katika mishipa yake.

Picha ya sehemu iliyokuwa ikionekana, ilionyesha kwamba alikuwa hospitalini lakini hakujua ni kitu gani kilitokea mpaka kuwa mahali hapo. Huku akiwa anajiuliza, mara mlango wa chumba hicho ukafunguliwa na wazazi wake kuingia.

Hapo ndipo kumbukumbu za tukio lililopita likaanza kujirudia kichwani mwake kama mkanda wa filamu, alikumbuka jinsi alivyokuwa mbele ya daktari ambaye aliwapa taarifa iliyomshtua na kuanguka chini.

Machozi yakaanza kujikusanya machoni mwake na kuanza kulia tena. Wazazi wake na mapacha wale, Ahmed na wakamfuata na kuanza kumbembeleza lakini hakunyamaza, kitu pekee alichokihitaji ni kumuona mpenzi wake tu, Aisha.

“Ninataka kumuona Aisha...” aliwaambia.
“Subiri kwanza, utamuona, ngoja maji yote yaingie mwilini mwake,” alisema baba yake.

“Baba...ninampenda Aisha, sitaki kumpoteza, ninampenda Aisha wangu,” alisema Razak huku akijifuta machozi, kama kawaida moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno.

Hawakuacha kumbembeleza, walijua kwamba aliumia sana lakini hawakuwa na jinsi, hata wao wenyewe walitakiwa kukubaliana na ripoti ya madaktari iliyosema kwamba msichana Aisha alikuwa na kansa isiyopona na ndani ya miezi mitatu tu, angefariki dunia.
“Hivi kweli Aisha ataniacha?” aliuliza Razak huku akiwaangalia wote waliokuwa mahali hapo.

Swali alilouliza lilikuwa jepesi sana, ilikuwa ni kumwambia ndiyo lakini kwenye kutoa jibu kulikuwa na ugumu mkubwa hivyo kubaki wakimwangalia pasipo kumwambia kitu chochote kile.

“Baba...” aliita.
“Nipo hapa kijana wangu...”
“Ninataka nimuoe Aisha...ninataka kumuoa Aisha haraka iwezekanavyo...hata akifa...nataka afe akiwa mke wangu...” alisema Razak.

“Razak kijana wangu....”
“Baba...ninataka kumuoa Aisha...”
“Ninajua hilo, subiri apone...”
“Atapona lini?”
“Hatujajua, ila atapona...” alijibu baba yake.

Yeye mwenyewe alijua kwamba Aisha asingepona lakini hakuwa na jinsi, alijitahidi kumtia moyo kijana wake, asijisikie vibaya.Ingawa alimdanganya lakini bado aliujua ukweli kwamba msichana huyo asingeweza kupona, labda angepata nafuu leo na kesho lakini mwisho wa siku ilikuwa ni lazima afariki dunia.

Waliendelea kukaa nchini India kwa zaidi ya wiki mbili, hali ya Aisha ilikuwa ikiendelea vizuri, walivyoona kwamba kidogo alikuwa mepata nafuu, wakaondoka na kurudi nchini Tanzania.

Huko, Aisha hakutakiwa kutembea, hakutakiwa kabisa kuusumbua mwili wake, alichotakiwa kufanya ni kukaa kwenye kiti cha matairi na popote alipotaka kwenda, basi kiti hicho kilisukumwa na mtu au kukisukuma yeye mwenyewe.

Nchini Tanzania, maisha yaliendelea kama kawaida. Huo ulikuwa muda wa kumuonyeshea msichana huyo jinsi alivyokuwa akimpenda, Razak hakuambiwa wala kusikia kwa msichana huyo, alimpenda mno na hakukuwa na mtu aliyemthamini kama Aisha.

“Ninakupenda Aisha, ninakupenda sana,” alisema Razak.
“Ninakupenda pia....ila nina swali...” alisema Aisha.

“Swali gani tena?”
“Unanipendaje na wakati mimi ni mgonjwa, mbaya zaidi nakwenda kufa hivi karibuni?” aliuliza Aisha huku akionekana kuwa na huzuni mbele.

“Ugonjwa si tatizo, nitakupenda maisha yangu yote, nina penzi zito lisilokwisha kwako,” alisema Razak kwa sauti ya chini, uda wote machozi yalikuwa yakimlenga.

Mikakati ya kufunga ndoa bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Watu walipewa taarifa kwamba ni miezi miwili na nusu ndiyo ilikuwa imebaki kabla ya ile siku iliyokuwa ikisubiriwa na watru wote.

Kwa sababu Razak alikuwa na biashara zake nyingine, alichokifanya, muda mwingi ulikuwa ni kukaa na Aisha, hakutaka kuona mtu yeyote anakuwa karibu naye zaidi yake, yeye ndiye aliyekuwa akikisukuma kiti chake cha matairi, yeye ndiye aliyekuwa akimlisha na kumfanyia mambo mengine.

“Kila ninapomwangalia Aisha, nakuwa na matumaini kwamba hatokufa, anaonekana kama mzima wa afya tele, sidhani kama atakufa, nadhani hata vipimo vya madaktari wakati mwingine vinadanganya,” alisema Razak, alikuwa akiwaambia wazazi wake.

“Kweli?”
“Ndiyo! Namuona ana nguvu, Aisha hawezi kufa,” alisema Razak huku akionekana kuwa na matumaini kwa kila sentensi aliyoizungumza mahali hapo.
****

Asubuhi ilipofika, Sabrina akaamka kutoka kitandani, mwili wake ulikuwa na uchovu mwingi kupita kawaida. Akainuka kutoka kitandani na kwenda bafuni kuoga, huko ndipo mawazo yalipoanza kurudi tena kichwani mwake, akaanza kumfikiria Sharifu huku muda wote hasira za wazi zilionekana usoni mwake.

Hakumpenda Sharifu, alimchukia hata zaidi ya alivyokuwa akimchukia shetani, alipanga kumtafuta zaidi, alipanga kumuua popote pale ambapo angemuona ili moyo wake ufurahi, apate tumaini jipya na kuwaokoa wanawake wengine kwa kuamini kwamba kwa kile alichokuwa akikifanya Sharifu, kisingeishia kwake, kingeendelea hata kwa wanawake wengine.

Siku hiyo hakupanga kufanya kitu chochote zaidi ya kutembelea katika klabu mbalimbali kwa ajili ya kumtafuta Sharifu ambaye aliamini kwamba anajulikana kwa kiasi fulani kutokana na ubilionea wa baba yake.

Alipomaliza kila kitu, akaanza kuondoka na kuelekea katika klabu moja ya usiku iitwayo Los Angeles ambapo akawaona wanaume kadhaa ndani, waliovalia kibishoo na kuanza kuwauliza kuhusu mtu huyo.

“Kuna mtu namuulizia...” alisema Sabrina.
“Nani?”
“Anaitwa Sharifu, mtoto wa bilionea Ashrafu,” alisema Sabrina.
“Wala simfahamu...”
“Hata mimi simfahamu...” alisema mwanaume mwingine.

Hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka zake kuelekea katika klabu nyingine. Siku hiyo alikuwa mtu wa kuzunguka kwenye kila klabu na kuwauliza watu kuhusu mwanaume huyo.
Hakukuwa na mtu aliyemfahamu, yaani ilikuwa ni kama mtu aliyekuwa akimuulizia hakuwa akijulikana kabisa.

Moyo wake ulimuuma mno kwani kwa jinsi alivyofikiria ni kwamba ingekuwa kazi rahisi sana kumpata Sharifu lakini baada ya kuanza kumtafuta, mbele yake kukawa na ugumu mkubwa mno.

Ilipofika saa kumi na moja jioni, akarudi zake hotelini na kuingia chumbani kisha kulala kwani alikuwa amechoka mno. Alikuja kushtuka saa mbili usiku ambapo akachukua simu ya mezani na kupiga sehemu ya chakula na kuagiza chakula.

Ndani ya dakika aroobaini na tano, akasikia mlango ukigongwa.
“Uligiza chakula?” aliuliza mwanaume aliyemletea chakula.
“Ndiyo! Pita...nashukuru sana,” alisema Sabrina.

Mwanaume huyo aliyekuwa mzuri wa sura akapita na kukipeleka chakula mezani. Wakati anaondoka, Sabrina akashindwa kuvumilia, akamsimamisha kwa lengo la kuzungumza naye kidogo kwani uzuri wa sura aliokuwa nao ulimchanganya sana.
“Samahani...”

“Bila samahani dada...”
“Nimefika hapa jana, kuna mtu nimekuja kumtafuta lakini sifahamu pa kumpata,” alisema Sabrina huku akimwangalia mwanaume huyo usoni mwake kana kwamba alikuwa akimchunguza.

“Mtu gani?”
“Ni mtoto wa yule mzee bilionea, sijui unamjua!”
“Nani?”
“Anaitwa mzee Ashrafu...”
“Huyu mzee aliyemuoa Mwafrika?”
“Ndiye huyohuyo...”

“Mbona kazi rahisi sana, anaishi katika Mtaa wa Albadir uliokuwa pembezoni mwa jiji hili, kilometa kama kumi kutoka hapa, unataka nikuelekeze?” aliuliza mwanaume huyo.
“Hapana! Ninayemtafuta si yeye, ni mtoto wake.”

“Ana watoto watatu kwa mkewe wa hapa, wote wanawake, unamuulizia nani sasa hapo?” aliuliza mwanaume huyo.
“Ninayemuulizia ni yule aliyezaa na mwanamke wa Kiafrika,” alisema Sabrina.

“Hahah! Sasa kumbe unamuulizia yeye?”
“Ndiyo! Anaitwa Sharifu...”
“Ukimuulizia kwa jina hilo, utasumbuka sana, anajulikana zaidi kwa jina la Kashkashbir...”

“Ndiyo lina maana gani hilo?”
“Mpenda wanawake...ungemuulizia kwa jina hilo, popote hapa Dubai, ungempata tu...ila usinichukulie vibaya bwana, asije akawa mshikaji wako halafu ndiyo namuharibia..” alisema mwanaume yule.

“Usijali....nitamuona vipi na wapi?”
“Huyu bwana hapatikani kirahisi, ila pa kumpata zaidi nenda Mango Garden...”

“Ndiyo wapi huko?”
“Hiyo klabu mpya iliyojengwa na Mwafrika mmoja kutoka huko Afrika Mashariki, ukienda hapo usiku, lazima umkute,” alisema mwanaume huyo.

Kwa kuwa hakuwa akipafahamu, akaanza kuelekezwa huko, hakukuwa mbali na mahali alipokuwa amefikia hivyo ilivyofika usiku, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kwenda katika hiyo klabu huku akiwa na uhakika wa kumpata Sharifu aliyekuwa akimtafuta kwa udi na uvumba.

Alipofika katika klabu hiyo, akalipia na kisha kuingia ndani. Kulikuwa na idadi kubwa ya watu, macho yake hayakutulia, yalikuwa yakiangalia huku na kule na kuonyesha dhahiri kwamba alikuwa akimtafuta mtu fulani.

Ndani ya klabu ile, kulikuwa na idadi kubwa ya watu lakini wengi wao walikuwa Waafrika ambao walifika humo kwa wingi kwani hata nyimbo nyingi zilizokuwa zikipigwa humo zilikuwa ni zile kutoka kwa wanamuziki kutoka Afrika.

Aliendelea kutafuta zaidi na zaidi, hakuweza kumuona. Ilipofika majira ya saa nane usiku, akaanza kusikia watu wakishangilia kwa nguvu, hakujua kulikuwa na nini lakini aliposogea kule watu walipokuwa wakishangilia, macho yake yakatua kwa mtu ambaye alikuwa akimtafuta sana, ndiyo alikuwa ameingia, mtu huyo alikuwa Sharifu.

“Ndiye yeye...” alisema Sabrina, hasira zikaanza kurudi tena kichwani mwake, chuki ikamuingia na kuutawala moyo wake, hakukuwa na kitu kingine alichokifikiria zaidi ya kumuua Sharifu tu...hivyo akajipanga, iwe isiwe ilikuwa ni lazima amuue, ikiwezekana humohumo klabu.
****

Je nini kitaendelea...
 
Sehemu ya 33

Japokuwa alikuwa na hasira mno lakini hakuweza kufanya kile alichokusudia kukifanya ndani ya klabu hiyo zaidi ya kumwangalia Sharifu kwa hasira.

Idadi kubwa ya watu waliokuwemo humo ikamfanya kuogopa kwa kuona kwamba angeweza kukamatwa na kisha kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa mauaji hayo aliyotaka kuyafanya.

Watu waliendelea kupiga kelele za shangwe. Sharifu alikuwa mtu maarufu, aliyependwa na wanawake wengi kutokana na utoaji wake.

Hakuwa mchoyo, alimpa fedha msichana yeyote aliyezitaka na ndiyo kitu kilichomfanya kupapatikiwa na wasichana wengi na kujikuta akilala nao kadiri alivyotaka.

“Who loves me?” (Nani ananipenda?) aliuliza Sharifu kwa sauti ya juu huku akiwa ameiinua mikono yake.
“Me...me..me...me..” (Mimi...mimi...mimi...mimi) wasichana walisema huku wakinyoosha mikono juu.

Sabrina akazidi kushikwa na hasira, alimchukia sana Sharifu kwa sababu mwanaume huyo aliifuta ndoto ya kuolewa aliyokuwa nayo kwa mwanaume aliyempenda ambaye kwa kipindi hicho hakuwa pamoja naye.

Alishindwa kufanya kitu chochote kile zaidi ya kujifichaficha mpaka pale disko lilipokwisha na yeye kurudi hotelini.

Alitaka kujipanga, huo ulikuwa mwanzo tu, kitendo cha kumuona Sharifu kilimpa uhakika kwamba angefanikiwa katika suala zima la kufanya mauaji, hivyo akajipanga.

Siku hiyohiyo mchana akaamua kwenda kwenye klabu hiyo, alitaka kuonana na mwanaume yeyote na kumwambia kwamba alitaka kuonana na Sharifu ili amuue kwani asingeweza kuvumilia kabisa, alitaka kufanya mambo harakaharaka ili arudi zake Tanzania na kwenda kumuomba msamaha Sharifu, ikiwezekana asimuoe msichana wake na amuoe yeye.

Alipofika katika klabu hiyo, nje, macho yake yakatua kwa wanaume kadhaa waliokuwa wakifanya usafi.

Macho yao yalipotua kwa Sabrina, kila mmoja akabaki akimwangalia kwa mshangao, alikuwa msichana mrembo kweli ambaye ilikuwa ni vigumu kwa mwanaume rijali kuacha kumwangalia mara mbilimbili.

“Karibu...” alisema mwanaume mmoja, hata kabla hajajibiwa, akaamua kujitambulisha.

“Naitwa Qadir, sijui wewe unaitwa nanii mrembo,” alisema mwanaume huyo.
“Naitwa Latifa...”
“Waooo...u mzuri sana, karibu sana....”
“Asante.”

Wanaume wengine wakaacha kufanya usafi na kubaki wakimwangalia Sabrina kwa jinsi alivyopendeza, alivalia suruali yake ya jinzi, kitopu kilichoacha kitovu chake nje ambacho kilikuwa chachu kubwa kwa wanaume hao kumwangalia kwa matamanio.

“Nikusaidie nini Latifa?” aliuliza Qadir.
“Nataka kuonana na Kashkashbir...”

alisema Sabrina.
“Kashkashbir! Huwezi kumuona mchana huu...” alisema Qadir.
“Kwa nini?”
“Klabu mpaka usiku.”
“Na yeye anaishi wapi?”

Kipindi hicho kilikuwa cha maswali tu, Sabrina alitaka kufahamu mengi kuhusu Sharifu na kwa kuwa mwanaume huyo alichanganyikiwa kutokana na urembo aliokuwa nao msichana huyo, akajikuta akijibu kila swali alilokuwa akiulizwa hivyo msichana huyo kuondoka lakini akimwambia Qadir kwamba kulikuwa na mwanamke aliyekuwa akimtafuta.

Mpaka anaondoka mahali hapo, hakukuwa na mtu aliyejua kama msichana huyo alikuwa na kisasi kizito moyoni mwake, wao walimuona kama msichana mrembo, mwenye tabasamu pana ambaye hakuwa na hasira zozote zile moyoni mwake.

Hotelini hakutulia, alibaki akimfikiria Sharifu huku wakati mwingine akirusha mikono yake huku na kule tena kwa hasira kali.

Kwa mchana huo, hakupumzika ipasavyo, ilipofika saa mbili usiku tayari alikuwa amekwishafika katika klabu ile tayari kwa kufanya kile alichokikusudia kukifanya usiku huo.

Watu wakaanza kuingia ndani ya klabu hiyo, siku hiyo, mapema sana ilionekana dalili kwamba siku hiyo watu wangejaa sana kutokana na kuwa na msanii kutoka nchini Kenya ambaye siku hiyo angetumbiza ndani ya ukumbi huo.

Yeye hakutaka kujali kuhusu muziki, kilichokuwa kimemleta mahali pale kilikuwa kitu kimoja tu, kumuua Sharifu na kisha kuondoka zake kuelekea hotelini ambapo kesho yake au ndani ya siku kadhaa, angepanda ndege na kurudi nchini Tanzania.

Kila mtu alikuwa bize na mambo yake au mtu wake, wapo waliokuwa na wasichana wao ambao kipindi kirefu waliwashikilia viuno, wapo waliokuwa wakicheza peke yao na wapo wengine ambao hawakuwa hata na mpango wa kucheza muziki, muda wote walikuwa kwenye makochi wametulia.

“Mambo vipi dada?” alisalimia jamaa mmoja kwa lugha ya Kiswahili kabisa kwani ndani ya klabu hiyo, Kiswahili ilikuwa lugha kubwa ya mawasiliano.
“Safi...”

“Mbona umekaa hapa kiunyonge hivyo?” aliuliza jamaa huyo.

“Nimeamua tu...”
“Jamani....naomba kampani yako nikacheze nawe...” alisema mwanaume huyo.
“Mimi?”
“Ndiyo!”
“Hapana! Kichwa kinauma...”

“Pole sana mrembo...”
Mwanaume huyo hakutaka kujali sana japokuwa kila alipomwangalia Sabrina, moyo wake ulisikitika mno kwa kumkosa. Sabrina aliendelea kukaa pale kochini mpaka shoo ya huyo msanii ilipoanza rasmi.

Hakutaka kuinuka, ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe lakini yeye hakutaka kujali zaidi ya kutulia pale kochini na macho yake yakiwaangalia wanawake wenzake ambao walikuwa bize kuvuta shisha.

Ilipofika saa 7:46, watu wakaanza kupiga kelele za shangwe Sabrina akajua kilichokuwa kikiendelea, mwanaume asiyempenda, aliyekuwa akimchukia alikuwa akiingia ndani ya klabu hiyo.

Harakaharaka akasimama na kuanza kuangalia, hakukosea, alimuona Sharifu akiingia kwa mwendo wa mapozi, maringo huku akiwapungia mikono watu waliokuwa ndani ya ukumbi huo.

“Nitamuua hata kwa kumchoma kisu...” alisema Sabrina huku akiangalia kwenye mkoba wake kama alikuwa na kisu, kilikuwepo.

Wakati Sharifu akiendelea kuwapungia watu mikono, Sabrina akainuka kutoka katika kochi alilokuwepo na kuelekea katika sehemu iliyokuwa na mlango wa kuelekea sehemu iliyokuwa na vyoo, alipofika karibu na mlango ule, alibaki amesimama huku akiangalia huku na kule.
“Dada! Huwa haturuhusu kusimama hapo,” alisema mwanaume mmoja aliyekuwa na mwili wenye misuli.

“Najisikia vibaya kaka yangu.”
“Na ndiyo maana tumewawekea makochi kwa wale watakaochoka, naomba uende kule,” alisema mwanaume huyo huku akionekana kumaanisha alichokuwa akikizungumza.

Sabrina hakutaka kujali sana, aliona kulikuwa na ugumu mkubwa wa kufanya kile alichotaka kukifanya hivyo njia rahisi ambayo ilikuja moja kwa moja kichwani kwake ni kuelekea nje ya klabu ile ambapo huko angemsubiri mpaka pale atakapotoka na kisha kumuwahi na kumchoma kisu kama alivyopanga.

Hakutaka kupoteza muda, harakaharaka akaanza kuelekea nje huku akipishana na Sharifu ambaye hakumgundua kutokana na taa za mchanganyiko ziizokuwa zikiwaka na kuzima mara kwa mara.

Akatoka nje, kama kulivyokuwa ndani, hata nje kulikuwa na idadi kubwa ya watu ambao wengi wao walionekana kuwa bize na mambo yao.

Sabrina hakutaka kusubiri sana, alichokifanya ni kuelekea sehemu ya kupaki magari na kutulia katika kiti kimoja kilichokuwa pembeni, kijasho chembamba kikaanza kumtoka, kila dakika aliangalia saa yake, mahali pale, alikuwa akimsubiri Sharifu atoke ili akamalishe kile alichotaka kukifanya.

“Saa 10: 34 mmh!” alisema Sabrina huku akiendelea kusubiri kwani alikwishakaa nje kwa saa mbili, bado Sharifu hakutokea, katika sehemu ya maegesho, ni magari manne tu likiwepo gari lake ndiyo yalikuwa yamebaki, mengine thelathini yaliyokuwa yamepakiwa hapo yalikwishaondoka.

Sabrina akaanza kuingia na wasiwasi, ukimya wa Sharifu kutoka ndani ya klabu ile ukamtia wasiwasi na kuhisi kwamba inawezekana mwanaume huyo alikwishamshtukia kwamba alikuwepo nje akimsubiri kama ilivyokuwa nchini Tanzania.

Kwa harakaharaka akaangalia huku na kule kuona kama kulikuwa na kamera za CCTV, hazikuwepo, kilichomchanganya, kwa nini alichukua muda mrefu namna hiyo.
“Au aliondoka?” alijiuliza.

Huku akiwa na maswali mengi kichwani mwake, mara mlango ukafunguliwa, mwanamke mmoja akatoka, shati lake lilijaa damu, alionekana kuchanganyikiwa, hapohapo akaanza umfuata Sabrina pale alipokuwa amekaa, kwa jinsi alivyoonekana, Sabrina akaanza kuogopa, akaona kwamba humo ndani alipotoka msichana yule, hakukuwa na amani, je kulikuwa na kitu gani kilichotokea? Kila alipojiuliza, akakosa jibu.

Msichana yule akamfikia, alionekana kama mtu aliyejeruhiwa kutokana na nguo zake kutapakaa damu.
*****

Je nini kitaendelea....
 
Sehemu ya 34

Si kila mtu alikuwa akimpenda Sharifu, kulikuwa na kundi kubwa la wanaume ambao kila siku walimuombea mabaya kijana huyo kutokana na aina ya maisha aliyokuwa akiishi.

Walimchukia mno kwani kwa kutumia fedha za baba yake aliwafanya kukosa amani na kuwaumiza mioyo yao hasa pale alipoanza kuwachukua wanawake nao na kulala nao, hakuishia hapo, kilichowakasirisha wengine ni kitendo chake cha kuwatambia kwamba alikuwa mtaalamu wa wanawake hivyo asingeweza kukataliwa.

Hilo likawafanya vijana waliochukuliwa wanwake wao kujipanga tayari kwa kumfanyia kitu kibaya. Walikuwa na ratiba yake, walijua fika siku ambazo alipendelea kwenda kwenye klabu hiyo ya usiku hivyo nao wakajiandaa vilivyo.

Wakati ameingia na kusalimiana na watu wengine huku wanawake wakishangilia, wanaume hao waliojigawa walijipanga katika kila kona ndani ya klabu hiyo na mwisho wa siku watu walipoanza kuondoka, wakaona hiyo ndiyo nafasi.

Sharifu hakujua, kila aliyemwangalia, alimtolea tabasamu na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya lakini nyuma ya pazia, hata wale wanaume waliokuwa wakimuonyeshea tabasamu, mioyoni mwao walikuwa na visasi vya damu.
“Kwa hiyo?” aliuliza mwanaume mmoja.

“Tukamuueni...”
“Hapahapa klabu?”
“Ndiyo! Tukisubiri mpaka nje, tutamkosa kama jana,” alisema kijana mmoja. Walichopanga kilikuwa ni kufanya mauaji ya aina yake, walijua kwamba humo ndani kulikuwa na kamere za CCTV hivyo hawakutaka kugundulika kabisa.

Walichofanya ni kumtuma kijana mwenzao aende sehemu ilipokuwa na swichi kubwa tayari kwa kuizima kipindi ambacho mwenzao alikuwa akipiga hatua kumfuata Sharifu, kweli suala hilo likafanyika.

Huo ndiyo mpango walioupanga, ilikuwa ni lazima Sharifu achomwe kisu siku hiyo. Ilipofika saa 10:32 alfajiri, mwanaume mmoja akainuka kutoka kwenye kochi alilokuwa amekaa na kuanza kumfuata Sharifu kule alipokuwa amesimama na wasichana kadhaa tena huku uso wa mwanaume huyo ukiwa na tabasamu pana kana kwamba alikuwa rafiki yake.


Alipobakiza hatua kama kumi kumfikia, hapohapo, tena ghafla kabisa taa zote za klabu zikazima, watu waliokuwa wakicheza muziki, wakatulia, kila mmoja akashangaa kwani haikuwa kawaida kwa klabu kama hiyo kukatika umeme.

Giza kubwa lilikuwa limetawala ndani ya klabu hiyo, kila mmoja alisimama alipokuwa na baada ya sekunde thelathini tu, umeme ukarudi na taa kuwaka.

Kilichosikia baada ya taa za jlabu kuwaka ni kelele za wasichana waliosimama karibu na Sharifu, hawakuamini macho yao mara baada ya kuona mwanaume waliyekuwa wakimpapatikia alikuwa chini huku akikukuruka na damu zikimtoka tumboni.

Watu wengine waliposikia kelele hizo, wakasogea kule waliposimama wasichana wale, walichokiona, hata nao hawakuamini kama Sharifu alikuwa amechomwa kisu, msichana ambaye siku hiyo ndiye aliyekuwa kwenye mipango ya kulala naye, akamuinamia na kujaribu kuyaokoa maisha yake lakini haikuwezekana.

“Sharifuuuu...Sharifuuu...” aliita msichana huyo lakini bado Sharifu alikuwa kwenye hali mbaya.

Watu wakashika vichwa vyao kwa mshtuko, hawakuamini kile walichokiona kwamba mwanaume mwenye pesa aliyeweza kuwanunulia watu pombe kali, alikuwa chini huku damu zikimtoka.

Kila mmoja akachanganyikiwa, hawakujua ni nani alikuwa amehusika ila walichokijua ni kwamba hata kitendo cha taa kuzimwa ulikuwa mpango wa watu fulani.

Mabaunsa wa klabu wakafika mahali hapo, wao wenyewe walipigwa na mshangao, hawakuamini kile walichokiona mbele yao, waliinama kwa lengo la kumsaidia huku yule msichana ambaye ndiye alikuwa na zamu ya kulala na Sharifu akikimbia kuelekea nje huku akionekana kuchanganyikiwa.

Mabaunsa wale wale wakamchukua Sharifu na kutoka naye ndani ya klabu na kuelekea katika sehemu iliyokuwa na magari katika eneo la kupakia magari na kisha kumuingiza kwenye gari moja kuelekea hospitalini.

Sabrina aliyekuwa pale nje alishindwa kuelewa ni kitu gani kilitokea, alibaki akimwangalia msichana yule, alikuwa akilia huku akizungumza mambo ambayo hakuyaelewa kabisa, hata mlango ule ulipofunguliwa, hakujua kama mtu aliyebebwa alikuwa Sharifu.
“Why are you crying?” (Unalia nini?) alimuuliza msichana huyo.

“They have killed him!” (Wamemuua!)
“Who is that?” (Nani huyo?)
“Sharifu..they have stabbed him!” (Wamemchoma kisu) alijibu msichana yule.

Sabrina hakuamini kile alichokisikia, hapohapo akaanza kulifuata lile gari lililombeba Sharifu na kutaka kuhakikisha kama kweli mtu huyo alikuwa amechomwa kisu kweli au la.

Watu walikuwa wengi nje ya klabu ile tena huku kila mmoja akionekana kushangaa ni kwa namna gani tukio la kikatili kama lile liliweza kutokea tena ndani ya klabu, sehemu iliyokuwa na idadi kubwa ya watu.

Alipofika huko na kuchungulia ndani ya gari, aliweza kumuona Sharifu akiwa ametulia, hakutingishika na dalilii zote zilionyesha kwamba alikwishafariki dunia.

Katika hali ambayo hata yeye mwenyewe aliishangaa, akajikuta akianza kumuonea huruma mwanaume huyo kitu ambacho hakuhisi hapo kabla kama kingeweza kutokea kutokana na chuki kali aliyokuwa nayo juu ya Sharifu.

Gari hilo likaondolewa mahali hapo kuelekea katika hospitali ya Al Zahra ambayo haikuwa mbali kutoka katika klabu hiyo.

Sabrina hakutaka kusubiri mahali hapo, naye akakodi teksi zilizokuwa zimeegeshwa pembeni ya klabu hiyo na kumwambia dereva alifuatilie gari lile lililombeba Sharifu kuelekea hospitali.

Moyo wake uligawanyika sehemu mbili, upande wa kwanza ulikuwa na furaha juu ya kile kilichokuwa kimetokea lakini upande mwingine ulikuwa na majonzi tele, ubinadamu ukamuingia na kusikitika mno kutokana na Sharifu kupata tatizo kubwa ambalo pia ulimwambia kwamba mwanaume huyo alikuwa amekufa kutokana na ile picha aliyoiona ndani ya gari.

Wakaingia hospitali pamoja, hata kabla gari halijasimama, harakaharaka Sabrina akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea kule mwili wa Sharifu uliposhushwa na kulazwa juu ya machela.

“He is already dead...” (Tayari amekwishakufa..) alisema mwanaume mmoja miongoni mwa watu walioubeba mwili wa Sharifu kufika hapo hospitalini.

Maneno hayo yalimchoma moyo wake, hakuamini kama kweli mtu aliyepanga kumuua tayari alikwishauliwa na mtu mwingine. Alibaki akiwa amesimama na hata nguvu za kuingia ndani ya hospitali ile hakuwa nayo kabisa.

Hakutaka kuuliza, hakutaka kusikia kile kilichoendelea ndani ya hospitali ile, alichokifanya, teksi ileile iliyomchukua imrudishe hotelini huku njia nzima akiwa analia kama mtoto.

“Ninarudi Tanzania, ni bora nikamuombe msamaha Razak ili anioe, sina jinsi, hata akitaka nipige magoti, nitapiga tu,” alijisemea Sabrina huku akitiririkwa na machozi, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu lakini kitu alichokuwa akikihitaji kwa wakati huo ni kumuomba msamaha Razak tu ili aweze kulirudisha penzi na kuwa kama zamani.

Baada ya muda, teksi ikafika hotelini hapo ambapo moja kwa moja akaelekea chumbani kwake, akaoga huku kituo cha televisheni cha taifa kikianza kutoa taarifa juu ya kifo cha Sharifu.

Hakutaka kujali sana, akalala na asubuhi alipoamka, akafanya mambo yake na siku mbili baadaye akaanza safari ya kurudi Tanzania ikaanza huku moyo wake ukiwa na hamu ya kuonana na Razak, amuombe msamaha na hatimaye awe wake wa kufa na kuzikana.
****
Hakukuwa na kitu kilichofanyika, bado mpenzi wake alikuwa kwenye hali mbaya, kila alipomwangalia, alijua kabisa kwamba msichana huyo alikuwa akienda kufa ila hakuwa na jinsi, alibaki akilia mno lakini hakukuwa na mabadiliko kabisa.

Hakutaka kumwambia Aisha, kwake ilikuwa siri kubwa na nzito ambayo alijiapiza kwamba ingekuwa siri zaidi moyoni mwake na kamwe asingeweza kumwambia mpenzi wake huyo.

Kwa kumwangalia tu, Razak hakuonekana kuwa na furaha hata mara moja. Moyo wake ulinyong’onyea na katika kipindi chote alikosa furaha kabisa.

Baba yake hakutaka kumuona akiwa kwenye hali ile kwa kuona kwamba ingekuwa rahisi sana kwa Aisha kugundua kile kilichokuwa kikiendelea, hivyo akamwambia abadilike.
“Utamfanya kugundua...” alisema baba yake.

“Kivipi?”
“Unakuwa na uso wenye majonzi, atajua kinachoendelea....”
“Kwa hiyo nifanye nini?”

“Tabasamu...”
“Nitabasamu bila kuwa na furaha? Nitatabasamu vipi na wakati yupo kwenye hali mbaya namna hiyo? Siwezi kutabasamu...” alisema Razak.

“Hiyo ndiiyo njia rahisi ya kumfanya kuwa na furaha, utabaki hivyo mpaka lini?” aliuliza baba yake.

Huo ndiyo ukweli, kitendo cha kumfanya kutabasamu kingemuweka mpenzi wake katika hali nzuri, hakutakiwa kuonekana kuwa na huzuni au majonzi yoyote yale, yeye kama mwanaume, alitakiwa kuvumilia, kumuonyeshea mpenzi wake kwamba moyoni mwake alikuwa na furaha tele.

Ndivyo alivyofanya, japokuwa mara kwa mara Aisha alionekana kuwa na huzuni mno lakini kitendo cha kumuona mpenzi wake akitabasamu kila wakati kikampa furaha kubwa, hakuamini kama kweli pamoja na matatizo yote aliyokuwa akipitia lakini mpenzi wake aliamua kumpa tabasamu kwa kuwa ndicho kitu alichokiamini kwamba kingempa furaha kipindi chote.

Wakati mwingine hawakuwa wakikaa nyumbani tu, waliondoka na kuelekea ufukweni kutembea huku Aisha akiendelea kuwa kwenye kile kiti chake cha mataili. Huko, kila mtu alibaki akimwangalia Aisha, alikuwa msichana mrembo mno ambaye aliwafanya wanaume wote kumuonea huruma kutokana na maisha aliyokuwa akiishi.

Ahmed na Mohammedi walikuwa pamoja naye kila kona, walimchukulia kama ndugu yao, walipata maisha mazuri kwa sababu yake na hata katika kipindi cha maisha yenye mateos aliyokuwa akiishi Aisha bado waliendelea kuwa naye.

Siku zikakatika, mipango ya harusi haikusimama, iliendelea kusonga mbele kama kawaida. Ndugu wa Razak waliokuwa wakiishi Uarabuni wakaanza kujivuta nchini Tanzania tayari kwa kuhudhuria harusi hiyo ambayo kwao ilioenekana kuwa ya maana sana.

Ndugu wengine ambao mioyo yao ilijawa na ubaguaji walipomuona Aisha, hawakutaka kumbagua kwani alikuwa msichana mrembo hata zaidi ya walivyokuwa wao.
“Ni msichana mrembo sana, ulimtoa wapi?” aliuliza ndugu yake mmoja.

“Nilimtoa mbali sana...”
“Wapi?”
“Wewe jua mbali sana...”
“Nataka kujua ili nione kama ana ndugu yake na mimi niweze kukaa na nioe sasa...”

“Lakini wewe si una mke?”
“Ndiyo! Ila sheria si wake wanne! Au umesahau?”
Kila aliyemuona Aisha alishindwa kuvumilia, kumuona msichana huyo na kubaki kimya pasipo kuuzungumzia uzuri wake kilionekana kuwa kitu kigumu sana hasa kwa wanaume na baadhi ya wanawake.

“Razak mpenzi, naomba nikuulize kitu...” alisema Aisha huku akimwangalia mpenzi wake machoni.

“Kitu gani?” aliuliza Razak huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Hivi ninaumwa nini?” aliuliza Aisha.
“Nani? Wewe?”
“Ndiyo! Naomba uniambie ukweli na usinifiche...”

Kabla Razak hajajibu swali hilo, akabaki kimya, alimwangalia Aisha machoni mwake, siku hiyo alionekana kumaanisha kwa kile alichokuwa amekiuliza, alitaka kufahamu ukweli, hakuambiwa kama anaumwa kansa ya utumbo mpaka (colon), alijikuta akiwekwa kwenye kiti, tatizo lake hakulifahamu kabisa.

Alibaki kumwangalia mpenzi wake, kwa muonekano wake tu alionekana kufahamu kitu lakini hakutaka kukiweka wazi. Razak alibaki kwenye hali hiyo kwa sekunde kadhaa kisha kuachia tabasamu pana.

“Kwa nini umeuliza hivyo?” aliuliza Razak huku tabasamu likiwa usoni mwake.
“Ninataka kufahamu tu, ninaumwa nini?” aliuliza Aisha.

“Unasumbuliwa na miguu...” alijibu Razak huku hata macho yake tu yalionyesha kwamba hakusema ukweli.

“Nikuulize kitu?” aliuliza Aisha.
“Uliza.”
“Unanipenda?”
“Nakupenda sana tu.”
“Mbona hutaki kuniambiia ukwelii?”

“Ukweli gani?”
“Juu ya ugonjwa ninaoumwa...”
“Hauumwi ugonjwa wowote mbaya mpenzi, si unajiona upo kwenye kiti cha mataili...”

“Ndiyo! Ninaumwa nini?”
“Miguu tu...”
Moyo wake ulimuuma mno, hakupenda kabisa kumdanganya mpenzi wake lakini katika hali aliyokutana nayo, hakuwa na jinsi, alitakiwa kufanya hivyo kwani vinginevyo alihisi angekuwa kwenye hali mbaya.

Aisha hakutaka kuridhika, kila alipojiangalia, alijua kwamba kulikuwa na ki8tu kilichokuwa kikiendelea katika mwili wake lakini mpenzi wake huyo hakutaka kumwambia ukweli.

Baada ya kujibu maswali hayo, Razak hakutaka kubaki chumbani hapo, akatoka na kuelekea sebuleni, huko, alibaki akilia mno, aliumia moyoni mwake lakini hakuwa na jinsi, kila kitu alichokuwa akikipitia mpenzi wake kilionekana kuwa kigumu na kilichojaa maumivu makali.

Baada ya wiki moja, Aisha akamuita Razak kwa ajili ya kuzungumza naye. Razak akaogopa kwani alijua kile ambacho Aisha alitaka kwenda kuumwambia, alijua kwamba mtu huyo alitaka kumuuliza tena swali lilelile kwamba alikuwa akiumwa nini.

Alipofika humo ndani, wakakaa kama kawaida yao, wakaanza kuzungumza mambo mengine kabisa, baada ya mazungumzo hayo, Aisha akajiweka vizuri tayari kwa kumwambia kile alichotaka kumwambia.

“Kuna nini? Mbona unanitia presha?” aliuliza Razak.
“Si kitu kibaya, ni kizuri tu...” alisema Aisha.

“Kipi?”
“Nina mimba yako...” alisema Aisha huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana. Badala ya Razak kufurahi, hapohapo akaanza kutokwa na machozi, akashindwa kuvumilia kuwa ndani ya chumba hicho, akatoka, huko sebuleni, akabaki akilia kwa sauti kubwa.

Aisha hakuelewa ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea, alichokifanya ni kuzungusha magurudumu ya kiti chake mpaka sebuleni, alipofika huko akajaribu kumuuliza Razak tatizo lilikuwa nini lakini kitu kilichomshangaza, mwanaume huyo hakujibu kitu zaidi ya kuendelea kulia kama mtoto.

Alichojuta moyoni ni kwamba alimpa mimba mpenzi wake ambaye mpaka kipindi hicho alikuwa na siku zisizozidi sabini, angekufa, kwa maana hiyo hata hicho kiumbe tumboni, kingekufa pia.
****

Je nini kitaendelea.....
 
Sehemu ya 16

Huo ulikuwa mtihani mkubwa kwake, hakuamini mtu kama yeye kupendwa na mwanaume mwenye fedha kama Razak, hakutaka kuamini, moyoni, alihisi kama alikuwa akitaniwa, na Razak hakumaanisha alichomwambia.

“Unanipenda mimi?” aliuliza Aisha huku akionekana kushtuka.
“Ndiyo!”

“Umenipendea nini?”
“Aisha...kila kitu ulichokuwa nacho, nimekipenda, nimependa jinsi ulivyo, kila kitu kwa pamoja, nimekupenda,” alisema Razak.

Razak akamsogelea Aisha pale alipokuwa na kisha kuubusu mdomo wake. Mwili mzima wa Aisha ulikuwa ukitetemeka kama mtu aliyesikia baridi kali.

Wakati yote hayo yakitokea, Ahmed na Mohammed walikuwa pembezoni mwa sebule huku wakichungulia kisiri, kila kitu kilichokuwa kikendelea, walikuwa wakikiona tu.

Hapo ndipo walipojua sababu ya Razak kumtafuta Aisha kwa udi na uvumba, mpaka kufikia hatua hiyo, tayari wakajua kwamba hata wao maisha yao yangekuwa mazuri kwani kwa Aisha, wao walisimama kama ndugu zao.

“Kumbe anampenda!” alisema Ahmad kwa mshangao.

“Nilijua tu, nililigundua hilo mapema kabisa,” alisema Mohammed.

Maisha yake yalikuwa ya kimasikini, hakuwahi kupata maisha mazuri tangu alipozaliwa. Mama yake alikufa miaka mingi iliyopita, alizaliwa huku mama yake akiwa mitaani kwa hiyo hata kipindi hicho bado aliendelea kuishi hukohuko mitaani.

Hakuwa na ndugu, kama alikuwa nao hakuwa akiwafahamu kabisa. Watu wa karibu aliokuwa amezoeana nao ambao kwake walikuwa kama ndugu ni watoto wa mitaani na wale mapacha wawili ambao kwake walikuwa kila kitu.

Alimkubali Razak, hata kama mwanaume huyo alikuwa na fedha lakini naye mwenyewe moyo wake ulianza kumuingiza mwanaume huyo ila hakutaka kumwambia kwani alijua fika kwamba kuna siku tu mwanaume huyo angetamka maneno hayo.

Alipokubaliwa, Razak hakuamini, alichokifanya ni kumnyanyua Sabrina kisha kumkumbatia kwa mahaba mazito, joto la miili yao, likakutana na kujisikia tofauti, kilichotokea baada ya hapo ni kuufungua ukurasa mpya wa mapenzi.
*****

Kelele zilikuwa zikisikika kutoka ndani ya jumba moja la kifahari, watu watatu walikuwa wakibishana, mmoja alikuwa mwanaume mzee, mwingine mwanamke mzee lakini huyo wa tatu alikuwa msichana mwenye umri usiozidi miaka ishirini, huyu alikuwa Sabrina.

Mara baada ya kuanza uhusiano mpya na Sharifu, Sabrina aliamua kuwaita wazazi wake na kuwaeleza kweli kwamba alikuwa amepata mwanaume mpya na si Razak ambaye alikuwa naye tangu alipokuwa mtoto mdogo.

Wazazi wake hawakuamini kile walichokisikia, walimkubali Razak, kwao, mwanaume huyo alionekana kuwa sahihi kuwa mkwe wao, hawakutaka kuona binti yao akiwa na mwanaume mwingine tofauti na Razak.

Walitoa baraka zote kama wazazi kwa kumwambia Sabrina kwamba waliridhia kuona mwanaume huyo akimuoa binti yao, hivyo wao kama wazazi kitu pekee walichokuwa wakikisubiria kilikuwa ndoa tu.

Baada ya kupita muda fulani, leo binti yao aliwaletea habari nyingine, mpya ambayo iliwasisimua sana baada ya kuwaambia kwamba alikuwa amemuacha Razak kwa sababu alipata mwanaume mwingine mwenye mchanganyiko wa rangi aitwaye Sharifu.

Wazazi wakachanganyikiwa, hawakuamini kile alichokisikia, walimwangalia binti yao, walihisi kama alichanganyikiwa, hawakuamini kabisa kile walichoambiwa.

Walimfahamu Razak, hakuwa mwanaume machepele, alikuwa mwanaume mpole aliyejitoa kwa kila kitu, wao kama wazazi walimpenda sana, sasa kitendo cha binti yao kuwaambia kwamba aliachana na Razak kwa ajili ya mwanaume mwingine, iliwachanganya.

“Haiwezekani Sabrina....” alisema baba yake kwa sauti kubwa.

“Nimeamua baba, mtake, msitake ni lazima Sharifu anioe...” alisema Sabrina.
“Mimi si ndiye mzazi?”
“Na mimi si ndiye mtoto?”

“Utaona, hakuna ndoa hapa, huwezi kuolewa na mwanaume mchafu hata kama ana fedha kiasi gani,” alisema baba yake kwa sauti kubwa, alionekana kukasirika mpaka mishipa ya shingo kumtoka.

Je nini kitaendelea...
Hatareee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom