Simulizi: Namchukia Mama Yangu

Sehemu ya 17

Baada ya kumuonesha mama nyumba yangu, tulimrudisha mpaka Temeke kisha nilirudi nyumbani kwangu kupumzika. Moyoni nilifurahi ajabu mama yangu kuona jumba langu la kifahari, mshtuko alioonesha nilijua hakuamini macho yake.

***
Pamoja na maisha na malezi mazuri kutoka kwa mpenzi wangu, lakini kuchelewa kupata mtoto kulinikosesha raha. Siku moja nikiwa kazini muda mwingi nilikuwa mtu wa mawazo sana kitu kilichomshtua da’ Suzy.

“Mwaija mdogo wangu haupo sawa?”
“Ni kweli.”
“Tatizo nini?”
Sikumficha nilimweleza kila kitu kuhusiana na kuchelewa kumzalia mtoto mzee Sambi.
“Sasa kama mlionekana hamna tatizo kipi kinachelewesha mtoto?”

“Hapo ndipo ninapochanganyikiwa.”
“Mmeisha tumia tiba mbadala?”
“Sasa kama huna tatizo tiba ya nini?”
“Mdogo wangu huenda ni chango, ukipata dawa za asili zitakusaidia.”

“Dada kama lingekuwa chango nisingepata ujauzito.”
“Mdogo wangu, lazima uangalie na jicho la tatu huenda una chango lisilouma na kusababisha mimba isiingie.”

“Mmh! Sijawahi kutumia dawa za asili toka nizaliwe.”
“Ndiyo unatakiwa ukatumie uone kwani wengi walikuwa na matatizo zaidi ya kwako leo hii wana watoto.”

“Hizo dawa nitapata wapi?”
“Nitakupeleka kwa mtaalamu.”
“Wapi?”
“Mbagala Maji Matitu.”
“Hiyo dawa itanisaidia kweli?” niliingiwa na wasiwasi japokuwa nilimuamini sana da’ Suzy.
“Dada nakwambia ndani ya wiki ukitumia kitu hicho.”

“Shoga nakuahidi nikishika mimba nitakupa milioni moja.”
“Wee iandae tu, nakuapia mwezi haukatika bila kunasa.”

“Basi dada naomba unipeleke,” nilijikuta nikipata shauku ya kwenda kwa huyo mtaalamu ili niweze kumzalia mtoto mzee Sambi.

“Hakuna tatizo.”
Tulikubaliana mwisho wa wiki anipeleke kwa mtaalamu wa tiba za asili anisaidie kupata mtoto. Maneno ya dada Suzy yalinipa faraja kwa asilimia ndogo.

Mwisho wa wiki nilimpitia dada Suzy na kukodi gari mpaka Mbagala Maji Matitu. Tulipofika tulikwenda moja kwa moja kwa mtaalamu aliyekuwa akikaa ndani kidogo kupita kituo kidogo cha polisi cha Maji Matitu.

Tulifika kwenye nyumba iliyokuwa imezungushiwa uzio wa makuti. Tuliingia ndani tulikuta watu kama sita wakiwa wamekaa kwenye mkeka na ndani kulikuwa na watu wawili.

Mganga alikuwa akitoka ndani alipotuona alitufuata na kutukaribisha. Alikuwa dada mmoja aliyekuwa na umri wa kawaida pia hata mavazi yake yalikuwa ya kawaida kuonesha si mganga wa kizamani wa kuvaa kaniki na ngozi.

Alikuwa na umbile fupi alivaa dela lililompendeza, pia mikononi alikuwa na pete za silver kila kidole na shingoni pia alikuwa na mkufu wa silver kichwani alikuwa ameseti nywele ukimuangalia haraka huwezi kuamini kama mganga.

“Jamani karibuni,” alitukaribisha kwa uchangamfu mkubwa.
“Asante dada,” tulijibu kwa pamoja.
“Samahani jamani, vumilie kidogo sina kazi kubwa nitawaiteni baada ya muda mfupi.”

“Hakuna tatizo.”
Mganga alituiacha na kuelekea ndani na kutuacha tumekaa kwenye benchi lililokuwa pembeni ya mkeka.

Baada ya muda alituita ndani, tuliingia ndani ya chumba ambako ndiko kwenye kilinge, ambako kulikuwa na vitu vyake vya kiganga na dawa. Baada ya sisi kuketi mganga alikaa mbele yetu kwenye kigoda na kutulia kwa muda kisha alisema:

“Ndiyo, karibuni.”
“Asante,” tulijibu kwa pamoja.
‘Mna tatizo gani?”
“Mwenzangu anahitaji mtoto.”
“Anahitaji vipi?” uliuliza huku akitutazama kwa zamu.

“Amekwenda hospitali na kuonekana hana tatizo lakini mtoto hapati,” alisema da’ Suzy aliyeonekana mzoefu wa sehemu zile.

“Na mwenzake naye alikwenda?”
“Ndiyo wote wapo sawa.”
“Basi tumuombe Mungu nina imani dawa nitakazompa zitamsaidia.”

“Halafu tulikana kujua talaka yake ya mwanzo ilisababishwa na nini?” da’ Suzy aliuliza kwa niaba yangu.

“Hakuna tatizo,” mganga alisema huku akinyanyukana kuchukua rubega la Kimasai na kujifunga kisha alivaa taji la kimasai na chini alivaa viatu vya tairi na kushikilia mkuki pembeni yake alilaza sime.

Nilijikuta nikiingiwa na woga lakini dada Suzy hakuonesha wasiwasi wowote na kujiuliza unataka kufanya nini. Baada ya kutulia kwenye kigoda chake alimwita mwanaume aliyekuwa nje ambaye alikuja kukaa pembeni yetu.

“Jamani nina imani mwalimu atakayepanda kuna maneno yatakushindeni kuyaelewa. Huyu atawasaidia kuwaelewesheni.”
“Hakuna tatizo.”

Baada ya kusema vile alichoma udi na kuuweka pembeni kisha akishika mkuki wake na kuuinamia kwa muda kisha alitulia kupandisha jini la Kimasai lililokuwa likitwa Lukuki.

“Heloo habari,” alisema baada ya kupandisha, nilitulia tuli kuangalia kwani jambo lile kwangu lilikuwa ndiyo siku ya kwanza.
“Nzuri,” da’ Suzy aliitikia.
Alianza kwa kutusalimia kwa kutushika mikono na kugusanisha kichwa chake kila aliyekuwemo ndani.

Alianza kuelezea tatizo langu huku nikibahatisha mawili matatu yaliyonishinda mkalimani alinisaidia kunifafanulia.
“Rafiki una matatizo mkubwa sana, tatizo yako si ya leo hata najiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu kweli?”

“Ndiyo,” ndiyo nilijibu.
“Tatizo lako limeanza baada ya ndoa yako, ikiwa pamoja na kuharibikiwa mimba, mume kuharibikiwa maisha kukosa kazi.

Kuvurugikiwa na maisha na kila kitu kusimama ni kweli?” mganga aliniuliza, yote aliyosema yalikuwa kweli alikuwa kama mtu anayejua maisha yangu.

“Ni kweli,” nilikubali.
“Mumeo aliondoka na aliporudi alikupa talaka isiyo na maelezo ni kweli?”

“Ndiyo ila alisema mama anajua.”
“Tatizo lako nitakutibu wala sitaki kulichimba sana kwa vile nitazalisha visivyotakiwa, kingine unatafuta mtoto bila mafanikio japo huna tatizo lolote, ni kweli?”
“Kwa nini usinieleze mbaya wangu?” nilitaka kujua.

“Huna moyo huo wa kusikia vitu vizito vilivyo kuzunguka, ila nakuahidi kukutibu na kukuondoa vifungo ulivyofungwa.

Vifungo ulivyofungwa ndivyo vilivyo sababisha upewe talaka, mshindwe kumaliza nyumba yenu mumeo awe na maisha magumu pia usishike ujauzito ambao ungemeza kila aina ya dawa bila mafanikio.”
“Mungu wangu! Na nani?” nilishtuka kusikia habari zile zilizokuwa zinafanana na maneno ya mume wangu.

“Matatizo yako siwezi kukueleza nani kusababisha kwa vile najua wanadamu mna mioyo midogo ila naweza kukutibu. Kwa kukufungua vifungo hivyo kwa uwezo wa Mungu utashika ujauzito tu.”
“Nitashukuru.”

“Leo nitakupa dawa ya kuoga ila kesho njoo asubuhi nitakuosha nuksi pia kukufungua vifungo na kukupa dawa ya kunywa. Mwezi haufiki utashika ujauzito.”
“Nitashukuru.”
“Kesho njoo na doti mbili za kanga mpya za kukuoshea.”

“Sawa.”
Baada ya kunipa maelezo ya kina kuhusu maisha yangu na kumruhusu jini la Kimasai kuondoka. Yule dada alirudi katika hali ya kawaida na kuelezwa yote aliyosema Lukuki jini la Kimasai.

Alinipa dawa ya kuoga na kutakiwa siku ya pili asubuhi na mapema sana nifike kwa mganga ili kuifanya tiba yangu iwe ya kwanza. Nilirudi nyumbani nikiwa bado siamini kama kweli kupitia dawa za yule dada nitapona kweli na kupata mtoto.

Nilipofika nyumbani nilijipumzisha kwenye kochi huku msichana wa kazi akiniletea juisi. Baada ya kunywa juisi nilikwenda chumbani na kujifungia ili kupumzisha akili yangu kutokana na kuzongwa na mawazo mengi. Sikutaka kelele za aina yoyote nilishukuru siku ile mzee wangu alikuwa amesafiri ilinipa uhuru mkubwa wa utulivu.

Kichwa kilikuwa kizito kutokana na kugubikwa na mawazo mazito yaliyo jifungafunga na kunifanya nishindwe kuelewa niliyoelezwa yana ukweli kwa asilimia kubwa swali likabakia nani mtendaji wa ubaya ule.

Kila nililowaza lilikuwa halikubaliki na kuona kama najichanganya mwenyewe kwa kufikiria kitu ambacho hata kwa mtutu kisingewezekana.

Mpaka usiku unaingia bado nilikuwa kwenye fumbo zito, chakula cha usiku kilinishinda na kunifanya nipande kitandani mapema. Nilikumbuka nilitakiwa kuoga dawa nilizopewa kwa mganga. Nilikwenda bafuni na kujimwagia maji ya dawa mwili mzima na kupanda kitandani kujilaza
 
Sehemu ya 18

Nilirudi nyumbani nikiwa bado siamini kama kweli kupitia dawa za yule dada nitapona kweli na kupata mtoto.

Nilipofika nyumbani nilijipumzisha kwenye kochi huku msichana wa kazi akiniletea juisi. Baada ya kunywa juisi nilikwenda chumbani na kujifungia ili kupumzisha akili yangu kutokana na kuzongwa na mawazo mengi.

Sikutaka kelele za aina yoyote nilishukuru siku ile mzee wangu alikuwa amesafiri ilinipa uhuru mkubwa wa utulivu.

Kichwa kilikuwa kizito kutokana na kugubikwa na mawazo mazito yaliyo jifungafunga na kunifanya nishindwe kuelewa niliyoelezwa yana ukweli kwa asilimia kubwa swali likabakia nani mtendaji wa ubaya ule.

Kila nililowaza lilikuwa halikubaliki na kuona kama najichanganya mwenyewe kwa kufikiria kitu ambacho hata kwa mtutu kisingewezekana.

Mpaka usiku unaingia bado nilikuwa kwenye fumbo zito, chakula cha usiku kilinishinda na kunifanya nipande kitandani mapema. Nilikumbuka nilitakiwa kuoga dawa nilizopewa kwa mganga. Nilikwenda bafuni na kujimwagia maji ya dawa mwili mzima na kupanda kitandani kujilaza.

Usingizi ulikuwa mbali nilijikuta nikiwa na mawazo mengi kuhusiana na maelezo ya kutoka kwa mganga kwa kuijua historia yangu kama nilimhadithia na kuona hata ujauzito wangu haukuharibika na kujua ni kwa amri ya Mungu kumbe kuna mkono wa mtu.
Hata kuvurugikiwa maisha na kupewa talaka yenye utata na fumbo zito ilikuwa na sababu ambayo bado nilifichwa.

Maneno ya mganga yalizidi kunichanganya sana baada ya kuyarudia yaliyonisibu kwa kuusema ukweli wa siri nzito iliyo moyoni mwangu ambayo nyingine hata dada Suzy sikumwambia.

Pamoja na kunieleza sababu ya kuharibikiwa maisha na kuniahidi atanisaidia kwa kunifungua vifungo vyote bado nilibakia na swali nani anayefanya hivyo?

Nilijikuta nikiyakumbuka maneno ya mtalaka wangu na kuamini alichokisema alikuwa na sababu ya kweli ya kunipa talaka. Lakini nilijikuta nikiendelea kumlaumu kama alijua kuna mtu katia mkono kwa nini hakuniambia nani aliyetenda vile.

Hata kama ni mama yangu mzazi, japokuwa jambo hilo nililipinga kwa nguvu zote, bado mimi sikuwa na kosa la kupewa talaka.
Nilijikuta nikiwaza peke yangu:

“Mmh! Inawezekana kweli aliyefanya vile ni mama yangu mzazi? Hapana ...hapana... mama yangu mzazi hawezi kufanya kitu kama kile, amefanya vile ili iwe nini?”

Wazo la labda mama yangu mzazi ndiye aliyefanya mchezo ule nililikataa kwa nguvu zote. Swali lililoniumiza akili lilikuwa kwa nini mtalaka wangu alimsema mama ndiye anajua kila kitu alikuwa na maana gani?

Nilijiuliza nani aliyenifunga au dada zangu kwa wivu wa mimi kuolewa? Lakini mbona wao waliolewa na kuachika iweje wanionee wivu?
Kwa kweli kila nililolifikiria kwangu lilikuwa zito ambalo lilitaka kupasua kichwa changu.

Usingizi ulinipitia baada ya kukaa sana kitandani na kushtuka siku ya pili baada ya kushtushwa na mlio wa simu. Nilipoangalia nilikuta ni da’ Suzy ndiye aliyenipigia.

Niliangalia saa ya juu ya droo ya kitanda na kuona kumekucha ilikuwa saa moja kasoro. Niliichukua simu huku kichwa kikiwa kizito kutokana na mawazo kunizidi uwezo pia kuchelewa kulala.

“Haloo da’ Suzy.”
“Abee, vipi imeishatoka nyumbani?”
“Dada wee acha tu, yaani simu yako ndiyo iliyonishtua usingizini, bila hivyo sijui ningeamka saa ngapi?”
“Kwani mzee leo kalala nyumbani?”
“Walaa, mawazo tu dada yangu.”

“Lakini yule dada si kasema atakusaidia?”
“Ni kweli lakini maneno aliyosema mganga na aliyosema Beka yanafanana lazima niseme ukweli nimechanganyikiwa sana niliposhindwa kumjua mbaya wangu.”

“Mdogo wangu yote hayo yataisha, kwanza mshukuru Mungu ameachwa na Beka lakini sasa hivi una maisha mazuri. Wengine wakiharibikiwa mpaka wanachanganyikiwa na kukata tamaa ya maisha kwani huandamwa na mikosi.”

“Mmh! Sawa.”
“Basi usiyape sana nafasi mawazo yanayoumiza sisi tusingekuwa hapa.”
“Lakini nani kanifanyia hivi?”
“Mwaija hebu kwanza kaoge ili tuwahi kwa mganga.”

“Sawa.”
Nilinyanyuka kitandani na kwenda bafuni kuoga harakaharaka na kutoka kumuwahi da ‘ Suzy. Sikutaka hata kufungua kinywa kwa vile nilikuwa nyuma ya muda tuliokubaliana kufika na mganga.
“Dada chai tayari,” msichana wa kazi alinishtua aliponiona naondoka bila kufungua kinywa.

“Mmh! Mdogo wangu kuna sehemu nimechelewa nitakunywa nikirudi.”
“Sawa dada japo ungekunywa hata nusu ya kikombe cha maziwa ya moto.”
“Nisamehe mpenzi nimechelewa sana.”
“Sawa dada.”

Nilitoka hadi barabarani na kukodi teksi mpaka Chang’ombe kwa da’ Suzy, niliyempitia kuelekea kwa mtaalamu Mbagala Maji Matitu. Kabla ya kufika tulifika tulinunua doti mbili mpya za kanga nilizoagizwa na mganga. Tulipofika tulipokelewa na mganga aliyekuwa na wateja wengi zaidi ya jana yake tuliyokwenda.

Nilijikuta nikipata mawazo mengi kichwani uwepo wa watu wengi pale ulitokana na nini. Nilipomuuliza da’ Suzy aliniambia ukiona watu wengi ujue ni ubora wa tiba zake umewavuta watu.

Alipotuona alitukaribisha kwa furaha siku zote yule dada uso wake ulijaa ucheshi. Baada ya kutukaribisha mganga alituchukua na kutupeleka nyuma ya nyumba ya chumba kimoja iliyokuwa imejengwa peke yake ndani ya uzio wa nyumba yake na kutueleza:
“Jamani nisubirini hapa kila kitu nimekiandaa kwa kazi yenu. Ngoja nikaandae kisha nitakuita.”

“Hakuna tatizo.”
Mganga aliondoka na kutuacha tukiwa tumekaa kwenye kochi la mbao lililokuwa halina mito tulilolikuta nyuma ya nyumba. Baada ya muda aliniita na kuingia ndani, nilikwenda ndani na kuingia chumbani kisha alinieleza nivue nguo zote kisha nijifunge kanga mpya nilizonunua na kunieleza nijifunge pea moja ya kanga kisha alinipeleka kwenye bafu lilikuwa pale uani na kunieleza nikae kwenye stuli aliyokuwa ameiweka mule bafuni.

Pembeni ya stuli kulikuwa na beseni lililokuwa na maji na kamba za ukindu saba zilizofungwa na dawa ya unga kama aliyonipa kwenda kuoga jana yake.

Baada ya kuingia na yeye bafuni alisimama nyuma yangu na kunishika katikati ya kichwa na kuzungumza anayojua, lakini yote yakiwa kumuomba Mungu kunifungua matatizo yangu na kuisafisha nyota yangu aliyofifia.

Ilikuwa umeingia ukungu na kushindwa kutoa mwanga wake halisi. Baada ya kusema kwa muda alitoa mkono kichwani mwangu na kunimwagia maji kwa kata kwa kuanzia kichwani huku akisema maneno kisha mikononi na kumalizia miguuni. Alinimwagia juu ya kanga niliyokuwa nimejifunika kisha mwili wote.

Baada ya kunimwagia maji mwili mzima kwa kumwagia juu ya kanga nilizojifunga aliondoa kanga ya kichwani na kuchukua ukindu mmojammoja uliofungwa na kuzungusha kwenye mikono na kuufyatua. Alifanya vile kwa sehemu za viungo vya mwili ambavyo wanasema ndimo watu wanatumia kuingiza uchawi wao kama kwenye magoti kifuani na kiunoni.

Kufungua kamba za ukindu alikuwa akifungua vifungo mwilini mwangu. Baada kumaliza zoezi lile alinieleza nioge maji yaliyobaki mwili mzima bila nguo kisha yeye alitoka nje.

Niliondoa nguo mwilini na kuoga mwili nzima, wakati huo alikuwa amekwenda ndani na kurudi na kanga zingine mpya na kunieleza nikimaliza nivae zile na nilizoogea alinieleza nizianike bila kuzikamua.

Nilifanya kama alivyonieleza na kutoka nje nikiwa nimejifunga kanga mpya, kisha niliingilia ndani mpaka kilingeni. Nilielezwa nivae nguo zangu.

Nilifanya vile na kukaa kwenye mkeka na kupata dua kisha nilipewa makombe ya kunywa na kuoga kwa siku tatu na miti ya kuchemsha kwa ajili ya kukifungua kizazi na dawa ya kunawa kabla ya kukutana na mwenzangu.

Nilitoa kiasi alichonieleza huku nikimuahidi nikishika ujauzito nitampa zawadi kubwa sana.
“Mdogo wangu tumuombe Mungu kila kitu kitakwenda vizuri.”

Niliagana na mganga na kumpitia da’ Suzy aliyekuwa bado yupo nyuma ya nyumba ameegemea ukutani na usingizi ulimchukua.
“Da’ Suzy,” nilimwita huku nikimtikisa.
“Abee, vipi tayari?” alishtuka usingizini na kufikicha macho huku akipiga miayo.
“Ndiyo twende zetu.”

“Mmh! Usingizi ulianza kuninyemelea.”
“Basi twende zetu.”
“Mmh!” alinyanyuka na kujinyoosha kisha akasema:

“Wacha nikamuage mama Amina,” mama Amina lilikuwa jina la mganga.
Kabla hatujaenda alikuja mganga kuonesha alisahau kitu.

“Samahani kuna kitu muhimu nilitaka kusahau kukuelezea.”
”Kitu gani? Nilimuuliza.
“Ukishika ujauzito njoo mara moja tufunge ili usiweze kutoka.”

“Sawa dada nimekuelewa nitafanya hivyo.”
Tuliagana na mganga na kwenda kutafuta usafiri. Kwa vile tulikuwa hatujala tulitafuta sehemu kupata kifungua kinywa cha haja na kisha nilimpeleka da Suzy kwake na kurudi zangu kwangu. Kutokana na uchovu nilipofika nyumbani nilipanda kitandani na usingizi mzito ulinichukua.
 
Sehemu ya 19

****
Nilitumia zile dawa kwa siku tatu kwa umakini mkubwa na kumaliza. Baada ya kumaliza kutumia makombe na dawa za kunywa nilikaa kusubiri matokeo ya dawa zile japokuwa sikuwa na uhakika wa kushika ujauzito kama nilivyoahidiwa na mganga.

Baada ya siku nne mzee Sambi alirudi, niliamini ule ulikuwa muda muhimu kutega mtoto. Usiku kabla ya kukutana naye mwili nilinawa dawa kwa bi mkubwa kabla ya kukutana na mwenzangu.

Nilifanya vile kisha nilikwenda kukutana na mwenzangu, niliendelea kufanya vile kwa wiki nzima huku nikiwa na matumaini madogo ya kushika ujauzito.

Mwezi ulikatika huku duka langu likiwa tayari limejazwa vitu vyote vya muhimu na kuanza kulifanyia matangazo ya kwenye magazeti na kwenye baadhi ya redio nchini.
***
Kupitiliza kuziona siku zangu kulinishtua lakini bado sikuamini kwa vile hali kama ile iliishawahi kunitokea hata nilipokuwa na mume wangu kwa kupitiliza miezi miwili, lakini mwezi wa tatu niliziona siku zangu na ziliendelea kama kawaida.

Mabadiliko ya hali yangu yalinishtua kidogo, nilimweleza mwenzangu ambaye alinishauri twende hospitali kuangalia afya yangu.

Nilikwenda hospitali na kufanya vipimo, tena nakumbuka siku ile nilikuwa na mzee Sambi. Baada ya daktari kuangalia majibu ya vipimo alivyonieleza nikapime alisema:

“Vipimo vinaonesha upo sawa, ila...”
Alishusha pumzi na kututazama usoni na kutabasamu kitu kilichonifanya nijiulize mbona anatabasamu ameona nini.

“Ila nini dokta?” mzee Sambi aliuliza wakati huo nilikuwa nimemuegemea begani.
“Hongereni.”

“Hongera ya nini?” mzee Sambi aliuliza.
“Inaonekana mambo si mabaya.”
“Kivipi?” safari ile niliuliza mimi.

“Inaonesha wewe ni mjamzito.”
“Nooo...nooo,” nilijikuta nikitikisa kichwa kukataa kama vile dokta ni muongo.
“Kwa nini unakataa?” aliniuliza akinishangaa.
“Hata siamini.”

“Kwa nini huamini.”
“Nimeitafuta sana mimba, siamini kama kweli Mungu kasikiliza maombi yangu.”
“Basi mama hongera sana kweli una ujauzito.”

“Nashukuru Mungu,” Nilisema kwa sauti ya kilio, furaha ya ujauzito ilinifanya niangue kilio cha kwikwi.

“Basi mpenzi, tumshukuru Mungu kwa kila jambo,” mzee Sambi alinibembeleza.
Baada ya maelezo ya daktari jinsi ya kuitunza mimba changa tulirudi nyumbani.

Njiani nilibakia na maswali ujauzito ule ni kudra ya Mungu au dawa za mganga mama Amina ambaye naye alimuomba Mungu?
Lakini kwa upande mwingine nilikubaliana na mama Amina ni mganga wa kweli kwa jinsi alivyonieleza ndivyo ilivyokuwa.

Nilipanga kumpelekea zawadi kubwa kwa ujauzito ule pia zawadi nyingine kama nikijifungua.

Kwa kweli ilikuwa furaha kubwa moyoni mwangu kushika ujauzito. Nilipofika nyumbani nilimjulisha da’ Suzy naye alifurahi sana, nilimsikia akipiga vigelegele upande wa pili kuonesha naye alifurahia shoga yake kupata ujauzito.

Ujauzito wangu ulifanya nigeuke malkia kwa mzee Sambi muda mwingi alihakikisha yupo karibu yangu huku akihakikisha sifanyi kazi yoyote ngumu mpaka nitakapojifungua.
Nilimfikishia taarifa mama kuhusiana na ujauzito wangu, mama alifurahi sana mwanaye kupata ujauzito. Furaha ya mama ilinifariji na kujisikia faraja moyoni mwangu.

“Mwaija angalie usirudie makosa ya awali wa kupoteza ujauzito wako,” mama alinionya.
“Mama sasa hivi nazingatia maelekezo ya madaktari ili kuifanya mimba yangu ikue vizuri.”

“Kama hivyo ni vizuri, mama yako nina hamu ya mjukuu.”
“Najua mama, tumuombe Mungu akupe mjukuu.”

“Inshaallah.”
Ukaribu wa mzee Sambi uliongezeka, muda mwingi hakucheza mbali na mimi huku akiniahidi ujauzito ukifika miezi minne angenipeleka Afrika Kusini na kukaa huko mpaka nitakapojifungua.

“Mwaija, katika kitu ambacho nilikiomba usiku na mchana basi ni hiki cha wewe kubeba ujauzito. Ujauzito ukifikisha miezi minne nakupeleka South Africa (Afrika Kusini) ambako utakaa mpaka utakapojifungua.”
“Kwani hapa kuna nini?”

“Katika kitu chenye thamani chini ya jua, ni hilo tumbo lako ambalo nataka nilitunze kuliko hata mboni za macho yangu.”

“Mpenzi unataka mtoto gani?”
“Japokuwa nataka wa kiume lakini yeyote atakayezaliwa ni zawadi yangu.”

Ukaribu wa mzee Sambi ilinifanya nikose muda wa kurudi kwa mganga kumueleza matokeo ya dawa aliyonipa ilinisaidia kushika ujauzito. Sikupenda kumweleza bwana yangu kuhusu ujauzito wangu ulipatikana kupitia kwa mganga.

Wakati huo mzee Sambi alikuwa ameninunulia Toyota Rav 4 kwa ajili ya kunipeleka popote kama hayupo. Kwa vile nilikuwa sijajua gari vizuri alinitafutia dereva kijana mmoja jirani yetu.

Muda mwingi alikuwa kijiweni nikiwa na shida nilimpigia na kuja mara moja kunisikiliza. Niliendelea kuona neema ya Mungu ikinifungukia kwa mambo yangu kuninyookea.

Miezi miwili ilikatika huku maendeleo kwenye ujenzi wangu yakipungua kasi japokuwa ilikuwa kwenye hatua za kumalizia. Mzee Sambi alinieleza nisiwe na wasiwasi muda si mrefu nyumba yangu itaisha.

Hali yangu ya ujauzito ilifanya niwe mtu wa kupumzika nyumbani hata kwenye super market yangu nilichelewa kuifungua mpaka hali yangu itakapokuwa vizuri, lakini kwa shauku ya mtoto aliyokuwa nayo mzee Sambi niliona mpaka nitakapojifungua.

Tatizo la kuchoka sana hospitali walisema tatizo la kuchoka sana litaisha baada ya ujauzito kukua, ile hali ilikuwa ya mpito. Pamoja na kuwa nachoka lakini nilipata huduma zote muhimu.

Mzee Sambi alihamia kwangu kwa wiki mbili akinieleza ameaga kwa mkewe amesafiri kikazi. Mtoto wa kike nilinenepa mbona nilideka nini nilichokitaka nikakosa.

Siku moja nikiwa nimejipumzisha nyumbani msichana wangu wa kazi alinieleza kuna mgeni nje.

“Dada kuna mgeni.”
“Mwanaume au mwanamke?”
“Mwanamke wa makamo.”
“Mwambia aingie.”

Baada ya muda aliingia mama mmoja aliyekuwa amevaa gauni la kitenge na kitenge kingine alijifunga chini na juu alitengeneza kilemba cha kitenge pia.
Vazi lile lilikuwa limempendeza sana yule mama ambaye alikuwa umri wa dada zangu.
“Karibu dada,” nilimkaribisha nikiwa nimejilaza kwenye kochi.

“Asante,” alijibu na kwenda kukaa kwenye kochi lililokuwa likitazamana na kochi langu.
“Shikamoo,” nilimwamkia huku nikijitahidi kukaa kitako.

“Marahaba, za hapa?”
“Mmh! Nzuri, karibu.”
“Asante, mzee Sambi nimemkuta?”
“Ametoka.”

“Ametoka saa ngapi?” aliniuliza huku akitembeza macho kila kona ya nyumba kama anakagua kitu.

“Asubuhi lakini hachelewi kurudi.”
“Samahani mama unatumia kinywaji gani?” msichana wangu wa kazi alimuuliza mgeni.
“Asante, situmii kitu,” mgeni alishukuru.

Nilipomuangalia kwa chati mkononi alikuwa ameshika ufunguo wa Land Cruiser VX, pia alikuwa na mkufu na hereni za dhahabu na mkononi alikuwa na pete vidole vitatu, hakika yule mama alikuwa anaonekana ni mtu mwenye maisha mazuri.

“Mama yangu ungekunywa hata juisi basi,” nilimbembeleza mgeni.

“Usihofu, siku nyingine.”
“Ulikuwa na shida gani?”
“Aah! Basi nitaonana naye.”
“Kwa hiyo akija nimwambie nani aliyekuja?”
“Nitamuona tu wala usihofu, naomba niwakimbie.”

“Japokuwa hukutaka kutuambia wewe ni nani, nikuruhusu dada yangu.”
Yule mama alinyanyuka na kutoka na kuniacha nikimsindikiza kwa macho. Baada ya kutoka nilijiuliza yule ni nani aliyekuja kumuuliza mzee Sambi.

Alikuwa mtu wa kwanza kuja kumuulizia mzee Sambi toka nihamie pale, wazo la haraka lilikuwa labda mwenye nyumba ambaye nilielezwa ni mwanamke alikuwa hakai maeneo yale.

Nilijiuliza alikuwa na shida gani ikiwa kodi yake alilipwa ya mwaka mzima. Niliachana naye na kuendelea na yangu.
Muda mfupi baada ya yule mama kuondoka, aliingia mzee Sambi. Kama kawaida nimpokea kwa kujilazimisha huku akinikataza kunyanyuka.

“Aah! Tulia unaenda wapi mpenzi?”
“Mpenzi unafikiri nisipofanya mazoezi nitalemaa si ulimsikia daktari.”
“Asubuhi si ulifanya, pumzika sitaki uteseke.”
“Sawa, lakini kukupokea ni moja ya mazoezi siyo mateso.”

“Haya mpenzi.”
Baada ya kupumzika nilimweleza ugeni uliofika kumuuliza muda mfupi kabla hajarejea.
“Mpenzi kuna mtu alikuja kukuulizia.”

“ Mtu?”
“Ndiyo.”
“Alikuja kuniulizia hapa?”
“Ndiyo.”
“Mmh! Mtu gani aliyekuja kukuuliza hapa?”
“Kuna mama mmoja alikuja kukuuliza inawezekana ni mwenye nyumba wako.”

“Mmh! Ana shida gani namba yangu ya simu si anayo!”
“Mi nitajuaje.”
“Amesemaje?”
“Amesema mtaonana baadaye.”

“Akuacha ujumbe wowote?”
“Hakuacha.”
“Kwani yupo vipi?”
“Mrefu mweusi amevaa kitenge kuanzia juu mpaka chini.”
“Ana mwanya?”
“Ndiyo.”

“Na ana meno mawili ya dhahabu?”
“Ndiyo, una mfahamu?”
“Ndiyo.”
“Ni nani?”
“Achana naye ni mwenye nyumba.”
“Sasa mbona amekuja bila taarifa?”
“Nitaonana naye, kama ana shida lazima atanipigia tu.”

“Mmh! Inaonekana mwenye nyumba hanajipenda sana.”
“Kawaida, baada ya kuniuliza ukamjibu sipo alisema kitu gani kingine?”
“Amesema mtaonana.”

“Basi hilohilo tu?”
“Ndiyo.”
“Mmh! Sawa.”
“Kwani vipi mbona kama umeshtuka?”
“Kawaida tu.”

Sikutaka kumuuliza sana niliamini yule ni mama mwenye nyumba wake. Usiku wa siku ile aliniaga kurudi kwake japokuwa alipanga kurudi kwake siku ya pili jioni.
“Vipi mbona ghafla,” nilimuuliza.
“Hapana kesho nitarudi.”

Pia sikutaka kumzuia kwa vile nilikuwa naye kwangu kwa wiki moja na nusu kitu ambacho kilikuwa hakijatokea, siku za nyuma alikuwa akilala mara mojamoja na kuondoka siku ya pili.

oh, aisee

Starxav
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom