Sehemu ya 48
Kama kawaida Gibson hakutakiwa kuwa mkweli kwa lolote lile, ilikuwa ni lazima kumfanya msichana huyo ajue alikuwa hana kosa, ajifanye kabisa alikuwa mtu mwema kuliko wanaume wote katika dunia hii.
“Ila unaposema sisi wanaume wote tupo hivi huwa unakosea sana,” alisema Alex.
“Kwa sababu gani?”
“Niliwahi kuwa na uhusiano na msichana mmoja aitwaye Upendo. Nilimpenda sana, nilimpa kila kitu alichokuwa akikihitaji katika maisha yake. Huwa ninapokuwa na msichana ninapenda mno kujitoa kwa kila hali ili awe na furaha,” alisema, kama kawaida alikuwa akitunga kauongo fulani kazuri sana.
“Ikawaje?”
“Yaani sijui nisemeje. Baada ya siku kadhaa, nikawa nimeamua kumnunulia zawadi fulani hivi, nikaenda kumpelekea nyumbani kwake. Akaipokea, nikamwambia ninataka tutoke kidogo kwa ajili ya dinner, akakubali hivyo akaenda kuoga,” alisema huku Shadya akisikiliza kwa makini kabisa.
“Ikawaje?”
“Sasa alipokuwa bafuni nikasikia simu yake imelia kama kuna ujumbe, si unajua hizi touch, meseji ikapop up pale juu, nilichokisoma, niliumia sana,” alisema Gibson, kwanza akanyamaza, akaangalia chini halafu akatingisha kichwa chake kuonyesha kuumizwa.
“Ikawaje?”
“Hawa wanawake hawa! Dah!”
“Ikawaje?”
“Tuishie hapo!”
“Hapana! Hebu niambie! Ujumbe ulisemaje?” aliuliza Shadya.
Kitu muhimu alichokifanya kijana huyo ni kuuchukua utulivu wa Shadya, alihitaji kumuweka katika hali ambayo ingemfanya kuwa makini sana kumfutilia kwa kile alichokuwa akikizungumza na kukiweka akilini mwake.
“Kuna jamaa alikuwa akidate nae, alimtumia meseji kumsifia jinsi walivyofanya ngono usiku uliopita. Unajua nilisikia maumivu ambayo sikuwahi kuyasikia,” alijibu Alex.
“Jamani poleeee...”
“Nashukuru! Ila ndiyo maisha! Kuumizwa ni kawaida, huwezi kuwa kwenye furaha kila siku na ndiyo maana uliponiambia kuhusu ishu yako, ilinigusa sana, imeniumiza mno na ndiyo maana nilihitaji namba ya jamaa ili nimtukane,” alisema, akaunganisha matukio.
Mpaka kufikia hapo tayari Shadya akahisi huyo alikuwa mwenzake, upande mmoja kumbe haikuwa hivyo, kama walivyokuwa wanaume wa vyuo vikuu, nae alitaka kupata alichokihitaji na kuondoka zake.