Simulizi: Muhanga Wa Mapenzi

U

unprejudiced

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2017
Messages
1,804
Points
2,000
U

unprejudiced

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2017
1,804 2,000
Inanitia uvivu nahisi kuikatisha
Tupo bosi. Toka nchi za mbali twasomaaa. Sema naonaga kukomment kama nataka kuingia kichwani mwa mtunzi na huharibu starehe na Element ya surprise.
 
SweetieLee

SweetieLee

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2018
Messages
1,081
Points
2,000
SweetieLee

SweetieLee

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2018
1,081 2,000
Eeh'
Mbona pamenoga.!! Victor tena???
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 59

Yule mlinzi aliongea kwa dhihaka. Alinichukulia kama mimi ni malaya tu ninayejiuza huko mtaani. Kwa kuwa nilikuwa na jambo langu ninalotaka kulijua, sikupenda kushindana na yule bwana.

Aliniletea daftari la kusaini, nikaandika jina la uongo kisha nikaruhusiwa kuingia ndani ya vyumba vile.
Niliogopa kumuuliza mlinzi huyo mwenyeji wangu yupo chumba gani, nilihofia angeweza kunitengenezea udadisi na kuniona mimi sikuwa mtu wa kawaida kwenye makazi hayo.

Baada ya kusaini niliingia ndani, nikawa nazipanda ngazi za ghorofa lile, katika kila korido ya ‘floor’ kulikuwa na korido ambazo zilikuwa na milango ya vyumba. Kulikuwa kimya. Utulivu ulikuwa wa hali ya juu. Ilikuwa ni kama vile hapakuwa na watu waliokuwa wakiishi kwenye vyumba ama nyumba hiyo.

Huyu mume wangu na mchepuko wake wanaishi wapi? Niliendelea kujiuliza kimoyomoyo. Niliendelea kuzikwea ngazi kwenda juu, ilikuwa ni kama kuna kitu kinaniambia endelea kupandisha juu.

Wakati namaliza ghorofa ya pili ile naanza orofa ya tatu, mara nikamwona mwanaume mmoja amenipa mgongo. Alikuwa ni mume wangu Alex. Alikuwa anaongea na simu akiwa emesimama kwenye dirisha la korido lililokuwa likiangalia upande wa nyuma wa ghorofa lile.

Nilipiga tambo refu, nikarudi nyuma haraka sana, nikajibanza kwenye kona, pale alipokua amesimama Alex, mume wangu aliendelea kongea na simu bila kujua lolote.

Alikuwa amevaa taulo bukta, miguuni alivaa sendozi. Alionekana ni kama alikuwa ametoka au anajiandaa kupumzika. Roho iliniuma, nilihisi kama nachunwa ngozi ningali hai. Mume anauma asikwambie mtu. Ingawa nilikuwa bado sijathibitisha kama yupo na mwanamke, niliamini kwa asilimia zote bwana yule yupo na mchepuko. wakiponda raha mule ndani.

Alipomaliza kuongea na simu alirudi ndani. Nilibaki pale kwenye kona, mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi, kuninyima kote kule haki yangu ya ndoa, kumbe haki hiyo alikuwa akipewa mwanamke mwingine.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 60

Ni tabia yake hiyo ndio imesababisha hadi nijikute naangukia kwa mpenzi wangu wa zamani, Victor, ambaye naye kila ninapokutana naye lazima anifanyie kwenye gari langu mwenyewe.

Machozi yalijikusanya machoni mwangu, kisha yakanibubujika mashavuni. Nikatoka kwenye maficho na kusogea kwenye malango wa chumba ambacho mume wangu alikuwa akiishi.

Nilisikia sauti ya redio ikitokea ndani, lakini katikati ya sauti ya redio, nikasikia sauti za mahaba zinazopishana kwa zamu, ajabu zote zilikuwa za wanaume na mojawapo ilikuwa ya mume wangu. sauti hiyo ilitoka katika namna ya kushangaza kidogo. Alikuwa analia kama mimi mbavyo huwa nalia!!!.

Akili yangu ilishindwa kufanya kazi sawa sawa, nikabakia nimefadhaika. Ndio. Ilikuwa lazima nifadhaike maana sauti ya mahaba ya mtu wa pili nayo nilikuwa naifahamu kabisa. Alikuwa ni Victor. Mchepuko wangu wa Tandale.

Nilishindwa kuelewa. Hawa wanaume wawili wanafahamiana vipi? Lakini humo ndani wanafanya mapenzi na wanawake gani? Wivu na hasira hasa dhidi ya mume wangu ukazidi kufukuta. Nikashika kitasa cha mlango na kukinyonga. Bahati nzuri kumbe ulikuwa haujafungwa. Nikasukuma mlango na kuingia ndani.

Lahaulaaa!!!.

Sikuamini kile nilichokuwa nakiona mbele yangu. Mume wangu Alex alikuwa anafanya mapenzi kinyume na maumbile na mchepuko wangu Victor. Yanii victor alikuwa amemgeuza mke mume wangu Alex.

Ilikuwa ni kama vile niko ndotoni! Nilikuwa nimesimama wima, macho yamenitoka pima. Kizunguzungu kikali kilikuwa kimenishika. Miguu ikaniisha nguvu, macho yakanilegea, bila kutarajia nikajikuta naanguka chini.

Alex na mwenziye nao walikuwa wameduwaa kama vile masanamu ya kuchonga. Wakagutuka na kuachiana baada ya kuniona nimeanguka chini na kuketi kitako.

Hakuna aliyeongea kitu, macho ya kila mtu yalikuwa na wasiwasi na mashaka, walivaa nguo haraka haraka.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 61

Mimi niliendela kuwa pale chini huku pumzi zikinitoka kwa shida.
Mume wangu alikuwa wa kwanza kumaliza kuvaa, uso wake bado ulikuwa na wasiwasi mwingi, hakuweza kuniangalia usoni, nikiwa pale chini pumzi zikinitoka kwa shida, mume wangu alinipita, akafungua mlango kisha nikamsikia akitimua mbio.
Victor anaye alikuwa anamalizia kuvaa viatu, naye alitaka kukimbia kama alivyofanya mwenziye.

“Kumbe wewe na mume wangu ni washenzi hivyo.” Nilimwambia Victor.
Kauli hiyo ikamfanya akugutuke, ni kama vile alishtushwa kusikia namtuhumu na mume wangu. “Huyu shoga ndio huwa mumeo?” Kauli hiyo ikanikata maini. Nikalia kama mtoto mdogo.

WIKI MBILI BADAYE

Alex alinitaliki. Siku napewa talaka yangu nilishangilia kwa furaha. Ndio, hakuna mwanamke katika dunia anayeweza kukubali kuwa na mwanaume ambaye ni shoga.

Sababu ya kuachana na mwanaume huyo ilibakia kuwa siri yangu na yeye, hata hivyo baada ya kuona jamii na serikali yangu inapambana dhidi ya tabia hizo za kishenzi, nikaona ni vizuri nikatoa ushuhuda wa mkasa huu ili iwe funzo kwa watu wengine.

MWISHO
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Story nyingine hii

 

Forum statistics

Threads 1,335,152
Members 512,245
Posts 32,497,194
Top