Simulizi: Muhanga Wa Mapenzi

Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Mtunzi Ally Katalambula

Sehemu ya 01

Jina langu naitwa Sofia ni mama wa mtoto mmoja. Katika familia yetu, mimi ni mtoto wa kwanza kati ya watatu, wadogo zangu wawili wote wakiwa ni wavulana. Nilitokea kwenye familia masikini, familia ya mzazi mmoja, yanii mama tu, ingawa kwa sasa naye tumekwisha mzika.

Kuhusu baba, yeye hatukuwahi kumjua wala kumwona maishani, ingawa mama alitueleza baba alikuwa ni raia wa nchi ya Nigeria ambaye alikutana naye kijiji cha Ntumbatu mkoani Morogoro alikokuwa akijishughulisha na ulanguzi wa viazi vitamu na kuvisafirisha jijini Dar es salam.

Mama anasema, baada ya kukutana na baba yetu raia wa Nigeria, penzi lao lilikuwa motomoto, kiasi cha kutosikia la muadhini wala mnadi swala, penzi liliponoga zaidi, akaamua kuhamia kijiji cha ntumbatu ambapo ndipo yule bwana alikokuwa akiishi.

Mama aliendelea kutusimulia kuwa, baada ya wazazi wake kupata habari kwamba yupo kwenye uhusiano na raia wa Nigeria, walimkanya kwa kumtahadharisha ajichunge na wageni kutoka nchi za mbali, hususani Afrika Magharibi kwani wanaume wengi wa huko ni matapeli.

Lakini kutokana na utamu wa penzi la baba yetu, mama aliweka masikio pamba, raha ya penzi ikamfanya anenepe na kuiona dunia yote ni yake.

Kama wasemavyo waswahili, hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, kufumba na kufumbua mama akajikuta amezalishwa watoto watatu na yule bwana.

Uzazi wa kila mwaka ukaifanya haiba ya urembo wake kunyauka, mama anasema, miaka michache baada ya kutuzaa sisi, tukiwa angali wadogo kabisa mwanaume huyo alimuaga alimwambia kuwa alikuwa amepata simu kutoka kwao, kwamba wazazi wake walikuwa wamefariki, akamwahidi akishamaliza mazishi ya wazee wake angerejea tena Tanzania kutuchukua ili tukaishi nchini Nigeria.

Mama akabikia na matarajio hayo. Yule bwana alivyondoka hakurudi tena. Hadi leo amebakia kuwa historia.

Mama anasema baada ya hali hiyo, ghafla maisha yalibadilika, akaogopa kurudi kwao, kwa kuwa awali aliwapinga wazazi wake juu ya tahadhari waliyompa. Ndipo kuanzia wakati huo mama akawa na jukumu moja tu. Kupambana kwa kila hali kuhakikisha watoto wake tunaishi maisha mazuri .
20190905_165222-jpg.1198891
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 02

Alijishugulisha na biashara ndogo ndogo na kilimo, faida kiduchu iliyokuwa ikipatikana ilishia kwenye kula, na matumizi madogo madogo ya nyumbani.
Mfumo huo wa maisha ulimfanya mama yangu aishi kwa presha na mkandamizo mkubwa nafsini hasa pale uhitaji wa huduma za msingi kama sare za shule, matibabu, ada, na mavazi.

Alijitahidi kwa nguvu zote, alipambana usiku na mchana, kutafuta pesa, lakini umasikini haukutuacha. Kuna kipindi nakumbuka, hali ya maisha ilipokuwa ngumu sana, mama alikuwa akijiuza kwenye vilabu vya pombe za kienyeji ili watoto wake tusilale njaa.

Jambo lile, liliniumiza sana na lilitudhalilisha familia nzima, majina yote mabaya alipewa. Malaya, kiguu na njia, jamvi la wageni, pozeo la masela, yote aliitwa yeye. Kila siku usiku kabla ya kulala, mama alituita chumbani, tukapiga magoti na kusali, kisha akatutia moyo kwa kutuaminisha elimu ndio kitu pekee kitakacholeta heshima katika familia.

“Someni kwa bidii watoto wangu, mkiwa na elimu mtakuwa na maisha mazuri, mtajenga nyumba nzuri, mtavaa nguo za kupendeza, watu wanaowabeza watawaheshimu.” Maneno yake niliyaweka akilini muda wote.

Nikiwa shule ya msingi, nilijitahidi kusoma kwa bidii. Bidii yangu ikanifanya niwe miongoni mwa wanafunzi wenye akili darasani. Katika mtihani namba nilizokuwa nikishika kama sio wa kwanza basi wa pili.

Pamoja na kwamba nilikuwa binti nisiyeheshimika mtaani, lakini darasani, nilikuwa na heshima kubwa, jambo hilo likanifanya niyaamini maneno ya mama na nikajikuta naipenda sana elimu.

Nilipohitimu darasa la saba, nilifaulu kwa alama za juu sana, nikachaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Kibasila iliyopo jijini Dar.

Kwa kweli niliweka heshima fulani kwanye familia yetu. Hata wadogo zangu Peter na Daud ambao niliwaacha darasa la tano, nao walitamani kuwa kama mimi.

Kama nilivyosema awali, mama alikuwa akipigana kufa na kupona kuhakikisha napata elimu bora, akiamini ndio urithi pekee utakaotutoa kwenye lindi la ufukara. Alipambana huku na kule kunitayarishia mahitaji muhimu tayari kwenda kuanza masomo yangu ya sekondari.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 03

Mungu si Athumani mwezi March ulipotimu, nilisafiri na mama hadi jijini Dar es salam, tukafikia kwa dada mmoja niliyetambulishwa kwake kama ni mama yangu mdogo, alikuwa ni mtoto wa mjomba wake mama. Aliitwa Mariamu. Msichana mzuri mwenye macho ya kuvutia..

Akaniambia, Kwa kuwa shule ya kibasila kwa wakati huo haikuwa na hosteli za wanafunzi, nitalazimika kuishi kwa ma’ mdogo Mariamu na kwa mahitaji yoyote, atakuwa anamtumia pesa yeye.

Siku chache badaye nilianza kidato cha kwanza nikiwa nimechelewa sana kwani wenzangu walikwishaanza tangu mwezi January. Mama alirudi kijijini Ntumbatu mimi nikabakia Dar nikiendelea na masomo ya sekondari huku nikiishi kwa ma’ mdogo Mariamu.

Maisha ya mimi ma’ mdogo, yalikuwa ya upendo tu, tuliishi vizuri ndani ya chumba kimoja alichokuwa akiishi huku akifanya kazi ya uwakala wa kusajili laini za simu kwenye kampuni moja ya mawasiliano hapa nchini.

Kitaluma sikuwa vizuri sana kwa ule mwaka wangu wa kwanza wa masomo, lakini mwaka uliofutia, yanii nilipoingia kidato cha pili, cheche zangu zilianza kuonekana.

Niliwaburuza wanafunzi wa kiume na wa kike kiasi cha jina langu kuwa gumzo, nilikuwa wa kwanza si kwenye majaribio tu bali hata kwenye mitihani ya kila muhula.

Nikiwa kidato cha tatu, wadogo zangu kule kijijini walimaliza darasa la saba, nao walifaulu kwa alama za juu na kuchaguliwa kujiunga na shule za vipaji maalumu nje ya mkoa.

Ilikuwa ni furaha kubwa kwa mama, lakini pia ilikuwa ni huzuni kubwa. Nasema hivyo kutokana na kwamba. Ni furaha kwa kuwa mama aliona fahari namna wanawe tulivyokuwa vichwa kwenye masomo, lakini alisikitika kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kutusomesha wote.

“Italazimika nimsomeshe dada yenu tu, siwezi kuwasomesha wote wanangu, nimejaribu kila mbinu ikiwa ni pamoja na kuomba msaada wa wafadhili, na serikalini nimekutana na siasa tu, nimeshindwa,”siku moja mama aliwaambia Peter na Daudi.

Ndugu zangu walibubujikwa na machozi, hata mimi nilijiskia vibaya sana, athari za umasikini zilikuwa zikituadhibu. Donge lilinikaba kooni. Kuanzia wakati huo nikaapa, nitasoma kwa bidii ili siku moja niwasadie wadogo zangu Peter na Daudi.
Niliingia kidato cha nne, nikafanya mtihani wangu wa mwisho vizuri.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Matokeo yalipotolewa na baraza la mtihani taifa tu. Ilikuwa ni kama ndoto ya kutisha maishani mwangu. Huwezi kuamini. Nilikuwa miongoni mwa wanafunzi waliopata ‘sifuri’

Sehemu ya 04

Matokeo ya kidato cha nne siyo tu yalinivunja moyo lakini pia yalisababisha nipitie kwenye historia chafu na ya aibu mno.

Nilikuwa miongoni mwa wanafunzi walifeli vibaya sana.

Nilikuwa nimepata ‘division four’ tena ile ya sifuri kabisa! Siwezi kusahau siku hiyo maishani, ilikuwa ni siku nzito sana, kile nilichokuwa nimetarajia kilikuja ndivyo sivyo.

Siyo mimi tu, kila mtu alishangaa kwa kile kilichotokea, kutokana na akili nilizokuwa nazo darasani hakuna aliyeamini kama ningeweza kupata sifuri kwenye masomo yangu.

Nakumbuka nililia kama mtoto mdogo, nilijiona kiumbe nisiye na bahati maishani, nikamini Mungu alikuwa mbali na mimi, na inawezekana alikuwa amenisahau kabisa.

Elimu ndio ilikuwa tegemeo langu kubwa, lakini kila kitu kikawa mithili ya ndoto mbaya sana. Sikuwa na pakushika tena.

Mama na ndugu zangu walipopata habari juu ya matokeo yangu, ilikuwa ni kama msiba umeikumba familia, majonzi yalitawala kwa kila mtu.

Kuna wakati niliwaza kunywa sumu nifilie mbali, lakini kila nilipomwangalia mama yangu, nikaona nitamwacha kwenye wakati mbaya sana duniani.

Siwezi kusahau nyakati hizo, nakumbuka, nilikuwa nikijifungia chumbani mwangu nikiwaza na kulia peke yangu.

Miongoni mwa mengi niliyoyawaza ni namna gani nitaikomboa familia yangu katika lindi la ufukara.

“Nimefeli masomo, lakini sijafeli maisha.” Nilijiambia kimoyomoyo. Nikajitahidi kusahau matokeo ya kidato cha nne. Japokuwa ilikuwa ngumu kufuta tukio hilo, lakini nashukuru mungu siku kadhaa tu niliweza kusahau matokeo yale.

Nikaendelea kukaa nyumbani nikisaidiana na ndugu zangu kwa shughuli za kilimo na biashara ndogondogo za viazi.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 05

Maisha hayakuwa ya furaha kwa upande wangu, kwanza hali ngumu ya maisha pili kukosa dira na tumaini.

Mwaka ulipita, mwaka wa pili, na hatimaye wa tatu. Nilikuwa binti wa miaka 20, mwanamwali nisiyemjua mwanaume yeyote maishani. Katika nyakati hizo za ujana wangu, ndipo katika hali isiyo ya kawaida, mama akashikwa na ugonjwa wa ajabu.

Alikuwa akianguka kama mtu mwenye kifafa, alikuwa akijipigiza kwa nguvu ardhini huku akitapatapa kama kuku aliyekatwa kichwa.

Awali tulidhani labda ni maralia imempanda kichwani, tulimkimbiza hospitali ya Wilaya ya Gairo kwa ajili ya matibabu.

Ajabu ni kwamba, vipimo vya kitabibu vilionesha mama hakuwa na tatizo lolote! Majibu hayo yalituchanganya sisi na madaktari, hata hivyo tukapewa rufaa ya kwenda hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi.

Kwa kuwa hatukuwa na fedha, tuliona ni kheri turudi kijijini Ntumbatu, tukiwa na mgonjwa wetu ili tujipange kwanza kifedha kabla ya kumpeleka Dar es salam.

Mama akawa anaugulia nyumbani, mimi na wadogo zangu, Peter na Daudi tukajikita kwenye utafutaji wa pesa za matibabu ya mama.

Kila siku asubuhi tulikuwa tukilangua viazi kwa wakulima, kisha tunavipeleka sokoni, huko tuliviuza kwa bei ya kutupa.
Kutokana na mtaji mdogo wa biashara kwa kweli ilikuwa ngumu sana kuipata pesa ya matibabu ya mama yetu, hali yake ikazidi kuwa mbaya.

Baadhi ya watu wakatushauri tumpeleke kwa mganga wa kienyeji, tukaambiwa kidogo huko gharama sio kubwa na pengine angeweza kupona kwa kuwa tatizo lake lilionekana limekaa ‘Kiswahili’ zaidi.

Tukampeleka.
Ilikuwa ni kama vile tumekwenda kuyamalizia maisha ya mama, kwani baada ya kumfikisha kwa mganga, siku tatu badaye mama akafariki dunia!!

Kilikuwa ni kipindi kingine cha maumivu maishani, ukiachilia mbali maumivu ya kufeli mtihani wa kidato cha nne, kifo cha mama ilikuwa ni pigo takatifu.

Niliendelea kumwona Mungu amenitelekeza kwenye dunia yenye mengi mateso, baada ya mazishi tukabakia watatu tu.

Mimi na wadogo zangu, zaidi ya mama mdogo wa Dar, hatukumjua ndugu mwingine yeyote.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 06

Tukandelea na maisha tukiwa watu wenye ukiwa mkubwa maishani. Siku zilikwenda sasa hali ya upweke wa kumkosa mama tukaanza kuizoea.

Siku moja nikiwa katika mihangaiko ya kila siku, nilikutana na rafiki yangu mmoja aitwaye Lizbeth, watu wengi walipenda kufupisha jina lake na kumwita Liz.

Huyu nilisoma naye shule ya msingi, kwa bahati mbaya urafiki wetu ulikoma baada ya mimi kufauli sekondari yeye akifeli, baada ya mimi kutimikia jijini Dar na kuendelea na masomo ya sekondari sikuwahi kujua habari za Liz zaidi ya kusikia tu aliolewa na bwana mmoja tajiri huko Dar es salam.

Baada ya kukutana naye sekoni, kwa kweli nlimsahau kwa jinsi alivyopendeza, aliavaa mavazi ya gharama, alinukia manukato ya bei mbaya, kichwani aliweka wigi ambalo gharama yake ilikuwa inazidi mtaji wa biashara yangu.

“Mwenzangu maisha mazuri, Liz,” nilimwambia, nafsi yangu ikakiri Liz alipendeza mithili ya malaika. “Ahante Sofia, hata wewe ukiyapatia maisha utakuwa bomba sana.”

“Mie nishajikatia tamaa, nasubiri nipate mume wa hapa hapa kijijini, angalau na mimi nimalizie maisha ya hapa duniani.” Nilimwambia kinyonge.

“Sikiliza nikwambie Sofia.”
“Ehe”
“Kuwa na maisha mazuri ni vile utakavyoamua mwenyewe.”
“Kivipi?” nikamuuliza kwa shauku.
“Njoo Dar es salam nikufundishe namna ya kuzikasa pesa,”alisema.

Mate mepesi yakanijaa kinywani. Tamaa ya kuwa na maisha mazuri kama ya Liz ikawa kubwa sana.

“Liz shoga yangu, nitashukuru sana kama utanitoa kwenye ufukara huu.” “Usijali Sofia, cha kufanya wewe anza maandalizi kabisa ya safari.”

“Lini tutaondoka?”
“Jumamosi ijayo.”
Kuanzia wakati huo nikawa mtu mwenye matarajio makubwa, tumaini lililokuwa limepotea, likarejea.

Niliwashirikisha wadogo zangu, Peter na Daudi juu ya safari ya Dar, hawakuwa na pingamizi. Hasa ukizingatia mimi ndiye nilikuwa mkubwa wao, na kiukweli mazungumzo yangu na wao ilikuwa ni kama kuwapa taarifa tu, hata kama wasingekubaliana na safari hiyo kamwe wasingeweza kunizua.

Na kwa kuwa, kidogo vijana wale walikuwa na uwezo kufanya vibarua vya hapa na pale ambavyo viliwapatia fedha, sikuwa na hofu juu ya ni namna gani wataishi pale nitakapokuwa mbali nao.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 07

Jumamosi ilipotimu, tulipanda noah hadi Morogoro mjini, huko tukapanda basi la Abood hadi jijini Dar. Tulifikia maeneo ya Sinza Vatcan, ndipo Liz alipokuwa akiishi.
Alipanga nyumba nzima, haikuwa nadhifu sana ukilinganisha na zile za Masaki ama Oystabay, angalau ilikuwa ni nyumba ya kawaida tu anayostahili kuishi binadamu.

Kwenye nyumba ile alikuwa akiishi na mfanyakazi wa ndani na mwanaye wa kiume wa miaka kumi. Fenicha ghali zilizopangwa sebuleni katika mpangilio mzuri, zilitoa taswira ya maisha mazuri ya watu waishio mule.

Liz alinionyesha chumba na bafu, nilioga tukala chakula cha usiku, kisha tukalala huku tukikubaliana kuzungumza michongo ya kazi siku itakayofuatia.

Nikiwa kitandani niliwaza mambo mengi kuhusu hatima yangu, nilimfikiria mara mbili Liz kama angeweza kunivusha kutoka kwenye lindi la ufukara uliokuwa umenizingira. Kwa kweli kwa mwonekano wa Liz niliamini hata kama asingeweza kunifikisha kwenye nukta niitakayo lakini ningeweza kupiga hatua fulani maishani.

Katika fikra hizo, nikakumbuka jambo jingine, katika mji wa Liz hakuwepo mumewe ilihali inatambulika kwamba Liz ni mke wa mtu. “Au amesafiri?” nilijiuliza kimoyomoyo. Sikulitilia manani sana jambo hilo, nikapitiwa na usingizi.

Nikalala.
Asubuhi na mapema, mtoto wa kike nilidamka. Sikufundishwa kulala hadi saa tatu, nilisaidiana na dada wa kazi kufanya shughuli mbalimbali za nyumbani, Liz alipoamka alikuta kila kitu kipo safi.

Alifurahishwa na tabia yangu, akanipenda zaidi. Kila nilipokuwa nikimwangalia Liz, japokuwa tulikuwa wasichana wa rika moja, lakini nilijiona hadhi yangu na yake ni mbingu na ardhi.

Bada ya kupata kifungua kinywa, ndipo Liz alipoanzisha mazungumzo juu ya kazi ambayo ningetakiwa kuifanya, ambayo ingenipatia fedha nyingi kwa muda mfupi.

“Unajua Sofia, wewe ni mwanamke mrembo na mwenye akili sana…” Liz alianza kueleza. Akaendelea.
“Nakuona ukingia kwenye mafanikio makubwa hata kunishinda.”

“Kwa nini?”
“Kwa sababu una akili nyingi.”
“Bado sijakuelewa Liz?”nikamuliza, sikuwa nimelewa mantiki ya maneno yake, bado hakuwa amesema ni kazi gani ninayotakiwa kufanya.
“Biashara utakayoifanya inahitaji uijue vizuri lugha ya kingereza.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 08

“Usiwe na pupa kila kitu utajua,”alisema, nikatulia kumsikiliza.

“Ninaposema una akili nyingi nina maana kabla ya kuingia kwenye hii kazi itabidi uingie darasani usome. kwa kipaji cha akili uliyonayo, na muda wa masomo unao takiwa kusoma, naamini masomo utakuwa umeyashika.”

Bado sikuwa nimelewa ni kazi gani, maelezo ya shoga yangu huyo alikuwa akizunguka tu, sikujua ni kwa nini alishindwa kunifungukia waziwazi kuliko mzunguko aliokuwa akiufanya.

Akaendelea kusema:
“Leo jioni masomo yataanza.”
“Kwani ni kazi gani hasa Liz?”uvumilivu ulinishinda nikamuuliza.
“Ni mambo ya mtandaoni.”
“Mtandaoni!!! Mtandao gani? na inafanywaje hiyo kazi?”

“Utajua kwanza inabidi uanze short course haraka iwezekanavyo.”
Nilichoka. Liz naye alionekana hakuvutiwa na namna nilivyokuwa na wahaka wa kujua kazi nitakayofanya ni ipi.

Sikutaka kumkwaza Liz, maji nilikwisha yavulia nguo sikuwa na budi kuyaoga, moyoni nikajisemea, utamu wa ngoma ni kuingia uwanjani na kucheza.

Jioni ya siku hiyo, alikuja mwanaume mrefu mweupe mtashati, alivaa miwani ya macho. Liz akanitambulisha kuwa huyo ni mwalimu atakaye nifundisha program mbalimbambali katika kompyuta ikiwemo namna ya kutumia ‘email na ‘website’ akaniambia jamaa huyo anaitwa Abdalla ila wao hupenda kumwita Dullah.

Jioni ileile nikaanza mafunzo, hapakuwa na masomo magumu, kwa masaa machache nikawa nimefahamu mambo chungu nzima hata yule mwalimu naye alishangwaza na uwezo wangu.

Siku ya pili masomo yalindelea chini ya mwalimu Dullah, niliendelea kuwa mwepesi wa kushika masomo yale hali iliyomfurahisha mwalimu wangu. Ndani ya wiki moja tu tayari nilikuwa nimekwisha ifahamu kompyuta sambamba na program zake muhimu. Liz alifurahishwa sana na hali ile.

“Kilichobakia ni kutengeneza pesa.”aliniambia akiwa katika tabasamu pana.

“Bila shaka utanieleza ni baishara gani itakayoniingizia ama kutuigizia fedha?”na mimi nikamuliza.
“Bila shaka Sofia, leo nitakueleza ni mchongo gani wa fedha tutafanya.”alisema, akaendelea.

“Kwanza kabla ya kukueleza nataka utambue kwa sasa mie sina mume, niliachana naye kwa talaka baada ya kuingia kwenye hii kazi…” Liz alisema, moyo ukanilipuka, nikaanza kuhisi huenda Liz alikuwa akijihusisha na kazi ya ukahaba.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 09

Hapo upo shoga?”
“Nipo, nakusikiliza Liz, endelea kuongea.” Nikaongea huku wasiwasi moyoni ukinijaa.

“Eeh!!...Kazi yenyewe ni kuuza picha za utupu mtandaoni.” Liz alinipasulia.
“Mungu wangu!!” nilitaharuki. UKIMYA mfupi ulipita baina yetu, jambo nililo elezwa na Liz liliniogopesha sana, katika maisha yangu niliwahi kujiapiza kwamba kamwe siwezi kuja kufanya umalaya ili nijipatie pesa.

Nilichukia mno kazi ya ukahaba, athari zake nilikuwa nikiziona kwa marehemu mama yangu, sikutaka yale yaliyokuwa yakimkuta mama na mimi yanikute. “

Siko tayari Liz, siwezi kujidhalilisha kwa sababu ya njaa,” niliongea kinyonge, Liz alikuwa kimya, alinisikiliza huku akinitizama katika jicho lilisema hujui lolote kuhusu maisha wewe. Angalia ya Liz iliniona kama mshamba fulani hivi ambaye naweza kukomba chai kwa kidole.

“Umalaya unaondoa heshima ya utu mbele ya jamii….”
“Nisikilize Sofia…”Liz alinikatisha. Aliongea kwa pozi, akaendelea.
“Kuuza picha zako kwa mtu aliyeoko Ulaya na bala la Asia, sio kujidhalilisha. Kamwe huwezi kuja kukutana na wanaume unawao wauzia picha zako. Sasa hapo umejidharirisha vipi?

“Picha moja unaweza kuiuza kwa dolla 10 hadi 20 ambayo ni zaidi ya shilingi elfu ishirini za kibongo hadi 30, huoni kama ni pesa nzuri Sofia? Huoni kama unaweza kutajirika kirahisi tena kwa muda mfupi tu?” Maneno ya Liz yaliningia ndani kabisa ya mtima wangu, moyo wangu ukatamani kabisa kazi ile, fedha zile nilizitaka sana, lakini kulikuwa na kama sauti fulani iliyokuwa inanisihi kutokubaliana na jambo lile moja kwa moja.

Liz ni kama alikuwa akitambua ni kitu gani kilikuwa kinapita akilini mwangu, naye akaniacha niamue mwenyewe. Akapiga kimya.

Nilifikiria kwa kina kisha nikamuuliza:
“Hizo picha chafu, nikishaziuza zinasambaa mitandaoni?”
“Wala. hilo halijawahi kutokea,” Liz alinijibu. “Na umesema hao wanaume siwezi kukutana nao kimwili?”

“Ndio.”
“Kama ni hivyo, nitafanya kazi hiyo, ila itakuwa kwa muda tu, nikipata pesa ambazo naweza kufanya biashara yoyote, nitaachana nayo.” Niliongea kwa yakini, sauti yangu na maneno yangu, yalibeba ujumbe uliomwambia Liz:

‘Nafanya kazi hiyo kwa kuwa nina dhiki lakini kamwe nisingeifanya.’
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 10

Liz alifurahi mno, aliniambia yeye amekuwa akifanya kazi hiyo kwa kipindi kirefu, hata mumewe waliachana naye kutokana na shughuli hiyo. “Nimejenga nyumba kijijini, nina viwanja kibao hapa Dar es salam, pia mtoto wangu anasoma shule nzuri, yote haya ni kutokana na kazi hii,” alinipasha.

Akaendelea
“Kwa muunganiko wetu wawili naamini tutatengeza pesa nyingi sana, kwa kuwa wateja wangu watapata kitu cha tofauti.

“Tena na hivi wewe unajua kuzungumza vizuri lugha ya Kingereza, tutauza hadi vipande vifupi vya video, tena kwa dau kubwa.”alisema.

Nilimsikiliza kwa makini. Nikamuuliza kitu:
“Hizo picha na video za uchi wanazifanyia nini? ”

“Wanaume ni viumbe wapumbavu sana, unadhani kuna cha maana anachofanyia kwenye hiyo picha yako ya utupu. Laa! Wao hujisikia raha tu kuona maumbile ya mwanamke.”

“Duh! Kweli wanaume ni wajinga sana.”
“Sana, tena mtu mwingine anaweza kuomba mtumie picha ya makalio yako yakiwa utupu, halafu akakulipa dolla 30 hadi 40.”
“Kweli?”
“Kabisa.”
“Huwa unawasilina nao vipi hao watu?”
“Natumia e-mail na skype kwa upande wa video.”

“Na wateja wapya unawapa vipi?”
Hao nawapata kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na Twiter

Tuliongea mengi siku hiyo, akanifundisha namna ya kujibinua na kujishebedua kwa pozi mbele ya kamera nikiwa uchi.
Mambo aliyokuwa akiyafanya Liz hayakutofautiana na wale wacheza muziki kwenye majukwaa ya makasino makubwa. ****

Awali Liz alinitambulisha kwa wateja wake kwa kutumia mtandao wa ‘Skype’ ambao alikuwa unaweza kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya video.
Bahati mbaya kwangu, siku hiyo hiyo ya kwanza tu kutambulishwa kwa wateja wake, mmoja akanitaka nivue blauzi nimwoneshe matiti yangu.

“Kuona titi moja dolla 20 yote mawili dolla 30,” Liz alimwambia.
Jamaa hakuwa na tatizo, akaomba akafanye malipo kwa njia ya Western Union kisha angerudi kuona matiti yangu yote mawili!

Baada ya kutoka hewani, Liz alishangilia, kuzipata dolla elfu 30 za haraka haraka. Kwa upande wangu nilikuwa na wasiwasi mno, sikuipenda kabisa kazi ile, lakini kwa kuwa nilikuwa nashida mno na pesa, ilikuwa ni lazima nifanye kazi hiyo.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 11

“Have you seen the money I send you?” jamaa aliongea kwa kimombo akimuuliza kama ameiona pesa aliyoituma.

“Yes I do.” Liz naye akajibu, akimanisha ameiona.
“Mlete mbele yangu haraka.” Alisema kwa sauti ya amri.

Liz akanitaka nisogee mbele ya kamera ya ‘laptop’ ili nianze kutoa huduma ‘live’ kwa bwana yule.

Nikiwa mbele ya kamera, jamaa aliniambia nianze kuvua nguo moja baada ya nyingine. Nikafanya hivyo.

Nikachojoa nguo moja, moja, hadi nilipobakia na nguo ya ndani tu, nikasimama wima na kumwangalia Muhindi yule mshenzi. Jamaa alionekana kupagawa vibaya sana kutokana na mvuto wa umbo langu.

Nilijihisi aibu kubwa, lakini kwa kuwa nilikwisha jitoa kwenye jambo lile, ilikuwa lazima nimalizie sehemu iliyobakia. Nikaishika chupi yangu, nayo nikaivua. Nikabakia kama nilivyozaliwa!. Mbele ya mwanaume.

Jamaa aliweweseka baada ya kuniona nikiwa mtupu, naye kule alikokuwa akafungua zipu ya suruali, akazishika nyeti zake akawa anajichua taratibu. Akawa ananiambia nigeuke kila upande ili apate kuniona vizuri, na mimi nikamfanyia manjonjo yalimfanya azidi kujipiga punyeto.

Tukaendelea kufanya upumbavu ule hadi jamaa alipojifikisha kileleni, baada ya kumaliza Liz akasogea kwenye kamera, akamwambia akitaka raha zaidi aje wakati mwingine na pesa nyingine, tukaagana na yule bwana, kisha akaondoka mtandaoni.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa maisha yangu ya ukahaba mtandaoni, nilifanya shughuli kwa malengo ya muda mfupi, lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo nilivyojikuta nikipenda kazi hiyo. Nilipata pesa nyingi sana.

Wadogo zangu niliwanunulia nguo, chakula pamoja simu, Kila mwisho wa wiki nilikuwa nikiwatumia pesa za matumizi.

Ilikuwa ni kazi iliyonipatia fedha nyingi na kwa muda mfupi, wakati mwingine tulikuwa tukijirekodi vipande vya video vya utupu na kuviuza kwenye tovuti mbalimbali za nje.

Maisha yangu yalibadirika kwa muda mfupi sana, nyumba aliyoiacha marehemu mama niliikarabati na iikawa moja ya nyumba bora kabisa pale kijijini.

Pamoja na kwamba nilikuwa na malengo ya muda mfupi katika kazi ile, lakini kila nilivyokuwa nikitengeneza pesa, ndivyo fikra za kauchana na shughuli ile zilizvyozidi kuyeyuka.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 12

Wadogo zangu niliwanunulia nguo, chakula pamoja simu, Kila mwisho wa wiki nilikuwa nikiwatumia pesa za matumizi.
Ilikuwa ni kazi iliyonipatia fedha nyingi na kwa muda mfupi, wakati mwingine tulikuwa tukijirekodi vipande vya video vya utupu na kuviuza kwenye tovuti mbalimbali za nje.

Maisha yangu yalibadirika kwa muda mfupi sana, nyumba aliyoiacha marehemu mama niliikarabati na iikawa moja ya nyumba bora kabisa pale kijijini.
Pamoja na kwamba nilikuwa na malengo ya muda mfupi katika kazi ile, lakini kila nilivyokuwa nikitengeneza pesa, ndivyo fikra za kauchana na shughuli ile zilizvyozidi kuyeyuka.

Kwa muda mfupi, nikajikuta nakuwa mjuvi kuliko hata shoga yangu Liz ambaye ndiye alikuwa mwalimu wangu kwenye kazi ile haramu.

Nilitengeneza pesa ndefu mno, kwa siku nilikuwa nikiingiza laki mbili hadi laki tatu, nilitengeneza chaneli na wanaume wenye pesa huko bala la Ulaya, Asia na Marekani, ilifikia hatua nikawa na wateja wengi kumshida hata Liz.

Pesa zangu nyingi ziliishia kwenye kujiremba na kujipodoa, urembo wangu niliugeuza mradi wa kujipatia fedha, pamoja na kufanya kazi ile ya kuuza picha za utupu mitandaoni, huwezi kuamini ndugu msomaji, mwili wangu ulikuwa bado haujaguswa na mwanaume yeyote maishani. Wanaume wengi wa Sinza waliishia kula kwa macho na kuniacha mtoto wa kike na bikira yangu.

Naamini jambo hili linaweza kuwa gumu kuamini, lakini ukweli huo ulibaki kuwa hivyo. Nilikuwa bado mwanamwali, niuzaye picha za utupu mitandaoni!.
Hata wanaume waliokuwa wakinunua picha zangu, walimini nilikuwa mwanamke nilioyekubuhu kwa umalaya.

Hakuna nilichokuwa najali nitaonekanaje mbele ya mtu yeyote, kama niliwahi kuwa na hofu juu ya kazi ile, basi hofu yote ilikwishatorokea dirishani na kuishia zake.

Nilifungua duka la vipodozi maeneo ya Sinza kwa Remy, watu waliokuwa wanayajua maisha yangu ya nyuma wote walibakia wakinishangaa.

Nikiwa bado naishi nyumbani kwa shoga yangu Liz, kama mjuavyojua roho zetu sisi wanawake, baada ya shoga yangu huyo kuona nimekuwa na wateja wengi kumzidi, akaanza kuwa na tabia za wivu.

Akawa ananikasirikia bila sababu, hila na husuda za hapa na pale zikawa nyingi, wakati mwingine alinizua nisitoe huduma bila sababu ya msingi.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 13

Nilichoka. Nikaona isiwe kesi, acha nijitenge naye.

Nikahama nyumbani kwake na kwenda kupanga Mbezi beach, mitaa ya jogoo. Na kwa kuwa nilishakuwa mjuvi wa biashara, wala haikuwa tabu kuendelea.

Ndani ya nyumba ile nilitenga chumba kimoja, kwa ajili ya kufanyia shughuli zangu za kipumbavu.

Nilipiga pesa ndefu, mara mbili ya ile niliyokuwa naipata nikiwa naishi kwa Liz.

Niliwaleta ndugu zangu mjini na kuwafungulia biashara, niliwanunulia nyumba nzuri maeneo ya Kunduchi huko wakawa wanaishi pamoja huku wakisimamia miradi mbalimbali.

Hadi wakati huo ndugu zangu walijua dada yao nilikuwa nikijihusisha na biashara, lakini hakuna hata mmoja aliyejua kama nilikuwa kahaba niuzaye picha chafu mitandaoni.

Maisha yaliendelea kuwa mazuri, nikanunua gari la kutembelea, nikawa na kila kitu mbacho kijana yeyote angependa awe nacho. Maisha magumu niliyopitia siku za nyuma ikabakia kuwa historia.Ulikuwa ni wakati mzuri mno maishan.

Siku moja nilikaa chini na kutafakari hatima maishani yangu, nikabaini pamoja na kwamba nina kila kitu kwenye maisha, lakini sikuwa mtu mwenye kufurahia maisha. Kama binadamu kuna kitu nilikuwa nakikosa maishani.
Mume.

Kama mwanamke niliyekuwa na mafanikio makubwa, nilihitaji nipate mume ambaye nitaanzisha naye familia. Lakini swali likawa ni moja, ni mwanaume gani atakubali kuwa na mwanamke auzaye picha chafu mtandaoni?

KILA nilipofikiria suala hilo, moyo wangu ulivunjika. Nilijiona mwanamke nisiye stahili ndoa. Kazi niliyokuwa nikifanya iliondoa thamani yangu yote. Pamoja na hali hiyo, hamu ya ndoa ilizidi kutambaa kwenye mishipa ya damu.

Nilitamani niwe mke wa mwanaume fulani, siku moja nilitaka niwe mama wa familia, mume mzuri nitakaye za naye watoto wawili, wa kwanza wa kiume, mwingine wa kike.

Sambamba na mafanikio makubwa niliyokuwa nayo kwa kweli nilikuwa na kila sababu ya kuwa na ndoto hizo. Ila kipingamizi kikabaki kuwa kimoja. Kazi niliyokuwa niifanya.

Siku hiyo ilikuwa ni siku nzito kwangu, niliona angalau niende pub nikapate moja moto moja baridi.

Unaweza kujiuliza tabia ya ulevi niliianza lini? Ukweli ni kwamba, siku za mwanzo nilipoanza kuuza picha za utupu mitandaoni, ilikuwa sharti nipate kilevi ili kuondoa aibu.
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 14

Hivyo ndivyo niliavyoanza kunywa pombe
Niliendesha gari hadi ilipokuwa pub ya Mango Garden, Kinondoni.

Niliona sehemu ile ingekuwa nzuri kwangu kupunguzia mawazo hasa kutokana na uwepo wa bendi ya Twanga pepeta ambayo kila mwisho wa wiki ilikuwa ikitumbuiza pale.

Nilichukua nafasi kwenye kona moja, katika meza pweke, muhudumu alipokuja, nikaagiza bia. Wakati huo ilikuwa yapata saa mbili usiku. Bendi ilikuwa ikitoa burudani stejini.

Nilipiga tarumbeta, chupa ilipotua chini, ilikuwa nusu. Dakika tatu tu, bia yote ilikwisha. Nikaagiza nyingine. Nayo hakuchukua muda. Nikaifuta.

Bado neno ‘ndoa’ liliendelea kutekenya akili yangu.
Lazima uolewe, lazima upate mume. Sauti hiyo ilikuwa ikijirudia kila wakati akilini mwangu.

Kadiri nilivyokuwa nikilewa pombe, ndivyo hali hiyo ilivyokuwa ikiongezeka.

Nikiwa nimefura kama koboko, mara mhudumu alinijia akiwa na sahani la nyama choma. Akaniambia:
“Hii ofa imetoka kwa jamaa yuleee!”alisema huku akisonta.

Niligeuka kule alikosonta nikamwona mwanaume mmoja mrefu mweupe, alikuwa ameketi kaunta kwenye kiti kirefu. Nilipogananisha naye macho, akanipungia mkono.

Sikuwahi kumjua mtu yule, sura yake ilikuwa ngeni machoni pangu, nikiwa sijajua kama natakiwa nikubali ama nikatae ofa ile, jamaa akanionyeshea tabasamu na uso uliosema.

“Pokea ofa yangu tafadhali.”
Hatiamye nilipokea kile chakula, nikawa natafuna zile finyango za nyama huku nikishushia na bia, nijua ni moja ya ofa kutoka wanaume wakware tu ambao wangeishia kula kwa macho.

Angalau mchanganyiko wa kinywaji na zile nyama choma ukanichangamsha. Utamu wake ukafifiza fikra zilizokuwa zikisurubu mtima wangu.

Mara jamaa aliyenipa ofa ile akanijia.
“Habari yako dada, naitwa Alex,” alijitambulisha, akanionyesha tena tabasamu lake, sikujibu salamu yake wala utambulisho wake. Nikabaki namwangali tu.
“Naweza kuketi?”
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
115,727
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
115,727 2,000
Sehemu ya 15

“Naweza kuketi?”
“Kaa,” nilisema mara moja kwa sauti ya shuruti.

“Naitwa Alex,”akarudia tena kujitambulisha.
“Sawa,” nikajibu katika namna fulani ya dharau na pozi za kike.

“We waitwaje?”
“Sofia.”
“Waishi wapi?”
“Mbezi.”
“Umekuja peke yako?”
“Wewe ni polisi ama mwandishi wa habari?” nikamuuliza kwa ukali. “Kwa nini?”

“Maswali mengi kama mpelelezi sipendi,” nikasema kwa ukali.
Jamaa akatabasamu. Bahati mbaya au nzuri tabasamu lile nikalitia machoni sio siri tabasamu lake ndilo lililomaliza jeuri yangu, alikuwa na tabasamu fulani hivi zuri sana, kila alitowapo vishimo vya mashavuni ambavyo a.k.a yake hujulikana kama ‘vidimpozi’ ilitokeza.

Na kuifanya sura yake kuwa ya kuvutia.
“Mie siyo mtu mbaya bibie…”akaniambia halafu akaniuliza tena.

“Umekuja na nani?” “Nimekuja peke yangu,” nikajibu. Akachia tabasamu lake, nikazidi kudata kwa mwonekano bomba wa ‘handsome boy’ yule.

“Umesema unaishi Mbezi beach?”
“Ndiyo.” "Kumbe tunaishi sehemu moja. Mbona sijawahi kukuona?"

"Nipo tu."
"Umeolewa?"
"Bado."
"Mchumba?"
"Sina."
"Kwa nini?"
"Sijapata."

"Yaani wanaume wote hawa waliojaa. Nawe u mzuri, wawezaje kukosa mchumba?"
"Bado hajatokea nimtakaye."
"Mimi je?"

Hapo ndipo nilipoanza mahusiano na Alex, siku hiyo tulicheza muziki, tukanywa pombe tukalewa chakari, safari yetu ikashia lodge ya Mapambano iliyopo Mwananyamala komakoma.

Kwa kweli ndugu msomaji, ule mkandamizo wa kuitaka ndoa uliyeyuka punde baada ya kufahamiana na Alex.

Muda mfupi ambao nilifahamiana naye, tulijikuta tunazoeana kama wapenzi wa muda mrefu sana. Alex alikuwa mtu mmoja mcheshi sana. Tukiwa ndani ya chumba cha ‘lodge’ mambo yalikuwa moto.

Kama nilivyosema awali. Katika maisha yangu ya ujana, sikuwahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote maishani. Pamoja na kufanya kazi ya kuuza picha za utupu mitandaoni.

Nilikuwa bikira. Alex aliniandaa vizuri tu kama mwanaume mwingine yeyote makini ambavyo angefanya. Alipochojoa nguo zangu, akadata na matiti yangu yaliyokuwa wima, yametuna kama vikombe vya kahawa.

Akawa anazimung’unya chuchu zangu kama mfyonzaji wa embe sukari, sikuwahi kufanyiwa michezo ile kabla, hivyo kitendo kile kiliamsha msisimko wa aina yake.
 

Forum statistics

Threads 1,335,156
Members 512,245
Posts 32,497,406
Top