Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Nilishasema narudia Wakatoliki ni mawakala wa shetani Makasisi wengi ni warawiti wana watoto wanazini na waumini wao asa wale kina mama na wadada wazuri wanaojipitisha kwao eti wanaenda kuungama kumbe wanaungamishwa vyote

Sent using Jamii Forums mobile app

Umeshawahi kulawitiwa. Ilikuwaje. Mb.... ilitaja dini. Hapa ni uwanja wa great Thinkers. Reasoning yako unapaswa kuiupgrade. Kwenye mambo hayo ya kus... Udini hautangazwi ni wewe tu mumeo alitaja dini na dhehebu lake. It’s never about someone’s else . It’s always about you and me. Unique you. It’s never about udini it’s about that someone who did bad to you. Inaposimama pale ni Mnyama. Pole mkuu.
 
Nilishasema narudia Wakatoliki ni mawakala wa shetani Makasisi wengi ni warawiti wana watoto wanazini na waumini wao asa wale kina mama na wadada wazuri wanaojipitisha kwao eti wanaenda kuungama kumbe wanaungamishwa vyote

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu vipi embu tupe ushuhuda ushawahi kulalitiwa nini? Maana huu ujumbe wako mzito sana afu umeongea kwa hisia kali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto wa Baba Paroko - Sehemu ya Tisa

Santa Alleanza

“Praise be to Jesus Christ father”. (Tumsifu Yesu Kristu Padri), alikuwa ni Padri Dominique akisalimiana na Padri Ángel Fernández Artime, Mkuu wa shirika la waSelesiani wa Don Bosco duniani.
“Forever Amen Dominique. What a suprise to get your call at midst of the night!”. (Milele Amina Dominique. Nimestaajabu kuona unanipigia usiku huu), Padri Artime alishangaa.
Padri Dominique alipiga simu usiku wa saa nane kwa saa za Italia. Alifahamu wazi kuwa muda huo Padri Artime angekuwa anamalizia tafakari tunduizi, wazungu huiita ‘meditation’.
Padri Artime kila siku kuanzia saa sita usiku mpaka saa nane hukaa kimya juu ya mkeka wake anaokuwa nao chumbani kwake ili kufanya ‘tafakuri’, alichagua muda huu mahsusi kwasababu kwa kawaida, wakati huu hauna usumbufu wala bugdha ya aina yeyote na ni mtulivu kwa ajili ya kuuganisha akili na roho katika ufanyaji tafakuri hiyo. Ni tabia aliyokuwa nayo tokea alipokuwa kijana mdogo, mwaka wa kwanza seminarini.
Padri Artime na Padri Dominique wakiwa wamepishana miaka saba kiumri huku Padri Dominique akiwa ni mkubwa walikutana huko Hispania wakati Padri Artime akiwa anachukua shahada ya kwanza ya masomo ya Teolojia ya kichungaji (Pastorial Theology) na Falsafa katika chuo kikuu cha kanisa cha Valladolid.
Yeye Padri Dominique alikuwa amekwenda kuchukua masomo ya shahada ya pili ya Falsafa na kile wazungu wanaita ‘Pedagogy’, au huitwa mafunzo ya namna ya kufunza.Wakati huu ni kabla ya yeye kwenda Marekani alipokutana na Padri Mapunda.
Padri Dominique alikuwa rafiki wa Padri Artime na walikuwa ni kama kaka na mdogo wake huku Artime akiwa ni mwenyeji wa Dominique aliyetokea Ufaransa. Uhusiano wao na ukaribu wao uliendelea kudumu na ndiyo sababu huweza kuwasiliana muda wowote bila kujali itifaki na kamwe Padri Artime hawezi kuacha kupokea simu ya Padri Dominique. Wanaheshimiana.
Kwa kawaida, Mkuu wa shirika duniani ni sawa na Baba Mtakatifu kwa shirika hilo husika kwa jinsi wanavyoheshimika na kuogopwa. Si rahisi kuwasiliana nae na ili uwasiliane nae basi utahitajika kufuata mlolongo mrefu. Tena ikisikika Mkuu wa shirika anakuja kuwatembelea huwa ni hekaheka. Ni sawa na kambi ya jeshi ije kutembelewa na Mkuu wa Majeshi. Mkuu wa Majeshi si Rais wa nchi lakini ni kawaida kuona hekaheka nyingi kwa wanajeshi wanapotembelewa na Mkuu wa Majeshi, hakuna tofauti na Rais.
Kwa Padri Dominique, Padri Artime alikuwa ni mtu mkubwa sana kicheo lakini kwa hali halisi waliwasiliana kama marafiki wa kawaida.
“Yes father, it’s because I know when the sun rise it will be difficult to get hold of you”(Ndio Padri, ni kwa sababu najua jua likichomoza itakuwa ni vigumu mimi kukupata). Padri Dominique alimjibu Artime.
Padri Dominique alimjibu hivyo akimaanisha kuwa kukipambazuka ni ngumu Padri Artime kupokea simu kwani anakuwa na ratiba ndefu ya siku. Usiku ule anajua ndio muda haswa wa kuongea nae kwani ana hakika hakuna kiumbe anaweza kumtafuta Padri Artime usiku wa manane namna ile, labda Papa.
“I acknowledge that Dominique, now tell me what is the matter? ”(Ni kweli Dominique, niambie kuna jambo gani?). Padri Artime aliuliza kwa unyenyekevu kama kawaida yake.
“It is my intention to resign from the role of the Ractorship and probably from the Priesthood”. (Ni nia yangu ya kutaka kujivua nafasi ya ukuu wa seminari na ikiwezekana kujivua nadhiri yangu ya kipadri), Padri Dominique alisikia akimjibu mkuu wake katika sauti ya kutetemeka.
“What are you talking about for Christ’s sake! What has happened? Have you informed your Provincial?”. (Yesu Kristu! Unasema nini? Nini kimetokea? Umeshamtaarifu mkuu wa shirika wa nchini mwako?), Padri Artime alionekana kushangaa.
“Artime, this is a brothery talk, not a hierachical one. I kindly request an appointment with you out of your tight daily schedule to discuss the matter”. (Artime, haya ni mazungumzo ya kindugu na si ya kirasimu. Tafadhali naomba miadi ya kuonana nawe japo natambua ratiba zinazokubana za kila siku). Padri Dominique alimjibu Artime aliyeonekana kutaka kuleta ukiritimba wa kiitifaki za kiofisi.
“I know Dominique, but I am very surprised that you would want to do all that out of a blue sky. On the other hand, I have to fly to Argentina to start a preparation for the apostolic and diplomacy visit of the Vicar of Jesus Christ. The visit is three months to come and Pope has appointed me to lead the preparation committee as one of the apostolic mission there is for the Youth. As such, I will be a bit tight. Can we hold this and have a discussion thereafter?”
(Nafahamu Dominique, ni kwamba nimeshangazwa tu kuwa unakusudia kufanya hayo ghafla. Lakini bila kujali hilo, ninahitajika kusafiri kuelekea Argentina kuanza maandalizi ya ziara ya kitume na kidiplomasia ya Mwakilishi wa Yesu Kristu. Ziara hii ni ndani miezi mitatu ijayo na Baba Mtakatifu ameniteua kuongoza kamati ya maandalizi kwa sababu moja ya lengo la kichungaji kule ni kwa ajili ya kukutana na vijana. Ni kwasababu hiyo nitakuwa nimebanwa sana, nikuombe usubiri kwanza mpaka ziara hii itakapokamilika. Tunaweza kuzungumza baada ya hilo Dominique?), Padri Artime alimsihi Padri Dominique.
“It is urgent. Three months are just too much Artime”. (Ni suala la dharura. Miezi mitatu ni mingi mno Artime), Padri Dominique alisisitiza.
“Ok, I will let you know tomorrow to tell you where to catch me for the matter, alright?”. (Sawa, nitakutafuta kesho kukutaarifu wapi utaweza kunipata kwa mazungumzo, sawa?). Padri Artime alimuuliza Padri Dominique kwa sauti ya upole na utaratibu.
“Thank you father. May the Grace of our Lord Jesus Christ, Love of God, the Father and the Communion of the Holy Spirit be with us all, now and forever. Amen”. (Asante sana Padri. Neema ya Bwana Yesu Kristu, Upendo wa Mungu Baba na Ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nasi sote sasa na hata milele. Amina), Padri Dominique alimalizia maongezi.
“Amen Dominique, (Amina Dominique). Padri Artime alimalizia na kukata simu ili aendelee kulala.
*********************************
Padri Angel Fernandez Artime na Baba Mtakatifu Fancis ni marafiki wa siku nyingi. Walijuana wakati Kadinali Jorge Mario Bergoglio alipokuwa ni Kadinali wa jimbo kuu katoliki la Buenos Aires huko Argentina. Wakati huo Padri Artime akiwa Mkuu wa shirika la Waselesiani wa Don Bosco nchini humo.
Kadinali Jorge Mario Bergoglio baadae alikuja kuwa Papa na kuitwa Papa Francis kwa kufuata utaratibu wa kanisa katoliki wa mtu kuchagua jina atakalotumia kuitwa mara tu anapotangazwa kuwa Papa. Hivyo, kitendo cha Padri Artime kuja kuteuliwa na mkutano mkuu wa shirika la Waselesiani wa Don Bosco kuwa Mkuu wake wa shirika kilimsogeza karibu na Papa Francis.
Kwa ziara hii ya Argentina, Papa Francis aliona hakuna mtu mwingine aliyefaa zaidi kuongoza ziara ile bali Padri Artime. Alimkabidhi kazi hiyo.
*******************************************
‘Vicar of Jesus Christ’ ama wenyewe wanavyoita kwa kilatini ‘Vicarius Filii Dei’ ni moja ya vyeo vya Baba Mtakatifu. Jina hilo humaanisha Mwakilishi wa Yesu Kristu hapa Duniani au kwa maneno mengine unaweza kusema neno analolitamka Baba Mtakatifu basi ni Yesu ametamka.
Vyeo vingine vya Baba Mtakatifu ni Papa (Pope), Askofu wa Roma (Bishop of Rome), Mrithi wa taji la Mitume (Successor of the Prince of the Apostles), Mkuu wa kanisa la Ulimwengu (Supreme Pontiff of the Universal Church), Mtawala wa Vatican (Sovereign of the State of Vatican City) na Mtumishi wa Watumishi wa Mungu (Servant of the Servants of God).
Vyeo vyote hivi hutumika katika matukio tofauti na wakati tofauti au cheo zaidi ya kimoja huweza kutumia kwa wakati mmoja.
Mfano, anapokutana na viongozi wa dunia hukutana nao kama Mtawala wa Vatican au kama Mtawala wa Vatican na Mkuu wa Kanisa la Ulimwengu kwa wakati mmoja. Anapokuwa kwenye Ibada nje ya Roma husimama kama Mwakilishi wa Yesu Kristu na Mkuu wa kanisa la Ulimwengu. Akiwa Roma yeye ni Askofu wa Roma. Akiwa na mkutano na ma kadinali wake husimama kama Mtumishi wa Watumishi wa Mungu na Mrithi wa Taji la Mitume.
Baba Mtakatifu ni Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani na Mkuu wa serikali ya Vatican vyote kwa wakati mmoja. Kanisa Katoliki huitwa pia Kanisa la Ulimwengu kutokana na neno Katoliki kutoholewa kwenye lugha ya Kilatini kwenye neno catholicus ambalo pia asili yake kabisa ni neno la Kigiriki la katholikos, wenyewe wagiriki huliandika καθολικός lenye maana ya Ulimwengu. Hivyo unaposema kanisa katoliki ni sawa na mtu anaesema Kanisa la Ulimwengu mzima.
Padri Artime ametumwa kuandaa ziara hii yenye misheni ya kichungaji na kisiasa. Ziara yenye msisimko mkubwa.
**********************************
Siku ile mara baada ya Padri Dominique kumaliza kuongea na simu na Padri Mapunda aliona siku zimefika za mambo yaliyofichika kuwekwa hadharani. Aliwaza na kuumia sana moyoni, alijua haiwezekani na haitakaa iwezekane kumwezesha Eric aingie seminarini kule Finland bila utaratibu mahsusi kufuatwa. Hakuona njia hiyo hasa ukizingatia mifumo ya kijasusi na ufuatiliaji ya kanisa katoliki.
Duniani kote husema jambo linaloendelea ndani ya kanisa na kanisa likawa kimya ni mambo mawili yametokea, ni aidha kanisa LINAJUA likaamua kunyamazia kwa sababu fulani fulani ama hilo jambo HALIPO. Kwa maneno mengine hakuna jambo linalotokea eti kanisa likashtuka kuwa lilikuwa halijui, hilo halipo.
Wachambuzi wengine husema ndani ya kanisa mifumo ya ufuatiliaji habari na ujasusi ni sawa na ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani kama vile CIA ya Marekani, Mossad ya Israel, IB ya Pakistan na mengine ya namna hiyo. Kwenye kanisa Katoliki wao hujiita Santa Alleanza.
Santa Alleanza
ndilo jina haswa la shirika la kijasusi la Vatican. Wenyewe huliita kwa kizungu ‘Holy Alliance’ ama Kiswahili litaitwa ‘Umoja Mtakatifu’. Waitaliano wameenda mbali zaidi wao huliita kwa kizungu ‘The Entity’ au kwa lugha yao husema ‘L'Entità’.
Shirika hili ni la siri kubwa labda kuliko mashirika mengine yote na hata kupata taarifa zake si jambo jepesi na linaloweza kufanywa na kila mmoja. Aliwahi kusikika aliyekuwa Mkurugenzi wa Kwanza wa CIA, shirika la kijasusi la Marekani Bw. Allen Dulles akisema shirika hili lenye kauli mbiu isemayo “Cum Cruce et Gladio” yenye tafsiri ya kizungu “With the Cross and Sword” au kiswahili ingesemwa “Kwa Msalaba na Upanga” liliundwa mwaka 1566 wakati hata CIA haijulikani kama itakuja kuwepo (CIA iliundwa mwaka 1947, September 18)
Inaaminina kuwa Santa Alleanza ndiyo walioandaa mpango wa kutaka kumpindua Malkia Elizabeth wa Kwanza (Queen Elizabeth I) kabla ya shirika lolote la Intelijensia duniani kuwahi kufikiri kupindua serikali yoyote.
Santa Alleanza pia inaaminika kuwa na kundi la wataalamu wa kijasusi wenye kufanya kazi kwa kasi ya ajabu tena wenye vifaa, miundombinu na utaalamu mkubwa na wa kisasa zaidi katika kutimiza majukumu yao kuliko watu wowote. Kundi hili wao huliita Gruppo Intervento Rapido (GIR) yaani kwa Kingereza ‘Rapid-Intervention Group’.
Kwa kutambua yote hayo Padri Dominique aliona ni bora ajivue ukuu wa seminari pamoja na uPadri ili hata Padri Mapunda akianzisha kelele za kutaka kumdhalilisha akute amechelewa.
Padri Dominique alilipenda kanisa na hakutaka udhaifu wake ulichafue, alitaka ajitoe kabisa mbele ya uso wa kanisa ili achafuke mwenyewe. Bila Padri Mapunda kujua, Padri Dominique aliandaa mpango wa kujivua wadhifa na nadhiri yake ya uPadri.
Aliona kusubiri miezi mitatu ili Padri Artime amalize ziara ingekuwa ni mingi sana kwa sababu Padri Mapunda anataka suala la mtoto wake lishughulikiwe haraka. Aliamua kumuwahi.
********************************
Huku Padri Mapunda yeye akiendelea kufikiri kuwa Padri Dominique anafikiria namna ya kumsaidia, alipokea barua iliyomfanya presha kupanda. Aliposoma maneno machache na kuona inahusu yeye kusimamishwa ukuu wa Seminari ya Kipalapala alianza kuvujwa jasho.
Aliishiwa nguvu na kuketi juu ya meza ili aweze kuisoma. Mzee wa umri wa miaka 65 hakujua ndani ya barua ile kuna maelekezo gani zaidi. Alihisi kuchanganyikiwa.
***********************************
Usikose Mwendelezo Wa Kisa Hiki Wiki Ijayo.
 
Wewe unawajua Wakatoliki walioko humu? Mimi nakosoa mfumo wa kikatoliki haufai kabisa kuigwa nandomaana Martine Ruther aliyekuwa ni mtu wa pili kutoka kwa Papa alimkosoa badala yake Papa akaamuru auwawe. Mapadri niwachafu kwa wake za watu ni wachafu kwa vijana wao uwaita Mabrother's ni wachafu kwa Masister wanaowahudumia sasa kwanini wasio wakatimiza haja zao za kimwili?

Simaanishi wote lakini %80ni wazinzi wakutupwa. Bora Muislamu kitabu chake kinamruhusu kuoa wake wanne najua siku wakiruhusiwa kuoa wataoa wanawake kumi kila mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usijali msafi.. pepo ni yako sisi wakatoliki moto wetu! But kwann upo hapa duniani na ww ni msafi kiasi hiko?? Hapakufai mkuu mahali pako ni mbinguni kwa wasio na dhambi

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Natamani nimfahamu mwandishi wa hii stori asee...habahatishi anajua anachokiandika.

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom