Ukti Jabue
Senior Member
- Oct 19, 2017
- 109
- 86
Mama anashtuka anashindwa kuficha hisia zake, kwel kikulacho.
Umenichekesha mpaka hamu ya kula inapoteaNjoo jamani uendelee! Mbona hivyo kuntoa hamu ya kula mwana wa mwenzio???
Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani inakata stimu sana! Inakuwa kama isidingo the need episode 1 mpaka kesho teno hiyo!
Umeona eeh, shunie anatutesa kiainaYaani inakata stimu sana! Inakuwa kama isidingo the need episode 1 mpaka kesho teno hiyo!
Sent using Jamii Forums mobile app
oh, aiseeSehemu ya 19
Tuliagana na mganga na kwenda kutafuta usafiri. Kwa vile tulikuwa hatujala tulitafuta sehemu kupata kifungua kinywa cha haja na kisha nilimpeleka da Suzy kwake na kurudi zangu kwangu. Kutokana na uchovu nilipofika nyumbani nilipanda kitandani na usingizi mzito ulinichukua.
****
Nilitumia zile dawa kwa siku tatu kwa umakini mkubwa na kumaliza. Baada ya kumaliza kutumia makombe na dawa za kunywa nilikaa kusubiri matokeo ya dawa zile japokuwa sikuwa na uhakika wa kushika ujauzito kama nilivyoahidiwa na mganga.
Baada ya siku nne mzee Sambi alirudi, niliamini ule ulikuwa muda muhimu kutega mtoto. Usiku kabla ya kukutana naye mwili nilinawa dawa kwa bi mkubwa kabla ya kukutana na mwenzangu.
Nilifanya vile kisha nilikwenda kukutana na mwenzangu, niliendelea kufanya vile kwa wiki nzima huku nikiwa na matumaini madogo ya kushika ujauzito.
Mwezi ulikatika huku duka langu likiwa tayari limejazwa vitu vyote vya muhimu na kuanza kulifanyia matangazo ya kwenye magazeti na kwenye baadhi ya redio nchini.
***
Kupitiliza kuziona siku zangu kulinishtua lakini bado sikuamini kwa vile hali kama ile iliishawahi kunitokea hata nilipokuwa na mume wangu kwa kupitiliza miezi miwili, lakini mwezi wa tatu niliziona siku zangu na ziliendelea kama kawaida.
Mabadiliko ya hali yangu yalinishtua kidogo, nilimweleza mwenzangu ambaye alinishauri twende hospitali kuangalia afya yangu.
Nilikwenda hospitali na kufanya vipimo, tena nakumbuka siku ile nilikuwa na mzee Sambi. Baada ya daktari kuangalia majibu ya vipimo alivyonieleza nikapime alisema:
“Vipimo vinaonesha upo sawa, ila...”
Alishusha pumzi na kututazama usoni na kutabasamu kitu kilichonifanya nijiulize mbona anatabasamu ameona nini.
“Ila nini dokta?” mzee Sambi aliuliza wakati huo nilikuwa nimemuegemea begani.
“Hongereni.”
“Hongera ya nini?” mzee Sambi aliuliza.
“Inaonekana mambo si mabaya.”
“Kivipi?” safari ile niliuliza mimi.
“Inaonesha wewe ni mjamzito.”
“Nooo...nooo,” nilijikuta nikitikisa kichwa kukataa kama vile dokta ni muongo.
“Kwa nini unakataa?” aliniuliza akinishangaa.
“Hata siamini.”
“Kwa nini huamini.”
“Nimeitafuta sana mimba, siamini kama kweli Mungu kasikiliza maombi yangu.”
“Basi mama hongera sana kweli una ujauzito.”
“Nashukuru Mungu,” Nilisema kwa sauti ya kilio, furaha ya ujauzito ilinifanya niangue kilio cha kwikwi.
“Basi mpenzi, tumshukuru Mungu kwa kila jambo,” mzee Sambi alinibembeleza.
Baada ya maelezo ya daktari jinsi ya kuitunza mimba changa tulirudi nyumbani.
Njiani nilibakia na maswali ujauzito ule ni kudra ya Mungu au dawa za mganga mama Amina ambaye naye alimuomba Mungu?
Lakini kwa upande mwingine nilikubaliana na mama Amina ni mganga wa kweli kwa jinsi alivyonieleza ndivyo ilivyokuwa.
Nilipanga kumpelekea zawadi kubwa kwa ujauzito ule pia zawadi nyingine kama nikijifungua.
Kwa kweli ilikuwa furaha kubwa moyoni mwangu kushika ujauzito. Nilipofika nyumbani nilimjulisha da’ Suzy naye alifurahi sana, nilimsikia akipiga vigelegele upande wa pili kuonesha naye alifurahia shoga yake kupata ujauzito.
Ujauzito wangu ulifanya nigeuke malkia kwa mzee Sambi muda mwingi alihakikisha yupo karibu yangu huku akihakikisha sifanyi kazi yoyote ngumu mpaka nitakapojifungua.
Nilimfikishia taarifa mama kuhusiana na ujauzito wangu, mama alifurahi sana mwanaye kupata ujauzito. Furaha ya mama ilinifariji na kujisikia faraja moyoni mwangu.
“Mwaija angalie usirudie makosa ya awali wa kupoteza ujauzito wako,” mama alinionya.
“Mama sasa hivi nazingatia maelekezo ya madaktari ili kuifanya mimba yangu ikue vizuri.”
“Kama hivyo ni vizuri, mama yako nina hamu ya mjukuu.”
“Najua mama, tumuombe Mungu akupe mjukuu.”
“Inshaallah.”
Ukaribu wa mzee Sambi uliongezeka, muda mwingi hakucheza mbali na mimi huku akiniahidi ujauzito ukifika miezi minne angenipeleka Afrika Kusini na kukaa huko mpaka nitakapojifungua.
“Mwaija, katika kitu ambacho nilikiomba usiku na mchana basi ni hiki cha wewe kubeba ujauzito. Ujauzito ukifikisha miezi minne nakupeleka South Africa (Afrika Kusini) ambako utakaa mpaka utakapojifungua.”
“Kwani hapa kuna nini?”
“Katika kitu chenye thamani chini ya jua, ni hilo tumbo lako ambalo nataka nilitunze kuliko hata mboni za macho yangu.”
“Mpenzi unataka mtoto gani?”
“Japokuwa nataka wa kiume lakini yeyote atakayezaliwa ni zawadi yangu.”
Ukaribu wa mzee Sambi ilinifanya nikose muda wa kurudi kwa mganga kumueleza matokeo ya dawa aliyonipa ilinisaidia kushika ujauzito. Sikupenda kumweleza bwana yangu kuhusu ujauzito wangu ulipatikana kupitia kwa mganga.
Wakati huo mzee Sambi alikuwa ameninunulia Toyota Rav 4 kwa ajili ya kunipeleka popote kama hayupo. Kwa vile nilikuwa sijajua gari vizuri alinitafutia dereva kijana mmoja jirani yetu.
Muda mwingi alikuwa kijiweni nikiwa na shida nilimpigia na kuja mara moja kunisikiliza. Niliendelea kuona neema ya Mungu ikinifungukia kwa mambo yangu kuninyookea.
Miezi miwili ilikatika huku maendeleo kwenye ujenzi wangu yakipungua kasi japokuwa ilikuwa kwenye hatua za kumalizia. Mzee Sambi alinieleza nisiwe na wasiwasi muda si mrefu nyumba yangu itaisha.
Hali yangu ya ujauzito ilifanya niwe mtu wa kupumzika nyumbani hata kwenye super market yangu nilichelewa kuifungua mpaka hali yangu itakapokuwa vizuri, lakini kwa shauku ya mtoto aliyokuwa nayo mzee Sambi niliona mpaka nitakapojifungua.
Tatizo la kuchoka sana hospitali walisema tatizo la kuchoka sana litaisha baada ya ujauzito kukua, ile hali ilikuwa ya mpito. Pamoja na kuwa nachoka lakini nilipata huduma zote muhimu.
Mzee Sambi alihamia kwangu kwa wiki mbili akinieleza ameaga kwa mkewe amesafiri kikazi. Mtoto wa kike nilinenepa mbona nilideka nini nilichokitaka nikakosa.
Siku moja nikiwa nimejipumzisha nyumbani msichana wangu wa kazi alinieleza kuna mgeni nje.
“Dada kuna mgeni.”
“Mwanaume au mwanamke?”
“Mwanamke wa makamo.”
“Mwambia aingie.”
Baada ya muda aliingia mama mmoja aliyekuwa amevaa gauni la kitenge na kitenge kingine alijifunga chini na juu alitengeneza kilemba cha kitenge pia.
Vazi lile lilikuwa limempendeza sana yule mama ambaye alikuwa umri wa dada zangu.
“Karibu dada,” nilimkaribisha nikiwa nimejilaza kwenye kochi.
“Asante,” alijibu na kwenda kukaa kwenye kochi lililokuwa likitazamana na kochi langu.
“Shikamoo,” nilimwamkia huku nikijitahidi kukaa kitako.
“Marahaba, za hapa?”
“Mmh! Nzuri, karibu.”
“Asante, mzee Sambi nimemkuta?”
“Ametoka.”
“Ametoka saa ngapi?” aliniuliza huku akitembeza macho kila kona ya nyumba kama anakagua kitu.
“Asubuhi lakini hachelewi kurudi.”
“Samahani mama unatumia kinywaji gani?” msichana wangu wa kazi alimuuliza mgeni.
“Asante, situmii kitu,” mgeni alishukuru.
Nilipomuangalia kwa chati mkononi alikuwa ameshika ufunguo wa Land Cruiser VX, pia alikuwa na mkufu na hereni za dhahabu na mkononi alikuwa na pete vidole vitatu, hakika yule mama alikuwa anaonekana ni mtu mwenye maisha mazuri.
“Mama yangu ungekunywa hata juisi basi,” nilimbembeleza mgeni.
“Usihofu, siku nyingine.”
“Ulikuwa na shida gani?”
“Aah! Basi nitaonana naye.”
“Kwa hiyo akija nimwambie nani aliyekuja?”
“Nitamuona tu wala usihofu, naomba niwakimbie.”
“Japokuwa hukutaka kutuambia wewe ni nani, nikuruhusu dada yangu.”
Yule mama alinyanyuka na kutoka na kuniacha nikimsindikiza kwa macho. Baada ya kutoka nilijiuliza yule ni nani aliyekuja kumuuliza mzee Sambi.
Alikuwa mtu wa kwanza kuja kumuulizia mzee Sambi toka nihamie pale, wazo la haraka lilikuwa labda mwenye nyumba ambaye nilielezwa ni mwanamke alikuwa hakai maeneo yale.
Nilijiuliza alikuwa na shida gani ikiwa kodi yake alilipwa ya mwaka mzima. Niliachana naye na kuendelea na yangu.
Muda mfupi baada ya yule mama kuondoka, aliingia mzee Sambi. Kama kawaida nimpokea kwa kujilazimisha huku akinikataza kunyanyuka.
“Aah! Tulia unaenda wapi mpenzi?”
“Mpenzi unafikiri nisipofanya mazoezi nitalemaa si ulimsikia daktari.”
“Asubuhi si ulifanya, pumzika sitaki uteseke.”
“Sawa, lakini kukupokea ni moja ya mazoezi siyo mateso.”
“Haya mpenzi.”
Baada ya kupumzika nilimweleza ugeni uliofika kumuuliza muda mfupi kabla hajarejea.
“Mpenzi kuna mtu alikuja kukuulizia.”
“ Mtu?”
“Ndiyo.”
“Alikuja kuniulizia hapa?”
“Ndiyo.”
“Mmh! Mtu gani aliyekuja kukuuliza hapa?”
“Kuna mama mmoja alikuja kukuuliza inawezekana ni mwenye nyumba wako.”
“Mmh! Ana shida gani namba yangu ya simu si anayo!”
“Mi nitajuaje.”
“Amesemaje?”
“Amesema mtaonana baadaye.”
“Akuacha ujumbe wowote?”
“Hakuacha.”
“Kwani yupo vipi?”
“Mrefu mweusi amevaa kitenge kuanzia juu mpaka chini.”
“Ana mwanya?”
“Ndiyo.”
“Na ana meno mawili ya dhahabu?”
“Ndiyo, una mfahamu?”
“Ndiyo.”
“Ni nani?”
“Achana naye ni mwenye nyumba.”
“Sasa mbona amekuja bila taarifa?”
“Nitaonana naye, kama ana shida lazima atanipigia tu.”
“Mmh! Inaonekana mwenye nyumba hanajipenda sana.”
“Kawaida, baada ya kuniuliza ukamjibu sipo alisema kitu gani kingine?”
“Amesema mtaonana.”
“Basi hilohilo tu?”
“Ndiyo.”
“Mmh! Sawa.”
“Kwani vipi mbona kama umeshtuka?”
“Kawaida tu.”
Sikutaka kumuuliza sana niliamini yule ni mama mwenye nyumba wake. Usiku wa siku ile aliniaga kurudi kwake japokuwa alipanga kurudi kwake siku ya pili jioni.
“Vipi mbona ghafla,” nilimuuliza.
“Hapana kesho nitarudi.”
Pia sikutaka kumzuia kwa vile nilikuwa naye kwangu kwa wiki moja na nusu kitu ambacho kilikuwa hakijatokea, siku za nyuma alikuwa akilala mara mojamoja na kuondoka siku ya pili.
***