Simulizi: Eliza na ndoa yangu (Kisa cha kweli cha kusisimua)

middotz

New Member
Oct 20, 2023
2
0
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA KWANZA (01)
middotz +255 655 969 973

Ilikua 2012 nilipata kumaliza kidato cha 4. Nilijijua kuwa nitafeli tu kutokana na sababu ambazo ndugu na mama yangu walijua. Kwanza kipindi hicho nilikua naumwa sana na nilikua nanguka gafla sikujua kwa kipindi hicho kama ni presha. Mama yangu alikua akiniasa nisome sana kwa bidii na nihakikishe nafaulu. Sasa kila nikikumbuka hayo masuala ya kuambiwa nihakikishe nafaulu najikuta nanguka ghafla nakupoteza fhamu, kwa wakati huo nilikua bonge na kilo 80.

Mama yangu alikua asikari magereza hivyo niliogopa sana. Nakumbuka kipindi cha mtihan wa moko nilianguka presha nikajikuta nipo hospitali. Baadae dokta aliniuliza kama kuna vitisho vyovyote napewa na wazazi wangu, ni kweli nilikua natishiwa. Baadae mama aliitwa nakuambiwa Kama ataendelea kunisistizia kuhusu shule anaweza kunipoteza, hivyo baadae waliona bora nifeli tu lakini niwehai.

Nilipomaliza kidato cha nne nilikuja kutamani kusomea Hotel Management. Nilipenda hiyo kozi kwakua niliona kwanza rahisi kwa upande wangu pia ada ya kawaida sana kwa wakati huo. Harafu sababu nyingine chuo kilikua karibu na nyumbani.

Niliomba nakuchaguliwa katika chuo kille ambacho kilikua Morogoro, nikanza kusoma pale chuo muda huo ile hali ya kuanguka ishanza kupotea. Sasa katika wanafunzi wote wakike Mimi kwa upande mmoja au mwingine nilikua nateseka sana, haswa upande wa kifedha maana mzazi wangu alikua ananipa elfu 30 nitumie mwezi mzima, harafu tunajitegemea kwa kula wenyewe. Sisemi hiyo ni hela ndogo hapana ila kama msichana bajeti yangu ilistahili kuwa kubwa kidogo kulingana na sababu za hapa na pale nazani hapo mnanielewa. Hivyo hali ikawa ngumu kwangu, nilikua mnyonge sana mbele za wenzangu pale chuoni, kutokana na hayo niliamua kila ijumaa niwe narudi nyumbani ili jumapili niwe narudi chuo, sababu kuu za kurudi ilikua kupunguza gharama nikiwa chuoni.

Maisha yaliendelea hivyo, sasa ikawa wenzangu wakagundua kwa kiasi maisha yangu yalivyo yakinyonge, wakanza kunidharau sana na kuniona mjinga sana. Dhihaka za hapa na pale kwakua tu sikuwa na mavazi mazuri zaid yao, pia sikuwa na pesa. Lakin mpenzi niliyekua nae kwenye mahusiano alikua maskini sana kiasi kwamba kunipa pesa kubwa sana ilikua elfu 5, sio kwamba alikua mchoyo hapana ndicho alicho barikiwa kwa kipindi kile.

Pia ukiachilia mbali kutokua na pesa pia alikua na wivu sana, alikua ananipenda Sana na mimi nilimpenda sana ila suala lake la wivu ilikuja kunichosha mnoo.
Hali hiyo yakua na wivu usio wa kawaida ulikuja kusababisha kuanza kupishana kiswahili mwishoni. Kipindi naanza chuo alikua anakuja kunichukua kila ijumaa nakurudi wote nyumbani, ukiachilia mbali wivu ila nilikua naboreka sana kwa kunichukulia dhaifu kwani aliamini nikirudi peke yangu nitatongozwa, ndio sio tatizo kutongozwa ila kunichukulia nitamkubali tu kila atakaenitongoza sikupenda kabisa.

Basi katika hayo yote kuna rafiki yangu mmoja nilikuja kumgundua kuwa ni mnafiki kwasababu alipenda kutusifia na kupenda jinsi tunavyoishi katika mahusiano yetu na mpenzi wangu japo hatuna pesa, kumbe alikua mnafiki kwasababu alijipendekeza kwa boy wangu na baadae akaanza kumpa taarifa za uongo. Kipindi hicho mimi nipo chuo kama nilivyosema nasomea hotel management ila mpenzi wangu yeye hakua na kazi yoyote ya maana, alipenda sana kucheza mpira pale kijijin na kukaa kijiweni tu kitendo ambacho mimi sikupenda kwasababu niliwaza maisha yetu ya baadae yatakuaje.

Kutokana na hayo nilianza kumshauri mwenzangu kuwa ni heli atafute kazi yeyote au asomee ufundi, nilimshauri hivyo kwa maana mimi nikimaliza kusoma nitapanga chumba na siwezi kuolewa wakati hatuna uwezo. Mwenzangu pamoja na kumshauri lakini hakuitikia kwa kumaanisha ila alikua anaishi akusema nitangalia huku yupo tu kijiweni, nilikua naumia sana maana hajishughulishi kwachochote.

Nilikua na kwaida ya kwenda kwao na kuna baadhi ya siku maalum hua naenda kwao, na mara zote katika siku hizo ilikua hawezi kwenda popote lazima anisubirie kwakua nakua lazima nitaenda tuu. Basi siku moja nilimfuata kwao ila nilishangaaa siku hiyo kwa mara yakwanza sikumkuta, nikarudi nyumbani kwetu, kwao yeye ni kijiji cha pili.

Baadae nikarudi tena sikumkuta kuuliza wakaniambia yupo mpirani. Nilienda hadi uwanjani na kweli nikamkuta uwanjani na ilikua desturi yetu kuwa nikienda mpaka uwanjani huwa lazma atoke uwanjani anifuate lakini sikuile hakufanya hivyo. Sikua na hiyana nilisubiria hadi alivyo toka tukaanza kurudi huku kanuna hakuwa sawa kivile, nilistuka kwakua sio kawaida yake kuwa vile ikanibidi nimulize

“mh! Niambie vip mbona hukunipa jibu umefikia wapi kuhusu kujisomesha?'' alinijibu jibu moja kwa ukali na kwa jazba

''Kama umepata mpenzi mwenye kazi au mwenye uwezo kuwanae tu mimi sipo tayar kuoa leo wala kesho….''

Aiseeee niliumia niliumia sanaaaa yan nilitamani ardhi ipasuke kwanza hajawai nijibu vibaya wala kunidharau hata sikumoja nilibaki kumshangaa nikamjibu sasa uku machoz yanatoka moyon niliapa kuwa

“Mimi Eliza kuja kurudi hapa kumfuata huyu mwanaume sitorudia tena labda sio mimi, kama kumpenda huyu mwanaume imekua fimbo basi liwalo na liwe”

Kiukweli nilikua nampenda sana kwasababu nishawahi kunywa hadi sumu kwajili yake, nishawahi kulazwa hospital mara mbili kwajili yake, na leo tena yajirudie yale yale! Hapana aisee siwez nimeshindwa. Nilirudi chuo lakin usingiz kuupata ilikua shida. Kiukweli nilikua nampenda sana boyfriend wangu na yeye niliamini ananipenda kutokana na wivu wake aliokua ananionyesha.

****

Baada ya kuzozana na boyfriend wangu nikapata nguvu baada ya siku kadhaa. Siku hiyo nikarudi zangu nyumbani, sasa kawaida kila kiwa narudi chuoni kutoka nyumbani lazima nipitie kwa boy wangu lakini sku hiyo sikupitia kutokana na kunidharau na maneno yake. Basi njiani wakati narudi chuoni nikiwa natoka kushuka daladala kuelekea chuo nikaona ghafla kuna gari inapunguza mwendo taratibu huku kama naitwa lakin nikapuzia wala sikuitikia.

Kwanza mimi niliamin wanaume wenye magari wengi wameazima, pili wengi niliamini ni malaya harafu kwakua sikuiwekea maanani niliona kama mkubwa sana kwangu na ukizingati pia sikuzoea kusimamishwa njiani. Niliendelea tu kutembea lakini nikaona mtu hachoki tu, mmh! nikaamua kuzuga kuingia dukani. Nilikaa humo dukani kwa dakika kadhaa badae nikatoka nikajua atakua kakata tamaa kaondoka, Hee! Ghafla kumbe alipaki pembeni akanza kunita tena mmh! nikaona huyu asije akajua ninapo soma ikawa mtihani maana sikupenda usumbufu kabisa.

Nilichofanaya nikamuliza
“Unasemaje?” akanambia
“Tusiongee sana inaonekana unaharaka ila naomba namba yako nikakutafuta”
“Sina simu”

Nilijibu kwa haraka ili niondoke zangu lakini nikaona anatafuta pen ila hakupata nilifurahi sana, aah! Katika kupekua akapata makapen akanipa namba yake kisha akanisihi sana nimtafute............... ITAENDELEA.

SWALI WADADA WEWE ALIYEKUTONGOZA ALITUMIA STYLE GANI KUJA KWAKO!? WAKINA KAKA ULITUMIA NJIA GANI HADI KUMPATA ULIYENAE AU NDIO HII NJIA MAARUFU YA KUOMBA NAMBA TU? TUELEZANE HAPA KWENYE COMMENT.

NUKUU “Muda mwingine mdada anafuatwa na mtu anampuuza puuza kumbe ndio mume wake bila kujua, Siku zote ikipangwa imepangwa tu huwezi kuipangua. Utakwepa kwepa lakini mwishoe pete inanasa kidoleni kama ishara ya pingu za maisha.

Muangalie na mchunguze kwa makini huyo anaekufuatilia ujiridhishe ndio ukubali maana hujui ya kesho unaweza kukubali kwa kumzuga kumbe ndio nitolee, watu wengine huwezi kuwazuga ukikubali umekubali” soma kifuatacho hapa hapa kwa @Middotz_

On X (Twitter) @middotz_
Instagram @middotz_
ksuneo.jpg
 
SIMULIZI: ELIZA NA NDOA YANGU
SEHEMU YA PILI
@Middotz_+255 655 969 973

ILIPOISHIA…………. Hee! Ghafla kumbe alipaki pembeni akanza kunita tena mmh! nikaona huyu asije akajua ninapo soma ikawa mtihani maana sikupenda usumbufu kabisa. Nilichofanaya nikamuliza

“Unasemaje?” akanambia

“Tusiongee sana inaonekana unaharaka ila naomba namba yako nikakutafuta”
“Sina simu”

Nilijibu kwa haraka ili niondoke zangu lakini nikaona anatafuta pen ila hakupata nilifurahi sana, aah! Katika kupekua akapata makapen akanipa namba yake kisha akanisihi sana nimtafute...............SONGANAYO

Baada ya kuchukua ile namba nikaondoka zangu huku nikimuona amesimama na gari yake, nilihisi atakua akinisindikiza kwa macho ila maajabu mimi hata sikumtazama usoni. Basi nilifika hostel nikawahadithia wenzangu jinsi yule mzee alivyonifuatilia, kwanza niliwambia

“kuna libabu limenichelewesha njian na kigari chake”

Basi tukacheka pale baadae nikachukua ile namba nikaweka kwenye mkoba wang.

Mkoba ambao nilikua nimetundika ukutani ndani yake nilijaza namba na business card nilizopewaga na wanaume walionisimamisha njiani lakin sikuwahi kuwatafuta. Kwa kweli nilikua nimemzoea boyfriend wangu na sio kumzoea tu ila nilikua nampenda mnoo japo alianza kunizingua.

Basi siku ikaisha ikafika usiku nikalala zangu, sasa usiku kila nikigeuka usingiz hauji nikawa nakumbuka tu yule mtu jinsi alivyonipa namba, mmh! Nilistuka Sana niliamka nikawaza Sana

''MMH! Mbona wanaume wengi walinipa namba lakin sikuwahi kuwawaza hivi?''

Baada ya kuona sipati jibu niliamua kuwaamsha wenzangu. Waliamka nikawambia wakaanza kutoa ushauri kila mmoja

''Eliza huenda uyo ndo Mume wako Mungu kakupangia'' Nikacheka nikisema

“Mwanaume mwenyewe mweusi”

Kipindi kile nilikua siwapendi wanaume weusi. Basi nikawambia kesho nitajaribu kumtafuta lakin sio kwa simu yangu kwasababu nilimuambia sina simu.

Tukakubaliana pale na Halima (huyu ni yule rafiki yangu anayejifanya napenda mahusiano yetu na boyfriend wangu) akaniambia usijali utatumia simu yangu.

Basi tukalala pale ilivyofika asubuhi tuliamka nakufanya usafi nakumbuka ilikua siku ya jumapili. Tulivyomaliza usafi tukiwa tumeoga tayar Halima akaniuliza

''Vipi humtafuti yule mtu?''

''Mh! Basi ngoja nimtafute'' nilimjibu, tukapiga simu (Yaani najuta kwanini nilimtafuta bora ningechana namba tu)

***

Nikampigia akapokea akauliza “Hlw naongea na nani?” Nikajibu

“Ni mimi Agness” nilidanganya jina, akauliza yupi

“Nikumbushe?”

“Ulinipa namba jana usiku!” (Yani ilikua kwenye simu tu lakin alifurahi sana) Basi akanza kuuliza maswali mfululizo

''Ahaa! ok! Niambie za asubuhi? Umeamkaje? Upo wapi kwasasa? Naweza kukuona? Umekunywa chai?”

Wakati wote huo nilikua nikijibu maswali yake, lakin alikua mtu asiyeamini kuwa ningemtafuta kwasababu wakati akinipa namba nilikua natabasamu mithili ya mtu anayepuuzia na kweli sikupanga kumpigia. Basi nikamjibu

“Nipo hostel na unaweza kuniona harafu bado sijanywa chai” (nikajifunza kauongo) akanimbia

“Nipe dakika 10 uanze kunielekeza”
“sawa” Nikajibu

Nikamwambia rafiki yangu anakuja sijui itakuaje! Tumbo likanza kunguruma kama naendesha kwa uoga sikuwahi simamma na mwanaume njiani au kuniita sehemu zaid ya boyfriend wangu. Dakika 10 zilifika akapiga nikatoka na rafiki yangu Halima maana simu ilikua yake na pia nilitaka aone jinsi ninavyotekwa nilikua muoga sana. Basi nikamuelekeza hapo ila hakuelewa hadi nikaanza kuchukia ila baadae nikamuelekeza kwa njia nyingine ya kutokea stand, kwel akaelewa akafika tukaonana.

Alikuja na gari ya kifahari ilikua tofauti na ile ya jana yake usiku, sikujua ni gari ya aina gani lakin pia mim sikujali gari wala nini. Basi wakati namfuata alikua ananichora tu ninavyotembea na tege langu. Nikafika nikaingia kwenye gari, nilishangaa tofauti namafikirio yangu ya jana kumbe ni kijana bwana ila alikua na aibu sana kwani hakuweza hata kuningalia usoni.

‘‘Hapa unafanya nin?''

''Nasoma'' nilijibu ''nimerisit' niliongezea jibu (nilidanganya)

“Ahaa! kumbe mwanafunzi?”nikajibu
“ndio” akauliza

“kidato cha nagapi?” Nikajibu

“Cha pili”, akaniambia

“Ok! Jitahid sana kusoma naamin mimi sitokua sababu ya wewe kufeli”.

Akaniambia “Nilikuja tu kukusalimia kesho nitaenda sehemu ila nikirudi nitakuja tena kukusalimia na nimekuletea vitafunwa hapa” (alileta mkate mkubwa, mawaziwa ya nido, Blueband, sukari kg zaid ya 5 na box la majani ya chai)

Nilibaki nashangaa tu. Basi nikamshukuru sana akanipa elf 5 akaniambia ya vocha nikashukuru sana. Kabla ya kushuka kwenye gari nikajikuta namkiss kwa nia ya kumuaga maana nilishazoea kwa boyfriend wangu.

Alizubaa akaniangalia nilijikuta navutiwa na macho yake flan ivi Amazing kwa kweli niliyapenda sana, na hapo ndo nilifaid sura yake. Nikashuka nakuelekea zangu hostel, Lakini kabla sijafika nikakutana na mwalimu wangu wa mapishi.............. ITENDELEA

JE MWALIMU WAKE ATAMFANYAJE NA KIFURUSHI CHAKE? USIKOSE KIFUATACHO HAPA KWA @Middotz_

NUKUU: “Siku zote mahusiano huanza kwa namna ya ajabu sana ambayo kila mmoja anajikuta tu yupo kwenye mahusiano na wakati huo yashapamba moto hata kujinausua huwezi tena.

Mara nyingi wakati huu unanza kusema mbona sijamchunguza na kwakua moyo ushazama huwezi kuwaza baya juu yake, huwazi akikusaliti, hufikirii kama alikua na mahusiano mengine ila hapo unawaza tu kwakua yeye anakupenda na wewe unampenda.

Ukiwaza matokeo chanya ni lazima pia Uwazie matokeo hasi hivyo ndivyo ilivyo kwenye POSTIVE lazimapatakua na NEGATIVE pia. Ukiwaza unapendwa sana waza pia kama anakudanganyaitakuaje”
FB_IMG_1706123361331.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom