Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA KWANZA

Erick Amuona Lucia Kwa Mara Ya kwanza

“Amani ya Kristu iwe nawe” “Iwe nawe pia” walikuwa ni Eric na Lucia wakipeana mikono ya amani katikati ya ibada ya mkesha wa Noeli Parokia ya Mavurunza Kimara Jijini Dar es salaam. Padre Masunga alisisitiza waumini wapeane mikono ya amani kwa kumaanisha na kuwa kama kuna mtu anajua ana chuki na mwenzake basi ni wakati wa kuombana msamaha kwani haitakuwa na maana waumini kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo huku wakiwa na chuki na visasi na majirani zao. Padre Masunga alisisitiza kuwa waumini wasalimiane kwa kujuliana hali tena kwa tabasamu.

Lucia, msichana mrembo sana mzuri kwa sura na umbo alikuwa akisalimiana na Eric kijana mtanashati tena mseminari. Lucia alikuwa na nywele ndefu za rangi ya blond, macho yake yalijaa kope nyingi utadhani ameongezea na za bandia alikuwa hawezi kumtazama mtu usoni kwa sekunde tatu kwa jinsi alivyojaa haiba na aibu.Alikuwa ni mrefu na mwenye umbo la wastani lakini cha mno kuhusu Lucia aliweza sana kujua kuvaa na kujipamba ilikuwa ni kawaida sana yeye kupita na kila mtu wa kike na wa kiume kumwangalia na kumpenda.Hakika alivutia sana kwa macho.

Eric alimpa mkono wa amani Lucia na ghafla alijikuta moyo wake unakwenda mbio kwa jinsi mkono wa Lucia ulivyokuwa laini. Lucia alimtazama machoni Eric kwa kuibia kisha aliangalia chini kwa aibu kama kawaida yake. Eric aliendelea kuushika mkono wa Lucia bila kuuachia, haikuwa kawaida kwani mtu hutakiwa kumshika mkono na baada ya kusalimiana hutakiwa kumwachia na kumsalimia mtu mwingine. Lucia alikuwa amekaa dawati la nyuma ya Eric.Baada ya sekunde kadhaa Eric aliuachia ule mkono wa Lucia na kuendelea kusalimia waumini wengine. Kisha ibada ikaendelea.

Ibada iliendelea huku akili ya Eric ikiwa imehama. Eric alikuwa ni mwanafunzi wa seminari kubwa ya Kipalapala Tabora. Alikuwa akiendelea na masomo yake ya upadre na sasa alikuwa likizo. Katika maisha yake Eric hakuwa amewahi kukutana na mwanamke kimwili. Ni kijana alielelewa kwenye familia yenye maadili sana na hakika hakuwahi kuwa na mahusiano na mwanamke ya kimapenzi japo mara nyingi alikuwa akiingia kwenye vishawishi hivyo. Eric siku zote aliamini padre hutakiwa kuwa mtakatifu na kuwa kwa kazi ile ya uchungaji anayoitaka ambayo hairuhusu kuoa alijitahidi sana kutojiingiza kwenye mahusiano ya kingono.

Ibada ilikuwa ikiendelea lakini Eric akili yake haikuwa pale. Alishindwa kuelewa nini kinatokea akilini mwake, inakuwaje anashindwa kuzingatia ibada mara tu baada ya kumuona Lucia.Wakati hayo yakiendelea Lucia nae alikuwa akitafakari kuhusu Eric kumng’ang’ania mkono wake bila kumsemesha chochote. Hakuwa akimjua Eric na kama ni mwanafunzi wa u padre lakini nae akili haikumtulia.

Ilipofika muda wa watu kwenda kupokea sakramenti Eric aliwahi sana ili aweze kurudi mapema na kukaa kumtazama Lucia. Wakati Lucia akiwa anarudi ndipo Eric aliweza kumtazama vizuri na kwa umakini. Mapigo ya moyo ya Eric yalikuwa yakienda kwa kasi sana. Lucia nae bila kujua alimtupia macho Eric na kujikuta anapoteza hatua na kutaka kudondoka. Eric hakuweza kujizuia alichukua karatasi iliyokuwa ndani ya misale yake (Kitabu kinachoonyesha masomo ya siku hiyo) akaandika “Naitwa Eric ningependa kuongea nawe baada ya Ibada kama hutojali.Asante” alipomaliza alikikunja na kutafakari namna ya kumpa Lucia alieketi nafasi ya nyuma yake.

Wakati akitafakari ulikuwa umefika muda wa kutoa sadaka ya pili hivyo vikapu vya sadaka vilikuwa vikipita kwenye viti unaweka sadaka halafu unampa mwenzako nae akimaliza anampa mwengine hivyo hivyo. Eric akaona hapo ndio muda wa kupenyeza ujumbe wake.Alipokipokea kikapu akaweka sadaka kisha badala ya kumpa wa pembeni yake yeye akageuka akampa Lucia kikapu lakini mkono mmoja akiwa ameshika kile kikaratasi akamshikisha Lucia vyote. Haraka Lucia akang’amua kuwa ule ujumbe ulikuwa wake hivyo akaweka sadaka kwenye kikapu na kumpa wa pembeni yake na kubaki na ule ujumbe. Baada ya dakika kadhaa kupita kwa siri Lucia alifungua kile kikaratasi na kusoma ule ujumbe. Mapigo ya moyo yalimwenda mbio kwani alianza kuhisi nini kitafuata na yeye hakuwa akimjua mwanaume mpaka umri ule. Lucia ndio kwanza alikuwa amejiunga na Chuo kikuu mwaka wa kwanza shahada ya Sheria.

Wakati hayo yakiendelea padre Masunga alisimama na kutoa tangazo kuwa katika ibada ile wapo vijana waliopo seminari wanaosomea u padre na angependa waumini wawafaham kwani ndio mapadre wao wa kesho. Vijana watatu walisimama lakini Eric hakusimama. Hakusimama kwa makusudi kwani kwa anachotaka kuongea na Lucia hakutaka kabisa Lucia ajue kama yeye anasomea u padre. “Nilimwona Eric hapa amekaa wapi mbona simwoni kusimama” alikuwa ni padre Masunga akimwita Eric asimame huku akizungusha shingo kumtafuta alipokaa. Haraka Eric alisimama kwa aibu. Waumini waliwapigia makofi na kisha walikaa.

Baada ya ibada Eric alihitajika kwenda kuonana na padre lakini yeye alitoka haraka ili amuwahi Lucia pale nje. Alipofika nje alimwona Lucia akiwa anatoka nje ya kanisa na alianza kumsogelea ili amsalimie lakini alipomkaribia Lucia alimkwepa na hakupokea mkono wake aliokuwa ameunyoosha tayari kumsalimia Lucia. Eric aligeuka na kumuona Lucia akiingia ndani ya Land Rover Discovery series 4 likiendeshwa na baba yake kisha likaondoka. “Eric padre anakutafuta” ilikuwa ni sauti ya Stanley rafiki wa Eric na mseminari mwenzake ikimwita kumtaarifu kuwa padre Masunga ana mwita Sakrestia (Chumba wanachotumia padre kujiandaa kabla na baada ya ibada). Eric alishtuka na kuanza kukimbia kuelekea sakrestia.

the Legend☆
Lol mh!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA TANO

Cc. Shunie instanbul lovelovelove kuku mweus

Barua Ya Askofu Kengele Yasababisha Simanzi Nzito. Mama Wa Eric Asababisha Sintofahamu

Eric ni kijana alielelewa na mama yake na wajomba. Alilelewa kwa taabu sana hata kuna wakati mama yake alikuwa akipata msaada wa kusomeshewa Eric kutoka shirika la kusaidia watoto wa wasiojiweza linalofadhiliwa na Jaques Laurento tajiri mmoja wa Kifaransa. Msaada huu aliupata baada ya kuwa akifanya kazi za usafi katika ofisi za shirika hilo zilizopo Masaki jijini Dar Es Salaam.

Mama yake Eric alieitwa MariaClara Alphonce alipata uja uzito wa Eric akiwa na miaka 19. Ni ujauzito ule uliosababisha afukuzwe na baba yake huko Sengerema na kukimbilia Dar kwani baba yake alitishia kumuua kwa kusema alimdhalilisha sana.

Baba yake MariaClara yaani mze Alphonce Mabula alikuwa ni katekista wa kanisa katoliki Jimbo la Sengerema Parokia ya Nyagawa. Ni yule mzee asiekosa ibada hata ziwe 12 kwa siku. Mzee Alphonce alitambulika pia kwa ukali uliopitiliza tena asie na masihara.

Aliongoza kwa kuwasema mabinti wa wazazi wenzake kuwa wana tabia mbaya na kuwalaumu wazazi wenzie kwa malezi mabovu ya mabinti zao. MariaClara alipopata ujauzito ilikuwa ni aibu isiyomithilika kwa mzee Mabula. Kwanza mamake MariaClara alikula kipigo cha mbwa koko ktoka kwa mumewe mzee Mabula kwa kuambiwa alikuwa wapi wakati binti yao akifanya ‘uchafu’. Alimpiga sana.

MariaClara yaani mamake na Eric alipoona kichapo kile alikimbia nyumbani na hakurudi tena. Mamake alimtumia salamu kuwa akimbilie Dar kwa mjomba wake aliekuwa akifanya biashara ya kuuza ng’ombe kutoka Sengerema kwenda Dar. MariaClara kwa kusaidiwa na mjomba wake mwingine aliekuwepo kule Sengerema alifanikiwa kwenda Dar na kuanza maisha huko.

Haikuwa rahisi kwani alipofika tu kitu cha kwanza mke wa mjomba wake alichotaka kujua ni ile mimba ni ya nani na nani atamlea huyo mtoto akizaliwa. MariaClara hakutaka kusema mimba amepewa na nani. Katu hakusema. Hata mjomba wake alipomuuliza MariaClara alidanganya kuwa mtoto yule alipewa na utingo wa moja ya malori yaliyokuwa yakienda kusweka ng’obe kule kijijini.

Alipoulizwa jina alidanganya, sasa kwa sababu mjomba wake ni mfanyabiashara hiyo ya ng’ombe alijaribu kuchunguza kwenye malori yanayokwenda kusweka ng’ombe Sengerema lakini hakuweza kumjua huyo utingo. Siri ya baba wa Eric alibaki nayo mamake Eric yaani MariaClara.

Ni katika mazingira yale MariaClara aliilea mimba ya Eric kwa taabu sana. Alianza kufanya kazi ndogo ndogo za kumuingizia kipato mpaka akajifungua na baada ya kupumzika aliendelea na kazi mbalimbali. Kazi kama za mama ntilie, usafi wa majumbani, kuuza genge ni shughuli zilizomlea Eric.

Katika makuzi ya Eric kila wakati mamake alimkumbusha kuwa hataki chochote kutoka kwa mwanae ila amuone akihudumu madhabahuni kama padre.

Katika ukuaji wa Eric MariaClara alimwambia mwanae huyo kuwa babake alifariki na kuwa Eric hana baba. MariaClara alijitahidi sana na kwa uwezo wote kumlea Eric katika mazingira na tamaduni za dini na maadili na hakika hilo alifanikiwa sana. Eric alikuwa ni aina ya kijana asietiliwa shaka hata kidogo.

Japo MariaClara alikimbia kwao kumwogopa baba yake lakini ilifikia hatua baba yake yaani mzee Alphonce alielewa kuwa wakati mwingine watoto hukengeuka na hivyo alimsamehe binti yake na kumtaka arudi nyumbani lakini MariaClara alikataa.

Kipigo alichoshuhudia mama yake akipigwa na babake kilimuumiza akili sana. Alimchukia sana baba yake kiasi kwamba hata mzee Alphonce alipokuja kuugua sana hakwenda kumtazama. Mama yake alimsihi sana aende lakini Maria alikataa. Maria alikuwa anaweza kwenda Sengerema na kushukia kwa wajomba zake na mama yake kwenda kuonana nae hapo lakini kwa miaka 10 tangu akimbie nyumbani katu hakuwahi kurudi.

Wakati wa kifo cha mzee Alphonce Mabula kila ndugu alimsihi Maria aende kumzika baba yake lakini Maria alishikilia msimamo wake kuwa yule si baba yake kwa kitendo alichomfanyia. Mzee Alphonce alizikwa.

Ni baada ya kukaa na kujitafakari sana ndipo Maria alipogundua alifanya makosa. Hasa baada ya malezi ya Eric kuchanganya na kuona uchungu anaoupata pale Eric anapofanya jambo kinyume na alichomfundisha. Aligundua baba yake alipatwa hasira kutokana na kitendo chake cha kubeba ujauzito huku yeye akiwa kinara wa kufundisha watoto wa wengine na mzee muheshimiwa pale parokiani.

Roho ilimuuma sana baada ya kugundua kuwa hata Eric hamjui babu yake na wao kuzaliwa wasichana watupu ilikuwa ni fahari sana kwa mzee Mabula kama angemjua Eric kama mzaliwa wa kwanza wa kiume kwake.

Ni katika hali hiyo Maria aliamua kurudi kijijini baada ya miaka 3 toka babake afariki na kufika kwenye kaburi la babake na kuomba msamaha huku akilia sana.

Alimwahidi babake kuwa ni kwa sababu hiyo atahakikisha Eric sio tu anakuwa mpenda dini kama yeye mzee Mabula bali atakuwa padre kama ambavyo yeye baba yao alitaka sana mtoto wa kiume ili awe padre. Maria alilia sana kaburini mwa mzee Mabula siku zile.

MariaClara tangu kuzaliwa kwa Eric alimpa jina la Nyagabona yaani jina la ukoo wa mama yake, ndio kusema Eric alijulikana kama Eric Nyagabona na hata baada ya ndugu kuuliza sana baba wa Eric mwisho walichoka wakakaa kimya na maisha yakaendelea.

****************************

Baada ya padre Mapunda kumaliza kuisoma ile barua ya askofu macho yaligeuka kuwa mekundu. Alisikitika sana, alimwangalia Eric kama dakika tatu hivi bila kuongea jambo.

Eric alikuwa ni miongoni mwa waseminari wenye akili sana. Alijituma, alikuwa na uelewa mkubwa wa mambo na katika vijana padre Mapunda alikuwa akijivunia katika seminari yake ile basi Eric asingekosa kwenye tatu bora.

Padre Mapunda hakuona sababu hasa ya Eric kusimamishwa masomo na askofu Kengele lakini kwa mujibu wa kanisa na taratibu utovu wa Utii ni kosa kubwa sana kwa kanisa. Ni sawa na jeshini mkubwa amwambie mdogo‘Mbeleee tembea’ halafu yule mdogo abaki amesimama anamwangalia tu. Yani askari kama huyu ataondolewa hapo haraka kwa sababu ipo siku mtakuwa kwenye uwanja wa vita umwambie apige adui risasi halafu atakugomea tena ili awe salama atakupiga wewe unaempa amri usije ukaamrisha mwingine ampige na kumuua. Ni watu hatari sana wanaokosa utii kwa mamlaka.

Ni kwa muktadha huo Eric kwa askofu Kengele alikuwa ni mtu hatari kwa kanisa na alistahili adhabu kali tena haraka kabla hajageuka kuwa bomu kubwa zaidi. Askofu Kengele aliwaza wale mapadre wanaofanya mambo kinyuma na maagizo halafu wanajizolea umaarufu na kuungwa mkono matokeo yake hata akisimamishwa anayumbisha parokia ama jimbo kwa wengine kumfuata ama kuhama kanisa kwa kuliona halina haki. Askofu Kengele aliona ni bora wakawa wanadhibiti watu wa namna hii katika hatua hizi za chini na ndio maana kwake ukosefu wa utii ni mbaya kuliko jambo lingie lolote.

Padre Mapunda hakuwa na la kuficha, alimwambia Eric kuwa barua ile imemwelekeza kumsimamisha masomo mpaka hapo askofu Kengele atakapoamua vinginevyo na kwa muda huo ampange Parokia ya Kwedizinga huko Tanga kama sehemu yake ya kuangaliziwa na mafunzo.

Askofu Kengele alisema atawasiliana na askofu Shemsika wa jimbo katoliki Tanga ili afanye maandalizi hayo.

Taarifa ile ilimuumiza sana Eric, alilia sana. Uchungu ule ulitokana na ukweli kwamba ukipelekwa kwenye uangalizi kama vile basi kuna mawili ni aidha unaishia huko na upadre utausikia bombani au yawezekana kweli askofu akakukumbuka na kukurudisha kumalizia masomo. Vyote viwili kwa Eric vilikuwa ni vichungu. Alilia kama mtoto mdogo alienyang’anywa titi la mama wakati ana njaa kali.

************************

Baada ya Eric na padre Mapunda kubembelezana Eric aliomba ampigie simu mama yake kumtaarifu, kwa wakati ule hata wazo kuwa kuna kiumbe kinaitwa Lucia halikuwepo. Lucia kwa wakati ule alipotea kabisa kwenye mawazo ya Eric na sasa alikuwa akipigania wito wake.

Eric alishika simu huku akitetemeka, alijua taarifa ile ina matokeo mawili. Moja ni kumfanya mama yake afariki kwa mshtuko ama kumfanya awe kichaa. Yaani MariaClara na kutaka Eric awe padre kulishamtengenezea addictionyaani ndio kitu pekee kilikuwa kikimpa matumaini ya kuishi kwa wakati ule.

Padre Mapunda alimwambia Eric kama anadhani taarifa ile itasababisha sintofahamu kwa mama yake basi amuachie yeye ndio ataangalia namna ya kuongea nae. Japo padre Mapunda hajawahi kuongea na mamake Eric na wala hamfaham ila taarifa za kuugua kwake anazifahamu kwa sababu ya ruhusa za mara kwa mara Eric alizokuwa akiomba kwenda kumtazama.

Eric aliomba aongee mamake mwenyewe.

“Shikamoo mama”, Eric alisalimia na mara baada ya maongezi mawili matatu Eric alianza kumweleza mama yake kilichotokea. Alimweleza huku akibubujikwa na machozi.

“Nisamehe mama nimekuangusha ila najua bado Mungu ananiita kumtumikia mama”, Eric alikuwa akiongea kwa uchungu uliochanganyika na kwikwi ya kilio huku akimtia moyo mama yake. Ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa Eric alikuwa ni kijana wa umri wa miaka 30 kwa jinsi alivyokuwa akilia.Mama yake alikuwa akisikiliza kwa makini huku kukisikika sauti ya kwikwi pia.

“Mama” Eric aliita baada ya kuona hakuna neno mama yake anajibu.

“Mama”, Eric aliita tena.

“Eric mpe simu Padre Mapunda”, MariaClara mamake Eric alimwambia Eric ampe ile simu padre Mapunda mkuu wake wa Seminari.

Eric alishangaa iweje mamake ameomba ombi lile. Katika miaka mitatu ya Eric kukaa seminari kuu ya Kipalapala mamake hakuwahi ongea na padre Mapunda. Kwanza alishangaa hata jina amelijuaje maana hakumbuki hata siku moja kuongelea mkuu wao wa seminari.

“Padre, mama anaomba kuongea na wewe”, Eric alimwambia padre Mapunda huku akimpa simu.

“Tumsifu Yesu Kristu mama”, Padre Mapunda alimsalimia mamake Eric kwa sauti ya upole na masikitiko.

“Milele amina Kapalata”, mamake Eric alimjibu padre Mapunda na kutulia kimya.

Hakika kama kuna kitu padre Mapunda kilimshtua basi ni kusikia mtu anamwita kwa jina la Kapalata. Jina hilo ni jina lake alilokuwa akilitumia utotoni tena alilopewa na babu yake mzaa mama yaani mzee Kapalata aliyekuwa Msukuma. Mara ya mwisho kuitwa jina hilo ni kama miaka 30 iliyopita.Isitoshe, si jina alilowahi kulitumia kabisa na aliitwa kwa nadra sana tena hasa na babu yake huyo ambae alishafariki. Alishtuka sana.

“Naongea na nani?”,padre Mapunda aliuliza kwa mshangao uliomfanya hata Eric ashangae.

“Unaongea na MariaClara mama wa huyo mwanao hapo Eric”, mamake Eric alijibu tena kiufupi na kutulia.

Padre Mapunda alikata simu haraka huku akiwa ametoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango wa korido za mahakama huku akimtazama Eric na mapigo ya moyo kiongezeka kwa kasi ya pikipiki ya msafara wa Rais.

****************************

Usiache Kufuatilia Sehemu Ya Sita Ya Simulizi Hii.

the Legend☆
Hehehe

Sio poa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee story imenoga. Ila inataka moyo ndio usionje the rest of your life. Kijana damu inachemka
 
Back
Top Bottom