MTOTO WA BABA PAROKO.
Sehemu ya name.
Padre Mapunda Ashuhudia Makubwa.Ashindwa Kuamini.
Ilikuwa ni mwaka 1996 wakati Padri Dominique na Padri Mapunda wote wakiwa masomoni huko Missouri Marekani katika chuo cha Theolojia cha Mtakatifu Aquinas, wote wakifanya shahada ya Uzamivu (PhD) katika Theolojia ambapo siri ya Padri Dominique ya kujihusisha na vitendo vya ulawiti watoto ilipovuja kwa Padri Mapunda.
Padri Dominique yeye ametokea shirika la Mtakatifu Yohana Bosco, wenyenye huliita Salesians of Don Bosco au hufupisha kwa kuandika SDB. Shirika hili liliasisiwa na mtawa wa Kiitaliano aliyejulikana kama John Bosco ama wenyewe waitaliano humuita Giovanni Melchiorre Bosco.
Neno ‘Don’ kwa wa italia ni neno lenye maana ya kumpa mtu heshima ya u baba na sasa lilitumika sana kwa ma padre, hivyo kusema Don Bosco unamaanisha ‘ Baba Padre Bosco’ .Ni mtawa aliyependa sana kujihusisha na vijana hivyo hata shirika lake duniani kote hujikita sana katika kupambana na changamoto wanazokutana nazo vijana.
Watawa wa shirika hili huwa na mafunzo ya juu ya namna ya kuishi na kulea vijana, hujua mambo yao ya wakati huo na namna gani wataweza kuwafanya wauishi ujana bila kumsahau Mungu. Duniani kote shirika hili limewekeza sana katika michezo ya aina mbalimbali na taasisi za kutoa elimu za vitendo kwa vijana. Ni vigumu kwa sehemu yoyote duniani ambapo shirika hili lipo na uulize vijana hata wasio wakatoliki na wasilifahamu.
Ni sababu hiyo hata Padri Dominique mahali popote alipokuwapo alikuwa karibu na vijana, akipenda kuongea nao na kushirikiana nao mambo mbalimbali. Ama kwa hakika vijana wengi na hasa watoto walimpenda. Kila mtu aliamini kuwa hali ile ilitokana na karama na utume wake kwa kanisa ikichagizwa na shirika analotokea, lakini kumbe kulikuwa na mengine nyuma ya pazia.
Wakiwa ni marafiki, Padri Dominique na Padri Mapunda walikaa kwenye makazi eneo moja pale chuoni. Kwasababu chuo kilikuwa ni cha kanisa, basi hapakukosa kikanisa kidogo, wazungu hukiita ‘chapel’ . Ni hapa huwa wakifanya ibada lakini pia, na wakazi wa jirani huruhusiwa kushiriki ibada.
Kinachowavutia wengi katika ibada hizi ni mahubiri yanayotolewa, huwa si ya kawaida bali ni mahubiri yaliyoshiba uchambuzi na umaridadi wa elimu ya hali ya juu. Wasomi wengi na vijana wengi wa vyuoni hupenda kuja kusali kwenye kanisa hili dogo kwani mbali ya kuhubiriwa tu, watokapo kanisani huwa wamejifunza kwelikweli.
Ilikuwa si ajabu kuona baada ya ibada watoto wengi wa kati ya umri wa miaka 11-16 wakimkimbilia Padri Dominique na kuanza kucheza nae. Walikaa nae chini kama Yesu na wanafunzi wake wakiulizana maswali na kupeana majibu.
Kwa muda mrefu Padri Dominique alikuwa na hulka ya kupenda kwenda na watoto wale chumbani kwake, tena wakati mwingine aliweza kuingia nao hata wawili ama watatu kwa wakati mmoja. Hakuna aliyewahi kufikiri wala kuwa na shaka ya kwamba kuna lolote linaweza kuwa linaendela ukizingatia heshima aliyokuwa nayo Padri Dominique miongoni mwa jamii na watumishi wa kanisa na chuoni kwa ujumla.
Ilikuwa ni vigumu kuwa na mawazo yoyote hasi kuhusu mahusiano yake na Watoto wale, watu wengi waliamini ni sehemu tu ya mazoea ya Watoto kwa kiongozi wao wa kiroho. Na hakuna hata siku moja mtoto alitoka akiwa analalamika ama kuonyesha sura ya tofauti. Tena vyumba vyao vilikuwa ni vya utulivu wa hali ya juu sana.
Siku moja kijana mmoja wa miaka kama 16 hivi alimfuata Padri Mapunda na kumuomba maongezi nae. Padri Mapunda miaka hiyo hakuwa mtu wa kupenda sana kukaa na kujadiliana na vijana wa kiume. Yeye muda mwingi alipenda kuwa na mabinti. Damu ilikuwa ikichemka sana miaka ile.
Kijana yule alimfuata na bila woga alimweleza kuwa angependa wakati huu alale na Padri Mapunda. Suala lile lilimshangaza sana Padri Mapunda kwanza kwasababu ya umri wa yule kijana lakini cha kushangaza zaidi ni kile alichomwambia. Alihisi amemsikia vibaya au anaota.
“Where are you from my son?”(Umetokea wapi kijana wangu?), Padri Mapunda aliuliza kwa huzuni kubwa.
“From Brooklyn”(Brooklyn). Kijana yule aliyejulikana kwa jina la Carter alijibu kwa kiingereza cha Waamerika wenye asili ya Afrika. Ulikuwa ukimwangalia kwa macho utagundua tu ni kijana aliekulia mtaani na mwenye kujua mambo mengi kuliko umri wake.
Ngono kinyume na maumbile ilikuwa si tu ni dhambi kubwa kwa padre Mapunda lakini hakuwahi kuamini kuwa ipo katika ulimwengu wa kawaida. Padri Mapunda na umri wake wote huo alidhani ni hadithi za kusadikika, lakini alikumbuka kisa cha Sodoma na Gomora katika Biblia. Mngoni wa Songea angejulia wapi mambo hayo? Alistaajabu sana.
“Did someone send you to have me trapped through these diabolical obscenities?”(Kuna mtu amekutuma kuja kunitega?), Padri Mapunda alihoji kwa mshangao.
“No one sir, I am just tired with your friend. I just wanna try a black guy”(Hapana,nimechoka tu na rafiki yako.Nataka kujaribu mtu mweusi). Carter alimjibu Padri Mapunda kihuni huku akisokota sokota nywele zake alizokuwa amesuka rasta, wenyewe wanaziita draids .
“My son, I cannot commit such an act which is against my faith, against the order of nature and religious teachings. You should stop too. Tell me how I can help you to stop this obscenity. God loves you, and he wants nothing other than having you stop and repent”.
(Mwanangu siwezi kufanya kitendo hicho ambacho ni kinyume na Imani yangu, kinyume na asili na pia kinyume na mafundisho ya dini. Mwenyenzi Mungu anakupenda, na hakuna atakalo kwako zaidi yaw ewe kubadilika na kutubu), Padri Mapunda alijibu kwa upole sana.
“Nope. Thanks” Yule kijana alijibu na kuanza kuondoka.
Padri Mapunda alibaki anamshangaa asijue afanye nini. Alihisi kama anaota. Alibaki akijiuliza kuwa kijana yule anamuonaje? Kwanini amfuate yeye? Alipata mkanganyiko mkubwa kimawazo.
Wakati akiwa katika hali ya mshtuko, ghafla alikumbuka kauli aliyoisema kijana yule katika mazungumzo yale mafupi. Kumbukumbu iliyomjia kichwani ni ile Carter aliposema kuwa ‘’Nimemchoka Rafiki yako’’. Kauli hii ilimshtusha kwa mara nyingine pasi na kujua ni nani miongoni mwa rafiki zake wanajihusisha na matendo yale ambayo ni ya laana kubwa ndani ya kanisa.
Kwa mara ya kwanza alianza kuhisi ni Padri Dominique kwani ndiye haswa rafiki yake mkubwa anayekuwa naye sehemu nyingi na mara nyingi. Lakini pia ni Dominique ambaye yupo karibu zaidi na vijana wale. Aliazimia kuanza kufuatilia kuufahamu ukweli.
************************************
Ilikuwa ni siku ya Mkesha wa Pasaka ya mwaka 1996 siku ambayo Padri Mapunda aliona uhakika kuwa shetani yupo ndani ya kanisa.
Kwenye mkesha ule aliyetoa mahubiri alikuwa ni Padri Dominique. Yeye ndiye haswa aliyekuwa akiendesha ibada ya misa na wengine kusaidiana nae. Kwenye mahubiri alisisitiza sana kuwa kufufuka kwa Yesu Kristu ni ishara ya kuanza maisha mapya ya wokovu.
Alisema, Yesu alikufa na hivyo sisi kusamehewa dhambi zote na kufufuka kwake ni ishara ya ushindi na kuwa waumini wafaa kuacha dhambi na kuanza maisha mapya ya wokovu. Hakusita kunukuu mstari wa biblia kutoka Isaya 53:5 uliosema ‘Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu,aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu. Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai; kwa kupigwa kwake sisi tumepona’ hakika mahubiri yake yalisisimua sana usiku ule.
Baada ya ibada ya misa Padri Mapunda aliwahi kuondoka na kumuacha Padri Dominique akiendelea kusalimiana na waamini kama kawaida yake. Padri Mapunda alienda na kusimama mbali kidogo sehemu yenye mwanga hafifu.
Akiwa amesimama pale ghafla alimuona Carter akielekea sehemu yenye makazi yao maPadri (wanafunzi) pale chuoni. Haraka mapigo yake ya moyo yalianza kumwenda mbio. Ni kama vile akili ilianza kukataa anachotaka kukishuhudia.
Baada ya muda alimuona Padri Dominique naye akitoka sakrestia (chumba maalum wanachotumia maPadri na watumishi wa ibada kujiandaa kabla na baada ya ibada ya misa) na kuanza kuelekea chumbani kwake.
Baada ya kuhakikisha Padri Dominique ametokomea, Mapunda akaanza kuelekea kwenye makazi yale. Alikatiza korido zote na hakuweza kumuona Carter. Alijiridhisha kabisa kuwa Carter aliingia na Padri Dominique chumbani kwake.
Padri Mapunda alikimbia chumbani kwake na kuanza kulia kwa uchungu sana. Hakuwa anajua kama kweli mtawa mwenzake aweza kuwa anafanya vitendo vile. Alilia sana na kuanza kujiangalia akiwa ndani ya mavazi yale ya kanzu nyeupe aliyotoka nayo kanisani.
Alisimama mbele ya kioo na kuanza kujitathmini kwa niaba ya Padri Dominique. Aliwaza na kujua kuwa ndani ya kanzu zile wanaficha mambo mengi. Alikumbuka mahubiri aliyotoka kutoa Padri Dominique dakika chache tu zilizopita na akatafakari muda huo anafanya nini, hakika alihisi kuchanganyikiwa.
Alitoka haraka na kwa hatua za taratibu sana akafika mlangoni mwa Padri Dominique. Ilikuwa ni usiku wa kama saa saba hivi kwa saa za Marekani. Hakukuwa na mtu anatembea tembea wakati huo. Alisimama mlangoni na kusikia miguno ya kimahaba kutokea kwenye chumba cha Padri Dominique. Roho ya Padri Mapunda ilijihisi kumchomoka. Alitamani avunje ule mlango lakini aliona si hekima.
Alitamani kupiga kelele ama kuita wenzake lakini pia aliona haitakuwa imesaidia na kinyume chake ingezidisha tatizo. Aliamua kugonga mlango.
****************************************
“Padri Dominiques êtes-vous toujours en ligne?”,(Padri Dominique bado upo hewani?) Padri Mapunda alimuuliza Padri Dominique aliyeonekana kuwa kimya baada ya kuambiwa amejihusisha na vitendo vya ulawiti.
“Boniface, vous avez formulé des accusations très scandaleuses?”(Boniface, umenipa tuhuma nzito na za ajabu sana), Padri Dominique alijikaza na kujifanya kushangaa.
“Non Dominique. Laissez-moi vous rappeler”.(Hapana Dominique. Ngoja nikukumbushe) Padri Mapunda alimwambia Padri Dominique.
Padri Mapunda alianza kumkumbusha usiku wa Pasaka ya mwaka 1996. Alimuuliza kama anakumbuka usiku ule alioenda kumgongea mlango usiku wa saa saba akiwa amelala na kijana Carter chumbani kwake na kumwambia amwachie aondoke usiku ule kwani wazazi wake walikuwa wakimtafuta na waliwasiliana nae.
Ukweli ni kuwa alikuwa akijua kinachoendelea na hakika alisikia yote waliyokuwa wakifanya. Alimweleza jinsi kijana yule alivyomweleza kila jambo lake na ni yeye alisababisha Carter kuacha mazoea na yeye baada ya kumuanzishia ushauri na kufanikiwa kumtafutia kazi Calfonia na kuondoka Missouri.
Alimkumbusha na kuumuuliza anajua kwanini Carter hakumuaga? Na si huyo tu alimtajia vijana wengine watatu aliowahi kuwafanyia vitendo hivyo na ilipofikia hatua anataka kumweleza ukweli baada ya kuwa na woga kwa muda mrefu ndio hapo Padri Dominique alipoondoka na kwenda kumaliza masomo yake huko kwao Ufaransa na hivyo Padri Mapunda kuachana na habari ya kuongea nae juu ya vitendo vyake vile.
“Voulez-vous que je vous envoie des photos?” (Unataka nikutumie picha?). Padri Mapunda alimuuliza Padri Domique.
“No no no”(Hapana) ,Padri Dominique alijibu kwa haraka.
Kwa jinsi Padri Mapunda alivyomwelezea,padre Dominique alijua kwa hakika kuwa padre Mapunda ana hakika na anachokiongea.
“Vous méritez d'être dans le groupe de ces prêtres à qui le pape demande maintenant de se rendre pour avoir sodomisé des adolescents”. (Unastahili uwe miongoni mwa hawa maPadri na maKadinali wanaoombewa msamaha sasa na Papa Francis kwa vitendo vyao vya ulawiti wa vijana wadogo), Padri Mapunda alizidi kugongoea msumari.
“S'il vous plaît Padri boniface, s'il vous plaît”(Tafadhali Padri Boniface, tafadhali), Padri Dominique alisikika akijibu huku akilia.
Hakutaka Padri Mapunda aendelee kumkumbusha vitendo vyake hivyo. Sasa ni mzee wa miaka 65, mkuu wa seminari matendo yake ya nyuma yanamuumiza sana moyo.
*********************************
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka shutuma nzito juu ya viongozi wa ngazi za juu kabisa wa kanisa Katoliki kujihusisha na vitendo vya kuwaingilia vijana wadogo kinyume na maumbile.
Vitendo hivyo vilivyofanywa miaka ya nyuma sasa vinaibuliwa na vijana wale ambao kwa sasa wameshakuwa watu wazima. Taarifa nyingi zikitokea Chile, Honduras na Marekani vimelitikisa kanisa na dunia nzima mpaka kumlazimu Baba Mtakatifu, Papa Francis kuomba msamaha kwa niaba ya kanisa.
Mathalani, huko Marekani mmoja wa makadinali mashuhuri Kadinali
Theodore Edgar McCarrick wa carlfonia amehusishwa kujihusisha na vitendo hivyo na vijana watano enzi za ujana wake. Huko Uskochi (Scotland), Kadinali
Keith O’Brien alijiondoa mwenye ukadinali na kujivua nafasi zote kwa vitendo vyake vya unyanyasaji wa kingono kwa vijana wa kiume.
Kadinali Keith O’Brien akiwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la St. Andrews na Edinburgh, mwaka 2013 aliandika barua kwa Baba Mtakatifu na kumtaka amruhusu kujivua ukadinali na uaskofu kwa kukiri kufanya vitendo vya hovyo kipindi cha nyuma.
Katika barua yake alinukuliwa akisema
“Kwa vijana wote niliowakosea nawaomba radhi na msamaha wa dhati. Kwa kanisa Katoliki la Uskochi mnisamehe sana” . Alilisisimua kanisa. Kadinali O’Brien alikuja kufariki mwezi Machi tarehe 19 huko Newcastle Uingereza akiwa na miaka 80.
*************************************
“Je vais parler au père Angel”, (Nitaongea na Padri Angel). Padri Dominique alimwambia Padri Mapunda.
“J'apprécierai”, (Nitashukuru). Padri Mapunda alijibu.
Ángel Fernández Artime ndiye Mkuu wa shirika la wa Salesians wa Don Bosco duniani. Akiwa ni mzaliwa wa Uhispania lakini makazi yake yakiwa makao makuu ya shirika hilo yalipo Roma Italia ndiye Padri Dominique anaetaka kuwasiliana nae.
“Merci père Dominique”, (Asante sana Padri Dominique). Padri Mapunda alishukuru.
“Je vous remercie”, (Asante). Padri Dominique alijibu na kukata simu.
Kila mmoja kwa upande wake alipumua kwa nguvu baada ya kukata simu asiamini walichokuwa wakijadiliana. Wote walibaki wakifanya tafakari tunduizi dhidi ya mwingine.
Wakiwa katika hali hiyo huku kwa Padri Mapunda alisikia mlango wa ofisi yake ukigongwa na aliporuhusu aingie anayegonga aliinga Padri Karata, msaidizi wake wa kazi, na kumwambia kuwa kuna barua yake imefika. Hakuchelewa, alimwomba ailete ili aiosome imetoka wapi na inataka nini.
Haraka aliisoma juu ilikuwa na nembo ya Baraza kuu la Maaskofu na maneno ya kilatini ‘In servientes est Christus’ yenye kumaanisha ‘Katika kumtumikia Kristu’ . Alipofungua kabla hajasoma maneno mengi neno la kwanza alilokutana nalo ni ‘Cessatio partes in Ractor’ yaani ‘Kusimamishwa kazi ya Ukuu wa Seminari’ .
Padri Mapunda alinyong’onyea.
***********************************
Je,Padri Dominique Atafanikiwa Kumsaidia Kijana Eric?Padri Mapunda Nae Kafikwa Na Nini?Usikose Mwendelezo Wa Kisa Hiki Kinachozidi Kunoga.