Simulizi: Nyumba Iliyojaa Dhambi

Simulizi: Nyumba Iliyojaa Dhambi

SEHEMU YA 63

Nikacheka sana, mimi huwa siamini kama kuna mwanamke anakuwa hatari kama mwanaume, na kama yeye alitamba sana kwamba alikuwa hatari, nilitakiwa kumuachia nione ukali wake ulikuwa wapi.

Nawajua watoto wa kike, huwa hawana pumzi za kutosha. Wapo hivyo, tena wote duniani. Katika kipindi cha dakika kumi za mwanzo, wanaanza kucheza kwa kasi sana ila baada ya hapo pumzi inakata na kukwambia nimechoka.

Hapo ndipo zamu yako inapokuja na kumwambia kwamba hutakiwi kuchoka, humu hujaja kulala, umekuja kufanya kazi tu.

“Hivi una pumzi kweli?” niliamua kumuuliza kwa meseji.
“Kwa nini umeniuliza hivyo?”
“Ninataka kujua. Una pumzi?” nilimuuliza.

“Utaona kesho. Nataka kukuonyesha kwamba kungwi wangu hakufanya kazi ya bure,” aliniandikia.

Huwa sinaga presha kabisa, baada ya kuniambia hivyo, nikachukua cd yangu ya Kamasutra na kuanza kuangalia, unajua alinitisha sana, nilihisi kwamba alikuwa mtu hatari.

Nilichukua mafunzo kabisa, sikutaka kupitwa na chochote kile, baada ya kumaliza kutazama, nikanywa maziwa na karanga nyingi nikijiandaa kwa ajili ya siku inayofuata.

Kweli bwana, siku hiyo ilipofika, Halima mwenyewe akanipigia simu na kuniambia nipange tuonanie wapi.

Sijui alikuwa akinitega! Nina kwangu, nimenunua nyumba, inakuwaje twende kwenye nyumba ya wageni?

Aje humuhumu, kwanza ndipo kwenye vifaa vyangu.
“Njoo kwangu!” nilimwambia.”
“Kwako?”

“Yaap! Wewe njoo, usiogope, timu nzuri inacheza uwanja wowote ule,” nilimwambia.
“Sawa! Ngoja nijiandae.”

Hii ni kwa wanaume wote. Kitu cha msingi ni kutafuta pesa. Achana na kunyanyua vyuma, haisaidii hata kidogo, utaonekana kama mlinzi tu lakini pesa ndiyo kila kitu.

Wanawake wanapenda pesa, wanapenda kutunzwa, wanapenda kununuliwa zawadi za kila aina na ndiyo maana kwa mtu kama Halima hakuwa akinisumbua hata kidogo kwa kuwa alijua kabisa nilikuwa na pesa.

Nikafungua friji na kuangalia vinywaji, vilikuwa vimepungua sana na hivyo nilitakiwa kuongeza kidogo.

Nikatoka na kwenda kwenye duka moja la vinywaji lililokuwa Sinza Kijiweni.
 
SEHEMU YA 64

Nilipofika hapo, macho yangu yakatua kwa msichana mmoja hivi, alikuwa mdogomdogo tu, alibana nywele zake kwa nyumba na kuvaa kisketi fulani kilichokwenda mpaka juu ya magoti yake kidogo.

Alikuwa mzuri, pembeni ya pua yake kulikuwa na kidoti. Wanaume walikuwa wakimwangalia, si kwamba alifungashia, bali ule uzuri wake ilikuwa ni balaa. Nililiacha gari nyumbani, hapo nilikwenda kwa bodaboda kwa kuwa hakukuwa mbali kabisa.

Nilimwangalia, nikasema haiwezekani, nikaanza kumfuata kwa nyuma, sikuona aibu yoyote ile, watu walikuwa wakimwangalia lakini nilijiamini mno.
“Hey Miss...” nilimuita lakini hakugeuka, aliendelea kwenda mbele huku akiwa na mfuko uliokuwa na boksi la soda.

Nikamfuata kwa kasi kidogo, nilipomkaribia, nikamshika mkono. Najua hakupenda lakini hakuwa na jinsi, akautoa mkono wake, akageuka na kuniangalia huku akionekana kuwa na hasira na mimi.

“Niache huko,” aliniambia huku akiniangalia.
“Samahani dada!" nilimwambia. Akageuka na kuendelea na safari.
“Unakuwa mkali sana, kwa nini? Au kwa sababu hunifahamu?” nilimwambia huku tukipiga hatua.

Hakunijibu, alikuwa kimya kama bubu na alivimba mno. Sikutaka kukata tamaa, niliwajua mademu, huonekana wagumu wakati mwingine kwa kuwa wanahitaji lugha fulani tamu, si ile ya kuonekana mhuni.

“Najua hunijui! Najua unaniona mtu wa ajabu kabisa, ila naomba nikwambie kitu kimoja,” nilimwambia kwa sauti ya chini. Hakujibu.

“Umependeza sana, yaani kama Tiwa Savage,” nilimwambia. Akabaki kimya tu.
“Jamani! Yaani pamoja na kukusifia hata asante! Niambie ahsante tu niridhike nirudi,” nilimwambia. Akabaki kimya.

“Miss! Naomba niambie niridhike nirudi, sihitaji kukupotezea muda wako,” nilimwambia kwa sauti ya chini lakini bado hakutaka kuzunguma lolote lile.

Baada ya muda fulani akafika kwenye nyumba moja na kufungua geti na kuingia ndani. Mtu mzima nikabaki nje, sikujua ni kitu gani nilitakiwa kufanya.
 
SEHEMU YA 65

Nikaanza kujiuliza kama ilikuwa ni sahihi kuondoka ama kubaki hapohapo.

Kiukweli yule msichana nilimpenda kwa kuwa alikuwa na sura nzuri, nilijisemea kwamba endapo ningeondoka basi ningemkosa, ili kuonyesha kwamba nilihitaji sana kuzungumza naye, nilisubiri kama dakika tano hivi, nikapanga kupiga hodi kumuulizia.

“Mh! Subiri kwanza,” nilisema.
Kwa wanawake kupo hivi, endapo tu ungeanza kuzungumza naye kwa kumtaja jina lake basi ungefanikiwa kumpata, kitu cha kwanza angekuwa anajiuliza umemjuaje, hiyo ingekuwa nafasi kwako kuanza kumchambua kama karanga.

Pembeni kulikuwa na duka, nikalisogelea, nikamuona mshikaji fulani akiuza, kwa kumwangalia tu nilijua kwamba alikuwa Mchaga, hivyo nikaanza kuongea naye.

Nilimuuliza kuhusu msichana yule, akaanza kunizungusha, hakutaka kuniambia ukweli.

Yeye ni Mchaga, nilijua udhaifu wake, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa elfu kumi na kumuwekea karibu na kidirisha cha duka lake.

“Niambie kidogo kuhusu yeye, halafu hii utakunywa soda,” nilimwambia huku nikimuonyeshea ile pesa. Ile kuiona tu, macho yakamtoka.

“Unamzungumzia msichana yupi?” aliniuliza.
“Yule aliyeingia nyumba hiyo nyekundu,” nilimjibu.

“Humo kuna wasichana watawili halafu mapacha, wewe unamzungumzia Doto au Kulwa?” aliniuliza.

“Mapacha?”
“Ndiyo!”
“Sasa kama mapacha hapo nitasema namzungumzia yupi? Wote watakuwa wanafanana...ila niambie wanaitwa nani!” nilimwambia.

“Mkubwa anaitwa Glory na mdogo anaitwa Esta.”
“Oh! Ahsante! Wanasoma?”
“Mmoja anasoma Ardhi na mwingine anasoma IFM,” alisema.

“Wa Ardhi yupi?”
“Esta!”
“Sawa.”

Nikampa ile elfu kumi, kwangu pesa haikuwa tatizo, nilichokuwa nikihitaji ni kumpata msichana niliyekuwa nimemfuata.

Yaani kipindi hicho sikukumbuka kabisa kuhusu Halima, nilikuwa bize na huyu msichana niliyekuwa nimemfuatilia.

Nilipofika getini nikaanza kugonga hodi bila kuogopa kitu chochote kile.

Niligonga kwa sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa na msichana mmoja mdogo, alifanana na yule aliyeingia, bila shaka alikuwa mdogo wake.

“Shikamoo!” aliniamkia.
“Marahaba! Esta yupo?” nilimuuliza.
“Ndiyo yupo.”

“Naomba uniitie!”
“Ingia...” aliniambia, nikazama ndani.
 
SEHEMU YA 66

Kwa jinsi alivyoniambia niingie ilionekana kuwa rahisi sana, wala sikuogopa, nilihisi kwamba hakukuwa na mtu, nilipozama tu, macho yangu yakatua kwa wazee wawili, nahisi walikuwa wazazi wao, walikaa kibarazani kwenye viti wakipunga upepo, nilipoingia tu, wakayapeleka macho kwangu na kuniangalia.

Nilishtuka mno, kijasho chembamba kikaanza kunitoka, nilitamani kukimbia lakini nilishindwa kabisa.

Mzee huyo alikuwa akiniangalia huku akionekana kuhitaji kufahamu ni kitu gani nilikuwa nakihitaji nyumbani hapo.

Nikapiga moyo konde, nikawasogelea, nikawasalimia kwa heshima kubwa na kuwaambia kwamba nilikuja kumuona Esta.

“Wewe ni nani?” aliniuliza.
“Nasoma naye!” “Unasoma naye wapi?”
“Ardhi!”
“Unamjua Esta?” aliniuliza kwa ukali kidogo.

“Namjua!”
“Sawa. Stela! Kawaite dada zako,” alisema mzee yule.

Tayari nilijua kulikuwa na balaa hapo, yule mtoto akaingia ndani kwenda kuwaita. Nilibaki pale nje na wazazi wao huku nikiwa na hofu mno ila uso wangu ulikuwa kwenye tabasamu pana.

Baada ya dakika moja, yule mtoto akarudi na hao dada zake, nilipowaangalia moyo ukapiga paa. Yaani kama duniani kulikuwa na mapacha waliokuwa wanafanana basi hawa walikuwa balaa.

Walifanana, walikuwa wazuri kiasi kwamba nilichanganyikiwa.
Kilichotokea sasa, sikujua yule msichana ambaye nilikutana naye nje alikuwa yupi kwani hata nguo alikuwa amebadilisha.

Niliwaangalia kwa makini lakini sikumgundua kabisa, nikabaki nikishangaa.

“Aya mchukue huyo Esta uongee naye, si umesema unasoma naye,” aliniambia yule mzee kwa sauti ya kutaka kunikomoa, mtu mzima nikaloa, halafu watu wenyewe nilivyokuwa nikiwaangalia, wote walikuwa wakinishangaa.

Yaani ghafla nilitamani tu ardhi ipasuke nitumbukie ndani, au niwe mchawi, nipotee na nitokezee nyumbani kwangu kwani hata huyo Esta sikumjua ni yupi kati ya wale wawili waliosimama mbele yangu. *
*
*
Je, nini kiliendelea?
 
Day, mtihani kweli kweli
 
Bado nimekaa karibu na smartphone yangu hapa kujua nini kitaendelea kujiri huko nyumbani kwa akina Esther
 
Hahaaaahaaa...dahh!nimecheka hapo alipoambiwa aondoke nae esta
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom