Simulizi: Muhanga Wa Mapenzi

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
3,915
2,000
Sehemu ya 61

Mimi niliendela kuwa pale chini huku pumzi zikinitoka kwa shida.
Mume wangu alikuwa wa kwanza kumaliza kuvaa, uso wake bado ulikuwa na wasiwasi mwingi, hakuweza kuniangalia usoni, nikiwa pale chini pumzi zikinitoka kwa shida, mume wangu alinipita, akafungua mlango kisha nikamsikia akitimua mbio.
Victor anaye alikuwa anamalizia kuvaa viatu, naye alitaka kukimbia kama alivyofanya mwenziye.

“Kumbe wewe na mume wangu ni washenzi hivyo.” Nilimwambia Victor.
Kauli hiyo ikamfanya akugutuke, ni kama vile alishtushwa kusikia namtuhumu na mume wangu. “Huyu shoga ndio huwa mumeo?” Kauli hiyo ikanikata maini. Nikalia kama mtoto mdogo.

WIKI MBILI BADAYE

Alex alinitaliki. Siku napewa talaka yangu nilishangilia kwa furaha. Ndio, hakuna mwanamke katika dunia anayeweza kukubali kuwa na mwanaume ambaye ni shoga.

Sababu ya kuachana na mwanaume huyo ilibakia kuwa siri yangu na yeye, hata hivyo baada ya kuona jamii na serikali yangu inapambana dhidi ya tabia hizo za kishenzi, nikaona ni vizuri nikatoa ushuhuda wa mkasa huu ili iwe funzo kwa watu wengine.

MWISHO
daaaamn', Yaani imekuwa so unexpected jinsi imeishia, whooops'..!!
Kwahiyo kumnyanyasa kote kule mkewe kumbe naye ana makubwa zaidi.??
thanks so much Shunie babie nimejifunza hakuna mkamilifu, kila mmoja ana siri zake kazichimbia moyoni..!!
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
121,933
2,000
daaaamn', Yaani imekuwa so unexpected jinsi imeishia, whooops'..!!
Kwahiyo kumnyanyasa kote kule mkewe kumbe naye ana makubwa zaidi.??
thanks so much Shunie babie nimejifunza hakuna mkamilifu, kila mmoja ana siri zake kazichimbia moyoni..!!
Umeona eenh kila mtu ana mazito yake jamani soma hiyo nyingine nimeweka link mamy
 

kisukari

JF-Expert Member
Jul 16, 2010
4,545
2,000
Asante sana shunie hadithi nzuri na inasikitisha. Mimi nimeiona Leo na nimeisoma leo. Sikuweza ku comment chochote
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,241
2,000
Wee ndio imeisha au umeikatisha shunii?? 😒😒 vipi kuhusu victor 😮😮 navokuuliza kama unakaa naye karibu
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
121,933
2,000
dah papara za ndoa watoto wa kike zinatucost sana kuna muda tunakuwa desperate mno mpaka unajikuta unaangukia sipo yan alex ni shoga? Kwa kweli viatu vya sofia kwangu ni vikubwa havinitoshi
Ukifikisha miaka 30 huna dalili ya kuolewa unachanganyikiwa anayekuja yeyote unakubali
 

Agustino87

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
5,628
2,000
daaaamn', Yaani imekuwa so unexpected jinsi imeishia, whooops'..!!
Kwahiyo kumnyanyasa kote kule mkewe kumbe naye ana makubwa zaidi.??
thanks so much Shunie babie nimejifunza hakuna mkamilifu, kila mmoja ana siri zake kazichimbia moyoni..!!
Mkuu kama hiyo miguu hapo kwenye avatar ni yako hongera sana.
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,241
2,000
Ukifikisha miaka 30 huna dalili ya kuolewa unachanganyikiwa anayekuja yeyote unakubali
wengine hata sio kwa hio miaka bali ni kwa presha za watu zinawafanya wawe hivo, like kwa nn huolewi? Ukute mtaani watu wote wanaolewa unabakia peke yako kama akili zako za kushkiwa lazima kila ajaye utataka ndoa, swala l ndoa linpasw kua automatic kichwan kwa mwanaume, hizi zakufos sizo, na ukiharib ukaolewa na mtu asie sahihi bas umejivurugia moj kwa moja
 

Kosugi

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
2,156
2,000
Sehemu ya 37

Muda si mrefu muhudumu alifika, alikuwa akisubiri oda yangu, nilipitia ‘menu’ nikaona kuna: ‘Hand-Batter fish, Chunky chips, British Beef and Ale Pie, Ham Hock, Pea Pie’ Breaded Whole nk.

Nilete Spaghetti Bolognese na Heinken baridi sikupenda kuagiza chakula ambacho ningekula halafu badaye kinishinde, nilitambua Spaghetti Bolognese ni kama tambi tu ningweza kuzimaliza.

Nilihudumiwa ule msosi, kwa kuwa nilikuwa na njaa, dakika tu, sahani ilikuwa nyeupe, nikabakia nakunywa Henken yangu ya baridi huku upepo wa bahari ukinipa burudani ya aina yake.

Tafuta pesa bwana wewe, maisha ndio haya haya. Burudani kama hizi ukiwa kapuku utaendelea kuzisoma kwenye riwaya na kuziona kwenye filamu.

Kuna wakati nikiwa naendelea kubugia kinywaji changu kile niliona kama niko katika pepo fulani hivi duniani.
Nikiwa pale, katika utulivu wa nafsi na akili mara nikakutwa na iliyo niondolea utulivu wote.

“Hey miss.” Nilisikia sauti niliyoitambua ikiniita. Sauti hiyo ilitokea nyuma yangu. Ilikuwa ni sauti nzuri ya kiume. Sauti ya Mr macho makubwa!!!.
****
Kwa mshituko glasi ya Henken ikaanguka chini bila kujua. Glasi ikavunjika Mr Macho makubwa akanivuta kwa pembeni nikae mbali na vipande vya chupa vya glass iliyovunjika.

Watu wote wakawa wananiangalia, aibu ilinishika asikwambie mtu. Mr macho makubwa alinishika mkono kisha akaniongoza kunipeleka sehemu nyingine.

Namna alivyonishika mkono na namna alivyokuwa akiniongoza, ilikuwa kama kondoo apelekwaye machinjioni na mchungaji wake. “Wajionaje mrembo?” Mr Macho makubwa alinisalimu baada ya kunikalisha na utulivu kurudi kwenye hali yake.

Mwili wangu ulikuwa unachuruzika jasho, kwa kweli kitendo cha kumwona mvulana yule katika eneo lile lilikuwa ni shambulio la moja kwa moja moyoni mwangu.
Ile nadhiri ya kumfuta na kumsahau moyoni mwangu sijui hata iliyeyukia wapi. Nikajikuta nafurahia uwepo wake.
Dada umeleta story fantastic ilonifunza mengi.
Yani sikuwahi kaa nikapoteza muda nikisoma story namna hii ila leo nimepoteza an hour and ahalf nikiisoma hii hadithi uloleta.
Thanks umenipunguza stress nilizopata leo.
Mungu akubariki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom