Simulizi: Muhanga Wa Mapenzi

Simulizi: Muhanga Wa Mapenzi

Sehemu ya 47

Badala ya kujibu naye akauliza yake.
“Pita ndani.”nilimwambia ila sikupenda ujio wake. Mwanaume huyo aliutesa sana moyo wangu. Alinikataa kwa sababu ya historia mbaya ya maisha yangu ya nyuma.

Kitendo cha kunitosa masaa machache kabla ya ndoa yetu ulikuwa ni mkuki mkali moyoni kila nilipokumbuka. Alingia ndani akaketi sofani, bado alionekana kuwa na mawazo mengi.

“Unasemaje Alex?” nilimuuliza. “Habari za siku nyingi Sofia.”
“Sema kilichokuleta Alex usipoteza muda kwa salamu zisizo na faida yoyote kati yet....” “Sofia...” alinikatisha.
“Sijaja kugombana na wewe. Aliasema, akaendelea.

“Nimekuja kukueleza kila kitu kuhusu lengo la yule mpumbavu aliyenitumia picha zako chafu siku moja kabla ya harusi yetu.” “Alex Kujua lengo lake lilikuwa lipi kuna faida gani leo hii? Itabadilisha nini?”

Niliposema maneno hayo, Alex alisimama akanisogelea, akaniangala machoni kwa hisia kali. Akaniambia:

“Baada ya kugundua mtu aliyetuma zile picha na sababu zake za kufanya hivyo, ndipo nilipobaini nilifanya kosa kubwa kukuacha Sofia.

Ni kweli niliumia kuona mwanamke ninayekaribia kumwoa akiwa anauza picha chafu za mwili wake mtandaoni, lakini nilitakiwa niyatizame mambo kwa mapana zaidi.” Alex aliongea kwa hisia kali. Alionekana ana kitu moyoni mwake.

Nakumbuka yule muhuni aliyedukua picha zangu chafu, alinipigia simu akitaka fedha ili atunze picha hizo. Baada ya kugoma kumpa alichotaka, ndipo alipoamua kumwonesha Alex hizo picha chafu na kuzua kizaazaa.

Sasa vipi wasaaa huu Alex aniambie eti mtu aliyekuwa na picha zile alikuwa akihitaji zaidi ya fedha, na mtu huyo ni nani? Niliwaza.

“Unaweza kuniambia umemtambua nini kuhusu jambo lile ?” nilimuliza. Angalau safari hii, ule munkari wa kutaka yule Alex aondoke ulinipungua.

Alex alichomoa simu yake na kubofya bofya kisha akaigeuzia kwangu.
“Huyu hapa. Ndio muhusika namba moja kwenye lile sakata,” alisema akinionesha picha ya mwanamke kupitia simu yake.

Mbele yangu nilimwona mwanamke mnene, mrembo lakini hanifikii mimi. Uso wake ulionekana kuwa wa upole lakini wenye chuki iliyojificha. Sura yake haikuwa ngeni, kuna mahali niliwahi kumwona lakini sikumbuki ni wapi.
“Unamjua huyu?” Alex aliniuliza.
 
Sehemu ya 48

“Sura yake sio ngeni.”
“Ndiye aliyekutuza box la zawadi lenye picha zako chafu ile siku yako ya Sendoff ...”

Naam! aliposema hivyo, nikakumbuka hiyo sura nilimuona ukumbini miezi 14 iliyopita, kweli usiku ule alikuwa ni moja ya watu walionipa zawadi mbalimbali.
Alex akaendelea kunieleza.
“Na aliyekupigia simu asubuhi ya siku ya pili ni jamaa anaitwa Abdallah, picha yeke hii hapa” alionionyesha.

“Mungu wangu!!” nilitaharuki baada ya kumwona Abadalla ama Dullah kama anavyopenda kuitwa. Kama utakumbuka huyu ni yule rafikiye Shoga yangu, Liz, ambaye wakati nahamia Dar ndiye alikuwa mwalimu wangu aliyenifundisha, matumizi ya ‘Computer na internet’ “Ni huyu!!!” nilipayuka.

“Ndio Sofia, hawa ndio wachawi wetu. Huyu Salma sijui hata alikutana wapi na Abdallah na kufanya kazi pamoja ya kutusambaratisha.

Abdallah ni mtu mwenye tamaa sana ya fedha ila Salma alidhamilia kututengenisha, ndio maana ikatafutwa historia yako ya maisha yako ya zamani ili inifikie.” Alex alisema kwa masikitiko.

“Kumbe ile siku Abdallah ndio alikuwa akiwasiliana na mimi mbwa yule.” “Ndio”
“Na wewe Alex umejuaje yote hayo?” nilimulizia nikiwa nimesawijika kwa munkari.

“Hiyo ni habari ndefu Sofia, lakini kwa ufupi Abdallah ndiye ametoboa siri hiyo baada ya kuhitilafiana na Salma.” Nilifikiria kidogo kisha nikamuuliza.
“Kwa hiyo mantiki ya kuja kunieleza yote hayo ni nini?”

“Nahitaji nirudi mikononi mwako Sofia.”
“Baada ya muda wote huo?”
“Moyo haujakusahau, chuki dhidi yako ilitokana na wivu mkubwa nilipatwa baada ya kuona picha zako, lakini ukweli ambao hakufutika akilini mwangu nafsi yangu ilikuwa bado inakuhitaji.” Aliniambia.

“Lakini historia yangu ya nyuma haijafutika na haiwezi kufutika, utawezaje kuishi na mwanamke aliyewahi kuunadi mwili wake kwa wanaume wengine?” Hasira na kilema cha utashi, kiliunyima fursa moyo wangu wa kuwa nawe, nilikuona mwenye makosa, sikuwaza kabisa kwamba sasa hivi ulikua mwanamke mpya ustahili kuolewa.”

Mwanaume yule alinisomesha kwa maneno na uso wenye hisia kali hadi moyo wangu wangu ukamwonea huruma. Tukarudiana.

**** Tulikuwa tumekumbatiana wote tukiwa katika hisia kali ya huba, tulifungua ukurasa mpya wa penzi lililopotea.
 
Sehemu ya 49

Katikati ya kumbato lile, mara simu yangu ya mkononi iliyokuwa kando ikaaita kwa nguvu, nikainyakua na kuweka sikioni.

Hellow”niliiongea.
“Victor hapa!!” sauti ya Victor mwanaume chakalaumu ilisikika. “Whaat!!” nilimaka. “NIPIGIEEE!!” sauti ya Victor ilisikika simuni. Nilibaki nimeganda kama sanamu, simu ilikuwa bado sikioni ingawa Victor alikiwisha ikata muda mrefu akingoja kupigiwa. “Ni nani huyo?” Alex aliniuliza. Lilikuwa ni swali gumu kujibika. Ningemwambia ni nani?

Victor mwanaume chakaramu nilimpenda nikafa nikaoza kwa muda mfupi sana. Nilitokea kumzimikia kwa kasi ya ajabu. Nikajitoa kwa ajili yake, tena bila kujali muda tulio fahamiana. Nikampa penzi ndani ya gari langu mwenyewe. Ghafla tu akatoweka, akaniacha peke yangu.

Moyo wangu ukaungulia kwa kumkosa, leo ananijia muda mchache baada ya mwanaume wangu wa zamani, Alex kunijia na kuniomba radhi.

Nilishindwa la kufanya, akili yangu ilinionya kurudi kwa Victor ila moyo wangu ulitamani. “Una nini mpenzi, mbona husemi?” kwa mara nyingine Alex akaniuliza.

Niligutuka katika lindi la mawazo na kumwangalia Alex usoni:
“Unataka kujua nawaza nini?” nilimuliza Alex nikiwa nimemkazia jicho.
“Ndio labda naweza kukusaidia.”

“Aliyenipigia simu ni mwanaume wangu, tulipotezana kwa muda sasa, leo ndio huyu anapiga.” Nilimwambia.

Alex alikosa raha ghafla baada ya kumweleza jambo hilo, naye aliniangalia kwa uso wa upole akaniambia:
 
Sehemu ya 50

“Sofia nakupenda, nakuhitaji katika maisha yangu kuliko kitu chochote. Nakuomba nikuchumbie tena kisha nikuoe haraka iwezekanavyo.”

Maneno ya Alex yaliniingia, yakavuruga kabisa mwenendo wa uwazaji wangu. Alex aligusa udhaifu wangu maishani. Katika maisha ya ukubwa wangu nilitamani ndoa kuliko kitu chochote.

“Unanipenda Alex?” “Zaidi ya sana sofia, nakupenda.”
“Huwezi kuniacha tena?” “Hata iweje, siwezi kukuacha muhibu wangu.”
“Niko tayari unioe, nakukabidhi tena moyo wangu,” nilisema.

Tulikumbatiana kwa hisia kali. Kufumba na kufumbua tukajikuta tumeangukia katika uwanja unatoa vipaji vyote duniani, a.k.a kitandani.

Sikumpigia tena Victor. Namba yake nikaifutilia mbali. Sikujua tena habari zake. Naye hakunipiga kabisa mbwa yule.

****
NDOA yangu na Alex ilimstajabisha kila mtu aliyekuwa akifahamu historia ya maisha yetu. Tulifunga ndoa kwa siri kwenye kanisa moja liko nje kidogo ya jiji. Ilikuwa ni harusi ndogo iliyojumuisha watu wachache sana.

Niliyaanza maisha ya ndoa nikiwa mke wa bwana Alex. Mwanaume huyo alinipenda asikwambie mtu, maisha yetu yalitawaliwa na vicheko na tabasamu. Ile ndoto ya kuwa mke wa mtu ilitimia.

Zilikuwa ni nyakati nzuri maishani mwangu. Nyumba niliyokuwa naishi awali niliipangisha baada ya kufunga ndoa na Alex, nilihamia katika nyumba yake nzuri iliyokuwa Kijitonyama. Hapo ndipo nilikuwa nikiishi na muhibi wangu Alex.

Miezi ilipita, mwaka ukakatika. Ndoa iliyokuwa na furaha na vicheko mara ikaanza kukumbwa na dosari. Kwanza nilikuwa sishiki mimba, lakini jambo la pili, mume wangu Alex, alikuwa na tabia mpya. Tabia ya kutosikiliza shida zangu za usiku.

Hakuwa mwenye kujali hisia zangu, kama nisipomtaka mimi angeweza kukaa hata miezi miwili bila kugusa mwili wangu. Sababu yake kubwa ilikuwa ni kuchoka na kazi.

Mwanzoni nilikuwa namwamini kwa sababu alizokuwa akinipa, lakini baada ya kufanya uchunguzi nikabaini, hakuwa akichoshwa na kazi. Ni kwa nini sasa anakuwa hivyo?

Hilo ni swali ambalo kila kukicha nililitafutia majibu. Je simrizishi mume wangu? Au hana hisia nami? Aidha amekinaiwa na penzi langu ama mwanaume huyu anaye mwanamke mwingine anaye mzuzua? Niliamini katika maswali haya,
 
Sehemu ya 51

moja itakuwa ndio chanzo cha Alex kukengeuka.
Ajabu nyingine ni kwamba, hata tatizo la mimi kutokushika mimba mume wangu hakuwa anajali. Mimi ndiye nilikuwa na kiu na mtoto kuliko Alex.

Siwezi kusema katika hili labda kulikuwa na presha fulani kutoka kwa ndugu wa mume wangu. Laa!. Mawifi na wakwe zangu hawakuwa na tatizo kabisa na maisha yangu na mume wangu. Shauku ya kuwa na mtoto nilikuwa nayo mimi mwenyewe.

Nilikwisha kwenda katika cliniki mbalimbali za magonjwa ya wanawake na kufanyiwa vipimo labda kama ninatatizo la kizazi, lakini majibu yalionesha nilikuwa sina tatizo lolote. Hii ilitoa maana kwamba tatizo alikuwa nalo Alex.

“Itabidi ukafanye vipimo Alex, kama kuna tatizo kwa upande wako upatiwe tiba. Kuwa na familia ni jambo muhimu kwenye maisha yetu mume wangu.” usiku mmoja nilimwambia kwa sauti ya upole.

“Shida yako nini we mwanamke, mbona unakosa heshima?” Alex alinifokea.
“Heshima ipi nimekukosea Alex, kukwambia ukafanye vipimo?”
“Umeanza kutunisha misuli humu na kujiona unaweza kuniendesha utakavyo?” mume wangu aliendelea kufoka kwa mambo ya ajabu kabisa.

“Kama nimekukosea nisamehe mume wangu, sikudhamiria kukukosea” nilimjibu na kukaa kimya. Sikupenda kujibizana na mwanaume ambaye tayari alikwisha paniki. “Mwanamke mjinga sana wewe, mkishakuwa na vijimali huwa mnakuwa washenzi kweli” Alex alifoka hadi cheche za mate zikamtoka. Mtoto wa watu nilikuwa kimyaa. Ya nini malumbano? Mwishowe nitandikwe vibao na jibaba lile.
 
Sehemu ya 52

Alex alinikasirikia mwezi mzima. Mwanaume huyo alikuwa na kisirani. Tulikaa miezi miwili bila tendo la ndoa. Kwa kweli yalikuwa ni mateso bila chuki.
Siku moja nikiwa natoka kazini, ndani ya gari langu.

Nilikuwa mtu mwenye mawazo mengi, ndoa yangu ilikuwa inaniumiza kichwa. Sikujua nifanye nini Alex wangu arudi yule wa zamani. Mara nyingi huwa nikiwa na mawazo mengi napenda kutafuta sehemu tulivu na kutuliza akili.
Nilichepuka upande wa pili wa barabara nikaingia kulia kulipokuwa na kituo cha mafuta. Nikaona ni vizuri nikajaze gari mafuta kisha nilekee Msasani Lounge.

Wakati nasogeza gari karibu, kijana mmoja akasogea kunihudumia, mhudumu yule alipokaribia dirishani mwa gari langu, moyo wangu ukapiga kite. Alikuwa ni Victor, mpenzi wangu wa zamani.

“WEWE!!” nilibweka kwa fadhaa.
“Sofia!!” Victor naye alitaharuki baada ya kuniona. Niliteremka garini tukasalimiana nikiwa mwenye tabasamu pana. “Unafanya kazi hapa?” nilimuliza.
“Ndio, nipo hapa nabangaiza.”

“Za siku nyingi?”
“Ni mbaya Sofia.”
“Kwa nini?”
“Maisha yangewezaje kuwa mazuri nikiwa nimekupoteza mwanamke mrembo kama wewe.”

Victor, mwanaume chakaramu aliniambia kwa suati nzuri ya kiume. Kwa sekunde chache sana tukio la kwenye gari langu nikiwa nafanya mapenzi na mwanaume huyo likajitengeneza kichwani mwangu.
Ingawa ilikuwa ni miaka mitatu imepita tangu nivunje amri ya sita na mwanaume huyo, lakini tukio hilo utadhani lilikuwa limetokea jana tu.

Penzi alilonipa Victor kwa siku moja tu, msisimko wake sikuwahi kuupata tena, na nakiri hii ndio sababu ya kutofutika kwa kumbukumbu hiyo.

“Bado unaishi Magomeni?” nilimuliza.
Kabla hajanijibu mara nikapigiwa honi na gari jingine lilikuwa nyuma yangu likihitaji huduma ya mafuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom