bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
MZIMU ULIOREJEA.
Sehemu ya 01.
Sayid Mwenny.
Upepo mkali ulivuma ulioambatana na radi sambamba na mvua kubwa iliyonyesha kwa hasira katikati ya Mji wa Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Angani hakukua na nyota iliyong'aa wala mbalamwezi kusawazisha nuru katika ulimwengu ule.
Kila mmoja alijifungia ndani ya nyumba zao akiwa usingizini, lakini wengine usingizi uliwapaa wakasikizia dhoruba iliyokua ikiendelea ndani ya nyumba zao.
Miti ilidondoshwa, dhoruba ilitawala na baadhi ya nyumba bati zao ziling'olewa huku kutwa zikidondoshwa na viumbe waliomo katika nyumba hizo kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabisa.
Kila mmoja alikuwa akijaribu kuokoa uhai wake.
Katikati ya jiji lile lile katika jumba moja la kifahari walioko katika nyumba hio hawakuguswa kabisa na dhoruba ile kutokakana na uimara wa ile nyumba yao.Waliichukulia mvua ile kama mvua nyingine iliyowapa starehe katika usingizi wao.
Hali ya makaburini pale haikua tofauti na hali ile ya katikati ya jiji. Mvua ilioambata na radi ilikua pia ilinyesha katika eneo lile la makaburi.
Mlinzi aliyekua anajulikana kwa jina la Kipele alikua mita kadhaa akitetemeka kwa kupigwa na mvua ile katika geti la kuingilia katika makaburi yale palipopendezeshwa na uzio uliotengenezwa kuzunguka eneo lote la makaburi yale.
Hakukua na sehemu nzuri ya kujibanza kukwepa dhoruba ile. Alishudia baadhi ya miti ikidondoshwa na kumtisha kabisa kuenda kusimama karibu ma miti ile. Akabaki kajikunyata akitetemeka kuikubali hali ile.
Mita kadhaa mbele kutoka geti la mlinzi mpaka katikati ya makaburi, palikua na kaburi moja ambalo lilikua limejengewa kifahari. Juu ya kaburi lile kulikua na kibao kilichoandikwa jina la __JACOB MSAKI__kwa kunakshiwa tarehe yake ya kuzaliwa pamoja na siku aliyokufa.
Juu ya kaburi lile kulikua na msalaba wa dhahabu.
Katika kaburi lile ghafla mtetemeko ulianza.Ulikua n mtetemo mdogo ambao ulikua katika kaburi lile tu. Ulikua n mtetemo uliowacha nyufa na kuanza kumomonyoa kaburi lile. Mara ghafla vumbi kutoka ndani ya kaburi lile likaanza kutoka.
Ilikua ajabu,. Lilikua ni vumba ambalo halikua na hata chembechembe ya tope likapanda kuelekea juu.
Mara ghafla jeneza la kifahari likatoka, pamoja na kwamba lilikua limeoza, pengine kwa kuwa lilifukiwa muda mrefu,lakini uzuri wake ulikuwa bado unaonekana waziwazi.
Baada ya kupanda juu likatua pembeni mwa kaburi lile. Ghafla mlango ukafunguka na mtu wa ajabu aliyekua ndani yake akaonekana. Ni wazi kabisa mfu alikua kafufuka kiajabu.
Kiumbe cha ajabu kilichooza na kutembelewa na mifinyifinyo katika suti iliyovubaa kilikua kinatoka katika kaburi lile.
Kumbe kile kikaingia duniani kwa jicho baya. Jicho lenye mng'ao uliotisha pindi kiumbe hai kingine kama kingepata bahati ya kuliona. Ghafla kikaachia tabasamu pana. Meno yaliyooza na mengine kutoboka yakaonekana na moshi mzito ukatoka katika domo lake.
Bado mvua ilikua inaendelea kunyesha sambamba na radi za hapa na pale lakini jitu lile halikushtushwa kabisa na hali ile ya mvua.
Maji ya mvua yalimlowanisha na kumwongeza nguvu ya furaha ya kuingia katika ulimwengu wa dunia hii waishio viumbe aina ya bin-Adam.
Jitu lile likanyoosha mkono mpana katika jeneza lile na ghafla shoti ikatoka kuliendea jeneza.
Ghafla jeneza likatoweka sambamba na eneo lile kusawazika pakawa kama mwanzo.
Jitu lile likaachia muayo mkubwa ulioambatana na radi ambao ulimfikia mlinzi getini na kuchukulia radi lile kama maradi mengine yaliyokua yanaendelea kupiga eneo lile.
Jitu lile likanyoosha mikono juu na kuachia cheko la dharau na kisha kutoweka katika eneo lile.
Katika nyumba ile ya kifahari ambayo wenyeji wake walikua wamelala fofofo, nje ya jumba lile palizuka jambo. Kilikua n kitu ambacho dakika chache nyuma kilitokea katikakati ya makaburi mjini Moshi. Lilikua ni jitu lile la kutisha. Likaangalia kushoto na kisha kulia likaachia tena cheko kubwa.
Lilikua ni cheko liilochukuliwa kama radi kwa waliobahatika kulisikia katika usiku ule mzito ambao ulikua n usiku wa manane.
Jitu likanyanyua mkono wake wa kulia juu na ghafla shoti za umeme zilizoambatana na radi zikatawala. Ghafla bisu lenye kumeremeta likatoka katika kono lake na kisha jitu lile likaachia cheko jingine na kisha likatoweka.
Ndani ya jumba lile katika chumba kimoja kipana walilala watu watatu. Mtu wa makamo pamoja na mtoto wao mdogo. Na wote walilala fofofo bila kushtushwa na mvua ilikua inanyesha.
Ghafla katika pembe ya kuta za nyumba ile likaibuka jitu. Lilikua ni jitu lilelile. Likamwangalia mwanaume aliyelala pale kwa dharau, likamnyoshea mkono ishara ya kumnyonga na mtu yule akawa anachezeshachezesha miguu ishara ya kutapatapa. Na si kwamba mtu yule aliyekua amelala hakua analiona lile jitu.Hapana.Ndani ya usingizi ule aliliona jitu lile na jinsi lilivyokua likimnyonga. Na ni wazi kabisa siku hiyo ndo ilikua mwisho wa maisha yake. Ni kweli asingeweza kusalimika kabisa.
"NILIAPA KUWAMALIZA KWA HIKI KISU, KWAHIVO SITOKUNYONGA"Jitu lile liliongea likinyanyu kile kisu juu likakishusha kwa nguvu kuelekea tumboni kwa yule bwana. "TUTAONA KUZIMU, MWANAHARAMU WEWE" Jitu lile lilitamka na kukishusha kisu kile katika mwa mbavu za mtu yule. Damu zikaruka na jitu lile likatoweka likiuacha mwili ulioharibika vibaya katika kitanda kile.
Mke na mtoto walilala fofofo na bado ilikua ni katikati ya usiku mnene.
Na huu ndio mwisho wa sehemu hii ya kwanza kabisa wa simulizi hii nzuri ya maisha iitwayo "MZIMU ULIOREJEA"