Simulizi: Mzimu uliorejea

Simulizi: Mzimu uliorejea

MZIMU ULIOREJEA

Sehemu - 55 -

Ilipoishia...
Kwak Martin!
Bila shaka u mzima,nafrah kwa ilo!...
Najua unashangaa juu ya barua hii ya kimaajabu ajabu usishangae kwa ili!
Dhumuni la barua hii ni kikueleza juu ya upatikanaji wa hazina ya marehemu baba yako

#Songa_nayo_sasa....
Mara ya mwisho kaka yako alikwambia urudi kijijini ukujua pa kuanzia!
Nenda katika kijiji chenu mtafute mganga Nwalau Nwalau yule yule unayemjua yupo kijijini kwa dhihara mwambie waitaji utajiri
Kuna masharti atakupa yatakayokufikisha katika hazina ile ya baba yako
Kumbuka hazina ile inalindwa na mizimu kuwa makini katika masharti na ukikosea kidogo kifo ni haki yako
Wengi walioenda hawakurudi
Ila kwa kuwa ni haki yako naimani utashinda...
Kila la kheri
Ni mimi

Zena Kureysh

Martin akashusha pumzi ndefu,akairudia kuisoma ile barua Mara mbili iliandikwa vile vile akaiweka mfukoni
Ni wazi alikuwa amechanganyikiwa
Akaingiza mkono mfukoni na kuitoa
Akapigwa na butwaa,barua aikwepo zaidi ya ile 10000

Macho yakamtoka...
Akuona haja ya kumsimulia mtu
Ni yupi angemuelewa achia mbali kumuamini?!
Akaendelea na kazi raha ikiwa imemtoweka,akipania kesho yake kuelekea kijijini...na ndivyo ilivyokuwa

***********************************

Hali ya kijiji kile ilibadilika,ukame ulitawala,kwa kuwa Martin alikuwa na kiakiba kidogo akachukua chumba katika nyumba vya wageni
Akutaka kwenda nyumbani kwao mwanzo alipania mpaka amalizane na kazi ya kuikomboa hazina ile ndo angerudi kwao...

Kwa kuwa alifika kijijini usiku alipumzika na hasubui alianza kuyatafuta makao ya bibi mganga yule
Kijijini kile kilikuwa ni kidogo akupata tabu kumpata...
"Hahahahaha waitaji utajiri?! Utaweza?!"
"Ndio bibi"
"Hahahaha kuna hazina ipo katika mapango ya maajabu uko milimani ni wajibu wako kuifuata wengi wameenda hawakurudi ni hatari ha ha ha ha "
"Nipo tayari bibi"
Mganga yule akamtumbulia macho Martin,macho ya mshangao
"Ok kama upo tayari ntakuelekeza,hayo mapango ntakupa dawa ukifika hapo utajipaka usoni na mapango Yale yatageuka na kuwa nyumba ya kisasa kuna ulinzi mkali wa mizimu tafuta njia yoyote uingie huko
Mizimu ile inahisia sana unaweza ukaendaaa...."

Mganga yule akamalizia na kumruhusu Martin kutoka kwa kinyume nyume
Martin akawa tayari kwenda katika mapango Yale
Aliyajua fika kwani anakumbuka wakati wakiwa watoto walikuwa wakikatazwa kwenda katika mapango hayo waloyaita 'mapango ya mizimu'
Pia ndiyo yalikuwa mapango yalotambikiwa na waganga na wazee kwa mila zao
Pindi ukienda kwa nia ya kutambika au kuangalia hayakuwa na shida yalikuwa kawaida tu
Ila ukienda kwa nia ya Hazina mizimu ile ilijua na kukugeuza kitoweo
Ni vipi Martin angeweza kuikomboa hazina ya baba yake?!
Akazidi kusonga mpaka katika pori lile,akawa anaelekea maeneo ya mapango Yale.....

NDANI YA MAPANGO

Walinzi wa falme hii kuna binadamu anakuja,kwa ajili ya hazina kuweni makinii,ulinzi uimarishwe
Sauti kubwa ilisikika katika masikio ya walinzi wale wakawa tayari kumkabili kiumbe yoyote ajaye...
Martin akujua juu ya hilo,yeye alizidi kusonga moyoni akiwa na amani
Baada ya kufika katika mapango Yale akaitoa dawa ile na kujipaka usoni akinuidhia maneno machache aloambiwa na mganga na ghafla Mbele yake pakatokea jumba La kifahari
Walinzi wakiwa pembeni yake,walinzi waloshika silaha ambazo akuziona kabla
Wazo kwamba ataingiaje likamvaa
Uwezo wa kuingia kule aukwepo kabisa...

Ghafla akaguswa nyuma alipogeuka tuu
Akaachia yowe,yowe lililowashtua mpaka walinzi wale wa Mbele
martin alikuwa hatarini tena katika mikono hatari ya viumbe vyenye uchu....akabaki akitetemeka akisubiria miujiza
"Wewe ni nani na unataka nini?!"
Akaulizwa swali ambalo katu akuweza kulijibu akikumbuka sharti alilopewa juu ya kutofunguwa mdomo wake
"Na kuuliza wewe ni nani?!"
Akapachikwa swali lingine kabla maumivu makali ayajatambaa katika mwili wake
Ni mkia wa taa alochapwa nao....
"Tuna kuuliza tena wewe ni nani na unataka nini?!"
"Mimi ni Martin na nataka Hazina"
Akavunja masharti pasina mwenyewe kujielewa akaropoka
Viumbe vile vilistaajabu vikamnyanyua mzoba mzoba mpaka ndani kabisa ya jengo lile katika jiko palipokuwa na sufuria kubwa ilochemka mafuta wakamtupa
akaachia mayowe huku akiporomoka kushuka chini ya mafuta Yale Yalochemka
Akiacha juu viumbe vile vikishangilia kwa kupata nyama ya kukaanga

CHINI YA ARDHI

HIMAYA YA WAFU

Ilikuwa ni katika hekalu la kifalme,hekalu lililotengenezwa kwa almasi na dhahabu tu!
Hekalu lililolindwa kwa ulinzi mkali
Ndani ya hekalu lile katika sebule nadhifu aliketi Mzee wa makamo kichwa chake kilijaa mvi...

Pembeni yake aliketi mwanaye aliyekuwa kava joho la kifalme na kakaa katika kiti cha mfalme pembeni yake walikwepo walinzi shupavu wenye silaha za jadi,silaha ambazo katika macho ya kibinadamu azikuleta maana kabisa
Walishika magamba ya konokono,na zaidi ya hapo hata viungo vyao vilikuwa ni silaha tosha

"Baba lazima nirudi duniani nikamchukue mpz wangu baba siwez ishi mwenyewe humu baba"
Jb alipeleka ombi lake kwa baba yake...

Basi usikose sehemu ya 56...
 
MZIMU ULIOREJEA

Sehemu - 56 -

Ilipoishia...

"Baba lazima nirudi duniani nikamchukue mpz wangu baba siwez ishi mwenyewe humu baba"
Jb alipeleka ombi lake kwa baba yake...

Songa nayo pole pole...

"Vizuri sana mwanangu ila mwenzako kwa sasa kaokoka ni vigumu kumsogelea!"
"Hapana baba Mimi ni shujaa na kama ni shujaa yule ana kiumbe changu ndani ni lazima nimchukue kumleta huku kuzimu"
"Sijakataa si una kumbuka vijakazi wako tulowatuma duniani wakamuue Maimuna wailete roho yake aje akiwa mfu awe miongoni mwetu unakumbuka kilichowakuta?!.....

Jb akarudisha kumbukumbu............
" pepo maiti nawatuma duniani mkaakikishe mnarudi na roho ya mpz wangu Maimuna ilobeba kiumbe changu,nawaamini na najua amshindwi na kitu"
Baada ya jb kuongea vile roho zile zikatoa heshima sambamba na kutoweka eneo lile...
Vilikuja kutoka juu ya makaburi yao,ilikuwa ni vigumu kwa binadamu wa kawaida kuviona vikatoweka tena vilikuwa vikimsaka MAIMUNA....

BARABARA YA KIBOROLONI
PEMBEZONI YA KANISA ANGlKANA

Wadada warembo wawili walikuwa wakipita njia huku wakiwa bize kwa stori,mmoja hapo akiwa ni Maimuna mtoto wa kamishna na mpz wa Jb
Wakiwa maeneo ya uwanja mkubwa wa kanisa wakiendelea na safari yao ghafla kizunguzungu kikali kikamvaa Mai,na kumpeleka chini
Watu wote waliokuwa katika kongamano lile la dini wakageuza vichwa vyao kumwangalia mtu yule alodondoka na kupiga makelele
Mchungaji akaagizwa apelekwe Mbele yake,bado Mai alilia moto vijana kadhaa wakambeba na kumpeleka Mbele ya mchungaji
"Ni nani nyinyi?!" Mchungaji yule akamuuliza Maimuna
"Sisi ni pepo maiti "
"Mnataka nini katika mwili huu"
"Roho yake"
"Mmetumwa na nani?!"
Maimuna akabaki kimya
Mchungaji akauliza tena mmetumwa na nani?!
Pepo wale bado hawakuwa tayari kuongea...

"Sasa nawahamuru kwa jina la Yesu christo mwachieni huyu Dada na mrudi mlipotoka toka toka kwa jina la yesu christo toka...."
Maimuna akazidi kupiga kelele moto,moto ni wazi hakuwa yeye ni pepo wale walotumwa na jb
Baada ya dakika chache Maimuna akatulia na pepo wale wakatoka
Alipozinduka alikuwa mzimaaa mzima wa afyaaa
Waumin wakaanza kuimba
"Mwambie farao nimeokoka sitorudi nyuma tena naenda kwa bwana...
Mwambie farao nimeokoka sitirudi nyuma tena naenda kwa bwana"
Kwa nzia siku hiyo Maimuna akaokoka na kuwa mwinjilisti mzuri katika kanisa lile

KUZIMU

HIMAYA YA WAFU

Ghafla mapepo wale wakiwa wanapiga kelele miili yao ikiwa imeungua kwa kuchomwa moto ikatokea Mbele ya jb na baba yake
Wakatoa heshima kwa mfalme na kuwaeleza kilichowakuta...

"Ina maana Maimuna kaokoka?!"
Jb akauliza kwa mshangao
"Yah ndo jibu hilo na kiumbe chako kipo hatarini"
"Hapana baba nitarudi duniani kupambania damu yangu haiwezekani"
Akazidi kumsisitizia baba yake baada ya kukumbuka akatingisha kichwa kwa masikitiko makubwa sana
"Mwanangu jb yule sasa ana nguvu kuliko wewe au kuliko sisi kitabu akishikacho akikunyooshea kuna uwezo mkubwa wa kupoteza maisha"
"Ila kumbuka ananipenda baba"
"Alikupenda kipindi ulipokuwa ujajifunua kwake kama mfu ila sasa si rafiki yako tena"
"Hapana ntaenda duniani kuikomboa nafsi yangu ntajivunia na nini kama mfalmeee....

Kabla ajamaliza kuongea kikasikika king'ora kikipiga kelele
Ishara ya hatari
"Kuna nini tena?!"
Baba jb akiwa anatetemeka akaoji
"Hata sijui" jb akamjibu
Walinzi walikuwa tayari kwa lolote na ghafla......

Na ghafla viumbe vyeusii tii,vyenye pembe katika vichwa vyao vikatokea
Vilikuwa kama vitatu,kutokea kwao muda huo huo vilishawekwa kati na walinzi shupavu wa Himaya ya KUZIMU

Ila baba yake Jb alipoviangalia akavitambua na kukumbuka miaka kadhaa nyuma wakati akiweka mazindiko katika hazina yake
'Si ruksa Mali hii kuchukuliwa na kiumbe chochote isipokuwa watoto wangu wawili Brayson au Jb au mke wangu! Kiumbe chochote kitakachoitaji kiangamizwe katika sufuria la mafuta"
Baada ya Mzee yule kutoa maelezo yake na kuachia mizimu kulinda wazo Fulani likamjia
Kwa kuwa kazi aliitoa kwa mzimu mkuu wa pango lile,alijua kwa vyovyote watakao kuwa lindoni ni mizimu tofauti tofauti kutokana na miaka itakavyoenda
Na si wote watakaowajua wanaye!,wazo flani likapita katika kichwa chake
Kuweka ulinzi mwingine wa siri ambao mizimu ile isingejua uwepo wao
Pia hii ingesaidia hazina ile kuwa salama zaidi!
Na ndio akavipachika viumbe vile vitatu,viumbe ambavyo vilikuwa Mbele yao muda huo vikija kwa king'ora
"Waacheni nawafahamu"
Baba jb akatoa amri,walinzi wake wale wakatawanyika na kurudi kila mmoja eneo lake
"Ehe kipi kikichotokea katika hazina yangu ewe viumbe Wang watiifu"
"Mtoto wako Bry yupo hatarini"
"What?!!"
Jb na baba yake wakashtuka kwa taharifa zile baba Martin akamwangalia jb kwa kumsuta...

"Nisamehe baba!,nilipitiwa na kichwa changu kilikuwa na mawazo juu ya malkia wangu nikaacha kufatilia maisha ya mdogo wa ngu juu ya kuifata hazina ile
Mara ya mwisho nilimuachia kazi zena binti Kureysh amwambie mahali ilipo hazina
Baba Martin akusema kitu akanyoosha mkono wake wa kuume juu katika ukuta na kutoa shoti sambamba na kuachia cheko Kali
Katika ukuta ule ikaonekana picha ya Martin akiwa kabebwa mzoba mzoba na kupelekwa katika sufuria lichemkalo moto akatupwa mule

" noooooooo"

Wote wakapiga kelele,ila baba mtu akaunyooshea mkono sufuria ile na ghafla Jb kule ndani akanata
Akaunyanyua mkono wake kwanguvu kwenda juu,na ghafla Jb akatupwa juu ya sufuria ile...
Baada ya tukio lile mzee yule akatoweka na kuacha walinzi na Jb wakibaki na mshangao...
"Lazima nirudi duniani kumkomboa malkia wangu"
Jb akala kiapo,mapenzi yana nguvu,akumuwazia kabisa mdogo wake...

Yeye alikuwa kwa Maimuna muda ule ule baada ya baba yake kutoweka naye akatoweka
Viumbe vile vilivyobaki vikajua kamfata baba yake kumbe kayafata matatizo....

Itaendelea...
 
MZIMU ULIOREJEA

Sehemu - 57 -

Ilipoishia...

Yeye alikuwa kwa Maimuna muda ule ule baada ya baba yake kutoweka naye akatoweka
Viumbe vile vilivyobaki vikajua kamfata baba yake kumbe kayafata matatizo....

#Endelea
Matatizo makubwa ambayo ayakuwepo katika uwezo wake....

************************************

HIMAYA YA MAPANGONI

PALIPO NA HAZINA

viumbe vile baada ya kumshusha Jb katika sufuria lile vikaachia cheko
Mate ya uchu wa kula nyama yakawatoka,ni takribani miaka mitatu awakuonja nyama katika pango lile

Wakati wakitingisha vichwa vyao ghafla tetemeko Kali la ardhi likawatetemesha na ghafla macho yao yakatua ndani ya sufuria ile...
Walishughudia kiumbe kile kimenata chenyewe,wakiwa bado wametawaliwa na bumbuwazi wakakishughudia kikirudi juu
Wakatokwa na mayowe jambo kama ilo alikuwahi kuwatokea kabla
Wakajua wameshaingiliwa na hadui wakawa tayari kukishambuliwa kabla awajapata amri ya kuachia Mara moja kutoka kwa mfalme wao
Mfalme wa mapango Yale!
Ni baada ya baba Martin kupotea akaja kutokea ndani ya mapango Yale Mbele ya mfalme mwenzake alompa dhima ya kuilinda hazina ile
"Nadhani umesahau juu ya watu wa aina tatu niliokwambia ndio walostahili kuimiliki au kuwa na ruksa ya kuchukua hazina ile"
"Salam kwanza baba Martin!"
"Salam gani wakati vijakaz wako wanataka kumtafuna mwanangu ndo maelewano yetu? Kwa nini ukuwapa taharifa ?!"
Mfalme wa mapango Yale akashtuka...

Akayatoa macho yake makubwa na kutazama eneo lilipo sufuria lile akashughudia vijana wake wakiwa tayari kumshambulia Martin akapaza sauti kuwaamrusha waache
Nao wakamtwiii
"Naomba msamaha Mimi kaka sikuwapa taharifa juu ya kuja kwa kijana wako lakin nawe swaiba ni msiri sana"
Wote wakaangua kicheko wakielekea maeneo alipo Martin

*************************************

*************************************

Jb alikuja kutokea katika nyumba aloishi Maimuna,ghafla akashtuka baada ya kuiona ni bahari na nyumba aikwepo
Akaachia kicheko hafifu,alijua ni mchezo,akanyoosha mkono wake katika bahari ile tayari kwa kuipiga kombora
Miale ya radi ikapiga kutoka mbinguni Jb akarushwa usawa wa bahari ile
Yowe likamtoka
Maji Yale yalikuwa yakichemka....

Kwa Mara nyingine tena Jb akawa kaingia SEHEMU ambapo siyo
Ghafla akaanza kuzama chini ya maji Yale,akazidi kupiga mayowe
MUNGU tu aliamua kumuonesha nguvu zake azipambanishwi na kitu chochote
Jb alipiga kelele akinyoosha mikono yake juu,ghafla akatupwa nje ya bahari ile...

Mwili wote ulilowana kwa jasho,baada ya kutupwa muda ule ule akatoweka kurudi katika ulimwengu wao
Bado mawazo yalikiumiza kichwa chake!,ni vipi ataweza kimmiliki Maimuna?!
Na kiapo alishakula,alikosa raha,
"Ina maana Mimi kwa MUNGU ni hadui?!,iweje asiwe upande Wang!"
"Yah! Wewe kwake ni hadui,ni lipi jema ulilomfanyia wewe amewafundisha kusamehe wewe umeangamiza viumbe vyake vingapi?!
Kwa nini ulipize kisasi?!"
Kuna sauti ikamjibu,sauti takatifu,Jb akazidi kukosa raha
"Hapana,ndiyo natakiwa nifanye kitu kumrejesha hapa May lazima"
Akaachia tabasamu dogo lililobadilika na kuwa cheko...
Alishapata jibu!,kipi cha kufanya...
Sasa alihisi MAY ni wake ikiwa atafanya vile alivyowaza....
Ni nini?!....

*************************************

Martin alishangaa viumbe vile vikitawanyika tena vikionekana kuwa na waswas,ghafla wazee wawili wqkatokea...
Mmoja akiwa na nguo za kifalme, na vile viumbe vyote vikatoa heshima,hakuwa na shaka kuwa yule ndo mfalme wao
Macho yake yakadondokeq kwa Mzee mwingine,akashtuka...
Sura yake ilishabiana vikubwa na ya mtu yule,alikuwa ni baba yake...
"Dah akuna haja hata ya kuntambulisha kwa mlivyofanana,ni mwanao copyright"
Yule alovaa nguo za kifalme akasema maneno Yale yalomshtua Martin,alihisi yupo ndotoni baba yake?!
Akabaki kamtumbulia macho Mzee yule kwa mshangao,akubahatika kumuona akiwa na akili kwani yeye akiwa na miaka mitatu kasoro baba yake yule ndo alikufa vitani...
"Karibu mwanangu na pole kwa matatizo yalokutokea duniani amini sasa yamefika mwisho...

Aliongea baba Jacob, akimnyanyua na kwenda sehemu nzuri ya kuongelea...

Martin akakabidhiwa rasmi hazina ile,akionywa kutokumuonesha au kumruhusu mtu mwingine kuja kuichukua labda mwanae au mke wake

ITAENDELEA...
 
MZIMU ULIOREJEA

Sehemu - 58 -

Ilipoishia...

Aliongea baba Jacob, akimnyanyua na kwenda sehemu nzuri ya kuongelea...
Martin akakabidhiwa rasmi hazina ile,akionywa kutokumuonesha au kumruhusu mtu mwingine kuja kuichukua labda mwanae au mke wake

#Endelea...
Akaoneshwa njia rahisi za kupitia,kuipata hazina ile....

BAADA YA SIKU CHACHE

Martin alirudi kwenye ile hadhi yake,tena zaidi akimiliki kampuni ya uuzaji na usafirishaji madini
Akawa mmoja wa matajiri wakubwa nchini Tanzania,japo mpaka muda huo akuwa na mke na akutaka kukurupuka,
Baada ya kufanikiwa alienda yalipo makazi ya mama yake,japo awali alimuogopa ila kwa kuwa hakukuwa na nguvu za Giza alimwelewa na mama akamuomba mtoto msamaha
Martin akawajengea nyumba nzuri kijijini,maisha ya mama yake yakabadilika,akawa akienda kijijini anafikia nyumbani kwa mama yake
Kabla ajaelekea msitu wa panda..
ambapo alipitia njia alizoelekezwa na kuchukua kiasi cha hazina,...na kurejea nacho mjini
Akazidi kujipaisha,wanawake mbalimbali wakijigongesha akiwemo mke wake alomsaliti siku kadhaa baada ya kufilisika
Martin hakuwa tayari kwa ilo,alifunga akimuomba MUNGU ampatie mke mwema....
Kila umuombapo yeye kwa nia dhahiri ukujibu muda huo huo,siku chache baadaye jibu lake lilapatikana....

Kivipi?!!!......

************************************

Mwanamke yule alikuwa mchafu ombaomba,mawazo yalijaa kwenye kichwa chake alitembea pasina kuangalia barabarani
Gari la kifahari,Martin alikuwa ndani yeke akiwa anasinzia,dereva naye alikuwa mbali kimawazo katu akumuona binti yule alikuja kushtuka akiwa hatua chache kumfikia na alipojaribu kupiga breki alishindwa
Akamgonga binti yule ombaomba na kumtupa hatua kadhaa,akiachia yowe
Martin akashtuka na kuyatoa macho kwa mshangao,
"Godluck my frandy umeua?!"
Martin akapaza sauti,God akusema kitu mikono aliweka kichwani,
Martin akafungua mlango na kutoka akipishwa njia na watu waloanza kuzingira eneo lile,akausogelea mwili ule...

Ghafla Martin akapiga yowe baada ya kuiona mwili ule,aliufahamu fika...
Martin akatoa macho ya mshangao,mdomo akauachama wazi,ishara ya mshtuko
Akamuinamia mtu yule na kumuinua kidogo akaweka mkono wake katika shingo yake...
"Ja..ja...Janeth my d ni w..ew"
Akapaza sauti,Dada yule akayafungua macho yake kwa shida
"Ni na..ni we...we" huku akijitahidi kukuumbuka akamuuliza,ni wazi sauti ile aikuwa ngeni maskioni mwake
Cha ajabu sasa hata raia walio onekana ni wenye hasira Kali walipigwa na butwaa baada ya kuona wawili wale wanajuana
Alikuwa ni Janeth yule yule ambaye Martin aliichakaza familia yao kwa kutembea na mama mtu hadi watoto miaka kadhaa nyuma,wakiwa matajiri Leo hii mbona Kurwa au Janeth alikuwa katika hali ile?!
Hakuwa na muda wa kuliuliza lile baada ya kushtushwa na minong'ono ya watu ndo akatambua mgonjwa alistahili kupelekwa hospitalin

Akisaidiana na God ambaye alikuwa ndo dereva wake,wakampakia katika gari na safari ya kuelekea hospital ikaanza dakika chache walikuwa katika hospital kubwa ya kcmc kwa kuwa Martin alikuwa na hela Janeth akapewa chumba cha 'vip' chenye huduma nzuri
Hali yake ilikuwa ni mbaya na alikuwa katika nusu kaputi,mwili ukichunguzwa aliitajika kufanyiwa operesheni ya kiuno kwani kilivunjika....

'Jamani Janeth ni kipi kilimkuta?' Martin alijiuliza pasina majibu,akubanduka hospitalini pale....

*********************************

Maimuna alimaliza kula baada ya kumaliza akaiendea "biblia" yake na kuichukua akaanza kuisoma taratibu,na kukariri baadhi ya vipengele,masaa mawili yakakatika akiwa pale kwenye kochi
Ghafla nywele zi kaanza kusisimka ni baada ya Jb kutokea nje ya nyumba yake na kuiona bahari
Kitendo cha nywele kusisimka na woga kumtawala kikamfanya aanze ibada Mara moja akaanza kukemea,alijua lazima kutakuwa na viumbe vibaya
Ni wakati akiomba Martin akapiga pigo moja lililomvuta mpaka katika maji Yale na kuanza kuzamishwa,katika maskio yake Jb alimsikia Mai akiomba kwa kukemea...

Ghafla akaacha,alikuwa kamaliza maombi, ndo pale Jb aliporudishwa nje ya ziwa lile lenye maji ya moto,hamu ikamuisha Jb akatoweka
Amani ikautawala moyo wa binti yule,furaha ikarejea alitambua wazi m'baya wake kakimbia japo akujua ni kiumbe gani mchawi,shetani,mzimu au pepo wachafu

Itaendelea...
 
MZIMU ULIOREJEA

Sehemu - 59 -

Ilipoishia

Amani ikautawala moyo wa binti yule,furaha ikarejea alitambua wazi m'baya wake kakimbia japo akujua ni kiumbe gani mchawi,shetani,mzimu au pepo wachafu

Songa nayo sasa...
Akaimba wimbo wa mapambio na kukiendea kitanda chake akajilaza...
"Nahisi kuna msukumo Fulani katika moyo wangu wa kumtumikia MUNGU na kuwa mchungaji lazima kesho nikaongee na mchungaji wangu"
Akajiwazia,ndio hamu kubwa ya kumtumikia bwana ilimuingia,aliitaji kuachana na kazi ile ya u polisi...kila tarehe yake ya kwenda zahanati ilipofika alienda na mtoto wake aliendelea vizuri alifurahi kwa ilo....

UPANDE WA PILI KWA MCHUNGAJI TIMOTHEO

Mchungaji wa kanisa anglikana,bwana Timotheo siku hii alikuwa peke yake katika kanisa lake akiendelea kuomba,alifumba macho yake akaomba na mwisho wakati anamalizia akasikia sauti nyuma yake ikiitikia ameen

Sauti nyororo,sauti nzuri,akageuza kichwa chake nyuma kumwangalia yule alooitikia akayatoa macho kwa mshangao,alikuwa ni binti Mrembo ambaye akuwa miongoni mwa watumishi wake
Akumjua kabisa
Akabaki kaduwaa

"Asifiwe Christo"
Dada yule akamsalimia,...akiacha kulitaja jina la yesu
"Milele amina karibu katika kanisa langu"
"Asant mchungaji nimekuja naitaji maombi mchungaji sina raha katika ndoa yangu nimeenda hospitalini kupima sina tatizo nahis tatizo lipo kwa mume wangu tupo katika ndoa kwa miaka 3 atujabahatika kupata mtoto kwa waganga nimeenda sijafanikiwa nisaidie mchungaji....."

Mchungaji yule akamwambie apige magoti naye akaanza kumuombea,wakati akiendelea na maombi mlango wa kanisa lile ulifunguliwa akaingia binti mkononi akiwa na biblia yake

Alikuwa ni maimuna kila hatua alokuwa akipiga nywele zilimsisimka,mapigo ya moyo yaliongeza kasi ya upigaji
Ni wazi kuwa kule ndani au nje ya kanisa lile apakuwa salama

Ni kwanin?!

Ndani ya kanisa akuamini kwa kuwa alijua kitu kibaya,pepo mchafu aingii katika nyumba takatifu wazo lile likamsukuma kuamini pepo mbaya yupo nje
Msukumo mkali ukamsukuma kurudi nje,yah ni msukumo wa shetani, ila msukumo mwingine ukamwambia aendelee na safari....

Ila akaona kutoka ndo vizuri zaidi!,
Kumbuka ndugu msomaji!
MUNGU baada ya kumuumba Adamu,na kuwaambia malaika wote wamsujudie adamu wote wakamtwii MUNGU wakamsujudia nabii adamu kasoro ibilisi naye pia kipindi icho alikuwa ni malaika aliemtwii MUNGU
Akakataa katakata na kusema
"Mimi umeniumba kwa moto huyu umemuumba kwa udongo,iweje nimsujudie hali ya kuwa utampeleka katika dunia na kuiharibu kwa kumwaga damu?!"

Baada ya ibilisi sheitwani kwenda kinyume na maamrisho ya ALLAH
MUNGU akamfukuza na kumuweka mbali na Rehema zake,na kumwambia wazi atakuwa katika moto wa jehannam,hapo ibilisi alicheka akamuomba MUNGU basi ampe nafasi ya kuwahadaa binadamu ili apate wafuasi wa kuingia nao motoni

MUNGU alimkubalia,hivyo ibilisi alitumia njia hiyo kuhadaa katika nafsi ya MAIMUNA ibilisi alimsihi arudi nje,lakini MUNGU alimsihi aendelee Mbele
Mai akiamini pepo awezi kuingia kanisani na uishia nje akaona atoke

Kosa kubwa sana!...

kitendo cha kutoka tu,binti yule aliyeitaji mtoto padri aliyeendelea kuomba akajifanya amepandisha mapepo akajidondosha
Na kujifunua akaanza kupiga kelele padri akafungua macho
Akapatwa na mshtuko,macho ya tamaa yakamvaa,ibilisi akamzidi nguvu
Akabaki ameganda....

Wazo Fulani la kumwingilia binti yule ambaye akumuona kabla likamjia naye akafanya ivyo.....
Ndani ya lile lile kanisa lake
Ghafla alama ya 666 ikajichora katika paji lake la uso
Akuiona,wakazidi kufurahia tendo lile mpaka walipotosheka
"Nenda na utapata mtoto"
Mchungaji yule akamwambia Dada yule alokuwa muda wote akitabasamu
"Asante mchungaji"
"Jina ulisema unaitwa nani vile?!"

"Zena bint Kureysh"

"OK"
Zena akavaa vizuri na kuanza kuondoka,ghafla akaachia cheko,cheko lililomshtua mchungaji timotheo ,na kutoweka
Mchungaji akashtuka na kutoielewa hali ile...bado alama 666 lilikuwa katika paji lake la uso
Baada ya mwanamke yule kutoweka ghafla,mchungaji yule akaanza maombi,..ya kukemea
Nguvu aliyokuwa nayo kabla ajafanya mapenzi na binti yule hakuwa nayo tena...

Akukawia kugundua hilo
Tayari ibilisi alishamuorodhesha katika watu wake,ilikuwa ni furaha ya JB,kwani kazi yake iliendelea vizuri...

Hata jumapili katika ibada alipopanda ilikuwa ni tofauti na siku zote,taratibu waumin wakaanza kupungua na kumkosesha raha mchungaji yule....
Siku hiyo akiwa katika chumba chake kidogo,ofisi alitembelewa na mgeni
Alikuwa ni jb,akakaribishwa vizuri na kuketi...

"Mimi kwa jina naitwa Jacob nimekuja kwako mtumishi nipate kukurudishia nguvu zako ikiwa utakubaliana na matakwa yangu"
Mchungaji alashtuka,na kumkazia jicho
Aliitaji sana kurudi pale alipokuwepo,
"Matakwa gani muheshimiwa?!"
"Saf sana,kuna mtumishi wako mmoja mgeni mgeni anaitwa MAIMUNA atakuja kwako kukuomba awe mchungaji usimkatalie na badala yake nitakupa fedha utakazomfungulia kanisa,wewe saivi utakuwa unatumia nguvu zetu ningependa naye umshawishi mpaka akubali kuwa pamoja nasi"
Mchungaji akuwa Mbishi akakubaliana na jambo lile,Jb akageuka upande mmoja na ghafla brufcase likatokea katika mkono wake akaliweka katika meza ya mchungaji yule.

Akalifungua!
Timotheo akatoa macho kwa mshangao,hizi ni ela chache sana milioni 150 ni kwa ajili ya matumizi na uanzaji wa kanisa chukua Pete hii pindi ukiniitaji utaipuliza Mara Tatu na usiache kuivaa...
Wakati wakiendelea na maongezi ghafla hodi ikaskika......
"Ndo huyo anakuja"

Usikose kuwa nami katika Sehemu ya -60-
 
MZIMU ULIOREJEA

Sehemu ya - 60 -

Ilipoishia...
Timotheo akatoa macho kwa mshangao,hizi ni ela chache sana milioni 150 ni kwa ajili ya matumizi na uanzaji wa kanisa chukua Pete hii pindi ukiniitaji utaipuliza Mara Tatu na usiache kuivaa...

Wakati wakiendelea na maongezi ghafla hodi ikaskika......

"Ndo huyo anakuja"

#Songa_nayo_sasa

Muda ule ule JB akatoweka......

************************************

Bado hali ya Janeth ilikuwa mbaya!,baada ya uchunguzi kukamilika daktari akamuitaji Martin ndani katika ofisi yake...

"Pole sana bwana Martin kwa tatizo lililokusibu,mkeo amepata athari katika kiuno chake na kwa bahati mbaya amevunjika sehemu mbaya atoweza kutembea"

Martin akuamini kile akisikiacho,moyo ulimpasuka alishindwa kuyazuia machozi kumtoka
Alijua dereva wake ndiye aliye mpa ulemavu mpz wake akukubaliana na matokeo Yale akaadhimia kumsafirisha mpaka India

Kila alipomuona mwanamke yule machozi yalimtoka
Bado alitamani kujua kilichotokea mpaka akawa akiishi katika maisha Yale ya ufukara na kuomba omba

"Martin mpz wangu ni story ndefu ila nimeteseka sana Mimi na sijui nitaishi vipi na ulemavu huu....

Janeth akashindwa kuongea akaangua kilio,Martin akaanza kumbembeleza na kumuaidi kuwa lazima atapona tu,kwa Janeth ilikuwa ni kama ndoto za alinacha....

" wazazi wangu na pacha wangu Jenipha walikufa katika ajali ya pamoja!"

"What?!"

"Ndiyo Martin na ndugu zangu upande wa baba,kina baba mdogo wakanidhulumu Mali na kupelekea Mimi kuwa ombaomba,mwingi wa mawazo"

"Basi usilie mpz madamu tumeonana kila kitu kitaenda vizuri"
Martin akaanza kuangaikia usafiri wa kumpeleka mpz wake yule India...

Baada ya kukamilisha kila kitu safari ya kuelekea India ikafuata,tumaini la Janeth kurudi katika hali yake ya kawaida lilikuwa dogo sana

*************************************

Baada ya hodi kusikika Mara ya kwanza mchungaji hakaruhusu Maimuna aingie
Binti yule naye pasina wasiwasi akakishika kitasa na kukifungua akaingia....

Ndani alipokelewa na tabasamu pana la mchungaji Maimuna akatabasamu,na kwenda kuketi

"Mchungaji kuna msukumo mkali unanisukuma natamani sana kuwa mtumishi, kumtumikia MUNGU katika mataifa mbali mbali"
Mchungaji akatabasamu...

"Maimuna unajua wewe ni Mrembo sana natamani ungekuwa mama mchungaji nimeiona kipawa chako.....
Aliongea mchungaji akisimama na kuuendea mlango....

Akaufunga
Maimuna akashtuka kwa kauli ile,akuamini kile akisikiacho
Alikuwa ni mjamzito na watumishi wote walijua ilo,iweje mchungaji ampende?

Akabaki kaduwaa
Ile ilikuwa ni janja ya shetani kumuingiza katika maovu
Kama jini Zeyna Kureysh alivyomuhadaa mchungaji...

Ghafla Maimuna akahisi mikono ikitambaa katika matiti yake huku akilambwa katika shingo yake
Akabaki ameganda
Mchungaji alikuwa nyuma yake
Kuna hisia mbili tofauti zilikuwa zikishindana katika moyo wake
Hisia moja ikim'force' akemee,ila hisia ingine ilimbembeleza amuache mchungaji yule asiye na mke amchezee,bila kujua kuwa kumuacha kufanya vile ni kuvunja amri ya sita
Kuwa mbali na makatazo ya Allah!
" wacha bhana kwanza utakuwa mama mchungaji, Pili utakuwa karibu zaidi ya kanisa Mara moja si mbayaaaa....."
Ibilisi alizidi kumsii
"Kemea kwa jina la yesu,usikubali uchezewe MAIMUNA kuwa mbali na shetani huyo....
Kauli ingine ikasikika pia
Mai akawa katikati,akashindwa kumzuhia mchungaji na kumuachia
Taratibu miguno ya kimapenzi ikamtoka
Alizidiwa na hisia....
Mwili wake ulimtetemeka kwa hasira,machozi yalimtiririka ila ilikuwa ana jinsi zaidi ya kukubali matokeo
Japo alimpenda sana Maimuna ilibidi akubali mchungaji afanye naye kitendo kile kiovu ili avunje nguvu zake...
Dakika chache baadaye ndani ya kanisa,ndani ya nyumba takatifu viumbe wale wawili walikuwa wakiivunja amri ya sita
Kwenda kinyume na maagizo ya MUNGU wetu
Katu hakujua kuwa katika paji lake la uso tayari alama 666 zilishajichora,alama ambazo zilimdhibitishia kama mfuasi wa shetani
Na hata baada ya tendo lile,lilimbadilisha kabisa MAI na kuwa mtu mwingine...
Siku chache baadaye akafunguliwa kanisa kubwa na kuanza kuhubir neno akitumia nguvu zile alizopewa
Nguvu hasi!,kutoka kuzimu
Akazidi kupata watumishi,umaharufu ukaongezeka
Mpaka anajifungua Mai alikuwa mtu mwingine kabisa
"Hivi karibuni ntamleta Mke wang na mwanangu"
Jb aliwaza akiwa katika kiti chake cha enzi
*********
Moyo wake ulimuuma baada ya daktari kumdhibitishia kuwa hatopona tena
Japo hali ya kiafya ilikuwa ni nzuri aliamua kumrudisha nyumbani Tanzania
Hapo ndipo Martin aliposikia juu ya mchungaji mmoja anayeponya,moyo ukamtuma akajaribu kuonana naye...
Katu akujua kama ni shemeji yake,baada ya Mai na Martin kuonana kwa Mara ya kwanza Mai akamdhihirishia Martin kwamba MUNGU yupo.

Japo ni kwa nje tu,ila uponyaji ulitendeka katika mwili wa Janeth
Na kwa Mara ya kwanza Janeth akarudi katika furaha yake
Siku chache baadaye wakafunga ndoa kati ya Janeth na Martin
Na miezi kadhaa Mbele tayari Janeth alibeba ujauzito
Baada ya miezi tisa wakapata mtoto wa kiume Martin akampa jina la kaka yake Brayson la ubatizo na JB la nyumbani kama zawadi kwa kaka yake
Furaha ikatawala katika mioyo yao na amani pia....

*************************************

TAMATI
Ni ajali mbaya ilotokea njia panda,ya Moshi,ilikuwa Maimuna katoka rombo kuubiri neno
Maimuna na mtoto wake walifia pale pale,kwa macho ya kibinadamu...
Wengi wa waumini wake walilia,wengine walipoteza fahamu...
Hayo yote yalijiri katika ulimwengu hai wa kibinadamu ila katika HIMAYA ya KUZIMU mambo yalikuwa tofauti
Sherehe kubwa ilifanyika ya kumpokea malkia wa kuzimu!
Maimuna akiwa kava shela lililomkaa vyema mkononi akiwa na mwanaye walikuwa wakiwasili rasmi kuzimu!
Moyo wake ulijaa amani na uwoga ulimtoka...
Furaha ilimtawala
:

Siku chache baadaye wakafungishwa ndoa na kuyaanza maisha upya kwa furaha na amani tele
Wakisubiri siku halali ya MOLA wao kuzitwaa roho zao
Bado zilikuwa ni nafsi zilizoishi...

Huo ndo ukawa mwisho wa Jb kurudi duniani...

© MWISHO ©
 
[emoji2398] MWISHO [emoji2398]
asante mkuuu siku imeisha
 
Mkuu, Stori nzuri. Apparently, lakini unaandika bila kuacha nafasi. Inatupa wasomaji wako wakati mgumu sana. Unaonaje ukizihariri sentensi zako zikawa katika mpangilio unaosomeka vizuri. Samahani lakini kama nitakuwa nimekuingilia sana.
 
Mkuu mimi sio mtunzi nimeshare tu na nyinyi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom